Thursday, May 26, 2016

Mahakama ya Tanzania inakusudia kuongeza idadi ya Majaji katika kanda yake ya Mwanza chief-justice

chief-justice2 
Na Lydia Churi- Mwanza
Mahakama ya Tanzania inakusudia kuongeza idadi ya Majaji katika kanda yake ya Mwanza ili kuongeza msukumo wa kumaliza kesi za mauaji kutokana na kanda hiyo kuongoza kwa kuwa na kesi nyingi za mauaji nchi nzima.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za kimahakama katika kanda ya Mwanza, Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman amesema ataongeza idadi ya majaji katika kanda hiyo ili kesi hizo za mauaji zimalizike kwa wakati.
Jaji Mkuu pia ameiagiza Mahakama Kuu kanda ya Mwanza kuzipa msukumo maalum kesi za mauaji ili kuhakikisha zinamalizika mapema na kupunguza mlundikano wa kesi katika mahakama za Tanzania.
Awali akisoma taaarifa ya hali halisi ya kesi katika Mahakama Kuu kanda ya Mwanza, Jaji Mfawidhi wa kanda hiyo Mheshimiwa Robert Makaramba alisema kanda ya Mwanza ndiyo inayoongoza kwa kuwa na kesi nyingi za mauaji nchini ambapo hadi kufikia Aprili mwaka huu kuna jumla ya kesi 512 za mauaji.
Pamoja na mkakati wa Jaji Mkuu kuongeza idadi ya Majaji ili kumaliza kesi hizo, Jaji Mfawidhi wa kanda ya Mwanza alisema wameshachambua kesi hizo za mauaji ambapo Jaji Kiongozi pia aliahidi kuwaongezea jumla ya Majaji 11 ili waweze kusaidia kusukuma kesi hizo.
Jaji Makaramba alisema kati ya mwezi Juni na Julai jumla ya vikao 11 vinatarajiwa kukaa ili kusikiliza kesi 123 zilizopangwa kusikilizwa. Alisema kati ya kesi hizo, 35 ni zile zitakazosikilizwa kwa mara ya kwanza na kesi 88 ni zile zitakazosikilizwa mpaka mwisho.
Alisema endapo vikao hivyo vitafanyika kama ilivyokusudiwa vitasaidia kupunguza kesi zilizopo mahakamani kwa miaka mingi.
Hadi kufikia mwezi April mwaka huu, Mahakama Kuu kanda ya Mwanza ina jumla ya kesi 2771 za aina zote zikiwemo zile za Madai ya kawaida, Madai ya Ardhi na za jinai. Ili kuongeza kasi ya usikilizwaji wa kesi hizo, kila Jaji amepangiwa kusikiliza kesi 346. Kanda hiyo ina Majaji nane (8).
Jaji Mkuu wa Tanzania ameanza ziara katika kanda ya Mwanza inayohusisha mikoa ya Geita, Mwanza na Mara ambapo atakagua shughuli mbalimbali za kimahakama katika kanda hiyo.

Zawadi Azania Bank Kids Run zatajwa

 Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho la Riadhaa Tanzania (RT), Tullo Chambo
akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu mbio maalum za watoto zijulikanazo Azania Bank Kids Runzitakazofanyika juni 5 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini. Kushoto ni Ofisa MasokoMwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea na kulia ni mratibu wa mbio hizo, Wilhelm Gidabuday. (Na Mpiga Picha Wetu)
 
Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea, akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mbio maalum za watoto zijulikanazo Azania Bank Kids Run zitakazofanyika juni 5 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho la Riadhaa Tanzania (RT), Tullo Chambo.
………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
 
WADHAMINI wakuu wa Mbio za Watoto za Azania Bank Kids Run 2016, Benki ya
Azania, wametangaza zawadi za washindi wa mbio hizo zitakazofanyika viwanja vya
Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, Juni 5.
 
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Baraza la
Michezo la Taifa (BMT), Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea,
alisema benki yake inajisikia fahari kuwekeza katika mbio hizo za watoto.
 
Alizitaja zawadi za mbio za kilomita 5 kuwa ni Sh. 200,000 kwa mshindi wa
kwanza, Sh. 150,000 kwa mshindi wa pili na Sh. 100,000 kwa mshindi wa tatu,
wote wakitarajiwa pia kupata medali, begi lenye vifaa vya shule na vya michezo.
 
Jibrea alibainisha kuwa mshindi wa kwanza wa mbio za Kilomita 2
atajinyakulia Sh. 100,000, mshindi wa pili Sh. 75,000 na mshindi wa tatu Sh.
50,000, pamoja na medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo.
 
Katika mbio za Kilomita 1, Jibrea alitaja zawadi za washindi kuwa ni Sh.
75,000 kwa mshindi wa kwanza, Sh. 50,000 kwa mshindi wa pili na Sh. 40,000 kwa
mshindi wa tatu, ambao watapata zawadi ya ziada ya medali, begi lenye vifaa vya
shule na michezo.
 
“Pia washindi wa nne hadi wa 10 wa mbio hizo, watapata kifuta jasho cha Sh.
15,000, begi lenye vifaa vya shule na michezo. Nia ni kuwafanya watoto
watakaoshiriki kutotoka bure mwishoni mwa mashindano, na zawadi zote za fedha
taslimu tutawawekea kwenye akaunti tutakazowafungulia katika Benki ya Azania,”
alisema Jibrea.
 
Ofisa huyo alifichua kilichowasukuma Azania Bank kudhamini mbio hizo kuwa
ni kurejesha sehemu ya pato lake kwa jamii, lakini pia kuwa sehemu ya
kuiwezesha jamii kujenga kizazi imara kinachoshiriki michezo kwa ustawi wa
taifa.
 
Kwa upande wake Mratibu wa Azania Bank Kids Run 2016, Wilhelm Gidabuday,
aliishukuru Azania Bank kwa kukubali kusapoti mbio hizo, na kuongeza kwamba kwa
kuwa msingi wa michezo yote ni mbio, basi anaamini Azania imewekeza mahali
sahihi.
 
“Hakuna mchezo duniani usiohusisha mazoezi ya kukimbia ama usiohitaji
mshiriki kuwa na mbio, iwe soka, ngumi, tenisi, nk. Ndiyo kusema Azania
imefanya uamuzi sahihi na tunawaomba wazazi na walezi wawasajili watoto wao kwa
ada ya Sh. 2,000,” alisema.
 
Alibainisha kuwa fomu za ushiriki zinapatikana katika matawi ya Azania Bank
popote jijini Dar es Salaam, ofisi za Shirikisho la Riadha Tanzania (RT),
pamoja na Ofisi za BMT zilizoko Samora Avenue katikati ya jiji.

