Friday, April 15, 2016

SUDANI YA KUSINI YAJIUNGA NA EAST AFRICA COMMUNITY

sam7 
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki CEAC) na Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir wakibadilishana hati za makubaliano ya kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada ya kusaini
sam1
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanua Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa  wakimsubiri  Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir alipowasili Ikulu na kupokelewa na kwa ajili ya kutia kusani mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki Leo April 15,2016.
sam2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanua Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir alipowasili Ikulu na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa ajili ya kutia kusani mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki Leo April 15,2016.
sam3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanua Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir alipowasili Ikulu na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa ajili ya kutia kusani mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki Leo April 15,2016, Kushoto ni Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.
sam5
Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit akikagua gwaride la heshima  wakati Rais Kiir   alipowasili Ikulu leo.
sam6
Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir akiwapungia mikono viongozi mbalimbali huku akiongozana na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakati alipowasili Ikulu
sam7
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki CEAC) na Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir wakibadilishana hati za makubaliano ya kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada ya kusaini 
sam8
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati Rais Kiir. Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Hassan Suluhu na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo ya utiaji saini.

SASA TUKO KWENYE KIWANGO KIZURI:KINNAH

Phiri15 
Kocha Mkuu wa Mbeya  City Fc  Mmalawi Kinnah Phiri amesema  sasa ana uhakika  nyota wake wako kwenye kiwango kizuri  kufuatia  matokeo ya  ushindi wa jumla ya bao 5  kwenye michezo miwili  iliyopita  kwenye  mfululizo  wa mechi za  ligi kuu ya Soka  Tanzania Bara inayoelekea  ukingoni hivi sasa.
Akizungumza na mbeyacityfc.com asubuhi ya leo kocha Phiri  ameweka wazi kuwa  ushindi wa 4-0 dhidi ya Coastal Union na  ule wa 1-0 dhidi ya Mgambo JKT mwishoni mwa juma lililopita umempa  imani kubwa kuwa wachezaji wake sasa  wameanza kuielewa vyema  falsafa yake hasa kwa kuweza kufanikisha ushindi bila  kuruhusu kufungwa bao katika michezo hiyo miwili.
Tulianza  kucheza  kwa  mchezo wa kawaida  sasa  tumeongeza, tunacheza kwa spidi kubwa wachezaji wangu sasa  wanajiamini kwa kiwango kikubwa, tumefunga bao 5 bila kuruhusu kufungwa bao lolote, hili ni uhakika tosha kuwa kikosi changu sasa  kiko imara kwenye ulinzi na pia  kiko vizuri kwenye ufungaji, kwa sasa  tuko kwenye mipango  mizito  kuhusina na mchezo ujao, alisema.
Akiendelea  zaidi kocha huyo aliyewahi  kuifundisha kwa mafanikio timu ya taifa ya Malawi alisema kuwa  mara baada ya kurejea  kutoka  jijini Tanga kwenye mchezo dhidi ya Mgambo JKT  alitoa siku chache za mapumziko kwa wachezaji wake na kuwataka  kujiandaa kwa mazoezi yatakayoanza  siku ya jumatatu tayari kwa mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar uliopangwa  kuchezwa  mwishoni  mwa mwezi huu.
Baada ya Tanga, nilitoa mapumziko ya siku saba, vijana watarejea  jumatatu tayari kwa mazoezi  kabla ya kuivaa Mtibwa, nina  imani siku saba  zitatosha  kuwaweka sawa kwa ajili ya mchezo huo, Sifahamu sana  kuhusu timu hiyo ya Morogoro, kwenye ratiba  inaonyesha watacheza kesho  ninaweza kufika  kuwaona au  nitatumia  muda kuangalia mchezo wao kwenye TV, nataka kujua baadhi ya mambo muhimu ili nijiandae  vizuri kuweza kupata ushindi.

