Ofisa Mwamasishaji Mwandamizi wa
Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA),
Nakadongo Fares (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es
Salaam leo kuhusu mambo mbalimbali yanayofanywa na mamlaka hiyo. Kushoto
ni Meneja Uhamasishaji Uwekezaji, Grace Lemunge.
Meneja Uhamasishaji Uwekezaji, Grace Lemunge (kushoto), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo na wanahabari.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Star
Infrastructure Development (T) Limited, Ananth Bhat akizungumzia mradi
wao wa uwekezaji uliopo mkoani Morogoro.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Katibu
Mkuu
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolph Mkenda,
(wakwanza
kushoto), akipitia taarifa ya michango yake, wakati alipotembelea banda
la PPF
ili kujionea jinsi wafanyakazi wanavyohudumia wananchi na wanachama
wanaofika
kutembeela banda hilo kwenye maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya
Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Adolph Mkenda (kulia),
akimkabidhi kadi ya uanachama mwanachama mpya aliyejiunga na PPF kupitia mfumo
wa Wote Scheme. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio
Afisa Mwendeshaji Mwandamizi, Paulina
Msanga, (kulia), akimpatia maelezo mwananchi huyu aliyetembelea banda la
Mfuko huo kwenye maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es
Slaam
Wananchi wakipatiwa maelezo na wafanyakazi wa PPF, walipotembelea banda la Mfuko huo
Afisa Masoko Mwandamizi wa PPF, Nelu
Mwalugaja (kulia), akiwapa maelezo ya shughuli mbalimbali zifanywazo na
Mfuko huo, Mwananchi huyu aliyefika na familia yake kwenye banda la PPF
Afisa Huduma kwa Wateja Mwajuma Msina, (kushoto), akimpatia maelezo Mwananchi huyu aliyefika kwenye banda la PPF
NA
MWANDISHI WETU
KATIBU
mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolph Mkenda, ameupongeza Mfuko wa
Pensheni wa PPF, kwa huduma zake za haraka na bora.
Profesa
Mkenda pia alitoa pongezi nyingi kwa Mfuko huo kuibuka mshindi wa kwanza kwenye
maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, 2016 kundi la Mifuko
ya Hifadhi ya Jamii na Makampuni ya Bima.
Aliyasema
hayo wakati alipotembelea banda la PPF kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere
Juma;pili Julai 3, 2016 “Nimefurahishwa na huduma zenu za haraka, kwani mimi
mwenyewe ni shahidi nilipohitaji taarifa za michango yangu, nimezipata chini ya
dakika 1 huu ndio ufanisi wa kazi tunaohitaji sisi kama serikali katika
kuwahudumia wananchi.” Alisema.
Profesa Mkenda
aliipongeza PPF kwa kuitikia vema wito wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, wa kutaka Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuelekeza nguvu zake
katika uwekezaji wa viwanda ili kupanua ajira.
Profesa
Mkenda alipata fursa ya kutembelea idara mbalimbali za Mfuko huo na kujionea
jinsi zinavyotoa huduma kwa wanachama na wananchi wanaotembelea banda hilo.
Miongoni
mwa kurugenzi alizotembeela ni pamoja na ile ya uendeshaji, mafao na michango
Profesa
Mkenda ambaye alikuwa kiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, William Erio,
alikabidhi kadi mpya za kujiunga uanachama wa Mfuko huo kupitian Mfumo wa Wote
Scheme ambao unatoa fursa kwa mtu yeyote mwenye shughuli ya kumuingizia kipato
kujiunga na kuchangia.
No comments :
Post a Comment