Wakonta
Kapunda : Msichana mwenye umri wa miaka (22) akitumia ulimi kuandika
meseji kwenye simu yake ya Mkononi wakati wa mkutano wake na waandishi
wa habari leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Dada yake Bi. Judith
Assenga.Binti huyo ameanza kutumia kiungo hicho katika kuandika baada ya
kupooza sehemu ya mwili wake kutokana na ajali mbaya aliyoipata mwaka
2012 akiwa na wenzake tisa wakati wa Mahafali ya Kidato cha Sita katika
Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe Mkoani Tanga.
Msichana
mwenye umri wa miaka (22) Bi. Wakonta Kapunda akifanya mahojiano maalum
na mwandishi wa Radio ya Kimataifa ya Ufaransa (Rfi) wakati wa mkutano
wake na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Binti huyo
anatumia ulimi na simu aina ya Smart Phone katika kuandika
baada ya kupooza sehemu ya mwili wake kutoka na ajali mbaya aliyoipata
mwaka 2012 akiwa na wenzake tisa Korogwe Mkoani Tanga.
Judith
Assenga(kushoto) dada yake na Wakonta Kapunda akimuelekeza jambo mdogo
wake wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Wakonta anatumia ulimi na simu aina ya Smart Phone katika
kuandika baada ya kupooza sehemu ya mwili wake kutoka na ajali mbaya
aliyoipata mwaka 2012 akiwa na wenzake tisa Korogwe Mkoani Tanga.
Mratibu
wa Masuala ya Habari katika Kampeni ya kumsaidia Wakonta Bw. Joseph
Kithama akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) namba ambazo
wadau wanaweza kutumia kumchangia Binti huyo anayehitaji msaada ili
apatae matibabu na kutimiza ndoto zake za kwasaidia wengine wenye
matatizo kama yake leo jijini Dar es Salaam.
Kutoka
kulia ni Wakonta Kapunda, Judith Assenga(dada yake na Wakonta), Mwajuma
Selkemani na Chritina Rubangula(waliokuwa wanafunzi wenzake na Wakonta)
wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Wakonta anatumia ulimi na simu aina ya Smart Phone katika
kuandika baada ya kupooza sehemu ya mwili wake kutoka na ajali mbaya
aliyoipata mwaka 2012 akiwa na wenzake tisa Korogwe Mkoani Tanga.
Vyuo vikuu vyatakiwa kuunga mkono Serikali katika kujenga Tanzania ya Viwanda
Na: Lilian Lundo – MAELEZO
……………………………………..
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amevitaka vyuo vikuu Tanzania
kuunga mkono serikali ya Awamu ya Tano juu ya uanzishwaji wa viwanda
kuelekea uchumi wa kati.
Prof. Ndalichako ameyasema hayo
leo katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua
maonyesho ya kumi na moja ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia
yatakayofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Julai 20 mpaka Julai 22 mwaka
huu.
“Vyuo vikuu vinatakiwa kuangalia
sera za nchi na mwelekeo wa Taifa kuelekea kukuza uchumi wa viwanda kwa
kuhakikisha wanatoa wataalamu ambao watashiriki katika uchumi wa viwanda
ambavyo vitaanzishwa nchini,” alifafanua Prof. Ndalichako
Prof. Ndalichako aliendelea kwa
kusema kuwa Serikali iko katika mkakati wa kuboresha vyuo vya ufundi kwa
kuanzia na vyuo vitatu vya ufundi vya Dar es Salaam, Arusha na Mbeya
ili kuboresha mafunzo wanayoyatoa kuendana na uhitaji uliopo katika
uanzishwaji wa viwanda.
Mbali na hayo, Wizara ya Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi inashirikiana na Wizara ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji katika uanzishwaji wa mafunzo katika
sekta adimu ikiwemo gesi kwa ajili ya kupata wataalamu watakaoajiriwa
katika viwanda vitakavyo anzishwa.
Vile vile wanafunzi wanaotarajia
kujiunga na vyuo vikuu hupewa maelekezo ya namna ya kuomba vyuo kupitia
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) pamoja na Baraza la Taifa la Elimu ya
Ufundi (NACTE) katika maonyesho hayo.
Maonyesho ya Elimu ya Juu, Sayansi
na Teknolojia hufanyika kila mwaka yakiwa na Lengo la kutoa elimu kwa
wazazi na wanafunzi wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu hapa nchi waweze
kujua kozi zinazotolewa katika vyuo hivyo pamoja na maelezo ya kozi
hizo.
