Mkurugenzi
Mtendaji wa BancABC Tanzania Bwana. Dana Botha (wa pili kulia),
akibadilishana mawazo na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla
waliyowaandalia wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika
kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara.
Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Wanaomsikiliza kutoka
kushoto ni, John Kazimoto, Jones Mwalemba, naJohn Du Toit.
Mkurugenzi
Mtendaji wa BancABC Tanzania Bwana. Dana Botha ( kulia), akizungumza na
baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla waliyowaandalia wateja wao
kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma
bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika
jijini Dar es Salaam juzi. Wanaomsikiliza kutoka kushoto ni, John
Kazimoto na Jones Mwalemba.
Mkuu
wa Idara ya Uwekezaji wa Kibenki ya Makampuni wa Kundi la BancABC, Dk.
Mabouba Diagne (wa pili kulia), akibadikishana mawazo na baadhi ya
wateja wa benki hiyo katika hafla waliyowaandalia wateja wao
kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma
bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika
jijini Dar es Salaam juzi.
Mkuu
wa Idara ya Uwekezaji wa Kibenki ya Makampuni wa Kundi la BancABC, Dk.
Mabouba Diagne (wa pili kulia), akimsikiliza mmoja wa wateja wa benki
hiyo, John Du Toit katika hafla waliyowaandalia wateja wao kuwajulisha
mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki
chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam
juzi.
Mkuu
wa Idara ya Uwekezaji wa Kibenki ya Makampuni BancABC Tanzania,
Khalifa Zidadu (kulia), akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo
katika hafla waliyowaandalia wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki
hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la
atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kushoto ni
Ofisa Fedha Mkuu wa Superdoll, Sateesh Babu Desu na Prasanthar Govinder
pia wa Superdoll.
Mkurugenzi
Mtendaji wa BancABC Tanzania Bwana. Dana Botha ( kulia), akizungumza na
baadhi ya wateja wa benki hiyo (hawapo pichani) katika hafla
waliyowaandalia wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika
kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara.
Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Wanaomsikiliza kutoka
kushoto ni, John Kazimoto na Jones Mwalemba.
Mkuu
wa Idara ya Uwekezaji wa Kibenki ya Makampuni wa Kundi la BancABC, Dk.
Mabouba Diagne (wa pili kulia), akifafanua jambo mbele ya baadhi ya
wateja wa benki hiyo (hawapo pichani), katika hafla waliyowaandalia
wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa
huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo
ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Bank
ABC imeanzisha huduma mpya kwa wafanyabishara wakubwa kuhamisha and
kuingiza mitaji yao ndani na nje ya nchi kwa kutumia teknolojia ya
kisasa ya elektroniki.Akizungumza katika hafla iliyofanyika Jumatano
hii, Mkuu wa kundi la Benki hiyo katika ukanda wa Afrika, Dk. Mabouba
Diagne alisema wametenga Dola za Kimarekani milioni 20 (zaidi ya Sh
billion 40) kwa ajili ya mpango huo unaolenga kuimarisha biashara
miungoni mwa nchi za Afrika.
“Tumeanzisha
huduma hii mpya kwa ajili ya kurahisisha na kukuza biashara miungoni
mwa wafanyabishara wakubwa barani Afrika. Tunataka wafanyabiashara
waweze kufungua milango yenye fursa nyingi za kibishara barani Afrika,”
Dk. Diagne alisema.Alisema Banc ABC imezimia kuwawezesha Watanzania
kutumia teknolojia mpya ya kuhamisha mitaji na fedha nyingi si ndani ya
nchi tu bali nje ambako kuna fursa nyingi za biashara zisizotumika.
“Mara
nyingi wafanyabishara wengi wa hapa nchini wanaofanyabishara nan chi
jirani wamekuwa wakilalamika kukosekana kwa huduma bora za kuhamisha
fedha kwa wingi. Sasa jawabu limepatikana kwa Banc ABC kuanzisha huduma
za kisasa za kuhamisha mitaji,” alisema.
Alisema
watu wanaweza kuhamisha mitaji hata fedha nyingi nchi za nje kwa
kutumia simu za mkononi bila kuathiri biashara.“Tumeanzisha huduma hii
kwa sababu biashara baina ya nchi za Afrika ni jambo muhimu la kuwezesha
nchi na wafanyabishara waweze kutumia fursa nyingi zilizomo barani
Afrika kutokana na bara hili kuwa na rasilimali nyingi asilia,” alisema
kiongozi huyo msomi mwenye shahada ya juu ya uzamili ya hisabati.
