Tuesday, May 10, 2016

MAJALIWA AKUTANA NA WAWEKEZAJI WA UMEME WA GESI TOKA JAPAN

jal1 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata ufafanuzi wa mikakati ya uwekezaji kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya  KOYO ya Japan, Bw.  Norio Shoji wakati alipokutana na ujembe wa kampuni hiyo  ofisini kwake jijini Dar es salaam May 9, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
jal2 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Kampuni ya Japan ya KOYO na   kampuni ya Kitanzania ya SSF Limited ambazo kwa pamoja  zimekusudia  kushirikiana ili kuwekeza kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua nchini. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam May 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
jal3 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na  Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya  KOYO ya Japan, Bw.  Norio Shoji  baada ya kukutana na Mtendaji huyo na ujumbe wake ofisini kwake jijini Dar es salaam May 9, 2016. Kampuni hiyo ikishirikiana na Kampuni ya Kitanzania ya SSF Limited inakusudia kuwekeza  kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua nchini. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) 
jal4 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya Japan ya KOYO na   kampuni ya Kitanzania ya SSF Limited ambazo kwa pamoja  zimekusudia  kushirikiana ili kuwekeza kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua nchini. Waziri Mkuu alifanya mazungumzo na viongozi hao  ofisini kwake  jijini Dar es salaam May 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Watanzania wahamasishwa kujitokeza kushiriki shindano la kuongeza kipato

index 
Mtaalam Mshauri wa Master Card Foundation Gabriel Kivuti akieleza jambo kwa  waandishi wa habari juu ya kushiriki shindano la kuongeza kipato lijulikanalo kama “Scaling Competition” kwa makundi yanayoruhusiwa kushiriki shindano hilo kuwa ni pamoja na vikundi vya akiba, bima ndogo ndogo na mifumo ya umoja wa fedha, fomu za maombi na mwongozo wa kushiriki shindano hilo zinapatikana katika tovuti ya www.frp.org .
M1 
Mtaalam Mshauri wa Master Card Foundation Gabriel Kivuti akifafanua jambo  katika semina ya namna shirika hilo linavyofanya kazi na jinsi ya kushiriki shindano la mwaka 2016 ili kupata washindi watakaopata msaada wa kifedha na kuboresha ushirikishwaji wa kifedha kwa wakulima wadogo Afrika.
…………………………………………………………………
Na: Lilian Lundo – Maelezo
 
Watanzania wameombwa  kujitokeza  kwa wingi  kushiriki shindano la kuongeza kipato lijulikanalo kama “Scaling Competition” kwa kutuma maombi yao  shirika la “Master Card Foundation, Fund For Rural Prosperity” ili kupanua na kuimarisha upatikanaji wa fedha Vijijini Tanzania.
Hayo yalisemwa na Mtaalam Mshauri wa Master Card Foundation Gabriel Kivuti leo, jijini Dar es Salaam katika semina ya namna shirika hilo linavyofanya kazi na jinsi ya kushiriki shindano la mwaka 2016 ili kupata washindi watakaopata msaada wa kifedha na kuboresha ushirikishwaji wa kifedha kwa wakulima wadogo Afrika.
“Master Card Foundation inafanya kazi na mashirika yenye maono  ili kuleta zaidi upatikanaji  wa elimu, mafunzo ya ujuzi na huduma za kifedha kwa watu wanaoishi katika umaskini barani Afrika, ikiongozwa na dira ya kuboresha mafunzo na kuongeza ushirikishwaji wa upatikanaji wa kifedha ili kupunguza umaskini,” alisema Kivuti.
Kivuti alisema kuwa, kaya nyingi  za vijijini barani Afrika hazishirikishwi katika masuala ya kifedha na zaidi ya asilimia 70 za familia Kusini mwa Jangwa la Sahara sehemu kubwa ya mapato yao yanatokana na shughuli za kilimo, wakati huohuo watoa huduma za kifedha wanakabiliana na changamoto kadhaa katika kuifikia  jamii, hivyo Master Card likaamua kusaidia miradi ambayo ina uwezo wa kuleta mabadiliko chanya.
Aidha, Kivuti alitaja makundi yanayoruhusiwa kushiriki shindano hilo kuwa ni pamoja na vikundi vya akiba, bima ndogo ndogo na mifumo ya umoja wa fedha, fomu za maombi na mwongozo wa kushiriki shindano hilo zinapatikana katika tovuti ya www.frp.org .
Jumla ya dola za Kimarekani milioni 10.6 zimetolewa kwa washindi wa mwaka 2015 kwa ajili ya maendeleo Vijijini, kampuni zilizoshinda  ni APA Insurance Ltd kutoka Kenya, Finserve Afrika Ltd/Equitel kutoka Uganda, M-KOPA LLC kutoka Tanzania,  Musoni Kenya Ltd kutoka Kenya na Olam Uganda Ltd kutoka Uganda. Kupitia kampuni hizo takribani watu milioni nane wanaoishi maeneo ya Vijijini watakuwa na fursa ya kupata huduma za kifedha ifikapo mwaka 2020