Wadau wa Maafa wajengewa uwezo kuandaa Kanzi Data ya Athari za Maafa.
Mratibu
wa Maafa Shirika la Umoja wa Mataifa la Upunguzaji Athari za Maafa
(UNISDR) Bw.Adam Fysh akielezea jambo wakati wa mafunzo ya kuandaa Kanzi
Data ya Masuala ya Athari za Maafa yaliyofanyika tarehe 19 na 20 Julai,
2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
Baadhi
ya wadau wa masuala ya maafa wakifuatilia maelezo kutoka kwa Mratibu wa
Maafa Shirika la Umoja wa Mataifa la Upunguzaji Athari za Maafa
(UNISDR) Bw.Adam Fysh (hayupo pichani) wakati wa mafunzo ya kuandaa
Kanzi Data ya Athari za Maafa nchini yaliyofanyika kuanzia tarehe 19-20
Julai, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mratibu
wa Maafa Shirika la Umoja wa Mataifa la Upunguzaji Athari za Maafa
(UNISDR) Bw.Adam Fysh akitoa ufafanuzi kwa kikundi ‘A’ cha majadiliano
wakati wa mafunzo ya kuandaa Kanzi Data ya Athari za Maafa yaliyofanyika
katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Julai 19 na 20, 2016.
Mkurugenzi
wa Idaya ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Brig. Jenerali, Mbazi
Msuya (katikati mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na
wadau wa masuala ya maafa mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya kuandaa
Kanzi Data ya Athari za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kulia kwake ni
Mratibu wa Maafa Shirika la Umoja wa Mataifa la Upunguzaji Athari za
Maafa (UNISDR) Bw.Adam Fysh.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
…………………………………………………………………………………………….
Na. MWANDISHI WETU
Shirika la Umoja wa Mataifa la
Upunguzaji Athari za Maafa (UNISDR) kwa kushirikiana na Idara ya Uratibu
wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu wameendesha mafunzo ya siku mbili kwa
wadau wa masuala ya maafa juu ya namna ya kutumia Kanzi Data ya takwimu
za Athari za Maafa kutoka Wizara na Taasisi za Serikali nchini.
Mafunzo hayo yalifanyika Julai 19
na 20, mwaka huu katika Ofisi ya Waziri Mkuu na kushirikisha Wizara na
Taasisi za Serikali ikiwemo; Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya
Ulinzi na Usalama wa Taifa, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Jeshi
la Zima Moto, Jeshi la Polisi, Mamlaka ya Hali ya Hewa, Mamlaka ya
Usafiri wa Majini na Nchi Kavu, TAMISEMI, Chuo Kikuu cha Ardhi, Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Mafunzo hayo yalijikita katika
kusaidia wadau wa masuala ya maafa katika kuongeza uwezo wa kuwa na
Takwimu sahihi za majanga yanayoikabili Nchi ya Tanzania.
Akizungumza wakati wa Mafunzo hayo
Mratibu wa Masuala ya Maafa Shirika la Umoja wa Mataifa la Upunguzaji
Athari za Maafa, Bw. Adam Fysh alieleza kuwa, Mafunzo
hayo yatasaidia kuongeza uboreshaji wa kumbukumbu za maafa nchini, “kama
ilivyokusudiwa, mafunzo yatasaidia kuwa na rekodi za kutosha,
yatasaidia ufuatiliaji, kuwa na tathimini za mara kwa mara, na
ulinganifu wa kujua nchi zingine zinafanya nini katika kukabiliaana
na athari za maafa, mafunzo haya pia yatasaidia wahusika kufanya maamuzi
sahihi na kwa wakati katika maendeleo hususani kwa kupunguza athari za
maafa hapa nchini”
Bw. Fysh aliongeza kuwa kiu yake
ni kuona nchi zinajikita katika utoaji wa taarifa zenye uhalisia na
sahihi ili kuwa na kumbukumbu na takwimu zenye kusaidia Dunia kujua
maafa yanayotokea, “Natamani kuona tunakuwa na takwimu sahihi na zenye
mpangilio zinazohusu athari za maafa hususani yanayoikabili nchi’
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Idaya ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig. Jenerali, Mbazi
Msuya alishukuru jitihada za Shirika hilo kwa kuona umuhimu wa
kuwajengea uwezo wadau wa masuala ya Maafa na kueleza kuwa mafunzo hayo
yamekuja kwa wakati na yataleta manufaa makubwa kwa Taifa.
