Thursday, February 25, 2016

MAJALIWA APOKEA VIFAA VYA HOSPITALI KUTOKA MAKAMPUNIYA PEPSI, COCACOLA NA AZAMCOLA

we1
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua baadhi ya vitanda na vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani ya sh. bilioni 10 vilivyotolewa na kampuni za vinywaji baidi za Coca cola- Kwanza, Azam  Cola  na Pepsi Cola- SBC  katika makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kulia  kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
we2
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua baadhi ya vitanda na vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani ya sh. bilioni 10 vilivyotolewa na kampuni za vinywaji baidi za Coca cola- Kwanza, Azam  Cola  na Pepsi Cola-SBC katika makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kushoto   ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
we3
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua baadhi ya vitanda na vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani ya sh. bilioni 10 vilivyotolewa na kampuni za vinywaji baidi za Coca cola- Kwanza, Azam  Cola  na Pepsi Cola-SBC katika makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kushoto   ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
we4
we6
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea moja ya vifaa vya hospitali kutoka kwa wawailishi wa makampini ya Vinywaji baridi ya Coca Cola- Kwanza, Azam Cola na Pepsi Cola-SBC  katika makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kushoto  Mkurugenzi wa Pepsi, Avinash Jha,Wapili kushoto ni  Reginald Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP na Wapili kulia ni Basil Gadzios wa Coca cola Kwanza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
we7
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana   baadhi ya viongozi vya makampuni ya vinywaji  baridi ya Coca Cola- Kwanza, Azam Cola na Pepsi Cola-SBC  katika makabidhino ya vofaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi bilioni 10 yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Pepsi, Avinash Jha, Reginald Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP na Basil Gadzios wa Coca cola Kwanza.  Kulia    ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO ATETA NA WAFANYABIASHARA MKOA WA ARUSHA,WAAHIDI KUUNGA MKONO SERIKALI

 
Waziri wa Fedha na Mipango,Dk Philip Mpango akizungumza na jumuiya ya Wafanyabiashara mkoa wa Arusha leo katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa na kuwakumbusha wajibu wao kulipa kodi stahiki ili kukuza uchumi wa nchi,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhil Nkurlu na Kamishna wa Kodi za ndani,Shogholo Mgonja.
Kamishna wa Kodi za ndani,Shogholo Mgonja akijibu hoja za wafanyabiashara mkoa wa Arusha huku Waziri wa Fedha na Mipango,Philip Mpango akifatilia kwa makini . 
Mfanyabiashara wa Usafirishaji ambaye ni Katibu wa Wamiliki wa magari ya abiria mkoa wa Arusha na Kilimanjaro(AKIBOA)Roken Adolf akiuliza maswali na kutoa maoni ya wanachama wenzake.
Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha nguo na bidhaa mbalimbali cha A to Z,Anuj Shah akizungumza namna mlolongo wa nyingi unavyowakera wawekezaji wa ndani.
Mkurugeni wa taasisi kilele inayohusika na kilimo cha mbogamboga na matunda ya TAHA,Jackline Mkindi aliiomba serikali kuweka mazingira mazuri na kupunguza kodi ili kuwezesha ndege za mizigo kutoa huduma zao hapa nchi badala ya kusafirisha mazao yao kupitia nchi ya Kenya.
Mkurugenzi wa Kibo Guides and Tanganyika Wildernes Camps akizungumza kwenye mkutano huo ambao aliiomba serikali kuwabana wafanyabiashara wa utalii wanaokwepa kodi.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Longido,Ernest Kahindi,Mkuu wa wilaya ya Monduli,Francis Miti na Mkuu wa wilaya ya Karatu,Omary Kwaang’ wakifatilia miongoni mwa maafisa wa serikali waliohudhuria mkutano huo.
Wafanyabiashara kutoka sekta mbalimbali waliohudhudia mkutano huo

