Thursday, July 21, 2016

Ziara ya Rais wa Benki ya Exim kwenye kituo cha kuhifadhia kumbukumbu.

2 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kulia)   akizungumza kumshukuru Rais wa Benki ya Exim ya nchini China Bw, Liu Lian’ge (hayupo pichani) mara baada ya kukagua kituo mahiri cha kutunza kumbukumbu (Internet Data centre) kilichopo eneo la kijitonyama Dsm.
3 
Rais wa Benki ya Exim ya nchini China Bw, Liu Lian’ge (wa kwanza kushoto) akizungumza mara baada ya kukagua kituo mahiri cha kuhifadhia kumbukumbu ambacho kilijengwa kwa ufadhili wa Benki ya Exim ya nchini china.
4 
Rais wa   Banki ya Exim ya nchini China Bw, Liu Lian’ge  (wa pili kutoka kulia) akizungumza na  Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kulia) wakati wakikagua kituo mahiri cha kuhifadhi kumbukumbu (Internet Data centre) kilichopo eneo la kijitonyama Dsm.
5 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto)  akishuka ngazi wakati wa kukagua kituo mahiri cha kutunzia kumbukumbu (Internet Data centre) kilichopo eneo la kijitonyama,  (wa kwanza kulia) ni Rais wa Benki ya Exim ya nchini China Bw. Liu Lian’ge.

TAIFA STARS KAMBINI AGOSTI MOSI, 2016

mkwasaserena 
Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa Jumanne ya Julai 26, 2016 anatarajia kutangaza kikosi kwa ajili ya kambi ya awali ya wiki moja ikiwa ni maandalizi ya kucheza na Nigeria katika mchezo wa kukamilisha ratiba ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Mkwasa maarufu kama Masters amesema lengo la kambi hiyo itakayoanza Agosti mosi, 2016 ni kuwaweka sawa kisaikolojia wachezaji kabla ya kuita kambi nyingine rasmi wiki ya mwisho ya Agosti kujindaa na mchezo dhidi ya Super Eagles ya Nigeria unaotarajiwa kuchezwa Lagos Septemba 2, mwaka huu.
“Kikosi change kitakuwa na vijana wengi, mimi ni muumini mkubwa soka la vijana ambao baadhi niko nao na ambao nitawaita, lakini pia mara baada ya ligi kuanza, nitaangalia wengine kabla ya kuwa na program ya ratiba ijayo ya michuano mbalimbali ya kimataifa itakayotolewa na CAF na FIFA,” amesema Mkwasa.
Taifa Stars ilipangwa kundi G kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambazo zitafanyika Gabon, mwaka 2017. Timu nyingine katika kundi hilo ni Nigeria, Chad na Misri ambayo tayari imefuzu baada ya kukusanya pointi 10, Nigeria ina pointi mbili; Taifa Stars ina pointi moja wakati Chad ilijitoa katikati ya mashindano na kukatisha ndoto za Tanzania kucheza fainali hizo.

WATAALAM WA ARDHI WATAKIWA KUTOA SULUHISHO LA MIGOGORO YA ARDHI NCHINI.

01 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sayansi) Prof. Simon Msanjila Akizungumza kwa Niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Wanataaluma ya Usimamizi wa Ardhi Kanda ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam.
02 
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Idrissa Mshoro akizungumza na Mtandao wa Wanataaluma wa Vyuo Vikuu Vinavyotoa Mafunzo yahusuyo Usimamizi wa Ardhi Kanda ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam.
03 
Washiriki wa Mtandao wa Wanataaluma wa Vyuo Vikuu Vinavyotoa Mafunzo yahusuyo Usimamizi wa Ardhi Kanda ya Afrika Mashariki  kutoka nchi 9 za Bara la Afrika wakifuatilia Mkutano wa mtandao huo leo jijini Dar es salaam.
 Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.
……………………………………………………………………………………………..
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Serikali imewataka wataalam wa vyuo Vikuu vinavyotoa mafunzo ya Usimamizi wa Ardhi waitumie taaluma yao katika kutafuta suluhisho la migogoro ya Ardhi inayowakumba wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza kwa Niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Wanataaluma ya Usimamizi wa Ardhi Kanda ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sayansi) Prof. Simon Msanjila amesema kuwa wataalam hao wanalo jukumu la kufuatilia migogoro inayotokea nchini na kuhakikisha wanatoa ushauri wa kitaalam utakaotoa majibu ya utatuzi wa migogoro hiyo.

Serikali Kutenga bil. 15 kukuza ujuzi wa Vijana Nchini.

1 
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama akizungumza na wadau mbalimbali hawapo pichani wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
4 
Wadau kutoka wa uchumi kutoka taasisi mbalimbali nchini wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama hayupo pichani wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
2 
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama wa kwanza kulia akimkabidhi cheti cha pongezi kwa kuwa mdhamini wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji Mkurugenzi Mtendaji wa ARIS Bw. Sanjay Suchak wa kwanza kushoto wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
3 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wa kwanza kushoto akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt.Hamis Mwinyimvua wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
………………………………………………………………………………………………….
Na Ally Daud-Maelezo
Serikali imetenga shilingi bilioni 15 kwa ajili ya kukuza ujuzi kwa vijana ili kuwawezesha kujikimu kimaisha na kuchangia kuinua uchumi wa nchi.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na Walemavu Bi. Jenista Mhagama amesema kuwa Serikali imetenga fedha hizo ili kukuza ujuzi wa vijana katika sekta mbalimbali kwa madhumuni ya kuwakwamua vijana katika uchumi.
“Tunatambua vijana ni nguvu kazi ya Taifa na wana mchango mkubwa katika kuinua uchumi wan chi hapa tulipo mpaka kufika uchumi wa kati hivyo katika kila bajeti tutatenga bilioni 15 kuwawezesha vijana kiujuzi” alisema Bi. Mhagama.
Aidha Mhe. Jenista ameongeza kuwa Serikali imeanza kupitia na kurekebisha upya sheria itakayowawezesha  wafanya biashara kuweza kumiliki uchumi wa nchi ili kufikia malengo waliyojiwekea hadi kufikia 2020.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni inayojihusisha na maswala ya Bima (ARIS) Bw. Sanjay Suchak amesema kuwa anashukuru kuona serikali imeweka mkakati wa kupitia upya na kurekebisha sheria itakayowaruhusu wafanya biashara kumiliki uchumi kwani kwa hali hiyo itawezesha kundi hilo kushiriki katika masuala ya ujenzi wa uchumi wa nchi.
Naye Mwenyekiti wa Sekta binafsi Nchini (TPSF) Bw. Reginald Mengi amesema kuwa ipo haja ya  watanzania hususani wakulima washirikishwe kwenye semina mbalimbali za kukuza uchumi wa nchi kwani asilimia 60 ya watanzania ni wakulima.
Mkutano huo wa Mashauriano ya ushiriki wa Watanzania katika uwekezaji umeandaliwa na Baraza la Taifa la uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi(NEEC) kwa lengo la kujadili jinsi ya kutumia fursa na kuwezesha nchi kukua kiuchumi limeanza Julai 21 na kumalizika 22 Julai mwaka huu.

