EALA EULOGISES HON HAFSA MOSSI AT SPECIAL SITTING
The
Speaker, Rt Hon Daniel F. Kidega communicates to the Assembly at the
start of the Special Sitting. In the foreground is Clerk, Kenneth Madete
(left) and Senior Clerk Assistant, Stephen Mugume
It was an emotional send-off for the late Hon Hafsa Mossi at a one-day
Special Sitting held in Arusha yesterday with EALA legislators
condemning in the strongest terms possible, the despicable, brutal and
dastardly murder.
With that, the Assembly underscored
the need for instituting independent investigations by credible
organization(s) to unearth the killers of the late Hon Mossi, while
remaining resolute that peace, security and stability should be
immediately restored in Burundi.
The
Resolution which condemned the killing of the fallen legislator while
paying special tribute to her, was moved by the Chair of the Committee
on Legal Rules
Privileges, Hon Peter Mathuki, seconded by Hon Dora Byamukama and
supported by the entire House.
In
the foregoing, the Assembly urged the Summit of EAC Heads of State to
ensure the on-going mediation deliberations are taken seriously by all
parties.
“The Assembly
calls
upon the Summit of the East African Community Heads of State to reign
in their powers and authority and take such stern measures as to ensure
that both sides in Burundi take the
ongoing mediation efforts seriously so that peace, security and
stability are restored in the said country in shortest time possible”, a section of the Resolution read.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI ATEMBELEA CHUO CHA USAFIRISHAJI
Mkuu
wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa
akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Eng. Edwin Ngonyani alipotembelea Chuo hicho kukagua miundombinu yake.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akitoa
maelekezo kwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof.
Zacharia Mganilwa kuhusu namna nzuri ya kukiwezesha Chuo hicho
kujiendesha kwa faida na kuboresha miundombinu yake.
Mkuu
wa Kitengo cha Uhandisi wa anga katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji
NIT Eng. Azizi Mdimi akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani injini ya ndege inayotumia kwa mafunzo
wakati alipokagua Hanga katika chuo hicho.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua
ndege inayotumiwa kufundishia wanafunzi wanaosomea utengenezaji wa ndege
na urubani alipotembelea Chuo cha Usafirishaji NIT.
WANACHAMA WA CUF KUPIGA HODI KWA IGP MANGU ENDAPO ATAENDELEA KUKIFUATILIA CHAMA HICHO
Naibu
Katibu Mkuu wa chama hicho, Tanzania Bara, Shaweji Mketo, akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam , wakati wa kutoa msimamo wa chama
hicho kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi dhidi ya vyama vya siasa hasa
cha Cuf. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Ulinzi Taifa, Mustafa Wandu na
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed
Mazrul.
MKURUGENZI wa Uchaguzi wa Chama cha Wananchi (CUF) Shaweji Mketo amesema iwapo Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu ataendelea kukifuatilia chama hicho wanachama wa chama hicho watekwenda ofisini kwake kumsalimia.
Mketo ameyasema hayo Makao Makuu ya Chama hicho Buguruni leo Dar es Salaam leo wakati Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrul alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msimamo wa chama hicho kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi dhidi ya vyama vya siasa hasa cha Cuf.
"Tunasema sisi Cuf hatumuogopi IGP na kama ataendelea kutufuatafuata haita pita wiki mbili tutamfuata kwenda kumsalimia ofisi kwake" alisema Mketo.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrulalisema chama hicho kimesikitishwa na kauli ya IGP aliyoitoa hivi karibuni wakati akihojiwa Tido Mhando wa Kituo cha Televisheni cha Azzam kuwa jeshi hilo wakati wowote litamkamata Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuwachochea wafuasi wake ili waichukie serikali iliyopo madarakani.
Alisema baada ya kuitafakari kauli hiyo ya IGP wamebaini kwamba hivi sasa IGP Mangu ameamua kuwathibitishia watanzania kuwa jeshi la polisi ni idara maalumu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).Mazrul alisema kwa muda mrefu IGP Mangu amekuwa akilitumia jeshi la polisi kushiriki katika matukio mbalimbali ya kuhujumu demokrasia na kukiuka haki za binadamu kwa lengo la kukinusuru Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na anguko kubwa la kukataliwa na wananchi kama ilivyothibitika kabnla na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana.
