Makonda awataka Wakuu wa Wilaya kuimarisha ulinzi na usalama
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda (kushoto) akimuapisha Mhe.Sophia
Mjema (kulia) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala leo katika Ukumbi wa Karimjee
Jijini Dar es Salaam.
Mhe.Sophia
Mjema (kulia) akionesha Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
pamoja na Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyokabidhiwa na Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) mara baada ya kuapishwa
kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala leo katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es
Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akimuapisha Mhe.Hashim
Mgandilwa (kulia) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni leo katika Ukumbi wa
Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akimuapisha Mhe.Felix
Lyaniva (kulia) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke leo katika Ukumbi wa
Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja
na Wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam (mbele) pamoja na
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam (nyuma)mara baada
ya kuisha kwa zoezi la kuapishwa lililofanyika leo nje ya Ukumbi wa
Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akimuapisha Mhe.Ally
Hapi (kulia) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni leo katika Ukumbi wa
Karimjee Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
……………………………………………………………………………………………
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Mhe. Paul Makonda amewataka Wakuu wapya wa Wilaya kuimarisha ulinzi na
usalama kwa wananchi waliopo katika Wilaya zao ili kudumisha amani.
Makonda alisema hayo leo jijini
Dar es Salaam wakati akizungumza na Wakuu wa Wilaya juu ya kuwalinda
wananchi na mali zao na kuhakikisha usalama unakuwepo katika Wilaya
wanazozisimamia.
Alieleza kuwa kwa kuwa wao ndio
wanaomuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli katika Wilaya zao, wanatakiwa kuhakikisha wametekeleza
ahadi zilizotolewa na Mhe. Rais wakati wa kampeni.
“Ningependa wakuu wangu wa Wilaya
mchukiwe kwa kusimamia Haki na Sheria kuliko kukumbatia uovu kwa
kuhitaji furaha ya muda mfupi, hakikisheni Sheria na Kanuni zilizopo
kwenye Katiba ndio ziwe muongozo wenu”, alisema Makonda.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es
Salaam aliwataka Wakuu wa Wilaya zake kuwasimamia Wakurugenzi wao ili
kuhakikisha wanatumia bajeti waliyopewa katika kutatua changamoto
zilizopo katika Wilaya zao.
Aidha, Makonda amewasisitiza
kuhakikisha kuwa kuanzia Julai 11 mwaka huu maeneo yote yanayofanya
biashara ya shisha kufungwa na kuweka maeneo maalumu kwa ajili ya
kuvutia sigara.
Wakuu wa Wilaya wapya wamepewa
wiki mbili za kutengeneza mpango kazi kwa kusoma ilani ya Chama cha
Mapinduzi (CCM), Hotuba ya Mhe.Rais John Magufuli aliyoisoma wakati wa
ufunguzi wa Bunge la 11 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na mazingira
ya kazi katika maeneo yao.
MOBISOL INTRODUCES LARGEST SOLAR HD TV IN EAST AFRICA DISPLAYED AT SABASABA FAIR
His Excellence Egon Kochanke Ambassador of the Federal Republic of Germany learning about Mobisol’s high quality solar appliances and HD solar Tv at Saba Saba Trade Fair.
Pic 2; Saba Saba visitor learning about Mobisol’s HD solar TV and solar home systems at the Mobisol booth in Nkurumah Hall at Saba Saba Trade Fair
—
Germany-based solar-service company Mobisol provides a range of solar home systems with an affordable payment plan and is currently showcasing its largest solar HD TV available at the ongoing Dar es Salaam International Trade Fair (Sabasaba).
Mobisol Tanzania Marketing Manager
Allan Rwechungura said that the largest solar HD TV recently launched
in other markets in East African countries has been optimized for the
use with Mobisol’s 200W Solar Home Systems.
“Our largest solar HD TV is of
high quality and comes with a two year warranty. Our customers can pay
for the solar TV using mobile money in convenient installments, as they
acquire the high quality TV together with their Mobisol solar system.
The TV was recently awarded by the The Global Lighting and Energy Access
Partnership as one of the best off grid appliances and is featured in
their 2016 guide for outstanding solar and off-grid appliances. We
encourage people to visit us at Sabasaba in Nkurumah Hall to see our
products; apart from the TV buyers can also acquire other solar-powered
appliances such as haircutters, music systems and radios, irons and
business solutions such as multiple phone chargers. Mobisol is also
focusing on conserving the environment – while, at the same time, the
electricity we provide offers an opportunity for people to utilize it
for various income generating activities which improve their economic
wellbeing”.
To date, Mobisol has installed
over 50,000 solar home systems across East Africa. Their systems come in
varying sizes from 80 to 200 Wp to match the various energy needs of
different households and its solar home systems provide enough
electricity to power entire households or businesses with bright LED
lights, and run radios, charge mobile phones and power a variety of
household and consumer appliances.
The larger systems can also power
small businesses enabling entrepreneurial customers to create additional
income. Mobisol has shops in most parts of Tanzania that are popular
known as MobiShop.
In 2015, Mobisol won the United
Nations Framework Convention on Climate Change (UNFCCC)’s Momentum for
Change Award and also a TV was recently awarded by LEAP as one of the
best off grid appliances and is featured in their 2016 guide for
outstanding solar and off-grid appliances.
“The Global Lighting and Energy
Access Partnership (Global LEAP) is the Clean Energy Ministerial’s
energy access initiative, and is led by the U.S. Department of Energy.
Global LEAP was launched as a commitment to the Sustainable Energy for
All campaign, and its programs and initiatives support the growth of
sustainable commercial clean energy access markets throughout the
developing world.
AGIZO LA KUZUIA UVUTAJI WA SIGARA NA MATUMIZI YA BIDHAA ZA TUMBAKU KATIKA MAENEO YA UMMA.
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inampongeza
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kupiga
marufuku matumizi ya Shisha na uvutaji wa Sigara hadharani kama afua ya
kupunguza madhara ya tumbaku na madawa ya kulevya katika jamii.
Uchunguzi wa kitalaam uliofanyika
umebaini kuwa Shisha ina madhara kwa afya ya watumiaji hasa vijana na
watoto. Watumiaji wa Shisha wanatumia kiwango kikubwa cha tumbaku kwa
muda mfupi, hali inayoongeza madhara yatokanayo na tumbaku kama vile: –
Saratani, Magonjwa ya Mapafu, Kibofu cha mkojo, Tezi dume, Koo, Mdomo na
Kiywa, Ngozi, Ini, Ubongo.