MAN UTD DORTMUND KUFUNGUA PAZIA LA MICHUANO YA ICC ITAKAYOONEKANA KUPITIA STARTIMES

  Na Dotto Mwaibale
 IKIWA chini ya kocha wake mpya Mreno, Jose Mourinho, Manchester United wanatarajia kushuka dimbani jijini Shanghai, China kuwakabili Borrusia Dortmund siku ya Ijumaa Julai 22, 2016 mechi itakayopigwa saa tisa za alasiri kwa saa za hapa nyumbani kupitia ving’amuzi vya StarTimes.
 
Akizungumzia juu ya habari hiyo njema kwa wapenda soka nchini Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amebainisha kuwa michuano hiyo itakuwa ni ya kusisimua kutokana na orodha ndefu ya timu kubwa zitakazoshiriki kama vile Real Madrid, Barcelona, Manchester United, Manchester City, Paris Saint-Germain, Juventus, Liverpool, Chelsea na Bayern Munich kwa uchache.
 
“Tunayofuraha kuwatangazia wateja wetu na watanzania kwa ujumla kuwa watapata fursa ya kutazama timu zao katika mechi za awali kabla ya kuanza kwa ligi kuu mbalimbali duniani kupitia ving’amuzi vya StarTimes pekee. Mechi zote za michuano ya ICC itaonekana moja kwa moja kupitia chaneli ya World Football inayopatikana katika kifurushi cha Mambo kwa malipo ya shilingi 12000/- tu kwa mwezi. Michezo yote itakuwa ni yenye msisimko mkubwa kwani timu zinazoshiriki ni kubwa, nyingi zikiwa ni mabingwa katika ligi kuu zao, zina wachezaji nyota na kikubwa zaidi zingine hazikuwahi kukutana kabla.” Alisema Bi. Hanif
 
“Hii ni fursa ya pekee kwa watanzania kwani tunafahamu ya kuwa ni wapenzi wakubwa wa mchezo huu na siku zote StarTimes tunajitahidi kuwapatia kile wanachokipenda. Hii ni mara ya pili tunaonyesha moja kwa moja michuano hii kwani mwaka jana tulifanya hivyo ambapo timu ya Real Madrid waliibuka mabingwa. Hivyo basi mashabiki watakuwa na shauku kubwa ya kujua ni timu gani itakayoibuka mabingwa au kama utarudi kwa Real Madrid,” alisema na kumalizia Bi. Hanif kuwa, “Ni wajibu wetu kuhakikisha wanafikiwa na matangazo ya vipindi vizuri na kusisimua kama hivi kwa ubora wa hali ya juu na gharama nafuu ambazo kila mtu atazimudu.”
 
Mchezo huo ni sehemu ya ufunguzi wa michuano ya kombe la mabingwa wa kimataifa almaarufu kama International Champions Cup au ICC itakayoanza kutimua vumbi Julai 22 na kumalizika Agosti 13, 2016 katika viwanja mbalimbali nchini Marekani, Ulaya, Australia na China.
 
Katika michuano hii wapenzi wa soka duniani watapat fursa kujionea kwa mara kwanza mechi ya watani wa jadi kutoka jiji la Manchester au unavyojulikana kama ‘Machester Derby’ miongoni mwa mashabiki wengi. Mechi hiyo itapigwa siku ya Jumatatu ya Julai 25 jijini Beijing, China.
 
Mchezo huo utanogeshwa si tu na ushindani baina ya wachezaji au mashabiki bali safari hii ni makocha waliopewa vibarua vya kunoa vikosi hivyo, Jose Mourinho wa Manchester United na Pep Guardiola wa Manchester City.
 
Ukiachana na mechi hiyo, pia macho ya mashabiki wengi yatakuwa yakisubiria kwa hamu kutazama mechi kali zitakazozikutanisha timu za, Real Madrid na  PSG,  Chelsea na Liverpool, Real Madrid na Chelsea, Bayern Munich na Real Madrid pamoja na Liverpool na Barcelona.
 
Kwa ujumla timu zitazoshiriki  michuano hii ni pamoja na Real Madrid, Barcelona, Manchester United, Manchester City, Paris Saint-Germain (PSG), Juventus, Liverpool, Chelsea, Bayern Munich, Liverpool, Tottenham Hotspurs, AC Millan, Inter Millan, Leicester City FC, Celtic FC, Atletico Madrid, Melbourne Victoria na South China.
 

SERIKALI YAANZISHA MPANGO MAALUM WA UPIMAJI WA ARDHI MAENEO YASIYOPIMWA JIJINI DAR ES SALAAM.

v 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Mozes Kusiluka akiwaeleza waandishi wa Habari kuhusu mpango wa Serikali wa kupima na kurasimisha maeneo yasiyopimwa katika jiji la Dar es salaam leo.
Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.
……………………………………………………………………………………………….
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeandaa mpango maalumu wa upimaji wa Ardhi na Urasimishaji wa maeneo yote yasiyopimwa katika jiji la Dar es salaam ambapo viwanja zaidi ya  laki tatu (300,000) vitapimwa na wamiliki wake kupewa Hati.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam kuhusu zoezi hilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Mozes Kusiluka amesema kuwa Serikali imeamua kuja na mpango huo kwa sababu ya ukubwa wa jiji hilo na wingi wa watu ulioambatana na ujenzi wa makazi holela.
“Katika mwaka wa fedha 2016/2017 tumepanga kuwa na mpango maalum wa jiji la Dar es salaam ambapo  wataalam wetu watakwenda, kuhakiki mipaka na kupima maeneo yote ambayo hayajapimwa na kutengeneza ramani zitakazoonyesha maeneo ya barabara na maeneo ya huduma nyingine kwa kushirikiana na wananchi husika.
Amesema kuwa baada ya zoezi la uhakiki Serikali itatoa hati za maeneo hayo na kusisitiza kuwa zoezi hilo litafanyika pia katika maeneo mengine ya miji mikubwa nchini yenye watu wengi ikiwemo jiji la Mwanza.
Dkt. Kusiluka amesisitiza kuwa urasimishaji utakuwa shirikishi kwa kuwahusisha watu wote wa maeneo yatakayopimwa na Serikali ambapo wananchi wenye nyumba watashirikiana na viongozi wa Serikali katika mitaa kupanga na kuimarisha mindombinu ya maeneo yao pamoja na kukubaliana maeneo ambayo barabara za mitaa zitapita, mitaro ya maji machafu, magari ya kupitishia huduma za dharula kama Zimamoto nay ale ya kubebea wagonjwa.
“Mpango wa urasimishaji ni Shirikishi, wataalam wa ardhi watakwenda kwenye maeneo yote yatakayopimwa hususan katika jiji la Dar es salaam na kukaa na wananchi wote,kupitia mipaka wakishirikiana na wananchi wote kwa uwazi ili zoezi hilo liwe na manufaa na tija kwa wananchi wote” Amesisitiza Dkt. Kusiluka.
Amesema kuwa licha ya kuwepo kwa sheria zinazoisimamia sekta ya Ardhi  nchini Tanzania bado sekta hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo migogoro ya Wakulima na wafugaji, migogoro ya kijinai ya mtu mm kuvunja nyumba au kuvamia eneo la mtu bila idhini, migogoro ya mipaka kati ya majirani na ile inayosababishwa na wananchi kutokujua sheria.
Mbali na sababu hizo amebainisha kuwa idadi ya watu na matumizi ya ardhi kwa shughuli mbalimbali imekuwa ikiongezeka wakati ardhi ikibakia ileile jambo linaloifanya sekta hiyo kuja na mikakati mbalimbali ya kukabiliana na changamoto hizo kupitia watalaam waliopo.
Amesema kuwa serikali imefanya mambo mbalimbali kuhakikisha kuwa inatatua kero za wakulima na wafugaji katika maeneo mbalimbali kwa kuwatumia wataalam wake kupima na kupanga maeneo ya vijiji mbalimbali, kutoa elimu pia kuajiri wataalam wa masuala ya Ardhi katika Halmashauri zote nchini.
Aidha amesisitiza kuwa Serikali imejipanga kupima maeneo yote ya ardhi nchini ambayo hayajapimwa kupitia mpango wa miaka 10.

