Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) akiwa ameongozana
na Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang Jiannan
(kuahoto) mara baada ya kumpokea katika viwanja vya Mahakama ya Rufaa
leo jijini Dar es salaam. Mhe. Zhang Jiannan pamoja na ujumbe wake yupo
nchini kwa ziara ya kikazi kwenye Mahakama ya Tanzania kwa lengo la
kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi na kuimarisha ushirikiano baina ya
Mahakama ya Tanzania na China.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) akisalimiana
na baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China mara
baada ya kuwakaribisha Mahakama ya Rufaa leo jijini Dar es salaam.
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati) akizungumza
wakati wa mkutano wa pamoja kati ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
na Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China uliolenga kukuza ushirikiano
na kubadilishana uzoefu wa utendaji wa Mahakama za Tanzania na China
leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano wa pamoja ulioongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania na Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China.
Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na wale wa Mahakam Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China wakibadilisha
uzoefu wa shughuli za kimahakama na masuala mbalimbali ya utendaji
wakati wa mkutano wa pamoja ulioongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania na Jaji
wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China jijini Dar es salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang Jiannan
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) akimweleza jambo Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang Jiannan wakati wa mkutano huo.
Jaji
wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang (kushoto)
akieleza namna Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China inavyofanya kazi
leo jijini Dar es salaam wakati wa kikao cha pamoja kilichowahusisha
Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na China. Wengine ni Jaji Mkuu wa
Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila.
Jaji
wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang (kushoto)
akipokea zawadi ya kinyago kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.
Mohammed Chande Othman.
Jaji
wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang (kushoto) akiwa
katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohammed Chande
Othman mbele ya Jengo la Mahakama ya Rufaa.
Jaji
Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Lila(kulia) akimweleza
jambo jaji wa Mahakamu Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China mara baada ya
kumkaribisha Ofisini kwake Mahakama Kuu leo jijini Dar es salaam.
Jaji
Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Lila(kulia) akiwa katika
mazungumzo na Jaji wa Mahakama Kuu ya China na baadhi ya Majaji kutoka
Mahakama hiyo waliomtembelea Ofisini kwake Mahakama Kuu jijini Dar es
salaam.
Jaji wa
Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang (wa pili kutoka
kushoto mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania
Mhe. Mohammed Chande Othman (katikati) na baadhi ya watendaji wa
Mahakama ya Tanzania mbele ya Jengo la Mahakama ya Rufaa leo jijini Dar
es salaam.
Jaji wa Mahakama
Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang ( kushoto) akiagana na
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohammed Chande Othman (kulia) mara baada ya
kukutana na kufanya mazungumzo naye leo jijini Dar es salaam.
Picha/Aron Msigwa.
……………………………………………………………………………………
Na Mwandishi- Mahakama ya Tanzania
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Juu
Nchini China Mheshimiwa Zhang Jiannan yuko Nchini kwa ziara ya kikazi
yenye lengo la kuimarisha uhusiano na ushirikiano uliopo baina ya nchi
za Tanzania na China.
Katika ziara yake Nchini,
Mheshimiwa Jiannan ambaye anamwakilisha Jaji Mkuu wa China, leo
alikutana na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande
Othman na kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi wa Mahakama zao.
Akizungumzia changamoto za
Mahakama nchini China, Mheshimiwa Jiannan alisema hivi sasa Mahakama za
China zinakabiliwa na upungufu wa Majaji ikilinganishwa na idadi ya kesi
zinazosajiliwa.
Kwa Upande wake, Jaji Mkuu wa
Tanzania alisema baadhi ya changamoto zinazoikabili Mahakama ya Tanzania
ni pamoja na upungufu wa Mahakama za mwanzo.
