Saturday, July 9, 2016

NINI KIMEMLETA BENJAMIN BIBI NETANYAHU BARANI AFRIKA?

 Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Bibi Netanyahu, (katikati), akitabulishwa na mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Balozi Augustin Mahiga, (kushoto)na Rais wa Rwanda, Paul Kagame (kulia), Rais wa Zambia, Edgar Lungu na Waziri Mkuu wa Ethiopia
Hailemariam Desalegn, kwenye Ikulu ya Naklasero nchini Uganda.
NA K-VIS MEDIA/NA MASHIRIKAYA HABARI
Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Bibi Netanyahu, amekuwa ni kiongozi wa kwanza wa juu wa serikali ya nchi hiyo aliyeko madarakani kutembelea barani Afrika, tangu Yitzhak Rabin, aliyepata kuwa waziri Mkuu wan chi hiyo amtembelee Mfalme Hassan II wa Morocco, mnamo mwaka 1993.
Kituo cha kwanza cha Netanyahu kutembelea Afrika iliku Uganda, akaenda Kenya, na kumaliziana Ethiopia.
Akiwa Uganda, Netanyahu alifanya mkutano na baadhi ya viongozi wa nchi za Kiafrika kutoka Sudan Kusini, Tanzania, iliyowakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa, Kikanda na Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga, na Zambia.
Hata hivyo pamoja na mkutano huo na viongozi wa kiafrika nchini Uganda, vyombo vya habari havikuutilia maanani zaidi mkutano huo na badala yake viliangazia zaidi tukio la kuzindua mnara wa kumbukumbu ya miaka 40 ya operesheni ya kijeshi iliyofanywa na Makomandoo wa Israeli wakati wakiokoa mateka raia wa Israeli kwenye uwanja wa ndege wa Entebe mnamo mwaka 1976.
Katika operesheni hiyo ya aina yake, kiongozi wa makomandoo hao, Yonatan Bibi Netanyahu, kaka wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, aliuawa.
Israeli ililazimika kutuma makomandoo wake kuokoa raia wake waliotekwa nyara wakiwa ndani ya ndege ya shirika la ndege la Ufaransa (Air France). Ndege hiyo ilitekwa nyara na wanamgambo wa Kipalestina, dakika 15 baada ya kuruka kutoka uwanja wa nege wa Tel-Aviv nchini Israel ikielekea Paris Ufaransa.
Wanamgambo hao wa Kipalestina, walifanya tukio hilo wakishinikiza wenzao waliokuwa wakizuiliwa kwenye magereZa nchini Israeli waachiliwe.
Tukio la kuuawa kwa Kaka wa Waziri Mkuu wa Israeli, ndio lililomsukuma kiongozi huyo kuingia kwenye siasa.
Hata hivyo mataifa mengi ya kiafrika hususan kusini mwa jangwa la Sahara, yalijuwa hayaiungi mkono Israeli kutokana na ukandamizaji wake dhidi ya Wapalestina.
Ukiacha Uganda, Netanyahu alikwenda Kenya, ambako enzi za utawala wa Kenyatta, Israeli ilikuwa swahiba wake, na hata  

 Netanyahu akisalimiana na Balozi Mahiga
 Netanyahu (kushoto0, na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn
 Netanyahu akiwa na Rais Museveni kwenye uwanja wa Entebe nchinihumo
 Netanyahu akiweka shada la maua kwenye mnara huo wa kumbukumbu

 Netanyahu akikagua gwaride la askari polisi nchini Kenya
 Netanyahu akikagua gwaride uwanja wa ndege wa Entebe nchini Uganda
 Netanyahu akiwa na Rais Uhuru Kenyatta, Ikulu ya Nairobi
Netanyahu akiteta jambo na mwenyeji wake, Rais wa Rwanda, Paul Kagame mjini Kigali
Kiongozi wa operesheni ya kuokoa mateka wa Israeli, Komandoo Yonatan Bibi Netanyahu. Kaka wa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Bibi Netanyahu. Kiongozi huyo aliuawa kwenye harakati za kuokoa mateka
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi (Picha ya Maktaba)

KATIBU Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, (pichani juu) amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, Frank Msaki kwa kufanya malipo hewa shilingi Milioni 305,820,000. soma zaidi hapo chini



Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo ambae ni Mwanahabari, Blogger na Mkulima (pichani).



