Sunday, August 21, 2016

TUME YA MIPANGO YAKAMILISHA MAFUNZO YA WATAALAMU WA KUFUNDISHA USIMAMIZI NA UTAYARISHAJI WA MIRADI YA UMMA

Mchumi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bi. Sauda Ponda akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Tume ya Mipango kwa niaba ya wahitimu.
Naibu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe akifunga mafunzo ya kuandaa wataalamu wa kufundisha masuala ya Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma, pembeni yake ni Kaimu Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Uchumi Jumla, Dkt. Lorah Madete.

Wajumbe wa mafunzo wakimsikiliza Naibu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe wakati wa kufunga mafunzo hayo.

Na Adili Mhina

Tume ya Mipango imekamilisha zoezi la kuandaa wataalamu wanaotarajiwa kutoa mafunzo juu ya usimamizi na utayarishaji wa miradi ya uwekezaji katika sekta ya umma kwa maofisa wa serikali walio chini ya Idara za Sera na Mipango na zile za Uwekezaji katika Wizara, Mikoa, Halmashauri, Mashirika pamoja na Taasisi mabalimbali za Umma hapa nchini.

Akifunga mafunzo hayo mwishoni mwa juma, Naibu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe alisema kuwa katika awamu hii ambapo Shilingi trilioni 59 kati ya trilioni 107 zinatarajiwa kutolewa na Serikali pekee katika kutekeleza Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, Serikali imeamua kujipanga upya ili kuhakikisha miradi yote itakayoanzishwa inaleta tija kwa wananchi.

“Tumeamua kujiandaa mapema kwa sababu tunatarajia miradi mingi mikubwa itaanzishwa katika kipindi hiki cha utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP II). Hivyo, ni muhimu huko mtakapoelekea kutoa mafunzo mhakikishe mnatoa mbinu sahihi za kukabili changamoto zinazojitokeza katika kutayarisha, kutekeleza na kusimamia miradi ya maendeleo”, Alisema Bw. Sangawe.

Sangawe aliongeza kuwa baada ya mafunzo hayo kuwafikia walengwa wote hakutakuwa na sababu kwa maofisa wa serikali kushindwa kuandaa, kutekeleza, kusimamia au kutoa ushauri sahihi pale serikali inapofanya uwekezaji kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Tume ya Mipango kwa niaba ya wahitimu wote, Mchumi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bi. Sauda Ponda alisema kuwa wahitimu wote walipata fursa ya kujadili, kuuliza na kufanya mazoezi mbalimbali katika vikundi kwa lengo la kuongeza uelewa na kuimarisha uwezo kwa ajili ya kwenda kutoa mafunzo kwa wahusika.

“Kwa niaba ya wenzangu wote napenda kutoa shukrani za pekee kwa Tume ya Mipango kwa kuandaa mafunzo haya, waalimu wetu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wametufundisha vizuri na wametupa mazoezi ya kutosha na sote tuko tayari kwenda kutoa elimu hii kwa wenzetu,”. Alisema Bi. Ponda.

Wataalamu hao waliotumia siku tano kuchambua kwa kina Mwongozo wa Usimamizi na Utayarishaji wa Miradi ya Uwekezaji katika sekta ya Umma ambao ndio unaopaswa kufuatwa katika kutekeleza miradi yote ya serikali, wanatarajiwa kugawanyika katika makundi mbalimbali yatakayotoa mafunzo kikanda ambapo zoezi hilo litaanza tarehe 22 mwezi huu.

MICHUANO YA OLIMPIKI: CASTER SEMENYA ATWAA MEDALI YA DHAHABU

Mwanariadha wa kike wa Afrika Kusini, Caster Semenya, ameshinda medali ya dhababu ya Olimpiki katika mbio za mita 800.

Semenya, 25, ameweka rekodi ya taifa lake ya kushinda kwa muda wa dakika moja na sekunde 55.28 na kumshinda kiulaini mshindi wa medali ya fedha, Francine Niyonsaba wa Burundi.