TBL GROUP YALIPA KODI SHILINGI BILIONI 81

tb1Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group ,Roberto Jarrin  akisisitiza jambo kwa  waandishi wa habari , wakati lipokuwa akitoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa kipindi cha mwaka jana na kutangaza mikakati ya  mwaka  huu,mkutano huo ulifanyika  makao makuu  ya kampuni  hiyo Ilala jijini Dar es Salaam leo Mei 26,2016.
tb2Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group ,Roberto Jarrin akisisitiza jambo kwa  waandishi wa habari , wakati lipokuwa akitoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa kipindi cha mwaka jana na kutangaza mikakati ya  mwaka  huu,mkutano huo ulifanyika  makao makuu  ya kampuni  hiyo Ilala jijini Dar es Salaam leo Mei 26,2016.
tb3 
Mwandishi wa gazeti la The East Africa Kidanka Christopher akiuliza swali kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group ,Roberto Jarrin  (hayupo pichani) kuhusiana na uzalishaji wa pombe za asili , wakati wa mkutano na wandishi wa habari wa kutoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa kipindi cha mwaka jana na kutangaza mikakati ya  mwaka  huu,mkutano huo ulifanyika  makao makuu  ya kampuni  hiyo Ilala jijini Dar es Salaam leo Mei 26,2016. \
tb4 
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliohudhuria katika mkutano wa TBL Group , wa kutoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni hiyo wakimsikiza kwa makini, Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group ,Roberto Jarrin (hayupo pichni) wakati wa mkutano huo ulifanyika  makao makuu  ya kampuni  hiyo Ilala jijini Dar es Salaam,  leo  Mei 26 2016.\
tb5 
Mtalamu wa upishi wa vinywaji wa TBL Group (Techincal Brewer) Emanuel Sawa akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya bia aina ya Castle Luger, jinsi inavyozalishwa wakati walipotembelea kiwanda hicho mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa  tathmini na waandishi hao
……………………………………………………………………………………………..
Kampuni ya TBL Group imelipa kodi ya mapato ya kiasi cha shilingi bilioni 81 katika kipindi cha mwaka 2015.
Akitoa  taarifa ya tathmini ya utendaji wa kampuni ya mwaka uliopita kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin pia amebainisha kuwa mbali na kampuni kulipa kiasi hicho cha kodi pia imekusanya kodi za serikali kiasi cha shilingi  bilioni165 ikiwa ni kodi ya mlaji (exercise duty) ,bilioni 114   ikiwa ni kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na bilioni 24 ikiwa ni malipo ya kodi nyinginezo ikiwemo kodi ya PAYE.
TBL Group ni kampuni inayoongoza  kulipa kodi nchini ikiwa imechagia pato la serikali kwa njia ya kodi kiasi cha shilingi Trilioni 2.3 katika kipindi cha miaka 10 “Kampuni yetu imechangia maendeleo ya taifa kwa njia ya kukusanya na kulipa kodi na mchango huo umekuwa ukitambuliwa na taasisi mbalimbali na kuitunukia tuzo ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo imeitunukia tuzo ya Mlipa kodi bora nchini kwa kipindi cha miaka mine mfululizo”.Alisema Jarrin.
TBL Group inajumuisha  makampuni ya- Tanzania Breweries Limited (TBL), Tanzania Distilleries Limited (TDL)  na  Dar Brew Limited.Biashara kuu ya kampuni ni kuzalisha na kuuza vinywaji ikiwemo bia za aina mbalimbali,vinywaji vikali na vinywaji vya asili.. 
Jarrin alibainisha hayo wakati akitoa ripoti ya utendaji wa kampuni katika kipindi cha mwaka 2015 na mikakati yake ya mbele katika kipindi cha mwaka 2016/17 kwa waandishi wa habari “TBL Group itaendelea kuunga jitihada za serikali zakukuza sekta ya viwanda nchini kwa kuendelea kujenga viwanda nchini na tangu kampuni hiyo ibinafsishwe mwaka 1994,imekuwa ikiendelea kuwekeza na tayari imewekeza Zaidi ya shilingi bilioni 150 kwa ajili ya kujenga viwanda vilivyokuwepo awali uwa vya kisasa Zaidi kuendana a teknolojia ya kisasa
Kampuni inavyo viwanda 10 nchini na miongoni wa viwanda vyake vilivyopo katika mikoa ya Mwanza,Mbeya na Dar es Salaam vimetunukiwa tuzo mfululizo za kuwa viwanda bora katika viwanda vinavyomilikiwa a kampuni mama ya SABMiller katika bara la Afrika.TBL Mwanza na Mbeya vikiwa katika kundi la viwanda 10 na 15 kwa ubora duniani.
Jarrin alisema biashara ya bia za kampuni ya TBL zinatawala soko kwa asilimia 78 nchini ikiwa inaongozwa na aina za bia za Safari, Kilimanjaro, Ndovu, Castle lager na Castle Lite .Pia kampuni inatengeneza  mvinyo na vinywaji vikali maarufu vinavyotamba kwenye soko kwa asilimia 73 ambavyo ni   – Konyagi, Valuer and Dodoma Wine –  Kwa upande wa vinywaji vya asili vinywaji vyake vinatawala soko kwa asilimia 8 ambavyo ni – Chibuku and Nzagamba –   Utafiti uliofanywa na taasisi ya CanBack kuhusiana na matumizi ya  pombe za asili nchini umebainisha kuwa matumizi ya pombe za asili nchini ni asilimia 50%
 Jarrin aliendelea kueleza kuwa TBL Group inaendelea kutoa mchango wa kukuza uchumi wa taifa kupitia katika sekta ya uuzaji vinywaji ambayo imetoa ajira zaidi ya milioni 2 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja zinazoendelea kuwanufaisha watanzania wa kada mbalimbali.Kwa upande wa sekta ya kilimo wakulima wa zao la Shahiri Zaidi ya 3000 wamenufaika kupitia mpango wa kushirikiana na kampuni.Katika kipindi cha mwaka 2015 mpango huu umewezesha ongezeko la uzalishaji wa zao hilo kufikia tani 15,574 kiasi ambacho kimevuka lengo la matumizi na mahitaji ya kampuni.
Pia imebainishwa kuwa zaidi ya wakulima 700 wananufaika na mpango wa kiwanda cha TDL wa kushirikiana nao atika kilimo cha zabibu kinachoendeshwa katika vijiji vya  Bihawana, Mpunguzi,, Mvumi, Hombolo, Mbabala, Veyula, Makang’wa, Mzakwe na Mbalawala .Chini ya mpango huo wakulima wanawezeshwa kupatiwa utaalamu wa kilimo kwa kushirikiana na taasisi ya Makutupora Viticulture Training and Research Center (MVTRC). Pia chini ya mpango huu watoto wa wakulima wa zao la zabibu wamekuwa wakisaidiwa kielimu kupitia  mfuko unaojulikana kama Zabibu na Shule Kwanza.
Jarrin pia alibainisha kuwa kampuni ya DarBrew imeweza kuleta mapinduzi ya uuzaji wa pombe za asili nchini kwa kuwawezesha watumiaji kupata kinywaji cha Chibuku na Nzagamba kikiwa kimefungwa kwa viwango mbalimbali na  katika mazingira ya usafi yanayolinda afya za watumiaji na hivi sasa imekuja na mkakati wa kuwainua akina mama kimapato kupitia kuuza bidhaa zake unaojulikana kama Chibuku Mamas ambao hadi kufikia sasa wanawake wapatao 130 wameishajiunga na mpango huu.
Kuhusu mtazamo wake wa hali ya biashara ya kampuni kwa sasa Jarrin alisema sekta ya uuzaji wa vinywaji inakabiliwa na changamoto mbalimbali mojawapo ni bei kubwa ya bia ambayo watumiaji wake wengi wanashindwa kuimudu,kuwepo na vinywaji visivyo katika mfumo rasmi wa ushindani katika soko,kukosekana kwa motisha katika uzalishaji wa malighafi za kutengeneza vinywaji nchini kwa kuwa zinatozwa kodi kubwa ya zuio kuliko malighafi zinazotolewa nje ya nchi.
Alisema baadhi ya mambo yanayostahili kufanyika katika uboreshaji wa sekta ili iendelee kuchangia pato la taifa ni kupunguza  kodi za malighafi zinazozalishwa nchini kama kimea kinachotumika kutengeneza bia pia kulasimisha pombe za asili  ziende sambamba na vinywaji vya sili vinavyolipiwa kodi na kuhakikisha  vinywaji vya asili vinapatikana katika mazingira ya usafi “Pamoja na changamoto nyingi zilizopo katika sekta hii tunaendelea kukabiliana nazo na tumedhihirisha uwezo wetu kwa kuwa na viwanda vyenye ubora wa hali ya juu nchini Tanzania”Alisema Jarrin

MISS TANZANIA USA AEESHA KAMARA ATEMBELEA HIGHLAND NURSERY SCHOOL, TABATA, JIJINI DAR

Miss Tanzania USA Pageant Aeesha Kamara akigawa penseli, vikiwemo vitabu, mabegi ya kubebea vitabu na vitu vingine mahitaji ya shule hiyo ya vidudu ya Highland Nursery school iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam. Vitu hivyo vilitolewa msaada na wadau kutoka Washington, DC.
Miss Tanzania USA Pageant, Aeesha Kamara akigawa mabegi ya kubebea vitabu kwa watoto wa Highland Nursery School ya Tabata jijini Dar es Salaam,
Miss Tanzania USA Pageant akiongea na watoto hao wa shule ya Highland Nursery School ya Tabata jijini Dar es Salaam.
Miss Tanzania USA Pageant Aeesha Kamara akiwa katika picha ya pamoja na watoto wa Highalnd Nursery school wakiwemo walimu wao.
 Watoto wakimsikiliza Miss Tanzania USA Pageant Aeesha Kamara (hayupo pichani) alipokua akiongea nao.
Watoto wakitega sikio kwa makini kumsikiliza Miss Tanzania USA Pageant Aeesha Kamara (hatyupo pichani) alipokua akiongea nao,

MAMIA WAJITOKEZA KUMUAGA MWANAHABARI MAKONGORO OGING’ KUZIKWA MKOANI MARA KESHO KUTWA.

 Picha ya Mwanahabari Makongoro Oging’ enzi za uwai wake.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers alikokuwa akifanyia kazi Makongoro Oging’, Eric Shigongo akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye lenye mwili wa marehemu Oging’ wakati wa kuagwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ilala ya Amana Dar es Salaam mchana wa leo.
 Mmiliki wa Blog ya Michuzi, Issa Michuzi akitoa heshima za kwa mwili wa marehemu.
 Mhariri wa Habari wa Gazeti la Champion, Salehe Ali akitoa heshima za mwisho kwa marehemu.
 Waombolezaji wakiwa na huzuni wakati wa kuaga mwili wa mpendwa wao Makongoro.
 Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV. Samu Mahela akitoa heshima za mwisho.
 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri wa Habari Tanzania (TEF), Absalom Kibanda akiwa kwenye shughuli hiyo ya kumuaga Makongoro Oging’
 Ndugu yake na Makongoro Oging’ akilia wakati wa kumuaga mpendwa wake Makongoro.
 Ndugu jamaa na marafiki wakiwa kwenye uagaji wa mpendwa wao.
 Uagaji ukiendelea.
 Mtoto wa marehemu akimuaga baba yake ‘hakika ni huzuni kubwa’
 Majane wa marehemu akiwa hajiwezi baada ya kumuaga mume wake.
 Mhariri wa habari wa gazeti la Uwazi alilokuwa akiandia marehemu Oging’ Elvan Stambuli akilia kwa uchungu wakati wa kumuaga Makongoro.
 Baba mlezi wa Makongoro Oging ambaye alimsomesha, akizungumza na wanahabari.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Makongoro kulipeleka kwenye gari kabla ya kuanza kwa safari ya kwenda mkoani Mara.
Jeneza likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari.

Temeke yapiga marufuku ufanyaji wa mazoezi barabara kuu

Manispaa ya Temeke    
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
   Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imepiga marufuku vikundi vya mazoezi vinavyofanya mazoezi kwenye      barabara kuu ya uwanja wa Taifa ili kuzuia foleni na ajali za barabarani.
Tamko hilo limetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Afisa Habari wa Halmashauri hiyo, Joyce Msumba alipokua akitoa ufafanuzi juu ya malalamiko ya wananchi kuhusu foleni ya magari inayosababishwa na wachezaji wanaotumia barabara kuu ya Temeke kuelekea uwanja wa Taifa.
“Halmashauri yetu imepiga marufuku wachezaji wote wanaokimbia kuelekea uwanja wa Taifa kupitia barabara kuu na badala yake wanatakiwa kutumia njia za waendao kwa miguu (service road) zilizopo pembezoni mwa barabara kuu”,alisema Joyce.
Joyce aliongeza kuwa kila kundi la wachezaji  wana viongozi wao ambao walishapewa maelekezo na Halmashauri juu ya suala hilo kwahiyo,viongozi hao wana wajibu wa kuwasimamia wanamichezo wao.
Kwa upande wake Afisa Utamaduni wa Halmashauri hiyo, Emmanuel Ndumukwa amewaomba wanamichezo hao kuzingatia sheria za barabarani ili kuepusha ajali.
“Mara nyingi tunawaeleza wanamichezo wazingatie sana sheria za barabarani pamoja na kutumia bendera nyekundu kama alama ya kuashiria uwepo wao katika barabara ili kuzuia ajali”,alisema Ndumukwa.

Makandarasi 4572 wafutiwa leseni nchini

mg5 
Bodi ya Usajili wa Makandarasi imefuta usajili wa jumla ya makandarasi 4572 kwa kushindwa kutimiza matakwa ya Sheria ya Usajili wa Makandarasi ya mwaka 1997.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Bw. Rhoben Nkhori wakati wa Mkutano wa Mashauriano wa CRB uliofanyika jijini Dar es Salaam na kufunguliwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Bw. Nkhori amesema kuwa katika jukumu la kuratibu mwenendo wa kazi za makandarasi, Bodi ilikagua miradi 2735. Katika miradi hiyo iliyokaguliwa, miradi 1873 sawa na asilimia 68.5 haikuwa na kasoro.
Ameongeza kuwa miradi mingine ilikuwa na kasoro za kutofanywa na makandarasi waliosajiliwa, kutozingatia usalama wa wafanyakazi, kutokuwa na bango wala uzio na miradi kutosajiliwa. Kwa mujibu wa Bw. Nkhori miradi yote iliyopatikana na upungufu wahusika walichukuliwa hatua mbali mbali kwa mujibu wa sheria.
Aidha, Bwana Nkhori amesema kuwa kwa mwaka jana, Bodi ilisajili miradi 3,172 yenye thamani ya shilingi trilioni4.23. Katika miradi hii asilimia 44.4 ilifanywa na Makandarasi wazawa na asilimia 55.6 ilifanywa na makandarasi wa kigeni.
Licha ya mafanikio hayo CRD ilikumbana changamoto kadhaa ikiwemo kuwasilisha nyaraka za kugushi wakati wa usajili hususani kadi za magari na mitambo, vyeti vya wataalam, kutumia majina ya makandarasi kwa udanganyifu kwa kuuza vibao, waendelezaji kutotoa taarifa sahihi za umiliki kwa Bodi na baadhi ya makandarasi kushindwa kuwalipa wafanyakazi na vifaa vya ujenzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi, Bi Consolata Ngimbwa amemwomba Mhe. Rais John Pombe Magufuli kuwapa kipaumbele Makandarasi wa humu nchini ili kuwawezesha kiuchumi. “Mhe. Rais tunaomba utupe kipaumbele kwani sisi tukipata hiyo miradi tutawekeza hapa nchi na kuongeza soko la ajira,”alisema Bi Ngimbwa.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema serikali yake itawapa kipaumbele makandarasi wazawa lakini akawataka wajipange na kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili ikiwemo kujiepusha na vitendo vya rushwa.
Mkutano huu pamoja na mamabo mengine utajadili jinsi ya kuwajengea uwezo makandarasi nchini. Kauli mbiu ya Mkutano huo ni “Juhudi za Makusudi za kukuza uwezo wa makandarasi wazawa, changamoto na mustakhabali.”

