Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim
Taalib (Kushoto) akikabidhi fomu ya Bima ya Afya kwa Ofisa Uendeshaji wa
PPF, Tumgonze KAbigumila baada ya kujaza kwa ufasaha.
Ofisa wa MAsoko wa PPF, Abib Kibiki (aliyesimama)
akiwaelekeza wasanii wa SHIWATA kujaza fomu za kujiunga na PPF na
nyingine kujiunga na Bima ya Afya.
Katibu Mkuu wa SHIWATA, Michael
Kagondela (kulia) akisaidiana na wasanii wa SHIWATA kujaza fomu za
kujiunga na BIMA ya Afya zinazosimamiwa na PPF.
………………………………………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
WANACHAMA zaidi ya 300 wa Mtandao wa Wasanii TAnzania
wamejiunga na Mpango wa TAifa wa Akiba ya Uzeeni (PPF) katika mpango
maalum wa Wote Scheme utakaofanya wajiunge na Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya na kupata mikopo mbalimbali.
Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim
Taalib alisema jana Dar es Salaam wakati wa kuandisha wanachama hao
kujiunga na PPF na kujaza fomu za Bima ya Afya, alisema kupitia mpango
wa Wote Scheme wanatarajia kuwashawishi wanachama wao zaidi ya 8,000
kujiunga.
“Tumepokea kwa furaha mpango wa
PPF kutunganisha kupata bima ya Afya, tunatarajia wanachama wettu wote
wajiunge ili wapate huduma muhimu za matibabu na mikopo mbalimbali kwa
maendeleo yao na familia zao” alisema Mwenyekiti Taalib.
Ofisa Uendeshaji wa PPF,
Tumgonze Kabigumila alisema PPF imejizatiti kusaidia jamii ya watanzania
kupata huduma muhimu za kijamiii kwa gharama ndogo.
Alisema katika mpango wa Wote
Scheme ujikita kusaidia watanzania wasio katika sekta rasmi kama vile
wavuvi, wakulima, wajasiriamali, wanamichezo na wasanii kupata huduma
muhimu.
Alisema kiasi cha chini cha
mwanachama kuchangia kwa mwezi ni sh. 20,000 kila mwezi na ataanza
kupata matibabu akikamilisha sh. 60,000 ambapo atapewa kadi ya bima ya
afya ambayo ataitumia katika hospitali zote nchini kwa magonjwa
mbalimbali.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza mbio
za Wabunge Hapa Kazi Tu Dodoma Half Marathon zilizoanzia Bungeni hadi
uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Januari 30, 2016. Kushoyo kwake ni
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na kushoto ni
Naibu Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson. Mwansasu (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………………………
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,Majaliwa ameyataka mashirikisho ya michezo
mbalimbali kumpa mpango kazi wa muda mrefu na mfupi ili kuiwezesha
Serikali kushirikiana nao kuleta maendeleo ya michezo nchini.
Mhe.Kassim Majaliwa,Majaliwa ameyasema hayo
leo Mijini Dodoma wakati akifunga mashindano ya Hapa Kazi Tu Half
Marathon yaliyoanzia katika Chuo cha Biashara (CBE) tawi la Dodoma na
kumalizikia katika uwanja wa Jamhuri yenye lengo la kuadhimisha kilele
cha Siku 100 za uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe.Dkt John Pombe Joseph Magufuli tangu aingie madarakani.
“ Serikali ya Awamu ya Tano tumejipanga
kuendeleza michezo nchini kwani michezo ni moja kati ya sekta muhimu kwa
maendeleo ya wanamichezo na nchi kwaujumla na pia ni moja ya
kujitangaza kimataifa kupitia michezo mbalimbali”Alisema Mhe Majaliwa.
Aidha Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amesema kupitia wizara yake atajitaidi
kuimarisha michezo hasa ukuzingatioa Serikali imeweka mkazo katika
michezo hivyo yeye kama waziri mwemye dhamana hiyo atalisimamia kwa
karibu suala la maendeleo ya michezo yote .
