Sunday, May 8, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI MAAFISA 586 KATIKA CHUO CHA MAAFISA WA JESHI MONDULI



MON1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
MON2 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
MON3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitunuku kamisheni kwa maafisa wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha Mafunzo ya kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha
MON4 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Afisa Mpya wa cheo cha Luteni Usu, Nasra Rashid ambaye alifanya vizuri zaidi kuliko Maafisa Wanafunzi wanawake katika chuo cha kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
MON5 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya wananchi General Davis Mwamunyange mara baada ya kuwasili kwenye chuo cha Mafunzo Kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
MON6 
Maafisa Wanafunzi wakipita kwa mwendo wa haraka  mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kutuniwa Kamisheni
MON7 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli TMA Meja Jenerali Paul Peter Massao kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya 586 katika chuo hicho cha Monduli.
MON8 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa wapya aliowatunuku Kamisheni katika cha Mafunzo Kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha. Wengine katika picha ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya wananchi  Jeneral Davis Mwamunyange , Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli TMA Meja Jenerali Paul Peter Massao, Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Maafisa wa ngazi za juu katika Jeshi la Ulinzi.
MON9 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi  wa Ngarenaro waliomsimamisha wakati akitokea kwenye chuo cha Mafunzo ya Kijenshi cha Monduli mkoani Arusha.
MON10 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitembea kikakamavu mara baada ya kutoka kukagua gwaride katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
MON11 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akizungumza na wanaanchi wa kona ya Mbauda mkoani Arusha.
MON12 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli mara baada ya kutazama picha za Majenerali wastaafu waliongoza Jeshi la Wananchi katika miaka ya nyuma.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli mara baada ya kutazama picha za Majenerali wastaafu waliongoza Jeshi la Wananchi katika miaka ya nyuma.
MON13 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi wa Kona ya Nairobi eneo la Arusha Tech mara baada ya kutoka kutunuku Kamisheni kwa maafisa Wapya katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi  cha Monduli mkoani Arusha. PICHA NA IKULU
…………………………………………………………………………………………………..
Na Mahmoud Ahmad,Monduli
Amiri jeshi mkuu na Rais   wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli amewatunuku Kamisheni  wahitimu wapatoa 586 kutoka Chuo cha Kijeshi TMA kilichopo Monduli Mkoani Arusha.
Raisi dkta jpm ambaye hii ni mara ya pili kuwatunuku maofisa hao wakijeshi katika chuo hicho cha kijeshi aliweza kuwapa zawadi mbalimbali kwa wale waliofanya vizuri katika mafunzo yao.
Aidha Raisi Magufuli alifurahiswa na kitendo cha Askari wanawake wapatao 6 miongoni mwa wahitimu 586 waliopata fursa ya kutunukiwa vyeo na kuibua shangwe na nderemo kwa wageni waliohudhuria Kamisheni hiyo
“Leo nimewatunuku vyeo vya kuwa watumishi katika Jeshi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nafasi hiyo naomba Mungu awasaidie’’alisema Raisi wakati akiwatunuku
 
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho cha kijeshi TMA Meja Jenerali Paul Masau akitoa taarifa fupi juu ya mafunzo ya wahitimu hao mbele ya Rais Magufuli  kuwa wahitimu wote waliohitimu mafunzo hayo ni Raia wa Tanzania.
Aliongeza kuwa kati ya wahitimu hao  kuna marubani ,Madaktari,na wengi wao ni wahitimu wa kidato cha sita katika masomo ya Sayansi  ambao watakuja kuongeza ufanisi kwa utendaji kazi katika jeshi kwa siku za usoni ili jeshi hilo liende kisasa zaidi.
‘’Miongoni mwa wahitimu wapo madaktari 80, marubani  6 wa ndege,huku 500 ni vijana ambao wamehitimu kidato cha sita katika masomo ya Sayansi na kufaulu vizuri ambao watasaidia katika kulijenga zaidi jeshi letu kwa siku za usoni’’alisema Meja Jenerali Masau.
 