MATUKIO KATIKA PICHA JIJINI DAR ES SALAAM

U4 
Dereva wa basi la mwendo kasi  akitii sheria za usalama barabarani kwa kusubiri watembea kwa miguu kuvuka katika alama za punda milia katika kituo cha Posta ya Zamani jijini Dar es Salaam.
U5 
Dereva wa daladala linalofanya safari zake kati ya Makumbusho na Posta akipakia abiria mahali ambapo hapana kituo na hivyo kuhatarisha usalama wa abiria na watumiaji wengine wa barabara hiyo kama alivyokutwa na mpiga picha katika makutano ya barabara ya azikiwe na Jamhuri jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG)

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA KUWAIT NA CONGO JIJINI DAR ES SALAAM

C1 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al Najem (kulia) masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Kuwait na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo.  Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni, kushoto ni Katibu Mkuu, Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.
C2 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini, Jean-Pierre Mutamba (kushoto) masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Kongo na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. 
C3 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akimsikiliza na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al Najem (kulia) wakati alipokuwa akizungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Kuwait na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo.  Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni, kushoto ni Katibu Mkuu, Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.
C4 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akimsikiliza Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini, Jean-Pierre Mutamba (kushoto) wakati alipokuwa akizungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Kongo na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.
C5 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kulia) akipokea zawadi ya Pambo kutoka kwa Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al Najem. Waziri Mwigulu alizungumza na Balozi huyo masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Kuwait na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo.  Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

KARIBU MJUMBE: MAKAMU WENYEVITI WA CCM BARA NA ZANZIBAR WAMKARIBISHA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM, RAIS DKT. MAGUFULI LEO

 Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais Dk. Ali Mohammed Shein, wakimuonyesha kiti cha kukaa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais Dk. John Magufuli, walipoingia ukumbini, kabla ya kuanza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, kilichoongozwa  na Mwenyekiti wa CCM, Dk Jakaya Kikwete,  katika ukumbi  wa Sekretarieti, katika jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo.Kamati kuu hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kupendekeza jina la Dkt Magufuli kuwa Mwenyekiti na baadae kuliwasilisha jina hilo kwenye Halmashauri kuu ya Taifa kwa ajili ya kupeleka kwenye mkutano.

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura afanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mziki Tanzania Bw.John Kitime kuhusu kuboresha tasnia ya Mziki nchini.

1 
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw.John Kitime akisaini kitabu cha wageni alipowasili ofisini kwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura kuwasilisha taarifa ya mapendekezo ya kuboresha tasnia ya Muziki hapa nchini leo Julai 21 Jijini Dar es Salaam.
2 
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura akizungumza na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw.John Kitime  mara baada ya  kupokea taarifa ya mapendekezo ya kuboresha tasnia ya Muziki hapa nchini leo Julai 21 Jijini Dar es Salaam.
5 
Afisa Utamaduni kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Habibu Msammy  akichangia mada wakati wa majadaliano kati ya  na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw.John Kitime  kuhusu maboresho ya tasnia ya Muziki hapa nchini leo Julai 21 Jijini Dar es Salaam.
index 
 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw.John Kitime akizungumza na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura ofisini kwa Naibu Waziri  wakati aki wasilisha taarifa ya mapendekezo ya kuboresha tasnia ya Muziki hapa nchini leo Julai 21 Jijini Dar es Salaam.
3 
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura akipokea  moja ya kazi ya muziki  wa dansi alizowahi kufanya Mzee Kitime baba wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw.John Kitime leo Julai 21 Jijini Dar es Salaam.
4 
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bw.John Kitime(kulia),  wa pili kushoto ni Afisa Utamaduni  kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Habibu Msammy  na kushoto katibu wa Naibu Waziri Bi. Anna Nkinda  leo Julai 21 Jijini Dar es Salaam.
( Picha zote na Shamimu Nyaki WHUSM)

KALA JEREMIAH, SUPER NYAMWELA KUPAMBA MSIMU MPYA WA JUKWAA LA SANAA LA BASATA

basata logo 
Wasanii Kala Jeremiah na Super Nyamwela wanatarajiwa kupamba msimu mpya wa programu ya Jukwaa la Sanaa ambayo imekuwa ikiendeshwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na chama cha waandishi wa habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) kwa miaka mitano sasa tangu mwaka 2011.
Msimu mpya wa Jukwaa la Sanaa unatazamiwa kuzinduliwa rasmi Jumatatu ya tarehe 25/07/2015 kwenye Ukumbi wa BASATA ulioko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam kuanzia saa saa 4:00 Asubuhi – 6:30 Mchana.
Wasanii hawa wanatarajiwa kuupamba uzinduzi huo kwa kutoa burudani mbalimbali sambamba na kuongea na wasanii wachanga katika kuwahamasisha na kuwajengea uwezo juu ya namna wanaweza kutumia fursa mbalimbali za mashindano ya kukuza vipaji katika kujijenga kisanaa.
BASATA linatambua kwamba kumekuwa na tatizo la wasanii katika kutambua na kuchangamkia fursa mbalimbali zilizoko katika sekta ya Sanaa hasa zile zilizomo kwenye mashindano mbalimbali ya kutafuta vipaji ambayo wasanii Kala Jeremiah na Super Nyamwela wamekuwa wakishiriki kikamilifu.
Ushiriki wa wasanii hawa katika kuwajengea hamasa na kuwapa changamoto wasanii wachanga utasadia katika kuwajengea uwezo wa kutumia fursa hizo.
Mbali na burudani na elimu hiyo, uzinduzi huu wa msimu wa mpya wa Jukwaa la Sanaa unaotarajiwa kuhudhuriwa na watu zaidi ya mia moja (100) utahusisha pia kongamano maalum ambalo litajikita katika kutoa elimu mbalimbali kuhusu sekta ya Sanaa kwa wadau watakaohudhuria.
Jukwaa la Sanaa ni programu iliyobuniwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa lengo la kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo sekta ya Sanaa lakini pia kusaidia waandishi wa habari kupata habari zihusuzo sekta ya Sanaa kutoka vyanzo mahsusi.
Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini
Imetolewa na Kitengo cha Habari
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)

