Tuesday, July 5, 2016

Dk. Kigwangalla akutana na balozi wa Korea kujadili kuhusu Hospitali ya Mlonganzira na ujio wa mobile clinic

Kwa muda mrefu Tanzania imekuwa na urafiki na Korea na katika kulidumisha hilo, Balozi wa Korea nchini, Song Geum-young amemtembelea Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla na kuzungumza mambo mbalimbali kuhusu ushirikiano wa Korea na Tanzania zaidi katika sekta ya afya na jinsi Korea ambavyo imekuwa ikisaidia uboreshwaji wa huduma za kiafya nchini.
Akizungumza na Mo Blog kuhusu ugeni huo, Dk. Kigwangalla alisema kuwa balozi Geum-young alitaka kujua kama naibu waziri anafahamu kuhusu ujenzi wa chuo na hospitali ya Mlonganzira ambapo alitaka kufahamu kama serikali itakuwa tayari kutoa watumishi wa afya 900 ambao watahudumia hospitali hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young kuhusu uhusiano wa Tanzania na Korea na jinsi ambavyo nchi hiyo imepanga kuendelea kuisaida Tanzania katika kuboresha huduma za kiafya nchini. (Picha zote na Rabi Hume, MO Blog)
Katika hilo Dk. Kigwangalla alimuhakikishia balozi kuwa serikali ipo tayari kutoa wataalam wa afya ambao watakuwa wakitoa huduma katika hospitali ya Mlonganzira ambayo itakuwa na vifaa vya kisasa kutoka Korea na itakuwa na vitanda 600 ambavyo vitakuwa vinatumiwa na wagonjwa wanaofika kupata huduma.
Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akifanya mazungumzo na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young, alipofika ofisini kwake kwa ajili ya kuzungumza mambo yanayohusu mahusiano ya Tanzania na Korea.
Jambo lingine ambalo walizungumza ni kuhusu msaada wa magari ya kutolea huduma za kiafya ambayo yanatembea ‘mobile clinic’ ambayo yatatolewa kwa kanda zote nchini na zaidi katika maeneo ambayo yanaonekana kuwa na ugumu kufikika na kuwa na vituo vya afya vichache.
Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young, wa kwanza kushoto ni Katibu wa Balozi wa Korea, Songwon Shin na wapili kulia ni Katibu wa Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Kulwa.
“Amesema watatuletea convoy zaidi ya sita (kila moja ina magari 10) ambayo yatagawiwa kwa kila kanda nchini, magari haya kila gari linakuwa na mengine 10 ambayo yanakuwa na huduma mbalimbali za kiafya kama chumba cha upasuaji, store ya madawa, maji na mengine ambayo yanahitajika kutoa huduma kwa mgonjwa,” alisema Dk. Kigwangalla.
Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young wakipiga picha ya pamoja baada ya kumaliza mazungumzo.
Aidha aliongeza kuwa magari hayo ya kutolea huduma za afya ambayo yanatembea ‘mobile clinic’ yanataraji kuletwa nchini mwakani mwezi Januari na kwasasa wizara imetakiwa kuandika andiko la mradi ili kuonyesha kuwa imekubali kuingia katika mradi huo ambao kwa kiasi kikubwa utaweza kurahisisha upatikanaji wa huduma za kiafya kwa maeneo ambayo yana vituo vichache vya afya.
Na Rabi Hume, MO Blog
Katibu wa Balozi wa Korea, Songwon Shin akibadilishana mawasiliano na Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla katikati ni balozi wa Korea nchini, Song Geum-young.
Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young baada ya kumaliza kufanya mazungumzo.

