Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka
kwa Balozi Mteule wa nchi ya Jamhuri ya Czech hapa nchini Pavel Rezac,
tukio hilo lilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Ikulu jijini Dar es
Salaam Balozi Mteule wa nchi ya Jamhuri ya Czech hapa nchini Pavel
Rezac.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Mteule wa nchi
ya Jamhuri ya Czech hapa nchini Pavel Rezac mara baada ya kukabidhi
hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi mteule kutoka
nchi ya Jamhuri ya Sudani Kusini Mariano Deng Ngor aliyefika Ikulu kwa
ajili ya kuwasilisha hati yake za utambulisho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Mteule wa nchi
ya Jamhuri ya Sudani Kusini Mariano Deng Ngor aliyefika Ikulu kwa ajili
ya kuwasilisha hati yake za utambulisho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka
kwa Balozi Mteule wa Brazil hapa nchini Carlos Alfonso Iglesias Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Mteule wa Brazil
hapa nchini Carlos Alfonso Iglesias Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Mteule wa
Tanzania nchini Kuwait Mahadhi Juma Maalim Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi Mahadhi alifika Ikulu kwa ajili ya kuagana na Mhe. Rais kwa ajili
ya kwenda kuanza kazi yake hiyo rasmi nchini Kuwait.
Kaimu Mnikulu Ngusa Samike kulia
akimkaribisha Balozi Mteule wa Brazil Carlos Alfonso Iglesias Ikulu
jijini Dar es Salaam katikati ni Kaimu Mkuu wa Itifaki James Mbwana
kutoka Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kikanda
na Kimataifa.
PICHA NA IKULU
MADAKTARI NA WAUGUZI JIJINI ARUSHA WAFIKIWA NA LANCET TANZANIA LTD,YAFUNGUA MAABARA YA KISASA JIJINI ARUSHA.
Dixon Busagaga
to Ahmad, Adam, me,
Francisgodwin2., MUHIDIN, Othman, Josephat, Cathbert, Mroki, Maggid,
Haki, John, Robert, Othman, Richard, Deogratius, Yusuf, Mbeya, Luke,
Shamim, Jestina, Maxence, Francis, MR, Khalfans2002
Mtafiti
wa magonjwa mbalimbali Dkt Ahmed Kalebi akizungumza na madaktari na
wauguzi kutoka katika Hospitali mbalimbali za jijini Arusha,wakati wa
warsha iliyofanyika katika jengo ilipo Benki ya ABC.
Baadhi
ya Madaktari na wauguzi katika Hospitali mbalimbali za jijini Arusha
wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Mtafiti wa Magonjwa mbalimbali
Dkt Ahmed Kalebi (hayupo pichani)
Mtafiti Dkt Kalebi akizungumza juu ya ugonjwa a kisukari namna ambavyo umekuwa ukiwasumbua watu wengi kwa sasa.
Madaktari na wauguzi wakifuatilia mada.
Dkt Kalebi akisikiliza maswali kutoka madaktari mara baada ya kuwasilisha mada kuhusu magonjwa mbalimbali
Mganga
Mfawidhi wa Hosptali ya mkoa wa Arusha,Mt Meru ,Dkt Jackline Urioh
akizungumza namna ambavyo watashirikiana na Lancet Tanzania Ltd katika
kutumia maabara ya kisasa iliyofunguliwa jijini Arusha kwa ajili ya
kufanya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali.
Mtafiti
Dkt Ahmed Kalebi (kulia) akimshukuru mganga mfawidhi Dkt Jackline Urioh
mara baada ya kutoa neno kwa niaba ya mganga mkuu wa mkoa katika warsha
hiyo iliyoenda sanjari na ufunguzi wa maabara ya kisasa ya Lancet.
Mmoja wa Madaktari waliohudhuria warsha hiyo akiuliza swali .
Washiriki wa warsha hiyo wakifurahia jambo mara baada ya kupata maelezo mbalimbali kuhusu magonjwa ya Saratani na Kisukari.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
WAZIRI WA CZECH REPUBLIC NA UJUMBE WA WAFANYABIASHARA WATEMBELEA KIWANDA CHA MAZIWA MILKCOM KIGAMBONI
Marian Jureck Waziri wa Kilimo wa
wa Jamhuri ya watu wa Czech Republic akiangalia chakula cha Ng’ombe
wakati alipotembelea mashamba ya ng’ombe na kiwanda cha MilkCom
kinachomilikiwa na makampuni ya OilCom Group kilichopo Kigamboni
wilayani Temeke jijini Dar es salaam akiongozana na ujumbe wa
wafanyabiashara kutoka nchini humo, Ujumbe huo ulikuja nchini kwa lengo
la kuangalia fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania na
ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizi mbili.(PICHA NA JOHN
BUKUKU-FULLSHANGWE-KIGAMBONI)
Marian Jureck Waziri wa Kilimo wa
wa Jamhuri ya watu wa Czech Republic akiongozwa na Mkurugenzi wa
kiwanda cha Milkcom Bw. Salum Nahdi wakati alipokuwa akitembelea kiwanda
hicho.