“Naahidi kushirikiana na vyama vya michezo
ili kuimarisha sekta ya michezo kwa kuweka mipango thabiti ya kusimamia
na kuiendeleza michezo ili iweze kuleta tjia katika jamii ya
watanzania”Alisema Mhe. Nnauye.
Mbio hizi za Hapa Kazi Tu Half
Marathon zilmeshirikisha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Dkt Tulia Ackson,baadhi ya mawaziri, wabunge na watu wa
rika zote kwa kukimbia umbali wa kilometa 2, kilometa5 na kilometa21 na
washindi kupewa zawadi za pikipiki, mabati na fedha taslimu.
Mashindano haya ya hapa kazi Half Marathon
yaliyoandaliwa na Chama cha Riadha Tanzania na kudhaminiwa na kampuni ya
GSM, TANAPA, Kilimanjaro International Airport,East Teanders, CRDB Bank
na DSTV yameandaliwa kwa nia ya kuandaa timu ya Riadha ya Tanzania
kujiandaa na mashindano ya Olompiki yatakayofanyika Rio de Janeiro
nchini Brazil.
Watumishi wa afya wawe wabunifu,Dkt.Kigwangala
Naibu waziri wa afya,maendeleo ya
jamii,jinsia,wazee na watoto,Dkt.Hamisi Kigwangala(katikati)
akizungumza na viongozi wa hospitali ya Mount Meru mara baada ya
kutembelea sehemu mbalimbali za hospitali hiyo,kulia ni mganga mkuu wa
mkoa Dkt.Frida Mokiti kushoto ni Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo
Dkt.Jackline Urio
Dkt.Kigwangala akiwa amembeba mtoto mchanga(hajapewa jina bado) wa Bi.Jamila Petro alipotembelea wodi ya wazazi hospitalini hapo
Licha ya kutembelea wodi
mbalimbali za wagonjwa,Dkt. Kigwangala pia alitembelea maabara ya
hospitali hiyo na kuridhika na vifaa vilivyopo kwenye hospitali,kushoto
ni mtaalamu wa viwango vya maabara,Felix zelote,akimpatia maelezo waziri
huyo
……………………………………………………………………………………….
Na Catherine Sungura_ WAMJW_Arusha
Watumishi wa sekta ya afya watakiwa kuwa wabunifu ili kuweza kutoa huduma kwa watu wote hususani wenye kipato cha juu
Watumishi wa sekta ya afya watakiwa kuwa wabunifu ili kuweza kutoa huduma kwa watu wote hususani wenye kipato cha juu
Hayo yamesemwa leo na Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dkt. Hamisi
Kigwangala wakati akitembelea hospitali ya mount meru mkoani arusha
Amesema hospitali zinatakiwa
kusimama zenyewe Kwa ukusanyaji wa mapato,hivyo ipo ulazima wa kujenga
au kukarabati majengo ambayo wanaweza kufanya wodi za kulipia ambazo
zitakua zenye ubora ambao utawafanya watu Wenye pesa kuja kupata huduma
kwenye hospitali za umma kuliko hivi sasa wanakimbilia hospitali binafsi
“Hii itaifanya serikali kupata pesa ambazo sehemu kubwa zitatumika kuwahudumia watu wenye kipato cha chini hospitalini hapo
Aidha,Dkt.Kigwangala alisema
licha ya serikali kupata pesa,watoa huduma pia wakiwemo
madaktari,wauguzi pamoja na kada zingine kupata motisha ambazo
zitawafanya kuwapa moyo wa kuwahudumia wagonjwa law hali na Mali.
“Kama matajiri hawaji kwenye hospitali Za umma,mnategemea hawa maskini watapata pesa wapi za kulipia huduma?aliuliza.
