Rais Paul Kagame na mwenyeji wake Rais
John Pombe Magufuli, wakipungia mkono wananchi waliojawa na furaha mara
baada ya kuzinduz rasmi maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar
es Salaam kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini
Dar es Salaam, Julai 1, 2016. Imeelezwa na wachambuzi wa mambo kuwa
ziara hii ya Rais Kagame hapa Tanzania, ni ya kihistoria ambayo imezidi
kujenga mwanzo mpya baina ya mataifa haya mawili jirani, baada ya
"mchafuko wa hali ya hewa" mwaka uliopita kufuatia kutokea kwa
kutoelewana baina ya rais Kagame na rais wa awamu ya nne, Jakaya
Kikwete. Rais Kagame katika hotuba yake aliyoitoa kwa kirefu kwa lugha
ya Kiswahili murua, alionyesha kufurahishwa mno na mapokezi na moyo wa
upendo ambao Rais Magufuli na Watanzania kwa ujumla waliouonyesha kwake
hadi akafikia kusema, "Ninaona niko nyumbani". Rais Kagame pia katika
hotuba yake alimalizia kwa kibwagizo cja "Hapa Kazi tu", kauli mbiu ya
Rais Magufuli.(PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
Mama Jannet Kagame (kushoto) na
mwenyeji wake Mama Jannet Magufuli, walipotembelea maonyesho ya biashara
ya kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 1, 2016. (PICHA NA K-VIS
MEDIA/KAHLFAN SAID)
Mama Jannet Kagame (kushoto) na mwenyeji wake Mama
Jannet Magufuli, walipotembelea maonyesho ya biashara ya kimataifa ya
Dar es Salaam, Julai 1, 2016. (PICHA NA K-VIS MEDIA/KAHLFAN SAID)
Rais Kagame akikagua gwaride la JWTZ wakati wa mapokezi yake uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere. (PICHA NA IKULU)
Mapokezi katika zulia jekundu Ikulu ya Dar es Salaam. (PICHA NA IKULU)
Rais Magufuli akiteta jambo na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame.(PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
Rais Magufuli akitoa hotuba yake kabla ya kumkaribisha mgeni wake, Rais Paul Kagame wa Rwanda.Rais Kagame akihutubia wakati akizindua maonyesho hayo viwanja vya Mwalimu Nyerere.(PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
Rais Kagame akihutubia wakati akizindua maonyesho hayo viwanja vya Mwalimu Nyerere.(PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
Rais Kagame akihutubia wakati akizindua maonyesho hayo viwanja vya Mwalimu Nyerere.(PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
Mama Jannet Kagame akijitambulisha. (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
Marais wakipungia mkoni wananchi (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
Wimbo wa Afrika Mashariki ukipigwa viwanja vya Sabasaba (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
No comments :
Post a Comment