Baadhi ya ng’ombe katika shabla la kampuni ya MilkCom
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Milkcom
Bw. Salum Nahdi kulia, Mh. Balozi wa Heshima wa Jamhuri ya Czech
Republic nchini Tanzania Mh.John Chaggama na SAid Nahdi Mkurugenzi wa
Makampuni ya OilCom Group wakifurahia jambo wakati wa ziara hiyo ya
ujumbe wa Czech Republic.
Baadhi ya wafanyabiashara hao wakikagua eneo la kukamulia maziwa.
Dk. Sajeev Kumar Meneja wa Shamba
la mifugo akitoa maelezo kwa Marian Jureck Waziri wa Kilimo wa wa
Jamhuri ya watu wa Czech Republic na ujumbe wake wakati alipotembelea
shamba hilo.
Marian Jureck Waziri wa Kilimo wa
wa Jamhuri ya watu wa Czech Republic akiuliza jambo wakati
alipotembelea shamba la ng’ombe la Milkcom.
Meneja wa Shamba la ng’ombe la
Milkcom akitoa maelezo kwa Marian Jureck Waziri wa Kilimo wa wa Jamhuri
ya watu wa Czech Republic na ujumbe wake wakati alipotembekea katika
shamba hilo.
Ng’ombe wa maziwa wakikamuliwa kwa mashine maalum.
Francis Gatara Meneja wa
uzalishaji kiwanda cha maziwa cha Milkcom akitoa maelezo kwa Marian
Jureck Waziri wa Kilimo wa wa Jamhuri ya watu wa Czech Republic wa tatu
kutoka kulia , kulia ni Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Bw. Salim Nahdi.
Marian Jureck Waziri wa Kilimo wa
wa Jamhuri ya watu wa Czech Republic wa pili kutoka kulia na baadhi ya
wafanyabiashara wakiangaliwa pakiti za maziwa ambayo tayari
yameshazalishwa kwa ajili ya kuingizwa kwenye soko.
Marian Jureck Waziri wa Kilimo wa
wa Jamhuri ya watu wa Czech Republic wa pili kutoka kulia na Mkurugenzi
wa kiwanda hicho Salim Nahdi wa tatu kutoka kulia wakionyesha pakiti
za maziwa yaliyokwasha tengenezwa tayari kuingiua kwenye soko.
Marian Jureck Waziri wa Kilimo wa
wa Jamhuri ya watu wa Czech Republic akipokea zawadi kutka kwa Salim
Nahdi Mkurugenzi wa kiwanda cha maziwa cha Milkcom.
Marian Jureck Waziri wa Kilimo wa
wa Jamhuri ya watu wa Czech Republic akiwa katika picha ya pamoja na
uongozi wa kiwanda cha Milkcom na ujumbe wa wafanyabiashara alioongozana
nao.
Ndanda Kosovo azikwa katika makaburi ya Kinondoni leo
SOURCE:http://globalpublishers.co.tz/tazama-picha-za-mazishi-ya-ndanda-kosovo-katika-makaburi-ya-kinondoni/
WAZIRI wa Habari, Vijana, Sanaa,
Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Mh. Paul Makonda wamewaongoza mamia ya waombolezaji katika
shughuli ya mazishi ya staa wa Muziki aliyefariki mwishoni mwa wiki
iliyopita, Ndanda Kosovo ‘Kichaa’ katika Makaburi ya Kinondoni jijini
Dar,
Mwanamuziki huyo Ndanda Kosovo
‘Kichaa’ amezikwa leo Jumatano kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar
ambapo maandalizi yamefanyika kwenye nyumba ya Ubalozi wa Congo DRC
iliyopo Kinondoni-Hananasif jijini.
Dodoo alisema wameamua kumzika
marehemu hapa nchini kufuatia wosia wake alioutoa mbele ya Waziri wa
Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye wakati
akizungumza na wanamuziki wa dansi katika Ukumbi wa Vijana Kinondoni
mwezi uliopita.
Katika kikao hicho Ndanda
alisimama na kusema endapo akifa basi maiti yake izikwe hapa Tanzania
kwa kuwa ndipo mahali alipopatia mafanikio makubwa ya kimuziki na
anahisi ndiyo sehemu ambayo atazikwa na watu wengi kuliko Lubumbashi
alikozaliwa
KUBENEA HAUKUMIA KIFUNGO CHA NJE
Mhe. Said Kubenea– Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA).
………………………………………………………………………………………………………….
Na. Raymond Mushumbusi– Dar es salaam.
Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu mbunge wa Ubungo (CHADEMA) Saeed
Kubenea kifungo cha nje cha miezi mitatu kutokana kosa la kutumia lugha
ya matusi dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda
ambaye sasa ni Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkoa wa Dar es Salaam.
NHC YAFUNGUA OFISI ZAKE ZA MAUZO YA MRADI WA KAWE-711
Pichani
waweza kuona mita chache kutoka mzunguko (round about) ya Kawe kuelekea
Mbezi Beach ya chini, pinda kona kulia kwako utauona Mradi Wa
Kawe-711. Karibu upate maelezo na kuona maendeleo ya mradi.
Unapovuka
mzunguko wa Kawe kuelekea Mbezi Beach ya chini unaweza kuona majengo ya
NHC Kawe -711 yaliyojengwa kwa mpangilio makini kata kulia kwako
utauona mradi huo. Karibu upate maelezo na kuona maendeleo ya mradi.
Majengo
ya mradi wa nyumba za makazi na biashara ya Kawe 711 yaliyojengwa kwa
mpangilio makini yanavyoonekana hivi sasa. Karibu upate maelezo na
kuona maendeleo ya mradi.
Unapochepuka
kulia utakutana na barabara ya vumbi mbele yako majengo ya mradi wa
nyumba za makazi na biashara ya 711 yaliyojengwa kwa mpangilio makini,
hapo ndipo zilipo ofisi za mauzo za mradi huo Karibu upate maelezo na
kuona maendeleo ya mradi.
Geti
la kuingilia kwenye mradi wa nyumba za makazi na biashara ya 711
yaliyojengwa kwa mpangilio makini, hapo ndipo zilipo ofisi za mauzo za
mradi huo. Karibu upate maelezo na kuona maendeleo ya mradi.
Bango la mradi huo
Jengo
la mradi wa nyumba za makazi na biashara ya 711 yaliyojengwa kwa
mpangilio makini, hapo ndipo zilipo ofisi za mauzo za mradi huo .Karibu upate maelezo na kuona maendeleo ya mradi.
Ufikapo
katika jengo hilo utakutana na sura za maafisa mauzo wachangamfu
watakaokuhudumia pale pale na kukuonyesha maendeleo ya mradi na sehemu
nyumba hizo zilipo kiasi kwamba sasa hautasumbuka kwenda mjini na
baadaye kuelekezwa zilipo site.
Ufikapo
katika jengo hilo utakutana na sura za maafisa mauzo wachangamfu
watakaokuhudumia pale pale na kukuonyesha maendeleo ya mradi na sehemu
nyumba hizo zilipo kiasi kwamba sasa hautasumbuka kwenda mjini na
baadaye kuelekezwa zilipo site.
Ofisi
za mauzo za mradi wa NHC Kawe 711 zinavyoonekana utakatibishwa maafisa
mauzo wachangamfu watakaokuhudumia pale pale na kukuonyesha maendeleo ya
mradi na sehemu nyumba hizo zilipo kiasi kwamba sasa hautasumbuka
kwenda mjini na baadaye kuelekezwa zilipo site.
Ofisi
za mauzo za mradi wa NHC Kawe 711 zinavyoonekana utakatibishwa maafisa
mauzo wachangamfu watakaokuhudumia pale pale na kukuonyesha maendeleo ya
mradi na sehemu nyumba hizo zilipo kiasi kwamba sasa hautasumbuka
kwenda mjini na baadaye kuelekezwa zilipo site.
Ofisi
za mauzo za mradi wa NHC Kawe 711 zinavyoonekana utakatibishwa maafisa
mauzo wachangamfu watakaokuhudumia pale pale na kukuonyesha maendeleo ya
mradi na sehemu nyumba hizo zilipo kiasi kwamba sasa hautasumbuka
kwenda mjini na baadaye kuelekezwa zilipo site.
UKATILI WA KIJINSIA SOKO LA TEMEKE STEREO JIJINI DAR ES SALAAM BADO KUNA CHANGAMOTO KUBWA
Katibu
wa Soko la Temeke AStereo, Omary Seif Mangilile akizungumza katika
kapmpeni ya kuongeza uelewa dhidi ya ukatili wa kijinsia masokoni
iliyofanyika katika soko la Temeke Stereo Dar es Salaam leo asubuhi.
Kulia ni Meneja wa Mradi huo wa kupinga ukatili huo, Grace Mateh kutoka
Shirika la Equality for Growth (EfG). Hata hivyo katika soko hilo bado
kunachangamoto kubwa ya vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia hasa
kwenye eneo la wauza mihogo kama ilivyoelezwa na baadhi ya
wafanyabiashara katika soko hilo.
Ofisa Ufuatiliaji na Tathimini wa EfG, Julius Samora akifafanua mambo kadhaa yanayohusu ukatili wa kijinsia katika kampeni hiyo.
Mwezeshaji katika kampeni hiyo Maulid Sufian akiongoza kupokea maswali na kujibu.