TAARIFA YA UFAFANUZI KUHUSU MKATABA WA LUGUMI

download (3)Kumekuwa na taarifa zinazoendelea kupotosha umma na baadhi ya vyombo vya Habari kuwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilipokuwa ikitekeleza majukumu yake tarehe 5 Aprili, 2016 ililitaka Jeshi la Polisi kuwasilisha Mkataba ulioingiwa Kati ya Jeshi hilo na Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd kuhusu mradi wa Utambuzi wa Alama za Vidole AFIS (Automated Fingerprint Identification System).
Ofisi ya Bunge inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hili kwamba, taarifa hizo si za kweli na zina lengo la kupotosha umma kutokana na kile kilicho amuliwa na kamati hiyo. Ukweli kuhusu jambo hili ni kwamba tarehe 5 Aprili, 2016, kamati hiyo ilikutana na kujadili Taarifa ya Ukaguzi wa hesabu zilizokaguliwa za fungu 28, Jeshi la Polisi kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2014 ambapo kamati pamoja na mambo mengine ilibaini dosari katika utekelezaji wa mkataba huo.
Kutokana na dosari hizo, kamati iliomba Afisa Masuhuli ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuwasilisha maelezo ya kina kwa maandishi kuhusu utekelezaji wa mradi huo kwa Ofisi ya Katibu wa Bunge ili kamati iweze kuchambua na kujadili maelezo hayo kabla ya kupendekeza kwa Bunge hatua zaidi za kuchukua. Kufuatia agizo hilo, kamati ilimwandikia pia Katibu wa Bunge taarifa kuhusu agizo hilo tarehe 12 Aprili, 2016 ili kupatiwa maelezo hayo kutoka kwa Afisa Masuhuli.
Aidha, Ofisi ya Bunge ilimwandikia barua Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani tarehe 12 Aprili, 2016 kuwasiilsha Taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Kamati Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyotokana na kikao hicho cha tarehe 5 Aprili 2016 kabla ya tarehe 18 Aprili, 2018 kama ilivyoshauriwa na kamati . Hivyo ni vyema Umma ukafahamu kuwa kilichoombwa na Kamati ni Maelezo ya utekelezaji wa Mkataba huo na sio Mkataba kama inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya Habari ambapo Ofisi ya Bunge iliomba maelezo hayo yawasilishwe kabla ya tarehe 18 Aprili, 2016. Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM 15 Aprili, 2016.

MOUNT KILIMANJARO WON AFRICA’S LEADING TOURIST ATTRACTION AWARD IN 2016.

02063.P100.101
kili2 
Mount Kilimanjaro, the highest mountain in Africa, and the highest free-standing mountain in the world, was declared Africa’s leading tourist attraction in 2016 during the World Travel Awards Africa and Indian Ocean Gala Ceremony in Zanzibar. The red carpet event attended by hundreds of tourism industry leaders was hosted by Diamonds La Gemma Dell’est,Nungwi the northern tip of Zanzibar, Tanzania on 9th April 2016.
Tanzania Tourist Board is honoured to see that Mt. Kilimanjaro has been voted as the leading tourist destination in Africa. This nomination will definitely contribute towards our efforts in promoting Destination Tanzania, especially in making the world know that Tanzania is home to Mt. Kilimanjaro; the pinnacle wonder of Africa, and as many know, it is affectionately known as the rooftop of Africa.
Mount Kilimanjaro is the world’s most accessible high snow–capped summit, a beacon for visitors from around the world and is also a UNESCO World Heritage Site.
In addition to Mt. Kilimanjaro, the following Tanzanian tourism companies also won different awards in various categories. http://www.worldtravelawards.com/about
Tanzania Tourist Board congratulates all companies nominated at the World Travel Awards Africa & Indian Ocean Gala Ceremony and is confident that their victory is a very strong tool in the marketing and promotion of destination Tanzania.  Likewise, Tanzania Tourist Board thanks all tourism stakeholders for voting for Mount Kilimanjaro and other Tanzania tourism facilities and making them become winners.
———————-
World Travel Awards™ was established in 1993 to acknowledge, reward and celebrate excellence across all key sectors of the travel, tourism and hospitality industry. Today, the World Travel Awards™ brand is recognized globally as the ultimate hallmark of quality, with winners setting the benchmark to which all others aspire.
Each year World Travel Awards™ covers the globe with a series of regional gala ceremonies staged to recognize and celebrate individual and collective successes within each geographical region. 
Issued by 
TANZANIA TOURIST BOARD

Wanarorya watakiwa kuwekeza Rorya.