Hata hivyo Naibu Waziri huyo
alisema wateja wengi wanapokuja kupata huduma Kwenye vituo vya huduma ya
serikali,wanakata tamaa kwakuwa wanakuta hakuna watoa huduma,dawa wala
vifaa tiba hivyo wanakimbilia huko pa kulipia
“Lengo letu sio kuua hospitali
binafsi bali tunataka muimarishe huduma za kulipia ili tupate pesa za
kuwahudumia wasio na uwezo na ninyi watoa huduma was serikali mpate
sehemu yenu ili muweze kufanya kazi kwa ufanisi
Serikali yahimiza matumizi sahihi ya takwimu.
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AHUDHURIA MKUTANO WA WAKUU WA AFRIKA ETHIOPIA LEO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea shada la Maua
kutoka kwa Mtoto Yuthra Bawaid alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Bolo Nchini Ethiopia leo Januari 30, 2016 kwa ajili ya kuhudhuria
Mkutano wa 26 kwa Wakuu wa Nchi za Afrika unaoanza leo mjini Addis Ababa
Ethiopia
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Gwaride la
Heshima kutoka kwa Jeshi la Ethiopia alipowasili Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Bole kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 26 kwa wakuu wa
Nchi za Afrika ulioanza leo Januari 30,2016 Mjini Addis Ababa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mwambata
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Nchini Ethiopia Meja Generali John
Bishoge alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole kwa ajili ya
kuhudhuria Mkutano wa 26 kwa wakuu wa Nchi za Afrika ulioanza leo
Januari 30,2016 Mjini Addis Ababa Ethiopia
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Bole kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 26 kwa wakuu wa
Nchi za Afrika ulioanza leo Januari 30,2016 Mjini Addis Ababa Ethiopia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifuatilia kwa Makini
mkutano wa 26 wa Wakuu wa Nchi za Afrika ulioanza leo Mjini Addis Ababa
Ethiopia. (Picha na OMR)
Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Tanzania Standard Newspapers Limited chafanyika leo jijini Dar es salaam
Mhariri Mtendaji wa magazeti ya
serikali ya Daily News, Habari Leo na SpotiLeo, Gabriel Nderumaki
akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi jijini Dar es Salaam jana
kilichokuwa kinajadili Bajeti ya nusu mwaka wa fedha 2015- 2016.Kulia ni
Katibu wa baraza hilo, Shafii Mpenda.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi
la Shirika la magazeti ya serikali ya Daily News, Habari Leo na
SpotiLeo, wakishiriki majadiliano wakati wa kikao cha baraza la
wafanyakazi kilichokuwa kinafanyika Dar es Salaam jana kujadili Bajeti
ya nusu mwaka wa fedha 2015- 2016 ya taasisi hiyo.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi
la Shirika la magazeti ya serikali ya Daily News, Habari Leo na
SpotiLeo, wakishiriki majadiliano wakati wa kikao cha baraza la
wafanyakazi kilichokuwa kinafanyika Dar es Salaam jana kujadili Bajeti
ya nusu mwaka wa fedha 2015- 2016 ya taasisi hiyo.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi
la Shirika la magazeti ya serikali ya Daily News, Habari Leo na
SpotiLeo, wakishiriki majadiliano wakati wa kikao cha baraza la
wafanyakazi kilichokuwa kinafanyika Dar es Salaam jana kujadili Bajeti
ya nusu mwaka wa fedha 2015- 2016 ya taasisi hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Dkt.
