Friday, June 3, 2016

JK AKUTANA NA BALOZI WA ZAMANI WA MAREKANI CHARLES STITH LEO

STI1Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimkaribisha Ofisini kwake,  Balozi wa zamani wa Marekani hapa nchini Tanzania, Balozi Charles Stith, alipomtembelea kwa ajili ya mazungumzo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mjini Dar es Salaam, leo Juni 3, 2016. (Picha na Bashir Nkoromo)
STI2Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimkaribisha Ofisini kwake,  Balozi wa zamani wa Marekani hapa nchini Tanzania, Balozi Charles Stith, alipomtembelea kwa ajili ya mazungumzo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mjini Dar es Salaam, leo Juni 3, 2016. (Picha na Bashir Nkoromo)

NAIBU WAZIRI WA HABARI MGENI RASMI AZANIA BANK KIDS RUN 2016

 Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Tullo Chambo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akimkaribisha Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank ya Azania, Othman Jibrea (katikati), kuzungumza na wanahabari kuhusu mbio hizo zitakazofanyika kesho kutwa. Kulia ni Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday.
 Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank ya Azania, Othman Jibrea (katikati), akizungumzia kuhusu mbio hizo.
 Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday (kulia), akizungumzia kukamilika kwa maandalizi ya mbio hizo.
 Mwanafunzi Rachel Stephen wa Shule ya Sekondari ya Mburahati (kulia) na Mwenzake Ali Muhidin kutoka Shule ya Msingi Muungano wakizungumzia ushiriki wa mbio hizo.
 Wanahabbari wakichukua taarifa hiyo.
Waratibu wa mbio hizo wakionesha fulana zitakazotumiwa na watoto watakao kimbia mbio hizo. Kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Peter Mwita, Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday, Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank ya Azania, Othman Jibrea na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Tullo Chambo.
……………………………………………………………………………………………………………………………….

Dotto Mwaibale NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika  Mbio za Watoto za Azania Kids Run 2016, 
 zitakazofanyika Jumapili Juni 5 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa Azania Kids Run 2016, zinazodhaminiwa na Benki ya Azania, Wilhelm Gidabuday, amesema kuwa Naibu Waziri Wambura atakuwa mgeni rasmi katika kinyang’anyiro hicho kitakachokuwa na mbio za kategori tano.

Gidabuday amebainisha kuwa, maandailizi yote ya Azania Kids Run 2016 yanaenda vema, ikiwamo idadi kubwa ya wazazi na walezi kujitokeza kusajili watoto wao, huku akiwataka wengi kutumia siku mbili zilizobaki kuhakikisha wanawapa vijana wao nafasi ya kushiriki.

“Mbio hizi zinazotarajia kushirikisha zaidi ya watoto 2,000, zinatarajia kufanyika Jumapili Juni 5, 2016 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, zikihusisha watoto chini ya miaka 16, ambako Naibu Waziri Wambura atakuwa mgeni rasmi,” alisema Gidabuday.
Amewasisitiza wazazi, walezi na wadau kujitokeza kusajili watoto wao na kwamba fomu bado zinapatikana katika matawi yote ya Benki ya Azania, Ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) zilizoko Samora Avenue na Ofisi za Shirikisho la Riadha Tanzania (RT).
Gidabuday ametumia nafasi hiyo kuwahakikishia wazazi na walezi wa watoto watakaoshiriki Azania Kids Run 2016 kuwa, usalama wa watoto wao wakati wa shindano utakuwa kipaumbele chao na kuwatoa hofu ya usalama wakati wa kukimbia.
“Barabara zote zitakazotumiwa na watoto kukimbilia zitakuwa na uangalizi maalum ikiwa ni pamoja na gari za huduma ya kwanza na matibabu kwa watakaohitaji kupatiwa huduma hizo,” amesema Gidabuday katika mkutano na wanahabari Dar es Salaam.
Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea, amezitaja zawadi za washindi mbalimbali wa mbio hizo, huku akiweka msisitizo kwa kutawaka wazazi kuendelea kusajili watoto wao kuwa sehemu ya tukio hilo la kihistoria.
“Mshindi wa kwanza mbio za Kilomita 5 ni Sh. 200,000, mshindi wa pili Sh. 150,000 na mshindi wa tatu sh. 100,000, pamoja na medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo, wakati mshindi wa nne hadi wa 10 watapata kifuta jasho cha sh. 15,000,” amesema.
Katika mbio za kilomita 2, Jibrea alitaja zawadi kuwa ni sh. 100,000 kwa mshindi, huku atakayeshika nafasi ya pili akitarajiwa kulamba sh. 75,000 na wa tatu kujitwalia sh. 50,000, kategori ambayo pia washindi wa nne hadi wa 10 watapata kifuta jasho cha sh. 15,000.

