Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia),
akipata maelezo ya mfumo wa utabiri wa hali ya hewa katika Uwanja wa
Kimataifa wa Songwe (SIA) kutoka kwa Mtaalam wa masuala ya hali ya hewa
uwanjani hapo, Wakati alipokagua uwanja huo mkoani Mbeya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia),
akipata maelezo kutoka kwa Bw. Baraka Mwambipile kuhusu namna ndege
zinavyoongozwa wakati wa kuruka na kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa
Songwe, Wakati alipokagua uwanja huo mkoani Mbeya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata
ufafanuzi wa michoro ya ujenzi wa jengo la abiria kutoka kwa Mhandisi wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) wakati alipokagua Uwanja wa Ndege wa
Songwe, Mkoani Mbeya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA) kuhusu
ujenzi wa jengo la pili la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Songwe,
wakati alipokagua uwanja huo Mkoani Mbeya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili
kulia) akiendelea na ukaguzi wa jengo la pili la abiria katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Songwe, Mkoani Mbeya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiendelea na
ukaguzi wa wa Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Songwe , Mkoani Mbeya.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia)
akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa kampuni ya Shapriya Co Ltd
anayejenga jengo la pili la abiria wakati alipokagua uwanja wa kimataifa
wa Songwe, Mkoani Mbeya.
………………………………………………………………………………………………….
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa Serikali haitaendelea na
ujenzi wa jengo la pili la abiria katika uwanja wa ndege wa Songwe
uliopo mkoani Mbeya mpaka tume ya watalamu iliyoundwa kuchunguza ili
kujiridhisha kama utaratibu ulizingatiwa kabla ya kuaza ujenzi huo.
Prof. Mbarawa ametoa kauli
hiyo mara baada ya kukagua jengo hilo linalojengwa na mkandarasi wa
Kampuni ya Db Shapriya ya Tanzania ambapo amesema hadhi ya jengo hilo
hairidhishi hivyo ipo haja ya kujiridhisha kama taratibu zote zilifuatwa
kabla ya ujenzi.
Amebainisha kazi ya tume hiyo ya
wataalamu ni kuhakiki namna utaratibu wa kumpata mkandarasi
ulivyofanywa, gharama halisi za mradi na fedha iliyolipwa kwa mkandarasi
kama inaendana na thamani ya jengo hilo.
“Serikali haiwezi kutoa fedha ya
kumalizia jengo hili kabla ya kujiridhisha ili kuhakikisha fedha
tutakazozitoa zitatumika kulingana na ilivyopangwa na thamani ya fedha
inaendana na jengo lenyewe”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Aidha Waziri Prof. Mbarawa
ameeleza ili kuwa na miundombinu imara na ya kudumu ni lazima
kuhakikisha miradi ya ujenzi wa miundombinu inasimamiwa vizuri na
taratibu za kupata mkandarasi bora zinafuatwa.
“Kutokuwa na miundombinu isiyo
imara ni sababu ya wahusika kuweka mbele maslahi binafsi na siyo ya
Taifa”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa
Pia ameutaka uongozi wa Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuhakikisha makosa yaliyojitokezo
kwenye ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Mwanza
hayajirudii katika kiwanja hiki.
Kwa upande wake Meneja wa Uwanja
wa Ndege wa Songwe Bw. Hamisi Amiri amemhakikishia Waziri Mbarawa
kusimamia ujenzi uliobaki kwa kuzingatia taratibu na makubaliano
yaliyowekwa ili jengo hilo lidumu kwa manufaa ya Taifa na Mkoa.
Uwanja wa Songwe ni kiungo muhimu
kwa wananchi wa mikoa ya Katavi, Rukwa, Njombe na Ruvuma na katika
mwaka huu wa fedha umetengewa kiasi cha shilingi bilioni 10 kwa ajili ya
kumalizia ujenzi wa jengo la abiria na taa uwanjani hapo.
TIGO YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MASOMO YA SAYANSI KWA SEKONDARI YA CHATO
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Chato wakiwa katika picha pamoja na vifaa vya masomo ya sayansi vilivyotolewa na kamouni ya simu ya tigo |
Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari Chato wakifuatilia matukio wakati wa kupokea
vifaa vya masomo ya Sayansi (Fizikia,Baiolojia na Kemia) vyenye thamani
ya Sh 30 Milioni kutoka kampuni ya TigoMtaturu:Hakuna demokrasia yoyote duniani inayohubiri wananchi kutoshiriki shughuli za maendeleo
Na Mathias Canal, Singida
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mh.
