Thursday, June 2, 2016

UJUMBE WA JIANGSU CHINA WAKUTANA NA DKT SHEIN LEO

na1 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu wa Chama cha Kikoministi cha China kutoka Kamati ya Jimbo la Jiangsu Bw.Luo Zhijon,(kulia) akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni,[Picha na Ikulu.] 02/06/2016.
na2 

na3 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na Ujumbe wa Chama cha Kikoministi cha China kutoka Kamati ya Jimbo la Jiangsu ukiongozwa na Katibu wake  Bw.Luo Zhijon,(kushoto) mara  ujumbe huo ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni,[Picha na Ikulu.] 02/06/2016.
na4 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na Ujumbe wa Chama cha Kikoministi cha China kutoka Kamati ya Jimbo la Jiangsu ukiongozwa na Katibu wake  Bw.Luo Zhijon,(wa tatu kulia) mara  ujumbe huo ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni,[Picha na Ikulu.] 02/06/2016.

Wadau wa watakiwa kutoa mchango wa kuboresha kanuni za upatikanaji wa mbolea nchini.

tur1 
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Florence Turuka akifungua warsha ya wadau wa mbolea iliyofanyika leo jiji Dar es Salaam kujadili na kuboresha sheria na kanuni zinazosimia sekta ya mbolea nchini ili kuwa na kilimo chenye tija kwa Watanzania na taifa kwa ujumla.
tur2 

tur3 
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Florence Turuka (katikati aliyekaa )akiwa picha ya pamoja na wadau wa mbolea mara baada ya kufungua warsha ya wadau ha oleo jijini Dar es salaam.
…………………………………………………………………………………………….
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Wadau wa mbolea wameaswa kuangalia namna ya kuboresha sheria na kanuni za kusimamia sekta ya mbolea kwa manufaa ya wananchi wanaojishughulisha na kilimo ili kiwe na tija kwa Watanzania na taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Florence Turuka alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa mbolea uliofanyika leo jiji Dar es Slaam.
Dkt. Turuka amesema kuwa maeneo ya kuzingatiwa katika warsha hiyo ni pamoja na kuboresha sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya mbolea ili kuwezesha sekta binafsi kushiriki katika kuinua kilimo kwa manufaa ya Watanzania.
Gharama hizo zinahusisha kufanyiwa majaribio mbolea zinazotoka nje ya nchi kabla ya kuanza kutumiwa na wakulima ambapo majaribio hayo yanafanyika kwa misimu mitatu ya kilimo.
Maeneo mengine ya kurekebisha ni pamoja na mlolongo wa tozo ambazo zimekuwa zikitozwa kwenye mbolea inayoingizwa nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika linalojishughulisha na matumizi ya mbolea Bara la Afrika anayesimamia eneo la Tanzania Dkt. Mshindo Msolla amesema kuwa kazi kubwa waliyonayo wajumbe katika warsha hiyo ni kuhakikisha sheria na kanuni wanazozifanyia kazi zitasaidia kuboresha upatikanaji wa mbolea zenye ubora unaotakiwa kulingana na mahitaji ya wakulima na waipate kwa wakati.
“Wakulima hapa nchini wananufaika na huduma zetu ambazo tunatoa ikiwemo kuwaunganisha na mawakala wakubwa wa pembejeo na makampuni yanayozalisha au kuingiza mbolea nchini” alisema Dkt. Msolla.
Kuhusu hali ya upatikanaji wa mbolea nchini, Dkt. Msolla amesema kuwa shirika hilo linatoa huduma katika mikoa 12 nchini ambapo wapo mawakala 30 wanahudumia mawakala wadogo 500.
Mikoa hiyo ni Arusha,Kilimanjaro,Manyara, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Ruvuma, Rukwa, Katavi na Kigoma.
Mawakala hao msimu wa mwaka 2014/2015 wamefanikiwa kuuza kwa wakulima mbolea tani 60,000 na mbegu tani 3000 ambazo zimekuwa na manufaa katika kuhakikisha upatikanaji wa mazao ya chakula na biashara nchini.
Aidha, shirika hilo limefanikiwa kuwaunganisha wakulima na makampuni ya mbolea sita ikiwemo YARA, Extra Trading, Premium Agrochemical pamoja na Minjingu.
Vile vile, Dkt. Msolla amesema kuwa wakulima wamenufaika na kujengewa maghala 14 hadi sasa yameanza kutumika ambayo yanauwezo wa kuhifadhi tani 50,000 kwa wakati moja hatua ambayo inasaidia kusogeza huduma karibu na wakulima wanapozihitaji.
Dkt. Msolla amesema kuwa Shirika hilo lenye makao yake makuu Afrika Kusini linatoa huduma kwa sekta ya mbolea katika nchi mbalimbali Barani Afrika ikiwemo nchi tatu za kipaumbele ambazo ni Tanzania, Msumbiji na Ghana, nchi nyingine ambazo shirika hilo linafanya kazi ni Ethiopia, Senegal, Ivory Coast na Nigeria.

