Thursday, March 10, 2016

Rais Magufuli amkaribisha katika dhifa Rais wa Vietnam Ikulu Jijini Dar es Salaam.

vie1

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozimbalimbali toka Tanzania na Vietnam kwenye halfa ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
vie2
Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang akizungumza na viongozi mbalimbali toka Tanzania na Vietnam katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
vie3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akigonga glass na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang ikiwa ni ishara ya ushirikiano kati ya Tanzania na Vietnam katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
vie4
Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang (Kulia) akiwa amenyanyua glass juu pamoja na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa,Majaliwa ikiwa ni ishara ya kutakia heri kati ya Tanzania na Vietnam katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
vie5
Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang (Kulia) akiwa amenyanyua glass juu pamoja na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa,Majaliwa ikiwa ni ishara ya kutakia heri kati ya Tanzania na Vietnam katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
vie6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli  na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang wakitoa heshima kwa nyimbo za mataifa hayo mawili.
vie7
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Generali Aldof Davis Mwamunyange (Wa pili kulia) akifatilia hotuba za Rais wa Tanzania na Vietnam katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspecta Generali Ernest Mangu, wa pili kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza Kamishna Jenerali  Casmir Minja, katikati ni Mkuu wa Usalama Rashid Othman na kushoto ni Kamanda wa Kanda maaalum Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro.
vie8
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi (katikati) akifatilia halfa ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kushoto ni Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson na kushoto ni Mnadhimu Mkuu mstaafu wa Jeshi la wananchi la Tanzania Luteni Generali Abdulrahman Shimbo.
Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO

CHAKULA CHA JIONI ALICHOANDAA RAIS MAGUFULI KWA HESHIMA YA RAIS WA VIETINAM

SON1
 Mkewa Rais Mama Janeth Magufuli  alimwongoza Mke wa Rais wa Vietinam, Mai Ti Hahn (kushoto) kwenda kwenye chakula cha jioni alichoandaa Rais John Magufuli ikulu jijini Dar es salaam Machi 9, 2016 kwa heshima ya Rais wa Vietinam, Truong Tang Sang. Wapili kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa na kulia ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
SON2
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mkewe Salma wakiingia kwenye  ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam kushiriki   chakula cha jioni alichoandaa Rais John Magufuli ikulu jijini Dar es salaam Machi 9, 2016 kwa heshima ya Rais wa Vietinam, Truong Tang Sang.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
SON3
Katibu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi Celestine Mushy wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashari, Kikanda na Kimataifa katika chakula cha jioni alichoandaa Rais John Magufuli ikulu jijini Dar es salaam Machi 9, 2016 kwa heshima ya Rais wa Vietinam, Truong Tang Sang.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
SON4
Rais John Magufuli akiteta na Rais Mstaafu Ali Hasan Mwinyi na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika chakula cha jioni alichomwandalia Rais wa Vietinam,  Truong Tang Sang, Ikulu jijini Dar es salaam Machi 9,2016.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
SON5
Rais John Magufuli akizungumza na  Marais Wstaafu Ali Hasan Mwinyi na Jakaya  Kikwete  Waziri Mkuu katika  chakula cha jioni alichomwandalia Rais wa Vietinam,  Truong Tang Sang, Ikulu jijini Dar es salaam Machi 9,2016. Kulia ni Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
SON6
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha UDP,John Cheyo chakula cha jioni ambacho Rais John Magufuli alimwandalia  Rais wa Vietinam,  Truong Tang Sang, Ikulu jijini Dar es salaam Machi 9,2016. Kulia ni Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 