“NAVY KENZO KUMSINDIKIZA MISS TANGA 2016”

NA, MWANDISHI WETU TANGA
MSANII wa Mziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania Navy Kenzo anatarajiwa kutumbuiza kwenye shindano la kumtafuta malkia wa Mkoa wa Tanga Miss Tanga 2016 litakalofanyika Julai 29 mwaka huu kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort.
Licha ya Navy Kenzo wasanii wengine ambao watasindikiza onyesho hilo kwa kutoa burudani ni kundi la mziki wa kizazi kipya mkoani Tanga,Wazenji Classic pamoja na Dances.
Akizungumza jana,Mratibu wa Onyesho hilo, alisema kuwa maandalizi ya kuelekea shindano hilo yanaendelea vizuri ambapo tayari warembo watakaoshiriki wameanza kuingia kambini .
Shindano hilo ambalo limeandaliwa na kituo cha Radio cha TK FM 88.5 kilichopo mjini Tanga kwa kushirikiana na Hotel ya Tanga Beach Resort wameelezea namna walivyo jipanga kuhakikisha onyesho hilo linakuwa na ushindani mkubwa kutokana na aina ya warembo waliopo .
  “Nisema tu tumejiandaa vizuri kuhakikisha shindano hilo linafanyika kwa umakini mkubwa ili kuwawezesha wadau wa tasnia ya urembo mkoani hapa kuweza kupata ladha halisi ya onyesho hilo kwani licha ya kuwaona warembo wakali wakini pia mzee wa kamatia chini atakuwepo kuwapagawisha
“Alisema.
Hata hivyo alisema kuwa mazoezi ya warembo watanaoshiriki onyesho hilo yanaendelea kwenye ukumbi wa New Hotel uliopo mjini hapa kuanzia saa kumi jioni.
Aidha alisema kuwa kabla ya kufanyika shindano hilo warembo hao watapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii mkoani hapa ikiwemo Mapango ya Amboni na Hifadhi ya Taifa ya Saadani.
Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

TAARIFA YA UTEUZI WA VIONGOZI KATIKA TAASISI ZA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

images 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dkt. ALI Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Dkt. Abdulhamid Y. Mzee, katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Juma Yakout Juma ametuliwa kuwa Naibu Katibu Msaidizi Baraza la Mapinduzi (Sera, Ufuatiliaji na Tathmini).
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti ameteuliwa Nd. Mwadini Makame Haji.
Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti Nd. Abdalla Issa Mgongo na Mkurugenzi wa Miundo ya Taasisi, Utumishi na Maslahi ya Watumishi Nd. Shaibu Ally Mwazema.
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Nd. Khalid Omar Abdalla na Katibu wa Tawala wa Wilaya ya Magharibi ‘A’ Nd. Mashaka Hassan Mwita.
Katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Nd. Issa Mlingoti Ally ameteuliwa kuwa Mratibu Mkuu wa Ofisi ya Uratibu wa Shughuli za SMZ, Dar es  salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti Nd. AMEIR Makame Ussi
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa shughuli za Serikali Nd. Khalid Bakari Amran, Mkurugenzi wa Idara ya sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa Nd. Riziki Daniel Yussuf na Ofisa Mdhamini wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Pemba Nd. Ali Salim Alim Matta.
Wizara ya Afya Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti Nd. Ramadhan Khamis Juma na Ofisa Mdhamini wa Wizara ya Afya  Pemba Nd. Ali Bakari Ali.
Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na UvuviMkurugenzi wa Umwagiliaji Maji Nd. Haji Hamid Saleh.
Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu na Utamaduni Dkt. Omar Abdalla Adam.
Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Nd. Abdalla A. Mwinyigogo na Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo Nd. Ramadhan Mussa Bakari.
Katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Nd. Omar Ali Omar Bhai ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi.
Wizara ya Ardhi, Mji, Nishati na Mazingira Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Nd. Tahir M. K. Abdalla na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Huduma za Maji na Nishati (ZURA) Nd. Hemed Salim Hemed.
WIZARA YA Biashara Viwanda na Masoko Mkurugenzi wa Mipango, sera na Utafiti Nd. Nana Mwanjisi.