HALMASHAURI MPYA YA MJI WA MBINGA MKOANI RUVUMA, YAAZIMIA KUNUNUA MITAMBO MAALUMU YA KUSAGA TAKA TAKA

Mkurugenzi wa halmashauri mpya ya mji wa Mbinga   OSCAY YAPESA.
…………………………………………………………………………………………………..
Halmashauri mpya ya mji wa Mbinga mkoani Ruvuma, imeazimia kununua mitambo maalumu ya kusaga takataka ili kuondokana na hatari ya kukumbwa na magonjwa ya milipuko inayotokana na uchafu ikiwemo kipindupindu , pia takataka hizo zitakazokuwa zikisagwa kwenye mitambo hiyo zitatumika kama mbolea kwenye mashamba ya wakulima.Story kamili hii hapa RUVUMA TV.

Cheka: Nitampa kipigo cha ‘mbwa mwizi’ Mzungu

c1
MKurugenzi wa kampuni ya Advanced Security Company Limited, Juma Ndambile (wa pili kulia) akimtambulisha bondia Francis Cheka (wa kwanza kulia) mbele ya bondia Geard Ajetovic  (wa kwanza kushoto) huku promota Jay Msangi (wa pili kushoto) akishuhudia.
c2
Promota Jay Msangi (katikati) akiutambulisha mkanda kwa mabondia Francis Cheka (wa kwanza kulia) na Geard Ajetovic (kushoto)
c3
Bondia Francis Cheka (kushoto) akipiga picha ya pamoja na Geard Ajetovic mara baada ya kukutana mara ya kwanza.
……………………………………………………………………………………………….

BLOGU YA WANANCHI YATIMIZA MIAKA MITATU SHEREHE KUFANYIKA KESHO HOTELI YA HYATT REGENCY KEMPISKY JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi Mkuu wa Blogu ya Wananchi, William Malecela ‘Le Mutuz’ , akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Blogu ya Wananchi, William Malecela ‘Le Mutuz’ , akionesha kompyuta mpakato kwa wanahabari ambayo alianza kuitumia baada ya kuanzisha blogu hiyo miaka mitatu iliyopita.
Mkurugenzi Mkuu wa Blogu ya Wananchi, William Malecela ‘Le Mutuz’ (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu blogu hiyo kutimiza miaka mitatu na semina itakayowakutanisha wasomi wasio na kazi kuhusu namna ya kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa.
………………………………………………………………………………………………
   

Ofisi ya Uhusiano, Kitengo cha Masoko TANESCO aelimisha umma kuhusu usalama na ubaya wa wizi wa umeme

 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha VETA NJIRO,
waliohudhuria kwenye mafunzo ya usalama na wizi wa umeme wa kwanza (Kushoto) ni
Afisa Huduma kwa wateja Bw. Juma Msuya.
 Mwanafunzi wa Chuo cha Veta kilichopo Oljoro mkoani Arusha
akiuliza swali kwa wataalamu wa TANESCO katika mafunzo hayo.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi  Oldonyo Sambu Mkoani Arusha wakiwa na zawadi zao walizopewa na wataalam wa TANESCO kama zawadi za kushiriki vyema katika mafunzo hayo na kujibu na kuuliza
maswali, kushoto ni Afisa Mahusiano na Wateja Mkoa wa Arusha Bw.Fred
Mbavai.
 Baadhi ya wanafunziwa Shule ya Msingi Mbweni ya jijini Dar es Salaam wakiwa tayari kuwapokea
wataalam kutoka TANESCO kwa ajili ya kupokea elimu kuhusu masuala mbalimbali ya umeme.
  Afisa Masoko  Bi. Jenifer Mgendi kutoka Shirika la Umeme (TANESCO)     akitoa zawadi kwa wanafunzi waliojibu maswali vizuri wakati wa utoaji elimu ya masuala ya umeme, katika Shule ya Msingi Tandika ya
jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kisukuru ya jijini Dar es Salaam, wakishangilia zawadi walizopewa wakati wa wataalam kutoka TANESCO walipotoa elimu ya masuala ya umeme. Katikati ni Afisa Uhusiano Bi.salama
Kasamalu.

