Tuesday, June 28, 2016

BALOZI SEIF ASEMA UGUNDUZI WA GESI ASILIA UTACHANGIA UKUAJI WA UCHUMI ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akifungua Semina juu ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi iliyofanyika katika ukumbi wa juu wa Baraza la Wawakilishi uliopo Mbweni. Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mh. Salama Aboud Talib na wa Pili kutoka Kulia ni Mwakilishi wa Kampuni ya Utafiti wa Mafuta na Gesi asilia ya Rakgas kutoka Nchini Ras Al – Khaimah Bwana Kamal Ataya.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia mada mbali mbali zilizotolewa kwenye Semina juu ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia.
Mtaalamu wa utafiti na uchimbaji mafuta na gesi kutoka Kampuni ya Rakgas ya Nchini Ras Al – Khaimah Bwana Osama Abdel akityoa mada kwenye semina ya mafuta na gesi ilitotolewa kwa wawakilishi wa Zanzibar.

FISHERIES MANAGEMENT PLAN III (FMP III) FOR LAKE VICTORIA FISHERIES LAUNCHED IN ARUSHA

The Permanent Secretary, Ministry of Agriculture, Livestock and Fisheries; Dr. Yohana Budeba (centre), launching and displaying the FMP III as delegates at the high table look on and applaud (L-R): Hosea Gonza Mbilinyi (Director of Fisheries at the Fisheries Development Division, Tanzania), Timothy Wesonga (Senior Livestock and Fisheries Officer, EAC Secretariat), Godfrey Monor (LVFO Executive Secretary) and Dr. Ali Said Matano (LVBC Executive Secretary).
​ The Permanent Secretary, Ministry of Agriculture, Livestock and Fisheries; Dr. Yohana Budeba (bottom centre) pauses for a group photo with representatives from Lake Victoria Environmental Management Programme Phase II (LVEMP II), the Lake Victoria Regional Beach Management Unit, LVFO, LVBC, Fisheries and Acquaculture Minitries from EAC Partner States and the East African Industrial Fishing and Fish Products Association(EAIFFPA) during the launch of the FMP III. 

The Lake Victoria Fisheries Management Plan III (FMP III) 2016 – 2020 whose goal is: “Recovery of biomass of Nile perch with Sustainable utilization of fisheries resources of Lake Victoria basin with equitable opportunities and benefits”, was yesterday launched at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania.

The FMP III is expected to guide the sustainable management of the fisheries resources and thus contribute to poverty alleviation and improvement of livelihoods, in line with the EAC Vision and Strategy Framework for Management and Development of the Lake Victoria basin; “a prosperous population, living in a healthy and sustainably managed environment providing equitable opportunities and benefits”.

Gracing the event as the Guest of Honour was Dr. Yohanna Budeba; the Permanent Secretary, Ministry of Agriculture, Livestock and Fisheries who launched the FMP III. In his remarks, he welcomed the fisheries stakeholders present at the meeting to the venue.

He began by emphasizing the value of fisheries as a resource within the EAC region, adding that it provides massive opportunities because it is a source of income, it creates employment opportunities in both industrial and artisanal processing, it is a source of food rich in omega III, iron, zinc and calcium which can go a long way in addressing malnutrition and stunted growth in children and it also attracts foreign exchange from exports in more than 20 countries internationally.

Also present at the launch was the Executive Secretary for Lake Victoria Fisheries Organization; Godfrey Monor who reported that there are several challenges that the Lake Victoria Fisheries is faced with which FMP III aims to address. These include: increased fishing pressure as a result of increasing demand and rising prices of fish and fisheries products; inadequate and unsustainable funding to implement research and agreed management interventions; increased illegalities due to weak enforcement; inadequate infrastructure for fish quality and safety, under developed aquaculture to meet the demand of fish and relieve fishing pressure from capture fishery, and other challenges caused by climate change. “In order to curtail the decline of natural resources within and around the Lake, the commitment from the Partner States should be translated to action for sustainability of our fisheries resources”.

RC MAKALLA AIOMBA BENKI KUU IFANYE UTAFITI KUHUSU UNUNUZI WA MAZAO YAKIWA SHAMBANI


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala (Katikati)akizungumza na viongozi wa benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya,kulia Mkurugenzi wa benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya Jovent Rushaka na Meneja Utawala na fedha Bakali Ally kushoto katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya ,June 28 -2016.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya  Amosi Makalla akizungumza na viongozi na wafanyakazi wa benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya mara baada ya kufanya ziara katika kwa engo la kujitabulisha .
Baadhi ya viongozi wa benki hiyo wakimsikiliza kwa makini Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla mara baada ya kufanya ziara katika benki hiyo June 28 mwaka huu.