RC MKOANI PWANI HANA GARI ALAZIMIKA KUTUMIA LA DC KISARAWE

index 
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKUU wa mkoa wa Pwani pamoja na katibu tawala wa mkoa huo hawana usafiri wa uhakika katika kutekeleza majukumu yao ya kazi hali ambayo inasababisha mkuu wa mkoa huo kutumia gari la mkuu wa wilaya ya Kisarawe ambae bado hajaripoti kazini.
Aidha baadhi ya wakuu wa wilaya magari yao ni mabovu ikiwemo gari la mkuu wa wilaya ya Kibaha huku maafisa tarafa 26 kati ya 27 waliopo mkoani hapo wanakabiliwa na tatizo la kukosa pikipiki wanazotumia kwenye kazi zao.
Akizungumzia changamoto zinazoikabili sekretarieti ya mkoa huo,mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo alisema analazimika kutumia gari la mkuu wa wilaya ya Kisarawe kwasasa.
Alielezea kuwa anatumia gari hiyo kutokana na mkuu huyo wa wilaya bado hajamwapisha kutokana na kutoa udhuru maalum na endapo mkuu huyo wa wilaya ataanza kazi yeye atakuwa hana gari la kutumia.
Mbali na hayo ,mhandisi Ndikilo alisema wanakabiliwa na changamoto nyingine ya uhaba wa fedha za matumizi ya kawaida (OC)ambapo uhaba huo unatokana na kushuka kwa ukomo wa bajeti  mwaka hadi mwaka hususan katika mwaka wa fedha 2015/2016 ulishuka kwa asilimia 40 ikilinganisha na ukomo wa fedha katika kipindi cha nyuma.
Alisema fedha pia za matumizi ya kawaida zinazopokelewa kila mwezi ni pungufu tofauti na kiasi cha fedha iliyopangwa hivyo kuathiri sekretarieti ya mkoa katika kutekeleza majukumu yake.
“Changamoto hii ni kubwa ambayo inasababisha kuzalisha changamoto nyingine ikiwemo madeni ya watumishi ambayo hadi sasa yamefikia mil.152”
“Watumishi hawapati stahiki zao kwa wakati na mazingira ya kazi yakikabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo watumishi wengine wanaamua kuhama na kwenda kufanya kazi kwingine ambapo wanafikiri wataweza kutumiwa vizuri na kupata maslahi mazuri”alisema mhandisi Ndikilo.
Akizungumzia juu ya upungufu wa vitendea kazi alisema pikipiki kwa maafisa tarafa ni tatizo jingine ambalo linahitaji kushughulikiwa.
Mhandisi Ndikilo alieleza ni tarafa moja ya Kaskazini Mafia iliyo nzima kati ya maafisa tarafa 27 waliopo mkoani Pwani.
Alisema kuwa maafisa tarafa hao ni mkono wa kulia wa wakurugenzi na wakuu wa wilaya ndio wanaochapa kazi katika pande hizo lakini hawana usafiri wa uhakika.
Alisema sekretarieti ya mkoa ,wataalamu na maafisa tarafa hushindwa kutembelea mamlaka za serikali za mtaa na maeneo mbalimbali kwa lengo la kufuatilia miradi  na shughuli zinazopaswa kufuatilia na hata wakitembelea inakuwa sio kwa kiwango kinachotakiwa .
Mhandisi Ndikilo alisema zipo hatua wanazozichukua ikiwa ni sanjali na kufikisha changamoto hizo katika wizara na idara husika ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi.
Hatua nyingine ni madeni ya watumishi kufikishwa hazina ili yaweze kulipwa licha pamoja na kuwasilisha taarifa hizo lakini hazina bado haijalipa kwa wakati.
Hata hivyo Mhandisi Ndikilo alielezea kwamba baadhi ya maafisa tarafa hawana ofisi za kudumu wanalazimika kutumia ofisi ambazo hazina hadhi huku kukiwa hakuna huduma muhimu za maji na umeme.
Mkuu huyo wa mkoa alisema ofisi ya mkoa imeshajenga ofisi 6 kati ya 27 zinazohitaji kwa maafisa tarafa hao.
Mhandisi Ndikilo aliiomba ofisi ya rais ,utumishi wa umma kuangalia kwa ukaribu matatizo hayo ili kuyatafutia ufumbuzi kwani ni moja ya sababu zinazokwamisha utekelezaji wa ufuatiliaji na jitihada za kuinua maendeleo ya mkoa kwa haraka.

MWENYEKITI WA CCM DK. JAKAYA KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU DODOMA LEO

1 
Rais Dk. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Mh. Dk. Jakaya Kikwete wakati akifungua kikao cha Kamati Kuu ya ya Halmashauri kuu ya  CCM kilichofanyika leo Makao Mkuu ya CCM Dodoma kupendekeza jina la Mwenyekiti mpya wa CCM ambapo jina hilo litapelekwa kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa kwa ajili kupelekwa kwenye mkutano mkuu   na kuthibitishwa katika Mkutano Mkuu maalum wa CCM unaotarajiwa kufanyika Julai 23 mwaka huu mjini Dodoma, Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.
2Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Mh. Dk. Jakaya Kikwete  akifungua kikao cha Kamati Kuu ya ya Halmashauri kuu ya  CCM kilichofanyika leo Makao Mkuu ya CCM Dodoma Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula na katikati ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurrahman Kinana.
3Rais Dk John Pombe Magufuli kushoto pamoja na Mwenyekiti wa CCM Dk Jakaya Kikwete na viongozi wengine wakiimba wimbo maalum wa CCM wakati mkutano huo uliofanyika leo Makao Mkuu ya CCM Dodoma
4
Mjumbe wa Kamati Kuu Ndugu William Lukuvi akizungumza na wajumbe wenzake Adam Kimbisa kushoto na Nape Nnauye Katibu Mwenezi wa CCM Taifa.
5
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM  Adam Kimbisa akuzungumza na wajumbe wenzake kutoka kushoto ni Nape Nnauye Katibu Mwenyezi wa CCM Taifa, Mama Zakia Megji , William  Lukuvi na Mohamed Seif Khatib.
6
Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa akisalimiana na Wajumbe wa kamati kuu wakati alipowasili kuhudhuria katika mkutano huo.
7
Wajumbe wa Kamati Kuu Mzee Steven Wasira kulia na Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka wakifurahia jambo kabla ya mkutano huo kuanza.
8 
Mjumbe wa Kamati kuu kutoka Zanzibar Sadifa Juma Khamis akizungumza na mjumbe mwenzake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Ndugu Abdallah Bulembo kutoka kulia ni Jerry Silaa na Hussein Mwinyi.

Kupinga utumikishwaji wa watoto si jukumu la serikali pekee

a2 
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Dkt. Abdallah Possi akionyesha Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Utumikishwaji wa Watoto Tanzania wa Mwaka 2014. Uzinduzi huu umefanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango.
………………………………………………………………………………………..
Benjamin Sawe-Maelezo.
Utumikishwaji wa watoto umekuwa ni tatizo kubwa duniani ambapo kutokana na tawkimu za makadirio za mwaka 2000-2012 za Shirika la Kazi Duniani asilimia 11 (watoto milioni 264) ya watoto wote duniani wenye umri wa miaka 5-17 wnatumikisahwa kwenye ajira za aina mbalimbali sawa na asilimia 11 ya watoto wenye umri huo.
Kwa upande wa Tanzania, utumikishwaji wa watoto kwa mwaka 2014/15 matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kati ya watoto milioni 15 wenye umri kati ya miaka 5 hadi 17 (watoto milioni 4.2) sawa na asilimia 28.8 wanatumikishwa katika kazi mbalimbali
Takwimu hizo zinaonesha kuwa sekta za kilimo na uvuvi zimeendelea kuwa sekta zinazoajiri watoto wengi zaidi ikiwa ni kiwango cha asilimia 92.1 ya watoto wote wanaojihusisha na shughuli za kiuchumi na wengi wao wanaishi vijijini.
Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti ya matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa watoto Tanzania Bara wa mwaka 2014, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa anasema matokeo ya utafiti huo yanaonesha kuwa watoto hutumia zaidi ya nusu ya muda wao wa siku ikiwa ni asilimia 58.8 kwa shughuli za kujihudumia na usafi huku wasichana wakionekana kutumia muda mrefu zaidi kwa shughuli hizo kwa kiwango cha asilimia 58.3.

WHO YATOA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI KWA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM.

