Wanafunzi
wa chuo Cha Uhasibu (TIA), jijini Dar es Salaam, wakipatiwa maelezo ya huduma
mbalimbali zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF walipotembelea banda la
Mfuko huo lililoko jingo la Wizara ya fedha kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara
ya Kimataifa ya Dar es Salaam, 2016 viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es
Salaam Julai 2, 2016. (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, (kulia), akizungumza jambo
wakati alipotembelea banda la Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwenye jingo la wizara
ya fedha viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 2, 2016 ambako
yanafanyika maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam. Hapa
waziri akipatiwa maelezo na Afisa Uendeshaji wa PSPF, Hadji Hamisi Jamadari
Afisa Kumbukumbu wa Mfuko Pensheni wa PSPF,
Lupakisyo J. Mwaipungu (kushoto), akimsikiliza Mwananchi huyu aliyetembelea
banda la Mfuko huo na kuamua kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari PSS
Julai 2, 2016
Baada
ya kueleweshwa umuhimu wa kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari
ambao una mafao mengi, mwananchi huyu akijaza fomu za kujiunga na mpango
huo
Wananchi wakijaza fomu na kuweka alama ya dole gumba kwenye fomu za kujiunga na mpango wa PSS
Mwananchi huyu akisoma kipeperushi chenye maelezo ya kina ya huduma zitolewazo na PSPF
Afisa
Uendeshaji wa PSPF, Hadji Hamisi Jamadari, akiwapa somo wananchi
waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye jengo la Wizara ya Fedha
Afisa wa PSPF, (Kulia), akimpatia maelezo mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo
Wanafunzi
wa chuo Cha Uhasibu (TIA), jijini Dar es Salaam, wakipatiwa maelezo ya huduma
mbalimbali zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF walipotembelea banda la
Mfuko huo lililoko jingo la Wizara ya fedha kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara
ya Kimataifa ya Dar es Salaam, 2016 viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es
Salaam Julai 2, 2016
Afisa wa PSPF, (Kulia), akimpatia maelezo mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo
Wananchi hawa (kulia), wakisikiliza kwa utulivu maelezo kutoka kwa maafisa wa PSPF kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko huo
Afisa
Uendeshaji wa PSPF, Hadji Hamisi Jamadari, (kushoto), akiwapatia
maelezo wanafunzi wa Chuo Cha Uhasibu (TIA) jijini Dar es Salaam,
walipotembelea banda la Mfuko huo
Mkuu wa wilaya mpya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella leo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi |
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Mhandisi Mwanaisha Rajabu akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martne Shigella |
Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Abdallah Issa akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga leo. |
Mkuu wa wilaya Mpya wa Handeni Mkoani Tanga,Godwin Gondwe akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella |
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Robert Gabriel akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella anayeshuhudia kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Said. |
Mkuu wa wilaya Mpya wa Handeni Mkoani
Tanga,Godwin Gondwe kulia akitete jambo na Mwandishi wa ITV na Radio One
Mkoani Tanga,William Mngazija mara baada ya kuapishwa
Mwananchi akitoa maoni yake katika mashine maalum baada ya kupata huduma kwenye Banda la
Maonesho la Mfuko wa Pensheni wa PPF,
Maonesho ya KImataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwananchi akitoa maoni yake katika mashine maalum baada ya kupata huduma kwenye Banda la
Maonesho la Mfuko wa Pensheni wa PPF,
Maonesho ya KImataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, (katikati), akizungumza jambo
wakati alipotembelea banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwenye
maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya
Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 2, 2016. Kulia ni Afisa Uhusiano wa
WCF, Zaria Mmanga, na kushoto ni Mhasibu wa Mfuko huo, Grace Tarimo
NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista
Mhagama, ameutaka Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), kujiweka tayari kulipa
mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi kama ambavyo Sheria ilivyoelekeza.
Waziri Mhagama aliyasema hayo leo Julai 2, 2016
wakati alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
inayoshiriki kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa, kwenye viwanja
vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Mifuko ya Hifadhi ya Jamii iko chini
ya Ofisi yake.
“Najua mnatakiwa kuanza kulipa fidia mwezi huu wa
Julai, vipi mko tayari na kama bado basi mjiweke tayari kufanya hivyo.” Alisema
Waziri.
Akimjibu Waziri Mhagama ambaye alifuatana na
maafisa wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii,
(SSRA), wakiongozwa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka
hiyo, Sarah Kibonde Msika, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Fulgence Sebera
alimwambia Waziri kuwa Mfuko umejiandaa kikamilifu kutoa fidia kwa wafanyakazi
ambapo elimu ilitolewa kwa wadau wengi wakiwemo madaktari kote nchini
watakaowafanyia tathmini wafanyakazi waliopata madhara mahala pa kazi.
Sebera pia alitoa wito kwa wadau kutembelea banda
la WCF ili kujipatia maelezo ya kina ,kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko huo
ikiwemo Fidia kwa Wafanyaakzi ambayo inaanza kutolea Julai mosi mwaka huu wa
2016.
Banda la WCF liko kwenye ukumbi wa Sabasaba kwenye viwanja vya
Mwalimu Nyerere.
Waziri akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakzi wa WCF, na maafisa wa SSRA
Afisa Uhusiano wa WCF, Zaria Mmanga, (Kushoto), akimpatia maelezo mwananchi huyu aliyetembelea banda la WCF
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi, (WCF), Masha Mshomba, (kulia), akijadiliana jambo na Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Fulgence Sebera, nje ya banda la WCF kwenye
maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam jijini Dar es
Salaam
Grace Tarimo, (kulia), Afisa wa fedha wa WCF, akimpatia maelezo mwananchi aliyetembelea banda la Mfuko huo
Waziri akiagana na Mkuu wa kitengo cha
Mawasiliano, Wizara ya Fedha na Mipango, Ben Mwaipaja, baada ya
kutembelea Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwenye Jengo la Wizarabya Fedha,
kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 2, 2016.
Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano cha SSRA, Sarah
Kibonde Msika
Zaria akimpatia maelezo mwananchi aliyetembelea banda la WCF
No comments :
Post a Comment