Saturday, July 9, 2016

WHITEDENT YASHEREHEKEA MIAKA 25 SOKONI, YAMWAGA MAGARI 25 KUSHINDANIWA NA WATEJA WAKE


 Kampuni ya ChemicotexCotex wazalishaji wa dawa ya meno aina ya Whitdent, imefanya sherehe kubwa ya kutimiza miaka 25 tangu iingie sokoni kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Julai 9, 2016.
Katika sherehe hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wizraa ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Anayeshughulikia viwanda), Dkt. Adelhem Meru, imezindua promosheni kamambe ambapo jumla ya magari mapya 25 yatashindaniwa. Pichani msichana mrembo akiwa amesimama mbele ya magari hayo wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo. (PICHA NA ALLY DAUDI-MAELEZO)
 Dkt. Meru akionyesha boksi la dawa ya Whitedent wakati wa sherehe hiyo


 Dkt. Meru akitoa hotuba yake
 
NA ALLY DAUDI-MAELEZO
Tanzania inatarajiwa kufikia uchumi wa kati kufikia mwaka 2020 kwa kutumia sekta ya viwanda vikubwa, vya kati na vidogo ili kupiga hatua katika maendeleo ya nchi.
Akizungumza hayo hafla ya kutumiza miaka 25 ya dawa ya meno ya whitedent iliyofanyika leo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dk.  Adellhem Meru amesema kuwa wameweka mkakati na malengo ya kukuza uchumi wa kati kwa kutumia Mchango wa viwanda.
“Mpaka kufikia mwaka 2020 lazima tufikie uchumi wa kati kutokana na Sekta ya viwanda ili tuweze kuendelea na kupata pato la taifa  kutoka  asilimia 7.5 mpaka asilimia 15 na kuwa na uchumi imara kama Watanzania” alisisitiza Dkt. Meru.
Aidha Dkt. Meru amesema kuwa katika malengo waliyojiwekea kwa serikali ya awamu hii ni kuhakikisha mpaka mwaka 2020 ajira nyingi zitatokana na viwanda kufikia asilimia 40 na kuendelea.
Katibu Mkuu huyo ametoa rai kwa watanzania kwa kuwataka wwapende zaidi  kutumia bidhaa za viwanda vya nyumbani kuliko kupendelea bidhaa zinazotoka nje ya nchi.
Mbali na hayo Dkt. Meru aliwapongeza kiwanda kinachotengeneza dawa ya meno ya Whitedent Chemi & Cotex kwa kutimiza miaka 25 tangu waanze kuzalisha bidhaa hiyo na kuwataka waendelee na uzalishaji wao kwa miaka 25 ijayo.
Kwa upande wa Afisa mkuu wa Chemi & Cotex Bw. Raja Swaminathan alisema kuwa katika kusheherekea miaka 25 ya bidhaa yao wametaka kuwashirikisha watanzania kwa kutoa magari 25 ili yashindaniwe na wananchi wote kwa miezi mitatu.
“Tungependa kila mtu awe na nafasi ya kushiriki katika mafanikio yetu kwa kucheza shindano hili kwa sababu bidhaa hii ni mali ya watanzania na inatengenezwa Tanzania “ alisisitiza Bw.Swaminathan.
 Wafanyakazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo
 Dkt. Meru akiteta jambo na Mkuu wa Operesheni wa CHEMICOTEX,  Raja Swaminathan
 Dkt. Meru akilishwa keki ya maadhimisho ya miaka 25 ya Whitedent kuwa sokoni
Dkt. Meru, akikaribishwa na wenyeji wake wakati akiwasili ukumbini

No comments :

Post a Comment