WAKULIMA WADOGOWADOGO NA WADAU WA KILIMO WAKUTANA KUJADILI BAJETI YA KILIMO NA MABADILIKO YA TABIA NCHI.

Meneja utetezi kutoka Shirika la Kimataifa la OXFAM Tanzania Bi. Eluka Kibona akifungua mafunzo juu ya uelewa wa Bajeti ya Kilimo na Mabadiliko ya Tabianchi yanavyoathiri sekta ya kilimo Tanzania hasa wakulima wadogo wadogo.
Mkurugenzi wa Forum CC Bi. Rebecca Muna akielezea umuhimu wa mafunzo hayo yatakavyoweza kuwasaidia wakulima wadodogo katika kukabiliana na tatizo la Mabadiliko ya tabianchi.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo wakiwa katika kikundi kujadiliana maswala mbalimbali juu ya namna ya kuandaa bajeti Muwezeshaji kutoka Forum CC Feizal Ally Akiongoza majadiliano juu ya uandaaji wa bajeti ya kilomo na mabadiliko ya tabianchi ambayo yanawathiri kwa kiasi kikubwa wakulima wadogo wadogo.

DK. SHEIN AWAAPISHA MANAIBU KATIBU WAKUU IKULU

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akimuapisha Dk.Islam Seif Salum kuwa Naibu Katibu Mkuu ,Mifugo na Uvuvi katika Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi, katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] {28/06/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akimkabidhi hati ya kiapo Dk.Islam Seif Salum baada yakumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu ,Mifugo na Uvuvi katika Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi, katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] {28/06/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd,Hassan Abdulla Mitawi kuwa Naibu Katibu MkuuHabari katika Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] {28/06/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akimkabidhi hati ya kiapo Nd,Hassan Abdulla Mitawi baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu Habari katika Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] {28/06/2016.

MICHELLE OBAMA NA WATOTO WAKE WATUA NCHINI MOROCCO

SHAMO WORLD YATOA MSAADA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA MAUNGA JIJINI DAR LEO.

Mwakilishi wa Kampuni ya Shamo World Foundtion, Salama akikabidhi baadhi ya Vitu vya msaada kwa Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre, Zainabu Maunga jijini Dar es Salaam leo wakati walipotembelea katika kituo hicho kilichopo karibu na kituo cha Polisi cha Hananasif jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo mwakilishi wa kampuni ya Shamo World Foundation amesema kuwa wameguswa kutoa msaada katika kituo hicho kwa kutenda matendo ya huruma wakati wa kipindi hiki cha Mwezi wa Ramadhani kwa watoto kwa kuwa wanamahitiji mengi pia ni kuwapunguzia ugumu wa maisha walezi wa watoto hao.
 
Nae Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre, Zainabu Maunga amewashukuru kampuni ya Shamo World kuwaona kwa jicho la pekee na kwenda kuwapa msaada katika kituo hicho.
 
Mwakilishi wa Kampuni ya Shamo World Foundation, Salama amesema kampuni hiyo wamekabidhi Kg 50 za Mchele, Kg 50 za unga wa ngano na unga wa ugali, Kg 50 za sukari pamoja na Maboksi 15 ya Tende pamoja na mafuta ya kupikia

WACHINA WACHARUKA BAADA YA KUONA KITABU CHA ELIMU YA KUJAMIANA CHINA

MIKATABA IMEISHA HAWATAKUWEPO 2016/17

ITALIA YAWATOA NJE YA MICHUANO YA EURO 2016 MABINGWA WATETEZI HISPANIA

YAMETIMIA !! BAADA YA KUJITOA JUMUIYA YA ULAYA, SAFARI HII TENA UINGEREZA YATUPWA NJE YA FAINALI ZA EURO 2016 BAADA YA KUTANDIKWA 2-1 NA ICELAND