1 
Mratibu wa Mradi wa Usalama Barabarani kutoka Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO), Marry Kessy.
2 
Mratibu wa Mradi wa Usalama Barabarani kutoka Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) , Marry Kessy akitoa elimu kwa waandishi wa habari kuhusu usalama barabarani jijini Dar es Salaam, ambapo waandishi wa habari walipata  kujifunza mambo yanayohusu usalama wa barabarani ikiwepo kupewa ripoti ya ajali ambazo hutokea duniani na Tanzania, umuhimu wa uvaaji kinga (helment), umuhimu wa uvaaji mkanda kwenye gari, madhara ya ulevi uendeshapo chombo cha moto na vizuizi kwa watoto.
???????????????????????????????????? Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani wa Jeshi la Polisi, ASP Masoko akitoa mada kuhusiana na sheria ya usalama barabarani ya Tanzania inavyofanya kazi, wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
4 
Mkufunzi wa Usalama wa Barabarani waShirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) , Callie Long akitoa elimu kwa waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya siku moja jijini Dar es Salaam.
5 6 7 8 Waandishi wa habari mbalimbali waliohudhuria mafunzo ya usalama barabarani ya siku moja jijini Dar es Salaam ambapo walipata  kujifunza mambo yanayohusu usalama wa barabarani ikiwepo kupewa ripoti ya ajali ambazo hutokea duniani na Tanzania, umuhimu wa uvaaji kinga (helment), umuhimu wa uvaaji mkanda kwenye gari  uendeshaji vyombo vya moto na vizuizi kwa watoto
(PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG)

NGOMA AFRICA BAND KUTUMBUIZA JUMAMOSI 23 JULAI 2016 TUBINGEN ,UJERUMANI

1 2 3Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band yenye makao yake kule Ujerumani,wanatarajiwa kutingisha jukwaa katika maonyesho International Afrika Festival Tubingen litakalo fanyika jumamosi hii 16 Julai 2016 katika viwanja vya Fest platz Tubingen ,Ujerumani ya kusini ambapo wapenzi wa muziki watapata burani ya aina yake kutoka kwa bendi hiyo iliyofanikiwa kuwanasa washabiki kila kona duniani,kikosi cha Ngoma Africa band kinachoongozwa na mkuu wake mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda ras Makunja mkuu wa viumbe wa ajabu Anunnaki Aliens kinadumu katika gemu la muziki kwa takribani miaka 23 sasa na kuwekwa katika rekodi ya kimataifa kuwa ndio bendi ya kiafrika inayodumu kwa muda mrefu barani ulaya.
usikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com

UJUMBE WA HUAWEI WAKUTANA NA RAIS DK.SHEIN

index 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Huawei Bw.Bruce Zhang wakati alipofika Ikulu na ujumbe wake leo kwa mazungumzo,
indexb 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Huawei Bw.Bruce Zhang wakati alipofika Ikulu na ujumbe wake leo kwa mazungumzo,
[Picha na Ikulu.] 20/07/2016.

MAKAMU WA RAIS ATUNUKU SHAHADA NA STASHAHADA KATIKA MAHAFALI YA NNE YA CHUO CHA ULINZI WA TAIFA

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye Mahafali ya Chuo Cha Taifa cha
Ulinzi ambapo wahitimu 38 walitunukiwa Stashahada na Shahada ya Usalama na Stratejia.
 
Mahafali ya Nne ya Chuo cha Taifa  cha Ulinzi ya kutunuku Stashahada na Shahada ya Uzamili kwa wahitimu 38.
Wahitimu 17 wamefuzu katika kozi ya Stashahada ya Usalama na stratejia na wahitimu 22 wamefuzu kwenye Shahada  ya uzamili ya usalama na statejia ambapo wahitimu kutoka nchi za Botswana ,Burundi, Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, South Africa, Zambia, Zimbabwe na China .
Mheshimiwa Makamu wa Rais amewatunuku Shahada wahitimu wote na wale waliofanya vizuri kwenye kozi zao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu wa Chuo Cha Taifa cha
Ulinzi ambapo wahitimu 38 walitunukiwa Stashahada na Shahada ya usalama na stratejia.Makamu wa Rais alimuwakilisha Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika mahafali hayo.

WAZIRI MKUU ATAKA CDA ITENGE ENEO LA BANDARI KAVU

g1 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibonyeza king’ola kuashiria  uwekaji jiwe la msingi la Mradi wa  Ukarabati na Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Dodoma Julai 302016. Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi,  Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Jordan  Lugimbana. Kushoto ni Meya wa manispaa ya Dodoma, Jafari Mwanyembwa na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa.
g2 
Waziri Mkuu,Kassim Majliwa akikagua upanizi na ukarabati wa uwanja wa ndege  wa Dodoma kabla ya kuweka jiwe la msingi mjini Dodoma Julai 20, 2016.
g3 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuweka jiwe la misngi la upanuzi  na ukarabati wa uwanja wa ndege wa Dodoma mjini Dodoma Julai 20, 2016.
g4 g5 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi walioshiriki katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la upanuzi na ukarabati wa uwanja wa ndege wa Dodoma Julai 20, 2016.  Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na kushoto  kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Lugimbana.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………………………
Aweka jiwe la msingi upanuzi wa uwanja wa ndege wa Dodoma
Asema ahadi ya kujenga uwanja wa kimataifa Msalato iko pale pale
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa mkoa wa Dodoma pamoja na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) kutenga eneo la bandari kavu ili mkoa huo uweze kupokea na kuhifadhi mizigo na kurahisisha biashara kwa mikoa jirani.
Ametoa agizo hilo leo jioni (Jumatano, Julai 20, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma mara baada ya kuweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa awamu ya kwanza ya ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Dodoma.
“Ninazo taarifa kiwa Benki ya Dunia kupitia shirika la Local Investment Climate (LIC) tayari wametenga fedha kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya kujenga bandari kavu na tayari fedha hizo zimeshapokelewa na Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kazi hiyo.”

UDOM WASHIRIKI MAONESHO YA VYUO VIKUU KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE

Mhadhiri Msaidizi kutoka chuo kikuu cha Dodoma, Lucian Ngeze akitoa ufafanuzi kuhusu kutenga matumizi ya LUKU ya nyumba moja kadili ya matumizi ya kila mtu.
Mhadhiri kutoka collage ya Education chuo kikuu cha Dodoma, Dk. Pambasi Tandika akimsikiliza mwanafunzi baada ya kumweleza jinsi ya kujiunga chuoni hapo wakati wa maonesho ya vyuo vikuu yaliyoshirikisha vyuo mbalimbali hapa nchini.
 
CHUO kikuu cha Dodoma chashiriki Maonesho ya Vyuo vikuu hapa nchini yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, ambayo yatafanyika kwa kwa takribani siku tatu kuanzia leo Julai 20 hadi Julai 22 mwaka huu.
Katika maenesho hayo Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ametembelea mabanda mbalimbali katika maonesho hayo ya Vyuo Vikuu(TCU)
Mhadhiri Msaidizi kutoka collage ya CIVE chuo kikuu cha Dodoma, Ms Tulibako Tulibonywa akitoa ufafanuzi mbele ya vijana waliotembelea kwenye banda la chuo hicho leo
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Kadaso Kipingili(Mwenye Tshart Nyeupe) akitoa ufafanuzi kuhusu maelezo kwa wananchi waliofika katika banda la chuo kikuu cha Dodoma leo wakati wa maonesho ya Vyuo vikuu yaliyoandaliwa na TCU.
Baadi ya wanafunzi wakisoma majarida kutoka chuo kikuu cha Dodoma leo katika maonesho ya
Afisa Tawala, Idara ya Utafiti na Machapisho kutoka chuo kikuu cha Dodoma kiwaonesha vijana jinsi ya kujiunga pamoja na kuwaeleza vigezo vya kujiunga na Chuo hicho.
Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma, Teng Peng akiwaonesha baadi ya vijana waliofika kwenye banda la Udom Comfusious
Baadhi ya mitambo iliyotengenezwa na wanachuo wa chuo kikuu chaDodoma ambayo inaweza kuongoza magari kwa kutumia umeme wa nguvu ya Jua.