WAZIRI MKUU KUMWAKILISHA RAIS MAGUFULI LONDON

JIL
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anatarajiwa kuondoka nchini leo jioni (Jumanne, Mei 10, 2016) kwenda London, Uingereza kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi unaojadili suala la kupambana na rushwa (Anti-Corruption Summit 2016) utakaofanyika Mei  12, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana, Waziri Mkuu alisema anaenda kumwakilisha Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli kwa sababu siku hiyo hiyo, atalazimika kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Museveni.
“Mheshimiwa Dk. Magufuli ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na siku hiyo hiyo, mmoja wa marais wa nchi wanachama anaapishwa. Kwa hiyo amelazimika kwenda kuhudhuria sherehe hizo,” alifafanua Waziri Mkuu.
Akizungumzia kuhusu mada ya mkutano huo, Waziri Mkuu amesema Tanzania inafanya vema katika mapambano dhidi ya rushwa na kwamba baadhi ya nchi zimeanza kuvutiwa na juhudi ambazo Serikali imekuwa ikichukua.
“Waziri Mkuu wa Uingereza ameandaa mkutano huu na alimwalika Mheshimiwa Rais Magufuli ili ahudhurie akiwa ni miongoni wa wakuu wa nchi 60 watakaohudhuria mkutano huo. Tanzania ni miongini mwa nchi mbili kutoka bara la Afrika ambazo zimealikwa kushiriki. Nchi nyingine ya kutoka Afrika ni Nigeria,” alisema.
Waziri Mkuu atafuatana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa na Kikanda, Balozi Dk. Augustine Mahiga, Mkurugenzi wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola, wataalamu wa sekta ya rushwa na wanasheria
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
2 MTAA WA MAGOGONI,
  1. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMANNE, MEI 10, 2016.

WAZIRI MKUU: SERIKALI ITAAGIZA TANI 70,000 ZA SUKARI

MAJALIWA 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Waandishi wa Habari kwenye makazi yake jijini Dar es salaam.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaagiza kutoka nje ya nchi tani 70,000 za sukari ambapo kati ya hizo, tani 11,957 zimeshawasili nchini na zitaanza kusambazwa kesho (Jumatano).
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Mei 10, 2016) wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Akitoa ufafanuzi wa sukari ambayo imekwishawasili nchini, Waziri Mkuu alisema tani 2,000 zitapelekwa mikoa ya Kaskazini, tani 3,000 (mikoa ya Kanda ya Ziwa), tani 2,000 (mikoa ya Kusini), tani 2,000 (Nyanda za Juu Kusini) na tani 2,000 (mikoa ya Kanda ya Kati).
“Tani nyingine 24,000 za sukari zitawasili Ijumaa hii na hadi zitoke bandarini itakuwa kama Jumapili kwa hiyo zinaweza kusambazwa kuanzia Jumatatu. Tani nyingine 20,000 zitawasili baadaye, ama mwishoni mwa mwezi huu au mapema mwezi Juni,” alisema Waziri Mkuu.
Amesema anawataka Watanzania wasihofu kuhusu uhaba wa sukari uliojitokeza hivi karibuni kwani umesababishwa na watu wachache. “Mheshimiwa Rais ameagiza watu waliohodhi bidhaa hii wakamatwe na sukari isambazwe. Lakini pia tunaagiza kwa muda mfupi kwa sababu viwanda vyetu vinatarajia kuanza uzalishaji ifikapo Julai,” alisema.
Amewataka wasambazaji wa sukari waziuze kwa wafanyabishara wadogo ili wao wawawuzie wananchi kwa bei elekezi ya sh. 1,800. Pia amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia zoezi la ukaguzi ili kubaini zaidi wale waliohodhi bidhaa hiyo.
Akifafanua kuhusu mkakati wa Serikali kuongeza uzalishaji wa sukari nchini, Waziri Mkuu amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha tatizo la uhaba wa sukari nchini linakwisha ifikapo 2019. “Wananchi wasiogope, Serikali imechukua hatua kwa udhibiti mzuri ili tusije kuporomosha soko letu la ndani,” alisema.
“Tunao mkakati wa kuboresha viwanda vya ndani, wenye viwanda wenyewe au kwa ubia na wawekezaji kutoka nje, wanaweza kufungua mashamba kwenye maeneo matatu tuliyotenga kwa ajili hiyo,” alisema.
“Serikali imetenga maeneo matatu yanayofaa kwa kilimo cha miwa huko Bagamoyo, Ngerengere na Kigoma. Huko wanaweza kulima na kujenga viwanda vya sukari na uzalishaji ukawa unapanda mwaka kwa mwaka hadi tutakapoweza kuimaliza hii gap iliyopo,” alisema.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
2 MTAA WA MAGOGONI,
  1. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMANNE, MEI 10, 2016.