Alisema ili kukabiliana na
upungufu huo, Tanzania inahitaji kuwa na Mahakama za Mwanzo 3000 nchi
nzima. Hivi sasa kuna Mahakama za Mwanzo karibu 960 nchini kote ambazo
hazitoshi ikilinganishwa na Idadi ya kata zilizopo Nnchi mzima.Jaji Mkuu
wa Tanzania alimshukuru Jaji Mkuu Kiongozi wa China kwa kuitembele
Mahakama ya Tanzania.
Katika ziara yake nchini, Jaji Jiannan ameongoza ujumbe wa Majaji na
Wizara yakemea mauaji ya mtoto sumbawanga
Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na watoto inalaani vikali tukio La mauaji ya mtoto
wa kike, umri miaka 9, ambaye alininajisiwa kwa zamu na watu
wasiojulikana, na hatimaye kumkata mapanga yaliyosababisha kuuawa kwa
mtoto huyo mdogo, katika kijiji cha Kapanga, wilaya ya Sumbawanga mkoani
Rukwa.
Madiwani Wete Kisiwani Pemba wala kiapo kupambana na wakwepa kodi
Na Masanja Mabula –Pemba
MADIWANI wa wadi kumi
zinazounda Baraza la Mji Wete Kisiwani Pemba , wamekula kiapo cha utii
na kuahidi kushirikiana na Uongozi wa Baraza hilo katika kupambana
na wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi
Watendaji wengine wa Mahakama wanne kutoka nchini China.
Halmashauri yatenga bajeti ya milioni 162 kuisaidia shule ya walemavu
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
iliyopo Mkoa wa Lindi imetenga jumla ya shilingi milioni 162 katika
mwaka wa fedha 2016/17 kwa ajili ya kuisaidia shule ya Msingi Nyangao.
Hayo yamesemwa leo na
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi. Olliver Vavunge alipokuwa
akikanusha kuhusu madai ya wazazi kutaka shule hiyo ifungwe kwa sababu
ya ukosefu wa huduma muhimu
Uchukuzi SC netiboli kuivaa CDA Dodoma kesho
Kocha wa soka Elutery Muholeli (wanne kulia) mwenye jezi za manjano akitoa maelekezo kwa wachezaji.
Mazoezi mpira wa Netball yakiendelea
Matalena Mhagama (mwenye fulana nyeupe kulia) akisubiri mpira.
…………………………………………………………………………………………………………
Mwandishi Wetu
TIMU ya netiboli ya Uchukuzi SC
iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kesho
itarusha karata yake ya kwanza kwa kuumana na wenyeji CDA Dodoma katika
mchezo wa netiboli, utakaofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri..
TAMKO KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI LILILOTOLEWA NA MHE. UMMY MWALIMU WAZIRI WA AFYA LEO
Kama mnavyofahamu, Serikali
kupitia Wizara yangu imeweka utaratibu wa kutoa kila wiki taarifa ya
mwenendo wa mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu nchini ili kuifahamisha
jamii hali ilivyo na hatua zinazochukuliwa na Wizara kudhibiti ugonjwa
huu. Hadi kufikia tarehe 17 April 2016, jumla ya wagonjwa 20,882
wametolewa taarifa, na kati ya hao ndugu zetu 329 wamepoteza maisha
tangu ugonjwa huu uliporipotiwa Agosti 2015.
Meneja wa bondia Francis Cheka “Chief Ndambile” awania ukatibu mkuu Kifa
Mkurugenzi wa Kampuni ya
Advanced Security Limited, Juma Ndambile ambaye pia ni meneja wa bondia
Francis Cheka akimwaga sera baada ya kupitishwa kuwania nafasi ya
Ukatibu Mkuu kwa Chama Cha Soka cha Manispaa ya Kinondoni (KifA)
Mkurugenzi wa Kampuni ya
Advanced Security Limited, Juma Ndambile (wa kwanza kushoto) akiwa na
bondia wake Francis Cheka wakati wa kukabidhi mkanda wa ubingwa Super
Middle kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye
(wa kwanza kulia).
