Sunday, August 21, 2016

RAIS MAGUFULI ATEUA MKUU MPYA WA WILAYA YA ARUSHA

 Bw.Gabriel Fabian Daqarro, Mkuu mpya wa Wilaya ya Arusha.

Mratibu wa Taasisi ya The Hope Campaign, Mpelo Kapama (kushoto), akiwaelekeza maofisa wenzake kabla ya kwenda kukabidhi msaada huo.
Mizigo ikitolewa kwenye gari.
Aman Issaya wa taasisi hiyo akiwa na kiroba cha sukari akielekea eneo la makabidhiano.
Mratibu wa Taasisi ya The Hope Campaign, Mpelo Kapama, akiwa amebeba kiroba cha sukari wakati taasisi hiyo ilipotoa msaada wa vyakula na vifaa vya shuleni kwa Kituo cha Yatima Group Trust Fund cha Chamazi Temekie jijini Dar es Salaam leo.


Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog.

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limesema litatumia fursa ya tukio la kupatwa kwa jua kama njia mojawapo ya kutangaza hifadhi za taifa hususani zinazopatikana katika mikoa ya nyanda za juu kusini na Magharibi mwa Tanzania.

1
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ilala wakati alipotangaza kupatikana kwa wanafunzi hewa 599 katika shule 6 za wilaya hiyo ambapo uchunguzi wa wanafunzi wengine hewa bado unaendelea.
2
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akisisitiza jambo wakati alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ilala wakati alipotangaza kupatikana kwa wanafunzi hewa 599 katika shule 6 za wilaya hiyo, Kulia ni Mkurugenzi wa Wilaya hiyo Bw. Edward Mpogolo.
3
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ilala wakati alipotangaza kupatikana kwa wanafunzi hewa 599 katika shule 6 za wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema ametangaza kupatikana kwa wanafunzi hewa 599 katika shule 6 za wilaya ya Ilala ambazo hakuzitaja, Mjema amesema baada uchunguzi huo kumegundulika wanafunzi idadi hiyo ya ambapo wahusika wote watachukuliwa hatua za kinidhamu lakini pia sheria itachukua mkondo wake kwani hayo ni makosa kama yalivyo makosa mengine
Wilaya ya Ilala ina shule za sekondari za serikali 46 na za sekondari 49 ukiacha shule za taasisi binafsi ,zoezi la ukaguzi bado linaendelea katika shule zote za msingi wilayani humompaka Septemba 1 mwaka huu ndiyo litamalizika.
Akizungumzia suala la Madawati mkuu wa wilaya huyo amewapongeza wadau wote waliochangia madawati mpaka kuhakikisha uhaba wa madawati katika wilaya ya Ilala unakwisha huku kukiwa ziada ya madawati 2821
Ameongeza kuwa kazi kubwa inayofuatia kwa sasa ni kuongeza vyumba vya madarasa ambapo kazi hiyo inaendelea vizuri .
Mh. Sophia mjema pia amemshukuru Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuanzisha mkakati wa wadau kuchangia madawati jambo ambalo limesaidia tatizo hilo kushughulikiwa kikamilifu na wadau mbalimbali, lakini pia akampongeza Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda kwa usimiamizi thabiti wa utekelezaji wa mkakati huo jambo ambalo limesaidia wilaya ya Ilala kumaliza kabisa tatizo la uhaba wa madawati katika shule za zake za msingi
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Kamanda Mohamed Mpinga akimkabidhi Mwanafunzi wa darasa la sita Antonia Anthony zawadi ya Begi na Cheti,kutoka shule ya msingi Mwananyamala baada ya kuibuka mshindi wa pili katika Kilele cha shindano la Uchoraji kwa ajili ya kuhamasisha usalama barabarani katika shule za msingi jijini Dar Es Salaam kwa mwaka 2016,hafla hiyo fupi iliyoandaliwa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania ilifanyika mapema leo katika viunga vya shue ya msingi Bunge.

Hii ni zawadi ya heshima (tuzo) iliyotolewa na kampuni ya Puma Energy Tanzania na kukabidhiwa kwa mshindi wa kwanza,Mwanafunzi wa darasa la sita kutoka shule ya Msingi Bunge,Veronika Inocent.


Mkurugenzi Mkuu kutoka kampeni ya Puma Energy Tanzania Ltd,Philippe Corsaletti akimkabidhi tuzo/zawadi ya Begi na cheti mwanafuzi wa darasa la sita kutoka shule ya Msingi Bunge,Veronika Inocent baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika Kilele cha shindano la Uchoraji kwa ajili ya kuhamasisha usalama barabarani katika shule za msingi jijini Dar Es Salaam kwa mwaka 2016,hafla hiyo fupi iliyoandaliwa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania ilifanyika mapema leo katika viunga vya shue ya msingi Bunge.