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya kuendelea kukifundisha kikosi hicho baada ya kushuhudia kikipokea kipigo cha mabao 2-1 toka kwa timu ya taifa ya Iceland ambayo hapo awali ilikuwa haipewi nafasi yeyote ya kufika mbali katika fainali za Euro 2016 zinazofanyika nchini Ufaransa.
Wachezaji wa timu ya taifa ya England, Joe Hart, Dele Alli na Gary Cahill wakiwa hawaamini kama kweli wameondolewa katika fainali za Euro 2016 baada ya kutandikwa 2-1 na Iceland usiku wa kuamkia leo.
Inauma sana, tumejitoa katika Jumuiya ya Ulaya, nasasa tumeondolewa katika fainali za Euro 2016? Niacheni niendelee kulia. Mtoto huyu shabiki wa timu ya taifa ya England akiwa na majonzi
Muonekano wa uwanja wa Stade de Nice kabla ya mtanange kati ya England na Iceland

ZOEZI LA UHAKIKI WA VYAMA VYA SIASA LAANZA KWA VYAMA VILIVYOPO DAR ES SALAAM

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Upande wa Uhakiki wa vyama vya Siasa , Bw. Sisty Nyahoza (kulia) akihakiki daftari lenye orodha ya wanachama wa Chama cha National League for Democratic (NLD) wakati wa zoezi la kuhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa chama hicho Oscar Emmanuel Makaidi na Katibu Mkuu wa NLD Tozzy Ephraim Matwanga.
Baadhi ya viongozi wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU) wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Msajili Msaidizi wa Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Upande wa Uperembe Bw. Ibrahim Mkwawa ( hayupo pichani) wakati wa uhakiki wa utekelezaji masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa lililoanza leo jinini Dar es Salaam.
Bw. Ibrahim Mkwawa, Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Upande wa Uperembe “Monitoring” (katikati) akikagua nyaraka mbalimbali za Chama cha Sauti ya Umma (SAU) wakati wa uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa lililoanza leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mhasibu Bi. Severa Assey kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa

TAASISI YA NITETEE YAITAKA SERIKALI KUTOA RUZUKU KWA TAASISI ZINAZOFANYA KAZI VIZURI

Mkurugenzi wa Taasisi ya Nitetee, Flora Lauwo akipungia mkono alipokuwa akitambulishwa bungeni Dodoma.
Flora Lauwo akitafakari jambo alipokuwa akifuatilia mwenendo wa mijadala ya Bunge mjini Dodoma.
Flora Lauwo (kushoto) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula katika viwanja vya Bunge, Dodoma

Serikali imetakiwa kuziangalia kwa jicho la tatu ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuanza kutoa ruzuku kwa taasisi za watu binafsi zinazofanya kazi ya kufuatilia na kubaini matatizo yanayowakumba wananchi kama afanyavyo, Flora Lauwo Mkurugenzi wa Taasisi ya Nitetee.

Licha ya serikali kutambua mchango unaotolewa na taasisi hizo, jamii nayo imeaswa kujitokeza kuwasaidia watu ambao wamekuwa wakisumbuliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia ,maradhi na wale wanaohitaji msaada wa kupata elimu .

Kufatia serikali kutambua mchango huo baadhi ya wadau kutoka sekta binafsi wanajitokeza na kubainisha changamoto zinazowakumba. Yapo malengo yanayowekwa na wadau hao ili kutimiza ndoto za kuwasaidia watanzania

“Lakini wapo Wajanja ambao wamekuwa wakinufaisha na misaada wanayopewa na wafadhili badala ya kuwasaidia walengwa,” alisema Lauwo.
 

Taasisi ya nitetee inajishughulisha na utatuzi wa matatizo yanayozikumba familia zinazoishi katika mazingira magumu ambapo mpaka sasa imeshazifikia kaya 36 pamoja na kuwapeleka watoto 20 shule.

MWANAUME JAPAN ACHANGANYIKIWA NA PENZI LA DOLI LA KIKE

Mwanaume mmoja nchini Japan amebainisha kuwa hatimaye ameipata furaha yake kutoka kwa mpenzi wake wa kike ambaye ni wa doli.

Mwanaume huyo Senji Nakajima, 61, amedai kuwa anafurahi uhusiano wake huo usiona dosari na doli hilo liitwalo Saori, ambapo wamekuwa wakifanya manunuzi pamoja na kutembea naye.

Nakajima ambaye ameoa mwanamke na amezaa naye watoto wawili, anaishi na doli hilo Jijini Tokyo, ambapo amelisifia kuwa ni muaminifu na haumchuni fedha zake.
                                          Senji Nakajima akiangalia TV na mpenzi wake doli 
                                        Senji Nakajima akimuogesha mpenzi wake huyo doli 
                                Doli Saori likiwa limepozi mithili ya mwanamke mrembo

No comments :

Post a Comment