Waziri Mkuu awahakikishia fursa za Uwekezaji wa Vietnam

TIH6
Na Anitha Jonas – MAELEZO
Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa amewahakikishia wawekezaji kutoka Vietnam kuwepo kwa fursa za uwekezaji nchini.
Majaliwa ameyasema hayo jana katika kongamano la ujumbe wa Rais wa Vietnam Mheshimiwa Troung Tan Sang pamoja na wadau wa uwekezaji kutoka nchini humo ambapo wanatarajia kufanya ziara ya siku nne nchini wakitazamia fursa za uwekezaji nchini.
“Nchi yetu inamazingira mazuri ya uwekezaji, usalama wakutosha na pia kuna uhahika wa soko kwani ipo mikataba ya kikanda ya kukuza masoko katika nchi wanachama kama EAC na SADC kwani katika nchi hizo kuna watu zaidi ya milioni 300”, alisema Majaliwa.
Akiendelea kuzungumza na wawekezaji hao Waziri Mkuu alisema serikali ya Tanzania imekuwa ikiboresha Mazingira ya uwekezaji nchini na hiyo imechangia ongezeko la wawekezaji.
Mbali na hayo Majaliwa alisema serikali imekuwa ikiboresha sheria na kuimarisha ushirikishwaji wa wadau wa sekta binafsi lengo likiwa ni kuchochea mazingiraya uwekezaji ikiwa ni kuimarisha uchumi wa taifa pamoja na kukuza kipato cha kila mtanzania.
Hata hivyo Waziri Mkuu aliipongeza Kampuni ya VIETTEL Tanzania Ltd kutoka Vietnam ambayo imewekeza katika Sekta ya Mawasiliano kwani imewasaidia watanzania wengi wa vijijini kupata mawasiliano.

RAIS WA ZANZIBAR AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA VIETNUM, AKUTANA NA MAALIM SEIF

kq1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, jana Ikulu Jijini Dar es Salaam akipofika kwa mazungumzo na ujumbe aliofuatana nao,[Picha na Ikulu.]
kq2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Ujumbe wake (kushoto) wakiwa katika mazungumzo na Ujumbe wa Rais wa Vietnam Truong Tan Sang jana Ikulu Jijini Dar es Salaam akiwa nchini kwa ziara ya Kikazi,[Picha na Ikulu.]
kq3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akiagana na mgeni wake Rais wa Vietnam Truong Tan Sang(kushoto) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jana Ikulu Jijini Dar es Salaam(katikati) mawair mbali mbali wa Vietnum walioungana na Rais Truong,[Picha na Ikulu.]
kq4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akifuatana na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang(katikati) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jana Ikulu Jijini Dar es Salaam(kulia) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Augustin Mahiga,[Picha na Ikulu.]
kq5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam jana akiwa katika mapumziko baada ya kuugua kwa matatizo ya kiafya,[Picha na Ikulu.]
kq6
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiteta na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad jana katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam alipofika kuonana  nae kiwa katika mapumziko baada ya kuugua kwa matatizo ya kiafya,[Picha na Ikulu.]

Watanzania wameaswa kuwa na tabia kuwekea akiba benki.