Wasanii wa kundi la Machozi la Temeke wakitoa burudani kwenye kampeni hiyo.
Wananchi, wafanyabiasha na wadau wengine wakiwa kwenye kampeni hiyo.
Wananchi, wafanyabiasha na wadau wengine wakiwa kwenye kampeni hiyo.
WABUNGE WA AFRIKAMASHARIKI WATEMBELEA THE GUARDIAN
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
……………………………………………………..
Wabunge
wa bunge la Arika Mashariki, (EALA), kutokaTanzania, wameendelea na
ziara yao ya kutembelea vyombovya habari hapa nchini, ikiwa ni mkakati
wa Jumuiya hiyo, kushirikisha vyombo vya habari ili
kuwafahamishawananchi wa nchi hizo manufaa ya jumuiya hiyo kwao.
LeoAprili 13, 2016, wabunge hao wakiongiozwa na Mwenyekiti wao Mh.
Makongoro Nyerere, wametembelea kampuni ya The Guardian, wachapishaji wa
magazeti ya The Guardian, Nipashe na Lete Raha, na kupata fursa ya
kuelezwa shughuli zifanywazo na waandishi wa habarikwenye kampuni hiyo
ambapo walitembelea kitengo cha habari mtandao, (E-NEWS), kitengo cha
usanifu gazeti na kumalizia kwa mkutano wa kubadilishana mawazobaina ya
wabunge hao na uongozi wa chumba cha habari cha The Guardian. Pichani,
msanifu wa gazeti la The Guardian, Ben Mgana (aliyekaa), akiwaonyesha
jinsi gazeti hilo linavyoandaliwa kabla ya kuchapishwa. Wakwanza kushoto
ni Mhari Mtendaji wa gazeti hilo, Wallace Maugo, Mkuu wa chumba cha
Habari cha The Guardian, Jesse Kwayu, (wapili kushoto) na wabunge wa
hilo wakiongozwa na wmenyekiti wao Mh. Makongoro Nyerere (watatu kulia)
MhaririMtendaji
wa The Guardian, Wallace Mauggo, (watatu kushoto) na Mhariri Mkuu wa
Chumba cha Habari cha The Guardian Limited, Bw. Jesse Kwayu)
wakiwaonyesha wabunge hao baadhi ya magazeti yanayochapishwa na kampuni
hiyo
Mwenyekiti
wa wabunge wa EALA-Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, 9wapili kulia),
akisalimianana Mkuu wa kitengo cha habari mtandao (E-NEWS), cha The
Guardian Limited, Mashaka Mgeta, wakati wabunge hao walipotembelea
chumba cha Habari cha The Guardian Mikocheni jijini Dar es Salaam
MAKABIDHIANO YA OFISI YA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt.Khalid Salum Mohammed (kulia) akikabidhiana
Ofisi na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora
Dkt.Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini leo katika ukumbi wa Tume ya Mipango
Vuga Mjimkongwe wa Zanzibar baada ya uteuzi uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheun,
Aliyekuwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji
Makeme Mwadini akitoa shukurani kwa wafanyakazi wa tume ya mipango
wakati wa makabidhiano ya Ofisi na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Khalid Salum Mohammed katika ukumbi wa Tume ya Mipango Vuga Mji Mkonge wa Zanzibar baada ya uteuzi uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheun.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt.Khalid Salum Mohammed alipozungumza na
wafanyakazi wa Tume ya Mipango na kwataka kuwa na mashikiano katika kazi
kulitea Maendeleo Taifa letu wakati wa makabidhiano ya Ofisi leo na Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini katika ukumbi wa Tume ya Mipango Vuga Mji Mkongwe wa Zanzibar baada ya uteuzi uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheun,
Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini akiagana na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Khalid Salum Mohammed baada ya makabidhiano ya Ofisi katika viwanja vya Ofisi ya Tume ya Mipango leo Vuga Mji Mkongwe wa Zanzibar baada ya uteuzi uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheun .[Picha na Ikulu.]
Maboresho ya sheria ya Vyama vya Siasa ndio Mkombozi wa Siasa nchini- Mhe. jenister Mhagama
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Mhe. Jaji francis S. K Mutungi pamoja
na Maaafisa Wandamizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakiwa
nje ya ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam Leo
kabla ya kuanza kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria
cha kupitisha bajeti ya mwaka 2016/2017 ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa.
Waziri
wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
akijibu hoja za wajumbe kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere
Jijini dar es salaam.
Mhe.
Dkt Abdallah Possi, Naibu Waziri (Ofisi ya Waziri Mkuu) Sera, Bunge,
Kazi , Vijana, Ajira na Ulemavu akiteta jambo na Msajili wa vyama vya
Siasa Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi kwenye kikao cha kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya mwaka 2016/2017 ya
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi
wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam.