Tanzania, Uganda zajadili utekelezaji wa Bomba la Mafuta

 index 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa wa kwanza kulia, akifuatiwa na Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Petroli Mwanamani Kidaya (katikati) na Mratibu wa Mradi, Salum Mnuna (kushoto) wakifuatilia majadiliano wakati wa kikao cha  Makatibu Wakuu wa nchi za Uganda na Tanzania, kilichohusu utekelezaji wa Mradi wa bomba la Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga, Tanzania.
Kikao hicho kilifanyika tarehe 04.07.2016, kabla ya kikao cha Mawaziri wan chi husika. Aidha, Wataalam wengine (hawapo pichani) waliohudhuria kikao hicho kwa upande wa Tanzania walitoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
Pia, kwa upande wa Uganda waliwakilishwa na Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini, wadau wa sekta hizo kutoka idara mbali mbali za Serikali na wawekezaji kampuni za Total, CNOOC na Tullow.
Vikao hivyo ni sehemu ya Maandalizi ya ripoti iliyowasilishwa katika kikao cha Mawaziri cha tarehe 5.07.201, Hoima nchini Uganda.
B 
Waziri wa Nishati na Madini (katikati mstari wa kwanza kulia) akiongoza Wataalam wa Watanzania katika kikao cha Mawaziri wa  Tanzania na Uganda kujadili utekelezaji wa Mradi wa bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga. Kikao cha Mawaziri kimefanyika tarehe 5.07.2016.

TFDA kudhibiti madahara ya Dawa

T1 
Meneja Uhusinao wa mamlaka ya Chakula naD awa (TFDA) Bi. Gaudensia Simwanza (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mkakati wa Mamlaka hiyo kudhibiti madahara ya Dawa ikiwa ni moja ya majukumu yake ili kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa Salama.kushoto ni Afisa Usajili wa  Dawa  kutoka  TFDA Dkt. Alex Nkyamba.
T2 
Afisa Usajili wa  Dawa  kutoka  TFDA Dkt. Alex Nkyamba akionesha kwa waandishi wa habari fomu inayotakiwa kujazwa na wananchi pale wanapopata madhara yatokanayo na dawa Leo Jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na vyombo vya habari.Kulia ni Afisa Uhusinao wa mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bi. Gaudensia Simwanza
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)  na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
 (Picha na Maelezo)

Rais Shein atembelea maonesho ya Sabasaba

S1 
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akiangalia baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na wajasiliamali  wanawake wakati alipotembelea banda la Wanawake na Maendeleo (WIPE) katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mke wa Rais wa awamu ya tatu Mama Anna Mkapa.
S2 
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein  akipata maelezo toka kwa mjasiliamali juu ya vyakula vilivyosindikwa wakati alipotembelea banda la Wanawake na Maendeleo (WIPE), Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam mapema hii leo.
S3 
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto), akiangalia mafuta ya kula yanayotengenezwa na wajasiliamali , wakati alipotembelea banda la Wanawake na Maendeleo (WIPE), Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo.
S4 
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akiuliza swali kwa mjasiliamali wakati alipotembelea banda la wanawake Wajasiliamali  (WIPE), Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo.
S5 
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo kuhusiana na uzazi wa mpango, wakati alipotembelea banda la Wanawake na Maendeleo (WIPE), Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo.
S6 
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo toka kwa Mkurugenzi wa VETA kanda ya Dar es Salaam Bw. Habibu Bukko wakati alipotembelea banda la VETA katika  Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam mapema hii leo.
S7 
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo toka kwa Mkurugenzi wa VETA kanda ya Dar es Salaam Bw. Habibu Bukko wakati alipotembelea banda la VETA katika  Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam mapema hii leo.
S8 
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Waziri  wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar Balozi  Amina Salum Ali,wakati alipotembelea banda la Wanawake na Maendeleo (WIPE) katika  Viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam mapema hii leo.                 
Picha na Eliphace Marwa – Maelezo

Serikali kujenga shule za michezo kwa kila mkoa.