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOANI MOROGORO LEO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Mwenge wa
Uhuru kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima
kutoka mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kukimbiza mwenge huo katika Mikoa na
wilaya zote za Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasha Mwenge wa Uhuru
kuzindua rasmi mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2016 leo Aprili 18, 2016
sherehe iliyofanyika katika uwwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro. Kulia
ni Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jmii, Vijana, Wanawake na Watoto –
Zanzibar Mhe. Modelin Kastiko.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Taifa kwenye
Sherehe za uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru kitaifa zilizofanyika leo april
18, 2016 katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan, akihutubia Taifa kwenye Sherehe za uzinduzi wa Mwenge wa
Uhuru kitaifa zilizofanyika leo april 18, 2016 katika Uwanja wa Jamhuri
Mkoani Morogoro.
Halaiki
(Picha na OMR)
CCM Z’BAR YATAKA WAHANGA WA MAFURIKO WASAIDIWE.
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM)
Zanzibar kimewataka viongozi wa serikali na chama kuharakisha kutoa
misaada kwa waathirika wa mafuriko bila ya kujali tofauti zao za
kisiasa.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu
Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Vuai Ali Vuai wakati akitembelea
maeneo mbali mbali ya Zanzibar yaliyoathiriwa na mafuriko hayo
KICHUYA MCHEZAJI BORA MWEZI MACHI
Mshambuliaji Shiza
Ramadhan Kichuya wa timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro amechaguliwa kuwa
mchezaji bora wa mwezi Machi kwa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu wa
2015/2016.
Kichuya
alionyesha kiwango cha juu katika mwezi huo uliokuwa na raundi nne,
hivyo kuisaidia timu yake kushinda mechi mbili kati ya tatu ilizocheza.
Katika
mechi hizo ambazo zote Kichuya alicheza, alifanikiwa kufunga mabao
mawili kati ya matano yaliyofungwa na timu yake. Alifunga dhidi ya
Coastal Union kwa ushindi wa mabao 3-0, na JKT Ruvu Stars ambapo Mtibwa
Sugar ilishinda mabao 2-1.
Uwezo
aliouonyesha kwa mwezi huo ulisababisha Kocha wa Taifa Stars, Charles
Mkwasa amwite kwa mara ya kwanza kwenye kikosi chake kwa ajili ya mechi
dhidi ya Chad iliyofanyika Machi 23, 2016 jijini N’Djamena.
Washindani
wa karibu wa Kichuya walikuwa washambuliaji Mbaraka Yusuf wa Kagera
Sugar, na Abdulrahman Mussa wa JKT Ruvu Stars ambao pia waling’ara kwa
upande wa timu zao kwa mwezi huo.
Kichuya
ambaye huu ni msimu wake wa pili kwenye Ligi Kuu, kwa kunyakua tuzo ya
mchezaji bora kwa Machi atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni
moja) na wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom.
Wachezaji
bora wa miezi mitatu iliyopita ni kiungo Thaban Kamusoko wa Yanga
(Desemba 2015), beki Shomari Kapombe wa Yanga (Januari 2016) na
mshambuliaji Mohamed Mkopi wa Tanzania Prisons (Februari 2016).
TFF YALAANI VURUGU ZA MASHABIKI
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), limelaani kitendo cha baadhi ya mashabiki wa mpira wa
miguu kufanya vurugu mara baada ya mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Toto
Africans uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
TFF imesikitishwa na kitendo
hicho cha mashabiki wa klabu ya Simba SC, na kusema inalaani kitendo
hicho ambacho sio cha kiuana michezo, huku ikiwataka wanachama,
washabiki kuheshimu viongozi wa klabu zao waliopo madarakani na kama
kuna masuala ya kujadili wakayajadili katika vilabu vyao.
Mashabiki wa klabu ya Simba
walifanya vurugu kwa kurusha mawe, wakilenga kuwadhuru viongozi wa klabu
hiyo pamoja na wachezaji, magari waliyokuwa nayo baada ya timu yao
kupoteza mchezo dhidi ya Toto Africans kwa bao 1- 0.
