MFUKO WA PENSHENI WA PPF KUTOA HUDUMA ZOTE KWA WATEJA WAKE VIWANJA VYA SABASABA 2016
Muonekano
wa nje ya Jengo la PPF lililopo Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya
Kimataifa vya Mwalimu Nyerere jijini Dar esSalaam (Sabasaba).
Maandalizi
Afisa
Mafao wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Tulla Mwigune (kulia) Afisa Michango
wa Mfuko huo, Saluna Aziz Ally (katikati) na Afisa Michango Glory
Maboya, wakijiandaa kuhudumia wateja leo asubuhi katika Maonesho ya
Biashara ya Kimataifa Sabasaba.
Afisa
Utafiti Neema Mjema (nyuma) na Mwanasheria wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,
Nyambilila Ndoboka, pia wakijiandaa kuweka mambo sawa kabla ya kuanza
kupokea wateja katika Bandao lao la Maonesho kwenye Viwanja vya Sabasaba
leo.
Afisa
Uwekezaji wa Mfuko huo, Jonas Mbwambo akiweka mambo sawa kabla ya
kuanza kupokea wateja katika Banda lao namba 86 viwanja vya Saba saba.
Afisa
Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Pauline Msanga, akitoa maelezo
kwa wananchi kuhusu Huduma za uendeshaji Mfuko huo, wakati
walipotembelea katika Banda lao lililopo kwenye Viwanja vya Sabasaba
jijini Dar es Salaam, leo.
Sehemu
ya wananchi waliotembelea Banda la Mfuko wa Pensheni wa PPF wakipata
elimu kuhusu Mafao yatolewayo na Mfuko huo na jinsi mwanachama
anavyoweza kujiunga na kuchangia.
Afisa Michango wa Mfuko huo, Saluna Aziz Ally, akimfafanulia mwanachama wake kuhusu uchangiaji wa michango ya Wanachama,
Afisa
Huduma kwa Wateja, wa PPF Mwajuma Msina, akizungumza na Mwananchi
aliyefika kutembelea Banda hilo wakati akimwelezea kuhusu huduma
zinazotolewa na Mfuko huo.
Afisa Mafao wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Tulla Mwigune (kulia) akifafanua jambo kwa mstaafu wa PPF.
Mtaalamu wa Mifumo ya Habari wa Mfuko wa PPF, Isabela Ngalawa,
akimwelekeza mmoja kati ya Wanachama wa Mfuko huo kuhusu 'PPF Taarifa
Mobile Apps' ili mwanachama aweze kupata taarifa za michango yake
kupitia simu yake ya mkononi.
Afisa
Huduma kwa Wateja, Mohamed Siaga, akizungumza na Mwananchi aliyefika
katika Banda la PPF kuhusu jinsi ya kujiunga na Mfumo wa 'Wote scheme
kutoka sekta isiyo rasmi
Mmoja
kati ya Wanasheria wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Nyambilila Ndoboka,
akimwelekeza jambo mwanachama wa Mfuko huo kuhusu masuala ya Kisheria,
wakati alipofika kutembelea Banda la Maonesho la PFF leo.
Afisa
Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Temeke, Sostenes Lyimo
(kushoto) akifafanua jambo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea Banda
hilo.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiwa katika picha ya
pamoja mbele ya Banda lao Namba 86 lililopo katika Viwanja vya Sabasaba
MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI DODOMA
Waziri
wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijibu maswali
ya Wabunge Leo Bungeni Mjini Dodoma kuhusu mpango wa Serikali wa
kuimarisha Viwanda vilivyopo hapa nchini na kujenga vipya katika Mikoa
mbalimbali.
Waziri
wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya ufundi Mhe. Dkt. Joyce
Ndalichako akieleza juu ya mkakati wa Serikali kuimarisha vyuo vya
Ufundi Stadi hapa nchini wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni
Mjini Dodoma.
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakiyembe akiteta jambo na
Mbunge wa Korogwe Vijijini Mhe. Steven Ngonyani Bungeni Mjini Dodoma
Leo.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango akijibu hoja za wabunge kuhusu
Muswada wa Marekebisha ya Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2016 Leo
Bungeni Mjini Dodoma.
Naibu
Waziri Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani
akitoa ufafanuzi kuhusu mikakati ya Serikali kuimarisha miundombinu ya
Barabara hapa Nchini.
