Tuesday, April 19, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MATHIAS MEINRAD CHIKAWE KUWA BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI JAPAN


CHI1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mathias Meinrad Chikawe kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan, Ikulu jijini Dar es Salaam.
CHI3
Rais Dkt. Magufuli akimpongeza Mathias Meinrad Chikawe mara baada ya kumuapisha kuwa  Balozi Mpya wa Tanzania nchini Japani
CHI4
Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan Mathias Chikawe akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuamuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
CHI5
Rais Dkt. Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan Mathias Chikawe pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

WAZIRI MAJALIWA AKITETA JAMBO NA SPIKA NDUGAI NA MBUNGE LULIDA

MAJI
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Spika wa Bunge, Job Ndugai  (kushoto)  wakizungumza na Mbunge wa Viti Maalum Riziki Lulida (kulia) kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 19, 2016. (Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu) 

MATUKIO BUNGENI MJINI DODOMA LEO

BU1
 Spika wa Bunge, Job Ndugai akiongozwa na Mpambe wa Bunge kuingia kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma  kuongoza kikao cha kwanza cha  mkutano wa tatu wa Bunge   Aprili 19, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
BU2
Ruth Owenya akiapa kuwa Mbunge  kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma Aprili 19, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
BU3
 Ritta Kabati akiapa kuwa Mbunge kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Aprili 19, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
BU4
Spika wa Bunge Job Ndugai   (kulia) akimwapisha  Ritta Kabati kuwa mbunge kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma  Aprili 19, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
BU5
 Spika wa Bunge, Job Ndugai akimwapisha Waziri Kiongozi wa Zanzibar Mstaafu,  Shamsi Vuai Nahodha kuwa Mbunge kwenye ukumbi wa Bunge  Mjini Dodoma Aprili 10, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
BU6
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza, Waziri Kiongozi  wa Zanzibar  Mstaafu , Shamsi Vuai Nahodha baada ya kuapishwa kuwa Mbunge, Bungeni mjini Dodoma, Aprili 19, 2016. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
BU7
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Bumbuli na Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, January Makamba, bungeni mjini Dodoma Aprili 19, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 

Katibu Mkuu Wizara ya Habari afungua mdahalo wa Vijana kujadili hatma ya ajira kwa vijana nchini

OL1
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifungua mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dar es Salaam
OL2
Mkurugenzi Mkazi Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) nchi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda Bibi. Mary Kawar akizungumza na vijana (hawapo pichani) wakati wa mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na shirikila hilo leo jijini Dar es Salaam.
OL3
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akitoa mada wakati wa mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dar es Salaam
OL4
Mtaalam wa ajira kutoka ILO Bw. Jealous Chirore akichangia mada wakati wa mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika hilo na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dar es Salaam
OL5
Mwakilishi kutoka YUNA – Chuo cha Bogamoyo akiuliza swali wakati wa mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dar es Salaam
OL7
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) nchi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda Bibi. Mary Kawar baada ya kufungua mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dar es Salaam.
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo

SERIKALI KUENDELEA KULINDA KAZI ZA WASANII NCHINI

FIS1
Mkurugenzi wa Elimu kwa mlipa kodi toka Mamlaka ya Mapato    Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo akionesha kwa waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam moja ya CD zilizokamatwa wakati wa msako wa kubaini wale wote wanaojihusisha na uuzaji na usambazaji wa kazi za wasanii bila kuwa na stempu za kodi katika bidhaa za filamu na muziki. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo na mwisho kulia ni Afisa Habari wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bi Mariam Mwayera.
FIS2
Mkurugenzi wa Elimu kwa mlipa kodi toka Mamlaka ya Mapato    Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo (katikati) akitoa wito leo Jijini Dar es salaam  kwa wasambazaji na wauzaji wa kazi za Filamu na muziki kuzingatia sheria na Kanuni zinazosimamia sekta hiyo kwa kuwa Serikali itawachukulia hatua kali wale wote watakaoenda kinyume cha sheria na taratibu zilizopo ikiwemo kutozwa faini isiyopungua milioni tano au kifungo kisichopungua miaka mitatu jela. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo,Kushoto ni Afisa Utamaduni wa Bodi ya filamu Bw. Wilhadi Tairo.
FIS3
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo akifafanua kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mikakati ya Bodi hiyo kuhakiksha kuwa kazi za wasanii wa filamu zinaendana na maadili ya Taifa.kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Richard Kayombo.
FIS4
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Bodi ya Filamu Tanzania ukilenga kueleza Mikakati ya Serikali katika kulinda haki za wasanii wa filamu na Muziki zinalindwa.
( Picha na Frank Mvungi- Maelezo)
……………………………………………………………………………………………………………..
Na Fatma Salum (MAELEZO)
Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeahidi kuendeleza msako wa wafanyabiashara wote wanaouza kazi za filamu na muziki bila kubandikwa stempu halali za kodi ili kuzilinda kazi hizo kwa ajili ya kuwanufaisha wasanii na kuhakikisha Serikali inapata mapato yake.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma kwa Mlipa Kodi kutoka TRA Richard Kayombo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Kayombo amesema TRA kwa kushirikiana na wadau wa tasnia ya muziki na filamu imedhamiria kuhakikisha kuwa bidhaa za filamu na muziki zenye stempu za kodi ndizo zinazoingizwa sokoni ili kulinda kazi za wasanii wa taifa letu dhidi ya dhuluma zinazofanywa na baadhi ya wafanyabiashara.
“Msako huu endelevu utahusisha kukamata bidhaa zote ambazo hazijabandikwa stempu za kodi na kuwachukulia hatua wahusika kwa mujibu wa sheria.” Alieleza Kayombo.
Aidha Kayombo amefafanua kuwa kwa kipindi cha mwezi Februari na Machi 2016, TRA kwa kushirikiana na Dalali wa Mahakama Yono Auction Mart & Company Limited ilifanya msako jijini Dar es Salaam na kukamata jumla ya CD na DVD zenye thamani zaidi ya shilingi Bilioni 1.3 ambazo zilisambazwa bila kufuata sheria hivyo kukwepa kodi ya ushuru ipatayo shilingi Milioni 31.9 na gharama za stempu zaidi ya shilingi Milioni 11.1.
TRA inawatahadharisha wale wote wanaosambaza na kuuza kazi za filamu na muziki ambazo hazijabandikwa stempu kuacha mara moja na kufuata utaratibu wa kupata stempu hizo katika ofisi za TRA ili wawe na uhalali wa kuuza bidhaa hizo kinyume chake hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

No comments :

Post a Comment