Dawati la malalamiko kufanya kazi masaa 24 hospitali ya Mwananyamala.

KIJ1 
Katibu Mkuu kiongozi Dkt. John Kijazi katikati akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani katika hafla fupi ya kupokea msaada wa magodoro 50 kutoka kwa Umoja wa Makanisa ya pentekoste  iliyofanyika katika hospitali ya Mwananyamala wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi na wa kwanza kushoto ni katibu Tawala wa Mkoa Bi. Theresia Mbando.
KIJ3 
Katibu Mkuu kiongozi Dkt. John Kijazi katikati akiongozana na  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi na wa kwanza kulia na wa kwanza kushoto ni  katibu Tawala wa Mkoa Bi. Theresia Mbando kuelekea wodini kusalimia wagonjwa wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada wa magodoro 50 kutoka kwa Umoja wa Makanisa ya pentekoste  iliyofanyika katika hospitali ya Mwananyamala .
KIJ4 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi wa kwanza kushoto akimsikiliza mmoja wa wagonjwa wanaotibiwa katika hospitali ya Mwananyamala  akitoa kero zake kuhusu hospitali hiyo wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada wa magodoro 50 kutoka kwa Umoja wa Makanisa ya pentekoste  iliyofanyika katika hospitalini hapo.
KIJ5 
Wananchi wakitoa malalamiko yao  kuhusu huduma zinzotolewa Hospitali ya Mwananyamala mbele ya  Katibu Mkuu kiongozi Dkt. John Kijazi na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi hawapo pichani wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada wa magodoro 50 kutoka kwa Umoja wa Makanisa ya pentekoste  iliyofanyika katika hospitalini hapo.
KIJ6 
Wananchi wakitoa malalamiko yao  kuhusu huduma zinzotolewa Hospitali ya Mwananyamala mbele ya  Katibu Mkuu kiongozi Dkt. John Kijazi na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi hawapo pichani wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada wa magodoro 50 kutoka kwa Umoja wa Makanisa ya pentekoste  iliyofanyika katika hospitalini hapo.
KIJ7 
Baadhi ya magodoro yaliyopokelewa hospitalini hapo.
……………………………………………………………………………………………..
Na Ally Daud-maelezo
Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. John Kijazi ameutaka uongozi wa hospitali ya Mwananyamala kuhakikisha kuwa dawati la malalamiko kwa wagonjwa linafanya kazi masaa 24 ili  kuboresha huduma katika hospitali hiyo.
Akizungumza katika hafla ya kupokea msaada wa magodoro Dkt. Kijazi amesema kuwa wagonjwa wanatakiwa kuhudumiwa kwa wakati na kusikilizwa malalamiko yao muda wote wanapopatwa na changamoto hospitalini hapo ili kuweza kuboresha huduma kwa watanzania.
“Nimepata malalamiko kutoka kwa wananchi ambao walipata matatizo usiku wa kuamkia leo na hakukuwa na mtu wa kuwasikiliza kwa  wakati na kushindwa kupata huduma bora walipokuwa na shida hivyo naagiza uongozi kuhakikisha dawati la malalamiko kufanya kazi masaa 24 ili kuondoa kero za Wagonjwa wote”.alisema Dkt Kijazi.
Aidha Dkt. Kijazi ameushukuru uongozi wa Umoja wa Makanisa ya Pentekoste kwa kutoa msaada wa magodoro 50 yenye thamani ya shilingi milioni 1.631 ili kuendeleza huduma bora kwa wagonjwa wa Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.
Akipokea msaada huo Dkt. Kijazi  alisema kuwa anawaomba viongozi wa Umoja huo na taasisi zingineziendelee na moyo wa  kuchangia kwenye shughuli za kijamii kadriwanavyoweza ili kuifikisha Tanzania salama katika kilele cha mafanikio.
“Nawaomba Umoja wenu, taasisi na wadhamini mbalimbali kuweza kusaidia kuinua na kukuza huduma bora za kijamii ikiwemo mahospitalini ili kusaidia serikali kupiga hatua katika kupambana na changamoto ya vifaa zinazoikabili hospitali ya Mwananyamala” aliongeza Dkt. Kijazi.
Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi amesema kuwa ana Imani na Serikali ya awamu ya tano katika kutatua kero za wananchi hususani katika Wilaya yake kwani ameshaona mfano wa kupokea msaada huo na kuungwa mkono na Katibu Mkuu Dkt. John Kijazi kwa kushirikiana vizuri kwenye shughuli hiyo.
“Nafurahi kukutana na kushirikiana  kwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi katika shughuli za kijamii hususani katika hili la kuendeleza huduma bora zitolewazo na hospitali ya Mwananyamala ili kuifikisha mbali Tanzania mpya” alisema Bw. Hapi.

TIGO YAMDHAMINI MWANAMUZIKI BEN POL KUBURUDISHA TAMASHA LA NYAMA CHOMA

 Mkuu wa Kitengo cha Burudani na Digitali wa Tigo, Paulina Shao (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu tamasha la nyama choma litakalofanyika  Viwanja vya Leaders kesho kutwa Jumamosi Mei 28, 2016 jijini Dar es Salaam, ambapo mwanamuziki Ben Pol atatoa burudani kwa udhamini wa kampuni ya Tigo. Kulia ni Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo, Carol Ndosi na katikati ni mwanamuziki Ben Pol.
 Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo, Carol Ndosi (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
 Mwanamuziki, Ben Pol (katikati), akizungumza katika mkutano huo.
 Mtaalamu wa Kidigitali, Samira Baamar (kushoto), akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
………………………………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
 
Kampuni inayooongoza kwa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imekubali kumdhamini mwanamuziki nguli na mtunzi wa nyimbo za muziki, Bernard Michael Paul Mnyang’anga, maarufu kama ‘Ben Pol’ kuburudisha katika tamasha la mwaka huu la Nyama Choma.
 
 Tamasha hilo ambalo linafanyika kwa mwaka wa tano sasa ni moja ya tamasha maarufu linalovutia watu wengi kutoka maeneo yote ya Dar es Salaam litafanyika kwenye viwanja vya Leaders Jumamosi Mei 28, 2016. 
 Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Mkuu wa Tigo wa masuala ya Dijitali Paulina Shao  alisema kuwa  kumuunga mkono Ben Pol kunaonesha  kuendelea kujikita kwa Tigo katika  kuwekeza katika kusaidia  sekta ya muziki ya ndani kwa kuhakikisha  wasanii  wanawezeshwa  kufikia viwango vya juu katika kazi zao.
“Kama kampuni ya maisha ya kidijitali, Tigo inatambua  mchango muhimu wa wasanii wa Tanzania  wanaoutoa katika sekta ya burudani. 
 
Hii ndio maana  tumewekeza kwa kiwango kikubwa  kuwasaidia wasanii  hususani wanamuziki  wa ndani katika kuhakikisha wanafahamika katika masoko ndani ya nchi, kikanda na kimataifa kwa kutumia majukwaa ya kidijitali yanayokuwepo na kushiriki  matukio mbalimbali  na hivyo kuongeza  mauzo ya  muziki wao  pamoja na nembo zao,” alisema Shao.
Aidha akiishukuru Tigo kwa uungwaji mkono huo, Ben Pol  aliisifu Tigo kwa juhudi  inazofanya bila kuchoka  katika kukuza  ukuaji wa  sekta ya muziki wa ndani  kupitia Jukwaa la Muziki  la Tigo.
“Ninaishukuru sana Tigo  kwa uungwaji mkono ambao ni muendelezo wa mtiririko wa  programu ambazo imezianzisha  ili kuinua maisha ya wasanii wachanga wa Tanzania,” alisema Ben Pol na kutoa changamoto kwa wasanii wanaoibukia kuwa wasione aibu  kuomba msaada  kutoka kwa mashirika kama Tigo.
 
Nguli huyo wa muziki wa Bongo Flava  kwa hivi sasa anatamba na  kibao ‘MoyoMashine’ ambayo aliitoka hivi karibuni.
Ben Pol ni miongoni mwa wasanii  wanaonufaika na jukwaa la Muziki la Tigo  ambalo lilianzishwa mwaka 2015 likiwa na lengo la  kuiunga mkono sekta ya muziki Tanzania  kwa kuwasaidia wasanii wa ndani  kupata kipato zaidi kutokana na mauzo ya  kazi zao  na kuwawezesha kufahamika katika masoko ya kimataifa  kupitia majukwaa hayo ya kidijitali  kama vile Music portal na Deezer, ambayo ni majukwaa ya kimataifa yaliyo kwenye mtandao yakiwa na  nyimbo kutoka sehemu mbalimbali  duniani  zaidi ya  milioni 36.

SERIKALI YAANDAA MPANGO KABAMBE WA MIPANGO MIJI (MASTER PLANS) ILI KUONDOA MIGOGORO YA ARDHI

Na Fatma Salum-MAELEZO, Dodoma.index
Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaandaa Mpango Kabambe wa Mipango Miji (Master Plan) utakaoainisha matumizi bora ya ardhi na kuondoa migogoro ya ardhi nchini.
Kauli hiyo ilitolewa jana Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Mhe. Angelina Mabula  wakati akijibu maswali ya wabunge kuhusu mpango wa Serikali kumaliza migogoro ya ardhi kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Mhe. Mabula alieleza kuwa Wizara yake inashirikiana na  Halmashauri za Wilaya na Miji 18 kwenye program ya Urban Local Government Supporting Programme (ULGSP) katika kuandaa Mipango Miji hiyo.
Pia Mhe. Mabula alibainisha kuwa Wizara inaandaa na kukamilisha programu ya kupanga, kupima na kumilikisha kila kipande cha ardhi Tanzania itakayotekelezwa kwa kipindi cha miaka kumi kuanzia 2015 hadi 2025.
“Serikali imekuwa ikiziagiza Halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya upimaji kwa kuwa inatambua umuhimu wa kupima viwanja na mashamba ili kuwa na matumizi bora ya ardhi yetu” alisema Mabula.
Aidha, Mabula aliongeza kuwa Serikali kupitia Mradi wa Benki ya Dunia ipo katika mchakato wa kununua vifaa vya upimaji ambavyo vitasambazwa katika kanda 8 za Wizara ya Ardhi ili Halmashauri zote zilizopo ndani ya kanda hizo ziweze kunufaika.
Alieleza kuwa makadirio ya awali ya gharama za mradi huo ni Dola za Kimarekani Milioni 4 ambapo Dola Milioni 2 zitatumika kwenye upimaji na Dola Milioni 2 zitatumika kwa ajili ya ununuzi wa Vifaa.
Katika kupunguza na kutatua migogoro ya ardhi iliyopo sasa, Mabula alisema kuwa Wizara ya Ardhi imeandaa kitabu cha orodha ya migogoro nchi nzima kinachoainisha vyanzo vya migogoro hiyo ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
Hali kadhalika, Mabula alisema kuwa Wizara imesambaza Sera na Sheria za Ardhi hasa kwenye maeneo yenye migogoro, wameimairisha mfumo wa kielektroniki  katika kutunza kumbukumbu, na kuboresha ofisi za Kanda ili kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi.

