NA K-VIS MEDIA/MASHIRIKA YA HABARI
RAIS
wa Uganda Yoweri Museveni, (71), huenda akawa rais wa “maisha” wa nchi hiyo,
endapo kipengele cha katiba ya nchi hiyo kinachoweka ukomo wa umri wa mika 75
kutoruhusiwa kuwania Urais, utaondolewa na bunge.
Tayari
pilikapilika za kuondoa zuiohilo zimeanza ambapo kwa mujibu wa taarifa za
vyombovya habari zinasema, Maafisa wa chama tawalanchini humo wamepitisha
azimio la kuondoa ukomo wa umri kuwania Urais na hivyo Raios Museveni huenda akaweza
kuwania tena kiti hicho mwaka 2021 ambapo atatimiza miaka 75 ambayo inachupia
matakwa ya sasa ya Katibaya Uganda yanayozuia mtu mwenye umri huo kuwania
Urais.
Museveni ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka1986, ni
kiongozi mwenye umri mkubwa zaidi kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwa
sasa. Rais Museveni anajivunia kuifanya Ugandakuwa na amani tangu aingie
madarakani tofauti na watangulizi wake ambapo marais wan chi hiyo walipinduliwa
mara kwa mara.
Museveni pia aliingiamadarakani kwa kuipindua serikali.
Mkutano wa Chama tawala cha NRM wilayani Kyankwanzi umepitisha
azimio hiloa mbapo Mwenyekiti wake Bi. Anne Maria Nankabirwa amesema, viongozi
wa NRM huko Kyankwanzi wanataka ukomo wa umri uondolewe ili kuruhusu viongozi
wenye uwezo kama Museveni kuendelea na uongozi.
Ofiri ya Rais Museveni imethibitisha maamuzi hayo Jumanne
Agosti 2, 2016 katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Wakati wa mkutano huo uliofanyika Ikulu ndogoya Kyankwanzi,
viongozi hao wa NRM wa wilaya hiyo wamemwambia Rais Museveni kuwa wanataka
ukomo wa umri kuwania urais uondolewe kwenye katiba ya nchi hiyo.
Hata hivyo Museveni aliwaambia viongozi hao kuwa
atajadiliana na KamatiKuu ya chama cha NRM na uongozi wa NRM juu ya swala hilo.
Wachambuzi wa mambo wanasema, kama mabadiliko ya katiba
yakifanyika na kupitishwa, na Rais Museveni kuwania tenaurais wan chi hiyo na
kushinda mwaka 2021, atakuwa ametawala Uganda kwa kipindi cha miaka 40
No comments :
Post a Comment