WAZIRI wa nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Jenista
Mhagama, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa
Pensheni wa PPF, na tuzo waliyotwaa ya ushindi wa kwanza kundi la Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii na Makampuni ya Bima kwenye maonesho ya 40 ya biashara ya
Kimataifa ya Dar es Salaa, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
Julai 2, 2016. Waziri aliupongeza Mfuko huo kwa kuibuka mshindi wa kwanza kundi
la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Makampuni ya Bima na kuitaka mifuko mingine
kufanya juhudi ili kufikia mafanikio hayo.
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi,
Vijana na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akimkabidhi Vumilia Joseph
Twigela, kadi ya uanachama wa Mfuko wa
Pensheni wa PPF, kupitia mfumo maalum wa
kuchangia unaohusisha watu wote wenye kipato, ujulikanao kama Wote Scheme,
wakati alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 40 ya biashara ya
kimataifa ya Dar es Salaam.
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi,
Vijana na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, ameupongeza Mfuko wa Pensheni wa
PPF, kwa kupata tuzo ya mshindi wa kwanza kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
na Makampuni ya Bima, kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dares
Salaam.
Biashara yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwananchi akitoa maoni yake katika mashine maalum baada ya kupata huduma kwenye Banda la
Maonesho la Mfuko wa Pensheni wa PPF,
Maonesho ya KImataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mwajuma
Msina, akimkabidhi Kitambulisho Mwanachama Mohamed Hassan (23) aliyejiunga na
huduma ya ‘Wote Scheme’ wakati alipotembelea kwenye Banda la Maonesho la Mfuko
huo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya
Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
***************************************
Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi,
Vijana na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, ameupongeza Mfuko wa Pensheni wa
PPF, kwa kupata tuzo ya mshindi wa kwanza kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
na Makampuni ya Bima, kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dares
Salaam.
Waziri alitoa pongezi hizo wakati alipotembelea banda la
PPF mwishoni mwa wiki ambapo alitoa changamoto kwa Mifuko mingine kufanya
juhudi ili kufikia mafanikio ambayo PPF imeyapata.
Waziri Mhagama ambaye alikuwa akitembelea Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii ambayo iko chini ya Wizara yake inayoshiriki maonyesho hayo,
alishuhudia wafanyakazi wa Mfuko huo wakitoa huduma mbalimbali kwa wananchi
waliofika kutembelea banda hilo ambapo miongoni mwa kazi alizofanya Waziri
Mhagama, ni kumkabidhi kadi mpya ya uanachama, Vumilia Joseph Twigela, ambaye
yeye pamoja na mfanyakazi wake wa ndani walijiunga na mfumo maalum wa kuchangia
unaohusisha watu wote wenye kipato, ujulikanao kama Wote Scheme.
“Ninawapongeza kwa kuibuka kidedea mbele ya Mifuko
mingine, na nitoe wito kwa wengine kufanya juhudi ili kufikia mafanikio yenu.”
Alisema Waziri Mhagama ambaye alifuatana na Maafisa wa Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, alitembelea idara ya uendeshaji ambayo
inahusika na utoaji elimu na kujiunga na uanachama.
Pia alitembelea idara ya Michango ya wanachama ambapo
Waziri alipewa maelezo ya kina kuhusu huduma zitolewazo na wafanyakazi wa PPF
kwa wanachama wanaofika kupatiwa huduma.
Hali kadhalika Waziri Mhagama alitembelea kurugenzi ya
uwekezaji na kuupongeza Mfuko huo kwa kuanza kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa
Rais ambaye alitaka Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuwekeza kwenye viwanda ili
kutengeneza ajira zaidi na kupata wanachama wengi.
No comments :
Post a Comment