Wednesday, March 16, 2016

RAIS MHE. JOHN POMBE MAGUFULI AKAGUA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA UJENZI WA KITUO CHA KUFUA UMEME CHA KINYEREZI II JIJINI DAR ES SALAAM


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam CCM, Ramadhan Madabida, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na Madini Dkt. Juliana Palangyo wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli wakati alipowasili kwenye ofisi za kituo cha kuzalisha umeme cha
Kinyerezi I nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida , Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mkurugenzi mkuu wa Tanesco
Felchesmi Mramba wakivuta utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ujenzi wa Kituo cha
Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka Meneja wa Kituo cha kufua umeme
cha Kinyerezi I Mhandisi John Mageni kuhusu utendaji kazi wa kituo hicho.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akianza ukaguzi katika
Mitambo ya kuzalisha umeme ya Kinyerezi I nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

WAZIRI PROF. MBARAWA AIPONGEZA TTCL

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akisalimiana na wafanyakazi wa TTCL mkoa wa Morogoro.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akisalimiana na wafanyakazi wa TTCL mkoa wa Morogoro.Mkuu wa Biasahara Kanda, Nyanda za Juu Kusini Juvenal Utafu akitoa maelezo kuhusu utendaji kazi wa TTCL mbele ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa
Mkuu wa Biasahara Kanda, Nyanda za Juu Kusini Juvenal Utafu akitoa maelezo kuhusu utendaji kazi wa TTCL mbele ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akikagua mitambo ya TTCL na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano mkoa wa Morogoro
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akikagua mitambo ya TTCL na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano mkoa wa Morogoro
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akikagua mitambo ya TTCL na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano mkoa wa Morogoro.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akikagua mitambo ya TTCL na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano mkoa wa Morogoro

KADA ACHANGIA UKARABATI WA JENGO LA CCM MANYARA

index 
Katibu wa CCM MKoa wa Manyara, Ndengiaso Ndekubali (katikati mbele) akimuonesha Jackson Kangoye  baadhi ya vyumba vya jengo la CCM la mkoa huo ambalo hivikaribuni lilitekekea kwa moto.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA MGENI RASMIN SIKU YA TEPE MEUPE LEO

14Matembezi yaliyoshirikisha wadau mbalimbali ya sekta ya Afya kwa ajili ya  maadhimisho ya siku ya Utepe Mweupe na
uzinduzi wa kampeni ya vifo vya Mama vitokanavyo na uzazi yaliyofanyika leo
March 16,2016 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
15
19 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia maonesho
yaliyoshirikisha wadau wa Taasisi mbalimbali za sekta ya Afya kwenye
maadhimisho ya siku ya Utepe Mweupe yaliyofanyika leo March 16,2016 katika
viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
16
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua mpango
mkakati wa miaka mitano wa kampeni ya vifo vya Mama vitokanavyo na uzazi kwenye
maadhimisho ya siku ya Utepe Mweupe yaliyofanyika leo March 16,2016 katika
viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
17
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana
na Mwendesha Mashitaka katika Mahakama ya Kimataifa Jaji Hassan Jallow wakati
Jaji Jallow alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo 
18
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza
na Mwendesha Mashitaka kwenye Mahakama ya Kimataifa Jaji Hassan Jallow, wakati
Jaji Jallow alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo
March 16,2016 kwa ajili ya kumuaga baada ya kuishi Tanzania kwa muda mrefu (Picha na OMR)

Simbachawene awataka ma RC wafanye kazi kulingana na kasi ya Rais

41Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa kutoka TAMISEMI Bi. Suzani Chekani akionesha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akiwasilisha mada kuhusu kuwajibika kwa kuzingatia sheria za nchi kwa wakuu wa mikoa wapya katika kikao kilichofika leo Jijini Dar es Salaam  kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene.
42Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jafo akizungumza na wakuu wa mikoa(Hawapo pichani) kuhusu suala la kutatua changamoto zilizopo katika mikoa katika katika kikao kilichofika leo Jijini Dar es Salaam kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene.
46 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene akizungumza na wakuu wa mikoa (Hawapo pichani) akiwataka kwenda kuwajibika kwa kwa kuzingatia sheria na kutatua changamoto za wananchi katika mikoa yao katika kikao kilichofika leo Jijini Dar es Salaam  .
43 44  Baadhi ya wakuu wa mikoa wakifatilia maelekezo toka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene (Hayupo pichani) katika kikao cha kuwakumbusha majukumu yao kama wakuu wa mikoa.45 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene  (kutoka wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa mikoa wapya walioapishwa jana kulia mwa Waziri ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jafo.
Picha zote na Raymond Mushumbusi  MAELEZO
……………………………………………………………………………………………
Na Jacquiline Mrisho Maelezo