Aidha, amebanisha kuwa, kategori ya mbio za kilomita moja mshindi atatwaa sh. 75,000, huku wa pili akibeba sh. 50,000 na wa tatu akijishindia sh. 40,000, ambako pia washindi wa nne hadi wa 10 watapata kifuta jasho kama kilivyotajwa hapo juu.
Pia kutakuwa na mbio za mita 50 na 100, ambazo zitakimbiwa na watoto chini ya miaka mitatu, ambako washindi washindi wote watafunguliwa akaunti katika Benki ya Azania, itakayokuwa na kianzio cha sh.15,000, sanjari na begi la shule lenye vifaa vyote muhimu.

WAZIRI MKUU NA MATUKIO BUNGENI DODOMA

cos1 
Waziri Mkuu. Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi bungeni mjini Dodoma Juni 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
cos2 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama (kulia)  na Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Nape Nnauye wakiteta na Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah Bungeni mjini Dodoma Juni 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
cos4 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Viti Maaluum, Lucy Mayenga kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
cos5 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Viongozi wa CCM kutoka Wilaya ya Ruangwa, Salum Seif Mapatu (kushoto) na Idrisa Said Mtalika kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
cos6 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Jakaya Kikwete kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
cos7 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Mzumbe waliotembelea Bunge kwa Mwaliko wa Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Jakaya Kikwete  (mwenye kanzu katikati) kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Kitime atarajia kuunda chama cha Waandishi wa habari za wanamuziki.

index 
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania John Kitime anatarajia kuunda Chama kwa ajili ya waandishi wa habari wanaoandika habari za wanamuziki ili waweze kupeleka taarifa sahihi za wanamuziki kwa wananchi.
Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Katibu huyo amesema kuwa kuunda chama hicho ni moja ya matarajio yake anayopanga kulifanyia shirikisho hilo.
“Kati ya vitu nilivyovipanga kuvifanya katika shirikisho hili, ninatarajia kuhamasisha uundaji wa chama cha waandishi wanaoandika habari za wanamuziki ili waweze kufanya kazi kwa pamoja ya kupeleka taarifa sahihi za wanamuziki kwa wananchi”, alisema Kitime.
Kitime ameongeza kuwa matarajio yake mengine anayotarajia kuyafanya ni kutoa elimu kwa wanamuziki kuhusu kazi zao kupitia semina mbalimbali pamoja na kuimarisha shirikisho hilo ili wanamuziki waweze kusimama, kukuza muziki pamoja na kunufaishwa na muziki.
Aidha, ameelezea kuwa vyama 8 ambavyo tayari vipo katika shirikisho hilo vitasaidiwa ili kuwa na nguvu ya kuweza kusimama na kuwasaidia wanamuziki inavyostahili kwa kuwa nia na madhumuni ya shirikisho ni kuwa na vyama vingi kwa kadri inavyowezekana.
Kitime ni mwanamuziki aliyeanza kazi zake rasmi mwaka 1965 na ni mmoja wa waasisi wa sheria ya haki miliki ya wanamuziki, mwaka 1993 alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa Dansi pia alishakuwa Mjumbe wa COSOTA, kwa sasa ni mwanamuziki wa bendi ya Kilimanjaro.

Mhe. Amani K. Mwenegoha awataka waandishi wa habari nchini kufanya kazi zao kwa ueledi