1 
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza na timu ya mpira wa miguu ya wasichana ya umri wa miaka 11 Fc Vito Malaika na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya kukabidhi Bendera ya Taifa kwa timu hiyo kwenda kushiriki mashindano ya mpira wa miguu ya Helsinki Cup nchini Finland Julai 8 mwaka huu  kushoto Mwakilishi wa Sport Development Aid Bw. Chigogolo Mohamed.
2 
Balozi wa Finland nchini Tanzania Pekka Hukka (kulia) akizungumza na timu ya mpira wa miguu ya wasichana ya umri wa miaka 11 ya Fc Vito Malaika na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya kukabidhi Bendera ya Taifa kwa timu hiyo kwenda kushiriki mashindano ya mpira wa miguu ya Helsinki Cup nchini Finland Julai 8 mwaka huu kushoto ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Annastazia James Wambura.
3Mwakilishi wa Sport Development Aid Bw. Chigogolo Mohamed akizungumza na timu ya mpira wa miguu ya wasichana ya umri wa miaka 11 Fc Vito Malaika na waandishi wa habari (hawapo pichani)  katika hafla ya kukabidhi Bendera ya Taifa kwa timu hiyo kwenda kushiriki mashindano ya mpira wa miguu ya Helsinki Cup nchini Finland Julai 8 mwaka huu.
4 
Kocha Mkuu wa timu ya wasichana ya mpira wa miguu ya Fc Vito Malaika akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya kukabidhi Bendera ya Taifa kwa timu hiyo kwenda kushiriki mashindano ya mpira wa miguu ya Helsinki Cup nchini Finland Julai 8 mwaka huu.
Nahodha wa timu ya mpira wa miguu Fc Vito Malaika, Alia Fikiri akizungumza na na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya kukabidhi Bendera ya Taifa kwa timu hiyo kwenda kushiriki mashindano ya mpira wa miguu ya Helsinki Cup nchini Finland Julai 8 mwaka huu.
6 
Baadhi ya wachezaji timu ya wasichana ya mpira wa miguu Fc Vito Malaika wakimsiliza Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (hayupo pichani)   katika hafla ya kukabidhi Bendera ya Taifa kwa timu hiyo kwenda kushiriki mashindano ya mpira wa miguu ya Helsinki Cup nchini Finland Julai 8 mwaka huu.
7 
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Annastazia James Wambura (wa pili kulia) akikabidhi Bendera ya Taifa kwa nahodha timu ya mpira wa miguu Fc Vito Malaika Alia Fikiri (kushoto) kwenda kushiriki mashindano ya Helsinki Cup nchini Finland Julai 8 mwaka huu.
8 
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Annastazia James Wambura akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Finland Tanzania Pekka Hukka wakati wa kukabidhi Bendera ya Taifa kwa timu ya mpira wa miguu ya wasichana ya Fc Vito Malaika inayoenda kushiriki mashindano ya  Helsinki Cup nchini Finland Julai 8 mwaka huu.
( Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM)
———————————–
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Serikali imeazimia kujenga na kuendeleza shule za michezo zilizopo katika mikoa yote nchini kwa kipindi hiki cha Serikali awamu ya tano.
Azimio hilo limetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura wakati akizungumza na timu ya mpira ya miguu ya wasichana ya Fc Vito Malaika katika hafla ya kukabidhi Bendera ya Taifa kwa timu hiyo kwenda kushiriki mashindano ya mpira wa miguu ya Helsinki Cup yatakayofanyika nchini Finland Julai 8 mwaka huu.
“Azima ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuendeleza michezo nchini kwa kuibua vipaji vya michezo na kuviendeleza kuanzia wakiwa shule” Alisema Mhe. Annastazia.
Mhe Annastazia Wambura ameongeza kuwa Serikali ya Tanzania inashirikia na Serikali ya Finland katika kuendeleza michezo shuleni na zaidi ya shule 462 nchini zitafaidika na miradi ya michezo ya vijana inayofadhiliwa na Serikali ya Finland.
Kwa upande wake Balozi wa Finland nchini Tanzania Pekka Hukka amesema kuwa wamedhamiria kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuendeleza michezo nchini hasa kwa vijana ili kujenga timu nzuri za baadae, na kwa sasa wanapeleka timu za vijana kwenda kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa ikwemo Helsinki Cup linalofanyika nchini finland Julai 8 mwaka huu.
Naye Meneja wa Timu ya wasichana ya mpira wa miguu ya Fc Vito Malaika Bakari selemani ameipongeza Serikali kwa juhudi zake za kuendeleza michezo hasa kwa vijana kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali na ili kuendeleza michezo na kukuza vipaji kwa vijana Serikali na wadau wa michezo wametakiwa kuwekeza kwa vijana ili kujenga timu zenye kuleta ushindani katika mashindano ya kitaifa na kimataifa.

