Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servaciaus Likwelile akitiliana
saini na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki ya Exim ya China Bw. Zhu
Ying kuhusu makubaliano ya awali ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango
cha kisasa (Standard Gauge), jijini Dar es Salaam,
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servaciaus Likwelile
akibadilishana hati ya makubaliano na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki
ya Exim ya China Bw. Zhu Ying mara baada ya kusaini makubaliano ya
awali ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge),
jijini Dar es Salaam,
………………………………………………………………………………………………..
Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania leo imetiliana saini na Benki ya Exim ya China makubaliano
ya awali ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard
Gauge).
Makubaliano hayo ya awali
yamefanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servaciaus
Likwelile kwa niaba ya Tanzania na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki ya
Exim ya China Bw. Zhu Ying.
Akizungumza katika hafla hiyo ya
utiliaji saini Dkt. Likwelile amesema hatua hiyo inawezesha hatua za
upembuzi yakinifu, usanifu na uundwaji wa timu za pamoja kuanza kuanisha
mahitaji halisi ya ujenzi wa mradi huo.
Zaidi ya Shilingi Trilioni 16 za
Tanzania zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa mradi wa reli ya kati
yenye urefu wa Kilometa 2,190 ambapo Benki hiyo itashirikiana na
Serikali ya Tanzania katika ujenzi wake.
Mradi wa ujenzi wa reli ya kati
utahusisha ujenzi wa reli kwa kiwango cha kisasa kutoka Dar es
Salaam-Tabora-Isaka-Mwanza na
Tabora-Mpanda-Kalemela-Uvinza-Kigoma-Isaka-Keza hadi Msongati.
DK. TULIA AKSON AONGOZA MBIO ZA KILOMITA 5 MJINI DODOMA
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Akson
akiongoza Mbio za Tulia Marathon KM 5 zilizofanyika leo asubuhi kuanzia
Bungeni Mpaka Nyerere Square zikishirikishwa wabunge mbalimbali wakuu wa
wilaya na vijana kama juhudi za kuunga mkono Juhudi za Rais John Pombe
Magufuli katika kuwaletea wananchi maendeleo nchini kushoto ni Anthony
Mtaka Rais wa Chama cha Riadha Nchini RT.
Baada ya mbio hizo walikwenda
kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha Watoto Yatima kiitwacho
kijiji cha Matumaini kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma.Wakati wa
kutoa msaada huo Dkt Tulia alisema kuwa ni vvema kila Mkoa ukawa na
vikundi mbalimbali kikiwemo cha Wazalendo wakafanya shughuli za Kijamii
kusaidia makundi mbalimbali
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Akson akiwa na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde
Rais wa Chama Cha Riadha Tanzania RT Bw. Anthony Mtaka , Mbunge wa Viti
Maalum mkoa wa Mbeya Mary Majelwa wakishiriki katika mbio hizo leo
asubuhi.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Akson
akipiga makofi kama ishara ya kushukuru mara baada ya kufika mwisho wa
mbio hizo zilizoishia Nyerere Square , kushoto ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde.
Vijana wakipasha mara baada ya kufika kwenye viwanja vya Nyerere Squre.
Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda kulia na Mbunge wa jimbo la
Chalinze wa pili kushoto wakishiriki katika mbio hizo pamoja na vijana
mbalimbali .
Programu za vyuo vikuu ambazo hazijasajiliwa na TCU na NACTE kufutwa
Na: Lilian Lundo – MAELEZO
………………………………………….
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Bi.
Maimuna Tarishi ameitaka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Baraza la
Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kufuta programu zinazotolewa na vyuo
vikuu hapa nchini ambazo hazijafanyiwa tathmini wala kusajiliwa.
Katibu
Mkuu huyo ameyasema hayo leo alipokuwa akifunga maonyesho ya kumi na
moja ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Julai 20 katika
viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
“Wakati
mwingine najiuliza inakuwaje chuo kinafundisha programu ambayo
haijatathminiwa wala kusajiliwa na TCU au NACTE, ni lazima tuwe makini
kwani tunahitaji elimu bora katika vyuo vyote nchini bila kuangalia kama
ni cha Serikali au ni Binafsi,” alifafanua Bi. Tarishi.
Aliendelea
kwa kusema kuwa, TCU na NACTE wanajukumu ya kuzifuta programu hizo na
kuanzisha programu zenye uhitaji mkubwa kama vile shahada ya mafuta na
gesi, Kompyuta na Ualimu wa Sayansi ambapo wataalamu katika maeneo hayo
wamekuwa wakihitajika zaidi katika kipindi hiki ambacho Serikali ya
Awamu ya Tano inajikita zaidi katika uanzishwaji wa viwanda.
Aidha
Bi. Tarishi amewataka TCU na NACTE kudahili wanafunzi wenye vigezo
vinavyohitajika na kusisitiza kuwa ni bora kuwa na wanafunzi wachache
katika vyuo vikuu kuliko kuwa na wanafunzi wengi ambao hawana sifa.
Wakati
huo huo Mkuu wa Kitivo cha Biashara Chuo Kikuu cha Zanzibar Salehe
Mwinyi amesema kuwa wanafunzi wengi wamejitokeza kutembelea banda la
Chuo hicho kutaka kujua pogramu zinazotolewa na wengi wao wameonyesha
nia ya kujiunga katika Chuo hiko.
Vile
vile Mwinyi amesema kuwa mwaka huu idadi ya wanafunzi waliotembelea
maonyesho hayo ni wengi zaidi kutokana na eneo lililochaguliwa kufikika
kwa urahisi kutoka pande zote za jiji la Dar es Salaam ukilinganisha na
mwaka jana ambapo yalifanyika viwanja vya Saba Saba na kutembelewa na
idadi ndogo ya wanafunzi na wazazi.