Alisema
suala la kubadilishana na kuhamisha mitaji ni biashara kubwa duniani
kwa sababu mitaji ni bidhaa muhimu kwa maendeleo ya nchi na watu.Mapema
mkurugenzi wa Banc ABC Tanzania, Bw Dana Botha alisema tayari benki hiyo
imeanzisha mtandao wa matawi 100 hapa nchini na kuwa miungoni mwa benki
imara.Naye Mtendaji Mkuu wa kundi la benki hiyo Dk. Blessings Mudavanhu
alisema kuwa benki hiyo ambayo imesajiliwa katika soko la fedha la
London, ilizindua aina ya bidhaa yake mpya na kujitanua kimataifa baada
ya kuungana na Atlas Mara.
“Tutatumia
jamvia la teknolojia ya habari na mawasiliano. Tunataka watu waanchane
na kuandika cheki nyingi na kutumia gharama kubwa za miamala ya katatazi
badala yake watumie simu za mkononi,” alisema Dk Madavanhu.Alisema
benki hiyo ambayo inaendesha biashara katika nchi za Tanzania, Nigeria,
Afrika kusini, Botswana Zimbabwe, Rwanda, Burundi na Zambia imedhamiria
kuwa benk kubwa inayokuza biashara miungoni mwa nchi za Afrika.
Katika
hafla hiyo kampuni kadhaa kubwa zilishiriki na kuvutiwa na huduma hiyo
mpya itakayotolewa na benki hiyo ya kimataifa. Kampuni hizo ni; Statoil,
Mount Meru (T) Ltd, Lake Oil. Superdoll na Puma Energy.
Kaimu
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA), Bw. Paul Rwegasha akimuonyesha uchafu zaidi Meneja Rasilimali
Watu Mafunzo, Bw. Abdul Mkwizu (kushoto), wakati wakifanya usafi eneo la
Kigilagila Relini, ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya Siku ya Mazingira
Duniani, Juni 5, 2016
Mkuu
wa Kitengo cha Mazingira cha Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA) Bw. Jofta Tuimanywa (aliyenyoosha mkono), akisisitiza jambo kwa
wafanyakazi wenzake, wakati wakifanya usafi kwa kushirikiana na wakazi
wa mitaa ya Kigilagila Relini na Vituka kwenye eneo la nyuma ya uzio wa
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA). Juni 5, 2016
ni Siku ya Mazingira Dunia.
Wakazi
wa Mitaa ya Kigilagila Relini na Vituka wakiwa pembeni ya kibao
kinachokataza utupaji wa taka, katika eneo la nyuma ya Kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), mara baada ya kumaliza kufanya
usafi. Juni 5 ni Siku ya Mazingira Duniani.
Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), Bw. Laurent Mwigune (mwenye suti) jana akishiriki zoezi la
kufanya usafi maeneo mtaa wa Kigilagila Relini, ikiwa ni muendelezo wa
zoezi la usafi kuelekea Siku ya Mazingira Duniani, Juni 5, 20916.
Kaimu
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA), Bw. Paul Rwegasha (mbele anayetzama kamera), akizungumza na
wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), na Wakazi wa
Mitaa ya Kigilagila Relini na Vituka, mara baada ya kumaliza kufanya
usafi nyuma ya ukuta wa JNIA, ikiwa ni muendelezo wa kuelekea
maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, Juni 5, 2016.
Wafanyakazi
wa TAA kuanzia kushoto Mwanaisha Athuman, Asha Lusehere na Magareth
Mushi , wakishirikiana na wakazi wa Mtaa wa Kigilagila Relini kufanya
usafi wa mazingira nyuma ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere. Juni 5 ni kilele cha Siku ya Mazingira Duniani.
JK AOMBELEZA MSIBA WA RAIS WA SAHARA MAGAHARIBI
Mwenyekiti
wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akisaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya Ubalozi wa nchi ya Sahara
Magharibi nchini,kufuatia kifo cha Rais Abdel Aziz Mohamed kilichotokea
siku ya tarehe 31,Mei 2016, kulia ni Mama Salma Kikwete.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya Ubalozi wa nchi
ya Sahara Magharibi nchini,kufuatia kifo cha Rais Abdel Aziz Mohamed kilichotokea siku ya tarehe 31,Mei 2016, kulia ni Mama Salma Kikwete.
Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya Ubalozi wa nchi
ya Sahara Magharibi nchini,kufuatia kifo cha Rais Abdel Aziz Mohamed kilichotokea siku ya tarehe 31,Mei 2016, kulia ni Mama Salma Kikwete.
Mke wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mama Salma
Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya Ubalozi wa nchi
ya Sahara Magharibi nchini,kufuatia kifo cha Rais Abdel Aziz Mohamed kilichotokea siku ya tarehe 31,Mei 2016, kulia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikete.
ya Sahara Magharibi nchini,kufuatia kifo cha Rais Abdel Aziz Mohamed kilichotokea siku ya tarehe 31,Mei 2016, kulia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikete.
Mwenyekiti
wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akizungumza na Balozi wa nchi ya Sahara Magharibi Brahim Salem Buseif
mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais Abdel
Aziz Mohamed.