Jeshi la Polisi baada ya
kuwasishi mashabiki kuondoka eneo la uwanja punde tu mchezo
ulipomalizika, mashabiki hao walikaidi na kuendelea kurusha mawe hali
iliyopelekea jeshi kutumia mabomu ya machozi kuwatanya katika eneo hilo.
Kufutia kitendo hicho, Jeshi la
Polisi lilihakikisha bus la timu ya Simba SC na viongozi wake wanaondoka
salama uwanjani baada ya kuwatawanya mashabiki hao, kwa kupitia mlango
wa karakana ya wachina waliojenga uwanja huo.
Aidha TFF imeviomba vyombo vya
Usalama na Ulinzi kuwachukulia hatua kali mashabiki waliohusika na
kitendo hicho, kwani kufanya vurugu ni kosa la jinai na wanapaswa
kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
PIZZA HUT OPENS IT’S FIRST STORE IN DAR ES SALAAM, TANZANIA
Vikram Desai Pizza Hut Owner adressing Journalist at Mkuki Mall in Dar es salaam last week.
Pizza
Hut, a division of Yum! Brands, the world’s largest restaurant company,
today announced the opening of its first restaurant in Tanzania.
Pizza Hut is the world’s largest
pizza chain with $12 billion in global sales and more than 15,000
restaurants in over 90 countries.
Dough Works Ltd, the franchise
holders of Pizza Hut for Tanzania, has worked very hard in securing
Pizza Hut’s placement in the country, which shows the confidence from
Yum! Brands in the Tanzanian economy and the investors of Dough Works
Ltd.
Dough Works Ltd has committed to a
multi million dollar investment in the Pizza Hut brand and the launch
of it’s first of many stores, which is located at the newly built Mkuki
Mall on Nyerere Road, Dar es Salaam.
The company has plans for rapid
expansion and growth with a target of over 30 stores across the country,
creating over 500 new jobs in the Quick Service Restaurant sector.
Dough Works Ltd Director Vikram
Desai says “We would like to thank all the regulators and vendors for
being very supportive and extending guidance on the opening of Pizza Hut
in Tanzania and we look forward to working together very closely on
building the QSR sector in the country.”
The new Pizza Hut restaurant
features ultra-modern design, digital menu boards, a children’s play
area, and indoor/outdoor seating for over 80 people.
MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO MHE. SAIDI MECK SADIKI ATEMBELEA LANGO LA LONDOROSI HIFADHI YA TAIFA KILIMANJARO
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Saidi Meck Sadiki (watatu kutoka kulia) na
Mkuu wa Wilaya ya Siha Dk. Charles Mlingwa ( wa kwanza kulia)
wakiwasili katika lango la Londorosi, Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro.
Katikati ni mwenyeji wao Betrita Loibooki, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa
Kilimanjaro.
Mkuu
wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro akiwasilisha taarifa fupi ya Hifadhi ya
Kilimanjaro kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Meck Sadiki
akiwa katika lango la Londorosi.
Mkuu
wa Idara ya Utalii Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro, Charles Ngendo
akionyesha maeneo ya hifadhi kwenye ramani kufafanua taarifa ya Mkuu wa
Hifadhi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Meck Sadiki akiongea na watumishi wa hifadhi, wilaya na mkoa katika lango la Londorosi.
Watumishi wa Hifadhi ya Kilimanjaro, Wilaya ya Siha na Mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro na ujumbe wake kutoka mkoani na Wilaya ya Siha
wakipewa maelezo juu ya vivutio na jiolojia ya uwanda wa Shira kutoka
kwa Charles Ngendo, Mhifadhi Utalii wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro.
Picha
ya pamoja ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro alipotembelea Hifadhi ya Taifa
ya Kilimanjaro. Hapa akionekana na msafara wake na viongozi wa hifadhi
ya Kilimanjaro wakiwa uwanda wa Shira (mita 3962)















No comments :
Post a Comment