44 WAMEBAKI KWENYE MCHUJO

Clinic_Wall2
Clinic_Wall3
Akizungumza na mbeyacityfc.com, mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya leo (Clinic day 5) kwenye uwanja wa Sokoine kocha msaidizi wa City, Mohamed Kijuso amesema kuwa Vijana 44 wamefanikiwa kuvuka  kwenye mchujo wa kwanza  hivyo wataingia kwenye wamu ya pili inayotaraji kuanza hapo kesho kwenye uwanja wa Sokoine.
“Tulikuwa na kundi kubwa la wachezaji zaidi ya 106, baada ya mchujo leo, tumefanikiwa kupata  44 ambao wataingia kwenye awamu ya pili hapo kesho,  lengo letu ni kuona tunapata Cream nzuri kwa ajili ya timu yetu ya vijana na pia  wachezaji saba ambao watakuwa tayari kucheza kwenye timu kubwa msimu ujao”, alisema. 
Kuhusu lini itakuwa siku ya mwisho, kocha huyo kijana alitanabaisha kuwa, mchakato huu wa kuska vipaji ulikuwa ufikie tamati hapo kesho lakini uongozi wa City umeamua kusogeza mbele mpaka siku ya jumamosi  ambapo wachezaji watakaopatikana kwenye mchujo wa kesho  watapata nafasi ya kucheza mchezo mmoja wa  kirafiki na timu ya  Ilemi Fc.
“Ilikuwa tuhitimishe kesho lakini tumesogeza mpaka jumamosi ambapo vijana wetu wapya watakaopatikana watacheza mchezo wa kirafiki , na baada ya hapo zoezi litafungwa tayari wa kusubiri maandalizi ya msimu mapema mwezi ujao” alimaliza.

TTCL YAZINDUA NEMBO MPYA NA HUDUMA YA 4G LTE

FO1 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), na wadau wa Sekta ya Mawasiliano (hawapo pichani), wakati uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo na huduma ya 4G LTE jijini Dar es Salaam.
FO2 
Mjumbe wa Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bi. Edwina Lupembe akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, katika hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo na huduma ya 4G LTE
FO3 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dkt. Kamugisha Kazaura akielezea mafanikio ya TTCL kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), katika hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo na huduma ya 4G LTE jijini Dar es Salaam.
FO4 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizindua nembo mpya ya Kampuni ya Simu ya Tanzania (TTCL), jijini Dar es Salam.
FO5 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dkt. Kamugisha Kazaura, wakati wa halfla ya uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo na huduma ya 4G LTE jijini Dar es Salaam.
FO6 
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), wakifatilia sherehe za uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo na huduma ya 4G LTE jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………………………
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya (TTCL), kuwa wabunifu ili kuhimili ushindani wa soko katika sekta ya mawasiliano na hivyo kuiwezesha kampuni hiyo kupata faida.
Akizungumza wakati akizindua nembo mpya ya kampuni ya TTCL na huduma ya 4G LTE inayowezesha huduma ya mawasiliano ya sauti na data kwa haraka Prof. Mbarawa amesema huu ni wakati wa kubadili mtazamo na kufanya kazi kisasa ili kuvutia wananchi kutumia huduma za TTCL.
“TTCL lazima mubadilike ili muweze kuendana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia na hivyo kumudu ushindani uliopo sasa katika sekta ya mawasiliano”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Amewataka TTCL kuhakikisha kituo mahiri cha kutunzia taarifa (Data Centre), kinaanza mapema mwezi Juni ili kuwezesha wadau wengi kunufaika na kituo hicho.
Prof. Mbarawa amesema Serikali inaunga mkono TTCL na imetenga masafa ya 800 MHZ ambayo yataiwezesha TTCL kushindana na makampuni mengine ya watoa huduma ya mawasiliano na kuwaunganisha wateja wengi kutumia huduma za mawasiliano na data.
“Uzinduzi wa nembo mpya ya TTCL na huduma ya masafa ya 4G LTE uendane na ubunifu kwa wafanyakazi ili muwavutie watumiaji wengi wa simu na hivyo kupata soko kubwa na kuifanya TTCL kuchangia kikamilifu pato la taifa”, amesisitiza Waziri Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesema mawasiliano ni kiungo muhimu cha kufanikisha ukuaji wa sekta za kilimo, taasisi za fedha, uwekezaji, ujasiliamali na utendaji kazi wa Serikali na sekta binafsi hivyo ubunifu katika utendaji utaiwezesha TTCL mpya kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amewataka wananchi kuzingatia maelekezo wanayopatiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuhusu namna ya kuzitambua simu na vifaa feki na hatua za kufuata ili ifikapo Juni 16 zoezi la kuzifunga simu feki litakapotekelezwa wasiathirike.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Bi. Edwina Lupembe amesisitiza kwamba TTCL imejipanga kuboresha huduma za fedha ili kuwezesha watumiaji wengi wa kampuni hiyo kunufaika na huduma ya kutuma na kupokea fedha.
“Tumekamilisha mradi mkubwa wa kusimika mitambo ya GSM, UMTS na LTE ambayo itakuwa na uwezo wa kutoa huduma ya mawasiliano 2G, 3G na 4G”, amesema Bi. Lupembe
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa mabadiliko ya muonekano wa TTCL yataendana na mtazamo mpya wa wafanyakazi wenye lengo la kuiwezesha kampuni hiyo kuwa ya kisasa hapa nchini.
Amesema TTCL imejipanga kuboresha simu za mezani, mkononi, na huduma za intaneti ya haraka ili iweze kupata wateja wengi na hivyo kuongeza mapato yake.
“Teknolojia ya 2G GSM, 3G UMTS na LTE imeongeza nguvu kwa kampuni yetu kuleta ushindani katika soko la mawasiliano na zitaendelea kuongeza ufanisi na ubunifu wa huduma zetu kwa bei nafuu”, amesisitiza Dkt. Kazaura.
Tayari huduma ya 4G LTE inapatikana katika maeneo mengi ya Ilala, Temeke na Kinondoni jijini Dar es Salaam.

RaisDk. John Pombe Magufuli akemea vitendo vya Rushwa kwa wakandarasi

MF01 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wakandarasi, Wahandisi na wadau mbalimbali wa sekta ya Ujenzi kabla ya kufungua rasmi Mkutano  wa Siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini CRB uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
MF1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipewa maelezo kuhusu katapila linalotumika katika kazi mbalimbali za ujenzi mara baada ya kufungua mkutano wa siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi jijini Dar es Salaam
MF2 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati akikagua baadhi ya mitambo na magari mbalimbali katika maonesho ya vifaa hivyo vinavyotumika katika sekta ya ujenzi.
MF3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati akikagua baadhi ya mitambo na magari mbalimbali katika maonesho ya vifaa hivyo vinavyotumika katika sekta ya ujenzi.
MF4 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia vifaa vya ujenzi katika moja ya mabanda mara baada ya kufungua mkutano wa siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi jijini Dar es Salaam.
MF5 
Wadau mbalimbali wa Sekta ya Ujenzi wakiwemo Wahandisi na Wakandarasi wakipiga makofi wakati wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano huo wa Mashauriano wa CRB jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
………………………………………………………………………………………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli amewataka wakandarasi nchini kujiepusha na vitendo vya rushwa ili kulisaidia Taifa kupiga hatua ya kimaendeleo.
Mhe. Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akifungua Mkutano wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini (CRB) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
“Mnaweka viwango vikubwa vya fedha kwenye miradi ili muweze kupata fedha ya kutoa rushwa, kwa nini mnafanya hivyo?”amewauliza Mhe. Rais Magufuli na kuwambia kuwa kama wapo watumishi wa serikali wanaowaomba rushwa ili wapate kazi waitaarifu Takukuru mara moja ili wachukuliwe hatua.
Mhe. Rais amewataka wakandarasi wazawa wajipange kufanya kazi na kuwaonya wasiwe wanaweka viwango vikubwa ambavyo vinachangia kuwakosesha zabuni.
 Akitoa mfano, Mhe. Magufuli alisema katika ujenzi wa mahakama za mwanzo hapa nchini, jengo moja lilikadiriwa kukamilika kwa milioni 200 lakini wakandarasi wa Tanzania walioomba zabuni hiyo walitoa kiwango cha kati ya shilimgi milioni  670 na bilioni 1.4. Amesema kwa jinsi hii hata mtu awe na huruma ya namna gani hawezi kuwapa kazi.
Amesema serikali yake itawajali kwanza wakandarasi wa hapa nchini lakini akawataka wajipange na pengine waungane ili kufanya kazi kwa pamoja.
Aidha, Mhe. Rais amesema ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Tanzania unakaribia kuanza lakini akauliza wakandarasi wa hapa nchini wamejipangaje katika kushiriki ujenzi huo.
Kuhusu ulipaji wa madeni ya wakandarasi, Mhe Rais amesema, serikali yake imekuwa ikilipa madeni hayo na itaendelea kufanya hivyo hadi deni litakapoisha. Amesema kwa kuanza serikali imelipa bilioni 650 na baadaye ikatumia bilioni 462 kutoka Mfuko wa Barabara kuwalipa wakandarasi.
Amesema wakandarasi ni watu wa muhimu sana katika maendeleo ya Taifa na ni injini ya maendeleo kwani wako kila sekta ya maendelo. Amesema kwa mfano  wako katika ujenzi wa mioundombinu, kwenye zana za kilimo,kwenye  uvuvi, na pia usafirishaji wakandarasi hawakosekani.

MATUKIO YA BUNGE LEO MJINI DODOMA 26/5/2016.

BU1 
Kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kikiendelea leo mjini Dodoma.
BU2 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson akifuatilia kwa makini michango ya wabunge wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu ndani ya Bunge mjini Dodoma.
BU4 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angela Kairuki akifuatilia jambo ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.
BU3 
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari wakifuatilia kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.
BU5 
Waziri wa Elimu,Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akijadiliana jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde bungeni mjini Dodoma.
BU6 
Waziri wa Elimu,Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi , Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kwa mwaka 20016/2017 mjini Dodoma. Wizara hiyo katika mwaka wa fedha 2016/2017 imeomba kupitishiwa shilingi Bilioni 1.39 . Picha/Aron Msigwa-MAELEZO.