NAIBU SPIKA ACKSON AFUNGUA SEMINA KWA WABUNGE KUHUSU UELEWA WA HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU

 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu), Dk Abdallah Possi (kulia), akiwasilisha mada katika semina ya Wabunge kukuza na kuimarisha usawa wa watu wenye ulemavu nchini, kwenye Ukumbi wa Bunge wa Msekwa mjini Dodoma jana. Kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Bukene, Seleman Zedi (CCM) na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akifungua semina hiyo
Baadhi ya wabunge wakihudhuria kwenye semina hiyo
Zedi akiongoza majadiliana wakati wa semina hiyo

Mkuu wa wilaya Bukombe aagiza maafisa tarafa kusimamia hifadhi ya mavuno kwa wananchi

mwen 
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Amani K. Mwenegoha ameagiza maafisa tarafa kusimamia kwa karibu shughuli za hifadhi ya mavuno yaliyopatikana katika Mvua  za  vuli Msimu wa 2015/2016  kwa kuhamasisha wananchi wenye mavuno mengi kila mahali kuhifadhi vizuri ili mavuno hayo yasiharibike na kuweka akiba ya kutosha kwaajili ya kaya zao.
 Pia ameagiza  Wakulima washauriwe kuuza ziada tu ya mavuno yao kwaajili ya kukidhi mahitaji yao muhimu  na kila kaya isimamiwe kuhakikisha imehifadhi mazao ya chakula cha kuwatosha  huku akiagiza Wafugaji  washauriwe kuvuna sehemu ya mifugo yao kwaajili ya kukidhi mahitaji yao muhimu na kununua nafaka kwaajili ya kaya zao.
Amesisitiza maelezo haya yawafikie viongozi ngazi za kata,vijiji na vitongoji kwaajili ya utekelezaji na taarifa iwasilishwe kwa Mkuu wa Wilaya kabla ya 13/05/2016.
Imetolewa na
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Bukombe
Geita      
06 Mei,   2016

MAKATIBU WAKUU WA VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA WAKUTANA NCHINI ZIMBABWE

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akitoa mada kwenye Kongamano la siku Nne la Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika. Kongamano hilo linafanyika Victoria Falls Zimbambwe lilianza tarehe 4 – 8 Mei, 2016. Vyama hivyo ni ANC ya Afrika Kusini, FRELIMO ya Msumbiji, MPLA ya Angola, SWAPO Party ya Namibia na CCM ya Tanzania.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akimpongeza Katibu Mtendaji Mkuu wa ZANU-PF Ndugu Ignatius Morgen Chombo kwa kufanikisha Kongamano  la Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika na anaeshuhudia katikati ni Katibu Mkuu wa FRELIMO Ndugu Eliseu Machava. Kongamano hilo linafanyika Victoria Falls, Zimbabwe tarehe 4 – 8 Mei 2016

 Picha ya pamoja ya Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika(FLM) wanaoshiriki Kongamano la siku Nne la kutafakari uimarishaji na uendelezaji wa ushirikiano wao na namna ya kukabiliana na changamoto walizonazo. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa ANC ya Afrika Kusini Ndugu Ndugu Gwede Mantashe, Katibu Mkuu wa FRELIMO ya Msumbiji Ndugu Eliseu Machava, Katibu Mkuu wa CCM ya Tanzania Ndugu Abdulrahaman Kinana, Makamu Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomnisti cha China (CPC) Ndugu Guo Yezhou, Katibu Mtendaji Mkuu wa ZANU-PF ya Zimbabwe Ndugu Ignatius Morgen Chombo, Katibu Mkuu wa MPLA ya Angola Ndugu Juliao Mateus Paulo na Katibu Mkuu wa SWAPO Party ya Namibia Ndugu Nangolo Mbumba. Kongamano hilo linafanyika Victoria Falls, Zimbabwe tarehe 4 – 8 Mei 2016.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa ANC ya Afrika Kusini, Ndugu Gwede Mantashe kwenye Kongamano la Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika(FLM) linalofanyika Victoria Falls, Zimbabwe tarehe 4 – 8 Mei 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA KUU LA UWT TAIFA DODOMA LEO