Msajili
wa Vyama vya Siasa Nchini Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi akitoa
ufafanuzi wa hoja za wajumbe kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti yam waka 2016/2017 ya Ofisi ya
Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa Saadan
wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam. Kushoto ni Waziri wa Sera,
Bunge, Kazi , Vijana, Ajira na Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na Manaibu
waziri ,Mhe Antony P. Mavunde na Mhe. Dkt Abdallah Possi
Mjumbe
wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe Richard Ndassa
akiwasilisha hoja kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba
na Sheria cha kupitisha bajeti ya mwaka 2016/2017 ya Ofisi ya Msajili
wa Vyama vya Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa Saadan wa
Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam. Kulia ni wajumbe wa kamati.
Waziri
wa Sera, Bunge, Kazi , Vijana, Ajira na Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
akijibu hoja za wajumbe kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere
Jijini dar es salaam. Kulia ni Mhe. Dkt Abdallah Possi, Naibu waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu .
Angelina
Sanga, Katibu kiongozi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria
akiwapitisha wajumbe (hawapo pichani) kwenye vifungu vya bajeti ya
mwaka 2016/2017 ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwenye kikao cha
kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa
Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam.
Waadhi
ya wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria
wakifuatilia kwa makini mawasilisho ya bajeti ya mwaka 2016/2017 ya
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya Ofisi ya Msajili wa
Vyama vya Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu
Nyerere Jijini dar es salaam
CHUO KIKUU ARDHI CHAWAPA MWONGOZO WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI ZA JIJI LA DAR NAMNA YA KUJIUNGA NA MASOMO YA ELIMU YA JUU KULINGANA NA UFAULU WAO.
Mtaalam
wa Jiografia kutoka Chuo Kikuu Ardhi Dkt. Mlenge Fanuel Mgendi
akiwahamasisha wanafunzi wa kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya
Wasichana ya Jangwani kupenda kusoma na kuweka bidii katika masomo
ambayo wanauwezo nayo ili yawasaidie kuendelea na Elimu ya Juu katika
chuo Kikuu Ardhi leo jijini Dar es salaam. Chuo Kikuu Ardhi kinaendesha
Programu ya utoaji elimu kwa wanafunzi wa sekondari katika shule
mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia kufanya uchaguzi sahihi wa kozi za
masomo wanazotarajia kuendelea nazo pindi watakapohitimu masomo ya elimu
ya Sekondari.
Mwanataaluma
wa Chuo Kikuu Ardhi Bi. Latifa Litwe (kushoto) akitoa elimu kwa
wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani namna ambavyo
Chuo Kikuu Ardhi kinawajengea uwezo kielimu wanafunzi wanaosoma katika
chuo hicho kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi na majanga mbalimbali
pamoja na ushauri kuhusu sekta ya Ardhi kwa ujumla hapa nchini ikiwemo
uhifadhi wa Ardhi na Sayansi ya Udongo.
Baadhi
ya wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Wasichana ya Jangwani
wakiangalia na kufurahishwa na moja ya Kazi ya Ubunifu wa Majengo na
mitaa iliyofanywa na wanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi mwaka wan nne leo
jijini Dar es salaam.
Mwanataaluma
wa Chuo Kikuu Ardhi Bw. Dennis Tesha akiwaeleke za wanafunzi wa shule
ya wasichana ya Jangwani namna bora kuchagua masomo yao ya baadaye
kulingana na sifa walizonazo watakapotaka kujiunga na vyuo vikuu hapa
nchini pamoja na kazi watakazofanya mara baada ya kuhitimu kulingana na
masomo yao.
Moja ya kazi ya Ubunifu wa jengo la ghorofa lilobuniwa na mwanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi.
Baadhi
ya wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Wasichana ya Jangwani
wakifurahia jambo mara baada ya kuangalia moja ya kazi ya ubunifu wa
majengo iliyofanywa na wanafunzi wa mwaka wan ne wa Chuo Kikuu Ardhi
walipokuwa wakizungumza na Afisa Uhusiano wa Chuo hicho Bi. Khadija leo
jijini Dar es salaam.
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA MWENDESHA MASHTAKA WA KIMATAIFA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na mwendesha
Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa Bw. Serge Prammertz wakati Bw. Serge
alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April
13,2016 kwa ajili ya kujitambulisha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na mwendesha
Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa Bw. Serge Prammertz wakati Bw. Serge
alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April
13,2016 kwa ajili ya kujitambulisha.
(Picha na OMR)
Mashindano ya Darts Afrika Mashariki kuanza Mwezi huu
Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo
wa Vishale Tanzania (TADA) Bi. Subira Waziri akiongea na waandishi wa
habari hawapo pichani leo jijini Dar es salaam kuhusu kuanza kwa
mashindano ya Afrika mashariki huku Tanzania ikiwa mwenyeji wa
mashindano hayo kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bi. Redempta
Mwebesa.