Muhimbili Yaendesha Zoezi la Kuchangia Damu Jijini Dar es Salaam

LIH1
Mkurugenzi wa Huduma Shirikishi za Tiba katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Praxeda Ogweyo akifungua zoezi la utoaji damu linaloendelea leo katika viwanja vya Karume mkabala na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Zoezi hilo linaendea hadi kesho.
LIH2
Mkurugenzi wa Huduma Shirikishi za Tiba katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Praxeda Ogweyo akiongoza zoezi la utoaji damu leo katika viwanja vya Karume mkabala na Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
LIH3
Muuguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Nemganga Kizega akipima afya ya Mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam, Merry Kapande aliyefika leo kuchangia damu katika viwanja vya karume mkabala na ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
LIH4
Wanafunzi wa Tambaza wakichangia damu leo katika zoezi linaloendelea leo jijini Dar es Salaam.
LIH6
Dk Patrick Shao ni mmoja wa wafanyakazi wa Muhimbili ambaye alifika katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu.
LIH7
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya  Tambaza na Jangwani wakisubiri kutoa damu leo katika viwanja wa Karume mkabala na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
………………………………………………………………………………………………………
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo emeendesha zoeti la kuchangia damu katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam ambako watu wamejitokeza kwa wingi kutoa damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu.
Zoezi hilo limeanza leo asubuhi na litaendelea hadi kesho. Wanafunzi wa Jangwani Sekondari na Tambaza ni kati ya makundi yaliojitokeza kutoa damu.
Pia watu mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kutoa damu akiwamu Mkurugenzi wa Huduma Shirikishi za Tiba katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk Praxeda Ugweyo, madaktairi wa muhimbili na kijana Joseph Starford Mgoha aliyetembea kwa mguu kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam kwa ajili ya kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli kutokana na utendaji wake uliotukuka.
Katika zoezi hilo Dk Ogweyo amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kuchagia  damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu.
Pia, amesema zoezi hilo litakuwa endelevu na amewaondoa shaka Watanzania kwamba utoaji wa damu hauna madhara yoyote kwa kuwa kabla ya mtu kutoa damu anaandaliwa kitaalamu ili kufanikisha kazi hiyo.

UTT-PID YATEMEBELEWA NA MKURUGENZI WA MIPANGO WIZARA YA FEDHA JIJINI DAR ES SALAAM

 Afisa Mtenaji Mkuu wa Taasisi ya Serikali ya Miradi na Manedeleo ya Miundombinu UTT-PID,
Dkt. Gration  Kamugisha (kulia), akimkaribisha Mkurugenzi wa Mipango, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Richard Mkumbo, wakati mkurugenzi huyo na tmu yake walipotembelea taasisi hiyo jijini
Dar es Salaam jana, kwa lengo la kujua maendeleo ya taasisi na changamoto wanazokabiliana nazo ili kutafuta ufumbuzi wa kuzishughulikia changamoto hizo. 
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Serikali ya Miradi na Manedeleo ya Miundombinu UTT-PID,
Dkt. Gration  Kamugisha(aliyesimama kushoto), akielezea mafanikio ya taasisi hiyo na changamoto inayokabiliana nazo wakati timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango ilipotembelea taasisi hiyo jijini Dar es Salaam jana. Timu hiyo iko kwenye ziara ya kukutana na watendaji wa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo hususan Ofisi ya Msajili wa Hazina. 
Mkurugenzi wa Mipango, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Richard Mkumbo, akifafanua jambo wakati wa mkutano huo
 Dkt. Kamugisha akielezea mafanikiona changamoto ambazo UTT-PID inapambana nazo