Kwa
upande wake, Fadia Suleiman mwanafunzi anayetegemea kujiunga na Chuo
Kikuu mwaka huu, amesema kuwa maonyesho hayo yamemsaidia kwa kiasi
kikubwa kujua ni programu gani asome kutokana na ufaulu wake wa kidato
sita.
Maonyesho
ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia ambayo huandaliwa na TCU
hufanyika kila mwaka yakitoa fursa kwa Vyuo Vikuu vya ndani na nje ya
nchi kutoa elimu kwa wazazi na wanafunzi wanaotegemea kujiunga na vyuo
vikuu kwa mwaka husika juu ya programu zinazotolewa na vyuo hivyo pamoja
na kutoa ushauri ni programu gani mwanafunzi asome kwa kuangalia ufaulu
wake.
MWENYEKITI WA CCM DK. JAKAYA KIKWETE: MAFISI YALINGOJA MKONO UDONDOKE LAKINI YALIAMBULIA PATUPU
Mwenyekiti
wa CCM na Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete akiimba wimbo maalum kabla
ya kufungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kwenye
ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma leo Julai 22,
2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Magufuli, Wapili
kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein,
kuliani ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Bara, Philip Mangula na wapili
kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Mkutano huo ni kwa
ajili ya kupitisha jina la Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa mwenyekiti
mpya wa CCM ambapo kesho atathibitishwa na Mkutano Mkuu Maalum kwenye
ukumbi wa Dodoma Convention Centre mjini Dodoma
Dk. Jakaya Kikwete akizungumza na
wajumbe hao wakati akifungua mkutano huo amesema kikao hicho kilikuwa
ni cha mwisho kwake kama mwenyekiti wa CCM , Akawashukuru wajumbe hao
kwa kumpa ushirikiano kwa miaka kumi yote akiwa Mwenyekiti na akaongeza
kwamba kama Chama cha Mapinduzi hakikupasuka mwaka jana hakiwezi
kupasuka tena kitaendelea kudumu na kudumu zaidi.
Amesema Kulikuwa na mafisi
yaliyokuwa yakingojea mkono udondoke tu ili yaweze kudaka na kula lakini
yaliambulia patupu chama kilisimama kidete na kuendelea na mipango
mizuri kwa ajili ya watanzania.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DODOMA)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania Mama Samia Suluhu, Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa
na Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu Rajab Luhwavi wakishiriki kuimba wimbo
maalum wa CCM kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo.
Mwenyekiti
wa CCM na Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete akfungua Mkutano wa
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya
Taifa ya CCM mjini Dodoma leo Julai 22, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa
CCM Mtarajiwa, Rais John Magufuli, Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti
wa CCM , Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein.
Mwenyekiti
wa CCM na Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete akifungua Mkutano wa
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya
Taifa ya CCM mjini Dodoma leo Julai 22, 2016. kutoka kulia ni Makamu
Mwenyekiti wa CCM , Bara, Mzee Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti
wa CCM na Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete akisisitiza jambo wakati
akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kwenye ukumbi
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma leo Julai 22, 2016.
Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Magufuli, Wapili
kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein.
Msemaji wa CCM Ndugu Christopher
Ole Sendeka akisalimiana na Mzee Mark Mwandosya katikati ni Mjumbe wa
NEC kutoka mkoa wa Singida Ndugu Mwigulu Nchemba.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa NEC kutoka Zanzibar Ndugu Mohamed Abood akisalimiana na Mjumbe
mwenzake kutoka Zanzibar pia Balozi Ali Karume katikati anayecheka ni
Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu Mzee Wilson Mukama.
Baadhi ya Wajembe wa NEC wakiwa kwenye mkutano huo kutoka kulia ni Mark Mwandosya, Profesa Peter Msola na Mzee Steven Waira.
Mpiga picha wa Makamu wa Rais Bw.
Adam Mzee kulia akiwaelekeza jambo waandishi wenzake kabla ya kuanza
kwa mkutano huo kutoka kushoto ni Emilian Malya kutoka Clouds Digital,
Bakari Kimwanga kutoka Mtanzania na Said Mwishehe kutoka Jambo leo.
Mjumbe wa NEC Godfrey Zambi akisalimiana na Mjumbe mwenzake Hussein Mwinyi katikati ni Khadija Aboud.
Christopher Olesendeka akibadilishana mawazo na wajumbe wenzake.
Baadhi ya wajumbe wakiwa tayari kwa mkutano huo
Wajumbe kutoka mkoa wa Pwani
Mzee Mark Mwandosya akizungumza na mjumbe mwenzake Peter Serukamba kutoka mkoani Kigoma
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa katikati akiwa na mkurugenzi wa Redio
Uhuru Angela Akilimali kulia na Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Uhuru
Selina Wilson wakiwa katika mkutano huo.
Wajumbe kutoka mkoani Mara wakiwa katika mkutano huo
Mwenyekiti wa CCM kotoka Mkoa wa
Mwanza Bw. Joseph Kasheku Msukumu katikati akiwasikiliza wajumbe wenzake
Januari Makamba kulia na Said Mtanda wakati walipokuwa wakijadiliana
jambo.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Ndugu Anthony Dialo akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa.
Wajumbe wa NEC kutoka mkoani Kilimanjaro.
MHE. UMMY MWALIMU AAGIZA KUTENGWA FEDHA YA MFUKO WA MAENDELEO YA WANAWAKE.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
(Mb.) akikagua shughuli za maendeleo za vikundi vya wanawake
wajasiliamali wa Kata ya Magoweko Wilayani Gairo, Mkoa wa Morogoro.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
(Mb.) akiendelea kukagua shughuli za maendeleo za vikundi vya wanawake
wajasiliamali wa Kata ya Magoweko Wilayani Gairo, Mkoa wa Morogoro
akiwa na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Ahmed Shabiby (kulia).