Waandishi wa Habari wakifuatilia
kwa makini mkutano ulioandaliwa na viongozi wa Chama cha Mchezo wa
Vishale Tanzania( TADA) hawapo pichani kuzungumzia kuhusu kuanza kwa
mashindano ya Afrika mashariki yanayotarajiwa kuanza April 29 mwaka
huu.
WAZIRI MHAGAMA AAGIZA IDARA YA MAAFA KUFANYA TATHIMINI YA MAAFA BAHI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
akiwasilisha bajeti ya ofisi yake wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Katiba na Sheria ya Kupitisha Bajeti uliofanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam Aprili 12,
2016
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ya kupitisha bajeti wakifuatilia
bajeti ya ofisi hiyo walipokutana kuijadili na kuipitisha bajeti hiyo
katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam Aprili
12, 2016.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na
Usimamizi wa Rasilimaliwatu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Issa Nchansi
akifafanua jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba
na Sheria ya kupitisha bajeti kilichofanyika tarehe 12 Aprili, 2016
katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kikao cha Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ya Kupitisha Bajeti Mhe. Mohamed
Mchengerwa ambaye ni mbunge wa Rufiji (katikati) akieleza jambo wakati
wa kikao hicho walipokutana kujadili Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
Aprili 12, 2016 katikaUkumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Dar
es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa
Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen Mbazi Msuya (katikati) akifuatilia
bajeti ya Idara yake pamoja na wataalamu wake kushoto kwake ni Charles
Msangi na kulia ni Daniel Alfei wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Katiba na Sheria ya Kupitisha Bajeti Aprili 12, 2016.
(Picha Zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WTA awards Travelstart Tanzania best travel agency
Abbas Rajani Managing Director
Travelstart Tanzania (C) shows its Best Travel Agency in Tanzania award
at the annual World Travel Awards (WTA) Grand Final Gala Ceremony 2016
in Zanzibar last weekend. Looking on Left is Former Big Brother
Contender who was the Master of Ceremony Abby Plaatjes and looking from
Right is the Usher of the WTA.
Abbas Rajani Managing Director
Travelstart Tanzania (C) shows its Best Travel Agency in Tanzania award
at the annual World Travel Awards (WTA) Grand Final Gala Ceremony 2016
in Zanzibar last weekend.
……………………………………………………………………………………………………………..
By Staff Writer
Travelstart Tanzania has won the
prestigious Best Travel Agency in Tanzania at the annual World Travel
Awards (WTA) Grand Final Gala Ceremony 2016 held over the weekend in
Zanzibar.
Each year World Travel Award
covers the globe with a series of regional gala ceremonies staged to
recognise and celebrate individual and collective successes within each
geographical region.
WTAs is recognised as the
“Oscars” of the global travel and tourism industry for being the most
prestigious, comprehensive and sought after awards programme in the
industry.
The award, which is judged by an
international jury of hospitality experts and peers, was presented to
Travelstart Tanzania, Tanzania’s only online travel agency.
Speaking soon after receiving
the award, Travelstart Tanzania Managing Director Abbas Rajani said
that it is happy to be recognised by the World Travel Awards panel of
experts and win the award.
He also said that the travel firm, they will continue on providing consumers lower fares as compared to other in the market.
“Being a young and progressive
company, Travelstart is indeed a market leader in travel affordability,
style and range in choice and service delivery excellence,” he said.
He pointed out that Travelstart
Tanzania is dedicated to transforming the travel booking industry by
tackling the complexities that travel for both travellers and suppliers
face including solving real problems to tackle the growing and vibrant
travel industry in Tanzania.
He underscored that Travelstart
will addresses complexities in the African travel market by directly
accessing local supply, solving language and currency problems as well
as the diverse plethora of payment methods.
He went further saying that
due to technology platform which meets the need of travel bookers on
mobile and desktop devices, Travelstart are joy on delivering an
exceptional service experience to its customers.
Travelstart Tanzania’s award for
being the leading travel agency in the country; the Travelstart Group,
which has offices in Cape Town, Dubai, Istanbul, Lagos, Cairo and Dar es
Salaam, walked away with ‘Africa’s Leading Online Travel Agency’ at the
2016 World Travel Awards.
However, Travelstart founded in 1999 in Sweden, started up in South Africa in 2006 to focus on the emerging market opportunity.
Travelstart provides travellers
with real-time access to thousands of flights from all carriers and
serves 2 million monthly users in 16 countries. Travelstart has offices
in Cape Town, Dubai, Istanbul, Lagos, Cairo and Dar es Salaam. For more
information, please visit
Meanwhile, World Travel Awards
was established in 1993 to acknowledge, reward and celebrate excellence
across all sectors of the tourism industry. Today, the World Travel
Awards brand is recognised globally as the ultimate hallmark of quality,
with winners setting the benchmark to which all others aspire. In 2016,
World Travel Awards will celebrate its historic 23rd anniversary year.