MKUU wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga,Godwin Gondwe  amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanawekeza kwenye kilimo kikubwa cha kisasa ambacho kitakuwa na tija kwao ili kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo na kukuza uchumi.
Gondwe alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wafanyabiashara, viongozi wa dini ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka kuona umuhimu wa kutumia fursa ya uwepo wa rutuba nzuri ya ardhi iliyopo wilayani humo kujikita kulima kisasa ili kuweza kupata mafanikio.
Alisema kuwa lazima wafanyabiashara watambue kuwa kilimo ndio njia pekee ambayo inaweza kuwainua kiuchumi na kuharakisha kasi ya ukuaji wa maendeleo iwapo watazingati na kukipa kipaumbele kila wakati
  “Niwaombeni suala la kilimo mlipe  msukumo mkubwa sana kwani hii ndio njia pekee ambayo inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wilaya yetu “Alisema.
Aidha pia alisisitiza umuhimu wa wananchi wa wilaya hiyo kutilia mkazo kulima mazao yanayostahimili ukame ikiwemo Alizeti, Ufuta,Viazi na Mihogo ili kuweza kukabiliana na tatizo la kutoku patikana mvua za uhakika kwa ajili ya kilimo cha mahindi.
 “ Ninajua katika kipindi hiki tumelima kwa wingi lakini hali ya hewa sio nzuri na mvua nazo zimekuwa hazipatikana kwa uhakika hivyo lazima wakulima tubadilike kwa kuanza kupanda mazao yanayostahimili ukame ili kuweza kuepukana na baa la njaa “Alisema DC Gondwe.
Sambamba na hayo,Mkuu huyo wa wilaya alizishauri taasisi za kibenki wilayani humo kuhakikisha zinatoa kipaumbele kwa wawekezaji wa kilimo ili waweze kuzalisha kwa wingi mazao ambayo yataweze kuinua kiuchumi lakini pia kuchangia pato la Taifa.
Hata hivyo ,Mkuu huyo wa wilaya alitumia pia fursa hiyo kuwaasa wakulima waliopata mazao kidogo kuhakikisha wanayatunza na kuacha kuyauza kwani kufanya hivyo kutaweza kusababisha hali ya njaa kwao
Naye Sherhe wa wilaya ya Handeni, Shabani Mohamed alisema kuwa wao watamuombea dua Mkuu huyo wa wilaya ili mungu amuwezeshe kuweza kutimiza majukumu yake ipasavyo na kusaidia kuchangia juhudi za maendeleo kwa wananchi.
 “Nikuambie Mh Mkuu wa wilaya ujio wako hapa Handeni watu wengi wamefurahi sana kwani uchapakazi wako unafahamika tokea ulipokuwa unafanya kazi kwenye kituo cha ITV na tunaamini uhodari huo pia utasaidia kuinua uchumi wetu “Alisema.
Alisema kuwa wao watahakisha wanampa ushirikiano wa hali ya juu ili kumuwezesha kutekeleza vema majukumu yake ya kuipa maendeleo wilaya hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha mshomba, (wapili kulia), akimpatia maelezo mwananchi huyu, Tobist Machenje, (kulia), wakati alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 40 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Afoisa Matekelezo wa Mfuko huo Gladness Madembwe, Afisa Uhusiano, Zaria Mmanga, Afisa wa Fedha, Edward Kerenge na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Fulgence Sebera.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha mshomba, (pichani katikati), akimpatia maelezo mwananchi huyu Tobist Machenje, (kulia), wakati alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 40 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Fulgence Sebera.
 NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha Mshomba, ametembelea mabanda ya wadau wa Mfuko huo ili kubadilishana mawazo na kuelewa shughuli za wadau hao, kwenye maonyesho ya 40 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.
Sambamba na kutembelea mabanda hayo Mshomba pia aliungana na wafanyakazi wake, katika kutoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la WCF na kuwaeleza shughuli za Mfuko huo ulioanzishwa mwaka mmoja uliopita na ushiriki wa maonyesho hayo ni wa kwanza kwa Mfuko huo.
Miongoni mwa mabanda aliyotembelea Mkurugenzi huyo ni pamoja na lile la Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Chama cha Waajiri Tanzania, (ATE), Mfuko wa Pensheni wa PSPF, GEPF, na UTT-PID. Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ulianzishwa kwa sheria namba 20 ya mwaka 2008 iliyorejewa mwaka 2015 ya Fidia Kwa Wafanyakazi. Na kazi kubwa ya Mfuko huo ni kutoa Fidia kwa Mfanyakazi aliyeumia au aliyepata magonjwa wakati akitekeleza majukumu yake ya kazi


 Wafanyakzi wa WCF wakiwa kwenye banda la Mfuko huo, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Edward Kerenge, Zaria Mmanga, na Aly Sheha
 Afisa wa Fedha wa WCF, Edward Kerenge, (kulai), akiwapatia maelezo wananchi waliofika kwenye banda la Mfuko huo
 Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakiongozwa na Meneja Masoko na Uhusiano Costantina Martin, (watatu kushoto). Wakwanza kulia ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Fulgence Sebera
 Mshomba(kulia), akisindikizwa na Meneja Masoko na Uhusiano wa PSPF, Costantina Martin, baada ya kutembelea banda la Mfuko huo
 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, (katikati), akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba, (kushoto) na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Fulgence Sebera, wakati Mshomba kutembelea banda la PSPF
 Mshomba akitembelea banda la UTT-PID
 Mshomba akisalimiana na wafanyakazi wa GEPF alipotembelea banda lao
 Mshomba akipitia jarida la Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), huku akipatiwa ufafanuzi na Meneja wa huduma za Kisheria wa ATE, Suzanne Ndomba-Doran, wakati alipotembeela banda la ATE. Kulia ni Mratibu wa mradi wa NHO, Joyce Nangai
 Mshomba akizungumza jambo na Suzanne Ndomba-Doran
 Mshomba akitembeela banda la OSHA
 Mshomba akiuliza kitu kwa maafisa hawa wa UTT-PID alipotembelea banda la taasisi hiyo

 Afisa Uhusiano wa WCF, Zaria Mmanga, (kulia), akimpatia maelezo, mwananchi huyu aliyefika banda la Mfuko huo kujua shughuli zake
 Afisa wa Fedha wa WCF, Grace Tarimo, (kulai), akimpatia amelezo ya shughuli za Mfuko, mwananchi huu aliyetembelea banda la Mfuko kujua kazi zake
 Afisa wa Fedha wa WCF, Grace Tarimo, (kulia), akimpatia amelezo ya shughuli za Mfuko, mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko kujua kazi zake

No comments :

Post a Comment