Friday, August 26, 2016

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA, YASIKITISHWA NA KAULI YA RD MAKONDA KUHUSU POLISI


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda


Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri akikabidhi cheti kwa mmoja wa mafundi Bw.Saidi Waziri kutoka Arusha wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.


Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri akikabidhi moja ya vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya karakana za TEMESA kwa Bw. Japhet Mwita mmoja wa washiriki wa mafunzo yaliyofanyika hivi karibuni katika hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.


Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri akionesha moja ya vifaa vilivyokabidhiwa na mafundi wa TEMESA kwa ajili ya karakana zao wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.

Kaimu Mtendaji TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan(kulia) akitoa neno kwa mafundi wa TEMESA wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016 kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri


NA THERESIA MWAMI TEMESA
Mafundi wa TEMESA wameshauriwa kutumia mafunzo waliyoyapata kuendana na mabadiliko ya teknolojia katika utengenezaji magari na vifaa vya umeme.
Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa Bodi ya Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi Wakala hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri amesema kuwa Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA imedhamiria na kuhakikisha kuwa magari na mitambo yote ya Serikali inatengenezwa kitaalam ili kuleta tija na thamani halisi ya fedha iliyokusudiwa pamoja na kukidhi kiu na matarajio ya wateja.
”Napenda kuwakumbusha kwamba mnayo dhamana kubwa ya kutengeneza magari ya Serikali hivyo kwa mafunzo mliyoyapata ninaamini mmejenga uwezo wa kutosha wa kuhudumia magari na vifaa vya umeme kwa kutumia mfumo wa kisasa” alisema Mhandisi Mashauri.
Ameongeza kuwa ni fursa pekee kwa mafundi waliopata mafunzo hayo kwenda kuwafundisha wenzao ambao hawakuweza kupata mafunzo hayo ili kuongeza kasi ya kutengenza magari na vifaa vya umeme na kupunguza changamoto zilizopo katika utengenezaji magari kwa kutumia mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Aidha Kaimu Mtendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan amewashukuru washirika wa TEMESA wakiwemo Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na kampuni ya Superdoll kwa kuwezesha kufanyika kwa mafunzo hayo ambayo yataleta chachu ya utendaji kazi wa mafundi na karakana za TEMESA zilizopo nchini nzima.
Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA kwa kushirikiana na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na kampuni ya Superdoll waliandaa mafunzo ya siku 14  yaliyoanza Agosti 9 na kumalizika Agosti 26, 2016 yaliyoshirikisha jumla ya mafundi 25 kutoka mikoa mbalimbali ili kuwapa uwezo wa kutengeneza magari kwa kutumia mifumo ya kisasa.



Baadhi wa mafundi wa Temesa kutoka mikoa mbalimbali nchini wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.
(PICHA ZOTE NA THERESIA MWAMI TEMESA)

 Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (katikati), akizungumza na wajumbe wa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wakati wa ziara yao ya kutembelea mradi wa Udart Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Max Malipo, ambayo imeingia ubia wa utendaji na Udart,  Mhandisi Juma Rajab, akizungumza na wajumbe hao katika ziara hiyo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (kulia), akiwapatia kadi za kupandia mabasi hayo wajumbe hao.
 Wajumbe wa kamati hiyo wakipita katika eneo la kukatia tiketi kwa kutumia gadi maalumu badala ya tiketi za kawaida.
 Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Anjelina Malembeka (kulia), akiteta jambo na  Esther Mahawe ndani ya basi la mwendo wa haraka Dar es Salaam leo, walipokuwa katika ziara ya kutembelea mradi wa Udart. Wengine nyumba kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza na Mariam Ditopile.
 Wajumbe hao wakiwa ndani ya basi hilo la kampuni ya Udart katika ziara hiyo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Udart, Lonadi Lwakatare akitoa ufafanuzi kwa wajumbe hao.
  Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (mwenye suti nyeusi mbele), akiwaongoza wajumbe hao katika ziara ya kutembelea makao makuu ya udart.
Mkuu wa Oparesheni wa Chumba cha kuangalia mienendo ya mabasi ya udart yakiwa barabarani, Mhandisi Mohamed Kuganda (kushoto), akitoa maelekezo mbele ya wajumbe wa kamati hiyo jinsi mfumo huo wa kuonesha mabasi hayo unavyofanyakazi.


Mkurugezi Msaidizi Lugha Bibi Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo akionesha cheti cha usajili wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) mara baada ya kuuzindua umoja huo huo katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.


Mkurugezi Msaidizi Lugha Bibi Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.


Rais wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) Bw. Hussein Tuwa akitoa neno wakati wa uzinduzi wa Umoja huo katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.


Katibu Mkuu wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) Ibrahim Gama akitoa maelezo kwa mgeni rasmi kuhusu Umoja wao wakati wa uzinduzi wa Umoja wa huo katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.


Mkurugezi Msaidizi Lugha Bibi Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamojja na viongozi na wajumbe wa kamati kuu ya Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) mara baada ya uzinduzi wa umoja huo katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.


Baadhi ya vitabu vya Riwaya vilivyoandikwa na wanachama wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI).

Baadhi ya watu waliohudhuria

No comments :

Post a Comment