Tuesday, April 19, 2016

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF), WATOA ELIMU KWA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NCHINI

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafnyakazi, WCF, Masha Mshomba, akizungumza wakati wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini, na kufanyika makao makuu ya Mfuko, barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam Aprili 19, 2016. Lengo la semina hiyo ilikuwa ni kutoa elimu kwa viongozi hao juu ya shughuli za Mfuko na faida ya wafanyakazi kupatiwa fidia endapo patatokea madhara awapo kazini. Wengine pichani ni mgeni rasmi, Pendo Z.Berege, (Mwakilishi wa Msajili wa vyama vya afanyakazi na waajiri, na Peter J. Mbelwa kutoka Mamlaka ya Udhibiti na usimamizi wa sekta ya hifadhi ya jamii, (SSRA).
 
 NA K-VIS MEDIA
MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, umeendesha semina ya siku moja kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini, ili kutoa elimu juu ya shughuli za Mfuko na wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi wao katika kuwalipia michango ya mwezi.
Semina hiyo iliyofanyika makao makuu ya Mfuko, barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam, Aprili 19, 2016, ilifunguliwa na mwakilishi wa Msajili wa vyama vya wafanyakazi na waajiri, Bi.Pendo Z.Berege.
Katika hotuba yake, Bi. Berege alieleza umuhimu wa waajiri kuwalipia michango wafanyakazi wake kama sheria inavyotaka, ili kuwawekea akiba pindi wapatwapo na majanga wakiwa kazini.
Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi ni taasisi ya serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi No. 20 ya mwaka 2008.
Akiwakaribisha wana semina kwenye semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Msomba alisema, Mfuko umeamua kuandaa semina hiyo ili kutoa elimu zaidi kwa wafanyakazi na kwa kutambua kuwa viongozi wa wafanyakazi ndio wadau wakuu wa Mfuko huo, semina hiyo itawasaidia kujua kazi za Mfuko lakini pia wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi katika kutoa michango ya kila mwezi.
Akitoa mada juu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Sebera Fulgence, alisema, Mfuko huo upo kisheria ili kutoa fidia kwa wafanyakazi waumiapo kazini.
Naye Bi.Amina Likungwala kutoka WCF, amesema katika mada yake ya Wajibu wa Vyama vya Wafanyakazi ambapo alisema, ni wajibu wa vyama kutoa elimu kwa wanachama wao ambao ni wafanyakazi lakini pia kuwaeleza waajiri umuhimu wa kutoa michango kwa wakati 
 Mshiriki akisoma kijitabu chenye maelezo ya kina kinachofafanua majibu ya maswali ya mara kwa mara ambayo wadau wanataka kujua kuhusu WCF


 Mgeni rasmi, Bi.Pendo Z.Berege akifuangua semina hiyo
 Bi Amina Likungwala kutoka WCF, akitoa mada kuhusu wajibu wa vyama vya wafanyakazi
 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Sebera Fulgence, akitoa mada "Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF)
 Mgeni rasmi, Bi. Pendo Z.Berege(kushoto) na Mkuu wa kitengo cha Ukauzi wa ndani cha Mamlaka ya Udhibiti na usimamizi wa sekta ya hifadhi ya jamii, (SSRA).Peter J. Mbelwa, wakiteta jambo
 
 Majadiliano yakiendelea
 Mmoja wa washiriki wa semina akizungumza kwenye kipindi cha majadiliano cha semina hiyo
 Baadhi ya wafanyakazi wa WCF wakichykua taarifa muhimu
Mshiriki akifuatilia kwa makini

MAONI; Kwa watumiaji wa barabara ya Bagamoyo watakumbuka kuwa nyakati za asubuhi na jioni ambapo idadi kubwa ya magari huwa barabarani kuwapeleka na kuwaruudisha watu kwenye shughuli za ujenzi wa taifa foleni ilikuwa kubwa ya kupindukia hususan kipande cha kutoka Maji Machafu, Kijitonyama hadi Morocco. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuliona hilo, aliagiza fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe za Uhuru wa Tanganyika, zipelekwe kufanya kazi ya upanuzi wa barabara hiyo, ili kupunguza adha ya foleni kwenye eneo hilo. Hivi sasa sehemu ya upanuzi wa barabara hiyo imekamilika na huwezi kuamini hata vipindi hivyo vya msongamano wa magari vijulikanavyo kwa kimombo kama "Rush Hour" sasa si tatizo tena, kama ambavyo picha hii iliyopigwa mapema leo Aprili 19, 2016 majira ya saa 1;30 inavyoonyesha hapa ilikuwa maeneo ya Victoria kuelekea Morocco. Big up JPM kwa uamuzi sahihi

No comments :

Post a Comment