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu (Mb.) akiendelea akiangalia moja ya mashine ya kufyatua matofali
wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za maendeleo za vikundi vya
wanawake wajasiliamali wa Kata ya Magoweko Wilayani Gairo,
Morogoro.Kulia ni Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Ahmed Shabiby (kulia).
……………………………………………………………………………………………
Na. Mwandishi –Wetu –Gairo Morogoro.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Mb.) leo amefanya ziara katika Wilaya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro kwa kukagua shughuli za vikundi vya wanawake wajasiliamali wa Kata ya Magoweko.
Akihutubia wanawake na wananchi walio jitokeza katika maonyesho ya shughuli hizo, Mhe Ummy alieleza kuwa Serikali imejipanga katika kumuwezesha mwanamke kiuchumi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Mb.) leo amefanya ziara katika Wilaya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro kwa kukagua shughuli za vikundi vya wanawake wajasiliamali wa Kata ya Magoweko.
Akihutubia wanawake na wananchi walio jitokeza katika maonyesho ya shughuli hizo, Mhe Ummy alieleza kuwa Serikali imejipanga katika kumuwezesha mwanamke kiuchumi.
Alisema,
uwezeshaji huo utafanyika kupitia mifuko mbalimbali ya kuwawezesha
wanawake, ikiwamo Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) uliopo katika
kila Halmashauri nchini na Benki ya Wanawake Tanzania.
Katika
hadhara hiyo Mhe Ummy alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Gairo, Bibi Agness Martin Mkandya, kuhakikisha Halmashauri hiyo
inatenga asilimia 5 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya Mfuko wa
Maendeleo ya Wanawake ili fedha hizo ziweze kutumika katika kukopesha
wanawake wajasiliamali.
Aidha, aliwaeleza wananchi kuwa serikali itatekeleza ahadi yake ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-20 kwa kutenga kiasi cha shilingi milioni 50 kwa kila Kijiji kama Mfuko wa Mzunguko (Revolving Fund) kwa ajili ya kukopesha vikundi vya wajasiriamali kupitia Ushirika wa Kuweka na Kukopa (SACCOS) katika vijiji husika; hivyo wanawake nao wazichangamkie fedha hizo kwa kuanza kujiandaa kujiunga katika vikundi ili fursa hiyo isiwapite.
Katika kukabiliana na changamoto ya masoko kwa bidhaa zinazotengenezwa na wanawake, Mhe Ummy alisema, Ilani ya uchaguzi ya ccm pia inaelekeza Halmashauri zote kutenga asilimia 30 ya thamani ya manunuzi yake kwa ajili ya bidhaa zinazotengenezwa na vikundi vya vijana au wanawake. Aidha, mbunge wa Jimbo la Gairo, Mhe Ahmed Shabiby aliwaeleza wananchi kuwa wataandaa utaratibu wa kuwa na maonyesho rasmi ya kutangaza kazi za wanawake wajasiliamali wa Wilaya hiyo.
Baadhi ya Wanawake walioshiriki katika shughuli hiyo walieleza kuwa kupitia shughuli za vikundi wameweza kushiriki katika shughuli mbalimbali za kujiongezea kipato ikiwa ni pamoja na kuhamasisha vijana kujiunga na vikundi hivyo, wakilenga pia kuwaelimisha vijana kuacha matumizi ya madawa ya kulevya. Aidha, wanawake hao waliainisha moja ya changamoto kubwa inayo wakabili kuwa ni ukosefu wa mtaji wa kutosha kuendesha biashara zao.
Kupitia hadhara hiyo Mhe Ummy aliwataka wazazi kutilia mkazo elimu kwa watoto wa kike. Alieleza kuwa Wilaya ya Gairo inakabiliwa na tatizo kubwa la mimba na ndoa za utotoni, tatizo ambalo kwa kiasi kikubwa linafifisha jitihada za serikali katika kumpatia mtoto wa kike Elimu.
Aidha, aliwaeleza wananchi kuwa serikali itatekeleza ahadi yake ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-20 kwa kutenga kiasi cha shilingi milioni 50 kwa kila Kijiji kama Mfuko wa Mzunguko (Revolving Fund) kwa ajili ya kukopesha vikundi vya wajasiriamali kupitia Ushirika wa Kuweka na Kukopa (SACCOS) katika vijiji husika; hivyo wanawake nao wazichangamkie fedha hizo kwa kuanza kujiandaa kujiunga katika vikundi ili fursa hiyo isiwapite.
Katika kukabiliana na changamoto ya masoko kwa bidhaa zinazotengenezwa na wanawake, Mhe Ummy alisema, Ilani ya uchaguzi ya ccm pia inaelekeza Halmashauri zote kutenga asilimia 30 ya thamani ya manunuzi yake kwa ajili ya bidhaa zinazotengenezwa na vikundi vya vijana au wanawake. Aidha, mbunge wa Jimbo la Gairo, Mhe Ahmed Shabiby aliwaeleza wananchi kuwa wataandaa utaratibu wa kuwa na maonyesho rasmi ya kutangaza kazi za wanawake wajasiliamali wa Wilaya hiyo.
Baadhi ya Wanawake walioshiriki katika shughuli hiyo walieleza kuwa kupitia shughuli za vikundi wameweza kushiriki katika shughuli mbalimbali za kujiongezea kipato ikiwa ni pamoja na kuhamasisha vijana kujiunga na vikundi hivyo, wakilenga pia kuwaelimisha vijana kuacha matumizi ya madawa ya kulevya. Aidha, wanawake hao waliainisha moja ya changamoto kubwa inayo wakabili kuwa ni ukosefu wa mtaji wa kutosha kuendesha biashara zao.