Naibu
Waziri Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani
akitoa ufafanuzi kuhusu mikakati ya Serikali kuimarisha miundombinu ya
Barabara hapa Nchini.
Mbunge
Viti Maalum Mhe. Martha Mlata akichangia hoja wakati wa uwasilishwaji
wa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2016.
Baadhi ya Wabunge wakimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Mpango (wa katikati) mara baada ya kupitishwa kwa muswada wa
Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma.
(Picha zote na Frank Mvungi-Dodoma)
Bunge limepitisha muswada wa marekebisha ya sheria ya ununuzi wa umma wa mwaka 2016
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
——————–
Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha muswada wa
marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma wa Mwaka 2016 wenye lengo la
kupunguza gharama na muda wa mchakato wa manunuzi Serikalini.
Marekebisho
hayo yametokana na gharama kubwa ambayo Serikali imekuwa ikitumia
kutokana na huduma na Bidhaa zinazonunuliwa na Serikali kuwa za juu
ikilinganishwa na bei ya wastani ya soko.
“Muswada
wa Marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2016 una lengo la
kuongeza ufanisi katika ununuzi wa Umma kwa kuondoa mapungufu yaliyopo
katika Sheria ya sasa kwa kupunguza gharama na muda wa michakato ya
ununuzi, kutoa upendeleo kwa kampuni za ndani, vikundi maalum, malighafi
na bidhaa zinazozalishwa nchini pamoja na kuweka viwango mahsusi kwa
bidhaa zitakazotumiwa na Serikali,” alifafanua Mwanasheria Mkuu wa
Serikali Mhe. George Masaju.
Mhe.
Masaju ameendelea kwa kusema kuwa sheria hiyo imeweka kifungu cha
dharura ili kuwezesha vitu vya kuokoa uhai na vinginevyo kununuliwa kwa
dharura pindi inapobidi.
Kwa
upande wake Mbunge wa Babati Vijijini Mhe. Jitu Soni yeye ameiomba
Serikali kuruhusu kununua vifaa tiba vilivyotumika ambavyo muda wake wa
kutumia hauna mwisho, kwa mfano vitanda vya kujifungulia ili kupunguza
gharama ya kununua vitanda vipya na kuweza kununua vitanda vingi kwa
wakati mmoja.
Aidha
Mhe. Jitu ameiomba Serikali kuirudisha tena Sheria hiyo Bungeni baada
ya mwaka mmoja ili kufanyiwa marekebisho na kuziba mianya yote ambayo
itakuwa imebainika mara baada ya utekelezaji wake kuanza.
Muswada
wa marekebisho ya sheria hiyo yanasubiri kusainiwa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli ili kuanza utekelezaji
wake.
Viwanda visivyo endelezwa kurudishwa kwa watanzania
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage
—————————————————
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Viwanda vilivyobinafsishwa na Serikali ambavyo haviendelezwi kutwaliwa ili kutolewa kwa wawekezaji wenye uwezo wa kuviendesha.
Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage ameyasema hayo leo mjini Dodoma alipokuwa
akijibu swali la Mbunge wa Tabora Mjini Mhe. Emmanuel Mwakasaka
aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa juu ya mwekezaji wa kiwanda cha
nyuzi Tabora kwa kushindwa kuendeleza kiwanda hicho.
“Wizara kwa kushirikiana na Ofisi
ya Msajili wa Hazina inaendelea na tathmini ya viwanda vyote
vilivyobinafsishwa na Serikali kikiwemo kiwanda cha nyuzi cha Tabora ili
kujiridhisha kama wawekezaji wa viwanda hivyo wanatimiza matakwa ya
mkataba na Serikali,” alifafanua Mhe. Mwijage.
Aliendelea kwa kusema kuwa, ikiwa
viwanda hivyo vitabainika kubadilishwa matumizi yake au kutoendelezwa
basi Serikali itavirudisha kwa watanzani ili viweze kuendelezwa.
Aidha Mhe. Mwijage amesema kuwa,
kwa sasa mwitikio wa kuviendeleza viwanda ambavyo vilikuwa havizalishi
ni mzuri kwani viwanda vingi vimeanza kufanya kazi lakini kwa wale ambao
watashindwa kabisa kuviendeleza basi viwanda hivyo vitarejeshwa kwa
watanzania.