0.1Mwenge wa Uhuru 2014 wilayani Rorya27
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
15DAR ES SALAAM
Mkuu wa Wilaya ya Rorya Mhe. Felix Lyaniva ametoa wito kwa wanarorya wanaoishi Jijini Dar es salaam kuwekeza kwenye fursa zilizopo katika wilaya hiyo iliyopo mkoani Mara.
Ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa wanarorya wanaoishi Da es salaam utakaofanyika katika ukumbi wa Karimjee siku ya  jumapili Februari 17, 2016 kuanzia saa nane mchana.
“Wilaya yetu ya Rorya ina fursa nyingi za uwekezaji zikiwemo za biashara, ardhi yenye rutuba, gesi asilia, mifugo pamoja na misitu, lakini pamoja na kuwa na fursa za rasilimali zote hizo bado ni miongoni mwa wilaya ambazo ziko nyuma kimaendeleo hivyo tunahitaji wanarorya wachukue hatua” alisema Mhe. Lyaniva.
Mhe. Lyaniva ameongeza kuwa licha ya wilaya ya Rorya kupiga hatua na  kuwa Halmashauri haijawa na kasi ya kuridhisha  kutokana na wanarorya waishio nje ya wilaya hiyo kutoshiriki ipasavyo kwenye fursa za kiuchumi na kwenye utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili wilaya hiyo.
Aidha, Mhe. Lyaniva ameelezea baadhi ya changamoto zinazowakumba wananchi wa Rorya zikiwemo za ugonjwa wa Ukimwi, njaa pamoja na ukosefu wa huduma bora za kijamii kama vile maji safi na salama, barabara, Hospitali, shule, vyuo vya ufundi pamoja na vituo vya kutosha vya ulinzi na usalama kwa upande wa Jeshi la Polisi.
Kabla ya mwaka 2007 Rorya ilikua sehemu ya Wilaya ya Tarime, kwa sasa Rorya imekua wilaya mojawapo kati ya wilaya nne zilizopo Mkoani Mara.

Dk.Abdalla Possi mgeni rasmi matembezi ya hiyari kuazimisha siku ya watoto wenye usonji

wal
Mwenyekiti wa Chama cha Kuhudumia Watu Wenye Usonji Tanzania (NAPAT) Dkt.Stella Rwezaula(wa tatu kulia) akiongea na waandishi wahabari kuhusu matembezi ya hiyari kuadhimisha siku ya usonji Aprilli 16, kushoto ni Katibu wa Chama cha Kuhudumia Watu Wenye Usonji (NAPAT) Bi. Ella Mgalla na wengine ni wajumbe.(Picha na Lorietha Laurence-Maelezo)
…………………………………………………………………………………………………..
Na Lorietha Laurence-Maelezo
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Dk.Abdalla Possi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika matembezi ya hiyari ya kuazimisha siku ya watoto wenye usonji  Aprili 16 mwaka huu.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Chama cha Kuhudumia Watu Wenye Usonji Tanzania (NAPAT) Dkt.Stella Rwezaula ameeleza kuwa lengo la matembezi hayo ni kutoa elimu kwa jamii kuhusu watu wenye matatizo ya Usonji.
“Jamii imekuwa ikiwanyima uhuru watu wenye usonji kwa kuwafungia ndani na hivyo kuwanyima haki zao za msingi ikiwemo kupata elimu ” alisema Dkt.Rwezaula.
Aliongeza kuwa watu wenye matatizo ya usonji wanapopatiwa msaada wa haraka na unaostahili ikiwemo huduma ya afya husaidia kuimarisha hali zao na baadaye kuwa msaada katika jamii yake.
“Usonji ni tatizo linalotokana na hitilafu katika ukuuaji wa ubongo wa mtoto na kupelekea mtoto kuwa na matatizo katika mawasiliano  na mahusiano ya kijamii na utambuzi  lakini linapogundulika haraka inasaidia kuimarisha hali ya mtoto“ alisema Dkt.Rwezaula.
Naye  Katibu wa Chama cha Kuhudumia Watu Wenye Usonji (NAPAT) Bi. Ella Mgalla ametoa wito kwa wazazi  kuwasaidia watoto wenye usonji  kwa kuwapeleka  katika shule maalum  ili waweze kupata elimu.
Pia ameeleza kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni ukosefu wa waalimu maluum wa kuwafundisha watoto wenye usonji pamoja na upungufu  wa shule maalum  ambapo mpaka sasa kuna shule 8 Tanzania nzima.
“Ninaiomba serikali iweze kutusaidia kwa kutoa mafunzo maalum kwa waalimu ambao watakuwa wakiwahudumia watoto wenye matatizo ya usonji na kuongeza idadi ya shule  ambapo kwa sasa ni mikoa minne tu inayotoa huduma hiyo ikiwemo Dar es Salaam shule mbili, Arusha shule nne, morogoro shule moja na Mwanza shule moja” alisema Bi.Mgalla
Chama cha  Kuhudumia Watu Wenye Usonji (NAPAT) kimeanzishwa mwaka 2012 kikiwa kinajumuisha wanachama 53 ambao ni wazazi, walezi na waalimu wa watoto wenye usonji.