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU KUPAKIA MIZIGO KUPITA KIASI.

images 
Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.
………………………………………..
SERIKALI imepiga marufuku upakiaji wa mizigo kupita kiasi (lumbesa) katika magunia kuanzia mwaka ujao wa fedha.
Kauli hiyo imetolewa jana Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (Mb) wakati akijibu hoja mbalimbali za Wabunge wakiochangia hotuba ya Wizara yake.
Amesema kuwa, kuanzia mwaka ujao wa fedha, Vyombo vy Dola vitakamata wafanyabiashara wote watakaokuwa wanapakia lumbesa.
Mhe. Mwijage alisema kuwam upakiaji huo wa mizigi kupita kiasi unawasababishia wizi kwa wakulima ambapo ametoa wito kwa wakulima na wafanyabiashara nchini kutumia vipimo halali wakati wanaponunua na kuuza mazao yao mbalimbali.
Katika hatua nyingine, Waziri huyo ametoa wito kwa wakulima kuacha tabia ya kuuza mazao yao yakiwa shambani au kabla ya kukomaa.
Alisema kuwa hali hiyo inawarudisha nyuma na kuwapunja wakati wangesubiri mazao yakomae wangepata fedha za kutosha.

11 WA KWANZA DHIDI YA YANGA HAWA HAPA

pngKOCHA mkuu wa Mbeya City Fc, Kinnah Phiri muda mfupi uliopita ametangaza kikosi cha nyota 11 watakaoanza kwenye mchezo  wa leo dhidi ya Yanga  katika kinyang’anyiro cha ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Katika kikosi hicho mlinda mlango Juma  Kaseja  anaendelea kusimama langoni sambamba na walinzi wa kulia na kushoto, John Kabanda na Hassan Mwasapili.
Wengine katika kikosi hichi ni kama ifuatavyo
1.Juma Kaseja 2. John Kabanda 3. Hassan Mwasapili 4. Tumba Lui 5.Haruna Shamte 6.Kenny Ally 7. Seleman Mangoma 8. Ramadhan Chombo 9. Salvatory Nkulula .10 Geoffrey Mlawa 11 Joseph Mahundi
SUB: Hanningtony Kalyesubula, Hamidu Mohamed, John Jerome,Ditram Nchimbi,Haruna Moshi,Raphael Daud na Yohana Moriss.
Mchezo huu namba 218 umepangwa kuanza saa 10:00 na utachezeshwa na mwamuzi Jimmy Fanuel kutoka Shinyanga, huku kiingilio kwa mashabiki kikiwa ni shilingi 5000 tu.

NAPE: UANACHAMA WA TFF KATIKA FIFA UPO.

