Said Salim
Bakhresa ambaye ni mwanzilishi kwa Kampuni ya Bakhresa Group, ni tajiri
wa tatu nchini Tanzania na kwa mujibu wa Forbes anakadiriwa kuwa na
Utajiri wenye thamani ya kiasi cha $600 milioni (Tshs 1.3 trilioni).
Kampuni zake zinajihusisha na Kilimo, Vinywaji, Usafirishaji, Biashara
za mafuta, Utangazaji, usindikaji na Ufungaji bidhaa mbali mbali. Tajiri
huyo anatarajia kutumia kiasi cha fedha cha USD 30 milioni (ambazo ni
sawa na Tshs bilioni 6.6 ili aweze kupata umiliki wa kiwanda cha
kutengeneza unga huko Zimbabwe.
Kwa mujibu wa Zimbabwe Mail, Kampuni ya Bakhresa ambayo ni moja ya
Makampuni makubwa nchini Tanzania, imekwisha wataarifu washindani wake
pamoja na Tume ya Ushuru nchini humo kwamba inatumaini kupata 100% ya
hisa za kampuni hiyo inayosuasua.
Mnamo mwaka 2014, Kampuni ya Bakhresa ilishinda Zabuni kuiwezesha
kupata umiliki wa hisa za kampuni ya BRI baada ya waliokua wamiliki wa
hisa hizo kutoa tenda kwa wawekezaji wowote kununua au kuwekeza mtaji
wake ili kufufua shughuli za Kiwanda hicho. BRI ni kiwanda
kunachotengeneza unga wa mikate na chakula cha mifugo na kimekua na
matatizo ya kuzungusha mtaji wake pamoja na kushindwa kulipa madeni yake
katika Benk za Muungano wa Zimbabwe na Washirika wa biashara.
Kampuni ya Bakhresa ni kampuni kubwa kwa upande wa viwanda vya
kutengeneza unga kwa Afrika Mashariki na nchi nyingine, na vilevile
ilionyesha wazi kwamba itatoa mtaji wa kiasi cha $ 30 milioni ambayo ni
sawa na Tsh 6.6 bilioni ili kuweza kukifufua kiwanda hicho cha BRI na
kukirudisha katika hali ya kuweza kuendeleza kutoa faida.
No comments :
Post a Comment