MTOTO CLARA MWANAFUNZI ASIYEONA AKIWA DARASANI AKITUMIA MASHINE MAALUMU YA KUANDIKIA NA KUSOMA

index 
Mtoto Clara Damian  mwanafunzi wa darasa la saba asiyeona akiwa darasani akitumia mashine maalumu ya kuandikia na kusoma katika shule ya msingi patandi iliyopo wilaya ya arumeru mkoani arusha shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa walimu na vitabu.
Picha na mahmoud ahmad arusha

PRIDE TANZANIA YATOA HUDUMA YA MIKOPO KATIKA maonesho ya biashara ya kimataifa ya 40 SABASABA

1Muonekano wa banda la kampuni ya PRIDE Tanzania katika maonesho maonyesho ya biashara ya kimataifa ya 40 yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
2 
Moja ya bidha zinazotengenezwa na wajasiriamali wanaowezeshwa na PRIDE Tanzania.
3 
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage (kushoto), akizungumza na wajasiriamali wa  PRIDE Tanzania wakati maonyesho ya biashara ya kimataifa ya 40 yanayoendelea jijini Dar es Salaam (kulia) alievaa tisheti nyeupe ni Afisa Undeshaji Mwandamizi  PRIDE Tanzania, Jumanne Bundala.
4 
Kushoto Mwenyekiti wa Bodi ya PRIDE Tanzani, Profesa Wiliam lyakurwa, na kulia Meneja Mkuu PRIDE, Shimimana Ntayabaliwe wakimsililiza mjasiriamali mbunifu wa mavazi kutoka Zakwetu Afrika, Bi Asha Sendege wakati wa maonyesho ya biashara ya kimataifa ya 40 yanayoendelea jijini Dar es Salaam
5 
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akitembelea banda la PRIDE Tanzani kujionea wajisiriamali wa PRIDE wakati wa maonyesho ya biashara ya kimataifa ya 40 yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
6 
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akiangalia moja ya bidha kwa matumizi ya nyumbani zinazotengenezwa na wajasiriamali wa PRIDE.
7 
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akiangalia batiki zinazotengenezwa na wajariamali.
8 
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akiangana na wafanyaka wa PRIDE  mara baada ya kutembelea banda hilo.
10 
Meneja wa wa PRIDE Tawi la Kibaha, Bi Shani Madege akiwaelezea wananchi waliotembelea banda hilo kuhusiana huduma zinazotolewa na PRIDE.
11 
Afisa Uendeshaji wa PRIDE Edward Ngw’andu akimuezea mmoja wa wananchi juu ya faida za mkopo kwa mashariti nafuu.12 Wafanyakazi PRIDE Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja nje ya banda la Pride maonyesho ya biashara ya kimataifa ya 40 yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

ALEX MSAMA ATOA MSAADA KWA VITUO SITA VYA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM


Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutoa zawadi za vitu mbalimbali kwa vituo 6 vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu jijini Dar es Salaam, leo ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Sikukuu ya Eidd el Fitr. Zawadi hizo zimetokana na fedha zilizopatikana katika Tamash la Pasaka.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama (kulia),
akimkabidhi mlezi wa Kituo cha Kulelea watoto Yatima cha Irshaadi, Juma
Kaseja, sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya Sikukuu ya Eidd
el Fitr, hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam
Baadhi ya watoto waliohudhulia hafla hiyo.
Msama akitoa zawadi za Sikukuu ya Eid el Fitr.

Baadhi ya vitu mbalimbali vilivyotolewa na kampuni ya Msama Promotions Ltd,mapema leo jijini Dar katika
vituo sita.

Baadhi ya watoto waliohudhulia hafla hiyo
.

Msama akitoa zawadi za Sikukuu ya Eid el Fitr.

Watoto wakipokea zawadi.

Msama akigawa zawadi mbalimbali kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Msama akimkabidhi mtoto Fahari Haji vitu mbalimbali kwa ajili ya Sikukuu ya Eid el Fitr.