NAPE 
Na Benedict Liwenga-MAELEZO, Dodoma.
…………………………………..
Kufuatia majadiliano na vikao mbalimbali vilivyofanyika mwaka 2005-2010, kumbukumbu zinaonyesha kuwa suala la uanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) lilifanyiwa kazi kwa ukamilifu na Serikali za pande zote mbili kwa ushirikiano na Vyama vyote viwili.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (Mb) wakati akijibu swali la Mhe. Mbunge wa Dimani Hafidh Ali Tahir lenye kipengele a,b na c lililotaka kujua ni nini matokeo ya Kamati iliyoundwa na Waziri Mkuu.
Mhe. Nnauye ameeleza kwamba, kwa kutambua umuhimu wa ZFA kupata uanchama wa FIFA, mwaka 2010 ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwamba, ukiongozwa na aliyekuwa Naibu Waziri Kiongozi, Mhe. Juma Shamhuna pamoja na aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Mhe. Joel Bendera walikwenda Zurich, Switzerland ambako walikutana na Rais wa FIFA wa wakati huo.
Aidha, Mhe, Nnauye amefafanua kuwa, katika msafara huo walifuatana na viongpozi wa TFF na ZFA na madhumuni ya safari hiyo ilikuwa ni kuwasilisha maombi ya ZFA kupewa uanachama wa FIFA.
“Mwezi Juni 2011, FIFA iliiandikia ZFA ikiwajulisha kuwa kwa mujibu wa taratibu zilizopo, isingewezekana Zanzibar kupata Uanachama wa FIFA kwa kuwa wananchama wao ni nchi zinazotambuliwa na Jumuiya ya Kimataifa kama ilivyoelezwa katika aya ya 10 ya Katiba yao”, alisema Mhe. Nnauye.
Mhe. Nnauye aliongeza kuwa, suala la usajili wa TFF au ZFA linafahamika vyema ndani ya Serikali ya Mapinduzi pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Hata hivyo, naomba kulihakikishia Bunge lako Tukufu kuwa, uanachama wa TFF katika FIFA upo kwa mujibu wa muafaka wa pande zote mbili.
Kwa kuzingatia utaratibu wa FIFA kuhusiana na suala hilo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imewaelekeza TFF nao wako tayari kufanya maridhiano na ZFA ili kukamilisha utaratibu wa wazi wa kukidhi mahitaji ya Zanzibar kushiriki katika masuala ya FIFA kupitia TFF bila kuathiri ushiriki wa klabu za Zanzibar katika mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).

SERIKALI YATENGA SHILINGI BILIONI 59.5 KWA AJILI YA KUWAWEZESHA WANANCHI VIJIJINI.

imagesBB 
Na Benedict Liwenga-MAELEZO, Dodoma.
…………………………………….
SERIKALI imetenga Shilingi bilioni 59.5 katika Bajeti ya mwaka 2016/17 kwa ajili ya kuwawezesha Wananchi vijijini kwa kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji na mtaa.
Taarifa hiyo imetolewa leo Bungeni na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Watu wenye Ulemavu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi (Mb) wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Esther Mahawe aliyetaka kujua ni lini fedha zingetolewa na Serikali imejipanga vipi kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wananchi juu ya njia bora ya kutumia fedha hizo.
Dkt. Possi amesema kuwa, fedha hizo zitatolewa mara baada ya kuidhinishwa na Bunge hilo na baada ya kukamilisha taratibu mahususi zinazolenga kuhakikisha uwepo wa tija katika matumizi ya fedha hizo.
Ameongeza kuwa, kuhusu mpango bora wa Elimu ya Ujasiriamali kwa wananchi, Serikali inaendelea kukamilisha maandalizi ya utaratibu maalum wa utoaji wa fedha hizo ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu ya Ujasiriamali.
“Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI imepewa kazi ya kuratibu utekelezaji wa mpango huo”, alisema Dkt. Possi.

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI DODOMA 10 MEI, 2016.

1 
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi (kulia) pamoja na Katibu Mkuu, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima wakiwa katika mazungumzo Bungeni mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa vikao vya asubuhi vya bunge hilo 10 Mei, 2016.
3 
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Jenerali Davis Mwamunyange (kulia) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Katibu Mkuu, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima Bungeni mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa vikao vya asubuhi vya bunge hilo 10 Mei, 2016.
2 
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akisoma taarifa Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa leo 10 Mei, 2016, Bungeni mjini Dodoma.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO, DODOMA.

KAMISHNA MSAIDIZI KITENGO CHA HAKI ZA MTOTO AFUNGUA NYUMBA ZA KUNDI LA WATOTO

Kaimu Kamishna msaidizi kitengo cha haki za mtoto na marekebisho ya tabia, Steven Gumbo akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa mradi wa nyumba za kundi la watoto wanaoelekea ujanani katika kituo cha kulelea watoto cha Aman Center kilichopo mjini Moshi.
Jengo jipya lililojengwa kwa ufadhili wa Emirates National Bank of Dubai (ENBD) kwa ajili ya watoto wanaoelekea ujanani katika kituo cha kulelea watoto cha Aman Center kilichopo mjini Moshi.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto cha Aman Center Meindert Schaap akimuonesha Kaimu Kamishna msaidizi kitengo cha haki za mtoto na marekebisho ya tabia, Steven Gumbo maeneo mbalimbali ya jengo hilo katika ramani.
Moja ya muonekano wa chumba katika jengo hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto cha Aman Center Meindert Schaap akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa jengo hilo.
Baadhi ya walimu na walezi wa watoto katika kituo cha kulelea watoto cha Aman Center wakifuatilia shughuli mbalimbali katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto cha Aman Center Meindert Schaap akiteta jambo na Kaimu Kamishna kitengo cha haki za mtoto na marekebisho ya tabia, Steven Gumbo wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto cha Aman Center Meindert Schaap akimkaribisha Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ,Agnes Urassa katika Hafla hiyo.
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Aman Center kilichopo mjini Moshi.