UTUMIKISHWAJI WA WATOTO BADO NI TATIZO NCHINI

a1 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo ya utangulizi kuhusu Utafiti wa Utumikishwaji wa Watoto Tanzania wa Mwaka 2014 katika uzinduzi wa matokeo hayo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango.
a3Mwakilishi wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania, Azfar Khan akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Utumikishwaji wa Watoto Tanzania wa Mwaka 2014.
a2 
 Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Dkt. Abdallah Possi akionyesha Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Utumikishwaji wa Watoto Tanzania wa Mwaka 2014. Uzinduzi huu umefanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL GHULA)
……………………………………………………………………………………….
Na: Veronica Kazimoto
UTUMIKISHWAJI wa Watoto bado ni tatizo kubwa nchini ambapo kati ya watoto watatu wenye umri wa miaka 5 – 17, mtoto mmoja anafanya kazi ambazo ni hatarishi katika maisha yake kiafya, kimwili na kisaikolojia.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Dkt. Abdallah Possi wakati wa uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Utumikishwaji wa Watoto Tanzania wa Mwaka 2014 uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam.
Matokeo ya Utafiti huo yameonyesha kuwa, kati ya watoto milioni 15 wenye umri kati ya miaka 5 – 17, watoto milioni 4.2 sawa na asilimia 28.8 wanatumikishwa katika kazi mbalimbali za kiuchumi.
Matokeo haya yameonesha kuwa hali ya utumikishwaji wa watoto umepungua kutoka asilimia 31.1 kwa mwaka 2006 hadi asilimia 28.8 kwa mwaka 2014.
“Kutokana na matokeo ya utafiti huu, ni dhahiri kwamba, utumikishwaji wa watoto bado ni tatizo kubwa nchini na duniani kwa ujumla. Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Kazi Duniani (ILO), asilimia 11 ya watoto wote duniani sawa na watoto milioni 264 wenye umri wa miaka 5 – 17 wanatumikishwa kwenye ajira za aina mbalimbali,” amesema Dkt. Possi.
Dkt. Possi amesisitiza kuwa ni wajibu wa jamii kuwekeza katika elimu kwa watoto kwa ajili ya kupunguza tatizo la utumikishwaji wa watoto ambao unakwenda kinyume na haki zao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema utafiti huu umebainisha kuwa, watoto wanafanya kazi zaidi katika sekta za Kilimo, Misitu na Uvuvi ambazo zinaajiri asilimia 92.1 ya watoto wote wanaojishughulisha na shughuli za kiuchumi.
Dkt. Chuwa ameongeza kuwa watoto hutumia zaidi ya nusu ya muda wao sawa na asilimia 58.8 kwa siku nzima kujihudumia na kufanya usafi binafsi ambapo wasichana wameonekana kutumia asilimia 59.2 na wavulana hutumia asilimia 58.3 kujihudumia.
Aidha, shughuli za kujisomea kwa watoto ni asilimia 15.5 ambapo wavulana wanatumia muda mrefu zaidi kujisomea kwa asilimia 16.4 na wasichana hutumia asilimia 14.6 kujisomea.
Utafiti huu umebainisha viashiria vya hali ya watoto wanaofanya kazi za kiuchumi na zisizo za kiuchumi, hali ya utumikishwaji wa watoto pamoja na athari mbalimbali ambazo watoto wanapata kwa kujihusisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Matokeo yameonesha pia, utumikishwaji ni mkubwa kwa watoto wasiosoma ikilinganishwa na watoto wanaosoma. Aidha, matokeo yameonesha utumishwaji ni mkubwa katika maeneo ya vijijini ikilinganishwa na maeneo ya mjini.
Utafiti huu wa Utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014 ni wa tatu kufanyika nchini ambapo utafiti wa kwanza ulifanyika mwaka 2001 na wa pili ulifanyika mwaka 2006. 

Tanzania yapewa tuzo za ustawi wa jamii na ushirikishaji wa wanawake katika mkutano wa AU

image.php 
Na. Immaculate Makilika – MAELEZO
………………………………………………
Serikali ya Tanzania imepewa tuzo 2 za masuala ya Ustawi wa Jamii  pamoja na ushirikishwaji wa wanawake katika ngazi ya maamuzi ya Serikali na Taasisi mbalimbali katika Mkutano wa 27 wa Umoja  wa Nchi za Afrika (AU) uliofanyika hivi karibuni Kigali nchini Rwanda.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi, Augustine Mahiga, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo yaliyojadiliwa katika mkutano wa 27 wa Umoja wa nchi za Afrika uliofanyika hivi karibuni Kigali nchini Rwanda.
“Tanzania imetambuliwa na AU kama nchi ambayo kwa miaka 15 sasa  imekua na mikakati mbalimbali  ya kitaifa ya kuzingatia haki za wanawake na kutimiza malengo ya Milenia,”  alisema Balozi Mahiga
Aliongeza kuwa Tanzania ni kati ya nchi tano bora katika bara la Afrika ambazo zimepewa tuzo hizo.
Katika hatua nyingine, Balozi Mahiga amasema kuwa katika mkutano huo wa 27 viongozi wa Afrika walizungumzia mambo mbalimbali ikiwemo  hati ya kusafiria Afrika (passport), ambayo itawezesha watu wa bara hilo kusafiri katika nchi zote za Afrika.
Balozi Mahiga aliongeza kuwa, lengo la kuanza kutumia hati hiyo ya kusafiria kwa nchi za Afrika ni kutoa vikwazo vilivyokuwepo wakati wa kutembelea na kusafiri ndani ya nchi hizo.
Aidha, Balozi Maiga amesema kwamba, kutolewa kwa hati ya kusafiria ya Afrika ni ishara ya Umoja na mshikamano, hati hizo zimeanza kutolewa kwa marais na viongozi wa Serikali wa nchi ambazo zilihudhuria mkutano huo. Hati hizo zitatumika kwa kuzingatia sheria za kila nchi.
Hali kadhalika, mkutano huo ulijadili migogoro ya nchi za Burundi na Sudani Kusini ambapo viongozi hao walikubaliana kupeleka Jeshi la Umoja wa Afrika nchini Sudani Kusini ili kutenganisha majeshi ya pande mbili zinazoendelea kupigana nchini humo.
Aidha, mgogoro wa Burundi bado unaendelea kupatiwa ufumbuzi kutokana na jitihada mbalimbali zinazoendelea kufanywa na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, ambaye aliteuliwa na mapema mwaka huu na viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkutano wa 27 wa Umoja wa nchi za Afrika wenye wanachama 54 ulifanyika Kigali nchini Rwanda tarehe 18 mwezi huu, ukiwa ni mkutano wa pili kwa mwaka huu ulikua na kauli mbiu inayosema mwaka wa haki za binadamu.

ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Angeline Mabula mkoani Tanga

1 
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula wakati akikagua nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Wilayani Mkinga wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Yona Maki (mwenye tai) na Meneja NHC Tanga Issaya Mshamba.
2 3 
Baadhi ya Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Wilayani Mkinga ambazo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula ameamuru watumishi wa wilaya hiyo waamie ifikapo tarehe 1 Agosti 2016.
4 
Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akiteta jambo na mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe (mwenye tai nyekundu) mara baada ya kujadili changamoto za ardhi katika wilaya hiyo.
5 
Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akiongea na wananchi wa Hale wilayani Korogwe mkoani Tanga na kutolea ufumbuzi migogoro ya Ardhi inayowakabili.
6 
Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akiongea na watumishi wa halmashauri ya manispaa ya Tanga.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO WIZARA YA ARDHI.
…………………………………………………………………..
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula ametoa Siku kumi na mbili kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga kuhama Tanga Mjini na kuhamia Wilayani Mkinga mahali zilipo nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizojengwa kwa ajili yao.
Naibu Waziri Mabula ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake wilayani Mkinga ambapo pamoja na mambo mengine alipata nafasi ya kutembelea eneo zilipojengwa nyumba hizo na kumuagiza Meneja wa NHC mkoa wa Tanga kuhakikisha tarehe 1 mwezi wa Agosti 2016 watumishi hao wanahamia katika nyumba hizo.
kwa sasa watumishi hao wamekuwa wakiishi Tanga mjini na kufanya kazi wilayani mkinga, hali inayowalazimu kusafiri zaidi ya kilometa 50 kilasiku kwenda na kurudi.
Mheshimiwa Mabula yupo katika ziara ya siku nne mkoani Tanga ambapo anatembelea Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya za Tanga mjini, Korogwe pamoja na kuzindua baraza jipya la Wilaya ya Kilindi. Hata hivyo mbali na mabaraza ya Ardhi mheshimiwa Naibu Waziri anatembelea miradi ya NHC pamoja na kutatua kero za migogoro ya Ardhi na changamoto za watumishi wa sekta za Ardhi mkoani Tanga.

UZINDUZI NA MAKABIDHIANO YA VIFAA VYA USAFI KWA MACHINGA JIJINI MWANZA WAGUBIKWA NA DOSARI YA UBADHIRIFU.

Mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa Machinga mkoani Mwanza-SHIUMA, Matondo Masanja, akizungumza hii leo katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) vyenye thamani ya Shilingi Laki Sita, kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi. Hafla hiyo imeambatana na Kauli Mbiu isemayo “Machinga Kukaa Katika Mazingira Safi Inawezekana, Tusonge Mbele Kwa Usafi”.
Na BMG

MKUU WA WILAYA YA LINDI AHAIDI KUSIMAMIA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI LINDI HADI KUKAMILIKA:

imagesNa: Mwandishi Wetu.
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mheshimiwa Shaibu Issa Ndemanga, leo ametembelea katika Shule ya Sekondari ya Lindi iliyopo katika manispaa ya lindi mjini kwa lengo la kuanza ujenzi wa shule hiyo ikiwa ni agizo la Waziri mkuu Kassimu Majaliwa ambaye aliitembelea shule hiyo ivi karibuni baada ya kuungua Moto na kuteketeza zaidi ya madarasa 8 katika shule hiyo.
Mkuu huyo wa Wilaya ambaye ameanza utendaji wake kwa kasi ikiendana na Kasi ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa jamhuri ya Muungano John Pombe Magufuli, aliitembelea shule hiyo kwa lengo la kuangalia changamoto zilizopo ikiwa ni pamoja na kujadili suala la Ujenzi wa barabara itakayotumika kwa ajili ya kuhakikisha vifaa vya ujenzi wa shule vinafika kwa usalama katika eneo hilo la madarasa wakati huu ambapo ujenzi unatarajiwa kuanza mara moja.
Akizungumzia ujenzi wa shule hiyo Mkuu huyo wa  Wilaya ya Lindi  Mjini alisema kuwa analazimika kufuatilia suala hilo lifanyike kwa haraka kutokana na kuwa agizo lililotolewa na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa alipotembelea shule hiyo wakati wa uchangiaji wa harambee kwa alengo la kufanikisha ujenzi huo kupitia wadau mbalimbali waliochangia Ujenzi wa Shule hiyo.
“Siyo jambo la taratibu hili, maana ni maagizo ambayo yametolewa na Mheshimiwa Waziri Mkuu kwamba ufanyike kwa haraka iwezekanavyo, kwa hiyo mimi nafuatilia kutimiza Kauli ya Waziri Mkuu ambaye alisimamia uhamasishwaji wa uchangiaji wa ujenzi wa majengo ya Shule yalioungua kwa Moto, na kama unavyoona mwenyewe tayari wadau wameendelea na zoezi la kutoa kile walichosema watatoa, na hapa leo nakagua kwanza Sehemu ya Barabara ambayo itajengwa kwa dharura ili kufikisha Vifaa eneo la Ujenzi lakini si hivyo tu hapa kuna changamoto nyingi ambazo zinatakiwa kufanyiwa ufumbuzi ikiwa ni pamoja na kupata mchoro wa jingo ambao unatakiwa uandaliwe kwa haraka na siyo vinginevyo, pili ni kwa hawa wajenzi ambao wanatakiwa kubuni barabara mbadala ambayo pamoja na kwamba itatumika kwa ujenzi huu lakini pia iwe ni barabara ambayo itakuwa ya kudumu kwa lengo la kuja kusaidia wakati mwingine kama itatokea tatizo kama hili, kitu kingine ni jinsi ambavyo wajenzi wanatakiwa kubuni mchoro wenye kiwango kwa ajli ya kuendana na dunia ya sasa, siyo tu bora mchoro, wahakikishe mchoro huo unakuwa kivutio na jingo lenyewe liwe ni jingo linalokidhi mahitaji kwa ajili ya shule hii, pamoja na kwamba changamoto ni nyingi lakini pia nimefika hapa kuangalia kile ambacho tayari kimepatikana na wapi kimehifadhiwa, si unajua unaweza kupata lakini ukose sehemu ya kuhifadhi, tunatarajia kupokea mifuko ya Simenti kutoka Dangote zaidi ya 4000 na mabati kama 400 ivi kwa hiyo ni lazima nifahamu ni wapi itakuwa stoo ya kuifadhi hivyo vifaa, na nataka kusimamia mimi mwenyewe ujenzi huu kwa haraka ili kutimiza maagizo ya Waziri Mkuu “ alisema Ndemanga

No comments :

Post a Comment