Pia imebainika kwamba matumizi ya
Shisha huambatana na kuongezewa dawa nyingine za kulevya na hivyo
hufanya watumiaji wa Shisha kupata uraibu wa dawa za kulevya. Matumizi
ya dawa hizo za kulevya ni kosa la jinai.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kurejea na kusisitiza agizo lake
la tarehe 12 Machi 2015 la kuzuia matumizi ya sigara na matumizi ya
bidhaa za tumbaku katika maeneo ya umma
Inakumbushwa kwamba agizo hili
limezingatia utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Bidhaa za Tumbaku,
Sura ya 121 T.L 2002, ya Sheria za Tanzania kipengele cha 12 (1) ambacho
kinakataza matumizi ya Tumbaku katika Maeneo ya Umma.
Madhumu ya Agizo hili ni kuilinda
Jamii kwa ujumla kutokana na madhara yatokanayo na moshi wa sigara.
Wizara inawakumbusha wananchi wanaotumia bidhaa za tumbaku kupunguza au
kuacha kabisa matumizi ya tumbaku. Aidha, agizo hili linaijumuisha jamii
yote katika kubaini madhara ya tumbaku na umuhimu wa kuzuia matumizi ya
tumbaku katika maeneo ya kazi na maeneo yote ya umma.
Agizo hili linawahusu wananchi wote nchini wanaopata huduma katika maeneo ya umma kama ilivyotafsiriwa na sheria husika.
Matumizi ya tumbaku hayaruhusiwi
katika maeneo yote ya umma. Maeneo haya yanajumuisha ofisi zote za
Serikali na tasisi zake zote, watu binafsi, vyuo, vituo vya huduma za
Afya zikiwemo Hospitali, vituo vya Afya na zahanati, vituo vya usafiri
wa Anga, Mabasi, bandari na treni, sehemu za mikutano, mapumziko,
bustani na fuko za maji,sherehe,michezo,masoko,maduka makubwa pamoja na
sehemu za kuabudu.Na kwa mtu yeyote anayeendesha shughuli katika maeneo
ya umma analazimika kutenga eneo maalum kwa ajili ya wavuta sigara.
Kwa kuwa Mhe. Waziri mwenye
dhamana na masuala ya Afya nchini ameona hatari hii ya Uvutaji wa sigara
na utumiaji wa bidhaa za tumbaku kwa afya ya Wananchi, kuanzia leo
tarehe 4/7/2016 matumizi ya Shisha nchini yamepigwa marufuku kwa wote
wanaojihusisha na matumizi hayo, na kwa wafanyabiashara wote
wanaojihusisha na upatikanaji wa Shisha nchini
Hivyo basi, kwa agizo hili katika
maeneo yote nchini ambako matumizi ya Shisha hufanyika ni marufuku
matumizi hayo kuendelea kutumika.
Aidha vyombo vya Dola na mamlaka husika vinahimizwa kusimamia kwa ukamilifu katazo hili.
EPZA YATENGENEZA AJIRA 36,000
Ofisa
Mwamasishaji Mwandamizi wa Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa
Mauzo ya Nje (EPZA), Nakadongo Fares (kulia), akizungumza na waandishi
wa habari Dar es Salaam leo kuhusu mambo mbalimbali yanayofanywa na
mamlaka hiyo. Kushoto ni Meneja Uhamasishaji Uwekezaji, Grace Lemunge.
Meneja Uhamasishaji Uwekezaji, Grace Lemunge (kushoto), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo na wanahabari.
Meneja
Mkuu wa Kampuni ya Star Infrastructure Development (T) Limited, Ananth
Bhat akizungumzia mradi wao wa uwekezaji uliopo mkoani Morogoro.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
———————————-
Na Dotto Mwaibale
MAMLAKA
ya Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) imeweza
kutengeneza ajira 36,000 kwa watanzania kupitia makampuni 140
yaliyowekeza hapa nchini.
Hayo
yamebainishwa na Ofisa Mwamasishaji Mwandamizi wa Mamlaka hiyo,
Nakadongo Fares Dar es Salaam leo wakati akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu mambo mbalimbali yanayofanywa na mamlaka hiyo kwenye
maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam 2016.
“Kupitia
makampuni 140 yaliyowekeza hapa nchini yameweza kutoa ajira kwa
watanzania 36,000 huku watoa huduma wakiwa 300,000” alisema Fares.
Alisema
kazi kubwa ya mamlaka hiyo ni kuhasisha uwekezaji katika kanda maalumu
za kiuchumi, kuvutia na kuhamasisha uhuishaji wa teknolojia mpya,
kuhamasisha uwekezaji kwenye viwanda usindikikaji wa malighafi
zinazopatikana nchini, kutengeneza fursa za ajira na kuongeza pato la
fedha za kigeni nchi.
Vyama Vya Siasa Zanzibar Kuhakikiwa
Ofisi ya Msajili wa Vyama
vya Siasa nchini Leo imekamilisha zoezi la kuhakiki vyama vya siasa 21
kwa upande wa Tanzania Bara . Zoezi la uhakiki wa vyama vya Siasa
visiwani Zanzibar litaanza Julai 11 mwaka huu.
Uhakiki wa Vyama utafanyika katika Ofisi za Vyama zilizopo
Zanzibar kwa maana ya Unguja na Pemba, zoezi hilo litajumuisha uhakiki
wa idadi ya wanachama ambao Chama cha Siasa kinapaswa kuwa nao kwa
mujibu wa masharti yalipo kwenye Sheria ya Vyama vya Siasa yam waka
1992.Ikumbukwe kuwa ,zoezi hili ni moja kati ya shughuli za kawaida za Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambalo hufanyika maramoja kila mwaka likilenga kufahamu utekelezaji wa masharti na matakwa ya sheria ya vyama vya siasa.
Bi. Esther Mwanri, Mwanansheria kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mara baada ya zoezi la uhakiki katika ofisi iliyopo Kinondoni Jijini Dar es Salaam. stori & picha na :ORPP
Afisa
Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Bi. Monica
Mwailolo (kushoto) akikagua taarifa za Chama cha Tanzania Labour Party
(TLP) wakati wa zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi hiyo iliyopo
Magomeni Jijini Dar es salaam, katikati ni Katibu Mkuu wa Chama cha
Tanzania Labour Party (TLP) Bi. Nancy Mrikalia akifuatiwa na Mwenyekiti
wa Chama hicho Bw. Augustine Mrema.
