Saturday, July 9, 2016

PROFESA MUHONGO AFUNGA RASMI MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA 40 YA DAR ES SALAAM



Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo(kulia), akimkabidhi cheti cha mshindi wa pili wa muonyeshaji bora kutoka Wizara za Serikali na wakala wake, Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel V. Manyele, wakati wa kufunga maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 40 ya Dar es Salaam leo Julai 8, 2016. Jumala ya mataifa 30 yalishiriki maonyesho hayo na Profesa Muhongo alikuwa mgeni rasmi. Wapili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolph Mkenda, na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendelezaji Biashara Tanzania, (TANTRADE), Edwin Rutageruka.(PICHA NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

 WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (pichani), amefunga rasmi Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 40 ya Dar es Salaam, leo Julai 8, 2016 kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Profesa Muhongo amefunga maonyesho hayo yaliyodumu kwa takriban siku 8 ambapo jumla ya mataifa 30 kutoka sehemu mbalimbali Duniani yalishiriki kuonyesha bidhaa zao, kutafuta masoko lakini pia kuuza bidhaa hizo. Waziri Muhongo pia alitoa vyeti vya ushiriki kwa makampuni mbalimbali ikiwa ni pamoja na tuzo kwa waonyeshaji bora pamoja na wadhamini wa maonyesho hayo
 Maelfu ya wananchi wakiwa kwenye maonyesho hayo Leo Julai 8, 2016
 Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolph Mkenda, akitoa hotuba yake
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendelezaji Biashara Tanzania, (TANTRADE), Edwin Rutageruka, akizunhgumza kwenye hafla hiyo
 Baadhi ya waonyeshaji wakiwa kwenye hafla hiyo ya ufungaji wa maonyesho hayo
 Msanii mahiri Mrisho Mpoto , a.k.a Mjomba (kushoto) pia alikuwepo
 Baadhi ya waonyeshaji wakiwa kwenye hafla hiyo ya ufungaji wa maonyesho hayo
 Waziri Profesa Muhongo, akimkabidhi cheti cha ushiriki mshindi wa pili muonyeshaji wa Kimataifa, mwakilishi kutoka Serikali ya Ujerumani
 Waziri Muhongo akimkabidhi cheti cha ushindi wa tatu muonyeshaji bora katika sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano mwakilishi wa kampuni ya simu ya Halotel
 Profesa Muhongo akimkabidhi cheti cha ushiriki, mshindi wa tatau katika kundi la juonyeshaji bora wa bidhaa za ngozi
 Waziri Muhongo akimkabidhi cheti cha mshindi wa tatu kundi la muonyeshaji bora wa magari na uunganishaji mitambo
 Profesa Muhongo akimkabidhi cheti cha ushindi wa tatu, muonyeshaji kutoka sekta ya uendelezaji vipaji na mafunzo
Profesa Muhongo, akimkabidhi tuzo ya mmoja kati ya wadhamini wa maonyesho hayo, Mwakilishi kutoka benki ya NMB, Josephine Kulwa

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipokea zawadi ya maua mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Hotel ya Southern Sun Jijini Dar es Salaam kufungua mashindano ya magari Afrika Mashariki (East African Classic Safari Rally) yanayofanyika kuanzia Julai 8 mpaka 10 mwaka huu.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akifurahi jambo pamoja na Rais wa Automobile Association of Tanzania Bw. Nizar Jivani(Kulia), Kaimu Katibu Mkuu Baraza la Michezo la Taifa(BMT) Bw. Mohamed Kiganja (wa tatu kulia) wakati wa ufunguzi wa mashindano ya magari Afrika Mashariki (East African Classic Safari Rally) yanayofanyika kuanzia Julai 8 mpaka 10 mwaka huu.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitambulishwa kwa baadhi ya madereva wa mashindano ya magari Afrika Mashariki (East African Classic Safari Rally) na Rais wa Automobile Association of Tanzania Bw. Nizar Jivani (Kulia) mashindano hayo yanayofanyika kuanzia Julai 8 mpaka 10 mwaka huu.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akijadiliana jambo na Rais wa Automobile Association of Tanzania Bw. Nizar Jivani (Kulia) wakati alipowasili katika ufunguzi wa mashindano ya magari Afrika Mashariki (East African Classic Safari Rally) yanayofanyika kuanzia Julai 8 mpaka 10 mwaka huu

DC GONDWE ATAKA WAFANYABIASHARA KUWEKEZA KWENYE KILIMO KIKUBWA WILAYANI HUMO


MKUU wa wilaya ya Handeni MkoaniTanga,Godwin Gondwe amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanawekeza kwenye kilimo kikubwa cha kisasa ambacho kitakuwa na tija kwao ili kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo na kukuza uchumi.

Gondwe alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wafanyabiashara, viongozi wa dini ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka kuona umuhimu wa kutumia fursa ya uwepo wa rutuba nzuri ya ardhi iliyopo wilayani humo kujikita kulima kisasa ili kuweza kupata mafanikio.

Alisema kuwa lazima wafanyabiashara watambue kuwa kilimo ndio njia pekee
ambayo inaweza kuwainua kiuchumi na kuharakisha kasi ya ukuaji wa
maendeleo iwapo watazingati na kukipa kipaumbele kila wakati “Niwaombeni suala la kilimo mlipe msukumo mkubwa sana kwani hii ndio njia pekee ambayo inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wilaya yetu “Alisema.

Aidha pia alisisitiza umuhimu wa wananchi wa wilaya hiyo kutilia mkazo
kulima mazao yanayostahimili ukame ikiwemo Alizeti, Ufuta,Viazi na
Mihogo ili kuweza kukabiliana na tatizo la kutoku patikana mvua za uhakika kwa ajili ya kilimo cha mahindi.

“ Ninajua katika kipindi hiki tumelima kwa wingi lakini hali ya hewa
sio nzuri na mvua nazo zimekuwa hazipatikana kwa uhakika hivyo lazima
wakulima tubadilike kwa kuanza kupanda mazao yanayostahimili ukame ili
kuweza kuepukana na baa la njaa “Alisema DC Gondwe.

Sambamba na hayo,Mkuu huyo wa wilaya alizishauri taasisi za kibenki
wilayani humo kuhakikisha zinatoa kipaumbele kwa wawekezaji wa kilimo
ili waweze kuzalisha kwa wingi mazao ambayo yataweze kuinua kiuchumi
lakini pia kuchangia pato la Taifa.

Hata hivyo ,Mkuu huyo wa wilaya alitumia pia fursa hiyo kuwaasa wakulima waliopata mazao kidogo kuhakikisha wanayatunza na kuacha kuyauza kwani kufanya hivyo kutaweza kusababisha hali ya njaa kwao.

Naye Shehe wa wilaya ya Handeni, Shabani Mohamed alisema kuwa wao
watamuombea dua Mkuu huyo wa wilaya ili mungu amuwezeshe kuweza kutimiza majukumu yake ipasavyo na kusaidia kuchangia juhudi za maendeleo kwa wananchi.

“Nikuambie Mh Mkuu wa wilaya ujio wako hapa Handeni watu wengi
wamefurahi sana kwani uchapakazi wako unafahamika tokea ulipokuwa
unafanya kazi kwenye kituo cha ITV na tunaamini uhodari huo pia
utasaidia kuinua uchumi wetu “Alisema.

Alisema kuwa wao watahakisha wanampa ushirikiano wa hali ya juu ili
kumuwezesha kutekeleza vema majukumu yake ya kuipa maendeleo wilaya
hiyo. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

No comments :

Post a Comment