index 
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Amani K. Mwenegoha amewataka waandishi wa habari nchini kufanya kazi zao kwa ueledi na kwa ufasaha kwa kuzingatia misingi na maadili ya taaluma za uandishi wa habari wakati wakifanya kazi za uandishi.
Mhe. Amani K. Mwenegoha ameyasema hayo jana akikanusha taarifa zilizoandikwa kwenye gazeti la Mwanahalisi na mwandishi Ansbert Ngurumo toleo na: 341 la Mei 30 mwaka 2016 siku ya Jumatatu ukurasa wa 10 na 11. Alisema katika gazeti hilo lenye kichwa cha Habari kinachosema “Ngono na Mwanafunzi yaleta msukosuko Ushirombo” mimi kama Mkuu wa Wilaya ya Bukombe nimetuhumiwa kutumia madaraka yangu vibaya kwa kumlinda na kumkingia kifua Afisa Tarafa wa Siloka Bw. Tumbo John Madaraka.
Sikuwahi  Kupokea  barua  yeyote kutoka kwa Matayo Paschal wala kuamrisha akamatwe ,pia sikuwahi  kuzungumza  na  mwandishi  yeyote kuhusu mtoto huyo,wala sijapokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Polisi Bukombe kuhusu mtoto huyo wala malalamiko yoyote kutoka kwa wazazi,mlezi au Mwalimu Mkuu wa Shule  aliyosoma mwanafunzi huyo” alisema Mkuu wa Wilaya Mhe. Amani Mwenegoha  akizungumza  na waandishi wa habari ofisini kwake jana.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Bukombe amekemea na kulaani kitendo cha mwandishi wa gazeti la Mwanahalisi kuandika habari bila kuzingatia  maadili ya kiuandishi kwa kufika eneo la tukio na kuonana na walengwa sio kuandika habari za kupelekewa au kusikia mtaani, angezingatia  kupata  taarifa kwa pande zote mbili ili kupata taarifa zenye ukweli,uwazi na uhakika”.
Pia ametoa wito kwa waandishi wa habari nchini kuwa wazalendo na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika  ujenzi wa nchi yetu kwa kufichua uovu utakaorudisha nyuma maendeleo ya jamii yetu  badala ya kuweka vibonzo visivyowakilisha maslahi ya nchi yetu na kuvunja moyo juhudi zinazofanywa na Rais wetu za kuinua Uchumi.
Wakati huo huo, Mkuu wa wilaya ya Bukombe Mhe. Amani K. Mwenegoha amesisitiza wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kutoa taarifa kwa vyombo vya serikali haraka kadri inavyowezekana inapotokea wana tatizo linalohusiana na watoto wao wanapokutana na changamoto ambazo serikali inaweza kushughulikia na imekua ikifanyika hivyo pale ambapo mzazi,mlezi au jamii inapotoa malalamiko au taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ambapo yamekua yakishughulikiwa na sheria imekua ikichukua mkondo wake.

KATIBU MKUU CHAMA CHA KIKOMINISTI BW. LIU ZHIJUN AKAMILISHA ZIARA YAKE ZANZIBAR NA KUELEKEA DAR-ES SAALAM

kom1 
WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais Baraza La Mapinduzi Issa Haji Gavu akizungumza na Mgeni wake Katibu  Mkuu  Chama cha Kikoministi Bw. Liu Zhijun  baada ya kukamilisha  ziara yake Nchini Zanzibar.
kom2VIONGOZI wa Chama cha Mapinduzi CCM wakimsindikiza mgeni wao Katibu  Mkuu  Chama cha Kikoministi Bw. Liu Zhijun wakati alipofika Bandarini Mjini Zanzibar.
kom3MWENYEKITI wa CCM  Wilaya ya Mjini Borafya Silima Juma akiagana na Katibu Mkuu  Chama cha Kikoministi Bw. Liu Zhijun  alipokuwa akiondoka  Bandarini  na kuelekea Dar es Saalamu.
kom4 
MKUU wa Mkoa  wa Mjini Magharib  Ayoub Mohammed akiagana na Katibu Mkuu  Chama cha Kikoministi Bw. Liu Zhijun  alipokuwa akiondoka  Bandarini  na kuelekea Dar es Saalamu.
kom5 
WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais  Baraza La Mapinduzi Issa Haji Gavu akiagana na Katibu Mkuu  Chama cha Kikoministi Bw. Liu Zhijun  alipokuwa akiondoka  Bandarini  na kuelekea Dar es Saalamu.kom6 
KATIBU Mkuu  Chama cha Kikoministi Bw. Liu Zhijun  aliyevaa nguo nyeusi akiingia katika Boti ya AV KILIMANJARO alikielekea Dar es Saalamu baada yakumaliza ziyaza yake Zanzibar.
 PICHA NA MIZA OTHMAN – HABARI MELEZO ZANZIBAR.