kim
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma
Watanzania wameaswa kujenga tabia ya kujiwekea akiba kupitia mabenki kwa manufaa yao na taifa kwa kwa ujumla ikiwa ni mchango wao katika kutekeleza kaulimbiu ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ili kufikia malengo waliojiwekea katika kujiletea maendeleo endelevu.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Fedha na Utawala kutoka Bodi ya Bima na Amana (DIB) iliyo chini ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Richard Malisa wakati akitoa mada juu ya bodi hiyo katika semina ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi hao katika kuandika, kutoa na kusambaza habari za sekta ya uchumi biashara na fedha.
“Pesa zinapowekwa na kuwa benki hutumika kuchangia kuinua na kuimarisha usalama wa akiba ya mtu binafsi na kwa upande wa nchi zinatumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo kuinua sekta ya elimu, afya, maji,  ujenzi wa barabara na kilimo” alisema Malisa.
Katika kuonesha umuhimu wa bodi hiyo nchini, Malisa alisema kuwa taasisi ama mtu binafsi anapoweka pesa zake benki, hiyo ni amana kubwa na muhimu kwa kuwa tabia hiyo ya uwekaji pesa ina tija na inaongeza usalama wa pesa ambayo ni njia salama ikilinganishwa na kutumia njia za zamani za watu kuweka pesa kwenye godoro ambayo sio salama.
Faida nyingine za mtu binafsi ama taasisi kuweka pesa zao benki ni kuongeza mtaji wake kwa kupata riba kulingana na muda pesa hizo zinapokuwa benki na mteja anauhakika pesa yake ipo salama kwa kuwa ipo mikononi mwa Bodi ya Bima na Amana endapo litatokea tatizo lolote kwenye benki alipoweka pesa zake.
Katika kufanikisha na kutekeleza majukumu yake, DIB inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uelewa mdogo wa mtu mmoja mmoja katika masuala ya kibenki na fedha kwa undani wake ili aweze kufanya maamuzi yatakayomfanya awe bora zaidi kiuchumi ikilinganishwa na hapo awali kabla ya kufahamu masuala ya kibenki na fedha ikiwemo kuongeza nidhamu ya matumizi.
Akitolea mfano Malisa amewaasa Watanzania wawe makini wanapochukua mikopo ambapo alisema kuwa watu wasikope kwa kufuata mkumbo ama kwa shinikizo fulani, bali wakepo kwa lengo la kuwekeza ili kuinua hali zao za kiuchumi katika maisha.
Hadi kufikia Juni 30, 2015 Bodi ya Bima na Amana ina akiba ya jumla ya kiasi cha Sh. biloni 220.5 ikilinganishwa na wakati ilipokuwa inaanzishwa na Serikali mwaka 1994 ambapo kianzio kilikuwa kiasi cha Sh. bilioni 1.5.
Aidha, katika semina hiyo Bw. Bernard Dadi kutoka Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo ya Taifa alisema kuwa BoT itaendelea kuboresha mifumo ya malipo ya hundi, kielektroniki ili kuongeza ufanisi kwenye mifumo hiyo, kuongeza usalama, kuongeza njia mbalimbali za malipo ili kupunguza malipo kwa fedha taslimu na kuongeza kasi ya malipo yaweze kuwa ya wakati kwa wateja popote walipo ndani na nje ya nchi.
Ili kuendana na wakati BoT kupitia Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo ya Taifa katika kuwahudumia wananchi katika masuala ya fedha na mabenki, imeanza kutumia mfumo wa TACH unaohusisha malipo ya hundi na malipo madogo ya kielektroniki (EFT) ambao umeanza kutumika tarehe 30 Aprili 2015 nchini.
Mfumo wa TACH unatumika na mabenki kutuma na kupokea hundi za wateja wao ikiwemo kulipa malipo madogo madogo yaliyojumishwa pamoja, mishahara, pension na hata malipo ya mtu mmoja mmoja.
Kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa TACH nchini, awali hundi zilikua  na muda tofauti wa siku za kuhakiki kulingana na kanda hali iliyopelekea muda wa siku za kuhakiki  za hundi ulikua ni siku 3, 7 na 14 kutegemeana na kanda.
Baada ya kuanzishwa mfumo wa TACH hali imekuwa tofauti ambapo kwa mfumo  huo sasa, hundi zote za Tanzania popote zitakapowasilishwa zitakuwa zinafanyiwa kazi ndani ya siku moja ya kuzihakiki hundi  hizo (T+1) mpaka hapo itakapolipwa.
Hatua hiyo imewapunguzia muda wateja ili waweze watapata hela zao mapema na hivyo kuzitumia kwenye shughuli zao za kiuchumi.
Aidha, Bw. Dadi aliongeza kuwa nchi washirika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zenyewe zinatumia unaojulikana kama EAPS ikiwa ni jitihada za kuunda umoja  wa kiuchumi miongoni mwa nchi hizo.
Mfumo huo wa malipo umeunganisha mifumo ya malipo (RTGS) ya nchi washiriki wa Afrika Mashariki ili kurahisisha malipo kati ya nchi washirika.
Kwa maana hiyo mabenki ya kibiashara ya nchi husika zina uwezo wa kutumiana na kupokea pesa za wateja wao kwa kutumia sarafu za nchi wanachama kufanya muamala.
Hadi sasa, mfumo huo umeunganishwa kwa Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, wakati Burundi na Sudan ya Kusini wako mbioni kujiunga.

KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI CHA MKOA WA LINDI CHAFANYIKA

 
 Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Jordan Rugimbana akisoma hotuba ya ufunguzi wa kikao cha Kamati ya Ushauri mkoa.
 Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Mhe. Nape Nnauye akizungumza kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri mkoa wa Lindi.
 Wajumbe wa Kikao cha Ushauri cha mkoa wa Lindi.
 Mbunge wa Jimbo la Lindi mjini Mhe. Hassan Kaunje akichangia maoni yake kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri  ya mkoa wa Lindi.
Kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo akutana na mkurugenzi wa radio France Internationale

ra1
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akimkaribisha Mkurugenzi wa Radio France Internationale(RFI) Bi.Cecile Megie ofisini kwake alipomtembelea kwa ajili ya kufahamiana na kuboresha mahusiano yaliyopo kwa miaka saba sasa.
ra2
Ujumbe kutoka Radio France International (RFI) wakifurahia jambo wakati wa kikao na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura(Hayupo pichani).
ra3
Mkurugenzi wa Radio France Internationale (RFI) Bi.Cecile Megie(kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura kuhusu msaada ambao wameipa shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) ili kusaidia katika kufikisha matangazo yake mbali Zaidi.
RA5
RA6
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura(kulia) akimpa zawadi ya kahawa kutoka Tanzania Mkurugenzi wa Radio France Internationale(RFI) Bi.Cecile Megie(kushoto) baada ya mazungumzo mafupi ofisini kwa Naibu Waziri uyo kuhusu kuimarisha mahusiano baina ya nchi izi mbili katika masuala ya Habari kati ya TBC na RFI.

