Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasili
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar
es Salaam.
Rais
wa Rwanda Paul Kagame akiwa na mkewe Jeannette Kagame wakipokea zawadi
ya maua mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasili jijini Dar
es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakifurahia vikundi vya ngoma za
asili vilivyokuwa vikiburudisha mara baada ya Rais wa Rwanda kuwasili.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakifurahia vikundi vya ngoma za
asili vilivyokuwa vikiburudisha mara baada ya Rais wa Rwanda kuwasili.
Rais
wa Rwanda Paul Kagame akiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili
kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Rwanda Paul Kagame akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JINIA.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo
za Taifa zikipigwa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza
ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo rasmi na Rais wa Rwanda Paul
Kagame pamoja na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Rwanda Paul Kagame akizungumza na Wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais Dkt. Magufuli.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais wa Rwanda
Paul Kagame. PICHA NA IKULU
MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU DODOMA
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu
ya Dodoma Julai 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu
ya Dodoma Julai 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu ya Dodoma Julai 1, 2016. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya
Waziri Mkuu, Uledi Mussa. (Picha na Ofisi ya
Waziri Wanufaika wa Mikopo ya Elimu Juu watakiwa kurejesha mikopo waliyopewa.kuu
Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Wanufaika wa Mikopo ya Elimu ya
Juu ambao tayari wapo katika ajira wametakiwa kurejesha marejesho ya
mikopo waliyopewa kutokana na mfuko wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
(HESLB) kutegemea fedha hizo kuendelea kuwakopesha wanafunzi wengine.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akiwasilisha hotuba
ya kuhitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la kumi na moja.
“Uwezo wa Bodi ya mikopo ya Elimu
ya Juu kuwahudumia walengwa unajengwa na fedha zinazotengwa kila mwaka
katika mipango na Bajeti pamoja na marejesho ya mikopo iliyoiva kutoka
kwa wanufaika,” alisisitiza Mhe. Majaliwa.
Aliendelea kusema kuwa Serikali
inaendelea kufanya maboresho ya kimfumo na kisheria ili kuimarisha
urejeshwaji wa mikopo. Aidha amewaagiza waajiri wote Nchini kutekeleza
wajibu wao wa kuingiza makato ya marejesho wa mikopo ya wanufaika kwa
wakati na kwa viwango vinavyotakiwa baada ya kuwasiliana na Bodi ya
Mikopo.
Vile vile Mhe. Majaliwa amesema
kuwa Serikali inaendelea kuimarisha mfumo wa utoaji wa mikopo kwa
wanafunzi wa elimu ya juu sambamba na kushughulikia changamoto
mbalimbali zilizopo katika Bodi ya mikopo ili kuhakikisha utoaji wa
mikopo unafanyika kwa ufanisi.
Pia Serikali inategemea kubadilisha utaratibu wa kutoa mikopo ili kuwafikia
wanafunzi wote wenye uhitaji zaidi wakiwemo yatima na wenye uwezo mdogo
kiuchumi bila kujali aina gani ya program wanazozisomea.
Waziri Mkuu awataka wabunge wa upinzani kurejea Bungeni
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
leo, Bungeni Mjini Dodoma amewataka wabunge wa upinzani ambao wamesusia
vikao vya Bunge tangu Mei 30 kuingia Bungeni na kuacha kususia vikao vya
Bunge kwani hakuna tija kwa Taifa.
Mhe. Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akitoa hutuba ya kuhitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la kumi na moja.
“kitendo cha baadhi ya
waheshimiwa wabunge kususia vikao vya Bunge hakitoi picha nzuri kwa
wananchi waliotuchagua kuwasilisha matatizo yao katika Bunge hili, hivyo
natoa rai kwa waheshimiwa wabunge hao kutafakari upya uamuzi wao na
niwasihi kwa busara zao waingie ili kwa pamoja na kwa ushirikiano tuweze
kutoa ushauri kwa Serikali,” alisema Mhe. Majaliwa.
Aidha Mhe. Majaliwa alitoa
ufafanuzi juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977
ambayo imetoa haki na kinga kwa waheshimiwa wabunge ili kujadili na
kuhoji utendaji wa Serikali kwa uhuru bila mashaka yoyote ya kuweza
kushitakiwa wanapotimiza wajibu wao wakiwa Bungeni.
Aliendelea kwa kusema kuwa kinga
ya aina hiyo haijatolewa kwa mwananchi yeyote yule Nchini ila kwa
Wabunge, hivyo basi hakuna mbunge aliyefungwa mdomo labda aamue
kujifunga mdomo yeye mwenyewe.
Mhe. Majaliwa amesema kuwa Bunge
linaongozwa na Katiba, Sheria na Kanuni za Kudumu za Bunge, hivyo ni
vyema zikafuatwa kuondoa manung’uniko yasiyo ya lazima na endapo kuna
utata katika jambo lolote ndani ya Bunge zipo taratibu zilizowekwa na
kanuni za kufuata ili kupata ufumbuzi na si kwa kususa kuingia Bungeni
kwani hakuna tija kwa Taifa.