Wafanyakazi bora Konyagi wapongezwa

Kampuni ya kutengeneza vinywaji ya TDL kilichopo chini ya TBL Group imewapongeza wafanyakazi wake bora katika msimu huu ambapo imewatunukia zawadi mbalimbali katika hafla iliyofanyika katika kiwanda cha Konyagi kilichopo jijini Dares Salaam Akiongea wakati wa hafla hiyo Mkuu wa Idara ya Uhandisi wa kampuni hiyo aliwapongeza kwa kufanya kazi kwa bidii na kuongeza kuwa kampuni inathamini mchango wa kila mfanyakazi wake na ndio maana imekuwa na utaratibu wa kuwapatia tuzo mbalimbali.
Wafanyakazi hao walishukuru mwajiri wao kwa kuthamini na kutambua mchango wanaoutoa kwa kampuni
KON1 
Meneja idara ya  uhandisi  wa Kiwanda cha Konyagi  cha  jijini Dar es Salaam, Aranyaeli Ayo (kushoto)   akikabidhi zawadi kwa wafanyakazi  bora wa kampuni hiyo , Katikati ni  ofisa rasilimali watu  Anna Magari  .Hafla hiyo ilifanyika kiwandani hapo jana
KON2 KON3Wafanyakazi bora wa kampuni ya Konyagi katika picha ya pamoja na Maofisa wa kampuni hiyo  muda mfupi baada ya kutunukiwa zawadi

MBARAWA AFUNGUA MKUTANO WA KUJADILI NAMNA BORA YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA VIWANDA

B1

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifungua mkutano wa Uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam leo (jana), wa pili kutoka kulia ni Balozi wa China nchini Dr.Lu Youqing.
B6 
Baadhi ya Wajumbe wa mkutano wa Uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika wakifuatilia hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani), katika mkutano wa Uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika.
B2Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akizungumza jambo na Balozi wa China nchini Dr.Lu Youqing wakati wa mkutano wa Uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam leo .
B3 
Balozi wa China nchini Dr.Lu Youqing kulia akiongea na mmoja wa wajumbe wa mkutano huo Prof. Ibrahim Lipumba mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam
B4 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa kushoto akiongea na mjumbe wa mkutano huo  mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa Uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam leo
B5 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa kushoto akifurahia jambo  na Prof. Ibrahimu Lipumba mjumbe wa mkutano wa Uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.katikati ni Balozi wa China nchini Dr.Lu Youqing. B7 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa mkutano wa Uwezeshaji viwanda baina ya China na nchi za Afrika.
Picha na Benjamini Sawe-Maelezo.

IDARA YA URATIBU WA MAAFA YAKUTANA NA WADAU WA MASUALA YA MAAFA KUTOKA UMOJA WA KIMATAIFA.

R1Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brg. Jen, Mbazi Msuya akizungumza jambo wakati wa kikao na wadau wa masuala ya Menejimenti ya maafa kutoka Umoja wa Mataifa (UN) katika ofisi yake tarehe 05 Julai, 2016.
R2 
Mhandisi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Bw.Fanuel Kalugendo akizungumza jambo wakati wa kikao cha kujadili masuala ya upunguzaji athari za maafa na wadau kutoka Ofisi za Umoja wa Mataifa katika Julai 5, 2016 Jijini Dar es Salaam.
R3 
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa kushoto) akiteta jambo na wadau wa masuala ya Menejimenti ya Maafa kutoka Ofisi za Umoja wa Mataifa Katikati ni Mwakilishi mkazi Umoja wa Mataifa Bw. Alvaro Rodriguez na Mratibu Bi. Mona Folkesson Julai 5, 2016.
R4 
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (watatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Idara ya Uratibu wa Maafa na wadau wa masuala ya Maafa kutoka Ofisi za Umoja wa Mataifa mara baada ya kujadili masuala ya menejimenti ya Maafa Ofisini hapo Juali5, 2016.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

CMSA YAZINDUA SHINDANO KWA WANAVYUO

Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nasama Massinda
Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nasama Massinda akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Shindano la insha na maswali kuhusu Masoko ya Mitaji kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam Julai 4, 2016.
Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) jana Jumatatu, Julai 4, 2016 imezindua shindano la insha na maswali kuhusu Masoko ya Mitaji kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu Juu ya Tanzania kwa mwaka 2016.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Bibi Nasama M. Massinda alisema shindano hilo lina lengo la kuongeza ueledi na ufahamu kuhusu masoko ya mitaji kwa wanavyuo hapa nchini hali ambayo inatarajia kuchangia ongezeko la ushiriki wa Watanzania kama wawekezaji, watoa dhamana na wataalum wa kutoa huduma katika masoko ya mitaji pindi wanapohitimu masomo yao.