Willy
Brown Nyantiga, Mhasibu kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
nchini akielezea jambo wakati wa zoezi la uhakiki ulioanyika katika
Ofisi za Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD). Kulia ni
Mwenyekiti Taifa wa chama hicho Bw.Kamana Masoud na Kushoto ni Msajili
Msaidizi wa Vyama vya Siasa” Gharama za Uchaguzi na Elimu kwa Umma””
Bibi. Piencia Kiure
WAKUU WAPYA WA WILAYA ZA MKOA WA MWANZA WAPEWA MAJUKUMU MARA BAADA YA KUAPISHWA.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumza katika hafla ya
kuwaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza hii leo, Julai
04,2016 katika viunga vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Na BMG
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amewataka wakuu wapya wa Wilaya za
Mkoa huo kuhakikisha wanashirikiana na kamati za ulinzi na usalama
pamoja na wananchi kwenye wilaya hizo ili kukomesha mauaji dhidi ya watu
wenye
ulemavu wa ngozi na vikongwe yanayochangiwa na imani potofu za kishirikina.
ulemavu wa ngozi na vikongwe yanayochangiwa na imani potofu za kishirikina.
Akizungumza
baada ya kuwaapisha wakuu hao wa wilaya zote saba za mkoa wa Mwanza,
Mongella amesema kwa muda mrefu mkoa wa Mwanza umekumbwa na matukio ya
mauaji ya watu wenye ualbino na vikongwe kutokana na imani za
kishirikina
na kwamba wakati umefika kuhakikisha matukio hayo yanakwisha.
na kwamba wakati umefika kuhakikisha matukio hayo yanakwisha.
Amesema
mkoa huo umejipanga vyema kuhakikisha matukio hayo yanakuwa historia
kwa kuwa hakuna binadamu mwenye mamlaka ya kutoa uhai wa binadamu
mwenzake kwa sababu yoyote ile.
Mkuu
huyo wa mkoa amewapa mwezi mmoja wakuu hao wapya wa wilaya kumaliza
tatizo la madawati pamoja na kuwachukulia hatua watumishi hewa 1,057
waliogundulika kwenye wilaya zote za mkoa wa Mwanza.
Mongella
amewata wakuu hao wa Wilaya kuhakikisha kwamba matumizi ya dawa za
kulevya katika wilaya zao yanakomeshwa ambapo amepiga marufuku matumizi
ya shisha katika hoteli na klabu zote za muziki pamoja uchezaji wa “pool
table” na unywaji wa pombe saa za kazi huku akitanabaisha kwamba
atakaeshindwa kutekeleza maagizo hayo ni dhahiri shahiri kwamba atakuwa
ameshindwa kusimamia majukumu yake.
Aidha
Mongella amemtaka mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kuhakikisha kwamba hadi
ifikapo Agosti mosi mwaka huu awe amewaondoa wafanyabiashara ndogondogo
waliosambaa kwenye maeneo mbalimbali ya katikati ya jiji Mwanza.
Wakuu
wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza walioapishwa, wamesema wamejipanga
vyema kushirikiana na viongozi wengine pamoja na wananchi katika Wilaya
zao ili kuhakikisha kwamba wanatekeleza vyema majukumu yao ikiwemo
kuimarisha suala la ulinzi na usalama katika jamii.
Wakuu
wapya wa Wilaya saba za Mkoa wa Mwanza walioapishwa hii leo ni Mary
Onesmo Tesha wa Nyamagana, Estomin Francis Chang’a wa Ukerewe, Hadija
Rashid Nyembo wa Magu,
Juma Samwel Sweda wa Misungwi, Emmanuel Enock Kipole wa Sengerema, Dkt.Leonard Moses Masale wa Ilemela na Mhandisi Mtemi Msafiri Simion wa Kwimba ambapo wote wamekabidhiwa vitendea kazi ikiwemo Katiba ya Tanzania pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015/20.
Juma Samwel Sweda wa Misungwi, Emmanuel Enock Kipole wa Sengerema, Dkt.Leonard Moses Masale wa Ilemela na Mhandisi Mtemi Msafiri Simion wa Kwimba ambapo wote wamekabidhiwa vitendea kazi ikiwemo Katiba ya Tanzania pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015/20.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Mh.Emmanuel Enock Kipole (kulia), akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kushoto).
Mkuu
wa Wilaya ya Ukerewe, Mhe.Estomin Francis Chang’a (kushoto) akiapa
mbele ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (kulia).
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Mhe.Hadija Rashid Nyembo, akiapa hii leo
BUNGE LA VIJANA 2016 LAAPISHWA MJINI DODOMA
Mkuu
wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge, Owen
Mwandumbya akihutubia alipokuwa akizundua rasmi Bunge la Vijana la mwaka
2016, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, mjini Dodoma jana. Mkutano huo ni
wa tatu toka kuanzishwa kwa Bunge la Vijana chini ya mradi Legislatures Support Project(LSP). Picha na Ofisi ya Bunge.
Wabunge
wa Bunge la Vijana la mwaka 2016, kutoka Vyuo mbalimbali vya Elimu ya
Juu wakila kiapo cha utii baada ya kuanza kwa mkutano wa tatu wa bunge
hilo, mjini Dodoma. Picha na Ofisi ya Bunge.
Spika wa Bunge la Vijana, Regnald Massawe (kushoto)
kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha akimuapisha Stella Wadson-kutoka Chuo
cha Ustawi wa Jamii kuwa Naibu Spika wa Bunge hilo baada ya kuanza kwa
mkutano wa tatu wa Bunge la Vijana la mwaka 2016, mjini Dodoma. Picha na
Ofisi ya Bunge
Wabunge wa bunge la vijana kutoka vyuo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa bunge hilo.
BALOZI WA KOREA ATEMBELEA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMIBILI
Balozi
wa Korea, Song, Geum-young akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Museru baada ya balozi huyo
kumtembelea mkurugenzi huyo LEO. Mazungumzo hayo yalihusu maendeleo ya
hispitali hiyo.Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Museru akitoa historia fupi ya MNH LEO kwa Balozi Korea, Song, Geum-young.