Dkt. Kamugisha (katikati), Mkuu wa Kitengo cha Sheria, UTT-PID, Tuzo Mpiluka, na Mkuu wa kitengo cha Operesheni, Alexsandar Nikolik
 Dkt. Kamugisha na kushoto ni Mkuu wa Operesheni wa UTT-PID, Alexsandar Nikolik
 Mkuu wa Kitengo cha Sheria, UTT-PID, Tuzo Mpiluka, akifafanua jambo, huku Dkt. Kamugisha (kushoto) na Mkuu wa kitengo cha usimamizi wa miradi, Joyce Mcharo
 Kaimu Mkuu wa Masuala ya kampuni (Head of Corporate Affairs), Eugenia Simon, (katikati), akizungmza huku Mkurugenzi wa Mipango wa wizara ya Fedha na Mipango, Richard Mkumbo, (kulia) na Mkuu wa kitengo cha usimamizi wa miradi, Joyce Mcharo
 Mkuu wa kitengo cha usimamizi wa miradi, Joyce Mcharo
 Msabaha A. Msabaha (kulia), Afisa mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, aliyefuatana na Mkurugenzi wa Mipango Richard Mkumbo, akizungumza kwenye kikao hicho. Kushoto ni Afisa Mwingine mwanadamizi kutoka wizara hiyo, Masoud Ridhiwani
 Afisa mwandamizi kutoka Wizara ya Fedhana Mipango, Masoud Ridhiwani akizungumza kwenyekikao hicho. Kshoto ni Mkurugenziwa Mipango, Richard Mkumbo.
 Mkuu wa kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi cha UTT-PID, Milton Shango, (kulia), akizungumza kwenye kikao hicho.
 Bw. Shango akifuatilia kikao kwa makini
Bw. Mkumbo akizungumza na uongozi wa juu wa UTT-PID

WAZIRI MBARAWA AZITAKA TAASISI ZA WIZARA YAKE KUSHIRIKIANA

BR1
Meneja wa Wakala wa Barabara mkoa wa Kilimanjaro Eng. Marwa Rubirya akitoa taarifa ya utekelezaji wa TANROADS kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Prof. Makame Mbarawa wakati alipotembelea taasisi hiyo mkoani Kilimanjaro. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Amos Makala akifatilia.
BR2
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na watendaji wa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kuhusu kufanya kazi kwa uwazi, weledi na uaminifu ili kuongeza mapato.
BR3
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Amos Makala akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (katikati) katika kikao cha viongozi wa sekta zilizo chini ya Wizara hiyo.
BR4
Mfanyakazi wa Wakala wa Majengo (TBA) mkoa wa Kilimanjaro Bi. Welo Makala akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani) katika kikao cha Waziri na Watumishi wa Sekta zilizo chini ya wizara hiyo.
BR5
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Amos Makala akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa mara baada ya kikao kati ya Waziri huyo na watumishi wa sekta zilizo chini ya Wizara yake.
BR6
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kulia mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
BR7
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifurahia jambo na baadhi ya watalii waliokuwa wakijiandaa kupanda Mlima wa Kilimanjaro katika geti la Machame mkoani Kilimanjaro.
BR8
Muonekano wa lango la Machame la kupanda Mlima Kilimanjaro inapoishia barabara ya KMT-Machame Km 14.9. Barabara hiyo ni muhimu kwa watalii wanaopanda mlima Kilimanjaro.
……………………………………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amezitaka taasisi zote zilizo chini ya wizara hiyo kufanya kazi kwa uwazi, weledi na uaminifu ili kuongeza mapato na kutimiza adhma ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025.