WIZARA YAKEMEA MAUAJI YA WAZEE NZEGA

download (2)
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto imesikitishwa na kulani viakli matukio ya mauaji ya wazee  kumi (10) yaliyotokea wilaya ya Nzega, mkoani Tabora kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi, 2016.
Inaelezwa kuwa, miongoni mwa chanzo cha mauaji ya wazee ni imani za kishirikina, uchu wa kumiliki mashamba na visasi mambo ambayo Serikali imekuwa ikiyakemea vikali. Wizara inawataka wananchi kushirikiana na uongozi wa Wilaya ya Nzega, kuhakikisha kuwa watuhumiwa wa mauaji haya wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kali ili kuwa fundisho kwa watu wengine.  
Wizara inasisitiza kwamba  wazee ni binadamu, na wanayo haki ya kuishi na kupata hifadhi ya maisha yao kwa mujibu wa Sheria za nchi. Vitendo vya mauaji ya kikatili wanavyofanyiwa wazee vinasababisha hofu kubwa kwa wananchi. Mauaji hayo yanawakosesha amani na vinadhohofisha ari ya kufanya shughuli za za maendeleo ya familia na taifa kwa ujumla. Familia inayoishi na mzee anayewindwa, itatumia muda mwingi kutekeleza jukumu la ulinzi na hivyo kupunuza tija na uzalishaji wa mwananchi mmoja na familia kawa ujumla. Kwa kutambua hili Wizara inahimiza wadau wote kuunga mkono jitihada za Serikali katika ulinzi wa wazee na kuboresha huduma zao ili kuelekeza nguvukazi katika uzalishaji.  
Wizara inapenda kutoa pole kwa familia ambazo zimeguswa na mauaji ya wazee waliopoteza maisha kwa kuuawa kinyama. Wizara inaitaka jamii itambue kuwa wazee wana haki ya kuthaminiwa utu wao, kupata huduma stahiki, na kushiriki haki zote za msingi bila ubaguzi wowote ambao unaweza kuhatarisha maisha yao ikiwemo haki yao ya kuishi. Aidha, Jamii ihakikishe kuwa wazee na wananchi wote, wanaishi katika hali ya usalama, amani na utulivu kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Taifa letu.
                                                                                 Erasto T. Ching’oro (Msemaji)
                                        Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
                                                                                            15/4/2016