Wabunge wa upinzani wamesusia
vikao vya Bunge tangu Mei 30, 2016 mpaka leo Juni 30 ambapo Bunge
limehitimishwa. Aidha wabunge hao wamekuwa wakiingia Bungeni kila
asubuhi na jioni kisha kutoka mara tu Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson
anapomaliza kusoma Dua maalum la kuliombea Bunge na Taifa.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi yajionea urushaji vipindi vya Bunge
Mhandisi
wa mitambo wa Studio za Bunge Bi. Upendo Mbele akitoa maelezo kwa
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (wa
kwanza kulia) na Ujumbe wake juu ya namna wanavyotekeleza majukumu ya
kurusha vipindi kwa kuzingatia sheria na Kanuni za Bunge wakati wa Ziara
iliyolenga kukabidhi ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (wa kwanza
kushoto) akifuatilia Kikao cha Bunge mapema Jana wakati wa ziara ya Tume
hiyo Bungeni Mjini Dodoma kabla ya kuahirishwa kwa Mkutano wa tatu wa
Bunge la kumi na moja .
Kamishna
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Prof. Amon Chaligha akiwa ndani ya Maktaba
ya Bunge wakati wa Ziara ya Tume hiyo Bungeni Mjini Dodoma.
Mkurugenzi
wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Ofisi ya Bunge Bw. Didas Wambura
(wa kwanza kulia) akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (hayupo pichani) na Ujumbe wake
wakati wa ziara ya Tume hiyo Bungeni Mjini Dodoma.
(Picha na Frank Mvungi-Dodoma)
Halmashauri zote Nchini zimetakiwa kutumia mifumo ya kielektroniki katika kukusanya Mapato
Na; Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
—————————
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
amezitaka Halmashauri zote Nchini kutumia mifumo ya kielektroniki katika
kukusanya mapato kuanzia Julai 01, 2016.
Mhe. Majaliwa aliyasema hayo
Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akihitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la
kumi na moja Juni 30, 2016.
“Napenda kutumia fursa hii
kuziagiza Halmashauri zote Nchini kwamba kuanzia tarehe Mosi Julai, 2016
zihakikishe zinatumia mifumo ya kieletroniki katika kukusanya mapato,
katika kulipa, kuweka na kutekeleza kikamilifu mikakati madhubuti ya
kuboreshha makusanyo,” alifafanua Mhe. Majaliwa
Aidha Mhe. Majaliwa amezitaka
Halmashauri hizo kutoelekeza vyanzo vyote vya mapato kukusanywa na
mawakala kwani vipo vyanzo ambavyo vinaweza kukusanywa kwa ufanisi na
Halmashauri zenyewe bila kutegemea mawakala.
Aliendelea kusema kuwa,
Halmashauri zitaelekezwa kwa waraka ni vyanzo vipi vitahitaji kutumia
mawakala na vingine vitakusanywa na Halmashauri zenyewe kwa kuzingatia
miongozo iliyotolewa na Serikali.
Mhe. Majaliwa aliitaja miongozo
hiyo kuwa ni pamoja na Halmashahuri aidha kwa kutumia mawakala au
Halmashauri zenyewe kuweka kwenye akaunti ya Halmashauri fedha zote
zinazokunywa kwa kutumia mifumo ya kielektroniki ili kupunguza na
kumaliza kabisa masuala ya (cash transactions).
Vile vile Halmashauri zikubaliane
na wakala ni kiasi gani cha asilimia ya makusanyo kitalipwa kwa wakala
na malipo yafanyike baada ya kukusanya na kuingizwa kwenye akaunti ya
Halmashauri.
Sheria ya Fedha ya Serikali za
Mitaa sura 290, inazipa uwezo mamlaka za Serikali za Serikali za Mitaa
kutoza na kukusanya kodi, ushuru na ada mbalimbali kama vyanzo vya
mapato vya Mamlaka za Serikali za Mitaa. Sheria hiyo pia inazipa mamlaka
hizo kuteua Mawakala wa kukusanya mapato hayo kwa niaba ya Mamlaka za
Serikali za Mitaa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu.
TAASISI YA METDO YAHIMIZA WAZEE WANAOLELEWA KATIKA KITUO CHA BUKUMBI KUSAIDIWA.
Ashraph Omary (wa pili kushoto) akizungumza jambo kwa niaba ya Wanachama/Wafanyakazi kutoka Taasisi ya METDO (Mining and Environmental Transformation For Development Organisation, walipotembelea Kituo cha Wazee Bukumbi kilichopo Misungwi mkoani Mwanza.
Wafanyakazi wa METDO wakiambatana na Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa daladala Kanda ya Ziwa, Hassan Dede pamoja na Wanafunzi wa Geita International School, waliwakabidhi wazee wanaolelewa katika kituo hicho msaada wa mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula.