Miraji Jumanne Mtaturu amsema hakuna demokrasia yoyote duniani
inayohubiri wananchi kutoshiriki shughuli za maendeleo hivyo mwananchi
anapaswa
kushirikishwa katika kuchagua viongozi wake, kukaa na viongozi wake kupanga miradi ya maendeleo kama vile kuchangia ujenzi wa shule, zahanati na maabara na maendeleo mengine.
Ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo kwa kutumia nguvu na akili katika kukamilisha na kumiliki miradi ya kijamii
ni njia mojawapo itakayowafanya wananchi kuwa na uchungu na mali pamoja na maendeleo katika jamii husika.
Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa kumekuwa na
matumizi mabaya ya demokrasia katika Wilaya hiyo hususani katika
shughuli za kijamii kama vile kuchangia ujenzi wa maabara jambo
lililopelekea Wilaya hiyo kuwa ya mwisho katika ujenzi wa maabara kwa
ajili ya shule za sekondari zilizopo katika Wilaya ya Ikungi.
“Wataalamu
wa Sayansi na viongozi mashuhuri wamewahi kusema Demokrasia bila
maendeleo sio demokrasia, Hayati Mwalimu julius Kambarage Nyerere na
Profesa Issa Shivji waliwahi kuandika kuwa demokrasia ya kweli ni ile
inayowasaidia wananchi kutoka katika hali moja kwenda kwenye hali
nyingine ambayo ni bora zaidi kuliko ile waliyo nayo, hivyo tukiongelea
kuwashirikisha wananchi katika mipango na mikakati ya kuondokana na
umasiki na si vinginevyo” Alisema Mtaturu
Dc Mtaturu amesema
kuwa kuwa mwenyekiti wa Kijiji kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM),
CHADEMA, ACT WAZALENDO, CUF au chama chochote hapaswi kuongoza wananchi
kwa matakwa yake binafsi bali ni lazima kufuata taratibu, kanuni, sheria
na taratibu zinazowaongoza katika kutekeleza majukumu yao.
Ameyasema hayo wakati wa kikao cha kazi kati ya Mkuu waWilaya Wakuu wa idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Weneyeviti wa Vijiji na
Watendaji wa Kata na Vijiji katika mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Amewaelekeza
wenyeviti wa Vijiji kuwa majukumu yao ni kuongoza vikao vya
Halmashauri ya Kijiji na kuongoza mkutano mkuu wa Kijiji sio kuuza ardhi
ya kijiji kiholela, Kumnyang’anya mtu ardhi au kupiga faini yoyote
wanayojisikia na ndio maana kunakuwa na watendaji wa Vijiji ambao ni
wataalamu hivyo wana majukumu muhimu katika kuwashauri wenyeviti wa
Vijiji.
Dc Mtaturu
pia amewataka viongozi hao kutambua kuwa uchaguzi ulimalizika Octoba
mwaka jana na chama kilichoshika dola ni Chama Cha Mapinduzi
(CCM) hivyo kutokana na uchaguzi huo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilipewa ridhaa ya kuongoza Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano 2015-2020 hivyo ilani inayotekelezwa na serikali ya awamu ya Tano ni ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo kwa vile kila kiongozi wa Kijiji yupo ndani ya serikali anapaswa kutelekeza ilani ya CCM kwani huo ni utaratibu wa vyama vinavyoshinda popote dunia.
Baadhi
ya watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Vijiji, na baadhi ya watendaji wa
Vijiji Wilayani Ikungi hawajawahi kupatiwa mafunzo ya
muongozo wa kiutendaji hali iliyopelekea baadhi yao kutotimiza wajibu wao na wengine kufanya kazi nje ya mipaka yao.
“ Kupitia kikao/mafunzo haya Uonevu wowote, kosa lolote, matumizi mabaya ya madaraka yatakayofanywa aidha na Mtendaji wa Kata,
Mwenyekiti wa Kijiji, Mtendaji wa Kijiji sitalifumbia macho nitakuchukulia hatua kwa mujibu wa sheria, kanuni, tulizowekeana kama serikali” Alisema Mtaturu
Sambama
na hayo Dc Mtaturu amewasihi viongozi hao kuwaunga mkono askari polisi
katika kuimarisha ulinzi na usalama kwani bila usalama na amani katika
jamii inayotuzunguka hakuwezi kuwa na maendeleo.
|
No comments :
Post a Comment