uw1 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia ngoma alipowasili katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM mjini Dodoma leo Mei 7,2016 kwa ajili ya kufungua mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa.
uw2 
Wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokua akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa wenye lengo la kukumbushana katika majukumu ya kiutendaji kwenye ngazi mbalimbali za Jumuiya hiyo pamoja na kumpongeza Makamu wa Rais kwa kuchaguliwa Mwanamke wa kwanza katika Ngazi hiyo Kuu  ya kitaifa. Mkutano huo umefunguliwa leo Mei 7,2016 katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini
uw3 uw4 
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la UWT Taifa wakimkabidhi zawadi za aina mbalimbali Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kumpongeza kwa kuchaguliwa Mwanamke wa kwanza katika Ngazi Kuu  ya kitaifa  wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa uliofunguliwa leo Mei 7,2016 katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma
uw6 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa wenye lengo la kukumbushana katika majukumu ya kiutendaji kwenye ngazi mbalimbali za Jumuiya hiyo pamoja na kumpongeza Makamu wa Rais kwa kuchaguliwa Mwanamke wa kwanza katika Ngazi hiyo Kuu  ya kitaifa. Mkutano huo umefunguliwa leo Mei 7,2016 katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.
uw8 
Wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokua akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa wenye lengo la kukumbushana katika majukumu ya kiutendaji kwenye ngazi mbalimbali za Jumuiya hiyo pamoja na kumpongeza Makamu wa Rais kwa kuchaguliwa Mwanamke wa kwanza katika Ngazi hiyo Kuu  ya kitaifa. Mkutano huo umefunguliwa leo Mei 7,2016 katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.           
uw9 
Wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokua akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa wenye lengo la kukumbushana katika majukumu ya kiutendaji kwenye ngazi mbalimbali za Jumuiya hiyo pamoja na kumpongeza Makamu wa Rais kwa kuchaguliwa Mwanamke wa kwanza katika Ngazi hiyo Kuu  ya kitaifa. Mkutano huo umefunguliwa leo Mei 7,2016 katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.         
uw10Mjumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa Mama Lupembe akisalimiana na kumpongeza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa Mwanamke wa kwanza katika Ngazi Kuu  ya kitaifa wakati wa Mkutano Mkuu wa UWT Taifa uliofunguliwa leo Mei 7,2016 katika ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM Mjini Dodoma.
uw11Makamu wa Raisv wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Mhe. Adam Kimbisa kabla ya kufungua Semina ya Mafunzo kwa ajili ya kuwajengea Uwezo Viongozi na Mkada wa Chma cha Mapinduzi iliyofunguliwa leo Mei 7,2016 katika Ukumbi wa MORENA Mjini Dodoma. (Picha na OMR)
uw13 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Semina ya Mafunzo kwa ajili ya kuwajengea Uwezo Viongozi na Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM iliyofunguliwa leo Mei 7,2016 katika ukumbi wa MORENA Mjini Dodoma.uw14 
akamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa bkatika picha ya pamoja na Viongozi na Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM baada ya  kufungua Semina ya Mafunzo kwa ajili ya kuwajengea Uwezo Viongozi na Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM iliyofunguliwa leo Mei 7,2016 katika ukumbi wa MORENA Mjini Dodoma.

UVCCM Z’BAR YAWATAKA VIONGOZI KUTEKELEZA AHADI

5Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka akiwahutubia mamia ya vijana katika moja ya mikutano ya umona huo kisiwani Zanzibar.
……………………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.
UMOJA wa vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) Zanzibar umewataka vijana wa umoja huo katika Mkoa wa Kaskazini Unguja  kuwakumbusha viongozi waliopo madarakani kwa sasa kutekeleza kwa haraka ahadi walizotoa wakati wa kuomba ridhaa ya kuingia madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa Marudio uliofanyika mwaka huu.
Umesema vijana wana haki ya kutumia vikao halali vinavyokubalika katika utaratibu wa kiuongozi ndani ya UVCCM kuwakumbusha viongozi wa chama hicho kutekeleza kwa vitendo ahadi walizotoa kwa wananchi wa Zanzibar.
 Akizungumza katika ziara ya UVCCM katika Mkoa huo, Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Abdulghafar Idrissa huko katika ofisi ya jimbo la Jimbo la Kitope iliyopo Kinduni Unguja.
Alifafanua kwamba CCM ni chama chenye viongozi makini wanaoahidi na wakatekeleza hivyo hakuna haja ya vijana kuendelea kulalamika badala yake wafuate utaratibu kuwakumbusha wahusika watekeleze majukumu yao kwa wananchi.
“ Vijana kumbukeni kuwa kwamba nyie ndiyo mliowaweka madarakani hao Marais, wabunge, wawakilishi na madiwani hivyo msiwaogope kuwakumbusha kwa kufuata taratibu wajibu wao wa kutekeleza ahadi zao kwenu na wakikataa basi rudini kwetu mtwambie na tutayafanyia kazi.”, alisema Idrissa.
Idrissa alisisitiza vijana hao  kuendelea kuwa wamoja ili waweze kunufaika na fursa mbali mbali zilizopo katika chama na serikali iliyopo madakani.
Alisema umoja na mshikamano ndiyo njia pekee itakayowawezesha vijana kubuni fursa za maendeleo  kwa lengo la kujikwamua katika wimbi la umasikini nchini.