Mashindano hayo yalihusisha shule kumi kwa upande wa Dar Es Salaam ambazo ni    Mwananyamala,Kisutu,Bunge,Kisiwani,Mchangani,Mnazini,Mwananyamala B,Mikocheni,Mtendeni,Kisutu,Kisiwani na Ugindoni,Shule nyingine tatu ni kutoa mkoa wa Geita ambazo zitashiriki na mchakato wa kuwapata washindi,matokeo ya washindi wa mwisho yatatangazwa wakati wa kilele cha cha wiki ya Usalama barabarani ambayo inatarajia kufanyika hivi karibuni 
Mwanafuzi wa darasa la sita kutoka shule ya Msingi Bunge,Veronika Inocent akilia kwa furaha mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika Kilele cha shindano la Uchoraji kwa ajili ya kuhamasisha usalama barabarani katika shule za msingi jijini Dar Es Salaam kwa mwaka 2016,hafla hiyo fupi iliyoandaliwa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania ilifanyika mapema leo katika viunga vya shue ya msingi Bunge.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Kamanda Mohamed Mpinga pamoja na Waandaji kutoka kampuni ya Puma Energy Tanzania na AMEND wakitafuta washindi watatu wa shindano la uchoraji katika masuala mazima ya kuhamasisha usalama barabarani 2016.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Kamanda Mohamed Mpinga akimkabidhi Mwanafunzi wa darasa la sita,Shaaban zawadi ya Begi na Cheti,kutoka shule ya msingi Bunge baada ya kuibuka mshindi wa tatu katika Kilele cha shindano la Uchoraji kwa ajili ya kuhamasisha usalama barabarani katika shule za msingi jijini Dar Es Salaam kwa mwaka 2016,hafla hiyo fupi iliyoandaliwa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania ilifanyika mapema leo katika viunga vya shue ya msingi Bunge.
Picha ya Pamoja na Washindi watatu shindano la Uchoraji kwa ajili ya kuhamasisha usalama barabarani katika shule za msingi jijini Dar Es Salaam kwa mwaka 2016.

Baadhi ya Wanafunzi walioshiriki na kuibuka na zawadi kutoka Kampuni ya Puma Energy Tanzania . 
Mkurugenzi Mkuu kutoka kampeni ya Puma Energy Tanzania Ltd,Philippe Corsaletti alisema kuwa shindano hilo linalenga kusaidia kuelimisha Wanafunzi wa shule za msingi katika masuala ya Usalama barabarani."Mpangp wetu wa usalama barabarani kwa mashule hapa Tanzania ulianza toka mwaka 2013 na mpaka sasa shule za msingi zipatazo 30 zimeshiriki,ikiwa ni jumla ya wanafunzi 38,638",alisema Philippe.Alisema kuwa shindano hilo pia linalenga kumpatia Mwanafunzi nafasi ya kushiriki mawazo


Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na Mkewe Mary wakimtazama mtoto Nchambi Peter aliyeungua moto  wakati walipotemblea hospitali ya wilaya ya Mpanda Agosti 21, 2016. Kulia ni Mam wa mtoto  huyo, Dotto Makengele. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkewe Mary  (kulia kwake)wakizungumza na wagonjwa wakati walipotembelea hospitali ya wilaya ya Mpanda wakiwa katika siku ya kwanza ya ziara ya mkoa w Katazi Agosti 21, 2016
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkewe Mary  (kulia kwake)wakizungumza na wagonjwa wakati walipotembelea hospitali ya wilaya ya Mpanda wakiwa katika siku ya kwanza ya ziara ya mkoa w Katazi Agosti 21, 2016
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkewe Mary  (kulia kwake)wakizungumza na wagonjwa wakati walipotembelea hospitali ya wilaya ya Mpanda wakiwa katika siku ya kwanza ya ziara ya mkoa w Katazi Agosti 21, 2016


Waziri Mkuu,Kassim Majlaiwa na mkewe Mary wakitazama watoto mapacha wa kiume waliozaliwa na  Bi Sikudhani Rashidi usiku wa kuamkia Agosti 21, 2016 katika hospitali ya wilaya ya Mpanda

 Askari wa Kikosi cha Uokoaji cha Zimamoto wakizima moto uliokuwa ukiteketeza ghala la Kampuni ya Boss Shopping Centre Ltd zilimo kuwa zikihifadhiwa bidhaa mbalimbali eneo la Viwanda Chang'ombe jijini Dar es Salaam leo mchana.
 wananchi wakijadiliana jambo eneo la tukio.
 Kazi ya uokoaji ikiendelea.

 Askari wa uokoaji wakiwa kazini.
 Mmoja wa wamiliki wa ghala hilo akisaini fomu  ya uzimaji wa moto huo.
 Moto ukiendelea kuwaka

Wananchi wakiwa eneo la tukio.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa mkutano na Watendaji wa Ofisi yake Idara ya Mazingira Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa mkutano na Watendaji wa Ofisi yake Idara ya Mazingira, kushoto ni Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na kulia ni Katibu Mkuu Oisi ya Makamu wa Rais Bw. Mbaraka Abduwakil Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Msaidizi Idra ya Mazingira Bi. Esther Makwaia akiwasilisha taarifa ya hali ya Mazingira nchini kwenye mkutano na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu, Ikulu jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa mkutano na Watendaji wa Ofisi yake Idara ya Mazingira mara baada ya kupata taarifa za maendeleo, mipango na mikakati ya Idara hiyo, kulia ni Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifafanua jambo kwenye mkutano wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Watendaji wa Idara ya Mazingira (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
                                                             .................................................

No comments :

Post a Comment