WABUNGE WAPONGEZA KUANZISHWA KWA TADB

mk1
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Florens Turuka (Kulia) akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
mk2
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB, Dkt. Anaclet Kashuriza (Aliyesimama) akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
mk3
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakifurahia jambo wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
mk5
Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi (Kulia) akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
mk6
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Mary Nagu (Katikati) akifuatilia maelezo yaMkurugenzi Mwendeshaji wa TADB (hayupo pichani) wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
mk8
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakitoa michango yao wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
mk9
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakitoa michango yao wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
mk12
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakitoa michango yao wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi  wetu
Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Kilimo, Mifugo na Maji imeipongeza Serikali kwa kuanzisha kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) yenye lengo la Kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania na kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.
Wakizungumza na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB wakati wa vikao vya kamati za Bunge vinavyoendelea jijini Dar es Salaam. Wabunge hao wamesema kuwa TADB imekuja wakati muafaka kwa kuwa itachagiza juhudi za kuinua na ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. Mary Nagu amesema kuwa licha ya umuhimu wa Sekta ya Kilimo, bado ukuaji wa sekta hiyo ulikuwa ukikabiliwa na changamoto mbali mbali kuu ikiwa ni Ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini.
“Kwa kweli tunapongeza kwa kuanzishwa Benki hii kwa kuwa kwa miaka mingi mikopo mingi kutoka taasisi za fedha imekuwa ikielekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa na kuwa na riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo,” alisema Mhe. Nagu.
Wabunge hao wametoa wito kwa Serikali kuiongezea mtaji Bnki hiyo ili kuongeza kasi ya utendaji kazi wa Benki hiyo.
Akizungumza kwenye kikao hicho, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Florens Turuka alisema kuwa TADB inajihusisha na aina zote za kilimo kwa ule wigo mpana wa maana ya kilimo, ambao inahusisha mazao, ufugaji, uvuvi, na bidhaa zitokanazo na misitu. Na kuongeza kuwa katika kusaidia minyororo ya thamani ya mazao ya kilimo, TADB itakuwa inatoa fedha kwenye hatua mbali mbali za Uzalishaji na uongezaji wa thamani kama vile Uzalishaji wa awali; uhifadhi; usindikaji; uchakataji; usafirishaji; na masoko.
“Uanzishwaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Nchini kama taasisi ya maendeleo ya fedha, kulitokana na Wizara yangu, na baadaye mawazo  ya Wadau mbalimbali chini ya uratibu wa Baraza la Taifa la Biashara kuhusu jinsi Tanzania inavyoweza kufikia mapinduzi ya kilimo,” aliongeza Dkt. Turuka.
Kwa mujibu wa  Dkt. Turuka, katika maazimio kumi (10) ya Kilimo Kwanza yaliyofikiwa mwaka 2009, azimio la tatu lilikuwa kuanzishwa kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo.  Hivyo uanzishwaji wa benki hii ni muendelezo wa Serikali katika kutimiza na kutekeleza maazimio ya “KILIMO KWANZA”.  Hii ilitokana hasa na kuwepo kwa changamoto mbali mbali kwenye Sekta ya Kilimo ikiwemo upatikanaji wa fedha na mikopo ya riba nafuu katika kuendeleza sekta ya kilimo nchini kwa miradi mikubwa ya kilimo, ya kati na midogo inayolenga kuimarisha minyororo ya thamani ya Kilimo.
Naye Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi alisema kuwa kama yalivyo matarajio ya Serikali, kuanzishwa na kuanza kufanya kazi kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Nchini, kunategemewa kuwa na umuhimu wa kusaidia upatikanaji wa mali ghafi kwa viwanda vya ndani hivyo kusukuma ndoto ya Serikali kufikia lengo lake la Kujenga Uchumi wa Viwanda.
Ameongeza pia TADB inatarajia kuhuisha uwekezaji kwenye Viwanda vidogo vidogo na vya kati vya usindikaji na uchakataji wa mazao ya Kilimo na mifugo pamoja na kuboresha kwa upatikanaji wa mikopo na huduma za kifedha kwenye miradi ya maendeleo ya Kilimo kwa riba nafuu zilizo chini ya viwango vya kibiashara kwenye soko.
Benki ya TADB ni mali ya Serikali kwa Asilimia 100 ya Hisa na kwa kuzingatia muundo wa uendeshaji wa shughuli za Serikali hususan kwenye masuala ya kifedha, Benki ya Maendeleo ya Kilimo iko chini ya Wizara ya Fedha na Mipango. Hali kadhalika, benki iko chini ya  Uangalizi wa Msajili wa Hazina kama yalivyo mashirika mengine ya Umma. Hata hivyo, kiutekelezaji, TADB inajihusisha moja kwa moja na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, kwani muktadha wa uanzishwaji wake umelenga moja kwa moja kwenye Sekta ya Kilimo kuliko Sekta nyingine yoyote.