‘Shindano hili lijulikano kama Capital Markets University Challenge lina sehemu mbili – insha na sehemu ya maswali kuhusu masoko ya mitaji kwa wanafunzi wa vyuo na taasisi za elimu ya juu, alisema Bi Massinda huku akiongeza kuwa wanafunzi watapata fursa ya kuongeza elimu juu ya kuwekeza akiba kwa njia endelevu na kuongeza matumizi ya Tehama kwa wanavyuo.

 
Wanavyuo watashiriki Shindano la maswali na majibu kwa kutumia simu za kiganjani kwa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwenda namba 0766 046046, na kwa kutumia tovuti na mtandao wa kompyuta. Kwa upande wa insha, wavyuo wanatikiwa kuandika insha kuhusu fursa na faida za kutumia masoko ya mitaji katika miradi ya maendeleo nchini. 

Insha hiyo inatakiwa isizidi kurasa nne (4) na kutuma kwa barua pepe kwenda challenge@cmsa-tz.org. Mshindi wa jumla katika kila shindano atapata zawadi ya 1,800,000/- huku mshindi wa pili akipata 1,400,000/-. Pia washindi kutoka vyuo vitatu bora – wavulana na wasichana, watapata fursa ya safari ya wiki moja kutembelea makao ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana jijini Dar es Salaam.

Capital Markets University Challenge ilizinduliwa mwaka jana ambapo liliendeshwa kwa mafanikio makubwa na kuvuka lengo la ushiriki kwa zaidi ya 300%. 


‘Mafanikio hayo yalitokana na jitihada za kuhamasisha matumizi ya technolojia ya habari kwa matumizi ya simu za kiganjani, mtandao wa kompyuta, barua pepe na wavuti, asema Bi Massinda huko akiongeza kuwa mafanikio hayo yaliandika historia mpya katika sekta ya masoko ya mitaji katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini.

Shindano ya Capital Markets University Challenges ilizinduliwa tarehe 4 Julai 2016 na likafika tamata Agosti 15, 2016.

Mkurugenzi wa Utafiti, Sera na Mipangowa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Nicodemus Mkama
Mkurugenzi wa Utafiti, Sera na Mipangowa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Nicodemus Mkama akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Shindano la insha na maswali kuhusu Masoko ya Mitaji kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam Julai 4, 2016.

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI NA MADINI DK. PALLANGYO AJIONEA ZOEZI LA UOKOAJI VIWANJA VYA SABASA

Ofisa wa Matukio ya Dharura wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico), Jeremia Ibambasi (kulia), akitoa maelezo mafupi kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dk Juliana Pallangyo ya uokoaji kwa mtu aliyemeza hewa chafu katika kiwanda cha uchanjuaji dhahabu katika maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam 2016 alipotembelea Banda la Wizara hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dk Juliana Pallangyo (kulia), akiangalia waokoaji wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico) jinsi wanavyomsaidia mtu aliyevuta hewa chafu kwenye kiwanda cha uchanjuaji dhahabu nje ya banda la Wizara ya Nishati na Madini katika maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam 2016 katika viwanja vya Biashara vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo mchana.
Waokoaji wakiondoka na majeruhi wakimpeleka lilipo gari la kubebea wagonjwa tayari kumpeleka mgonjwa Hospitali.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dk Juliana Pallangyo akiagana na maofisa mbalimbali wa wizara yake baada ya kwisha kwa zoezi hilo la uokoaji.