Alisema jeshi la polisi limekuwa na utaratibu wa kukamata raia, kuwapiga kuwabambikia kesi, kuwashikilia na kuwatesa katika vituo vya polisi bila ya kuwafikisha mahakamani.
Mazrul alisema hadi sasa zaidi ya wananchi 400 wameathiriwa kutokana na hujuma za jeshi la polisi kwa kuwabambikia kesi.
Naibu
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrul
(wa nne kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo,
wakati akitoa msimamo wa chama hicho kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi
dhidi ya vyama vya siasa hasa cha Cuf. Wengine ni maofisa mbalimbali wa
chama hicho.
MAWAZIRI WA MAJI AFRIKA WATEMBELEA CHANZO CHA MAJI CHA RUVU CHINI
Meneja
wa Mtambo wa Ruvu Chini Mhandisi Emmanuel Makusa akiwaelezea baadhi ya
Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika waliotembelea mtambo huo kujifunza
namna Tanzania inavyojidhatiti kuwapatia maji wananchi wake.
Baadhi
ya Mawaziri wa Maji wa nchi za Afrika wakitembelea maeneo mbalimbali ya
mtambo Ruvu Chini kujifunza namna Tanzania inavyojidhatiti kuwapatia
maji wananchi wake.
MH. JAFFO ASEMA UPENDO NDIO MSINGI WA UTUMISHI BORA
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa Mh Stephen Mhapa ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa ALAT akimpokea Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mh. Seleman Jaffo katika ukumbi wa siasa ni kilimo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mh. Seleman Jaffo amefanya ziara katika halmashauri ya Iringa ambapo alipokelewa na Mkuu wa wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela akiongozana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa Mh Stephen Mhapa.
Katika ziara hiyo alikagua miradi ya maendeleo na kufungua miradi ya vyoo katika shule ya msingi Mikongati tarafa ya Kalenga, maabara ya zahanati ya Kising'a na madarasa ya shule ya sekondari Mikongati.
Pia alizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Iringa. Katika hotuba yake Mh Jafo alisistiza suala la upendo kazini na kujenga nidhamu katika utendaji. Pia aliwaomba wananchi watunze miradi iliyo kamilika ili idumu muda.
Akimkaribisha Naibu Waziri, Mheshimiwa Kasesela aliomba seriakli kuharakisha fedha ili kukamilisha miradi ya maji na barabara, pia kuomba uwezekano kila barabara zinapo jengwa yatengwe maeneo kwa ajili ya emergence unit ili kuokoa miasha ya watu mara ajali zinapotokea.
Aiendelea " leo Mh waziri umezindua maabara hapa Kising'a lakini eneo hili lipo barabara kuu ya kuelekea Dodoma ajali zinapotokea tunapata tabu sana kuokoa maisha ya wananchi ni muhimu sasa Tanroads wana disign barabara mpya ziwepo pia fedha za kujenga vituo vya dharura ambavyo vyawezwa kuunganishwa na vituo vya kupumzikia wananchi ili halmashauri zetu zipumue mara yatokeapo majanga".
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akisoma taarifa ya wilaya kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mh. Seleman Jaffo (kulia) huku Katibu Tawala Bwana Joseph Chitinka ( Kushoto) akisililiza.
Pia akiongea kwenye mkutano wa watumishi Mkurugenzi wa halmashauri Bwana Robert Munyusi pamoja na Katibu tawala wilaya ya Iringa Bwana Robert Chitinka wote kwa pamoja walimpongeza Naibu waziri kwa kasi kubwa ya utendaji kazi wake.
Ziara ilimalizika kwa kumtembelea Mwalimu aliye fiwa na mwanae wakati ziara ikiendelea. Naibu waziri aliwafariji wafiwa na kutoa ubani kisha kuendelea na safari kuelekea Dodoma.
KAUNTI YA KISII NCHINI KENYA YAPIGA MARUFUKU WANAFUNZI KUUZIWA PETROLI
Vituo
vya mafuta katika Kaunti ya Kisii nchini Kenya vimepigwa marufuku
kuwauzi mafuta ya petroli watoto, kufuati wimbi la uchomaji moto
shule.
Kamishna
wa Kaunti ya Kisii, Kula Hache, amesema uamuzi huo umefikiwa na
kamati ya ulinzi katika mkutano wao.
Amesema
wanunuzi wa petroli watakaokaidi kuonyesha vitambulisho vya taifa
katika vituo vya mafuta wasiuziwe mafuta.
No comments :
Post a Comment