DAWASCO KUGHARAMIA GHARAMA ZA UUNGANISHAJI KWA WATEJA WAPYA

Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Katika kutekeleza agizo la serikali la kuwafikia wateja laki 4 (400,000) ifikapo June
2016 ,Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (Dawasco) ,linaendelea
na zoezi
  la uunganishaji wa huduma ya
Maji kwa wananchi wote wa jiji la Dar es salaam pamoja na miji ya Bagamoyo na
Kibaha mkoani Pwani huku ikigharamia gharama zote za uunganishaji ambazo awali
zilikuwa zikilipwa na mteja.


Akiongeana waandishi wa habari hivi Afisa mtendaji mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian
Luhemeja ameeleza kuwa kwenye awamu hii ya zoezi la uunganishaji wateja wapya
shirika litagharamia gharama zote za maunganisho ambazo ni gharama za
uunganishaji, mabomba na vifaa vya uunganishaji ambapo mteja atawajibika kurudisha
gharama hizo za maunganisho kidogo kidogo kila mwezi kwa kipindi cha miezi 12
baada ya kupata huduma ya Maji.
 
“Dawasco itamuunganishia huduma ya maji na kugharamia gharama zote uunganishaji ila
mteja atawajibika kurudisha ile gharama kidogokidogo kila mwezi kwa kipindi cha
miezi 12 baada ya kupata huduma ya Maji hii itasaidia hata wale ambao kipato
chao ni cha chini kuweza kuunganishiwa huduma ya Maji” alisema Luhemeja.
Pia Mhandisi Cyprian Luhemeja ameleeza kuwa zoezi hili la uunganishia wateja wapya ni
la kipindi cha miezi miwili tu cha Mei na Juni 2016 hivyo wananchi wote watumie
fursa hii kwa kufika katika ofisi za Dawasco za kanda ili kupata huduma hiyo.
“Zoezi
hili la kugharamia  gharama za
uunganishaji huduma ya maji kwa wateja ni kwa kipindi maalum cha miezi miwili
tu ambacho ni Mei na Juni hivyo wananchi watumie fursa hii kujitokeza iliwaweze
kuunganishiwa na katika kipindi chote cha zoezi Ofisi za Dawasco zitakuwa wazi
kuanzia jumatatu hadi jumapili” alisema Luhemeja.
Hata
hivyo Dawasco imeeleza kuwa wananchi pamoja wateja wake wameweza kuwasiliana na
kituo  cha huduma kwa wateja kupitia
namba 022-2194800 au 0800110064 (bure) ili waweze kupata huduma na maelezo
zaidi kuhusiana na zoezi hilo la uunganishaji huduma ya Maji.

Rais Mstaafu JK akutana na waandishi wa habari kutoka Malaria No More

JKE1 
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani leo jijjini Dar es salaam, waandishi hao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
JKE2 
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani leo jijjini Dar es salaam, waandishi hao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa malaria. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya “Malaria No More” Martin Edlund.
JKE3 
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete akiongea na waandishi wa Habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani leo jijjini Dar es salaam, waandishi hao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana kutokomeza ugonjwa wa malaria.
JKE4 
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa Habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani leo jijjini Dar es salaam, waandishi hao wapo nchini kwa ziara ya siku tano kujionea namna Tanzania inavyopambana kutokomeza ugonjwa wa malaria.

TANZIA UK DIASPORA GLASGOW.

Tunasikitika kuwatangazia msiba wa Mtanzania mwenzetu 
Bi Mwasaburi Haji
kilichotokea Jumamosi jioni huko Glasgow Scotland.
 
Mipango ya mazishi inaendelea na mtajulishwa tarehe ya mazishi.
Msiba uko nyumbani kwa Marehemu
2/1, 105 Mcculloch St. Glasgow, G41 1NT.
 
Kwa wale mlioguswa mnaweza kutuma rambi rambi zenu kwenye account ya
ndugu wa marehemu 
A. AZIZ.
Nationwide.
Account No: 01491791
Sort code: 07 04 36.
Kwa mawasiliano zaidi mnaweza kumpigia ndugu wa Marehemu
A. AZIZ – 07411445644 Inna Lillahi wa Inna Ilayhi Rajiun.

No comments :

Post a Comment