Serikali yawapa miezi miwili waishio kijjiji cha michezo Changamani kuhama.

CH1 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akitoa agizo la kuhama kwa wananchi wa eneo la changamani Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam(Hawapo Pichani) kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha Michezo.
CH2 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akisistiza jambo mbele ya wajumbe wa kikao kati ya Serikali na wananchi wa eneo la changamani Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam katika kikao cha kujadilina kuhusu wananchi hao kuhama eneo hilo kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha Michezo.
CH3 
Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius Mgaya akichangia hoja katika kikao kati ya Serikali na wananchi wa eneo la changamani Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam katika kikao cha kujadilina kuhusu wananchi hao kuhama eneo hilo kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha Michezo.
CH4Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw.Mafuku Rajabu akifafanua jambo katika kikao kati ya Serikali na wananchi wa eneo la changamani Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam katika kikao cha kujadilina kuhusu wananchi hao kuhama eneo hilo kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha Michezo.
CH5 
Eneo la Changamani kijiji cha Michezo ambalo wananchi wake wanatakiwa kuhama ndani ya miezi miwili kupisha uendelezwaji wa eneo hilo kwa ajili ya michezo mbalimbali.
Picha na Raymond Mushumbusi WHUSM
………………………………………………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi WHSUM.
Serikali imewapa miezi miwili wananchi waishio katika kijiji cha michezo cha Changamani kilichopo Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam  kuhama katika eneo hilo kupisha uendelezwaji wa kijiji cha mchezo.
Agizo hilo limetolewa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge alipokutana na wananchi hao katika kikao cha kujadili na kukubaliana muda wa kuhama katika eneo hilo leo Jijini Dar es Salaam.
“Ndugu zangu tumejadiliana wote na kukubaliana kuwa baada ya miezi miwili mtakuwa mmeshaama katika eneo hilo kupisha uendelezwaji wa kijiji cha michezo kwa ajili ya shughuli za mbalimbali za michezo” alisisitiza Bw. Nkenyenge.
Naye Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw.Julius Mgaya amesema kuwa mpango wa kuwahamisha wananchi hao unalenga kutekeleza mradi wa kijiji cha michezo kitakachojengwa kwa ajili ya kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo mbalimbali.
Kwa upande wake mmoja ya wawakilishi wa wananchi hao Bw.Atillio Mballa amesema wamekubaliana na muda huo waliopewa na watafikisha ujumbe huo kwa wenzao na kabla ya muda hujafika watakuwa wameshatekeleza agizo hilo.
Katika mpango wa kukuza na kuendeleza michezo nchini Serikali imejipanga kukuza sekta ya michezo nchini na kuifanya kuwa moja ya rasilimali itakayochangia katika pato la taifa.

TAARIFA KUTOKA TFF

tff_LOGO1
CAF YAMTEUA MICHAEL WAMBUR
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limemteua Michael Richard Wambura kuwa Kamishna wa mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Rwanda na Msumbiji unaotarajiwa kufanyika jijini Kigali, Juni 3, 2016.
Wambura ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), atakuwa Balozi mzuri katika mchezo huo unaokutanisha timu ambazo nchi imepana nazo. Msumbiji iko Kusini mwa Tanzania wakati Rwanda iko Magharibi mwa Tanzania.
TAIFA STARS KWENDA KENYA KESHO
Kikosi cha timu ya soka ya Tanzania – Taifa Stars, chini ya makocha Charles Boniface Mkwasa na Hemed Morocco kinatarajiwa kuondoka kesho saa 12.00 alfajiri kwenda Nairobi, Kenya kucheza na Harambee Stars katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa
Mchezo huo ni maandalizi ya kujiandaa kucheza Misri Juni 4, 2016 katika mchezo wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2017) wakati Kenya pia itakuwa na mchezo dhidi ya Congo.

TANZANIA KUTOANDAA CECAFA CUP

tff_LOGO1 
Shirikisho a Soka Tanzana (TFF), limetangaza kutoandaa michuano ya kuwania Kombe la timu za nchi wanachama wa Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), maarufu kama Kombe la Kagame kwa mwaka 2016 kama ilivyopendekezwa.
Sababu za TFF ya kutoandaa fainali hizo ni kwa kubanwa na ratiba ya michuano ya kitaifa na kimataifa
Awali mkutano mkuu wa CECAFA, uliamua Zanzibar iwe mwenyeji wa michuano ya Kagam
Baadaye kwa sababu zilizo nje ya uwezo wa ilionekana Zanzibar hawataweza kufanya
Baada ya hapo TFF ilianza kuangalia uwezekano wa mashindano haya kwa kumshirikisha mabingwa wa 2015/16 ambao ni Yanga
Kutokana na ratiba ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAFCC) iliyotolewa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), kipindi ch Juni hadi Agosti, 2016 Yanga watakuwa na kwenye michuano ya CAF hatua ya makundi hivyo ushiriki wao CECAFA utakuwa mgumu ilihali michuano ya CECAFA imepangwa kufanyika Juni na Julai, mwaka huu.

MKURUGENZI MKAZI WA BENKI YA DUNIA NCHINI ATEMBELEA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU

mn1Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akielezea majukumu ya ofisi hiyo kwa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia hapa nchini Bi. Bella Bird (kulia kwake) alipotembelea leo, Makao Makuu ya Ofisi hiyo iliyopo Barabara ya Kivukoni Jijini Dar es Salaam.
mn2Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akielezea majukumu ya ofisi hiyo kwa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia hapa nchini Bi. Bella Bird (kulia kwake), Menejimenti ya NBS na wageni walioambatana na Mkurugenzi Mkazi huyo alipotembelea leo, Makao Makuu ya Ofisi hiyo iliyopo Barabara ya Kivukoni Jijini Dar es Salaam. ( PICHA NA EMMANUEL GHULA)Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
mn3Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Abina Chuwa akimkaribisha Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird (kushoto) alipotembelea leo Makao Makuu ya Ofisi hiyo iliyopo Barabara ya Kivukoni Jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………………………………………………..
Na Veronica Kazimoto
26 Mei, 2016.
BENKI ya Dunia imeahidi kuendelea kuisaidia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kifedha ili iweze kutekeleza majukumu yake ya utoaji wa Takwimu Rasmi nchini.
Akizungumza leo alipotembelea Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia hapa nchini Ms. Bella Bird amesema kutokana na umuhimu wa takwimu katika kupanga na kupima matokeo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo, Benki ya Dunia itaendelea kuisaidia NBS ili iendelee kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kutoa takwimu kwa wakati.
 “Ili Ofisi ya Taifa ya Takwimu iweze kutoa takwimu kwa wakati, inahitaji kuwekeza katika matumizi ya technolojia ya kisasa ya ukusanyaji wa takwimu, hivyo Benki ya Dunia itaendelea kutoa msaada wa kiufundi na kifedha ili kufikia malengo yaliyoainishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya utoaji wa takwimu rasmi nchini”, amesema Ms. Bella Bird.
Mkurugenzi huyo Mkazi amefafanua kuwa Benki ya Dunia inatambua umuhimu wa takwimu katika maendeleo ya nchi zote duniani ikiwemo Tanzania katika kupanga sera na kutekeleza miradi mbalimbali ya nchi husika.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa ameishukuru Benki ya Dunia kwa misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikiisaidia Ofisi ya Taifa ya Takwimu ambayo imeongeza tija katika ukusanyaji na utoaji wa takwimu rasmi nchini.
“Napenda kuchukua fursa hii kuishukuru Benki ya Dunia kupitia ujio wako kuitembelea Ofisi ya Taifa ya Takwimu na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na ofisi hii ikiwa ni pamoja na ukusanyaji na utoaji wa takwimu rasmi hapa nchini,” amesema Dkt. Chuwa.
Dkt. Chuwa amesema Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeendelea kupanua wigo wa uzalishaji wa takwimu nchini ikilinganishwa na karne zilizopita.
Benki ya Dunia inaisaidia Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kutoa ushauri wa kitalaam pamoja na fedha kupitia Mpango Kabambe wa Kitaifa wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu nchini ambapo awamu ya kwanza itakamilika mwezi Juni, 2018.

TAKUKURU yawahamasisha wananchi kushishiriki kampeni ya LONGA NASI

TAKU 
Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Uratibu na utoaji Habari,Idara ya Elimu kwa Umma toka Taasisi ya Kuzuia na Kupmbana na Rushwa (TAKUKURU) Bw. Matai Kirumbi  akizungumza na waandishi wa habari  leo Jijini Dar es salaa kuhusu faida za kampeni ya LONGA NASI iliyozinduliwa na Taasisi hiyo hivi karibuni ikilenga kuhamasisha wananchi kushiriki vita dhidi ya rushwa kwa kuwafichua wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo. Kushoto ni Afisa Uhusiano nwa Taasisi hiyo Bi Angela Mulanduzi.
…………………………………………………………………………………………………………….
Frank Mvungi – MAELEZO
TAKUKURU yawahamasisha wananchi  kushishiriki kampeni ya LONGA NASI  ili kukomesha vitendo vya rushwa hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Uratibu na utoaji Habari,Idara ya Elimu kwa Umma toka Taasisi ya Kuzuia na Kupmbana na rushwa (TAKUKURU) Bw. Matai Kirumbi wakati wa mkutano na vyombo vya Habari.
Akizungumzia Kampeni hiyo,  Kirumbi amesema inalenga kuwajengea uelewa wananchi kuhusu mapambano dhidi ya rushwa ili kuzuia vitendo vya rushwa .
Katika Kampeni hiyo wananchi wanatakiwa kutoa taarifa za kuwepo kwa vitendo vya rushwa au viashiria vyake kwa kupiga namba 113 au *113# kupitia simu  ya kiganjani .
Huduma hiyo  inapatikana kupitia mitandao ya AIRTEL,TIGO,HALOTEL,VODACOM na  ZANTEL ambapo wananchi hawatatozwa gharama yoyote.
“Taarifa 8000 zimeshapokelewa na Taasisi yetu tangu kuzinduliwa kwa Kampeni hii na nyingi ni za wananchi kuombwa hongo na tayari tunazifanyia kazi “alisisitiza Kirumbi.
Akifafanua kuhusu taarifa hizo Kirumbi amesema kuwa zinaonyesha wananchi wamepokea vizuri kamapeni hiyo iliyozinduliwa tarehe 24/5/2016 na Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan.
Katika kampeni hiyo wananchi watajengewa ujasiri zaidi ili kuongeza ushiriki wao katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kutoa taarifa na kutoa mrejesho wa kero zilizotatuliwa.
Matarajio ni kuongezeka kwa ubora wa huduma za jamii kwa kuwa fedha za umma zitatumika kama ilivyopangwa katika huduma kama vile kununua dawa.
Akizindua kampeni ya LONGA NASI jumanne tarehe 24,Mei 2016 katika viwanja vya Mwembeyanga Wilayani Temeke Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan alisisitiza suala la ushiriki wa kila mmoja katika mapambano dhidi ya rushwa nchini alisema”Tunahitaji nguvu za pamoja ili kumaliza tatizo la rushwa nchini”.