Kutoka
kulia ni Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare, Mkuu wa Idara ya
Upasuaji, Dk Julieth Magandi na Mkurugenzi wa Uuguzi, Sister Agnes Mtawa
wakifuatilia mazungumzo LEO katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Aminiel Aligaesha (kushoto), Mkuu
wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali (EMD), Dk Juma Mfinanga
(katikati) na Mkuu wa Idara ya Watoto, Merry Charles wakifuatilia
mazungumzo hayo LEO.
Balozi wa Korea, Song, Geum-young akisaini kitabu cha wageni.
NDIKILO ASEMA WAKATI WA PROPAGANDA UMEISHA TUFANYE KAZI
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
MKUU wa mkoa wa Pwani
mhandisi Evarist Ndikilo, ametoa rai kwa wananchi mkoani humo kuungana
kwa pamoja na serikali ya awamu ya tano kufanya kazi ili kuinua uchumi
na maendeleo ya mkoa na Taifa kijumla.
Aidha amesema wakati wa
malumbano ya kisiasa na propaganda umekwisha hivyo jamii iwe nyuma ya
mh Rais Magufuli na serikali yake kujenga maendeleo ya nchi.
Akizungumza mara baada
ya kupokea taarifa ya tume ya uchaguzi kutoka kwa afisa uchaguzi tume ya
Taifa ya uchaguzi, Adam Nyando, mkuu huyo wa mkoa alisema wakati wa
kukaa na kuzungumzia itikadi za kisiasa umekwisha kilichobaki ni
kukubaliana na matokeo yaliyotangazwa na sio vinginevyo.
“Walioshinda wameshinda, aliyekosa kakosa, maji yameshamwagika, lakini kwa watanzania wote tumeshinda kwa kuwa tuna amani “
“Nawasihi wote tuungane
kufanya kazi ili kuleta maendeleo ya Taifa, tuchape kazi ili yote
yaliyoahidiwa wakati wa uchaguzi yapate nafasi kutekelezwa” alisema
mhandisi Ndikilo.
Hata hivyo mhandisi
Ndikilo alielezea kuwa kijumla mkoani Pwani zoezi la uchaguzi mkuu
lilikwenda vizuri hadi kipindi cha kutangazwa kwa matokeo.
Alisema wapo baadhi ya
watu walisema na kufikiri nchi isingetoka salama na ingetumbukia kwenye
machafuko ya kisiasa baada ya uchaguzi mkuu badala yake hali ipo shwari.
Alisema mungu
alituepushia na kutuondoa huko na sasa tupo shwariiii huku CCM ikiwa
imeshinda ambapo Rais wa nchi ni John Magufuli.
Mhandisi Ndikilo
alieleza baadhi ya nchi huwa wakitumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa
wenyewe, uvunjifu wa amani ama vurugu nyakati za uchaguzi hivyo kwa
Tanzania haina budi kumshukuru mungu kwa kutuvusha na kuendelea kuwa na
amani.
Awali akimkabidhi mkuu
wa mkoa huyo taarifa ya tume ya uchaguzi afisa tume ya Taifa ya
uchaguzi, Adam Nyando, alisema kwa sasa tume ya uchaguzi inajielekeza
kufanya majukumu mbalimbali ikiwemo elimu ya mpiga kura na zoezi la
uandikishaji wapiga kura.
Alisema majukumu hayo
yataenda sambamba na maandalizi ya mchakato wa kura ya maoni kwa kuanzia
na kurekebisha sheria ya kura ya maoni.
Akieliza anasema
uchaguzi mkuu umemalizika kwa amani na utulivu hivyo tume inaendelea na
majukumu yake mengine kwa maslahi ya Taifa.
Hata hivyo alielezea kuwa zoezi la uandikishaji wapiga kura utakuwa ni endelevu.
Nyando alisema sheria inasema kati ya uchaguzi mmoja na uchaguzi mwingine lazima kuwe na uandikishaji unaofanyika.
Mratibu wa uchaguzi
mkoani Pwani, Shangwe Twamala, alisema changamoto zilizojitokeza katika
uchaguzi mkuu 2015 zitashughulikiwa mapema kabla ya chaguzi zijazo.
Katika Uchaguzi mkuu
uliopita CCM ilishinda majimbo yote 9 ya mkoani Pwani na Rais na makamu
wa Rais Samia Suluhu walishinda kwa kupata kura nyingi dhidi ya vyama
vingine vya upinzani.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akizungumza na Wakuu wa Mikoa na Wilaya Unguja na Pemba,alipowakumbusha
majukumu yao na kuwataka wafanye kazi sheria na taratibi kwa kazi
iliyopo sio kufanya kazi kwa mazoea, aliyasema hayo leo katika ukumbi wa
Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 04/07/2016.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akizungumza na Wakuu wa Mikoa na Wilaya Unguja na Pemba,alipowakumbusha
majukumu yao na kuwataka wafanye kazi sheria na taratibi kwa kazi
iliyopo sio kufanya kazi kwa mazoea, aliyasema hayo leo katika ukumbi wa
Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 04/07/2016
Washauri wa Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakiwa katika
mkutano uliofanywa na Rais kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya leo katika
ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar ambao mkutano huo umewataka wakuu hao
kutekeleza majukumu yao kama sheria za Utumishi zinavyoeleza na sio
kufanya kazi kwa mazoea,[Picha na Ikulu.] 04/07/2016.
Baadhi
ya Wakuu wa Wilaya za Unguja na Pemba wakifuatilia kwa makini maelezo
yaliyotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika mkutano uliofanyika leo
katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja kwa ajili ya kukumbushwa majukumu
yao katika maeneo yao kazi,[Picha na Ikulu.] 04/07/2016.
Tigo, Milvik kushirikiana kutoa Bima watakayoimudu Watanzania
Dar es Salaam Julai 4, 2016-
Tigo Tanzania itashirikiana na na Milviki Tanzania na kampuni ya bima
ya Resolution kuanzisha huduma mpya ya Bima iliyoboreshwa ikijulikana
Bima Mkononi. Tigo imekuwa ikitoa huduma kama hiyo kwa kipindi cha
miaka mitano iliyopita kwa wateja wake zaidi ya 500,000 kupitia Tigo
Bima.
Huduma
ya Bima Mkononi inatoka huduma ya kipekee kama vile bima ya maisha,
ugonjwana ajali kwa mtu binafsi kwawateja ambao wanaotumia huduma ya
Tigo Pesa.