Amos Makalla azindua mashindano ya UMISSETA Copa Coca Cola mkoani Mbeya

co1 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akihutubia wadau wa michezo na wanafunzi wakati wa Uzinduzi wa mashindano ua UMISSETA ambayo mwaka huu yamedhaminiwa na kampuni ya Coca Cola.Uzinduzi huo ulifanyika katika uwanja wa Sokoine ambapo kulifanyika michezo mbalimbali na burudani za kila aina zilikuwepo.
co2 
Meneja wa Kiwanda cha Coca Cola  tawi la Mbeya, Gary pay (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla ndani ya Uwanja wa Sokoine Mbeya kwenye uzinduzi wa mashindano ya UMISSETA 
co3 
Mkuu wa Mkoa Amos Makalla akigagua moja ya timu wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo kwenye uwanja wa mpira wa Sokoine.
co4 
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali walihudhuria katika uzinduzi hyuo wa mashindano ya UMISSETA wakiwa katika uwanja wa Sokoine.
co5 
Burudani za muziki pia zilikuwepo kama kinavyoonekana kikundi hiki kikitumuiza katika uzinduzi huo.
co6 
Mkuu wa Mkoa Amos Makalla akipiga mpira kuashiria uzinduzi wa mashindano ya UMISSETA  mkoani humo.