“Nawapongeza Shirika kwa kuona ni
vyema kuifikia Tanzania kwa kuijengea uwezo wa namna ya kuweka taarifa
muhumu za masuala ya Maafa katika kanzi data. Hii itatusaidia sana
katika kupanga mipango yetu kwa namna bora zaidi na vile vile itarahisha
katika kufuatilia kufanya tathmini”, Alisema Brig. Msuya
Naye Mtaalam wa Masuala ya Hali ya
Hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa, Bi.Hellen Msemo
alieleza kuwa mafunzo hayo yatasaidia kutoa fursa za kimaendeleo kwakuwa
takwimu za athari za maafa zitasaidia kuwa na mipango mizuri ya
maendeleo ya nchi na kuipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuona umuhimu
wa kuratibu mafunzo hayo.
Mafunzo ya kutumia Kanzi Data ya
takwimu za Athari za Maafa tayari yamezifikia nchi 31 duniani huku
Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi kumi na tatu za Afrika zilizonufaika
na elimu hiyo.
MWIGULU NCHEMBA ASHIRIKI KONGAMANO LA VIONGOZI WA DINI
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (wapili kulia)
akisalimiana na Katibu Mkuu wa Baraza la Kuu la Waislamu (BAKWATA),
Suleman Said Lolila wakati Waziri huyo alipokuwa anawasili katika Hoteli
ya Serena, Dar es Salaam, kwa ajili ya kushiriki Kongamano la Viongozi
wa Dini lililojadili masuala ya ugaidi. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya
Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba, na wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa
Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Dk Leonard Mtaita.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba akizungumza na viongozi
wa dini kuhusu masuala mbalimbali ya amani nchini katika Kongamano la
Viongozi wa Dini lililofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es
salaam. Katika hotuba yake, Waziri Mwigulu aliwataka viongozi hao
kutokuhusisha kosa lifanyalo na mtu au watu fulani kulifananisha na dini
yake, amewaomba viongozi hao watoe ushirikiano kwa kutoa taarifa za
matukio mbalimbali ya kiuhalifu nchini. Kutoka kulia ni Askofu Mkuu wa
Jimbo Kuu Katoliki Tabora, Paul Ruzoka, Mufti Mkuu wa Tanzania,
Abubakary Zubeiry Bin Ally na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo
Tanzania (CCT), Dk Leonard Mtaita.
Sehemu
ya viongozi wa dini walihudhuria katika Kongamano la Viongozi wa Dini
nchini lililofanyika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Kongamano
hilo ambalo lilihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu
M.L Nchemba (hayupo pichani), lilijadili masuala mbalimbali ya ugaidi
pamoja na ushirikiano wa dini mbalimbali nchini. Hata hivyo Waziri
Mwigulu aliwataka viongozi hao kutokuhusisha kosa lifanyalo na mtu au
watu fulani kulifananisha na dini yake, amewaomba viongozi hao watoe
ushirikiano kwa kutoa taarifa za matukio mbalimbali ya kiuhalifu nchini.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (watatu kulia) akiandika
maelezo ya hotuba ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT),
Dk Leonard Mtaita (kushoto) katika kongamano la viongozi wa dini
lililofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Kongamano
hilo lilijadili kuhusu ugaidi na ushirikiano wa madhehebu mbalimbali ya
dini nchini. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Mstaafu, Alex
Malasusa. Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakary Zubeiry Bin Ally (wapili
kushoto), Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora, Paul Ruzoka (watatu
kushoto) na Mufti wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar.
Mkurugenzi
wa Idara ya Sheria wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin Komba
akimfafanulia jambo Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakary Zubeiry Bin Ally
(kushoto) mara baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L
Nchemba (hayupo pichani) kuzungumza na viongozi wa dini kuhusu masuala
mbalimbali ya amani nchini katika Kongamano la Viongozi wa Dini
lililofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Afisa Sheria wa Wizara hiyo, Berious Nyasebwa.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
MKAZI WA MLANDIZI KIBAHA PWANI APATA UPOFU BAADA YA KUMEZA DAWA AINA YA FANSIDER AOMBA MSAADA ML.18
Seleman
Mgoto ambaye amepoteza uwezo wa kuona kabisa macho yake mawili baada ya
kutumia dawa hizo wakati akizungumza na waandishi kuhusina na
changamoto aliyonayo na kuomba msaada kwa wadau mbali mbali kuweza
kumsaidia.