Jennifer Mgendi alipania Tamasha la Pasaka

images (12)
Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI na Msanii mahiri wa Filamu Tanzania, Jennifer Mgendi  amelipania Tamasha la Pasaka linalotarajia kuanza Machi 26-28 katika mikoa ya Geita, Mwanza na Kahama.
Kwa mujibu wa Mgendi hivi sasa analisubiri kwa amu tamasha hilo ambalo lina malengo ya kusifu na kuabudu kupitia nyimbo mbalimbali za Injili sambamba na viongozi wa dini mbalimbali.

BAKITA waaswa kuhamasisha matumizi ya Lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi

BUR1
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Anastazia James Wambura akizungumza na Katibu Mtendaji BAKITA (hayupo pichani) alipotembelea ofisi za Baraza la Kiswahili Taifa (BAKITA) kufahamu mambo mbalimbali yanayofanywa na Taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam. 
BUR2
Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili Taifa (BAKITA) Dr. Selemani Sewange (katikati) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Anastazia James Wambura (kushoto) alipotembelea ofisi za BAKITA kufahamu mambo mbalimbali yanayofanywa na Taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni maafisa Utamaduni kutoka Wizara hiyo.
BUR4
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Anastazia James Wambura (kushoto) akikabidhiwa kitabu kiitwacho Furahia Kiswahili kilichoandaliwa na BAKITA alipotembelea ofisi za BAKITA kufahamu mambo mbalimbali yanayofanywa na Taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam. Anayemkabidhi ni Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili Taifa (BAKITA) Dr. Seleman Sewange
BUR5
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Anastazia James Wambura akipitia Kamusi kuu ya Kiswahili aliyopewa baada ya kutembelea ofisi za BAKITA kufahamu mambo mbalimbali yanayofanywa na Taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam.
BUR6
Mtaalamu kutoka Idara ya Istilahi na Kamusi Taasisi ya BAKITA Bw. Mayolwa John (kushoto) akimwelezea Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Anastazia James Wambura (kulia) kazi zinazofanywa na Idara hiyo alipotembelea ofisi za BAKITA kufahamu mambo mbalimbali yanayofanywa na Taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili Taifa (BAKITA) Dr. Selemani Sewange
BUR7
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Anastazia James Wambura (wapili kushoto) akiangalia mfumo wa mradi wa kukuza kiswahili katika kompyuta ulioandaliwa na BAKITA alipotembelea Taasisi hiyo kufahamu mambo mbalimbali wanayoyafanya jana jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili Taifa Dr. Selemani Sewange na kushoto ni Afisa Utamaduni Bw. Christopher Mhongole.

KIBONZO CHA NATHAN MPANGALA LEO

mpa

TAMKO LA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU SIKU YA FIGO DUNIANI, TAREHE 10 MACHI, 2016

LO1
Siku ya Figo Duniani huadhimishwa duniani kote kila AlhamisI ya pili ya mwezi Machi tangu mwaka 2006. Mwaka huu itaadhimishwa leo tarehe 10/3/2016.
Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Figo mwaka 2016 ni “Chukua Hatua Mapema Kuepuka Magonjwa ya Figo kwa Watoto”. Kauli mbiu hii inalenga kuhamasisha jamii juu ya matatizo ya figo yanayoikabili jamii yetu hususani watoto.

WATOTO CHINI YA MIAKA 5 KUNUFAIKA NA UPIMAJI WA AFYA BURE KUTOKA KWA BANGO SANGHO

Bango Sangho
Mwenyekiti wa Umoja wa Jamii ya watu kutoka India, Bengali waliopo Tanzania (Bango Sangho), Kunal Banerjee akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kambi ya upimaji afya kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano inayotayotaraji kufanyika katika Shule ya Msingi Kibugumu iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mmoja wa madaktari watakaoendesha zoezi la upimaji afya kwa watoto hao Dkt. Ali Mzige kutoka Kliniki ya Al Hilal ya jijini Dar es Salaam.