AAkitangaza
kuzinduliwa kwa huduma hiyo jijini Dar es Salaam leo Meneja wa Milvik
Tanzania,Tom Chaplin alisema, “Huduma hii itasaidia kuziba pengo kati
ya wateja na hivyo kuongeza upenyezaji wa huduma hiyo kwa njia ya simu
katika maeneo yaq mjini na vijijini nchini Tanzania, tunaamini Bima
Mkononi itakuwa ni kicdhocheo kikubwa cha kusukuma ujumuishwaji wa
huduma za fedha katika sekta isiyo rasmi kwa kuwawezesha Watanzania
kuzifikia huduma za bima wanazozimudu kutoka kwenye simu zao.”
Chaplain
aliongeza, “Tunawaomba Watanzania ambao hawajaweza kuzifikia huduma
za afya ambao wanazimudu ao bima ya kawaida ya afya kuanza kutumia
huduma hii kwa sababu inatoa ulinzi dhidi ya majanga ya kifedha na
afya duni kwao na familia zao.”
Akizungumza
katika uzinduzi huo Mkuu wa Huduma za kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel
alisema, “Kuzinduliwa kwa huduma hii kupo kwenye mikakati ya Tigo ya
kuboresha mageuzo katika mfumo wa maisha ya kidijitali na katika
kuongoza kwake katika kutoa teknolojia ya kisasa na ubunifu kwa
kuwezesha huduma ya Bima Mkononi kufikiwa kupitia Tigo Pesa.”
Aliongeza, “Huduma hii mpya itakuwa ni fursa kubwa kwa wateja wa Tigo
kuipata huduma ya bima kwa urahisi kwa sababu huduma ya Bima Mkononi
inalenga kuwapatia Watanzania njia mbadala kwa bima za afya na
maisha.”
Aliipongeza Milvik kwa ushirikiano wake na kuahidi kuwa Tigo imelenga kuendelsa kuunga mkono kupitia huduma ya Tigo Pesa.
Hivi
karibuni Tigo ilizindua kampeni mpya ya NITIGOPESA ambapo wateja
kutoka mitandao yote ya simu wanaweza kupata huduma za kifedha kutoka
kwa wateja na wafanyabiashara kote nchini.
MAJALIWA AKUTANA NA WAZIRI HAMAD RASHID WA ZANZIBAR
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Kilimo, Maliasili na
Uvuvi wa Zanzibar Hamad Rashid Ofisini kwake jijini Dar es salaam Julai
4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Kilimo, Maliasili na
Uvuvi wa Zanzibar Hamad Rashid Ofisini kwake jijini Dar es salaam Julai
4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MFALME WA AFRO POP TWENTE PERCENT ARUDI KWENYE GEMU NA SAUTI YA GHARAMA
Producer
nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto)
akiweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha
usimamizi wa kazi za msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20%
(Twenty per Cent) akishuhudiwa na Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha
Attorneys (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na meneja
uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu kushoto) kwenye
studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.
Producer
nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto)
baada ya kuweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA
kurasimisha usimamizi wa kazi za msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu
kama 20% (Twenty per Cent) wakisimamiwa na Wakili msomi Iddi M. Gogo wa
Alpha Attorneys (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na
meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu
kushoto) kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar
es salaam.
Msanii Abbas
Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) akiweka saini
kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha usimamizi wa
kazi zake huku akishuhudiwa na Producer nguli wa muziki nchini John
Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto), Wakili msomi Iddi M. Gogo wa
Alpha Attorneys (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na meneja
uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu kushoto) kwenye
studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.
Msanii Abbas
Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) wakipongezana na
producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water baada ya
kuwekeana saini mkataba wa kufanya kazi pamoja chini ya lebo ya
KOMBINENGA kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini
Dar es salaam.
(Picha na Sultani Kipingo)
———————————–
Na Sultani Kipingo
Mfalme wa Afro Pop nchini Abbas
Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) anavunja ukimya na
kurejea kwa kishindo kwenye anga ya muziki, huku akiwa msanii wa kwanza
kusaini mkataba na lebo mpya ya KOMBINENGA inayoendeshwa na producer
nguli John Shariza a.k.a Mann Water.
Twenty Percent, ambaye mwaka 2011
alitwaa tuzo saba za Kilimanjaro Music Awards (KTMA) kwa mpigo, huku
Mann Water akisomba tuzo mara mbili mfululizo za producer bora (mwaka
2013 na 2014), tayari amesharekodi vibao vitano na anatarajia kuachia
ngoma moja mpya ya kwanza Julai 18, 2016, katika kuandaa albamu yake ya
SAUTI YA GHARAMA.
“Nimerudi kuwachinja tena” anasema
Twenty Per cent, akiwa anakamilisha kurekodi katika studio za
Combination Sounds iliyoko Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es salaam.
“Nimerudi kurudisha sauti ya gharama kwa jamii. Sauti inayofundisha.
Sauti inayoonya. Sauti inayoburudisha. Sauti inayozengua kila mtu, ”
anaogeza.
Tayari Tweny Per cent ameshasaini
mkataba wa miaka mitano na lebo ya KOMBINENGA, katika hafla fupi
iliyofanyika Jumapili katika ofisi za Combination Sounds. Kuanzia sasa
shughuli zote za msanii huyu zitasimamiwa na lebo hiyo chini ya Producer
Mann Water.
Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha
Attorneys ndiye aliyefanikisha zoezi hilo la kutiliana saini mkataba
lililoshuhudiwa pia na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel
Moses.
“Namkubali sana Twenye Pa kwani ni
msanii aliyetimia na hutumii shuruba wakati wa kurekodi maana ana
kipaji cha ajabu cha kutunga akiwa wima na kukariri hapohapo”, anasema
Mann Water, ambaye ameshafanya kazi na wasanii nyota kibao wakiwemo
Lady Jay Dee, Ali Kiba, Ommy Dimpoz, Christian Bella, MB Dogg, Juma
Nature, Mr Blue na wengine wengi.
Twenty Percent alitamba sana tokea
mwaka 2006 kwa wimbo wake wa “Manemane” uliomfanya ashinde tuzo ya KTM,
kabla ya kuweka historia ya kusomba tuzo saba kwa mpigo mwaka 2011.
wakati huo nyimbo zilizompandisha chati zilikuwa ni “Tamaa Mbaya” na
“Ya nini Malumbano” na “Maisha ya Bongo”
Mbali na Muziki Twenye Percent pia
alitamba sana kwenye tasnia ya filamu ambapo alicheza kwenye mchezo
uliofahamika kwa jina lake la 20%. Baada ya hapo akaamua kupumzika kwa
muda na kujishugulisha na shughuli za kilimo. “Kilimo kinaendelea vyema
na sasa nimeamua kurudi kwenye gemu ili kuwachinja tena” alimalizia,
akiinuka kuelekea kwake Kimzichana, Mkuranga, Mkoa wa Pwani, anakoishi.