Wakazi Dar ‘kuonja’ daraja la Kigamboni bure kesho

magu
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake kesho  wanatapa fursa ya kulitumia kwa mara ya kwanza Daraja la Kigamboni linalotarijiwa kufunguliwa rasmi na Rais John Pombe Magufuli siku ya Jumanne ya wiki ijayo ili ‘kuonja’ na kujionea ubora wa daraja hilo kisasa.
Akizungumza  jijini Dar es Salaam jana, Meneja mradi kutoka kampuni ya China Railway Construction Engineering Group ambao wametekeleza mradi huo kwa ushirikiano na kampuni ya China Railway Major Bridge Group Bw. Zhang Bangxu,  alisema  siku ya kesho, wataruhusu wakazi hao na magari kupita katika daraja hilolililogarimu Dola za Kimarekani milioni 135 kujengwa.
“Kama wajenzi kesho tutaruhusu magari kupita kwenda upande wa Kurasini na upande wa Kigamboni siku ya Jumamosi tu kama ikiwa ni sehemu ya majaribio yetu kitaalamu ikiwa ni pamoja na kutumia fursa hiyo kufanya majaribio ya mitambo na mashine zote ambazo zitatumika katika kufanya tozo mbali mbali baada ya kuanza rasmi kwa mradi,” alifafanua
Kwa mujibu wa Bw. Bangxu, daraja la Kigamboni ndiyo daraja refu kuliko yote katika ukanda wa Afrika Mashariki lililotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya matumizi ya kamba (cable) kubeba uzito wa daraja, ambayo itaunganisha jiji la kibiashara la Dar es Salaam na eneo la Kigamboni na Kurasini. Ujenzi ulianza mnamo Tarehe moja Februari mwaka 2012.
“Pamoja na kujengwa katika ubora wa hali ya juu, daraja hili lina jumla ya njia sita yaani njia tatu kwa kila upande, pamoja na njia mahususi kwa ajili ya waenda kwa miguu na waendesha baiskeli ambayo ina upana wa mita 2 na nusu (2.5 meters) katika kila pande. Daraja hilo litaruhusu magari yenye uzito usiozidi tani 30 kupita.,’’ aliongeza
 Bw. Bangxu alisema kwamba kaskazini mwa daraja hilo, litaungana na barabara lenye urefu wa kilometa  moja ambayo inakatiza reli ya TAZARA kisha kuungana na barabara ya Mandela. Kwa upande wa Kigamboni, daraja litaungana na barabara lenye urefu wa Kilometa 1.5 ambayo inaungana na barabara ya Kigamboni Ferry – Kibada.
Aliongeza kwamba kukamilika kwa daraja hili ni ishara ya maendeleo kwani inatarajiwa kuchochea kasi ya maendeleo ya mji wa kisasa wa Kigamboni (Kigambani satellite city), kutengeneza fursa za ajira katika sekta ya ujenzi wa maeneo ya makazi pamoja na sekta za huduma ambazo  zitastahimili ongezeko kubwa wa idadi ya wakazi wapya katika mji huo mpya.
Kukamilika kwa daraja hilo kunatajwa kuwa kutawapafusra wakazi wa Kigamboni na viunga vyake ikiwa ni kutoa njia mbadala ya kufikia makazi yao, biashara zao au shuguli zao za ujenzi wa taifa kwa njia ya barabara.
Maeneo ya Kigamboni na Kurasini kwa sasa hufikika kwa kutumia vivuko viwili vya MV Magogoni na MV Kigamboni ambazo kwa pamoja zinaumezo wa kubebe abiria 1000 na magari 78 kwa kila safari.
Mradi huo umedhaminiwa kwa kwa ubia kati ya Shirika la Hifadhi ya Jamii ya Taifa (NSSF) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

RAIS WA SUDANI KUSINI, MHE. JENERALI SALVA KIIR MAYARDIT AWASILI NCHINI

sal1
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
sal2
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (wa tatu kulia) akisalimiana na Kamanda Mkuu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Siro  mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
sal3
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye kofia nyeusi) akishuka katika ndege ya Shirika la Kenya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
sal4
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga (wa tatu kushoto) akiwa tayari kumpokea Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
sal5
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) akisalimiana na baadhi ya viongozi waliokuja kumpokea mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
sal6
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) akipita katikati ya gwaride la Jeshi mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
sal7 sal9
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga (kushoto) akisalimiana na Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
sal10
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Richard Sezibera (wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.