KATIBU WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA JIMBO LA JIANGSU AFANYA ZIARA YA SIKU MBILI ZANZIBAR.

chi1 
KATIBU wa Chama cha Kikomunisti cha China katika Jimbo la Jiangsu Luo Zhijun, akivishwa shada la mauwa mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
chi2 
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Ussi Gavu, akisalimiana na Katibu wa Chama cha Kikomunisti cha China katika Jimbo la Jiangsu Luo Zhijun wakati mgeni huyo alipowasili katika uwanja wa ndege mjini Zanzibar.
chi3 
Katibu wa Chama cha Kikomunisti cha China (aliyevaa shati jeupe) Luo Zhijun, akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Ussi Gavu (wa kwanza kushoto).
chi4 
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Ussi Gavu, akizungumza na Katibu wa Chama cha Kikomunisti cha China Jiangsu Luo Zhijun katika ukumbi wa watu mashuhuri (VIP) uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Abeid Karume Zanzibar. Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar.

Zaidi ya Bilioni 4 kutumika kuwezesha wajasiriamali Kinondoni

bil1 
Afisa uhusiano wa Manispaa ya Kinondoni  Bw. Sebastian Mhowera akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mikakati ya Manispaa hiyo kuwawezesha wanawake na vijana kupitia mfuko maalum ulioanzishwa na Serikali ili kutoa mikopo kwa wajasiriamali hao ili kuwajengea uwezo kushiriki kujenga uchumi.kulia ni AfisaUhusiano wa Manispaa hiyo Bw.Bornwell Kapinga.
…………………………………………………………………………………………………………….
Frank Mvungi-Maelezo
Serikali kutumia zaidi ya bilioni 4 kuwawezesha wajasiriamali wadogo katika Manispaa ya Kinondoni katika Kipindi cha mwaka 2016/2017 ili kuchochea kasi ya ukuachi wa uchumi.
Kauli hiyo imetolewa Leo Jijini Dar es salaam na Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Sebvastian Mhowera wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.
Akifafanua Mhowera amesema fedha hizo zitatolewa kupitia Mfuko wa wanawake na Vijana unaolenga kuwawezesha kishiriki katika shughuli za uzalishaji hali itakayachangia kukuza uchumi.
Kwa Sasa manispaa ya Kinondoni inajumla ya Vikundi 546 vya wanawake na vijana vyenye jumla ya wajasiriamali 2729 ikilinganishwa na vikundi 40 na wanufaika 200 waliokuwepo mwaka 2013.
Wajasiriamali wanaonufaika na fedha za mfuko huo ni wale wanajishughuisha na shughuli za Kiuchumi ikiwemo kilimo,Biasharandogondogo,Ushonaji,Ufugaji,Uvuvi,Mafundi seremala,wasusi.
Pia Mhowera alitoa wito kwa wajasiriamali wa Wilaya ya Kinondoni kujitokeza  kuchangamkia fursa zinazotokana na mfuko wa wanawake na vijana.
Kuanzishwa kwa mfuko huu katika manispaa ya Kinondoni ni utekelezaji wa agizo la Serikali Kuu lililoagiza Halmashauri zote nchini kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya mfuko wa kuwawezesha wanawake na vijana.
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inaandaa maonesho kwa ajili ya wajasiriamali  wadowadogo wanaonufaika na Mikopo ya Mfuko wa wanawake na vijana inayotolewa na Manispaa hiyo ambapo maonesho hayo yatafanyika mwishoni mwa wiki ijayo.

No comments :

Post a Comment