Serikali ya Mtakia Ushindi Melisa

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka
Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Leah Kihimbi (kulia) akimkabidhi
Bendera ya Taifa kwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars Tanzania Bi. Melisa
John (kushoto) leo Jijini Dar es Salaam anayetarajia kwenda nchini Nigeria
kushiriki michuano ya shindano hilo kwa nchi za Afrika,wa pili kushoto ni
Meneja Mahusiano Airtel Bw.Jackson Mmbando.
 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Leah Kihimbi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam,wakati wa kumuaga mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania  Bi. Melisa John (kulia) anayetarajia kushiriki
mashindano hayo  nchini Nigeria Juni 11mwaka huu litakaloshirikisha nchi za tisa za Afrika (kushoto) Meneja Mahusiano Airtel Jackson Mmbando . 
 
Meneja Mahusiano Airtel Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari kuhusu dhamira ya Airtel ya kuwawezesha Vijana katika sanaa ya muziki leo Jijini Dar es Salaam,(katikati) Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Leah Kihimbi na (kulia) mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania Bi. Melisa
John.
 
Mshindi wa Shindano la Airtel Trace Music Stars Tanzania Bi. Melisa John (kulia) akiimba moja ya  nyimbo kwa waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam  (hawapo picha)  alipokuwa akiagwa na kukabidhiwa bendera ya Taifa kwa ajili ya kuwakilisha nchi katika mashindano yanayotarajiwa kufanyika nchini Nigeria Juni 11 mwaka huu, (katikati) Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Leah Kihimbi na (kushoto) Meneja Mahusiano Airtel Jackson Mmbando akifurahia wimbo huo.( Picha na Anitha Jonas).
 
Na Lorietha Laurence
Taasisi na Mashirika binafsi nchini zimeombwa kushirikiana na serikali  katika  kutekeleza sera ya Taifa ya Utamaduni ya mwaka 1997 inayosisitiza kukuza na kuendeleza sanaa na wasanii  kwa lengo la  kuinua vipaji na kutimiza ndoto za vijana wengi wanajihusisha na sanaa.
 
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi. Leah Kihimbi wakati wa kukabidhi bendera ya Taifa kwa mshindi wa Airtel Trace Music Star Bi. Melisa John ambaye ataiwakilisha nchi katika mashindano ya Airtel Afrika nchini Nigeria.
 
Bi.Kihimbi ameleeza kuwa fursa inayotolewa na Kampuni ya Airtel ni adhimu na mfano tosha kwa makampuni, taasisi na mashiriki mengine nchini kuunga mkono juhudi hizo kwa kuanzisha program za kuwakwamua vijana kiuchumi kupitia sanaa ya muziki.
 
“Sanaa ya muziki ni kazi kama kazi nyingine,hivyo nashukuru kampuni ya Airtel  kwa kuamua kuunga mkono serikali katika mpango huu wa kuibua vipaji vya vijana  kupitia sanaa ya muziki” alisema Bi.Kihimbi.
 
Aidha aliongeza kuwa nafasi aliyoipata Melisa ni adhimu hivyo haina budi kutumia fursa hiyo vizuri kwa kuikuza talanta yake  ya kuimba na hatimaye kukua kimuziki na kuweza kuitangaza nchini kitaifa na kimataifa.
 
Naye Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando amesema kuwa kampuni yao ipo tayari kuendelea kuwekeza katika sanaa kwa kuwawezesha vijana pamoja na wanamuziki chipukizi kuweza kufikia ndoto zao kupitia Airtel Trace Music Star.
“Tunafurahi kuwawezesha wanamuziki chipukizi vijana kupata nafasi adimu za kufanya kazi na magwiji wa muziki duniani kama Akon na Keri Hilson hivyo tunaomba watanzania watumie fursa
hii kwa kushiriki katika mashindano ya Airtel Trace Music Star ili waweze kukuza vipaji vyao”alisema Bw. Mmbando.
Kwa upande wake mshindi wa Airtel Trace Music Star Bi.Melisa John ameishukuru Serikali na Airtel kwa ushirikiano wao katika kukuza tasnia ya muziki na kuchochea ajira kwa vijana
wengi na kuahidi kurudi na ushindi.
Shindano la Airtel Trace Music Star Kitaifa yalifanyika jijini Dar es Salaam ambapo Bi.Melisa John aliibuka mshindi na kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika mashindano hayo kimataifa yatakayoshirikisha nchi tisa ambazo ni Niger,DRCongo,Gabon,Malawi,Nigeria,Madagascar,Kenya,Zambia na Ghana yanayotarajiwa kufanyika nchini Nigeria Juni 11 mwaka huu. 