VIDEO-ACT WAZALENDO WATANGAZA SIKU RASMI YA MAPOKEZI YA KIONGOZI WAO ZITTO NA WALE WA UKAWA
Katibu
wa Itikadi mawasiliano na uenezi wa chama cha ACT WAZALENDO Ndugu ADO
SHAIBU akizngumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mapokezi
ya kumpokea kiongozi yao na mbunge pekee wa chama hicho ZITTO KABWE
ambaye naye amekumbwa na timua timua ya bungeni,mapokezi ambayo
yatafanyika Jijini Dar es salaam siku ya Jumapili
…………………………………………………………………………………
Na EXAUD MTEI
Katibu wa Itikadi mawasiliano na
uenezi wa chama cha ACT WAZALENDO Ndugu ADO SHAIBU akizngumza na
wanahabari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mapokezi ya kumpokea kiongozi
yao na mbunge pekee wa chama hicho ZITTO KABWE ambaye naye amekumbwa na
timua timua ya bungeni,mapokezi ambayo yatafanyika Jijini Dar es salaam
siku ya Jumapili
Na EXAUD MTEI
Story ambayo bado ipo maskioni
mwa watanzania walio wengi ni mwenendo wa bunge la Jamhuri ya muungano
wa Tanzania na mizengwe yake ambayo imesababisha wabunge saba wa vyama
vya upinzani kusimamiswa kushiriki shughuli za bunge kwa vipindi Tofauti
tofauti akiwemo mbunge kutoka ndani ya chama cha Act wazalendo Mh ZITTO
ZUBERI KABWE na wabunge wa vyama vya UKAWA.
Sakata hilo limeendelea kuchukua
Headline katika maeneo mbalimbali ambapo asubuhi hii chama cha ACT
wazalendo kupitia kwa kiongozi wao ADO SHAIBU wamejitokeza mbele ya
wanahabari kueleza msimamo wa chama chao kuhusu sakata hilo.
Akizungumza na wanahabari leo
Katibu huyo wa itikadi mawasiliano na uenezi wa ACT ADO SHAIBU ameeleza
kuwa chama hicho kimeandaa mapokezi ya kiongozi wao ambaye amekumbwa na
adhabu hiyo mapokezi ambayo yanataraji kufanyika Jijini Dar es salaam na
baadae kufwatiwa na mkutano mkubwa wa hadhara ambao umepangwa kufanyika
katika viwanja vya ZAKIEM mbagala lengo likiwa ni kuwapa nafasi wabunge
hao kueleza ukweli wa yale yanayoendelea bungeni Dodoma.
Pamoja na mandalizi hayo chama
hicho kimewaandikia barua makatibu wa vyama vya upinzani ambao nao
wanapinga adhabu hiyo kutoka CHADEMA,CUF,na NCCR-MAGEUZI kuwaomba
kuungana nao katika mapokezi hayo ambayo yamepewa jina la OPERATION
LINDA DEMOCRASIA na bado hawajapata majibu yao lakini wanaamini
wataungana nao katika Operation iyo ambayo itafwatiwa na mikoa mingine
takribani minne.
Wazanzibari wahimizwa kupanda miti
MJUMBE
mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Ali Mzee (katikati), akipanda mti
katika zoezi la upandaji miti lililofanyika uwanja wa michezo Malindi
mjini Zanzibar jana, kwa lengo la kuhuisha mandhari ya eneo hilo ambalo
limeanza kuathiriwa na athari za kimazingira. Kushoto ni Mwenyekiti wa
jumuiya ya Green World Family Foundation iliyodhamini zoezi hilo Nazir
Ahmad Bachoo iliyodhamini shughuli hiyo. (Picha na Haroub Hussein).
………………………………………………………………………………………………….
Na Salum Vuai, MAELEZO
JAMII nchini imehimizwa kujenga
utamaduni wa kupanda miti ili kuirejeshea Zanzibar uoto wa asili na
kuiepusha na janga la kimazingira.
Akizindua zoezi la upandaji miti
lililofanyika pembezoni mwa uwanja wa soka wa klabu ya Malindi mjini
Zanzibar, mjumbe mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Ali Mzee, amesema miti
ni uhai kwa kila binadamu.
Mzee alisema ni jambo la
kusikitisha kwamba mazingira ya Zanzibar yamegeuka kutoka rangi ya
kijani iliyokuwepo zamani na kuwa yabisi, hali inayosababisha kuongezeka
kwa joto.
“Bila miti, viumbe hutaabika na
nchi inakuwa kavu na maradhi hasa presha huongezeka kila uchao. Lazima
tuzinduke kwani tusipopanda miti, tunakaribisha janga kwa taifa,”
alisema Mzee.
Aidha alivitaka vyombo vya habari
kuandaa vipindi na makala mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu kwa
wananchi juu ya umuhimu wa kupanda miti.