WAKUU WA WILAYA MKOA WA MWANZA WALA KIAPO
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amewaapisha wakuu wapya wa Wilaya za
Mkoa wa Mwanza na kuwapa vitendea kazi ikiwapo katiba ya Jamhuri ya
muungano wa Tanzania na Ilani ya Chama Tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM)
ya Mwaka 2015- 2020, kwa ajili ya kwenda kutimiza wajibu wao wa kikatiba
kwenye wilaya walizo pangiwa.
Akizungumza baada yakuwaapisha,
Mhe. Mongella, amewataka waende wakasimamie shughuli za kuhimiza
maendeleo, suala la ulinzi na usalama kwenye wilaya zao, huku akitilia
mkazo ukomeshwaji wa mauwaji ya watu wenye ulemavu wa Ngozi albino
pamoja na Vikongwe, amesema, ikiwa jamii ya watu hao itapata madhara
basi ni dhahiri Mkuu huyo wa Wilaya atakuwa ameshindwa kusimamia
majukumu yake.
Mkuu huyo wa mkoa pia, amerudia
kauli yake nakuwataka viongozi hao wapya watambue wanajukumu zito
lililoko mbele yao, ikiwa ni pamoja na kukomesha Utumiaji wa dawa
zakulevya.
Aidha ameonya uchezaji wa Pool
na unywaji wa Pombe wakati wa saa kazi, huku akimsisitiza mkuu wa
Wilaya ya Nyamagana kuhakikisha ifikapo Agosti mosi, suala la wafanya
biashara wanaofanya biashara kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi liwe
limepatiwa ufumbuzi.
Mongella amesema, katika mkoa wa
Mwanza, Hotel na Clabu, yeyote ile, iwe ya kawaida au ya Kitalii,
ikibainika inafanya biashara ya Shisha, hawata ivumilia na badala yake
wataifutia Leseni ya biashara.
Walio apa mbele ya Mkuu wa Mkoa,
ambao waliteuliwa na Mhe. Rais Tarehe 26, Juni, 2016 ni Emmanuel Enock
Kipole, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Estomin Francis Chang’a Mkuu wa
Wilaya ya Ukerewe, Hadija Rashid Nyembo Mkuu wa Wilaya ya Magu, wengine
ni Juma Samwel Sweda Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Dkt. Leonard Moses
Masale Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mary Onesmo Tesha Mkuu wa Wilaya ya
Nyamagana na Mhandisi Mtemi Msafiri Simioni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba.
TAARIFA YA MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI, PAMOJA NA MLIPUKO WA UGONJWA WILAYANI CHEMBA NA KONDOA, MKOANI DODOMA
Serikali
kupitia Wizara yangu imeweka na utaratibu wa kutoa taarifa ya mwenendo
wa magonjwa ya mlipuko yanayoikumba nchi yetu kwa wakati husika ili
kutoa elimu na kuifahamisha jamiii hatua zinazochukuliwa na Wizara
kudhibiti magonjwa hayo.
Ugonjwa wa kipindupindu ulioanza
tangu Agusti 2015, bado upo nchini na hadi kufikia tarehe 03 Julai 2016,
jumla ya wagonjwa 22,216 wametolewa taarifa. Kati yao ndugu zetu 345
wamepoteza maisha.
Takwimu za wiki iliyopita kuanzia
tarehe 27 Juni hadi 03 Julai 2016 zinaonesha kuwa, kasi ya ugonjwa wa
kipindupindu imepungua sana ambapo idadi ya wagonjwa wapya walioripotiwa
wiki hiyo ni 31, na pametokea kifo 1, ikilinganishwa na wagonjwa 365
bila kifo walioripotiwa wiki iliyotangulia ya Juni 20 hadi 26, 2016.
Mkoa ambao bado umeendelea kuripoti ugonjwa wa kipindupindu ni mmoja tu
nao ni Morogoro katika Halmashauri ya Kilosa (23) na Morogoro Vijijini
(8). Aidha, katika wiki hii kumeripiotiwa kifo cha mtu mmoja
kilichotokana na ugonjwa wa kipindupindu kutoka Halmashauri ya Kilosa.
Pamoja na changamoto za utoaji
taarifa sahihi na utunzaji wa kumbukumbu za taarifa za wagonjwa wa
Kipindupindu kupitia mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa ya milipuko,
tafsiri kubwa tunayoipata kutoka kwenye takwimu hizi ni kwamba kwa sasa
ni dhahiri kuwa mlipuko huu wa ugonjwa wa kipindupindu uliodumu kwa
miezi 10 unakaribia kuisha, ila kuna haja ya jitihada za ziada katika
mkoa wa Morogoro ili kuutokomeza ugonjwa huu katika nchi nzima.
Pamoja na muelekeo huo, ninatoa
rai kwa viongozi wa ngazi za vituo vya kutolea huduma za afya, wilaya na
mikoa kuendelea kutoa taarifa sahihi na kwa wakati za wagonjwa wa
Kipindupindu ili kufanikisha juhudi za kupambana na mlipuko huu hapa
nchini. Aidha katika hali ya sasa ya kuwa na wagonjwa wachache, natoa
agizo kwamba wagonjwa wote wanaohisiwa kuwa na ugonjwa huu wa
kipindupindu wathibitishwe kwa vipimo vya maabara na kupatiwa matibabu.
Aidha napenda kusisitiza kwamba hatua za Kisheria zitachukuliwa kwa
yeyote atakaebainika kutotoa taarifa sahihi za wagonjwa wa Kipindupindu
na magonjwa mengine ya mlipuko.
Vile vile nasisitiza kwamba ni
budi Mikoa yote kuendelea kuchukua hatua za tahadhari ili kuzuia
maambukizi, na pia kuendelea kutoa taarifa sahihi kila siku na kusimamia
kikamilifu hatua mbalimbali za udhibiti wa mlipuko huu.