MAJALIWA ATOA MAAGIZO KUHUSU MGOGORO WA MASHAMBA NGARA

 Afisa Ardhi wa  Wilaya ya Ngara, Betty Munuo wa Pili kushoto na
Mwenyekiti wa kijiji cha  Rwakalaman, Brighton  Kemkimba  (kulia)
wakimsikiliza Waziri Mkuu wakati alipozunguma katika kijiji cha   Kasulo wilayani  Ngara  machi16, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipitia majina ya watu wanaomiliki ardhi
kubwa katika  vijiji vya kasharaza na Rwakalemela wilayani Ngara
aliyokabidhiwa na Afisa Ardhi wa wilaya hiyo Betty munuo katika mkutano
aliohutubia kwenye kijiji cha Kasulo wilyani Ngara Machi 16, 2016. 
 (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

ZIARA YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA CHATO MKOA WA GEITA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Bibi Jafari baada ya kuwahutubia wananchi
wa kata ya Kasulo wilayani Ngara Machi 16, 2016. Alikuwa katika siku ya mwisho ya zira ya mkoa wa Kagera.
 Wananchi wa Kalebezo wilayani Chato  wakionyesha mabango wakati Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa alipopita kijijini kwao  akitoka Ngara kuelekea Chato mkoani Geita machi  16, 2016.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Busanda, Lolesia Bukwimba baada
ya kuwasili kwenye   Ofisi ya Mkurugenzi  wa Wilaya ya Chato kuanza ziara ya  Mkoa wa geita Machi 16, 2016. 
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

WAZIRI KITWANGA AFANYA MAZUNGUMZO NA WAKUU WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA ZANZIBAR, AWAOMBA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI SIKU YA KUPIGA KURA

32 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akisalimiana na Brigedi Kamanda wa 101 KV Zanzibar, Brigadia Jenerali, Cylir Mhaiki, kabla ya kufanya mazungumzo na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mjini Zanzibar. Kulia ni Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi, Zanzibar, Ali Abdalla Maalimmosi. Waziri Kitwanga yupo Zanzibar kwa kwa ziara ya kikazi ya kuangalia hali ya uimarishaji wa usalama visiwani humo.
33 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akizungumza na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mjini Zanzibar. Waziri Kitwanga aliwataka wakuu hao kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao unazidi kuimarishwa katika maeneo mbalimbali ya visiwani humo. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi mjini humo.
34 
Brigedi Kamanda wa 101 KV Zanzibar, Brigadia Jenerali, Cylir Mhaiki (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) wakati wa kikao cha Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mjini Zanzibar na Waziri huyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi, Zanzibar.
35 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar mara baada ya kumaliza mazungumzo na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama visiwani humo. Waziri Kitwanga amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi siku ya uchaguzi Machi 20, 2016 bila kutishwa na mtu yeyote, na kila mwananchi aondoe hofu siku hiyo kwani vyombo vya ulinzi vimejipanga vizuri kwa ajili ya kuusimamia uchaguzi huo.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

WAZIRI MKUU AAGIZA KUFUTWA UMILIKI WA MASHAMBA MAKUBWA 11 WILAYANI NGARA

JIL 
 Yana ukubwa ekari 7,700 katika vijiji viwili tu
     Aagiza Afisa Ardhi arudishwe kutoka Rorya kusaidia uchunguzi
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza kufutwa mara moja umiliki wa mashamba makubwa 11 yenye ukubwa wa ekari 7,700  kwenye  vijiji vya Kasharazi na Rwakalemera wilayani Ngara Kagera, ambayo hayana hati na yametelekezwa.

Fastjet yaongeza safari Dar es Salaam – Nairobi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
                 ………………………………………………………………..
Dar es Salaam, Machi 15, 2016 – Shirika la ndege la gharama nafuu Afrika, Fastjet Tanzania limeongeza
idadi ya safari zake  kwenye njia yake ya Dar es Salaam  na Nairobi ikiwa ni mwitikIo  mkubwa kwa mahitaji ya abiria.