Vile vile Mhe. Mwijage amesema
kuwa dhana ya Serikali ya awamu ya Tano ya kujenga uchumi wa viwanda
inaenda pamoja na kurejesha Serikalini viwanda vyote vilivyobinafsishwa
lakini haviendelezwi ili vitolewe kwa wawekezaji wengine.
Sambamba na hayo Mhe. Mwijage
amesema kuwa kufufua viwanda, hasa viwanda vya nguo ni pamoja na
wakulima wa pamba kulima zao hilo kwa wingi kwa ajili ya uchakataji
pamoja na kudhoofisha uingizaji wa nguo za mitumba nchini.
Wizara hiyo inaendelea na
kushawishi wawekezaji mbalimbali ili kujenga viwanda vingi iwezekavyo
kwa ajili ya uchakataji wa mazao yanayolimwa nchini pamoja na mifugo.
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam YASHIRIKI MAONESHO YA SABASABA
Mtendaji
Mkuu wa Mahakama Tanzania Bw. Hussein Kattanga akisikiliza maelezo
kutoka kwa Mtendaji Mkuu Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Bi. Mary
Shirima wakati wa maonyesho ya kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijin
Dar es Salaam
Wanausalama
wakiimarisha ulinzi katika viwanja vya sabasaba ili wafanyabiashara na
wananchi waweze kufanya shughuli zao kwa amani.
Mwanafunzi
kutoka chuo cha VETA wa pili kutoka kulia akiwaelekeza baadhi ya
wananchi ubunifu wa kutengeneza boti itakayokuwa inatembea barabarani
kwa kuendeshwa na dereva mpaka baharini
Picha na Benjamin Sawe
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) LAANZA KUTOA HUDUMA KATIKA MAONESHO YA 40 YA KIMATAIFA ya SABASABA
Banda la Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC) likiwa katika Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya
Biashara, yanayofanyika kila mwaka katika viwanja vya Mwalimu Nyerere
Sabasaba jijini Dar es salaam tayari limeanza rasmi kutoa huduma zake
katika viwanja hivyo.
Afisa
Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),Bi
Edith Nguruwe akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda la (NHC)
kuhusina na huduma zinazotolewa na Shirika hilo.
Afisa Mauzo Mwandamizi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Emmanuel
Limo (kushoto), akimuelezea Wananchi Kuhusiana na mradi wa SAFARI CITY
uliopo Arusha alipotembelea banda hilo katika maonesho ya Sabasaba.
Afisa
biashara (NHC), Clara Lubanga akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa Wananchi
aliotembelea banda hilo kuhusiana uzwaji wa nyumba (katikati), Afisa
Mauzo wa (NHC), Joseph Haule.
Afisa Mauzo (NHC), Jasson Ipyana akimuelezea mwananchi kuhusina na miradi ya nyumba ya bei nafuu ilioko nchini.
Bw: Klison Sanane (kushoto), akifafanua miradi mbalimbali ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Aika Swai (kushoto), akielezea kuhusiana na utaratibu wa unaoutumika katika ununuzi wa nyumba za (NHC) huku baadhi ya wadau kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakimsikiliza kwa umakini.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG.
Rais Magufuli Awataka wakuu wa Wilaya na mikoa kuchapa kazi.
Na Daudi Manongi,MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Magufuli amewataka wakuu wa wilaya na mikoa
kuchapa kazi kwa bidii kwani viongozi hao ndio wawakilishi wa wananchi
wa vijijini.
Mhe.Rais Magufuli ameyasema hayo
alipokuwa akizungumza wakati wakuu wa wilaya na mikoa walipokuwa Ikulu
wakila kiapo cha maadili ya viongozi kabla ya kwenda kuapishwa na wakuu
wa mikoa yao.
Rais Magufuli pia amewataka
viongozi hao kufanya kazi na kutimiza majukumu yao kwani wananchi wana
changamoto nyingi,na wao waende kutatua matatizo ya wananchi walio
maskini.
Aidha amewataka viongozi hao
kutokuwa chanzo cha kutengeneza matatizo katika jamii na hivyo wasimamie
haki na ukweli,wasiwe wala rushwa,wazingatie maadili na kuwatumikia
wananchi wote bila kujali itikadi za vyama zao,dini au kabila uku
akiwataka kutekeleza waliyohaidi kwenye ilani ya chama cha mapinduzi.