Tunaendelea kuisihi jamii
kuungana na Halmashauri, Mikoa pamoja na Wizara katika juhudi za
kupambana na kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu kwa kuzingatia
yafuatayo:
Mrisho Mpoto Anguruma Usiku wa Kili Challenge
Balozi wa Kampeni ya Kili
Challenge Msanii Mrisho Mpoto amekonga nyoyo za mashabiki na
wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwenye mnada maalumu wa
bidhaa mbalimbali za kuchangia fedha za Kampeni ya Kili Challenge kwenye
ukumbi wa Lapa Mchauru Mkoani Geita.
Kili Challenge ni mfuko
unaochangisha fedha kila mwaka kwa kudhamini watu kupanda mlima
Kilimanjaro ili kuchangisha fedha kwa ajili ya kupambana na janga la
ukimwi Tanzania. Mfuko huu unaratibiwa na Mgodi wa Geita (GGM) kwa
ushirikiano na Taasisi ya Kupambana na Ukimwi Tanzania (TACAIDS) pamoja
na wadau wengine mablimbali. Hadi sasa zaidi ya Taasisi
30zinazojihusisha na Ukimwi zimenufaika na mfuko huu wa Kili Challenge
na watu zaidi ya 500 kutoka duniani pote, wamepanda mlima Kilimanjaro
kupitia mfuko huu.
Akiimba kwa hisia Mrisho Mpoto
pamoja na Msanii mwenzake Mwimbaji wa mziki wa “Live” Ibrozama Mkungwe
maarufu kwa jina la “Beka” walitumbuiza wimbo wa “Sauti Nenda” remix
ikiwa ni mahususi kuwakumbusha watanzania kwamba Ukimwi bado upo na ni
jukumu la kila mmoja wetu kuchukua hatua dhaditi katika mapambano hayo.
Msanii
Mrisho Mpoto “Mjomba” akiwa na Msanii Ibrozama Mkungwe “Beka” wakiimba
kwa hisia wimbo “Sauti Nenda” kwenye mnada wa Kili Challenge uliofanyika
katika mgodi wa GGM mjini Geita kwa ajili ya kuchangisha fedha za
kusaidia serikali katika mapambano dhidi ya Ukimwi.
Balozi
wa Kili Challenge Mrisho Mpoto maarufu kama “Mjomba”akitumia mtindo
wake wa kughani mashairi kwa kuongea kwa hisia ametoa wito kwa jamii
yote Tanzania kuendelea kupambana na janga hili ili Kufikia sufuri 3 –
Zero ya Maambuki, Zero ya Unyanyapaa na Zero ya vifo vitokanavyo na
Ukimwi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita Bw Terry Mulpeter(kushoto)
akifurahia jambo na Mkuu wa Wilaya ya Geita anayemaliza muda wake Bw
Omar Mangochie(kulia) wakati wa hafla ya mnada wa Kili Challenge
uliofanyika Mgodi wa dhahabu GGM ili kuchangisha fedha katika mapambano
dhidi ya Ukimwi Tanzania.
“Sauti
nenda,usipitie masikioni kama tulivyozowea,pitia kwenye moyo na
uwaambie tumechoshwa na majina ya unyanyapaa tunayoitwa, waambie
hatupendi kuitwa..ana ngoma,…….ana miwaya……kanasa……….”Alisikika balozi
wa Kili Challenge Mrisho Mpoto kwenye mashairi ya Wimbo wake mpya wa
“Sauti Nenda” wimbo aliouimba “live” akishirikiana na msanii “Beka”.
Akizungumzia Kampeni ya Kili
Challenge, Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) Bw
Terry Mulpeter alisema kuwa mwaka huu Mgodi wa Dhahabu wa Geita kwa
kushirikiana na tume ya kudhibiti na kupambana na UKIMWI(TACAIDS) na
wadau wengine wanatarajia watu zaidi ya 100 watashiriki katika kupanda
mlima Kilimanjaro na kuuzunguka kwa kutumia baiskeli kwa jumla ya siku 7
ili kuchangisha fedha na kuisaidia serikali katika mapambano dhidi ya
Ukimwi.
Zoezi rasmi la kupanda Mlima
Kilimanjaro litaanza tarehe 16 Julai ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mh. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita Bw Terry Mulpter (katikati) akiwa
na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Geita Mh.Omar Mangochie na Balozi wa
Kili Challenge Msanii maarufu Afrika Mashariki na Kati bwana Mrisho
Mpoto “Mjomba” kwenye picha ya Pamoja na watoto na walezi wa kituo cha
watoto Yatima “Moyo wa Huruma” mjini Geita ambapo wazazi wa watoto hawa
wamepoteza maisha kwasababu ya janga la Ukimwi. Kituo hiki chenye watoto
zaidi ya 100 kinaendesha shughuli zake kwa udhamini wa mfuko wa Kili
Challenge na Mgodi wa dhahabu wa Geita GGM.
Kocha wa kimataifa wa kuogelea asema siku moja Tanzania itatoa mabingwa wa Dunia
Mkufunzi
klabu ya Hamilton Aquatics, Katy Morris akiwaonyesha waogeleaji
chipukizi jinsi gani ya kuanza kuogelea kwa staili ya backstroke.
Waogeleaji
chipukizi chini ya miaka minne wakishiriki katika mafunzo hayo kwa
vitendo kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya DIA
yaliyoandaliwa na klabu ya Dar Swim Club chini ya ukufunzi kutoka klabu
bingwa ya mchezo huo nchini Dubai, Hamilton Aquatics.
Mkufunzi
wa klabu ya Hamilton Aquatics, Katy Morris akiwaonyesha waogeleaji
chipukizi jinsi gani ya kuelea ndani ya maji kwa staili ya backstroke Waogeleaji
Adam Kitururu na Celina Itatiro wakifanya mazoezi baada ya kupatiwa
mafunzo ya kuogelea kwa staili ya backstroke huku wakiwa na glasi katika
paji lao la uso. Lengo lakufanya hivyo ni kuogelea kwa kufuata masharti
ya staili hiyo.
Kocha Nebojsa Durkin (wa pili kulia) akiwaelekeza makocha wa Dar Swim Club mbinu mbalimbali za kisasa za kuogelea Kocha
Katy Morris akiwasimamia waogeaji chipukizi (watoto) jinsi gani ya
kuelea kwenye maji na kuongelea kwa freestyle na backstroke
Kocha
Katy Morris akiwasimamia waogeaji chipukizi (watoto) jinsi gani ya
kuelea kwenye maji na kuongelea kwa freestyle na backstroke
…………………………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Wakufunzi wa kimataifa wa
mchezo wa kuogelea wa klabu bingwa ya Mashariki ya Kati (Middle East)
ijulikanayo kwa jina la Hamilton Aquatics ya Dubai, Nebojsa Durkin ma
Katy Morris wamesema kuwa Tanzania inaweza kupata sifa kubwa katika
michezo duniani kupitia mchezo wa kuogelea.