ESRF yafanya warsha kujadili Mpango wa Maendeleo Endelevu (SDG)

Na Rabi Hume, Modewjiblog
Katika kusaidia kukamilika kwa Mpango wa Maendeleo Endelevu ambao unataraji kumalizika 2030, Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) imefanya warsha ambayo imekutanisha wadau mbalimbali ili kuona ni jinsi gani wanaweza kubadilishana mawazo ili kufanikisha mpango huo nchini.
Mgeni rasmi katika warsha hiyo alikuwa ni Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha, Anna Mwasha ambaye wakati akifungua warsha hiyo alisema kuwa mpango huo ni muhiu wa nchi yetu kwa sababu unakwenda kubadili maisha ya kila Mtanzania ili kuondokana na umaskini na kuwa katika maisha bora kama jinsi malengo 17 ya mpango huo yanavyojieleza.
Mo Dewji Blog ilipata nafasi ya kuhudhuria mkutano huo na kukuandalia habaroi picha jinsi warsha hivyo ilivyofanyika katika ukumbi wa ESRF.
DSC_2311
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ufunguzi katika warsa iliyoandaliwa na ESRF ili kuzungumzia Mpango wa Mendeleo Endelevu (SDG). (Picha zote na Rabi Hume, Modewjiblog)
DSC_2313
DSC_2330
Baadhi ya washiriki waliohudhuria warsha hiyo wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii, Dkt. Tausi Kida wakati akifungua warsha hiyo.
DSC_2341
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo akitoa neno kwa niaba ya UNDP ambao ndiyo wasimamizi wa mpango huo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida na Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha, Anna Mwasha
DSC_2354
Mgeni rasmi katika warsha hiyo, Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha, Anna Mwasha akifungua warsha hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF).
DSC_2367
DSC_2384
Washiriki wakiendelea kufatilia kinachoendelea katika warsha hiyo.
DSC_2478
Stephen Chacha kutoka Shirika la Beyond 2015 for Africa akizungumza jinsi Mpango wa SDG unaweza kufanyika nchini.
DSC_2481
DSC_2521
Mmoja wa washiriki, Dkt. Kitila Mkumbo akichangia mada zilizokuwa zikijadiliwa.
DSC_2457
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.

MPANGO MPYA WA UGAWAJI VYANDARUA KWA WAJAWAZITO NA WATOTO WAZINDULIWA MKOANI MTWARA

Mganga
mkuu wa mkoa wa Mtwara Dr Wedson Sichalwe akionesha moja ya vyandarau
vitakavyokuwa vikigawiwa katika vituo vya afya kwa wakina mama
wajawazito na wenye watoto wa chini ya umri wa miezi tisa mkoani mtwara
katika mpango wachandarua kliniki, mpango unaotarajiwa kuzinduliwa
jumamosi hii na mkuu wa mkoa huo bi halima dendegu. wanao shuhudia
kushoto kwake ni meneja wa kinga wizara ya afya na ustawi wa jamii bi
theresia shirima, mkurugenzi wa program ya malaria kutoka taasisi ya
john hopkins university david dadi na kulia kwake ni mratibu wa afya ya
mama na mtoto- rch bi albertina mlowola.
mganga
mkuu wa mkoa wa mtwara dr wedson sichalwe akisisitiza jambo wakati
akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa mpango mpya
ugawaji vyandarua kwa wakina mama wajawazito na wenye watoto wa chini ya
umri wa miezi tisa mkoani mtwara katika mpango wa chandarua
kliniki.pamoja nae walioketi kushoto kwake ni meneja wa kinga wizara ya
afya na ustawi wa jamii bi theresia shirima, mkurugenzi wa program ya
malaria kutoka taasisi ya john hopkins university david dadi na kulia
kwake ni mratibu wa afya ya mama na mtoto- rch bi albertina mlowola.
Mkurugenzi
wa program ya malaria kutoka taasisi ya john hopkins university david
dadi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wa mkoani mtwara hawapo
pichani kuhusiana na zinduzi wa mpango mpya ugawaji vyandarua kwa wakina
mama wajawazito na wenye watoto wa chini ya umri wa miezi tisa mkoani
mtwara katika mpango ujulikanao kama chandarua kliniki, unaotarajiwa
kuzinduliwa jumamosi wiki hii na mkuu wa mkoa wa mtwara bi halima
dendego.
Meneja
wa kinga wizara ya afya na ustawi wa jamii bi Theresia Shirima,
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wa mkoani mtwara hawapo pichani
kuhusiana na uzinduzi wa mpango mpya ugawaji vyandarua kwa wakina mama
wajawazito na wenye watoto wa chini ya umri wa miezi tisa mkoani mtwara
katika mpango ujulikanao kama chandarua kliniki, unaotarajiwa
kuzinduliwa jumamosi wiki hii na mkuu wa mkoa wa mtwara bi halima
dendego.
 
JITIHADA
za kutokomeza malaria nchi zimeanza kuonyesha matunda baada ya takwimu
za ugonjwa huo mkoani Mtwara kuonyesha zimeshuka kutoka asilimia 33
mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 17 kwa mwaka 2011/2012 kitaifa
zikifikia asilimia 9 toka asilimia 33.
 
Takwimu
hizo zimeshuka ikiwa ni jitihada zinazofanywa na serikali kwa
kushirikiana na USAID pamoja na wadau mbalimbali kuhakikisha jamii
zinatumia vyandarua vyenye kinga kujikinga na ugonjwa huo ili kuupunguza
au kutokomezwa kabisa.
 
Takwimu
hizo zimetolewa na Mganga mkuu wa mkoa, Dk Wedson Sichalwe alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mpango wa chandarua Kliniki
utakaozinduliwa rasmi tarehe 28 mwezi huu na mkuu wa mkoa Halima Dendego
kwa lengo la kufikisha vyandarua kwa jamii ambao utahusisha wajawazito
na watoto wa miezi tisa watakaohudhuria vituo vya afya.
 
“Tunataraji
kuzindua mpango wa usambazaji wa vyandarua vyenye viatilifu vya muda
mrefu kupitia kliniki a wajawazito na watoto katika vituo vya kutolea
huduma za afya ikiwa ni mojawapo ya juhudi zinazofanywa na serikali
kupambana na ugonjwa wa malaria kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
katika kuhakikisha malaria inapungua na madhara yake kwa
wananchi,”alisema Sichalwe
 
Aidha
Dk Sichwale alisema katika mwaka 2015 jumla ya mahudhurio ya wagonjwa
yaliyotokana na malaria kwa mkoa huo ni 208,473 ikiwa ni wagonjwa wa nje
yani OPD sawa na asilimia 17.5.
 
Naye
Afisa mpango wa taifa wa kudhibiti malaria wizara ya afya,maendeleo ya
jamii,jinsia ,wazee na watoto, Theresia Shirima alisema ipo mikakati
mbalimbali ya kuhakikisha vyandarua vinafikishwa kwa jamii ikiwa ni
pamoja na kupitia shuleni kila mwaka na kwa kaya kila baada ya miaka
kadhaa ambayo iliwezesha kufikia jamii kwa asilimia 85 ambayo
wanaiendeleza ili kufikia asilimia 100.
 
“Hatutumia
wajawazito na watoto pekee,zipo njia mbalimbali za kufikisha vyandarua
kwa jamii, na kwa mkoa wa Mtwara lipo zoezi linaloendelea la kugawa
vyandarua shuleni ikiwa ni njia ya kufikia ambayo ni awamu ya nne kwa
mwaka wa nne na kwenye kaya tunatoa mara moja baada ya miaka kadhaa
ambayo iituwezesha kufikia asilimia 85,”alisema Shirima
 
Akizungumza
mratibu wa afya ya uzazi na mtoto Albertina Mlolowa aliwataka
wanajawazito kuhudhuria kliniki na kupatiwa huduma pasipo kubaguliwa na
kusema hii inatokana na baadhi ya wajawazito kutokuhudhuria kliniki
wakihofia kuulizwa weza wao na kusema suala la afya ya uzazi ni kwa
manufaa ya baba na mama.
 
“Nawaomba
kina mama wajawazito wasiogope kuhudhuria kliniki na weza wao kwa faida
yao,hii inatokana na baadhi ya wajawazito kutokuhudhuria kliniki
wakihofia kuulizwa weza wao.lakini watambue suala la afya ya uzazi ni la
mama na baba hivyo wanapohudhuria wote kunasaidia kuondoa hatari amabyo
inaweza kujitokeza hapo baadae kama maambukizi mapya na wakati mwingine
kumsababishia mama kukosa huduma kwa wakati,”alisema Mlolowa
Mpango
wa chandarua kliniki unatekelezwa na mradi wa Vectorworks ambao ni
mradi wa miaka mitano 2014-2019 ukiwa na dhumuni la kuongeza upatikanaji
na matumizi ya vyandarua vyenye viatilifu vya muda mrefu

Tigo yamdhamini Ben Pol kuburudisha ‘Tamasha la Nyama Choma’

index 
Kampuni inayooongoza kwa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imekubali kumdhamini mwanamuziki nguli na mtunzi wa nyimbo za muziki, Bernard Michael Paul Mnyang’anga, maarufu kama ‘Ben Pol’ kuburudisha katika tamasha la mwaka huu la Nyama Choma.
 Tamasha hilo ambalo linafanyika kwa mwaka wa tano sasa ni moja ya tamasha maarufu linalovutia watu wengi kutoka maeneo yote ya Dar es Salaam litafanyika kwenye viwanja vya Leaders Jumamosi Mei 28, 2016.
 Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Mkuu wa Tigo wa masuala ya Dijitali Paulina Shao  alisema kuwa  kumuunga mkono Ben Pol kunaonesha  kuendelea kujikita kwa Tigo katika  kuwekeza katika kusaidia  sekta ya muziki ya ndani kwa kuhakikisha  wasanii  wanawezeshwa  kufikia viwango vya juu katika kazi zao.
 “Kama kampuni ya maisha ya kidijitali, Tigo inatambua  mchango muhimu wa wasanii wa Tanzania  wanaoutoa katika sekta ya burudani. Hii ndio maana  tumewekeza kwa kiwango kikubwa  kuwasaidia wasanii  hususani wanamuziki  wa ndani katika kuhakikisha wanafahamika katika masoko ndani ya nchi, kikanda na kimataifa kwa kutumia majukwaa ya kidijitali yanayokuwepo na kushiriki  matukio mbalimbali  na hivyo kuongeza  mauzo ya  muziki wao  pamoja na nembo zao,” alisema Shao.
 Aidha akiishukuru Tigo kwa uungwaji mkono huo, Ben Pol  aliisifu Tigo kwa juhudi  inazofanya bila kuchoka  katika kukuza  ukuaji wa  sekta ya muziki wa ndani  kupitia Jukwaa la Muziki  la Tigo.
 “Ninaishukuru sana Tigo  kwa uungwaji mkono ambao ni muendelezo wa mtiririko wa  programu ambazo imezianzisha  ili kuinua maisha ya wasanii wachanga wa Tanzania,” alisema Ben Pol na kutoa changamoto kwa wasanii wanaoibukia kuwa wasione aibu  kuomba msaada  kutoka kwa mashirika kama Tigo.
Nguli huyo wa muziki wa Bongo Flava  kwa hivi sasa anatamba na  kibao ‘MoyoMashine’ ambayo aliitoka hivi karibuni.
 Ben Pol ni miongoni mwa wasanii  wanaonufaika na jukwaa la Muziki la Tigo  ambalo lilianzishwa mwaka 2015 likiwa na lengo la  kuiunga mkono sekta ya muziki Tanzania  kwa kuwasaidia wasanii wa ndani  kupata kipato zaidi kutokana na mauzo ya  kazi zao  na kuwawezesha kufahamika katika masoko ya kimataifa  kupitia majukwaa hayo ya kidijitali  kama vile Music portal na Deezer, ambayo ni majukwaa ya kimataifa yaliyo kwenye mtandao yakiwa na  nyimbo kutoka sehemu mbalimbali  duniani  zaidi ya  milioni 36.