Heart Marathon kufanyika Aprili 26 Mwaka huu
Mratibu wa Heart Marathon Dkt. Omary
Chillo (katikati) akiongea na waandishi wa habari kuhusu mashindano ya
mbio maalum za kupambana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza
zijulikanazo kama Heart Marathoni zinazotarajiwa kufanyika Aprili 26
mwaka huu jijini Dar es salaam, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati
ya maandalizi ya Heart Marathon Dkt. Chaka Halfani na kulia kwake ni
Kaimu Katibu Chama cha Riadha Tanzania Bi.Ombeni Zavala.
Mratibu wa Heart Marathon Dkt. Omary Chillo (wa kwanza
kulia) akiongea na waandishi wa habari kuhusu mashindano ya mbio maalum
za kupambana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza zijulikanazo kama
Heart Marathoni zinazotarajiwa kufanyika Aprili 26 mwaka huu jijini Dar
es salaam, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Heart
Marathon Dkt. Chaka Halfani na Mratibu Msaidizi Heart Marathon
Bi.Catherine ikangaa.
4 Mwenyekiti wa Kamati ya
maandalizi ya Heart Marathon Dkt. Chaka Halfani akionyesha kwa
waandishi wa habari namba watakazopewa washiriki wa mbio maalum za
kupambana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza zijulikanazo kama Heart
Marathoni zinazotarajiwa kufanyika Aprili 26 mwaka huu jijini Dar es
salaam,kulia kwake ni.Mratibu wa Heart Marathon Dkt. Omary Chillo na
Kaimu Katibu Chama cha Riadha Tanzania Bi.Ombeni Zavala .
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Heart Marathon Dkt.
Chaka Halfani akionyesha kwa waandishi wa habari fulana watakazovaa
washiriki wa mbio maalum za kupambana na ongezeko la magonjwa
yasiyoambukiza zijulikanazo kama Heart Marathoni zinazotarajiwa
kufanyika Aprili 26 mwaka huu jijini Dar es salaam,kulia kwake
ni.Mratibu wa Heart Marathon Dkt. Omary Chillo.(Picha na Lorietha
Laurence-Maelezo).
…………………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………………
NA Beatrice Lyimo-MAELEZO
Taasisi ya Tanzania Health
Summit imeandaa mbio maalumu za kupambana na ongezeko la magonjwa
yasioambukiza yajulikanayo kama Heart Marathon zitakazofanyika Aprili
26, 2016 katika viwanjwa vya michezo vya Chuo Kikuu jijini Dar es
salaam.
Hayo yamesemwa na Mratibu
Kamati ya Maandalizi ya Mbio hizo Dkt. Omary Chillo ambapo amesema kuwa
lengo lake ni kusaidia juhudi za Serikali na wadau wa Sekta ya Afya
kupunguza tatizo linalokuwa kwa kasi la magonjwa yasioambukizwa hapa
nchini.
“Watanzania wote kwa ujumla
tunawaalika kushiriki katika mbio za Heart Marathon zitakazoambatana na
upimaji wa magonjwa yasiyoambukizwa na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa
ugonjwa wa Kisukari, Shinikizo la Damu, Uwiano wa urefu na uzito, wingi
wa mafuta mwilini pamoja na Saratani ya matiti” alisema Dkt. Chillo.
Amesema mbio hizo zinatarajiwa
kuwa na washiriki zaidi ya 2,000 kutoka taasisi, makampuni, mashirika,
familia na jamii kwa ujumla, rika tofauti ikiwemo watoto, vijana na
wazee, makundi ya walemavu na watu wenye magonjwa yasioambukiza
watashiriki.
Aidha, Dkt. Chillo ameongeza
kuwa mbio hizo zimegawanywa kwa umbali tofauti ambazo ni mbio ndefu za
Kilometa 21.1 kwa ajili ya wakimbiaji wazoefu, kilometa 10 kwa
wakimbiaji wa kati, Kilometa 5 wakimbiaji wa kawaida, kifamilia na
kampuni pamoja na mbio za watoto chini ya miaka 12 watakimbia umbali wa
mita 700.
Kauli mbiu kwa mwaka huu katika mbio maalumu za kupambana na ongezeko la magonjwa hayo ni “Epuka magonjwa yasioambukiza”
Viingilio katika mbio hizo
maalumu zitakuwa kuanzia elfu tano kwa watoto wa chini ya umri wa mika
13 hadi Shilingi 10,000 kwa mtu mmoja ambapo watu wenye ulemavu
hawatalipia kiingilio.
WARSHA YA WADAU WA MAZINGIRA ILIYOANDALIWA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAFANYIKA.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akifungua warsha ya
wadau wa Mazingir wa ndani na nje ya Nchi iliyoandaliwa na Ofisi ya
Makamu wa Rais juu ya kujadili jinsi Wafadhili wanavyoweza kusaidia
Ofisi katika kuimarisha mambo mbalimbali ya mazingira.