Waziri Mkuu awataka Mawazi kuzingatia Maadili

1
Waziri Mkuu Mhe. Kassimu Majaliwa,Majaliwa akizungumza na mawaziri na manaibu waziri wakati wa semina ya Maadili kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-IKULU)
2
Waziri ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akizungumza wakati wa semina ya Maadili kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.
4
Kamishna Tume ya Maadili kwa viongozi wa Umma Jaji Mstaafu salome Kaganda akizungumza wakati wa semina ya Maadili kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.
5
Baadhi ya Mawaziri na manaibu Waziri wakiimba wimbo wa Tanzania Nakupenda ikiwa ni ishara ya kuonesha uzalendo kwa nchi kabla ya kuanza semina ya Maadili kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.
7
Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Bi Virginia Blaser akijadiliana jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Profesa Jumanne Maghembe huku mawazili wengine wakisililiza mazungumzo hayo.
8
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(kulia) akimsikiliza  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. JumanneMaghembe kabla ya kuanza kwa semina ya Maadili kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam katikati ni Waziri ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage
9
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kushoto) akizungumza jambo pamoja na mawaziri wenzake kabla ya kuanza kwa mafunzo semina ya Maadili kwa mawaziri na manaibu waziri yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam ,kulia ni  Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Uratibu, Bunge,Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Muhagama(Kulia na katikati ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt Hussein Mwinyi.
10
Naibu Waziri wa mambo ya Ndani Mh. Hamad Masauni  kushoto  akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mh. Luhaga Mpina huku mawazili wengine wakupitia makabrasha yao kabla ya kuanza kwa semina hiyo.
11
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa semina hiyo kwa mawaziri na manaibu iliyotolewa na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.
…………………………………………………………………………………………………………………………

Timu ya Tenisi ya Tanzania yashika namba mbili Afrika

TENNIS
Na. Lilian Lundo  – Maelezo
Timu ya mchezo wa Tenisi kwa walemavu (wheelchair tennis) ya Tanzania imeshika namba mbili Afrika katika mashindao ya mchezo huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Nairobi.
Hayo yalisemwa na kocha wa timu hiyo Bw. Riziki Salum leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na vyombo vya habari juu ya ushindi walioupata

BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA RAIS IKULU LAKUTANA LEO

IKU
Katibu Mkuu Ikulu Mhe Peter Ilomo akiongoza kikao cha Baraza la Wafanyakazi  Ofisi ya Rais Ikulu katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 25, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA BALOZI A TANZANIA NCHINI KUWEIT LEO

mam1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Kuweit Dkt. Mahadhi Juma Maalim wakati Balozi Mahadhi alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo Februari 25, 2016 kwa ajili ya kujitambulisha.
mam2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Kuweit Dkt. Mahadhi Juma Maalim wakati Balozi Mahadhi alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu         Dar es salaam leo Februari 25, 2016 kwa ajili ya kujitambulisha. (Picha na OMR)
mam3

TAASISI YA KIISLAMU YA MUZDALIFAT YATOA VIFAA MBALIMBALI VYA HOSPITALI ZANZIBAR.

taa1
Baadhi ya vifaa mbalimbali vya Hospitali vyenye Thamani ya Dola za kimarekani 3,45000 (laki tatu arobaini na tano Elfu)vilivyotolewa na Taasisi ya Kiislamu ya Muzdalifat kwa kushirikiana na Taasisi ya Helping Hand yenye makao Makuu nchini Marekani.
taa2
Wanafunzi wa skuli ya Sekondari ya Farouk Aktas Muslim iliopo kisauni Wilaya ya Magharibi B Unguja  wakihudhuria katika Hafla ya Utoaji wa Vifaa mbalimbali vya Hospitali vyenye Thamani ya Dola za kimarekani 3,45000 (laki tatu arobaini na tano Elfu)kutoka Taasisi ya Kiislamu ya Muzdalifat kwa kushirikiana na Taasisi ya Helping Hand yenye makao Makuu nchini Marekani.
taa3
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Salum katikati akipata maelezo kwa Muakilishi wa Taasisi ya Helping Hand Mohammad Habibu kuhusiana na Vifaa mbalimbali vya Hospitali vyenye Thamani ya Dola za kimarekani 3,45000 (laki tatu arobaini na tano Elfu)vilivyotolewa na  Taasisi ya Kiislamu ya Muzdalifat kwa kushirikiana na Taasisi yake yenye makao Makuu nchini Marekani.hafla iliofanyika Kisauni Wilaya ya Magharibi B Unguja.
taa4
Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Muzdalifat Farouk Hamadi akitoa hotuba ya kumkaribisha Mgeni rasmi katika Hafla ya kutoa Vifaa mbalimbali vya Hospitali iliofanyika Kisauni Wilaya ya Magharibi B Unguja.
taa5
Naibu katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Salum akikabidhiwa Vifaa mbalimbali vya Hospitali vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 3,45000 (laki tatu Arobaini na Tano Elfu) na Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Muzdalifat Farouk Hamadi.wa kwanza kushoto ni Muakilishi wa Taasisi ya Helping Hand yenye makao makuu Nchini Marekani Mohammad Habibu.
taa6
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Salum akitoa hotuba baada ya kupokea Vifaa mbalimbali vya Hospitali vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 3,45000 (laki tatu Arobaini na Tano Elfu) vilivyotolewa na Taasisi ya Muzdalifat Kisauni Wilaya ya Magharibi B Unguja.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