RAIS DKT. MAGUFULI AWATAKA MAKANDARASI WAZAWA KUWA WAZALENDO

mg3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wakandarasi  nchini wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) ambapo aliwataka makandarasi wazawa kuwa wazalendo na nchi yao ikiwemo kuepuka vitendo vya rushwa katika maeneo ya Kazi.
mg1 
Baadhi ya Makandarasi nchini wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wakandarasi  nchini wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).
mg4 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wageni na watendaji wa serikali wakati akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).
mg5 
Kaimu Msajili kutoka Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) Rhoben Nkori akiongea wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB)na kuahidi kuendelea kuwapa kipaumbele makandarasi wazawa na kukabiliana na changamoto zinazowakabil.
mg6Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) Mhandisi Consolata Ngimbwa akiongea na wakandarasi(hawapo pichani) ambapo aliwataka makandarasi wazawa kufanya kazi kwa weledi na kusisitiza kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa makandarasi wenye nia ya kuwakwamisha.
mg7 
Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na wakandarasi  nchini wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) ambapo aliwaahidi makandarasi nchini kuwasimamia kikamilifu na kuwapa fursa na kazi mbalimbali za ujenzi nchini.
mg8 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea baadhi ya mabanda wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).
mg9 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea baadhi ya mabanda wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).
mg10 mg11
Rais Dk John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Bodi ya Wakandarasi na viongozi wa mkoa wa Wizara ya Ujenzi wa mkoa wa Dar es salaam.
mg12 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa tuzo kwa wawakilishi wa makampuni mbalimbali waliowezesha kufanyika kwa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).
mg13

BAJETI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAPITISHWA, USAFIRISHAJI WA WANYAMA HAI NJE YA TANZANIA WAPIGWA MARUFUKU KWA MIAKA 3.

 Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne akijibu hoja na michango mbalimbali ya wabunge zilizoelekezwa kwenye wizara hiyo wakati wa Majumuisho ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017
ambayo imetengewa kiasi cha  shilingi bilioni 135.7.
Baadhi ya wabunge wakimpongeza wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe mara baada ya Bajeti ya Wizara hiyo kupitishwa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017 ambayo
imetengewa kiasi cha  shilingi bilioni 135.7.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akimweleza jambo Mbunge wa Bunda mjini Mhe. Esther Matiku (CHADEMA) nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kupitishwa kwa Makadirio ya Mapato na Matumizi
ya Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii bungeni mjini Dodoma.
 ……………………………………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
 Dodoma.
Serikali imesimamisha utoaji wa vibali na uuzaji wa wanyama hai kutoka katika hifadhi za Taifa kwenda nje ya Tanzania kwa kipindi cha miaka 3 mpaka hapo itakapotangazwa tena.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe ametoa agizo hilo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu hoja na michango mbalimbali ya wabunge iliyoelekezwa kwenye wizara hiyo wakati wa Majumuisho ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017 ambayo imetengewa kiasi cha  shilingi bilioni 135.7.
Prof. Maghembe ameiagiza Idara ya Wanyamapori ipange na kuweka utaratibu mpya utakaotumika kusimamia biashara hiyo pindi itakaporejeshwa tena baada ya kumalizika kwa muda wa zuio la Serikali la miaka 3 ikizingatia  mazingira ya uhifadhi wa wanyama hao.
USAFIRISHAJI WA WANYAMA HAI NJE YA NCHI.
Amesema kumekuwa na taarifa za baadhi ya watanzania wasio waaminifu ambao wamekua wakijihusisha na vitendo vya kusafirisha wanyama hai waliokatazwa kinyume cha utaratibu jambo ambalo limeisababishia Serikali ipoteze mapato kutokana na wanyama hao.
Kuhusu wanyama wanaoruhusiwa kusafirishwa kama nyani, Kenge,ndege, kobe, wadudu na tumbili amesema kuwa wamekuwa wakisafirishwa  kinyume na utaratibu na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kwa ajili ya kutumiwa na makampuni ya kimataifa kwenye shughuli za utafiti wa kisayansi wa tiba na chanjo.
Amesema makampuni hayo yamekuwa yakinufaika binafsi kwa kupata fedha nyingi pindi yanapofanikiwa kupata chanjo au tiba husika huku maeneo waliokotoka yakipata fedha kidogo jambo ambalo serikali ya awamu ya tano imeamua kulifanyia kazi.

Maliasili na Tamisemi wasaini mkataba wa makubaliano uendelezaji misitu

index1
Baadhi ya wajumbe wakiwa katika mkutano huo
index2 
Wizara ya maliasili na utalii kupitia wakala wa huduma za misitu leo wamesaini mkataba wa makubaliano kuhusu ushirikiano wa uendelezaji misitu na wizara ya TAMISEMI.
Maeneo ya kuzingatia katika mkataba huo yametajwa kuwa ni kuimarisha ushirikiano katika Misitu  na utawala bora, uperembaji miradi inayofadhiliwa na mfuko wa misitu Tanzania pamoja na kuboresha ukusanyaji, ugawaji, utumiaji na ufuatiliaji wa matumizi ya asilimia 5 ya tuzo za upandaji miti.
Awali kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi alisema wizara yake inalenga kuimarisha utendaji wake hivyo aliwaagiza watendaji kusimamia misingi ya mkataba huo wa makubaliano katika utekelezaji wa majukumu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake Katibu Mkuu TAMISEMI Injinia  Musa Iyombe ambaye amewakilishwa na Bw. Mohamed Pagawa aliwataka Maafisa Misitu kufanya kazi kwa ushirikiano kama Mkataba Unavyotaka lakini pia kuzingatia sheria, kanuni na Utaratibu katika uendelezaji wa Rasilimali Misitu
Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi ya Rasilimali Misitu Bw. Mohamed Kilongo akitoa ufafanuzi kuhusu makubaliano hayo amesema tathmini ya Rasilimali Misitu inakabiliwa na changamoto kuu mbili na amezitaja kuwa ni uharibifu Mkubwa wa Misitu unaofikia kiasi cha hekta 372,000 kwa mwaka na mahitaji ya mazao ya misitu kwa mwaka yanazidi uwezo wa Misitu kwa zaidi ya Meta za ujazo Milioni 19.5.
Amesema ili kukabiliana na changamoto hizo kunahitajika jitihada za pamoja kuboresha usimamizi wa rasilimali za misitu na kupunguza uharibifu katika hifadhi zetu. Kazi kubwa iliyopo mbele yetu ni kupanda miti hekta 185,000/= kwa mwaka kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya Mazao ya Misitu.

TAMISEMI yaziagiza Halmashauri zote kukamilisha agizo la Rais ifikapo Mwezi Juni.

index 
Na Daudi Manongi
MAELEZO Dar es Salaam
HALMASHAURI za Miji na Wilaya nchini Miji zimekumbushwa kukamilisha zoezi la upatikanaji wa madawati kwa shule za msingi na sekondari ifikapo juni 30 mwaka huu ili kutekeleza agizo lililotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Rai hiyo imetolewa  leo  na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Rebecca Kwandu wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizi kuhusu uchakavu wa madarasa na ukosefu wa madawati unaozikabili shule za kinesi A na B zilizopo wilaya ya Rorya mkoani Mara.
“Suala la upungufu wa madawati na uchakavu wa madarasa ni changamoto ya kitaifa na kwamba lilishatolewa agizo na mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kuhusu halmashauri zote nchini kuhakikisha ifikapo Juni 30 mwaka huu kila mwanafunzi anaketi kwenye Dawati” Alisema  Kwandu.
Kwa mujibu wa Gwandu alisema Serikali ya awamu imepania kuinua kiwango na ubora wa elimu nchini kupitia mikakati na sera ya elimu bure nchini kote.
Aliongeza kuwa hatua hiyo imeibua changamoto kubwa kwa wanafunzi wengi kujitokeza kwa asilimia kubwa na hivyo ni wajibu wa halmshauri hizo kukidhi mahitaji ya madawati ili wasome katika mazingira mazuri.
“Mpaka sasa Serikali imeendelea kutoka pesa kwa ajili ya elimu bure nchini kote na kumekuwepo kwa changamoto mbalimbali kama upungufu wa walimu,madawati na madarasa ambapo serikali inafanya jitihada za kila namna ili kutatua changamoto hiyo”
Akifafanua zaidi Gwandu alisema Serikali inaandaa harambee mbalimbali na kuongeza wigo wa utoaji wa vibali vya kuchangia maendeleo ya elimu kwa hiari ili kutoa  nafasi kwa wadau mbalimbali wenye nia ya kufanya.