Mapema, Mwenyekiti wa jumuiya ya
Green World Family Foundation iliyodhamini zoezi hilo Nazir Ahmad
Bachoo, alisema jumuiya yake inathamini mazingira na imeamua kulifanya
zoezi la upandaji miti kuwa endelevu.
Alisema ni jambo lililo wazi
kwamba dunia nzima sasa inalia na hali ya joto litokanalo na ongezeko la
hewa ukaa (carbon dioxide), inayosababishwa na upungufu wa miti na
kuongezeka kwa vyombo vya usafiri barabarani vinavyozalisha moshi kwa
wingi.
“Umefika wakati sasa kila mmoja
ahamasike kupanda na kuitunza miti katika eneo analoishi na yale
yanayomzunguka, ili ilete manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho,”
alisisitiza.
Kwa upande wake, mratibu wa zoezi
hilo na mwanaharakati wa mazingira Mohammed Abdulrahman Bajbeir,
alisema Zanzibar imejaaliwa kuwa na wataalamu wengi wa masuala ya
mazingira, lakini bado hawajatumika kikamilifu kuisaidia nchi.
Kwa hivyo amezishauri mamlaka za
juu kutanabahi na janga la kimazingira linaloinyemelea Zanzibar kutokana
na utashi wa binadamu ambao wamekuwa wakikata miti ovyo bila kupanda
mingine.
“Zanzibar ya sasa sio kama ile ya
zamani ambayo ilijaa kila aina ya miti pembezoni mwa barabara na
mitaani. Tunafyeka miti kujenga nyumba za makaazi na maduka tukisahau
kwamba miti ni muhimu kwa uhai wetu. Tubadilike,” alieleza Bajbeir.
Wananchi mbalimbali wa mitaa ya
Malindi, Mchangani na Mbuyuni wakiwemo wanasoka wa zamani wa klabu ya
Malindi SC walioshiriki zoezi hilo, walieleza umuhimu wa kuilinda miti
hiyo ili kuunusuru uwanja wa michezo, kwani umekuwa ukiharibiwa sana na
watu wanaoweka magari pamoja na mifugo.
Jumla ya miti 41 ya aina
mbalimbali ilipandwa kuzunguka uwanja huo, na itakuwa ikilindwa na
wananchi kwa kushirikiana na vijana wa ulinzi shirikishi na polisi jamii
wa shehia ya Malindi.
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZUNGUMZA NA WATANZANIA WANAOISHI NCHINI PAPOA NEW GUINEA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza na Wazee na Watanzania wanaoishi Nchini Papur New Guinea
katika ukumbi wa Airways Hotel mjini Guinea Baada ya kukamilisha ziara
yake ya kikazi ya kumwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano wa
nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific uliojadili
masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa
Nchi wanachama kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na
Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa uliomalizika Jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza na Wazee na Watanzania wanaoishi Nchini Papur New Guinea
katika ukumbi wa Airways Hotel mjini Guinea Baada ya kukamilisha ziara
yake ya kikazi ya kumwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano wa
nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific uliojadili
masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa
Nchi wanachama kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na
Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa uliomalizika Jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akipokea zawadi ya Picha yenye Nembo inayotumika Nchini Papua New Guinea
kutoka kwa Wazee na Watanzania wanaoishi Nchini Papur New Guinea baada
ya kuzungumza nao katika ukumbi wa Airways Hotel mjini Guinea
alipokamilisha ziara yake ya kikazi ya kumwakilisha Rais Dkt. John
Magufuli katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na
Pacific uliojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa
ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP
katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa
uliomalizika Jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania wanaoishi Nchini Papur New
Guinea baada ya kuzungumza nao katika ukumbi wa Airways Hotel mjini
Guinea alipokamilisha ziara yake ya kikazi ya kumwakilisha Rais Dkt.
John Magufuli katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika,
Caribean na Pacific uliojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo
endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama kuimarisha majukumu ya
Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa
kisiasa uliomalizika Jana. (Picha na OMR)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania wanaoishi Nchini Papur New
Guinea baada ya kuzungumza nao katika ukumbi wa Airways Hotel mjini
Guinea alipokamilisha ziara yake ya kikazi ya kumwakilisha Rais Dkt.
John Magufuli katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika,
Caribean na Pacific uliojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo
endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama kuimarisha majukumu ya
Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa
kisiasa uliomalizika Jana. (Picha na OMR)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza na Wazee na Watanzania wanaoishi Nchini Papur New Guinea
katika ukumbi wa Airways Hotel mjini Guinea Baada ya kukamilisha ziara
yake ya kikazi ya kumwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano wa
nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na Pacific uliojadili
masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa
Nchi wanachama kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na
Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa uliomalizika Jana.