Mchezaji Taifa Stars apongeza Tamasha la Pasaka

IMG_2026
Na Mwandishi Wetu
ALIYEKUWA beki wa kushoto wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Alphonce Modest amelipongeza Tamasha la Pasaka linaloandaliwa na Kampuni ya saa Promotions kwa sababu linawakumbuka wenye uhitaji maalum

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, AMWAKILISHA MAKAMU WA RAIS KUZINDUA TAWI JIPYA LA BENKI YA AMANA MBAGALA DAR ES SALAAM, LEO.

jia1
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji, akifunua kitambaa kama ishara ya kuweka Jiwe la msingi katika Jengo la Benki ya Amana, wakati alipokuwa akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuzindua Tawi jipya la Benki hiyo lililofunguliwa Mbagala Zakiem jijini Dar es Salaam, leo Feb 25, 2016. Kulia ni Mbunge wa Viti maalumu CCM, Mariam Kisangi (kulia kwa Waziri) ni Mkurugenzi wa Amana Benki, Dkt. Muhsin Salim Masoud (na wa pili kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Abdallah Al-Nahdi. Picha na Sufianimafoto Blog
jia2
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi Tawi jipya la Benki ya Amana, wakati alipokuwa akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuzindua Tawi hilo lililofunguliwa leo Feb 25, 2016 Mbagala Zakiem jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Benki hiyo, Dkt. Muhsin Salim Masoud (kushoto) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Abdallah Al- Nahdi. Picha na Sufianimafoto Blog
jia3
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi Tawi jipya la Benki ya Amana, wakati alipokuwa akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuzindua Tawi hilo lililofunguliwa leo Feb 25, 2016 Mbagala Zakiem jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Benki hiyo, Dkt. Muhsin Salim Masoud (kushoto) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Abdallah Al- Nahdi. Picha na Sufianimafoto Blog
jia4
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji, akisoma hotuba yake ya uzinduzi wa Tawi jipya la Benki ya Amana lililofunguliwa Mbagala Zakiem jijini Dar es Salaam, ambapo Mhe. Kijaji alimwakilisha Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwenye uzinduzi huo. Picha na Sufianimafoto Blog
jia5
Mkurugenzi wa Benki Amana, Dkt. Muhsin Salim Masoud, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji, kuzindua Tawi hilo kwa niaba ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan. Picha na Sufianimafoto Blog.
jia6
Baadhi ya wadau na wananchi waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wakimsikiliza Mhe. Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji, wakati akihutubia katika uzinduzi huo, leo. Picha na Sufianimafoto Blog
jia7
Baadhi ya wadau na wananchi waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wakimsikiliza Mhe. Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji, wakati akihutubia katika uzinduzi huo, leo. Picha na Sufianimafoto Blog
jia8
Baadhi ya wadau na wananchi waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wakimsikiliza Mhe. Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji, wakati akihutubia katika uzinduzi huo, leo. Picha na Sufianimafoto Blog

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI MIKOA YA MWANZA, GEITA NA KAGERA