KAMPUNI YA SAFARI INDOOR DIGITAL (SID) KUTOA ELIMU KUPITIA MABASI.

index
Kampuni ya Safari Indoor Digital pamoja na kampuni ya mabasi ya Kilimanjaro Express leo hii wamezindua rasmi huduma ya kisasa ya kutoa elimu mbalimbali kwa abiria kupitia TV (Screen) za kwenye mabasi.
Hayo yamesemwa na Meneja operesheni wa kampuni ya Safari Indoor Digital Bi.Doreen Minja alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam.
Bi Doreen amesema kuwa katika programu hiyo kampuni yao ya safari indoor digital watatumia screen za ndani ya mabasi ya kampuni ya Kilimanjaro express na jitihada mbalimbali zinafanyika ili huduma hii kufika katika mabasi yote.
Aidha huduma hiyo itasaidia kumpatia abiria habari mbalimbali anapokuwa safarini kama haki yake ya msingi katika Nyanja za kijamii,kiuchumi na elimu na hasa elimu ya afya,sheria na biashara uku ikimwezesha abiria kutambua mambo mbalimbali ndani ya nchi na nje.
Hata hivyo kampuni ya Safari Indoor Digital watakuwa na kipengele cha matangazo kwa kanda ambacho kitasaidia abiria kuweza kutambua fursa mbalimbali za mkoa uendao na hata kujua viongozi wa mkoa husika na watashirikiana na jeshi la POLISI na SUMATRA na chama cha kutetea abiria Tanzania (CHAKUA) kwa ujumla kutoa elimu katika screen hizo kuhusu haki mbalimbali za abiria,sheria za usalama barabarani  kwa kutengeneza kipindi maalum kitakachoelimisha jamii kuhusu suala hilo.
Nao chama cha kutetea abiria Tanzania (CHAKUA) kimewaasa abiria wote nchini kuitumia fursa hii vizuri kwani itawasogezea huduma za muhimu karibu kwani hata namba za simu za Polisi,Sumatra na Chakua zitapatikana katika screen hizo pindi linapotokea tatizo safarini.

Waziri wa Ujenzi akutana na Katibu Mkuu wa Shiraka la Mawasiliano la Jumuiya ya Madola

mb1Pokea picha ya Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Katibu Mkuu wa Shirakawa La Mawasiliano la Jumuiya ya Madola,   Eng.  Shola Taylor wakati alipokutana naye mjini Daodoma leo.
mb2Katibu Mkuu wa Shirakawa La Mawasiliano la Jumuiya ya Madola,   Eng.  Shola Taylor akitoa ufafanuzi baadhi ya mambo wakati alipokutana na Pokea picha ya Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano mjini Dodoma.
…………………………………………………………………………………………………
Pokea picha ya Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Katibu Mkuu wa Shirika La Mawasiliano la Jumuiya ya Madola,   Eng.  Shola Taylor akiwa na mazungumzo nae ofisini kwake, Dodoma kuhusu kuipatia Tanzania msaada wa  kiufundi wa kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mitandao yaani the National Cybersecurity Strategy na the National Broadband Strategy.
Tanzania imekidhi vigezo vya kupatiwa msaada huo kwa kuwa tayari nchi ina sera,  sheria,  kanuni inayosimamia na kuendeleza Sekta ya TEHAMA nchini. Nyaraka hizo ni pamoja na Sera ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2016,  Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015. Pia uwepo wa miundombinu mbalimbali ya TEHAMA kama vile Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na Kituo Mahiri cha Kutunzia Data.
Wadau mbalimbali zaidi ya 60 wa kutoa Taasisi za Serikali,  Sekta binafsi na mashirika yasiyokuwa ya Serikali wamekutana kwa pamoja na kujadiliana namna ya kuandaa Mkakati wa Taifa wa Usalama kwenye Mtandao. Kikao hicho kimefanyika Dar es Salaam kuanzia tare he 31 Mei, 2016 na kumalizika tarehe 3 Juni,  2016.
  Aidha, Tanzania ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Madola ambapo ni mwanachama hai anaestahili kupatiwa msaada huo kutoka Jumuiya hiyo. Nchi nyingine za Afrika ambapo zinaandaa Mkakati huo ni pamoja na Botswana, Rwanda na Malawi na nchi ambazo tayari zina Mkakati huo ni Uganda.