Kupitia hadhara hiyo Mhe Ummy aliwataka wazazi kutilia mkazo elimu kwa watoto wa kike. Alieleza kuwa Wilaya ya Gairo inakabiliwa na tatizo kubwa la mimba na ndoa za utotoni, tatizo ambalo kwa kiasi kikubwa linafifisha jitihada za serikali katika kumpatia mtoto wa kike Elimu.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI ATEMBELEA CHUO CHA USAFIRISHAJI
Mkuu
wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa
akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Eng. Edwin Ngonyani alipotembelea Chuo hicho kukagua miundombinu yake.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akitoa
maelekezo kwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof.
Zacharia Mganilwa kuhusu namna nzuri ya kukiwezesha Chuo hicho
kujiendesha kwa faida na kuboresha miundombinu yake.
Mkuu
wa Kitengo cha Uhandisi wa anga katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji
NIT Eng. Azizi Mdimi akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani injini ya ndege inayotumia kwa mafunzo
wakati alipokagua Hanga katika chuo hicho.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua
ndege inayotumiwa kufundishia wanafunzi wanaosomea utengenezaji wa ndege
na urubani alipotembelea Chuo cha Usafirishaji NIT.
Mkuu
wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa
akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin
Ngonyani moja ya kitabu kinachotumiwa kufundishia marubani na wahandisi
wa ndege alipotembelea maktaba ya chuo hicho.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua
mtambo unaopima magari ili kujua ubora wake kabla ya kuanza kutumika
hapa nchini alipotembelea Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT.
(Picha na Benjamin Sawe-Maelezo)
UMMY MWALIMU AZINDUA UJENZI WA WODI YA WAZAZI KATIKA KITUO CHA AFYA CHA GAIRO
Waziri
wa afya,Maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu akikata
utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi ya wodi ya wazazi kwenye kituo cha
afya Gairo.
Waziri
Ummy Mwalimu akiwasikiliza watumishi wa kituo hicho cha afya(hawapo
pichani),kushoto ni mbunge wa jimbo la Gairo Mhe.Ahmed Shabiby(wa kwanza
kushoto)Mkuu wa Wilaya hiyo mhe.Siriel Mchembe(wa pili kulia) na wa
kwanza kulia ni Mkurugenzi wa halmashauri bi.Agnes Mkandya
Waziri
Ummy akimsikiliza mwananchi(hayupo pichani)kwenye kituo cha afya gairo
mara baada ya kuzindua ujenzi wa wodi ya wazazi,kulia ni bi. Agnes
Mkandya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo
Waziri
wa afya akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa halmashauri
hiyo,mara baada ya kuzindua ujenzi wa wodi ya wazazi inayojengwa kwenye
kituo cha afya gairo.
(picha na wizara ya afya)
……………………………………………………………………………………….
Na.Catherine Sungura,Gairo
Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wametakiwa kuweka kwenye mipango yake na kiwe kipaumbele chao ujenzi wa Hospitali ya wilaya.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akizindua ujenzi wa wodi ya wazazi inayojengwa kwenye kituo cha Afya mjini hapa inayodhaminiwa na mbunge Ahmed Shabiby.
Waziri Ummy amesema wodi hiyo ikikamilika itawasaidia akina mama wengi wa halmashauri Hiyo pamoja na vijiji vya jirani kufika kituoni hapo kujifungua”suala ya uzazi kwa mwanamke ni haki yake ya msingi,hivyo kuwa na wodi yao ni haki yao pia na kwa afya zao na za watoto wanaojifungua”
Aidha,amesisitiza juu ya utekelezwaji wa sera ya afya inayohusu matibabu bure kwa akina mama wajawazito,wazee na watoto chini ya miaka mitano.
“Nazikumbusha hospitali na vituo vya afya nchini kuwapa kipaumbele kwa kuwapatia matibabu makundi haya,pia muweke dirisha litakaowahudumia wazee,na hii ndio muhimu mlitekeleze”
Kwa upande wa watumishi,Waziri Ummy Karnataka waendelee kufanya kazi kwa uadilifu kwa mujibu wa sheria na taratibu Za taaluma zap na kuzingatia viapo vyao katika kuwahudumia wananchi ili kusiwepo na malalamiko yatakayoleta matatizo.miongoni mwao.
“Nakuagiza Mkurugenzi wa halmashauri uhakikishe unatatua changamoto za watumishi ikiwemo kuwalipa posho za sare za kazi, likizo na stahiki zao nyingine watumishi hawa”
Awali akisoma taarifa ya Wilaya,mkuu wa wilaya hiyo bi. Siriel Mchembe alitaja changamoto kubwa kwa upande wa huduma za afya ni kukosekana kwa hospitali ya Wilaya Mkuu wa wilaya ya Gairo juu ya hali ya huduma za afya wilayani humo, alieleza changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya ikiwemo ukosefu wa hospitali ya wilaya, gari la kubebea wagonjwa, upungufu wa watumishi pamoja na kutokuwepo kwa zahanati na vituo vya afya katika kata na vijiji hali inayopelekea wananchi kuzifuata huduma za afya umbali mrefu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akizindua ujenzi wa wodi ya wazazi inayojengwa kwenye kituo cha Afya mjini hapa inayodhaminiwa na mbunge Ahmed Shabiby.
Waziri Ummy amesema wodi hiyo ikikamilika itawasaidia akina mama wengi wa halmashauri Hiyo pamoja na vijiji vya jirani kufika kituoni hapo kujifungua”suala ya uzazi kwa mwanamke ni haki yake ya msingi,hivyo kuwa na wodi yao ni haki yao pia na kwa afya zao na za watoto wanaojifungua”
Aidha,amesisitiza juu ya utekelezwaji wa sera ya afya inayohusu matibabu bure kwa akina mama wajawazito,wazee na watoto chini ya miaka mitano.
