Wednesday, June 29, 2016

MFUKO WA PENSHENI WA LAPF WASHIRIKI MAONYESHO YA SABA SABA 2016

L 
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. James Mlowe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sababu za ushiriki wa Mfuko katika maonyesho ya biashara ya kimataifa (Saba Saba 2016).
L2 
Afisa Mifumo ya kompyuta kutoka Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. Yohana Nyabili akitoa maelezo kwa mwanachama wa Mfuko pamoja na kumpatia taarifa ya michango yake mara baada ya mwanachama huyo kutembelea banda ya Mfuko kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa (Saba Saba 2016).

KONGAMANO LA KUBADILISHANA UZOEFU WA MAFUNZO YA TAALUMA UFARANSA NA TANZANIA LAFANYIKA DAR

Reginald Mengi
Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald Mengi akifungua kongamano hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.
Dkt. Tausi Kida
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki na wadau wengine katika kongamano hilo.
Balozi wa Ufaransa nchini, Mh. Malika Berak
Balozi wa Ufaransa nchini, Mh. Malika Berak akizungumza kwenye kongamano hilo.
ESRF Conference Hall
Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki kutoka sekta binafsi, serikalini pamoja na taasisi mbalimbali walioshiriki kwenye kongamano hilo.
KONGAMANO kubwa la aina yake limefanyika mjini Dar es salaam ambapo washiriki walizungumzia namna ya kuendeleza rasilimali watu katika eneo la utaalamu na taaluma katika shughuli mbalimbali za uendelezaji wa makampuni na viwanda.

Kongamano hilo ambalo lilihudhuria na watu wenye kariba kubwa katika masuala ya viwanda na biashara akiwemo Dkt. Reginald Mengi ambaye ni Mwenyekiti wa makampuni ya IPP na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF);na Balozi wa Ufaransa nchini Malika Berak liliangalia uhaba wa wataalamu na namna ya kuuondoa uhaba huo wakati taifa linaelekea katika uchumi wa kati unaotegemea viwanda.

Wengine waliokuwepo katika kongamano hilo Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero na maofisa wa serikali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akikaribisha washiriki na wadau wengine alisema kwamba mafunzo hayo yaliyoratibiwa kwa pamoja katika wataalamu wa Ufaransa, ESRF na Benki ya Maendeleo ya Afrika yamelenga kudadavua tatizo lililopo na kulipatia ufumbuzi.

Dkt. Tausi Kida
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (katikati) akisalimiana na mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald Mengi (kulia) alipowasili katika ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Ufaransa nchini, Mh. Malika Berak.

No comments :

Post a Comment