Serikali yabaini tani 4,579.2 zilizokuwa zimefichwa Kwenye maghala

indexF
rank mvungi-Maelezo
Taasisi ya kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU) yabaini kuwepo kwa sukari iliyofichwa  tani 4,579.2 iliyonunuliwa toka Kiwanda cha Sukari Kilombero.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentine Mlolowa Taasisi  hiyo imeanza uchunguzi dhidi ya swala hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa mnamo tarehe 05 Mei, 2016 timu ya uchunguzi ilitembelea maghala yaliyopo Tabata Jijini Dar es salaam na kubaini uwepo wa sukari hiyo.
 TAKUKURU tayari imetembelea  Maghala ya mfanyabiasha Haruni Daudi Zacharia ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Al-Naeem yaliyoko Mbagala na Tabata ambaye ni miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wa sukari hapa nchini na anayetuhumiwa kuficha bidhaa hiyo. Ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Aidha uchunguzi  uliofanywa na Taasisi hiyo ulibaini kuwepo kwa njama za dhati za kutouza  sukari iliyokutwa katika maghala hayo kulikofanywa na mfanyabiashara huyo kwani hata sehemu ya Maghala ilipo sukari hiyo hapakuwa na dalili za upakiaji wa sukari  hiyo ili iweze kusambazwa.
Taarifa hiyo imeendelea kufafanua kuwa katika eneo la Kitumbini  kumekuwa na wananchi wengi wanaohitaji  bidhaa hiyo na wachache sana waliweza kuuziwa  licha ya ukweli kwamba sukari ilikuwepo.
Katika uchunguzi wake TAKUKURU pia  imebaini kuwepo kwa mikakati ya dhati iliyokuwa ikifanywa na mfanyabiasha huyo kwa kununua sukari yote toka viwanda vya ndani na kisha kuihifadhi na kuuza bidhaa hiyo kidogo kidogo kwa wastani wa tani 250 kwa siku wakati alikuwa na uwezo wa kuuza zaidi jambo lililochangia uhaba wa sukari katika soko.
Kuficha bidhaa ni kosa la uhujumu uchumi na ni  kinyume na Aya ya 3 Jedwali la kwanza Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 [Chapisho la Mwaka 2002]. Serikali haitavumilia hujuma za namna hii na itachukua hatua kali dhidi ya mfanyabiashara yeyote ataekwenda kinyume na sheria hii.
TAKUKURU  imetoa wito kwa wafanyabiashara wote wa sukari kuacha vitendo vya kuficha sukari na vyombo vya uchunguzi vinafuatilia kote nchini na yeyote atakayebainika kufanya hujuma hizo atakabiliwa na mkondo wa Sheria.
OGORO YA ARDHI IMALIZWE NA SERA MPYA YA ARDHI
wn1Hamisi Maduka Kaimu mwenyekiti wa Kijiji cha Kigwa B wilaya ya Uyuwi Mkoani Tabora akitoa maoni yake mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ambaye alisistiza ulipaji wa fidia za Ardhi uzingatie uhalisia wa thamani ya eneo husika.
wn2 
Abdallah Moto mkazi wa Kijiji cha Kigwa B wilaya ya Uyuwi Mkoani Tabora akitoa maoni yake kwa Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 kuhusu suala la kupewa kipaumbele utoaji wa hati miliki kwa wanavijiji.
wn3Shakira Masudi mkazi wa Kijiji cha Kigwa B wilaya ya Uyuwi Mkoani Tabora akitoa maoni yake mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ambaye alitaka Sera itambue wamiliki wa Ardhi wa maeneo wa muda mrefu katika kutoa Hati.
wn4Mwl. Hadija Nyembo mkuu wa wilaya ya Kaliua mkoa wa Tabora akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 wakati akitoa maoni yake kuhusu Umiliki wa Ardhi mkoani Tabora.
wn5Hanifa Selengu Mkuu wa wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 wakati akitoa maoni yake kuhusu Umiliki wa Ardhi mkoani Tabora.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Ardhi.
……………………………………………………………………………………………………………………………….
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza zoezi la ukusanyaji wa maoni na kuipitia upya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ili kuiboresha. Zoezi hilo limeanza Mwaka huu wa 2016 ambapo linashirikisha kanda nane za Ardhi ambazo ni Kanda ya Dar es salaam, Kanda ya Mashariki, Kanda ya Kusini, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kati, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kaskazini.
Na kwa sasa kamati maalumu ya kukusanya maoni ipo mkoani Tabora ikikusanya maoni ya wananchi na wadau mbalimbali wa sekta ya Ardhi ili kupata sera iliyoridhiwa na wengi.
Katika sekta ya Ardhi Serikali ya Tanzania imekuwa ikitekeleza Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 kwa takribani miaka 20 hadi sasa, hata hivyo zimejitokeza changamoto nyingi ambazo zinalazimu kufanya mapitio ya sera hiyo.
Migogoro na malalamiko yanayotokana na ardhi ni changamoto zinazo chukua nafasi kubwa katika jamii yetu na imekuwa ikiigharimu  kwa kiasi kikubwa katika kuitatua.
Kuongezeka kwa migogoro hii imekuwa ni changamoto zinazoikabili sekta ya ardhi pamoja na watumiaji mbalimbali wa ardhi hususan wakulima na wafugaji, wawekezaji, wananchi, vijiji na hifadhi.
Hata hivyo, kuongezeka kwa mahitaji ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji hususan katika sekta za kilimo, madini, viwanda na wananchi kutonufaika na uwekezaji unaofanywa katika ardhi na hivyo kusababisha migogoro baina ya wananchi na wawekezaji.
Aidha kutokuwepo kwa mipango ya matumizi endelevu ya ardhi mijini na vijijini na hata sekta ya ardhi kuvamiwa na madalali ni changamoto iliyoifanya Serikali kuamua kuipitia upya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995.
Changamoto zote kwa pamoja, zimelazimika kufanyika kwa mapitio ya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ili kutoa mwelekeo mpya na usimamizi wa ardhi kwa manufaa ya watanzania wote.
Ardhi ni Sekta mama na hivyo basi Sera ya ardhi ni sera mama katika masuala yote ya maendeleo ikiwemo kilimo na mifugo, ambayo shughuli zake zinafanyika kwenye ardhi.
Na sasa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza zoezi la ukusanyaji wa maoni na kuipitia upya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ili kuiboresha. Zoezi hilo limeanza Mwaka huu wa 2016 ambapo linashirikisha kanda nane za Ardhi ambazo ni Kanda ya Dar es salaam, Kanda ya Mashariki, Kanda ya Kusini, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kati, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kaskazini.

Rais Atoa Agizo Kuhusu Sukari

TANZANIA UK DIASPORA TASKFORCE YATOA PONGEZI KWA DKT. ASHA ROSE MIGIRO.

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAZUNGUMZIA KUHUSU UTEKELEZAJI WA AHADI YA UADILIFU KWA WATUMISHI WA UMMA

ut1Mtangazaji wa kipindi cha Rushwa ni Adui wa Haki Bi. Miriam Chisoro (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji wa Maadili wa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Mathew Kirama (kulia) wakati  wakijadili mada kuhusu Ahadi ya Uadilifu  kwa watumishi wa umma ofisini kwa mkurugenzi huyo mapema leo.
ut2Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji wa Maadili wa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi  wa Umma Bw. Mathew Kirama (kulia) akisisitiza umuhimu wa utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa umma wakati wakijadili mada hiyo na Mtangazaji  wa kipindi cha Rushwa ni Adui wa Haki Bi.Miriam Chisoro (kushoto) ofisini kwa mkurugenzi huyo mapema leo

No comments :

Post a Comment