Katika mbio hizo mwanariadha wa Kenya, Margaret Nyairera Wambui ametwaa medali ya shaba na kuweka rekodi yake mwenye mpya ya kutumia dakika moja na sekunde 57:69.
        Mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya akimaliza mbio za mita 800
Caster Semenya akiwaliwaza mwanariadha wa Canada Melissa Bishop (kushoto) na Muingereza Lynsey Sharp (kulia)

MAJALIWA ATEMBELEA KIJI CHA KATUMBA WILAYANI MPANDA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua mnara uliojengwa na wakimbizi waliopewa uraia wa Tanzania ili kumshukuru Mungu kwa kupewa urais huo wakati alipokitembelea kijiji Katumba mkoani Katavi Agosti 21, 2016. Kushoto kwake ni mkewe Mary na kushoto i Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Mbuga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakifurahia baada ya kuzindua mnara uliojengwa na wakimbizi waliopewa uraia wa Tanzania ili kumshukuru Mungu kwa kupewa urais huo wakati Waziri Mkuu alipokitembelea kijiji Katumba mkoani Katavi Agosti 21, 2016. Kushoto kwake ni mkewe Mary na kushoto i Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Mbuga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuzindua mnara uliojengwa na wakimbizi waliopewa uraia wa Tanzania katika kijiji cha Katumba mkoani Katavi Agosti 21, 2016 ili kumshukuru Mungu kwa kupewa uraia huo. Kushoto kwake ni mkewe Mary na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Raphael Mbuga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Makazi ya Wakimbizi ya Katumba mkoani Katavi, Bwana Igwe baada ya kuwasili kambini hapo kuzunguma na wananchi akiwa katika ziara ya mkoa wa Katavi Agosti 21, 2016. Wapili kulia ni mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa kijiji cha Katumba mkoani Katavi wakati alipoingia kwenye kijiji hicho kuzungumza na wananchi akiwa katika ziara ya mkoa wa Katavi Agosti 21, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Raphael Mbuga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkuano wa hadhara katika kijiji cha Katumba mkoani Katavi Agosti 21, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

ZIARA YA MAJALIWA MPANDA

Wasanii wa kijiji cha Katumba wilayani Mpanda wakicheza ngoma ya Kasimbo wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipohutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo akiwa katika ziara ya mkoa wa Katavi Agosti 21, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia kwake) wakiwapungia wananchi wa Mpanda wakati walipowasili kwenye uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda kuhutubia mkutano wa hadhara Agosti21, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wananchi wakionyesha mabango wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasili kwenye uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda kuhutubia mkutano wa hadhara Agosti 21, 2016. Katika hotuba yake Waziri Mkuu alizitolea majibu kero zote zilizoandikwa kwenye mabango hayo akiwahusisha watendaji wa Halmashauri, mkoa na wilaya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Mpanda wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipohutubia mkutano wa hadahara kwenye uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda Agosti 21, 2016. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Mbuga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongea na wananchi wa Mpanda kwenye uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda alipohutubia mkutano wa hadhara Agosti21, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAHOJIANO NA MJASIRIAMALI NA MWANAHARAKATI DIANA GASPER

Katika huyu na yule wiki hii, tumezungumza Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Kinyago Travels and Tours na Stuka Tanzania Diana Gasper, ambaye pamoja na mambo mengine, amezungumzia historia yake, ya kampuni zake na harakati nzima za biashara na harakati za kuikomboa jamii ya Tanzania
Amezungumza mengi.

KASESELA AWASWEKA NDANI WALINZI WAWILI WA KAMPUNI YA ULINZI YA AMAZON KWA KUNYANYASA WANANCHI

Leo saa 3 na dakika 25 Usiku mkuu wa wilaya Mh Richard Kasesela alipokea wakina mama 3 wakiwa wanatetemeka kwa baridi, wakilalamika kumwagiwa maji walipokuwa wamekaa kwenye eneo la kusubiria wagonjwa walio lazwa hasa kwa wale walio toka mbali. 

Maji hayo yalimwagwa na walinzi wa kampuni ya Amazon ambao ndio wamepewa kandarasi ya ulinzi hospitali ya Rufaa ya Iringa.
Mkuu wa wilaya Iringa, Richard Kasesela alifika hospitali kujionea mwenyewe hali halisi, baadae pia akapata taarifa kuwa jana yake Mlinzi alimpiga mzee aliyekuwa ameleta chakula hospitali na kumwaga kwa mateke. 

Mkuu wa wilaya aliamuru mlinzi huyo na mwenzake wakamatwe pia mwenye kampuni afike kituo cha polisi haraka iwezekanavyo.
"Hali hii imeudhi sana hasa ukiona jinsi wakina mama walivyo nyanyasika wengine vyombo vyao na chakula kuroweshwa maji." alisema Mh Kasesela.

No comments :

Post a Comment