“Nazikumbusha hospitali na vituo vya afya nchini kuwapa kipaumbele kwa kuwapatia matibabu makundi haya,pia muweke dirisha litakaowahudumia wazee,na hii ndio muhimu mlitekeleze”
Kwa upande wa watumishi,Waziri Ummy Karnataka waendelee kufanya kazi kwa uadilifu kwa mujibu wa sheria na taratibu Za taaluma zap na kuzingatia viapo vyao katika kuwahudumia wananchi ili kusiwepo na malalamiko yatakayoleta matatizo.miongoni mwao.
“Nakuagiza Mkurugenzi wa halmashauri uhakikishe unatatua changamoto za watumishi ikiwemo kuwalipa posho za sare za kazi, likizo na stahiki zao nyingine watumishi hawa”
Awali akisoma taarifa ya Wilaya,mkuu wa wilaya hiyo bi. Siriel Mchembe alitaja changamoto kubwa kwa upande wa huduma za afya ni kukosekana kwa hospitali ya Wilaya Mkuu wa wilaya ya Gairo juu ya hali ya huduma za afya wilayani humo, alieleza changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya ikiwemo ukosefu wa hospitali ya wilaya, gari la kubebea wagonjwa, upungufu wa watumishi pamoja na kutokuwepo kwa zahanati na vituo vya afya katika kata na vijiji hali inayopelekea wananchi kuzifuata huduma za afya umbali mrefu.
WANACHAMA WA CUF KUPIGA HODI KWA IGP MANGU ENDAPO ATAENDELEA KUKIFUATILIA CHAMA HICHO
Naibu
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrul
(wa nne kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo,
wakati akitoa msimamo wa chama hicho kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi
dhidi ya vyama vya siasa hasa cha Cuf. Wengine ni maofisa mbalimbali wa
chama hicho.
Naibu
Katibu Mkuu wa chama hicho, Tanzania Bara, Shaweji Mketo, akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam , wakati wa kutoa msimamo wa chama
hicho kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi dhidi ya vyama vya siasa hasa
cha Cuf. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Ulinzi Taifa, Mustafa Wandu na
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed
Mazrul.
wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
……………………………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
MKURUGENZI
wa Uchaguzi wa Chama cha Wananchi (CUF) Shaweji Mketo amesema iwapo
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu ataendelea kukifuatilia
chama hicho wanachama wa chama hicho watekwenda ofisini kwake
kumsalimia.
Mketo
ameyasema hayo Makao Makuu ya Chama hicho Buguruni leo Dar es Salaam
leo wakati Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar,
Nassor Ahmed Mazrul alipo kuwa akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu msimamo wa chama hicho kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi dhidi
ya vyama vya siasa hasa cha Cuf.
“Tunasema
sisi Cuf hatumuogopi IGP na kama ataendelea kutufuatafuata haita pita
wiki mbili tutamfuata kwenda kumsalimia ofisi kwake” alisema Mketo.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrul
alisema
chama hicho kimesikitishwa na kauli ya IGP aliyoitoa hivi karibuni
wakati akihojiwa Tido Mhando wa Kituo cha Televisheni cha Azzam kuwa
jeshi hilo wakati wowote litamkamata Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim
Seif Sharif Hamad kwa kuwachochea wafuasi wake ili waichukie serikali
iliyopo madarakani.
Alisema
baada ya kuitafakari kauli hiyo ya IGP wamebaini kwamba hivi sasa IGP
Mangu ameamua kuwathibitishia watanzania kuwa jeshi la polisi ni idara
maalumu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mazrul
alisema kwa muda mrefu IGP Mangu amekuwa akilitumia jeshi la polisi
kushiriki katika matukio mbalimbali ya kuhujumu demokrasia na kukiuka
haki za binadamu kwa lengo la kukinusuru Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kutokana na anguko kubwa la kukataliwa na wananchi kama ilivyothibitika
kabnla na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana.
Alisema
jeshi la polisi limekuwa na utaratibu wa kukamata raia, kuwapiga
kuwabambikia kesi, kuwashikilia na kuwatesa katika vituo vya polisi bila
ya kuwafikisha mahakamani.
Mazrul alisema hadi sasa zaidi ya wananchi 400 wameathiriwa kutokana na hujuma za jeshi la polisi kwa kuwabambikia kesi.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
Jeshi
la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria
zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu
na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada
hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu. Hata hivyo kuna matukio
mawili ya mauaji yameripotiwa kutokea katika wilaya za Chunya na
Mbarali kama ifuatavyo.
Tukio la kwanza.
NEEMA
NELSON MBUNGA [25], mfanyabiashara ya mazao, mkazi wa Mengele –
Chimala, aliuawa kwa kukatwa mapanga kichwani na mikononi akiwa amelala
chumbani kwake.
Tukio
hilo lilitokea tarehe 19.07.2016 majira ya saa 02:00hrs katika kijiji
cha Mengele, kata ya Chimala, tarafa ya Ilongo wilaya ya Mbarali.
Watu wawili wanashikiliwa na Polisi kuhusiana na tukio hilo akiwemo
kaka wa marehemu ANYAMISYE NELSON [34], mkazi wa Mengele – Chimala
ambaye alikuwa amelala chumba cha pili katika nyumba hiyo ambayo
haikuvunjwa sehemu yoyote na mtuhumiwa wa pili aliyekamatwa ni FREDY
LUPONELO CHOTA [32], mkazi wa Chimala. Chanzo cha tukio hilo bado
kinachunguzwa. Begi dogo la marehemu limekutwa eneo la shule ya msingi
Mengele umbali wa mita takribani 300 kutoka eneo la tukio likiwa na
vitambulisho na nguo.
Tukio la pili.
Watu
wawili SHIJA MIGUDA [40] na mke wake KABULA KATABI [35], wakazi wa
kitongoji cha Mpembe waliuawa kwa kukatwa mapanga mwilini wakiwa
wamelala nyumbani kwao, baada ya mlango wa nyumba kuvunjwa.
