Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi.
Kufuatia
vyombo vya habari mbalimbali nchini kutoa habari ambayo inamhusu
Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi kuwa anatakiwa kufika
mahakamani Agosti, 24 mwaka huu kujieleza kwanini asifungwe kwa
kushindwa kutekeleza hukumu ya kulipa Dola 598,750 (Bil. 1.20), wakili
wa Dk. Mengi, Deogratias Ringia amekanusha habari hiyo.
Katika
taarifa ambayo imetolewa na wakili Ringia, amesema kuwa akiulizwa na
watu mbalimbali kama ni kweli kuna hati imetolewa na Mahakama Kuu
ikimtaka mteja wake Dk. Mengi kufika mahakamani kujieleza kwanini
asifungwe baada ya vyombo mbalimbali kuripoti kuwa anatakiwa kufika
mahakamani lakini jambo hilo halina ukweli.
"Mhusika
mkuu katika kesi hiyo ni kampuni nayoitwa KM Prospecting Limited ambayo
Dk. Mengi siyo mwanahisa wala mkurugenzi katika kampuni hiyo. Kampuni
hiyo ndiyo iliingia kwenye mkataba na wadai iliyopelekea kesi hiyo ya
madai," alisema Ringia.
Ringia
alisema hatua ya kumuunganisha Dk. Mengi katika kesi hiyo lilikuja baada
ya mahakama kuamua hoja mbili zinazohusu kesi hiyo ndipo wadai ambao ni
wafanyabiashara Muganyizi Lutagwaba, Eric Mshauri na Charles Mgweo
kumuingiza Dk. Mengi katika kesi licha ya kuwa hausiki.
Baadhi ya
vyombo vya habari vilivyoandika habari hiyo ni pamoja na gazeti la Jambo
Leo, Daily News, The Citizen na mtandao wa Habari Leo Online.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwapungia wananchi
wa Inyonga baada ya waziri Mkuu kutawazwa kuwa Chief wa Wakonongo na kupewa
jina la Chief Kayamba wa Kwanza katika mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Inyonga Agosti 22, 2016. Kulia ni Cheif
wa Wakonongo, Kayamba wa Pili. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakimsikiliza Chifu Kayamba wa
Pili (kulia) wakati Waziri Mkuu alipotwazwa kuwa Chief wa Wakonongo
na kupewa jina la Kayamba wa Kwanza katika mkutano uliofanyika kwenye
uwanja wa Shule ya Msingi Inyonga wialyani Mlele Agosti 22, 2016
Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa akionyesha Mpango wa Mafunzo ya Ujasiriamali katika jimbo la
Nsimbo mkoani Katavi aliouzindua kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara
katika kijiji cha Katumba akiwa katika ziara ya mkoa huo Agosti 21, 2016
Wananchi
wakionyesha mabango wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasili kwenye
uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda kuhutubia mkutano wa hadhara
Agosti 21, 2016. Katika hotuba yake Waziri Mkuu alizitolea majibu kero
zote zilizoandikwa kwenye mabango hayo akiwahusisha watendaji wa
Halmashauri, mkoa na wilaya
Wananchi
wakionyesha mabango wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasili kwenye
uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda kuhutubia mkutano wa hadhara
Agosti 21, 2016. Katika hotuba yake Waziri Mkuu alizitolea majibu kero
zote zilizoandikwa kwenye mabango hayo akiwahusisha watendaji wa
Halmashauri, mkoa na wilaya
Mke wa Waziri Mkuu, Mama
Mary Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Mpanda wakati Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa alipohutubia mkutano wa hadahara kwenye uwanja wa Kashaulili mjini
Mpanda Agosti 21, 2016. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Mstaafu,
Raphael Mbuga
Waziri Mkuu Majaliwa kihutubia wananchi
Wasanii wa kijiji cha
Katumba wilayani Mpanda wakicheza ngoma ya Kasimbo wakati Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa alipohutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo akiwa katika
ziara ya mkoa wa Katavi Agosti 21, 2016







No comments :
Post a Comment