
KISHINDO CHA UZINDUZI WA MSIMU WA TIGOFIESTA 2016 CHAZIZIMA JIJINI MWANZA USIKU WA JANA
Mkali
wa singeli ManFongo na Shilole wakilivamia jukwaa la Tigo Fiesta 2016
katika tamasha hilo kubwa liliofanyika usiku wa jana jijini Mwanza na
kukutanisha wasanii nguli katika muziki wa kizazi kipya na Msanii wa
kimataifa toka Nijeria Wizkid .
Umati
wa wakazi wa Jiji la Mwanza wakitoa shangwe wakati burudani mbalimbali
zikiendelea katika Tamasha la Tigo Fiesta 2016 viwanja vya CCM Kirumba
hapo usiku wa jana.
Alikiba
alikuwa kivutio kwa mashabiki wengi mara baada ya kufanya suprize na
kutoa burudani ya kukata na shoka huku mashabiki zake wakifuatisha
nyimbo zake moja baada ya nyingine katika Tamasha la Tigo Fiesta 2016
katika viwanja vya Kirumba Jijini Mwanza.
Benpol akilishambulia jukwaa la Tigo Fiesta 2016 lilifnayika jana katika viwanja vya CCM kirumba Jijini Mwanza.
Msanii wa kizazi kipya Dayna Nyange akitumbuiza umati uliohudhuria Tamasha la Tigo Fiesta 2016 jijini Mwanza hapo usiku wa jana.
GARETH BALE AIONGOZA REAL MADRID KUPATA USHINDI
Mshambuliaji Gareth Bale ametumia
sekunde 72 kufunga goli lake la kwanza kwa msimu huu na kisha
kuongeza la pili wakati Real Madrid ikiifunga Real Sociedad kwa mgoli
3-0 katika mchezo wa La Liga.
Mchezaji Marco Asensio, 20, naye
alifunga goli akionekana kuongozwa vyema na Bale na kuifanya Real
Madrid kutoonekana kumkosa mshambuliaji wake nyota Cristiano Ronaldo
ambaye hakushuka dimbani.
Gareth Bale akiruka juu na kupiga mpira wa kichwa uliojaa wavuni
Beki Markel Bergara akiteleza na
kumkata buti Mateo Kovacic wa Real Madrid









No comments :
Post a Comment