Wakufunzi hao walisema hayo
katika semina inayoendelea ya mchezo huo kwa waogeleaji na makocha wa
klabu marufu ya Dar Swim Club (DSC).
Durkin alisema kuwa
amefuraishwa na vipaji vya mchezo huo kutoka kwa waogeleaji wa DSC na
anaamini kuwa siku moja, Tanzania itatoa bingwa wa dunia kupitia mchezo
huo.
“Nimefurahi kuona kuwa mchezo
una mwamko sana na wachezaji wanaupenda, pia Tanzania ina makocha wazuri
wenye elimu ya kutosha, naamini kama juhudi hizi zitaendelezwa, nchi
itapata wawakilishi wazuri katika mashindano ya kimataifa na kuweza hata
kutwaa ubingwa wa Dunia,” alisema Durkin ambaye ni raia wa
Serbia.Alifafanua kuwa amefuraishwa na waogoeleaji chipukizi ambao umri
wao ni chini ya miaka minne.
“Nimevutiwa kuona hata
Tanzania hasa klabu ya DSC ina waogeleaji watoto ambao wanaupenda
mchezo, hii imenivutia sana, hapa utapata wachezaji ambao wataupendea
mchezo kuanzia utotoni na huu ndiyo mwamko ambao utaleta matunda katika
mchezo,” alisema.
Kwa upande wake, Katy ambaye ni
mwanadada alisema kuwa wadau wa mchezo huo wanatakiwa kusaidia kufikia
malengo hayo kwani bila uwekezaji mkubwa, bado mchezo utakuwa chini
kutokana na ukosefu wa vifaa mbalimbali vya kisasa.
Katy alisema kuwa DSC
imeonyesha nia ya kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa na kuomba
wadau waunge mkoni. Mafunzo hayo yamedhaminiwa na kampuni za Alios
Finance Tanzania, Europcar, DSC, DIA na kampuni ya utafiti na uchimbaji
wa mafuta ya Maurel & Prom.
Katibu Mkuu wa DSC, Inviolata
Itatiro amesema kuwa lengo lao ni kuona Tanzania inafanya vizuri katika
mchezo huo kimataifa. Alisema kuwa DSC imeamua kupambana katika kuleta
maendeleo ya mchezo wa kuogelea hapa nchini.
“Tunahitaji sapoti katika
mchezo huu, lengo ni kuona waogeleaji wanapata maendeleo makubwa kwa
kufikia viwango, nawaopongeza wadhamini Alios Finance Tanzania,
Europcar, DSC, DIA na kampuni ya utafiti na uchimbaji wa mafuta ya
Maurel & Prom kwa kutuunga mkono, gharama za kuwaleta walimu kutoka
nje ni kubwa sana,” alisema Inviolata.
MAJALIWA AFUTURU KATIKA MSIKITI WA KHOJA SHIAITHNA-ASHERI -DAR ES SALAAM
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na viongozi
wa Msikiti wa Khoja Shia Ithna-Asheri wa jijini Dar es salaam wakati
alipowasili msikitini hapo kushiriki katika fuatari ambayo mgeni Rasmi
alikuwa Waziri mkuu, kassim Majaliwa Julai 3, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa Msikiti wa Khoja
Shia Ithna-Asheri wa jijini Dar es salaam wakati alipowasili msikitini
hapo kushiriki katika fuatari Julai 3, 2016. Kushoto ni Sheikh wa Mkoa
wa Dar es salaam, Alhaji Mussa Salum na kushoto kwa Waziri Mkuu ni
Mwenyekiti wa Khoja Shia Ithna-Asheri. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mufti Mkuu wa Tanzania,
Abubakary Zubery bin Ally baada ya kuwasili kwenye msikiti wa Khoja Shia
Ithna-Asheri jijini Dar es salaam kushiriki kwenye futari iliyoandaliwa
msikitini hapo Julai 3, 2016. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa
Dar es salaam, Ramadhan Madabida. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan
Mwinyi wakishiriki katika swala kabla ya kufuturu kwenye Msikiti wa
Khona Shia Ithna-Asheri wa jijini Dar es salaam Julai 3, 2016. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali
Hassan Mwinyi alipozungumza katika futari iliyoandaliwa katika Msikiti
wa Khoja Shia Ithna-Asheri wa jijini Dar es salaam Julai 3, 2016. Wanne
kushoto ni ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Abukakary Zubery bin Ally na
watano kushoto ni Mwenyekiti wa Khoja Shia Ithna-Asheri, Azim Dewji.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais wa Awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi
wakimsikiliza Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakary Zubery bin Ally wakati
alipozungumza katika futari iliyoandaliwa katika Msikiti wa Khoja
Shia Ithna-Asheri wa jijini Dar es salaam Julai 3, 2016. Kushoto ni
Sheikh wa mkoa wa Dar es salaam, Alhaji Mussa Salum. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Mwenyekiti
wa Khoja Shia Ithna-Asheri, Azim Dewji akizungumza katika futari
iliyoandaliwa kwenye Msikiti wa Khoja Shia Ithna-Asheri wa jijini Dar
es salaam Julai 3, 2016. Mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru Mwenyekiti wa MOHAMMED ENTERPRISES
GROUP, Gulam Dewji ambaye alitoa mchango wa madawati 500 katika futari
iliyoandaliwa kwenye Msikiti wa Khoja Shia Ithna-Asheri wa jijini Dar
es salaam Julai 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa wakizungumza katika futari iliyoandaliwa kwenye
Msikiti wa Khoja Shia Ithna-Asheri wa jijini Dar es salaam Julai 3,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa wakizungumza katika futari iliyoandaliwa kwenye
Msikiti wa Khoja Shia Ithna-Asheri wa jijini Dar es salaam Julai 3,
2016. Kushoto ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakary Zubery bin Ally na
wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Khoja Shia Ithna-Asheri, Azim
Dewji(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi
ya washiriki wa futari iliyoandaliwa kwenye Msikiti wa Khoja Shia
Ithna-Asheri jijini Dar es salaam wakimsikiliza mgeni rasmi Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza Julai 3, 2016. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments :
Post a Comment