Pia amewataka viongozi hao kuweke
mkazo katika kutatua kero za wananchi na kuwataka kutimiza kwa vitendo
kwa kushirikiana na viongozi watakaowakuta katika maeneo yao
waliyopangiwa.
Hata hivyo amewataka viongozi hao
kusimamia mapato ya Serikali katika miradi yote kwenye maeneo yao ili
kuhakikisha serikali inapata kodi ambayo itasaidia katika maendeleo ya
Taifa hili.
Makamu wa Rais awataka wakuu wa wilaya na mikoa kukamilisha zoezi la madawati kabla ya June 30.
Na Daudi Manongi,MAELEZO
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu
amewataka wakuu wa wilaya na mikoa kuhakikisha wanamaliza zoezi la
upatikanaji wa madawati kwa shule za msingi na sekondari.
Mhe. Suluhu ameyasema hayo leo
Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati wakuu wa wilaya na mikoa walipokuwa
Ikulu wakila kiapo cha maadili ya viongozi kabla ya kwenda kuapishwa na
wakuu wa mikoa yao.
Aidha amewaagiza viongozi hao
kusoma alama za nyakati kwa kuangalia makosa ya waliokuwepo kabla yao
ili kuhakikisha hawarudii makosa yaleyale.
Mhe.Suluhu pia amesema kuwa
Serikali haitaki kusikia wananchi wanalia njaa na hivyo wakuu wa wilaya
wahakikishe chakula kinapatikana katika maeneo yao kwani hilo ni jukumu
lao.
Aliongeza kuwa wakuu wa wilaya
wana majukumu makubwa ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote za
muhimu katika maeneo yao kwani wananchi wana mategemeo makubwa juu yao.
Aidha ameagiza wakuu wa Wilaya
hao kufanya kazi karibu na Maafisa Tarafa ili kujua kero za wananchi na
kuzifanyia kazi kwa kasi ili wananchi wafaidike na maendeleo yawafikie
kwa haraka.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene
ivi karibuni aliwaagiza wakua wa wilaya na mikoa kuhakikisha wanatimiza
agizo la Rais John Pombe Magufuli kuhakikisha hakuna mwanafunzi
atakayekaa chini kwa uhaba wa madawati kufikia June 30,2016.
Waziri Mkuu ahagiza wakuu wa Wilaya na Mikoa kutembelea Vijijini ili kujua matatizo ya wananchi.
Na Daudi Manongi,MAELEZO
Waziri mkuu Mhe.Kassim Majaliwa
ameagiza wakuu wa wilaya na mikoa kufanya ziara katika maeneo yao hasa
vijijini ili kujua matatizo ya wananchi wao kwa ukaribu na kuyapatia
ufumbuzi.
Mhe.Majaliwa ameyasema hayo leo
hii Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wakuu wa wilaya na mikoa
walipokuwa Ikulu wakila kiapo cha maadili ya viongozi kabla ya kwenda
kuapishwa na wakuu wa mikoa yao.
Aidha Waziri Mkuu amesema kuwa
wakuu wa mikoa na wilaya waache kukaa maofisini mwao badala yake
watembelee wananchi na hasa wale wa hali ya chini ili kujua matatizo yao
ya Ardhi na kupatia ufumbuzi migogoro ya wafugaji na wakulima.
Pia Mhe.Majaliwa amewasisitiza
wakuu hao kutambua kwamba majukumu waliyonayo ni makubwa na wananchi
wana mategemeo makubwa juu yao na hivyo ni budi wakatekeleza wajibu wao
na kuhakikisha watanzania wanapata huduma zote za muhimu kwa kutumia
elimu, uwezo, uadilifu, uaminifu na uwajibikaji walionao ili kufanikisha
maendeleo kwa wananchi.
Aliongeza kuwa wakuu hao wana
jukumu kubwa la kusimamia pesa za serikali pesa za miradi zinakokwenda
katika halmashauri za wilaya zao na kukazia kuwa Serikali haitasita
kuchukua hatua kwa yeyote ambaye hatofanya kazi zake kikamilifu.
Waziri mkuu amewaagiza wakuu wa
Mikoa kushirikiana kwa karibu na wakuu wa Wilaya ili kutafuta ufumbuzi
wa matatizo ya maeneo yao kwani wananchi wana kiu ya maendeleo katika
maeneo yao.
No comments :
Post a Comment