Tukio
hilo limetokea tarehe 19.07.2016 saa 02:30hrs kitongoji cha Mpembe,
kijiji cha Mwiji, kata ya Lualaje, tarafa ya Kipembawe, wilaya ya
Chunya. Chanzo cha tukio hili ni imani potofu za kishirikina kufuatia
marehemu hao kutuhumiwa kuwa ni wachawi hapo kijijini. Watuhumiwa ambao
ni majirani na marehemu walikimbia baada ya tukio, ufuatiliaji
unaendelea.
WITO:
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi EMANUEL .G
.LUKULA anatoa wito kwa jamii hasa wahalifu kuacha tabia ya kuwa na
tamaa ya utajiri wa haraka kwa kujipatia kipato haraka kwa njia ya
mkato / haramu badala yake wajishughulishe kwa kufanya kazi halali na
kupata kipato halali. Aidha Kamanda LUKULA anatoa rai kwa yeyote mwenye
taarifa juu ya mtu / watu waliohusika katika matukio hayo azitoe katika
mamlaka husika ili wakamatwe na sheria ichukue mkondo wake vinginevyo
wajisalimishe mara moja. Pia anaendelea kutoa wito kwa jamii kuepukana
na tabia ya kusadiki imani potofu za kishirikina kwani zina madhara
makubwa kwa jamii ikiwemo kupoteza nguvu kazi ya Taifa.
[EMANUEL G. LUKULA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFANYA MAZUNGUMZO NA WAJUMBE WANAWAKE WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambapo aliwaambia
umoja na mshikamano ni nguzo muhimu kwa wanawake .
Aliwataka kutumia fursa zinazopatikana mjini na kujiunga na Majukwaa ya Wanawake.
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka Wilaya ya Uvinza ,Asha Baraka
akichangia jambo wakati wa Mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
Sehemu ya Wajumbe wakifuatilia mazungumzo baina yao na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan.
WASIFU WA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI MGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI WA CCM
WASIFU WA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI
MGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI WA CCM
1.0. MAISHA YAKE
Ndugu
John Pombe Joseph Magufuli alizaliwa Oktoba 29, mwaka 1959 katika
kijiji cha Chato, Wilayani Biharamulo katika Mkoa wa Kagera. Hivi sasa
Chato ni Wilaya katika Mkoa wa Geita. Ndugu Magufuli ni Daktari wa
Falsafa (PhD) ya Kemia. Ana mke na watoto saba. Alichaguliwa kuwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Oktoba, 2015 kwa tiketi ya
Chama Cha Mapinduzi (C.C.M). Aliapishwa na kuanza rasmi majukumu yake ya
kuiongoza Tanzania tarehe 5 Novemba, 2015.
Tangu
ameingia madarakani, Rais Dkt. Magufuli, ameonesha kuwa ana sifa zote
muhimu za uongozi. Ana dira, maono na malengo kuhusu anakotaka Taifa
liende. Ana mikakati ya kutekeleza dira na maono yake. Haogopi kufanya
maamuzi makini. Ana kiu ya kuona Taifa linapata maendeleo. Amejipambanua
kuwa yeye ni mtetezi wa wanyonge na dhamira yake kubwa ni kuona
wananchi wanapata huduma bora za jamii na kero zao zinaondoka.
2.0. ELIMU NA MAFUNZO
Rais
Dkt. Magufuli alianza elimu ya msingi katika Shule ya msingi Chato
mwaka 1967 na kumaliza mwaka 1974. Mwaka 1975 alianza masomo ya
sekondari katika Shule ya Seminari ya Katoke Mkoani Kagera. Mwaka 1977
alihamia shule ya sekondari ya Lake iliyopo Mkoani Mwanza na kuhitimu
kidato cha Nne mwaka 1978. Kuanzia mwaka 1979 hadi 1981 alifanya masomo
ya kidato cha Tano na Sita katika shule ya Sekondari ya Mkwawa Mkoa wa
Iringa .
Mwaka
1981 hadi 1982 alisoma Chuo cha Ualimu Mkwawa na kuhitimu Stashahada ya
Ualimu ya Masomo ya Kemia na Hisabati. Mwezi Julai hadi Disemba mwaka
1983, Dkt. Magufuli alipata mafunzo ya kijeshi katika Jeshi la kujenga
Taifa kikosi cha Makutupora mkoa wa Dodoma. Mwezi Januari hadi Machi
1984 alihamishiwa kikosi cha mafunzo Jeshi la Kujenga Taifa Makuyuni,
Arusha. Mwezi huo wa Machi alihamia kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa
Mpwapwa Dodoma na kumaliza mafunzo mwezi Juni 1984.
Mwaka
1985 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kusoma Shahada ya kwanza
ya Sayansi na Ualimu akijikita katika masomo ya Kemia na Hisabati.
Alitunukiwa Shahada hiyo mwaka 1988. Mwaka 1991 hadi 1994 alisoma na
kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika fani ya Kemia iliyotolewa na Chuo
Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu cha Salford cha Uingereza. Mwaka
2006 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya Shahada ya
Uzamivu katika Fani ya Kemia na kufanikiwa kuhitimu mwaka 2009.
3.0. UZOEFU WA NDANI YA SERIKALI
JAMII ZINAZOZUNGUKA MAENEO YA HIFADHI NCHINI ZISHIRIKISHWE KULINDA MALIASILI ZA TAIFA
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa kwanza kulia)
akizungumza na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo, Massana
Mwishawa (wa pili kulia) alipotembelea hifadhi hiyo tarehe 21 Julai,
2016 kwa ajili ya kujionea kero mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi. Kushoto aliyesimama na Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu kwa
jina la Msukuma.
jina la Msukuma.