Ali Mzige
Mmoja wa madaktari watakaoendesha zoezi la upimaji afya kwa watoto hao Dkt. Ali Mzige kutoka Kliniki ya Al Hilal ya jijini Dar es Salaam akifafanua jambo kuhusiana na umuhimu wa kupima afya za watoto katika mkutano na waandishi wa habari.
“Tunataka kusaidia marafiki zetu wa Tanzania na katika kuendelea hilo tutatoa huduma ya bure kwa watoto kupima afya zao na tunataka wazazi wawalete watoto ili wapime afya,” alisema Banerjee.
Husna Abdallah
Mtaalamu wa afya ya uzazi kutoka Kliniki ya Al Hilal, Bi. Husna Abdallah akitoa msisitizo kwa akina mama kuzingatia kanuni za afya ya uzazi wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam.
Zawadi Chogongwe
Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, Zawadi Chogongwe (kulia) akiuliza swali kwa wataalamu wa afya wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na kambi ya upimaji afya kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano inayotayotaraji kufanyika katika Shule ya Msingi Kibugumu iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

UZINDUZI WA MRADI WA UIMARISHAJI MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA MKOA WA SHINYANGA

Hapa ni katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambako kumefanyika uzinduzi wa mradi wa Uboreshaji Mifumo ya Sekta za Umma unaojulikana kwa jina la Public Sector Systems Strenghening (PS3) unaofadhiliwa na shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
Lengo la mradi huo ni kuimarisha mifumo ya ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora,rasilimali watu,fedha utoaji taarifa na tafiti tendaji katika halmashauri za wilaya na taifa kwa ujumla. Mkutano wa uzinduzi huo utakaofanyika kwa siku mbili Machi 09,2016 hadi Machi 10,2016 umehudhuriwa na Kiongozi wa timu ya mradi,katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga,wakuu wa wilaya,meya wa manispaa ya Shinyanga,wenyeviti wa halmashauri za wilaya,wataalam kutoka kutoka ofisi ya Waziri mkuu na wadau mbalimbali zikiwemo taasisi,mashirika na taasisi za umma na binafsi-Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde yupo eneo la tukio ametusogezea picha 30 ,Tazama hapa chini

Kaimu katibu tawala mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe ambaye pia ni mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga akitambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano huo wa uzinduzi wa mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta za umma Public Sector Systems Strenghening(PS3) utakaotekelezwa kwa muda wa miaka mitano na utafanya kazi na serikali kuu pamoja na halmashauri 97 katika mikoa 13 ya Tanzania bara.

Wakuu wa wilaya tatu za mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini,wa kwanza kushoto ni Vita Kawawa kutoka wilaya ya Kahama,akifuatiwa na Josephine Matiro kutoka wilaya ya Shinyanga na Hawa Ng’umbi kutoka wilaya ya Kishapu

Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizindua mradi wa PS3 ambapo alisema mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa 13 nchini ambayo itanufaika na mradi huo ambapo alidai umeanza kwa wakati muafaka kwani sasa serikali iliyopo madarakani inataka mabadiliko katika kuhakikisha kuwa serikali inahudumia wananchi ipasavyo

Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam (kushoto) akifuatilia hotuba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.Rufunga alisema mradi huo utakuwa na tija kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa halmashauri 6 za mkoa wa Shinyanga

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga aliwataka watendaji wa serikali katika ngazi ya mkoa na mamlaka za serikali za mitaa kutoa ushirikiano katika kutekeleza mradi wa Uboreshaji Mifumo ya Sekta za Umma kutokana na kwamba wao ndiyo wana mawasiliano ya moja kwa moja na wananchi wa kawaida.

Tunamsikiliza mgeni rasmi……

Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta za umma unaofadhiliwa na shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID)

Meneja wa Mradi wa PS3 Dkt Emmanuel Malangalila akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo ambapo alisema mradi huo utatekelezwa kwa muda wa miaka mitano umeandaliwa na shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) Kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania na kutekelezwa na mashirika saba likiwemo shirika la Abt Associates Inc ambalo ndiyo mtekelezaji mkuu.

No comments :

Post a Comment