SERIKALI YATOA UFAFANUZI KUHUSU TUHUMA ZILIZOTOLEWA NA MWANDISHI WA ” THE ECONOMIST” GAZETI LA KIINGEREZA.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Zamarad Kawawa (kushoto),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam mchana
huu wakati akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma zilizotolewa na mwandishi wa ”
The Ecomist” Gazeti la Kiingereza linatoka kwa wiki dhidi ya Serikali
ya Tanzania. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania
(TCI), Daud Biganda.
Meneja
Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TCI), Daud Biganda (kulia),
akitoa ufafanuzi wa Uchumi tangu Rais Dk. John Magufuli aingie madaraka
na miradi iliyosajiliwa na kituo hicho.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Taarifa akichukuliwa na wanahabari.
……………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI
imekanusha habari zilizoandikwa na gazeti la Kiingereza linalotpka kila
wiki lililodai kuwa Rais Dk.John Magufuli anaongoza nchi kwa msukumo
licha ya kuonekana mzuri na kuwa taarifa hiyo imelenga kuupotosha umma.
Habari
iliyoandikwa kwenye gazeti hilo ilikuwa na kichwa kilicho andikwa
“Government by gesture, A President who looks good but governs
impulsively”
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akitoa ufafanuzi
wa habari hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Zamarad
Kawawa alisema taarifa hiyo haikuwa na uzalendo na amewataka wanahabari
kuwa makini na habari zenye mlengo wa kupotosha taifa.
“Nawaombeni wanahabari wenzangu kuweni makini na taarifa zenye mlengo wa kupotosha umma” alisema Zamarad.
Akitoa
ufafanuzi kuhusu suala la uchumi Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji
Tanzania (TIC), Daud Biganda alisema taarifa hiyo siyo sahihi na
imelenga kupotosha na inavuruga ukweli kwani Tangu Rais Dk.John Magufuli
aingie madarakani kwa kipindi cha kati ya mwezi Desemba 2015 na 2016,
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeweza kuandikisha miradi ya
uwekezaji ipatayo 551 yenye thamani ya dola za kimarekani milioni
9,211.88 kati ya miradi hiyo miradi 229 yenye asilimia 42 inamilikiwa na
watanzania, miradi 215 yenye asilimia 39 inamilikiwa na wageni na
miradi 107 yenye asilimia 19 inamilikiwa kwa njia ya ubia kati ya
watanzania na wageni.
Biganda
alisema kuwa miradi yote hiyo ya uwekezaji ilitarajiwa kuzalisha ajira
zipatazo 55,970 na kuleta matokeo mengine kwa watanzania na kuwa
imesajiliwa na TIC.
Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mitanda kuandaliwa
Katibu
Mkuu wa Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya madola Dkt. Shola Taylor
kushoto akisalimiana na Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano mhandisi Peter Philip uwanja wa ndege wa Mwalimu
Julius Nyerere wakati akimpokea kwa ajili ya uandaaji wa Mkakati wa
Kitaifa wa Usalama kwenye Mitandao
Katibu
Mkuu wa Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya madola Dkt. Shola Taylor
(wa nne kutoka kushoto) waliopo mbele akiwa katika picha ya pamoja na
wadau na wataalam wa Sekta ya Mawasiliano wanaoandaa Mkakati wa Kitaifa
wa Usalama kwenye Mtandao nchini.
Mkurugenzi
wa Utawala na rasilimali watu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Bibi Kitolina L. Kippa. akimkaribisha Katibu Mkuu wa Shirika
la Mawasiliano la Jumuiya ya madola Dkt. Shola Taylor kuzungumza na
wadau na wataalamu wanaoandaa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye
Mtandao nchini (hawapo pichani).
Katibu
Mkuu wa Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya madola Dkt. Shola Taylor
akizungumza na wadau na wataalamu wanaoandaa Mkakati wa Kitaifa wa
Usalama kwenye Mtandao (hawapo pichani) mbele ya vyombo vya habari
Wadau
na wataalamu wanaoandaa Mkakati wa Kitaifa wa Usalama kwenye Mtandao
wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Shirika la Mawasiliano la Jumuiya ya madola
Dkt. Shola Taylor (hayupo pichani)
MWANZA YAZINDUA KAMPENI YA KUZUIA UHALIFU
Viongoziwa
dini wakiwa katika kikao, kilicho wahusisha waandishi wa Habari wa mkoa
wa Mwanza, wakati wa Uzinduzi wa kampeni ya kuzuia uhalifu mkoa wa
Mwanza yenye lengo la kupiga vita uhalifu wa aina yoyote katika mkoa wa
Mwanza ambayo inahusisha wadau mbalimbali pamoja na wananchi katika mkoa
huo.