Mkuu
wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo, Massana Mwishawa (wa pili
kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani
(wa kwanza kulia) sehemu ya fukwe za hifadhi hiyo ambazo ni makazi ya
Mamba na Ndege wa aina mbali mbali alipotembelea hifadhi hiyo tarehe 21
Julai, 2016 kwa ajili ya kujionea kero mbalimbali na kuzitafutia
ufumbuzi. Kushoto aliyesimama na Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini,
Joseph Kasheku maarufu kwa jina la Msukuma.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa pili kulia) akiteta
jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mwl. Herman Kapufi (kulia) katika
fukwe ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo alipotembelea hifadhi
hiyo tarehe 21 Julai, 2016 kwa ajili ya kujionea kero mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi. Kushoto anaesaini kitabu cha wageni ni Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu kwa jina la Msukuma.
BENKI YA CRDB YAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI 100-KIGOMA
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la
Kasulu mkoani Kigoma Paul Chacha akizungumza wakati wa hafla ya
kumkabidhi Mkuu wa Wilaya Kakonko madawati 100 yenye thamani ya Sh. Mil 5
yaliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa
madawati katika Shule za Msingi wilayani humo.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya Kakonko mkoani Kigoma Lusubilo Mwakabibi
(aliyesimama katikati) akizungumza muda mfupi kabla ya benki ya CRDB
haijakabidhi madawati 100 yenye thamani ya Sh. Mil 5 kwa ajili ya shule
za msingi wilayani humo.
Mkuu
wa wilaya Kakonko mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala akizungumza kabla
hajapokea madawati 100 yaliyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya Shule
za Msingi wilayani humo.
Mkuu wa wilaya Kakonko mkoani
Kigoma Kanali Hosea Ndagala (kulia) akipokea kutoka kwa Meneja wa Benki
ya CRDB tawi la Kasulu mkoani Kigoma moja ya madawati 100 yaliyotolewa
na benki hiyo kwa ajili ya wanafunzi wa Shule za Msingi wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagaa (kulia) akipokea sehemu ya msaada wa madawati 100 kutoka kwa Meneja
wa CRDB Tawi la Kasuu, Paul Chacha. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa
Hamashauri ya Wilaya ya Kakonko, Lusubilo Mwakibibi (katikati) na ofisa
wa CRDB.
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagala (walioka kulia) akiwa na Meneja wa CRDB Tawi la Kasulu, Paul Chacha (katikati) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kakonko, Lusubilo Mwakibibi. Kushoto waliosimama ni Katibu Tawala wa Kakonko, Zainab Mbunda.
Mkuu
wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagala (kulia)
akimshukuru Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Kasulu, Paul Chacha baada ya
kupokea msaada wa madawati 100 kwa ajili ya Shule za Msingi Wilayani
humo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko,
Lusubilo Mwakibibi.
Mkuu
wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala (katikati) akiwa na Meneja
wa CRDB Tawi la Kasulu, Paul Chacha (wa pili kulia), Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Kakonko, Lusubilo Mwakibibi (kushoto) na Katibu Tawala wa
Kakonko, Zainab Mbunda.
RIPOTI YA KIUCHUMI BARANI AFRIKA YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM
Ofisa
Uchumi wa Idara ya Afrika wa Nchi Zinazoendelea kutoka Geneva
(Unctad), Claudia Roethlisberger, akizungumza na wadau mbalimbali wa
masuala ya uchumi wakati wa uzinduzi wa ripoti ya maendeleo ya kiuchumi
barani Afrika iliyofanyika jijini Dar es Salaam,jana. Kulia ni Ofisa
habari Umoja wa Mataifa Kitengo cha Mawasiliano (UNIC),Stellah Vuzo.
Ofisa
habari Umoja wa Mataifa Kitengo cha Mawasiliano (UNIC),Stellah
Vuzo,akizungumza katika uzinduzi wa ripoti hiyo ya maendeleo ya kiuchumi
barani afrika. Kushoto ni Ofisa Uchumi wa Idara ya Afrika wa Nchi
Zinazoendelea kutoka Geneva (Unctad), Claudia Roethlisberger.
Mtafiti
wa Shirika linalojishughulisha na masuala ya utafiti wa masuala ya
uchumi (REPOA),Stephen Mwombela,akichangia mada katika mkutano huo.
Wadau mbalimbali wa masuala ya uchumi nchini wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa ripoti hiyo .
………………………………………………………………………………
NA ELISA SHUNDA
SERIKALI
za Afrika zimeshauriwa kuchukua hatua ya kuzuia ukuaji wa madeni ya
mataifa yao ili kuepusha migogoro inayoweza kutokea kama iliyowahi
kutokea miaka ya mwishoni mwa 1980 na 1990.
Pia zimetakiwa kuongeza vyanzo vipya vya mapato kwaajili ya kugharamia maendeleo ya nchi zao.
Kauli
hiyo imetolewa jijini hapa jana na Ofisa Uchumi Idara ya Afrika,Nchi
zinazoendelea ambaye ni mwakilishi kutoka Geniva, Claudia
Reothlisberger, wakati alipokuwa akizindua Ripoti ya Maendeleo ya
Kiuchumi Barani Afrika.
“Ripoti
hii ya UNCTAD inayozinduliwa leo(jana) inayohusu Maendeleo ya Uchumi
barani Afrika, lakini tufahamu imekuwa ikichapishwa kila mwaka kuanzia
mwaka 2000,lengo likiwa ni kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na
hasara ya uwezekano wa ushirikiano mkubwa wa kiuchumi na uchumi wa dunia
kwa kufanya utafiti na uchambuzi sambamba na kujenga maridhiano na
ushirikiano wa kiufundi,
“Ripoti
hii ambayo imezinduliwa chini ya Umoja wa Mataifa kuhusu Biashara na
Maendeleo (UNCTAD), inasisitiza kuwa kukopa inaweza kuwa sehemu muhimu
ya kuboresha maisha ya wananchi wa afrika lakini lazima kupata uwiano
kati ya wakati wa sasa, na baadaye kwa sababu madeni ni hatari
yanapokuwa sio endelevu” alisema.