Dada
wa Seleman Mgoto Luiza Mdachi wakati aliozungumza na waandishi
kuhusiana na matatizo aliyiyapata kaka yake ya kupoteza kabisa uwezo wa
kuona na jinsi familia yake ambayo ipo katika wakati mgumu.
(PICHA NA VICTOR MASANGU).
……………………………………………………………………………………………
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA PWANI
MKAZI
mmoja ajulikanaye kwa jina la Seleman Mgoto (42)anayeishi katika
kitongoji cha Janga kilichopo eneo la Mlandizi Wilayani Kibaha Mkoa wa
Pwani ameathirika macho yake mawili na kupoteza kabisa uwezo wa kuona
baada ya kutumia dawa ya kutibu malaria aina ya Fansider hivyo
anahitaji msaada wa kiasi cha shilingi milioni 18 kwa ajili ya kwenda
kupatiwa matibabu zaidi nchini India.
Hayo
yamebainika baada ya mwandishi habari hizi kuweza kufika nyumbani kwa
kaka yake maeneo ya mlandizi ambapo ndipo anapoishi kwa sasa baada ya
kupatwa na tatizo hilo na kuweza kuzungumza naye kuhusiana na mkasa wa
tukio hilo lililompata.
Akizunguza
kwa masikitiko makubwa Mgoto alisema kwamba mnano agosti 2012
alikuwa anaumwa na alipokwenda kupimwa aligundulika kuwa na wadudu
tisa wa ugonjwa wa malaria ndipo alipoandika dawa aina ya fansider na
kuamua kwenda kuzinunua katika moja la duka la madawa lililopo maeneo
hayo ya mlandizi na baada ya kuzimeza hali yake baada ya siku mbili
ilianza kubadilika kutokana na sumu kali iliyokuwepo mwilini mwake .
“Mimi
mwezi agosti mwaka 2012 ndugu zangu waandishi niliweza kuumwa na
nilipoenda kupima afya niligundulika nina malaria, na baada ya hapo
niliweza kuandikiwa dawa na nikaenda kununua dawa aina ya fansider, ila
baada ya siku mbii hali yangu iiweza kubadilika na nilipokwenda kituo
cha afya niilazwa kwa ajili matibabu zaidi,”alisema.
Aidha
akifafanua kuhusina na kuangaika katika hospitali mbali mbali kwa ajili
ya matibabu alisema kwamba mara ya mwisho alikwenda kuwaona madaktari
bingwa wa hospitari ya CCBRT ya jijini Dar es salaam ambapo walimwambia
macho yake kwa hapa Tanzania hayawezi kutibiwa mpaka aende nchini India
ndio yanaweza kupona.
Pia
katika hatua nyingine amesema kwamba kwa sasa maisha yake yamekuwa ni
magumu sana kutokana na kutokuwa na kipato chochote kile anachokiingiza
ukizingatia ana familia mke pamoja na watoto watatu ambao wanamtegemea
kwa kila kitu ambapo watoto wengine wawili wapo wanasoma sekondari
hivyo kunahitajika mahitaji mengine ya msingi.
Mwenyekiti
wa kamati maalumu ya kumsaidia kwenda kupatiwa matibabu nchini India
Eria Chaofu pamoja na Luiza Mdachi ambaye ni dada yake wamesema kwamba
familia imeangaika kwa hali na mali kwa kipindi cha miaka mitatu
katika hospitali mbali mbali kwa ajili ya kumtibia bila ya kupata
mafanikio yoyote kutokana na kutokuwa na uwezo wa kifedha. miaka mitatu
Aidha
Mwenyekiti huyo amemwomba Rais wa awamu ya tano Dr.John Mgufuli
kumsaidia mgonjwa huyo pamoja na wadau wengine wakiwemo wakuu wa wilaya,
wabunge, wakuu wa miko pamoja na Wizara ya afya ili aweze kwenda
kutibiwa na kurudi katika hali.
Kwa
mtu yoyote ambaye ameguswa na anahitaji kumsaidia mchango wake kwa
hali na mali Seleman Mgoto ambaye amepoteza uwezo wa kuona kabisa wa
macho yake mawili,atume kwa tigo pesa –0655-413939 au M-PESA 0754-413939 na akaunti namba NMB -80110000915 kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu nchini India kwani zinahitajika shilingi milioni 18.
No comments :
Post a Comment