Baadhi
ya Washiriki wa Uzinduzi wa Kampeni yakupambana na Uhalifu chini ya
Chama cha kupambana na Uhalifu na dawa za kulevya nchini OJADACT,
Mwenyekiti
wa OJADACT. BW. Edwin Soko akitoa maelezo ya awali wakati wa uzinduzi
wa kampeni ya kuzuia uhalifu, iliyo zinduliwa na chama hicho
kwakushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, SACP. Ahmed Msangi, akifungua Uzinduzi huo
ulioandaliwa baina ya OJADACT na wadau wa Ulizi na Usalama, uliofanyika
katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Picha zote na Atley Kuni- Msemaji wa OJADACT. Tanzania
Wachuuzi wa samaki Wete bandarini wagoma kurejea ndani ya soko
Na Masanja Mabula –Pemba
WACHUUZI wa samaki katika
soko la Bandarini Wete , wamegoma kurejea ndani ya soko hilo wakiutaka
uongozi wa Baraza la Mji Wete kuhakikisha unarejesha huduma muhimu ndani
ya soko hilo ikiwemo maji pamoja na vyoo.
Wamesema kwamba uwamuzi wa
kutoka na kuanza kuuza samaki nje ya soko ni kutokana na kuharibika kwa
miundo mbinu ya maji ndani ya soko , jambo ambalo linahatarisha usalama
wa maisha yao na wateja wanaokwenda kupata mahitaji ya kila siku .
Wakizungumza na kamati ya
kusimami mwendendo wa wachuuzi wa samaki iliyoundwa na Mkuu wa Wilaya
ya Wete , walisema hawako tayari kurejea ndani ya soko hilo , hadi
uongozi wa Baraza la Mji utakapojipanga kurejesha huduma muhimu za
kijamii .
Mwenyekiti wa Kamati ya wavuvi
ambaye pia ni dalali wa samaki sokoni hapo Mohamed Kombo alisema endapo
huduma hizo zitarejeshwa ndani ya soko hilo , wachuuzi wote watarejea
na kuuza samaki wao kwani watakuwa na usalama wa maisha yao .
“Uongozi wa Baraza unmekusudia
kutudhalilisha , hili sio soko , maji hakuna na vyoo hakuna isiotoshe
lipo chini yam nada unafikiri nani atakayekuja kununua sakami kwa
mchuuzi wakati mnada uko hapa hapa ? ”alihaoji .
Naye Hossein Sharif Mchuuzi wa
samaki na dalali , alisema uwamuzi wa kuhama kuuza samaki ndani ya soko
ni kuwapunguzia kazi wanafanyakazi wanaosafisha ndani ya soko , kwani
wanapata usumbufu kufuata huduma kwa kichwa kwa ajili ya kusafisha baada
aya saa za kazi .
Alisema awali Uongozi wa Baraza
ulifanikisha kuunganisha huduma ya maji kwa muda , lakini huduma hiyo
ilidumu kwa muda wa wiki mbili na kukatwa , kuacha soko likiwa katika
hali tete hasa kipindi hichi cha magonjwa ya mripuko .
Kwa upande wake Khatib Said
Kombo aliiambia kamati hiyo kwamba vyoo vipo mbali na soko na haviko
katika hali nzuri , hivyo ni vyema kuangaliwa upya na kufanyiwa
marekebisho ili viweze kutumika .
Akijibu malalamiko hayo
Mkurugenzi wa Baraza la Mji Wete , Mgeni Othman Juma alisema baadhi ya
sababu zilizotolewa na wachuuzi hao sio za msingi na kwamba ambazo ni za
msingi aliahidi kuzipatia ufumbuzi wa haraka .
“Tayari uongozi wa Baraza
umelipa fedha kwa mamlaka ya Maji (ZAWA) Wilaya ya Wete kwa ajili ya
kurejesha huduma hiyo ndani ya soko , na huduma hii itarejea ndani ya
kipindi cha wiki moja , lakini wakati tunasubiri hilo kufanikishwa
tunawaomba wachuuzi warejea ndani ya soko ”alisisitiza.
Hata hivyo uchunguzi uliofanywa
na mwandishi wa habari hizi umebaini kwamba Mamlaka ya Maji Zanzibar
(ZAWA) Wilaya hiyo ilifikia uwamuzi wa kuikata huduma ya maji katika
soko hilo kwa kuwa yalikuwa hayatumiki na yalisababisha miundo mbinu
kupasuka baada ya kuzidiwa na presha yake
NANI MKALI DAR LIVE JUMAMOSI HII
Jumamosi hii ya Juni 4 mbona ‘Kitanuka’ Dar Live! Ni usiku wa nani mkali kutoka kwa mastaa wa taarab, bongo fleva na singeli.
Ni onyesho kubwa la na mwisho
kabla kuelekea mapumziko ya mwezi mtufu wa Ramadhan ambapo Isha Mashauzi
akiwa na kundi zima la Mashauzi Classic atapanda jukwani na Snura, Roma
Mkatoliki, Sholo Mwambana Man Fongo.
