Friday, August 26, 2016

MAJALIWA ASHIRKIKI MKUTANO WA APRM- NAIROBI




Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni  kabla ya kuanza kwa Mkutano wa African Peer  Review Mechanism Forum (APRM)kwenye ukumbi wa hoteli ya Intercontinental jijini Nairobi Agosti 26, 2016. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na ujumbe wake wakishiriki katika Mkutano wa African Peer  Review Mechanism Forum (APRM)kwenye ukumbi wa hoteli ya Intercontinental jijini Nairobi Agosti 26, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika maungumzo na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya (kulia), Rais wa Msumbiji,  Filipe Nyusi (wapili kulia) na Mwenyekiti  wa Umoja wa Afrika (AU), Madame Nkosazana Dlamini- Zuma kabla ya kuanza kwa Mkutano wa African Peer  Review Mechanism Forum (APRM) kwenye ukumbi wa hoteli ya Intercontinental jijini Nairobi Agosti 26, 2016

JESHI LA ZIMAMOTO HUFIKA KWENYE MATUKIO KWA WAKATI LICHA YA KUKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI

MANCHESTER UNITED KUKUTANA NA ROBIN VAN PERSIE LIGI YA UROPA

Timu ya Manchester United itakutana na mshambuliaji wake wa zamani Robin van Persie katika Kundi A la michuano ya Ligi ya Uropa.

Kikosi hicho cha Jose Mourinho kitakutana na mshambuliaji huyo Mdachi akiwa na Fenerbahce, pia kundi hilo zipo timu za Feyenoord na Zorya Luhansk ya Ukraine.

Kwa upande mwingine Southampton, imewekwa Kundi H, ikivaana na timu yenye fedha nyingi Inter Milan, Sparta Prague pamoja na Hapoel Be'er Sheva.



Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akizungumza na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa  la Misaada la Japan,(JICA) Bw. Hiruchi Kato  (kulia kwake) na ujumbe wake , jijini Nairobi Agosti 26, 2016 ambako  anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa sita Wa Tokyo International Conference o n Africa Development (TCAD). Kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Japan Mathias Chikawe. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yono Auction Mart & Co. Ltd, Scholastika Christian Kevela (kushoto), akiwaonesha waandishi wa habari Dar es Salaam leo (hawapo pichani), mkataba wa kimataifa walioingia na Kampuni ya Bidders Choice ya Afrika Kusini wa ushirikiano kwa ajili ya kufanya mnada wa mitambo ya kampuni ya uchimbaji ya Acacia inayomiliki mgodi wa dhahabu Bulynhulu uliopo mkoani Shinyanga. Kulia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Yono, Stanley Kevela.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Yono, Stanley Kevela (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yono Auction Mart & Co. Ltd, Scholastika Christian Kevela (kushoto), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. Kulia ni  Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Yono, Stanley Kevela. Nyuma kushoto ni Ofisa wa kampuni hiyo, Salome Sabas na kulia ni Abdrew Kevela. 
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Udalali ya Yono Auction Mart imeingia mkataba wa ushirikiano na Kampuni ya Bidders Choice ya  Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya mnada wa mitambo ya kampuni ya uchimbaji ya Acacia inayomiliki mgodi wa dhahabu Bulynhulu uliopo mkoani Shinyanga .

No comments :

Post a Comment