● Aziagiza Halmashauri kushughulikia migogoro ya ardhi
● Azitaka kulisaidia Shirika la Nyumba ili lijenge nyumba za gharama nafuu
● Asema Halmashauri zinunue nyumba zinazojengwa na NHC kwa ajili ya watumishi wao
● Alipongeza NHC kwa kasi ya ujenzi wa nyumba bora katika Halmashauriza Miji na Wilaya
mab01
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akisalimiana na Watumishi wa Hamashauri ya Mji wa Buchosa alipowasili kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi
MAB1
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akipewa maelezo na mtaalam wa mifumo ya uwekaji kumbukumbu za umiliki wa ardhi alipotembelea idara ya ardhi Wilayani Misungwi. Aliyoko katikati ni Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo Bw. Mshana.
MAB2
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula na Mbunge wa Chato Mhe.Dkt  Medard Kalemani wakikagua eneo la  Kijiji cha Rusungwa lenye mgogoro mkubwa wa ardhi unaofanya wananchi wa kijiji hicho kukosa ardhi ya kulima na uwekaji huduma za jamii kama shule baada ya eneo la ekari 500 la kupewa mwekezaji.
MAB4
Meneja wa NHC Mkoa wa Kagera Bw. Deogratius Batakanwa akimpewa maelekezo na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula ya kuhakikisha kuwa anatoa elimu ya kutosha itakayowezesha wananchi, taasisi na Halmashauri ya Muleba kukamilisha ununuzi wa nyumba zilizojengwa na NHC Wilayani Muleba.Naibu Waziri alitembelea nyumba hizo na kulipongeza Shirika la Nyumba kwa ujenzi wa nyumba bora.
MAB5
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akiwa  katika picha ya pamoja na Madiwani wa Halmashauri ya Muleba baada ya kuhutubia Baraza lao na kuliomba liwezeshe ununuzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani humo. Pia aliagiza Baraza hilo kushiriki kikamilifu katika kutatua  migogoro mingi ya ardhi iliyoko katika Wilaya hiyo.
MAB6
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akikagua nyumba zilizojengwa na NHC eneo la Bombambili Mkoani Geita kwa ajili ya kuuza. Amewataka wananchi na Halmashauri ya Mji wa Geita kununua nyumba hizo ili kuliwezesha Shirika kuendelea kujenga nyumba katika Halmashauri zingine.
MAB7
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Mabula akiwa na Mbunge wa Chato Mhe. Dkt Medard Kalemani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini wakikagua nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Chato. Katika ziara hiyo Naibu Waziri ameishauri Halmashauri ya Chato kununua nyumba hizo ili NHC iongeze ujenzi wa nyumba zingine kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya nyumba Wilayani humo.
MAB8
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za NHC Mkoa wa Kagera alipotembelea na kusalimiana na wafanyakazi wa Shirika hilo.
MAB9
Meneja wa NHC Mkoa wa Mwanza Injinia Benedict Kilimba akitoa maelezo ya mradi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Bombambili Geita, kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula alipotembelea mradi huo. Mhe. Naibu Waziri  ameziagiza Halmashauri nchini kusaidia uwekaji wa miundombinu kwenye maeneo ya ujenzi wa nyumba hizo pamoja na kutoa ardhi bure kwa NHC ili nyumba zinazojengwa ziwe na gharama nafuu kwa mnunuzi.
MAB10
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Bibi  Mwajuma Nyiruka akitoa taarifa ya sekta ya ardhi ya Wilaya yake kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula alipoitembelea Halmashauri ya Misungwi kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi.
MAB11
Baraza la Madiwani Muleba wakimsikilza Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline  Mabula (hayuko pichani) alipohutubia Baraza hilo.

KAMPUNI YA KUOSHA MAGARI KWA KUTUMIA MVUKE YA SHINE ECO WASH LIMITED YATUA JIJINI DAR ES SALAAM

AD1
Baadhi ya magari ya wateja yakiendelea kuoshwa katika kampuni ya Shine Eco Wash Limited yenye makazi yake Mlimani City jijini Dar es Salaam.
AD2
Mmoja wa wafanyakazi katika kampuni ya Shine Eco Wash Limited yenye makazi yake Mlimani City jijini Dar es Salaam akiendelea na kazi ya uoshaji.
AD3
Kazi ya uoshaji wa magari ikiendelea katika kampuni hiyo
……………………………………………………………………………………………………………….
Na Greyson Mwase
Kampuni inayojishughulisha na uoshaji wa magari kwa njia ya mvuke imeanza kutoa huduma zake jijini Dar es Salaam.