MAKAMPUNI BINAFSI HAYAHUSIKI ULINZI WA NDANI OFISI ZA BANDARI.

mel
Na Jacquiline Mrisho -MAELEZO
 DAR ES SALAAM
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imesema kuwa makampuni binafsi ya ulinzi yanayofanya kazi bandarini hayahusiki na ulinzi wa sehemu nyeti za za Mamlaka hiyo.
Akitoa ufafanuzi huo leo jijini Dar es salaam, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Bi. Janeth Ruzangi amekiri kuwepo kwa makampuni yanayofanya kazi ya ulinzi bandarini na amefafanua kuwa hayahusiki kwa namna yoyote ile kulinda sehemu za ndani za ofisi zilizoko bandarini.
“Ninapenda kuwafahamisha wananchi kuwa Bandari inalindwa na walinzi wa aina tatu ; Jeshi la polisi, Polisi wasaidizi walioajiriwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (Auxilliary Police) pamoja na walinzi wa Makampuni binafsi”
Ameongeza kuwa makampuni hayo yanalinda maeneo ya nje ya bandari yakiwemo maegesho ya magari ya watumishi wa mamlaka kama ilivyo kwenye ofisi nyingine.
Aidha,amefafanua kuwa Polisi wa bandari walioajiriwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania wako kwa mujibu wa sheria zilizotungwa na Bunge na wamepata baadhi ya mafunzo ya kipolisi.
Ikumbukwe kuwa agizo la kuwandoa walinzi wa makampuni binafsi kwenye maeneo nyeti ya bandari lilitolewa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mwezi Februari mwaka huu alipofanya ziara ya kushtukiza bandarini hapo.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KUHUSU MATUMIZI YA DARAJA LA KIGAMBONI

kigamboni
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Daraja la kigamboni litaanza kutumika siku ya Jumamosi tarehe 16, Aprili, 2016 kuanzia saa 12:00 asubuhi.
Katika siku za mwanzo, magari yatapita bila kulipia tozo hadi Serikali itakapokamilisha taratibu na kutangaza utaratibu wa kulipia.  Aidha, watembea kwa miguu na waendesha baiskeli watavuka bure katika Daraja la Kigamboni.  Hata hivyo maguta na mikokoteni haitaruhusiwa kutumia daraja hilo kutokana na sababu za kiusalama.
Magari yatakayoruhusiwa kupita katika Daraja la Kigamboni katika siku hizo za mwanzo ni yale yenye uzito usiozidi tani 10, hatua ambayo itasaidia kufuatilia mwenendo wa upitaji wa magari katika daraja, barabara za juu (Interchange) katika eneo la Kurasini, pamoja na kuhakikisha kwamba magari yanayotoka au kuingia katika daraja hayasababishi msongamano wa magari katika Barabara ya Nelson Mandela, Barabara ya Kilwa na maeneo mengine ya jiji.  Baada ya utaratibu kukamilika magari ya aina zote yenye uzito unaoruhusiwa kisheria yataruhusiwa kupita katika daraja.
Mambo muhimu ambayo madereva na watumiaji wengine wa barabara wanatakiwa kuzingatia ni:-
  • Kuzingatia sheria ya Usalama Barabarani ikiwa ni pamoja na kufuata mwendo kasi unaotakiwa ili kuepuka ajali na kuepuka uharibifu miundombinu ya daraja
  • Kufuata alama za barabarani zilizowekwa katika ‘Interchange’ ya Kurasini ili kwenda kwenye uelekeo sahihi.
  • Kuzingatia alama zilizowekwa kwenye milango (Toll Gates) ya Kituo cha kulipia tozo (Toll Plaza) ili kuepuka uharibifu wa miundombinu ya kituo hicho.
  • Madereva na watumiaji wa barabara wengine watakaosababisha uharibifu wa aina yeyote wa miundombinu ya daraja watatozwa faini au kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria.
  • Kutunza mazingira kwa kuepuka kutupa takataka katika eneo la daraja.
Aidha, Wizaraya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inawataka madereva wa magari ya mizigo wanaoegesha katika barabara ya Nelson Mandela wakisubiri kuingia bandarini watafute eneo stahiki la maegesho na kuyaondoa magari hayo kwani hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaoenda kinyume na agizo hili.
Msongamano wa magari hayo husababisha uharibifu wa barabara na usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara katika eneo hilo.
Imetolewa na;
Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu  (Ujenzi)
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
14 Aprili, 2016

No comments :

Post a Comment