BARABARA ZA MKOA WA PWANI ZAHARIBIKA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA

27 
Makamu Mwenyekiti wa  kikao cha bodi ya barabara Mkoa wa Pwani Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze akifafanua jambo katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
31 
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani kushoto  Zainabu Vulu akiwa na wajumbe wengine waliohudhuria katika kikao hicho, wa kati kati ni Mwenyekiti wa  halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamisi Dikupatile.
30 
Meneja wa wakala wa barabara Tanroad Mkoa wa Pwani Tumaini Salakikye akitolea ufafanuai na kujibu maswali yalioulizwa na wajumbe wa kikao hicho juu ya miundombinu ya barabara.
28 
Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akichangia hoja katika kikao hicho cha bodi ya barabara.
29Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kibaha Leornad Mlowe akitolea ufafanuzi kuhusiana na kero ya ubovu wa barabara katika Wilaya ya Kibaha.
Habari Picha – na Victor Masangu Pwani.

WAZIRI KITWANGA ATUA ZANZIBAR, AKUTANA NA MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA POLISI

22 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimsalimia Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omari Makame, mara baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kwa ajili ya ziara ya kikazi Zanzibar. Kulia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Sururu.
23 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimuuliza jambo Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omari Makame, mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kwa ajili ya ziara ya kikazi Zanzibar. Kulia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Sururu.
24 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akikagua gadi maalumu iliyoandaliwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Polisi Zanzibar alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, mjini Magharibi Zanzibar.
25 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu) akizungumza na Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar, Makamanda wa Polisi, Wakuu wa Upelelezi pamoja na Maafisa Wanadhimu wa mikoa mitatu ya Unguja. Kulia meza kuu ni Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omari Makame.
26 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akipewa maelezo na Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omari Makame (kulia) wakati wa kikao chake na Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar, Makamanda wa Polisi, Wakuu wa Upelelezi na Maafisa Wanadhimu wa mikoa mitatu ya Unguja.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

“Mwanamke wa Afrika bado anakabiliwa na changamoto – Waziri Ummy Mwalimu

Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu ( Mb) ametoa hutuba kwa niaba ya Kundi la Nchi za Afrika wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW). Mkutano huu wa wiki mbili unawakusanya wawakilishi kutoka serikali mbalimbali duniani na Asasi za Kiraia ambapo hujadiliana na kubalishana uzoefu na kuelimishana kuhusu hatua mbalimbali ambazo serikali zao zinachukua katika kuboresha maisha ya mwanamke na mtoto wa kike.

08b03dc1-8077-433f-a8db-425449efcc49
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu akitoa hotuba katika Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW).
9222e2ae-9627-4a09-abd3-72692b57d550
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu akiwa katika Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW). Kushoto kwake ni Mwakilishi wa Tanzania wa Kudumu Katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manong.
Akitilia msisitizo hoja na haja ya kupanua wigo wa wanawake kushika nafasi katika ngazi za juu za maamumizi, Ban Ki Moon amesema, ingawa nchi nyingi zimejitahidi sana kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za juu za uongozi bado kuna Nchi Tano ambazo hazina wanawake katika Mabunge yao ili hali Nchi nyingine 7 hazina mawaziri wanawake katika serikali zao.
Naye Rais wa Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa Bw Monges Lykketoft, akizungumza wakati wa mkutano huo, pamoja na kusisitiza umuhimu wa utekelezaji wa Agenda 2030 ambayo ameitaja kuwa ni jumuishi ameendelea kupigia chapuo la kutaka Katibu Mkuu ajaye wa Umoja wa Mataifa awe Mwanamke.
Na Mwandishi Maalum, New York

ZIARA YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA NGARA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na waumishi wa Shirika la
Umeme Nchini TANESCO baada ya kuwasili kwenye eneo unapowekwa mtambo
mpya wa kufua umeme mjini Ngara ambao aliweka jiwe la msingi la ujenzi
wake Machi 15, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akiweka jiwe la msingi la usimikaji mtambo
mpya wa kufua umeme wa Ngara akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi
15, 2016. Kushoto ni Naibu Waziriwa Nishati na Madini Dkt. Kalemani.
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa kizungumza na wakimbizi wa Burundi walioko
katika kambi ya  Lumasi  iliyopo wilayni Ngara. Alikuwa katika ziara ya
mkoa wa Kagera Machi 15 2016
 Baadhi ya wakimbizi wa Burundi walioko kwenye kambi ya Lumasi iliyopo
wilayani Ngara wakimsikilza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati
alipowahutubia akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 15, 2916.
 Moja ya mabango ambayo yalibebwa na wananchi wa Ngara katika mkutano
uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Ngara Machi 15, 2016.
  Waziri Mkuu Kassim Majliwa akizungumza na Watumishi na Viongozi wa Mkoa
wa Kagera kuhitimisha ziara yake mkoani humo kwenye ukumbi wa
Halmashauri ya wilay ya Ngara Machi 15,
Waziri Mkuu, Kassim  Majliwa akiagana na viongozi kambi ya wakimbizi wa
Burundi ya Lumasi iliyoko Ngara  viongozi wa wilaya na UNHCR baada ya
kuitembelea akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 15, 2016.
 (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

SEMINA YA SIKU YA HAKI ZA WATUMIAJI WA HUDUMA ULIMWENGUNI.

5Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Ally Simba akihutubia washiriki wa semina hawapo pichani wakati akifunga semina, siku ya watumiaji wa huduma Ulimwenguni.
3Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano upande wa sekta ya Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo, akihutubia kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika ufunguzi wa semina ya siku ya haki za watumiaji wa huduma Ulimwenguni.
1
4Baadhi ya washiriki wa semina wakimsikiliza mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano upande wa sekta ya Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo hayupo pichani siku ya watumiaji wa huduma Ulimwenguni inayoadhimishwa tarehe 15 Machi, ya kila Mwaka.
2  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano upande wa sekta ya Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Ally Simba (kushoto) siku ya watumiaji wa huduma Ulimwenguni.

MWIGULU NCHEMBA AANZA SAFARI YA KUHAKIKISHA WAFUGAJI WANAACHA KUFUGA KIHOLELA,WAFUGE KWA VITARU.

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh:Mwigulu Nchemba akimuangalia mmoja wadume
la ng’ombe anayetumika kuzalisha Mitamba kwenye kitaru namba 9 shamba
la kitengule-Karagwe.
Baadhi ya ng’ombe waliopo kitaru namba 9 shamba la kitengule

HAFLA YA MCHAPALO WA UZINDUZI WA INTANETI YA KASI YA TIGO 4G LTE JIJINI MWANZA YAFANA


Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe  Joseph Mkirikiti(katikati),Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula(kulia),Mbunge wa Ilemela Angelina Mabula(wa pili kuhoto),Mkuu wa Kitengo cha Biashara Olivier Prentout(kushoto) na  Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Ali Maswanya(wa pili kulia)wakipiga ngoma ikiwa ni ishara ya  uzinduzi wa mtandao wa tigo wa 4G jijini Mwanza
Wageni waalikwa wa uzinduzi wa mtandao wa tigo wa 4G jijini Mwanza,wakibadilisha line zao ili wapate zinazoweza kuendana na kasi hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe  Joseph Mkirikiti(kulia),Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula(katikati) na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Ali Maswanya,wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa mtandao wa tigo wa 4G jijini Mwanza.
Wageni waalikwa wa uzinduzi wa mtandao wa tigo wa 4G jijini Mwanza,wakinunua Modem  za 4G,ambapo ziliuzwa kwa punguzo la bei.

GESI YENYE UJAZO WA FUTI TIRIONI 2.17 YAGUNDULIKA BONDE LA RUVU MKOANI PWANI

 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhomgo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu kugundulika kwa futi za ujazo wa Gesi Tirioni 2.17 katika Bonde la Ruvu mkoani Pwani,  katika eneo la Mamba Kofi One ikiwa ni moja ya ugunduzi ulifanywa na Kampuni ya Dodsal ikishirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli na Tanzania (TPDC). Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Justin Ntalikwa.
 Makamu wa Rais Uendeshaji na Meneja Mkuu wa  Kampuni ya Haydrocarbons and Power Limited (DODSAL), Tom Gray (kulia), akizungmza katika mkutano huo kuhusu kugundulika kwa gesi hiyo ambayo itachimbwa na kampuni yake hiyo. 
 Meneja Utafiti wa Shirika la Maendeleo ya Mafuta na Gesi Tanzania,  Venosa Ngowi (wa pili kulia), akizungumza katika mkutano huo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu, Dk.Juliana Pallangyo wakiwa katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.

HOSPITALI YA KAIRUKI KUTIMIZA MIAKA 29 YA KUTOA HUDUMA ZA AFYA

indexMkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kairuki,Dk.Asser Mchomvu  .KAI1 KAI2 KAI3
Na Mwandishi wetu
…………………………..
Hospitali ya Kairuki (KH) inatimiza miaka 29 mwezi huu siku ya Alhamisi tangu ilipoanzishwa tarehe 17.03.1987.

No comments :

Post a Comment