Msemaji wa ukumbi wa Dar
Live,Juma Mbizo amesema onyesho hilo la kipekee limezingatia muziki wa
kila nyanja ili kuleta ladha isiyochuja mwanzo hadi mwisho wa onesho
hilo.
Mbizo amesema kupitia onyesho
hilo mashabiki watajionea wenyewe ni muziki upi wenye nguvu zaidi kati
ya taarab, bongo fleva, singeli na hata rumba kutokana na ukweli kuwa
Isha Mashauzi mbali na taarab lakini pia ana ngoma zake kali za muziki
wa rumba.
Naye Isha Mashauzi amesema
atalitendea haki onyesho hilo hasa kutokana na ukweli kuwa hajapanda
jukwaa la Dar Live kwa takriban miaka miwili na hivyo hiyo ni nafasi
pekee ya kukata kiu ya mashabiki wake ya watakaofika kwenye ukumbi huo
mkubwa zaidi wa burudani ulioko maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam.
KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AKAGUA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA ASKARI, NA KITUO CHA POLISI KUNDUCHI, OYSTERBAY POLISI NA MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest
Rwegasira (wa tatu kutoka kushoto) akielekea kukagua miradi ya ujenzi wa
nyumba za polisi zilizopo katika eneo la Kunduchi jijini Dar es Salaam
jana, wanne kutoka kushoto ni Bw. Bernard Chagula ambaye ndiye Msimamizi
Mkuu wa Mradi huo anayesimamia kwa niaba ya Jeshi la Polisi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Jenerali Projest Rwegasira
(wa kwanza kutoka kulia) akionyeshwa mchoro wa ramani ya jengo mojawapo
linaloendelea kujengwa huko Kunduchi jiji Dar es salaam kwa ajili ya
nyumba za kuishi askari wa jeshi la polisi,(wa pili kutoka kulia) ni
Bw. Bernard Chagula ambaye ndiye Msimamizi Mkuu wa Mradi huo
anayesimamia kwa niaba ya Jeshi la Polisi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Jenerali Projest Rwegasira
aliyenyosha mkono akitoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi juu ya miradi
hiyo inayoendelea kujengwa, wanaomsikiliza ni baadhi ya viongozi wa
Jeshi la Polisi na wakandarasi wanaotekeleza mradi huo eneo la Kunduchi
jijini Dar es Salaam.
Bw.
Bernard Chagula (wa nne kutoka kushoto) ambaye ndiye Msimamizi Mkuu wa
Miradi ya ujenzi wa nyumba za polisi anayesimamia kwa niaba ya Jeshi la
Polisi, akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Jenerali Projest Rwegasira(wa pili kutoka kulia) baadhi ya
majengo(hayapo pichani) yanayoendelea kujengwa katika eneo la Polisi
Oysterbay jiji Dar es salaam ambapo Katibu Mkuu huyo alifanya ukaguzi
kujionea maendeleo yaliyofikiwa tangu kuanza kwa mradi huo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Jenerali Projest Rwegasira
(watatu kutoka kushoto) akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa Jeshi la
Polisi na wakandarasi wanaotekeleza mradi huo eneo la Mikocheni jijini
Dar es Salaam, nyuma yao ni baadhi ya majengo yaliyokwisha kujengwa.
WADAU WA WATAKIWA KUTOA MCHANGO WA KUBORESHA KANUNI ZA UPATIKANAJI WA MBOLEA NCHINI.
Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Florence Turuka akifungua
warsha ya wadau wa mbolea iliyofanyika leo jiji Dar es Salaam kujadili
na kuboresha sheria na kanuni zinazosimia sekta ya mbolea nchini ili
kuwa na kilimo chenye tija kwa Watanzania na taifa kwa ujumla.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Udhibiti wa Ubora wa Mbolea Tanzania
(TFRA) Lazaro Kitandu akibainisha baadhi ya changamoto zinzoikabili
sekta ya mbolea nchini ikiwemo bei ya mbolea kulingana na uwezo wa
wakulima wengi na muda mrefu wa majaribio kwa mbolea inaingia nchini.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika linalojishughulisha na matumizi ya mbolea Bara la
Afrika anayesimamia eneo la Tanzania Dkt. Mshindo Msolla akitoa neno la
shukrani baada ya ufunguzi wa warsha ya wadau wa mbolea kujadili na
kuboresha sheria na kanuni zinazosimia sekta ya mbolea nchini ili kuwa
na kilimo chenye tija kwa Watanzania na taifa kwa ujumla. Wa kwanza
kushoto Mgeni rasmi ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo
na Uvuvi Dkt. Florence Turuka.
Mtaalamu
wa Udongo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Dkt.