Mkoa wa Lindi wazindua Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya sekta za umma PS 3

zam1 
Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi Akisoma hotuba ya uzinduzi  wa mradi wa PS3 mkoani Lindi, kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya Umma,Mh.Zambi  alisema kuwa mradi huo utafanyika katika mikoa 13, ambayo itaanza na mradi huo Lindi ikiwa  ni mmoja wapo.
zam2 
Washiriki wa Uzinduzi huo kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Lindi pamoja na washiriki toka katika Halmashauri 6 za Mkoa Huo wakiwa katika Picha ya Pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Lindi(Mwenye suti ya bluu katikati waliokaa)Mara baada ya  Uzinduzi wa Mradi huo Mjini Lindi
zam3 
Bw Conrad Mbuya ,Mkurugenzi wa Shughuli  za Mikoa PS 3  akitoa maelezo Kwa washiriki toka Halmashauri zote za Mkoa wa  Lindi jinsi mradi utakavyo fanya kazi na afua zitakazo zingatiwa katika kutekeleza mradi huo.
zam4Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria Ofisi ya Rais  TAMISEMI,Edwin Mgendera alipokuwa akitoa maelezo kuhusu jukumu la TAMISEMI katika uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Lindi, kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya Umma
zam5 
Washiriki wa Uzinduzi huo kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Lindi pamoja na washiriki  wengine wakiwa katika majadiliano ya Pamoja wakati wa Uzinduzi huo
zam6 
Kutoka Kushoto Ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa,Mariam Mtima,Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea,Pololeti Mgema na Mkuu wa Wilaya ya Liwale Ephraim Mbaga Wakifuatilia kwa Umakini Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi wakati wa Ufunguzi huo.Picha na Habari kwa Hisani ya Abdulaziz Video-Lindi
………………………………………………………………………………………………………..
Katika kuimarisha Ubora wa Utoaji huduma za Umma na Matumizi yake kwa ajili ya Kuboresha na kuimarisha Mifumo,Mkoa wa Lindi Umezindua Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya sekta za umma utakaowezesha Jamii katika Ngazi ya halmashauri kutumia rasilimali kwa Uwazi na kuwezesha ushirikishwaji wa wananchi katika kupanga  na kufuatilia matokeo ya kila sekta
Mpango huo utakaosaidia utoaji wa ushauri wa kitaalamu na kuwajengea uwezo wafanyakazi ili  kuongeza Usawa wa mgawanyo wa rasilimali watub kwa ajili ya utoaji bora wa huduma katika maeneo yenye Uhitaji zaidi ikiwemo mfumo wa ajira pamoja na kudumisha watumishi katika Ajira Serikalini
Akizindua Mradi huo wa PS 3,Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi amesema  kuwa mradi huo wa uhimarishwaji wa mifumo ya sekta za Umma nchini utasaidia kuondoa tatizo sugu la watumishi hewa endapo utekelezaji wake utafanyika vizuri.
Awali akitoa  taarifa katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mradi katika Mikoa, Dk.Conrad Mbuya alisema mradi huo utahakikisha mifumo iliyopo katika ngazi ya Halmashauri inaimarishwa kupitia kitita cha afua zilizoundwa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi wa Tanzania.
Kufuatia Uzinduzi wa Mradi huo,Mkuu wa Wilaya ya Lindi Yahya Nawanda pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa Abuu MjakA walieleza  kuwa mradi huo pia utasaidia ongezeko la pato la ndani kwa ajili ya huduma za umma ikiwemo ushirikishwaji wa Madiwani katika Utekelezaji wa mradi huo Utakaoboresha Utendaji na Uwajibikaji katika kutoa huduma kwa Jamii
Mradi huo uliozinduliwa leo unatekelezwa katika mikoa 13 ya Tanzania Bara ambayo ni Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma,Mara,Mbeya, Morogoro, Mtwara,Mwanza, Njombe, Rukwa na Shinyanga pamoja na Lindi.

No comments :

Post a Comment