JOSE MOURINHO AONGEA NA WAANDISHI WA HABARI NA KUSEMA ANAHITAJI UBINGWA WA LIGI KUU YA UINGEREZA


KAMPUNI YA EMOTEC YAJIPANGA KUTOA HUDUMA BORA ZA TEHAMA

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Emotec Limited, Bw. Moses Hella, akielezea moja kati ya gunduzi za kampuni yake kwa wageni (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kuazimisha miaka minne ya Chinese AlumniAssociation.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Emotec Limited, Bw. Moses Hella (kulia) akielezea moja kati ya gunduzi ya kampuni yake kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Profesa Elisante Ole Gabriel (Wapili Kulia) wakati wa hafla ya kuazimisha miaka mine ya Chinese Alumni Association nchini hivi. 
Kampuni mpya ya masuala ya TEHAMA nchini Tanzania, Emotec Limited yaeleza kuwa imejizatiti katika kutoa huduma bora na zenyeubunifu wa hali ya juu kwa wateja wake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Emotec, Bw. Mosses Hella imesema kuwa kampuni yake ina mpango wa kuwa inayoongoza katikautoaji wa huduma na bidhaa bora katika soko la TEHAMA nchini.

“Tumedhamiria kutoa bidhaa za gharama nafuu, huduma bora, za kibunifu na suluhisho kwa wateja wetu. Lengo letu kuu ni kuwa kampuni yenye ubunifu zaidi iliyojizatiti katika utoaji wa huduma bora naza gharama nafuu katika mausuala ya TEHAMA nchini.” Alisema Bw. Hella.

RAIS BARACK OBAMA AMFANYIA SHEREHE YA KUZALIWA MWANAE MILIA



Rais Barack Obama wa Marekani amemfanyia bonge la sherehe ya kuzaliwa binti yake Milia wakati akitimiza miaka 18.



Sheria hiyo ilifanyika ikitumbuizwa na Kendrick Lamar ambapo Rais Obama alimuimbia wimbo wa Happy Birthday Milia licha ya kutozingatia vina vyake.
Rais Obama akimuimbia Milia huku Kendrick Lamar akipiga makofi na kutabasamu kulia ni nyota Janelle Mona 
                      Birthday girl Milia akiwa na furaha tele katika siku yake ya kuzaliwa

BANDA LA MFUKO WA GEPF LAWA KIVUTIO KIKUBWA KWA WAJASIRIAMALI KATIKA VIWANJA VYA MAONESHO YA SABA SABA MJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na walemavu Mh Jenista Mhagama akipata maelezo kutoka kwa maafisa wa GEPF ya jinsi Mfuko ulivyofanikiwa kutoa huduma kwa wajasiriamali.
Pichani Mh Jenista Mhagama akitia saini kitabu cha kumbukumbu za wageni waliopita katika banda la GEPF.
Uzinduzi wa Boda boda Scheme ulivutia wadau wengi wa sekta ya hifadhi ya jamii nchini. Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kahyarara baada ya kupata maelezo ya mafanikio ya Boda Boda Scheme kutoka kwa Afisa masoko Bw Valence Masebu.
Wanachama wa Mfuko toka Jeshi la Polisi wakifurahia jambo na Afisa Masoko Bw Adam Hamza baada ya kukabidhiwa statements za michango yao.

ICELAND YAPOKELEWA KISHUJAA BAADA YA KUTOLEWA HATUA YA ROBO FAINALI

Wachezaji wa timu ya soka ya Iceland wamepokelewa kishujaa baada ya kurejea kutoka katika michuano ya Euro 2016, huku maelfu ya mashabiki wao wakiwa mitaani ya mji Reykjavik
kuwashuhudia.

Timu hiyo ilienda Ufaransa ikiwa ni moja ya taifa dogo kabisa kuwahi kushiriki michuano ya Euro, likiwa na wananchi wapatao 332,529.

Hata hivyo Iceland haikujali ugeni wala udogo katika michuano hiyo kwani ilifanya vyema hadi kutinga robo fainali ambapo ilitolewa na Ufaransa kwa magoli 5-2.
         Wachezaji wa Iceland wakiwa juu ya basi lao wakishangiliwa na mashabiki wao 
Wachezaji wa Iceland wakiwapungia mikono mashabiki wao kuwashukuru kwa mapokezi makubwa

No comments :

Post a Comment