Balozi wa Ujerumani Nchini
Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa Kundi la Washirika wa Maendeleo
wanaojihusisha na Mazingira hapa Nchini Mh. Egon Kochanke akiongea
wakati wa warsha hiyo.
. Sehemu ya Wahudhuriaji wa
Warsha hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh.
January Makamba(hayupo pichani) alipokuwa akifungua warsha hiyo.
Sehemu ya Wahudhuriaji wa Warsha
hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba(hayupo pichani) alipokuwa akifungua warsha hiyo.
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA KONGAMANO LA WAFANYABIASHARA KATI YA TANZANIA NA OMAN
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akifungua Kongamano la Uwekazaji kwa Wafanyabiashara baina ya Tanzania
na Oman kuhusu kuangalia fursa za uwekezaji katika Nyanja mbalimbali za
kiuchumi kati ya Nchi mbili hizo, Kongamano hilo limefunguliwa leo April
13,2016 katika Hoteli ya Hyatt Regence Dar es salaam.
Washiriki
wa Kongamano la Uwekezaji kiuchumi kati ya Tanzania na Oman
wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan alipokua akifungua Kongamano hilo kuhusu kuangalia
fursa za uwekezaji katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi baina ya Nchi
mbili hizo, Kongamano hilo limefunguliwa leo April 13,2016 katika Hoteli
ya Hyatt Regence Dar es salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Uwekazaji kwa
Wafanyabiashara baina ya Tanzania na Oman kuhusu kuangalia fursa za
uwekezaji katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi kati ya Nchi mbili hizo
baada ya kufungua Kongamano hilo leo April 13,2016 katika Hoteli ya
Hyatt Regence Dar es salaam.Picha na OMR
Mette-Marit aitaka jamii kuwa na mtazamo tofauti kwa watu wanaoishi na UKIMWI
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Katika
kuhakikisha watu wanaoishi na UKIMWI wanaishi kwa furaha bila
kunyanyapaliwa na watu wanaowazunguka, jamii imetakiwa kuwa na mtazamo
tofauti kwa watu wanaoishi na ugonjwa huo.
Hayo
yalisemwa na mke wa mtoto wa mfalme wa Norway, Mette-Marit ambaye pia ni
balozi kimataifa wa Shirika la Umoja la kupambana na HIV na UKIMWI
(UNAIDS) wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kazi
anazozifanya kwa UNAIDS kama balozi ambaye anazunguka maeneo mbalimbali
duniani ili kuelimisha jamii kuhusu UKIMWI.
Mette-Marrit
alisema kuwa watu wenye UKIMWI ni kama watu wengine hivyo wana haki ya
kupata huduma bila kunyanyapaliwa ili waweze kuishi kwa uhuru kama watu
wengine na ili kufanikisha hilo ni wajibu wa kila mtu kuwasaidia
waathirika.
“Watu
kuwa na UKIMWI sio mwisho wa maisha inatakiwa kwanza jami kuwa na
mtazamo tofauti na inatakiwa kila mtu kusaidia mapambano ya UKIMWI sio
jambo la mtu mmoja mmoja,” alisema Mette-Marit.
Balozi
wa Kimataifa wa UNAIDS, Mette-Marit akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu kazi anazofanya kama balozi wa UNAIDS kwa kipindi cha miaka 10
tangu aanze kazi hiyo.
(Picha zote na Rabi Hume, Modewjiblog)
Nae
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), Dkt. Fatma
Mrisho alisema Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ili
kupambana na UKIMWI lakini pia ili kufanikisha mapambano hayo wanahitaji
kushirikiana na taasisi ambazo zitawasaidia katika mapambano hayo.
Lakini
pia Dkt. Mrisho amezitaka serikali za mitaa kuacha kusubiri mpaka
serikali imepeleke pesa ndiyo wawasaidie watu wanaoishi na UKIMWI na
hivyo waweke utaratibu wa kutumia sehemu ya mapato yao ili kusaidia
mapambano hayo.
“Serikali
haijalala katika mapambano tunahitaji kushirikiana na taasisi ambazo
zinatusaidia kupunguza maambukizi mapya na tunaona Mette-Marit amekuwa
akifanya jambo zuri anazunguka sehemu nyingi ili kusaidia kupunguza
maamukizi mapya ya UKIMWI,” alisema Dkt. Mrisho.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), Dkt. Fatma Mrisho
akizungumzia kuhusu juhudi zinazofanywa na serikali katika mapambano ya
UKIMWI.
Mkurugenzi
mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na Ukimwi, UNAIDS
nchini Tanzania, Warren Naamara akizungumzia ugonjwa wa UKIMWI.








No comments :
Post a Comment