Consolatha Mhaiki akichangia mada juu ya matumizi ya mbolea ni
yanavyopaswa kuendana na aina ya udogo kwa uzalishaji bora wa mazao
wakati wa warsha ya wadau wa mbolea iliyofanyika leo jiji Dar es Salaam
kujadili na kuboresha sheria na kanuni zinazosimia sekta ya mbolea
nchini ili kuwa na kilimo chenye tija kwa Watanzania na taifa kwa
ujumla.
Baadhi
ya wajumbe wakifuatilia mada wakati wa warsha ya wadau wa mbolea
iliyofanyika leo jiji Dar es Salaam kujadili na kuboresha sheria na
kanuni zinazosimia sekta ya mbolea nchini ili kuwa na kilimo chenye tija
kwa Watanzania na taifa kwa ujumla.
Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Florence Turuka (katikati
aliyekaa )akiwa picha ya pamoja na wadau wa mbolea mara baada ya
kufungua warsha ya wadau ha oleo jijini Dar es salaam.
(Picha na Eleuteri Mangi MAELEZO)
……………………………………………………………………………………………………….
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Wadau
wa mbolea wameaswa kuangalia namna ya kuboresha sheria na kanuni za
kusimamia sekta ya mbolea kwa manufaa ya wananchi wanaojishughulisha na
kilimo ili kiwe na tija kwa Watanzania na taifa kwa ujumla.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Dkt. Florence Turuka alipokuwa akifungua mkutano wa wadau wa mbolea
uliofanyika leo jiji Dar es Slaam.
Dkt.
Turuka amesema kuwa maeneo ya kuzingatiwa katika warsha hiyo ni pamoja
na kuboresha sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya mbolea ili
kuwezesha sekta binafsi kushiriki katika kuinua kilimo kwa manufaa ya
Watanzania.
Gharama
hizo zinahusisha kufanyiwa majaribio mbolea zinazotoka nje ya nchi
kabla ya kuanza kutumiwa na wakulima ambapo majaribio hayo yanafanyika
kwa misimu mitatu ya kilimo.
Maeneo mengine ya kurekebisha ni pamoja na mlolongo wa tozo ambazo zimekuwa zikitozwa kwenye mbolea inayoingizwa nchini.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika linalojishughulisha na matumizi
ya mbolea Bara la Afrika anayesimamia eneo la Tanzania Dkt. Mshindo
Msolla amesema kuwa kazi kubwa waliyonayo wajumbe katika warsha hiyo ni
kuhakikisha sheria na kanuni wanazozifanyia kazi zitasaidia kuboresha
upatikanaji wa mbolea zenye ubora unaotakiwa kulingana na mahitaji ya
wakulima na waipate kwa wakati.
“Wakulima
hapa nchini wananufaika na huduma zetu ambazo tunatoa ikiwemo
kuwaunganisha na mawakala wakubwa wa pembejeo na makampuni yanayozalisha
au kuingiza mbolea nchini” alisema Dkt. Msolla.
Kuhusu
hali ya upatikanaji wa mbolea nchini, Dkt. Msolla amesema kuwa shirika
hilo linatoa huduma katika mikoa 12 nchini ambapo wapo mawakala 30
wanahudumia mawakala wadogo 500.
Mikoa hiyo ni Arusha,Kilimanjaro,Manyara, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Ruvuma, Rukwa, Katavi na Kigoma.
Mawakala
hao msimu wa mwaka 2014/2015 wamefanikiwa kuuza kwa wakulima mbolea
tani 60,000 na mbegu tani 3000 ambazo zimekuwa na manufaa katika
kuhakikisha upatikanaji wa mazao ya chakula na biashara nchini.
Aidha,
shirika hilo limefanikiwa kuwaunganisha wakulima na makampuni ya mbolea
sita ikiwemo YARA, Extra Trading, Premium Agrochemical pamoja na
Minjingu.
Vile
vile, Dkt. Msolla amesema kuwa wakulima wamenufaika na kujengewa maghala
14 hadi sasa yameanza kutumika ambayo yanauwezo wa kuhifadhi tani
50,000 kwa wakati moja hatua ambayo inasaidia kusogeza huduma karibu na
wakulima wanapozihitaji.
Dkt.
Msolla amesema kuwa Shirika hilo lenye makao yake makuu Afrika Kusini
linatoa huduma kwa sekta ya mbolea katika nchi mbalimbali Barani Afrika
ikiwemo nchi tatu za kipaumbele ambazo ni Tanzania, Msumbiji na Ghana,
nchi nyingine ambazo shirika hilo linafanya kazi ni Ethiopia, Senegal,
Ivory Coast na Nigeria.
WIZARA YA ARDHI YAKUTANA NA WADAU KUTOKA TAMISEMI KUJADILI MASUALA MBALIMBALI KUHUSU SEKTA YA ARDHI.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Dkt Yamungu Kayandabila akisisitiza jambo kwenye kikao na wadau kutoka TAMISEMI kuhusu maendeleo ya sekta ya Ardhi nchini
No comments :
Post a Comment