BIMA YA AFYA KUANZA HUDUMA YA MAMA NA MWANA

NH1 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Bw Bernard Konga, akitoa
salamu za Mfuko kwa wajumbe wa baraza hilo lilikofanyika katika ukumbi
wa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro
NH2 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Bw Bernard Konga,(katikati)
akizungumza na baadhi ya wajumbe ndugu Gudluck Kirambe, kulia na
meneja wa mkoa wa Kilimanjaro ndugu Fidelis Stephen.
NH3 
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF) wanaohudhuria kika
NH4 
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF) wanaohudhuria kika
NH5 
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF) wanaohudhuria kika
……………………………………………………………………………………………………………………..
Kilimanjaro
MFUKO wa taifa wa bima ya afya (NHIF) utaanzisha huduma mpya ya
itakayojulikana kama mama na mwana afya kadi ili kuboresha huduma za
bima ya afya kwa kundi hilo ambalo lipo katika uhitaji maalum.
Kauli hiyo imetolewa mjini hapa na kaimu mkurugenzi mkuu wa mfuko huo,
bw Bernard Konga alipokuwa akitoa salamu za Mfuko huo kwa wajumbe wa
baraza hili linaloanza kikao chake mjini hapa.
Bw konga amesema lengo la huduma hiyo mpya ni kuwawezesha kina Mama
Wajawazito na Watoto kupata huduma za matibabu za uhakika zitolewazo
na mfuko wa taifa wa Bima ya afya.
Chimbuko la hatua hiyo linafuatia matokeo mazuri na mafanikio makubwa
ya mradi unaoendeshwa kwa pamoja kati ya NHIF na benki ya maendeleo ya
ujerumani ya KfW katika mikoa ya Tanga na Mbeya. hatua iliyofikiwa kwa
sasa ni kupata maoni ya wananchi kabla ya kuanza utekelezaji wake
katika mwaka wa fedha wa 2016/17.
Awali, akifungua kikao cha baraza hilo, mkuu wa wilaya ya Siha Dr
Charles Mlingwa, aliyemuwakilisha mkuu wa mkoa huo Meck Sadiki,
aliushukuru mfuko huo kwa kuwa wabunifu katika utoaji wa huduma kwa
makundi mbalimbali kwa kuzingatia uwezo wao wa kulipa. Ameutaka mfuko
huo kutafsiri hotuba za mheshimiwa Rais kuhusu dhana ya afya bora kwa
wote kwa kuweka mikakati katika eneo hilo.
Dr Mlingwa pia amesema wilaya ya Siha ni moja ya wilaya zilizofanikiwa
sana kuboresha huduma za matibabu ambapo kwa miaka miwili mfululizo
imeweza kupunguza sana vifo wa watoto wachanga na kufikia mtoto mmoja
kwa kila watoto laki moja.

MAJALIWA:VITA DHIDI YA RUSHWA SI NGUVU YA SODA

an1 
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema vita inayoendeshwa na Serikali ya awamu ya tano dhidi ya wala rushwa na wale wanaofanya ufisadi siyo nguvu ya soda kama wengi wanavyofikiri.
“Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kupambana na wala rushwa na mafisadi. Wala hatutanii. Hawa tutacheza nao na wala wasidhani vita hii ni nguvu ya soda. Tutaendelea kuwasaka hadi tufike mwisho,” alisema Waziri Mkuu wakati akizungumza na Watanzania waishio Zambia katika mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Lusaka, Zambia juzi jioni (Jumanne, Mei 24, 2016).
“Hatutaki tabia iliyokuwepo ya mwananchi anakuja ofisini kutaka huduma lakini hasikilizwi hadi atoe chochote, sisi hiyo tabia hatutaki kuisikia kabisa. Tumedhamiria kurudisha heshima kwenye utumishi wa umma na nimeanza kupata faraja kwani sasa hivi (nimeambiwa) katika baadhi ya taasisi unasikia mtu akiulizwa una shida gani, nenda pale, jambo ambalo zamani halikuwepo,” alisema.
Alisema Serikali imeamua kupigia debe dhana ya utumishi wenye uadilifu kwa sababu huo ni utamaduni mpya. “Ni kipindi kigumu kidogo cha mabadiliko lakini tumesimamia mabadiliko haya na ndiyo maana watumishi wote tumewasisitizia kuwa suala la uaminifu, uadilifu na uwajibikaji ni muhimu,” alisema na kuongeza:
“Hatutamvumilia mtumishi yeyote ambaye hatakuwa tayari kuwatumikia Watanzania au atakayeendekeza uzembe lakini pia hatutamuonea mtu yeyote. Hapa tunasisitiza usawa na hatutaki kutengeneza gap kati ya mwananchi mtumishi na wa mwananchi wa kawaida, tunataka kila mwananchi aione Tanzania ni nchi yake na kila kinachozalishwa ni sehemu yake. Tukifika hapo, tunaamini kila mmoja ataweza kuisemea nchi yake.”
Akizungumzia kuhusu ubadhirifu wa fedha za umma, Waziri Mkuu alionya kwamba Serikali imelipa kipaumbele suala la uaminifu na uadilifu kwenye fedha za Serikali na kwamba haitakuwa tayari kuona fedha hizo zikifujwa.
“Hivi sasa Serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo na fedha hizo zitaenda vijijini. Tunataka zikafanye kazi iliyokusudiwa, na wale wadokozi wajue kuwa wamekalia kaa la moto,” alisema huku akishangiliwa.
Alisema watumishi wa umma wana wajibu wa kusimamia kazi zilizopangwa na kuhakikisha miradi iliyolengwa inakamilika. “Kama fedha zimeletwa kujenga zahanati simamia zahanati ijengwe na ni lazima zahanati hiyo ionekane,” alisema.
Alisema bajeti ya mwaka huu imeongezeka kutoka sh. trilioni 21 hadi trilioni 29 lengo kuu likiwa ni kuleta maendeleo kwa wananchi. “Ndiyo maana tumepandisha bajeti ya maendeleo kutoka asilimia 27 hadi asilimia 40. Ole wake atakayepokea fedha hizi halafu zisifanye kazi yake, ukiipoteza wewe utafute njia ya kwenda,” alisema huku akishangiliwa.
Akifafanua zaidi, Waziri Mkuu alisema vita inayoendeshwa imelenga kuifanya Tanzania ibadilike na itoke kwenye uchumi wa chini na kuingia uchumi wa kati. “Swali la msingi ni je tunafikaje hapo? Jibu ni kupitia uzalishaji wa bidhaa viwandani,” alisema.
“Nyote ni  mashahidi wa jinsi ambavyo shilingi yetu imekuwa ikishuka thamani kulinganisha na dola ya Marekani. Tulitoka sh. 1,600/-, tukapanda hadi sh. 1,900/- na sasa tumefikia sh. 2,180/-. Hii ni kwa sababu tunaagiza zaidi bidhaa kutoka nje ya nchi badala ya kuzalisha, hatuwezi kuendelea hivi na ndiyo maana tumeamua kuwa nchi ya viwanda. Leteni mitaji nyumbani muwekeze,” alisisitiza.
Akijibu swali kuhusu Serikali kutafuta njia ya kutoa mikopo kwa Watanzania waishio nje ya nchi, Waziri Mkuu alisema mkopo ni mkataba kati ya taasisi ya kifedha na mkopaji kwa hiyo Serikali haiwezi kubeba dhamana hiyo. “Benki wanataka ijue taarifa zako mkopaji, wanataka wajua dhamana zako ni zipi, wajiridhishe na shughuli unazofanya. Je panakopesheka hapo?,” alihoji.
Hata hivyo, aliwaeleza kwamba wakitaka kuwekeza nyumbani wanaweza kupata mikopo kutoka benki ya maendeleo ya kilimo (TADB), Benki ya Rasilmali (TIB Corporate na TIB Development). “Hizi benki ni za wakulima na wajasiriamali, na zina masharti yake, kwa hiyo ni lazima wakakague eneo lako au mahali unapofanyia biashara au wakague leseni yako na ukweli wa maombi uliyopelekea. Sasa ukiwa Zambia watawezaje kukukopesha? Kwa hiyo ukitaka fedha uwe nyumbani,” alisema.
Akijibu swali ni vipi Serikali itawasaidia wanadiaspora kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wakiwa nje ya nchi, Waziri Mkuu alisema Serikali haijawahi kujaribu jambo hilo licha ya kuwa ilikwishapokea mapendekezo kadhaa kutoka nchi mbalimbali lakini kwa vile wameliuliza, yeye analibeba na kwenda kulifanyia kazi.

Tigo yatoa kompyuta 20 zilizounganishwa na intaneti kwa sekondari 3 Mtwara

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego(katikati) akikata utepe katika makabidhiano ya kompyuta ishirini zenye thamani ya 33m/- zikiwa na huduma ya intaneti ya bure iliyo gharimu 22m/- katika Shule ya Sekondari Sino,mkoani Mtwara, kushoto ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwana Goodluck Charles, na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Fatuma 

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego(katikati) akitoa hotuba kwa wakazi wa mtwara na wanafunzi  katika makabidhiano ya kompyuta ishirini zenye thamani ya 33m/- zikiwa na huduma ya intaneti ya bure iliyo gharimu 22m/- katika Shule ya Sekondari Sino,mkoani Mtwara, kushoto ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwana Goodluck Charles, na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Fatuma A

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sino,mkoani Mtwara wakimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego, vipi wanavotumia kompyuta katika masomo yao ya sayansi, kompyuta hizo 20 zenye thamani ya 33m/- zilizounganishwa na intaneti ya bure yenye thamani ya 22m/- zimetolewa na Tigo
Wanafunzi wakishuhudia makabidhiano hayo
 Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidijitali ya Tigo Tanzania leo imetoa kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi milioni 33 zikiwa na huduma ya bure ya intaneti iliyogharimu 22m/- kwa shule  tatu za sekondari mkoani
Mtwara. Msaada huo uko katika mkondo wa malengo ya kampuni  ya kuleta mabadiliko ya kidijitali katika sekta ya elimu nchini.
 
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika Shule ya Sekondari Sino mkoani Mtwara Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Goodluck Charles alisema, “Msaada huu kwa shule hizi tatu ni sehemu ya
mkakati wa kampuni wa kuleta mageuzi katika mtindo wa maisha ya kidijitali. Msaada huu wa leo umekuja baada ya kukabidhi kompyuta 10 kwa Shule ya Msingi Chuda mkoani Tanga  na kompyuta 25 zilizounganishwa na intaneti kwa Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure mkoani Mwanza mwaka jana.
 
“Msaada kwa shule ya Sekondari ya Masasi, Tandahimba na Sino ni kielelezo cha kweli cha uwekezaji wa Tigo katika miradi tofauti yenye mchango kijamii kupitia mkakati wetu wa kuwekeza kijamii unaowezesha jamii kupokea zana za kisasa za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katikanyanja zote za kijamii ikiwemo sekta ya elimu,” alisema Charles.
 
Tukio hilo ambalo lilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego ambaye alizitaka sekta binafsi kuisaidia serikali katika mikakati yake katika kuboresha mazingira ya kujifunzia katika shule zilizopo nchini.
 
Dendego alisema, “Naipongeza Tigo  kwa ukarimu wao wa kuzisaidia shule hizi natoa wito kwa watu binafsi kampuni za biashara na wadau wengine kujitokeza katika kuunga mkono juhudi za kuboresha
sekta ya elimu.”
 
Akipokea msaada huo kwa niaba ya wakuu wenzake wa shule za sekondari, Mkuu wa Shule ya Sekondari Sino Riyadh Kadhi alisema kwamba kompyuta hizo zitawawezesha wanafunzi kuwa na uelewa wa kiteknolojia na kuwawezesha  kuipata teknolojia ya habari mapema katika elimu yao. “Tunafurahi kwa hatua hii ya Tigo; tuna
matumaini kwamba  kompyuta hizi zitawaweka wanafunzi wetu katika ngazi moja na wenzao katika mashule mengine yaliyo maeneo ya mjini na duniani kwa ujumla,” alisema Kadhi.

No comments :

Post a Comment