Taasisi ya METDO kupitia kwa msemaji wake, Ashraph Omary, iliwahimiza wanajamii kwa kushirikiana na taasisi za serikali na binafsi kuwasaidia wazee wanaoishi katika kituo hicho ili kuondokana na changamoto zinazowakabiri ikiwemo ukosefu wa mavazi, chakula, matibabu pamoja na ujenzi wa uzio kituoni hapo ikiwa ni miongoni mwa changamoto zilizoanishwa kuwakabiri wazee hao.
Imeandaliwa na BMG
KOCHA KUTOFANYA MABADILIKO MAKUBWA KATIKA KIKOSI CHA SERENGETI BOYS
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya
Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, Bakari
Nyundo Shime, amesema hatarajii kuwa na mabadiliko makubwa ya kikosi
katika mchezo dhidi ya vijana Shelisheli utakaopigwa kesho Jumamosi
Julai 2, 2016 kwenye Uwanja wa Stade Linite mjini Victoria.
“Timu haitakuwa na mabadiliko
makubwa. Almost kikosi kitakuwa ni kilekile cha Dar es Salaam kwa
sababu nitampumzisha Job (Dickson Nickson) tu katika mchezo wa kesho,
na nafasi yake atacheza Enrick (Vitalis Nkosi),” amesema Shime leo
Julai 1, 2016 kabla ya kwenda kwenye mazoezi ya mwisho
yatakayofanyika Uwanja wa Linite.
Shime maarufu kwa jina la Mchawi
Mweusi, amesema anauchukulia mchezo huo kwa uzito uleule na kuongeza
ana sababu za kiufundi na kimbinu kumpumzisha Job katika mchezo wa
marudiano kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika kwa vijana, zitakazofanyika mwakani huko Madagascar.
Kwa hali halisi ilivyo timu iko vema
na ikathibitishwa na Shime mwenyewe akisema: “Kikosi kiko vema kwa
maana ya wachezaji wako vizuri na kambi iko vizuri kwa sababu hakuna
majeruhi.” Pia Daktari wa timu hiyo, Shecky Francis Mngazija
alithibitisha.
“Sioni kama kuna dalili zozote za
hujuma na kimbinu tumejipanga vema. Tumefuta matokeo ya Dar na tuko
huku tunataka matokeo mapya. Mbinu zangu siku zote ni ushindi wa
nyumbani na ugenini,” amesisitiza.
Serengeti Boys ilitua kwenye Kisiwa
cha Mahe uliko Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Visiwa vya Shelisheli
jana Juni 30, 2016 majira ya saa 11 jioni.
BODI YA USHAURI YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA YAFANYA ZIARA YA KUANGALIA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA KAZI ZA MAMLAKA
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Burhani Nyenzi pamoja na wajumbe
wakiangalia utendaji kazi wa rada ya hali ya hewa iliyopo Bangulo, Pugu.
Mwenyeji wa ziara hiyo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA na katibu wa Bodi
hiyo Dkt. Agnes Kijazi.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Burhani Nyenzi pamoja na wajumbe
wakiangalia utendaji kazi wa rada ya hali ya hewa iliyopo Bangulo, Pugu.
Mwenyeji wa ziara hiyo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA na katibu wa Bodi
hiyo Dkt. Agnes Kijazi.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Burhani Nyenzi pamoja na wajumbe
wakiangalia utendaji kazi wa rada ya hali ya hewa iliyopo Bangulo, Pugu.
Mwenyeji wa ziara hiyo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA na katibu wa Bodi
hiyo Dkt. Agnes Kijazi.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Burhani Nyenzi pamoja na wajumbe
wakiangalia utendaji kazi wa rada ya hali ya hewa iliyopo Bangulo, Pugu.
Mwenyeji wa ziara hiyo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA na katibu wa Bodi
hiyo Dkt. Agnes Kijazi.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Burhani Nyenzi pamoja na wajumbe
wakiangalia utendaji kazi wa baadhi ya vifaa vya hali ya hewa katika
kituo cha hali ya hewa JNIA. Mwenyeji wa ziara hiyo alikuwa Mkurugenzi
Mkuu wa TMA na katibu wa Bodi hiyo Dkt. Agnes Kijazi.
MAMLAKA ZA JIJI LA LAGOS ZAFUNGA MAKANISA NA MISIKITI KWA KELELE
Mamlaka za Jiji la Lagos nchini
Nigeria imeyafunga makanisa 70 na misikiti 20 kwa katika mikakati
yake ya kupunguza kiwango kikubwa cha kelele jijini humo.
Kampeni hiyo ya kukabiliana na
kelele pia imezikumba hoteli 10 pamoja na klabu za starehe, katika
Jiji la Lagos lenye watu milioni 20.
Serikali imeahidi kuhakikisha
inataka kulifanya Jiji hilo la Lagos kuwa halina kelele ifikapo mwaka
2020, kwa kudhibiti kelele za mziki, honi za magari na kutoka kwenye
makanisa na misikiti.
No comments :
Post a Comment