WIZARA YALAANI MAUAJI YA MTOTO MARIAM DEOGRATIUS (4) ALIYEBAKWA NA KUUAWA ENEO LA MAKOKO, MUSOMA MKOANI MARA

download (2)
Wizara inalaani vikali tukio la kubakwa na kuuawa kikatili kwa mtoto Mariam Deoratius, umri miaka 4, ambaye alifanyiwa ukatili huo na watu wasiojulikana, eneo la Makoko, Manispaa ya Musoma, mkoani Mara, mapema wiki hii. 
Wizara imesikitishwa na mazingira ya mauaji ya mtoto huyo mdogo asiyekuwa na hatia, ambaye aliokotwa kwenye banda linalojengwa akiwa ameharibiwa sehemu zake za siri, kutokwa na damu nyingi na akiwa amefariki dunia. Mauaji haya ni ukiukwaji mkubwa wa haki ya kuishi ya mtoto ambayo ndiyo ni haki yake ya msingi. Haki hii inapovunjwa inarudisha nyuma jitihada za Taifa letu kufanya jamii zetu kuwa mahali salama kwa watoto kuishi.
Wizara inaamini kuwa, Mamlaka zinazohusika na ulinzi wa watoto dhidi ya ukatili katika Mkoa wa Mara hususan Manispaa ya Musoma, kuhakikisha mtuhumiwa anafikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili haki iweze kutendeka, na kuwa
fundisho kwa wanaoendeleza ukatili wa watoto. Kwa tukio hili, jamii inahimizwa kubadilika na kuhakikisha kuwa ulinzi wa watoto ni jukumu la wazazi, walezi na watu wote katika jamii.
Wizara inatoa pole kwa wazazi, ndugu, marafiki na familia ya mtoto Mariam aliyeuawa katika umri mdogo na tunawaomba kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.
  1. S.  Nkinga
              KATIBU MKUU
               25/02/2016

WAZIRI LUHAGA MPINA AKIHOJIWA TBC LEO

mpi1
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano  Mazingira Mh. Luhaga Mpina ,katika vipindi vya radio na Televison asubuhi ya leo, kwenye studio za  Shirika la Utangazaji la Taifa TBC katika kipindi cha Televisheni  cha Jambo Tanzania cha TBC1 na kipindi cha Aasubuhi hii katika kituo cha TBC Taifa..Picha na Evelyn Mkokoi Ofisi ya makamu wa Rais

Wawekezaji sekta ndogo ya gesi watakiwa kuongeza kasi utekelezaji miradi

moe1
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt.  James Mataragio (katikati) akiongea jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kushoto) na wawekezaji wa Kampuni za kutatifi na kuchimba mafuta na gesi nchini. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio.
moe2
Baadhi ya Wawekezaji wa Kampuni za kutafiti na kuchimba mafuta na gesi nchini, wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani) wakati wa kikao chake na wawekezaji hao.
moe3
Baadhi ya Wawekezaji wa Kampuni za kutafiti na kuchimba mafuta na gesi nchini, wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani) wakati wa kikao chake na wawekezaji hao.
moe4
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Dodsal, K. Surendran, akitoa taarifa ya utafiti kuhusu Kampuni hiyo kugundua gesi eneo la Ruvu. Wengine wanaomsikiliza ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati). Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt.

WAANDISHI NCHINI WATAKIWA KUTOKUWA TEGEMEZI NA BADALA YAKE WATUMIE FURSA ZA KIUCHUMI

????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
NA VICTO R MASANGU, PWANI   
WAANDISHI wa habari hapa nchini wametakiwa kuachana na tabia ya kuwa  tegemezi na badala  yake wahakikishe  wanazitumia fursa  mbali mbali za kiuchumi  kwa lengo la kuweza

 

No comments :

Post a Comment