Aidha
alisema kwa mujibu wa ripoti hiyo ilibaini kuwa angalau dola za
kimarekani bilioni 600 zinahitajika kila mwaka ili kufikia Malengo ya
Maendeleo endelevu(SDGs) barani Afrika.
Alisema
licha ya ripoti hiyo kubaini pia kwa sasa nchi nyingi za afrika
zimeanza kuondokana na utegemezi wa misaada rasmi ya maendeleo kutokana
na kutumia vyanzo vyake vipya vya fedha na vyenye ubunifu lakini
zinapaswa kuangalia vyanzo vya mapato vya nyongeza ambavyo vitasaidia
afrika kufikia malengo yake.
“Ripoti
hii ambayo pia imepewa kichwa kidogo kuwa Mienendo ya Madeni na Fedha
za maendeleo barani afrika ilionyesha kuwa zipo nchi kadhaa za Afrika
zilikopa sana katika masoko ya ndani, na nchi hizo ni Nigeria, Ghana,
Kenya,Tanzania na Zambia” alisema.
Kwa
upande wake Mchumi kutoka Benki ya Maendeleoa ya Afrika(AfDB), Prosper
Charles alisema kuwa ni wakati sasa serikali kuwa macho na hatari za
kukopa kutokana na masharti magumu yaliyopo katika kipindi hiki.
“Ili
kufikia malengo endelevu ya ya millennia ni lazima serikali ijizatiti
kutekeleza miradi yake haswa mipango yake ambayo itasaida kuondokana na
hatari ya deni la taifa”alisema.
Imeandaliwa na Shunda blog/elisashunda@gmail.com/0719-976633.
Mbunge wa jimbo la Ukonga, Mwita Waitara akabidhi madawati shule ya msingi Kilimani .
Mbunge wa jimbo la Ukonga, Mwita Waitara, akimkabidhi madawati mwalim Mkuu msaidizi wa Shule ya Msingi Kerezange dar es Salaam.
Mbunge
wa jimbo la Ukonga, Mwita Waitara, akimkabidhi mpira mwalimu wa michezo
wa shule ya Msingi Kilimani, Abdull Mukhusin, iliyopo Kipunguni wakati
alipoenda kukabidhi madawati kwa shule tatu.
Mbunge
wa jimbo la Ukonga, Mwita Waitara akisalimiana na wanafunzi wa shule
ya msingi Kilimani iliyopo Kipunguni wakati alipoenda kukabidhi
madawati kwa shule tatu za jimbo lake.
Mbunge
wa jimbo la Ukonga, Mwita Waitara akiongea na wanafunzi wa Shule ya
msingi Kilimani iliyopo Kipunguni wakati alipoenda kukabidhi madawati
kwa shule tatu za jimbo lake.
Picha na Mpiga Picha Wetu
MAWAZIRI WA MAJI AFRIKA WATEMBELEA CHANZO CHA MAJI CHA RUVU CHINI
Meneja
wa Mtambo wa Ruvu Chini Mhandisi Emmanuel Makusa akiwaelezea baadhi ya
Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika waliotembelea mtambo huo kujifunza
namna Tanzania inavyojidhatiti kuwapatia maji wananchi wake.
Baadhi
ya Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika wakitembelea maeneo mbalimbali ya
mtambo Ruvu Chini kujifunza namna Tanzania inavyojidhatiti kuwapatia
maji wananchi wake.
Naibu
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwewe akiwaeleza baadhi
ya Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika namna mradi wa Ruvu Chini
unavyowahudumia baadhi ya wakazi wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani na
wakazi wa mkoa wa Dar es salaam.
Mhifadhi
wa Mji Mkongwe wa Bagamoyo Noel Laswai akiwaeleza baadhi ya Mawaziri wa
Maji wa nchi za Afrika namna mji wa kale wa Kaole ulivyokuwa tangu
karne ya 13.
MAKAMU WA RAIS AHUTUBIA KWENYE MKUTANO WA KUMI WA BARAZA LA MAWAZIRI WA MAJI AFRIKA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia kwenye Mkutano wa Kumi wa Baraza la Mawaziri wa Maji katika
Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Convention Center ,Dar es Salaam
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge
wakati wa Mkutano wa Kumi wa Barazala La Mawaziri wa Maji
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mkutano huo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
amewaambia wajumbe wa mkutano wa kumi wa Baraza la Mawaziri Afrika kuwa
muda umefika wa kuacha kuongea na kuweka mkazo kwenye kutelekeza
malengo tuliyojiwekea ya kufikia dira ya maji ya Afrika ya mwaka 2025
Ikumbukwe
ya kwamba misaada kutoka kwa wafadhili inakikomo kwa hivyo ni muhimu
kwa nchi kujiwekea malengo ambayo miradi hiyo itaendelea kuwepo hata
misaada ikifika kikomo.
Ushirikiano
katika matumizi ya vyanzo vya maji ambavyo vinapakana na nchi zetu
Kuendelea kutumia mipango ya ushirikiano iliyopo kama vile ili
kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa bara la Afrika
Taasisi za kifedha za bara kama vile Benki ya Maendeleo ya Afrika iwe
katika mstari wa mbele wa kuunda na kupanga mikakati itakayosaidia ili
kuhamasisha upatikanaji vya fedha
aliwaomba
kuwa azimio litakalofikiwa litoe muongozo kwa wadau wote wakiwemo
washirika wa maendeleo kuhusu namna nchi wanachama wanaweza kukabiliana
na changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama ili kuweza kufikia
dira ya Afrika ya maji ya mwaka 2025 na goli namba 6 la malengo ya
maendeleo endelevu.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
No comments :
Post a Comment