Mahadhi Juma Maalim kuwa Balozi wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Luteni Jenerali Venance Salvatory
Mabeyo kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi
Clodwig Mathew Mtweve kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ikulu
jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi
Paul Amani Moses Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Ikulu
jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Mnadhimu Mkuu wa
JWTZ MStaafu Luteni Jenerali (Rtd) Samuel Albert Ndomba baada ya
shughuli ya kiapo Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Ombeni Sefue na viongozi wa Jeshi la Wananchi na Jeshi la Polisi katika
picha ya pamoja baada ya kuapishwa Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa
Tanzania Kuwait na Katibu Tawala wa Mikoa ya Katavi na Mwanza Ikulu
jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na viongozi wa Jeshi la
Wananchi na Jeshi la Polisi katika picha ya pamoja baada ya kuapishwa
Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na Katibu Tawala wa
Mikoa ya Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30,
2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akifurahia jambo na viongozi
wa Jeshi la Wananchi na Jeshi la Polisi katika picha ya pamoja baada ya
kuwaapisha Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na Katibu
Tawala wa Mikoa ya Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo
January 30, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na msemaji wa JWTZ
Luteni Kanali Ngeleba Lubinga baada ya kuapishwa Mnadimu Mkuu wa TPDF,
Balozi wa Tanzania Kuwait na Katibu Tawala wa Mikoa ya Katavi na
Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Naibu Inspekta
Jenerali wa Polisi Abdulrahman Kaniki baada ya kuapishwa Mnadimu Mkuu
wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na Katibu Tawala wa Mikoa ya Katavi
na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016.
PICHA NA IKULU
SERIKALI YATOA VIPAUMBELE VYAKE KWA WANANCHI.
Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu akisistiza wakati wa
mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam
kuhusu mapato na matumizi ya Serikali yalivyoboreshwa na uchumi wa nchi
kuimarika na kutengemaa.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile leo jijini
Dar es salaam kuhusu Serikali ilivyojipanga kuboresha na kuhudumia sekta
mbalimbali nchini ikiwemo elimu, umeme, maji na miundombinu.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango)
…………………………………..
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
Serikali
imetoa jumla ya Sh. Bilioni 318.406 kwa mwezi wa Januari mwaka 2016,
kwa ajili ya miradi ya maendeleo nchini na Sh. Bilioni 538.5 kwa
mishahara ya watumishi wa Umma.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Servacius Likwelile alisema kuwa Serikali inajivunia kufanikiwa kutumia fedha za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo hadi sasa Serikali imetumia kiasi cha Sh. Bilioni 71.2 tu kutoka fedha za nje.
Dkt. Likwelile alisema mapato yanayokusanywa nchini yamewezesha kutekeleza sera ya elimu bure ambapo mwezi Desemba mwaka 2015 Serikali ilitoa kiasi cha Sh. Bilioni 18.77 kwa shule za msingi na sekondari kwa ajili ya ruzuku, ada na chakula kwa shule za bweni pamoja na mahitaji mengine ambapo mwezi wa Januari 2016 Serikali imetoa kiasi cha Sh. Bilioni 18.77 kwa ajili ya kutekeleza Sera hiyo.
Aliongeza kuwa katika ulipaji wa madeni ya wakandarasi nchini , Serikali imetoa Sh. Bilioni 130 kwa mwezi Januari mwaka 2016 ambapo mwezi Desemba mwaka 2015 ilitoa Sh. Bilioni 193.
Kwa upande wa Mfuko wa Barabara, Katibu Likwelile alifafanua mradi huo umetengewa kiasi cha Sh. Bilioni 47.89 na kuongeza kuwa Benki kuu ina fungu la mfuko huo ambapo nayo imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 76.3.
Dkt. Likwelile alisema kuwa Halmashauri zitapelekewa kiasi cha Sh. Bilioni 20.52 kwa ajili ya kuboresha barabara na jumla mfuko huo kufikia kiasi cha Sh. Bilioni 274.71.
Akifafanua kuhusu miradi ya umeme, Dkt. Likwelile alisema kuwa mwezi Desemba mwaka 2015 Serikali ililipa deni la TANESCO kiasi cha Sh. Bilioni 80 za mradi wa Kinyerezi II na kwa mwezi Januari mwaka 2016 kiasi cha Sh. Bilioni 40 zimetengwa kwa ajili ya mradi huo.
Hali hii imefikisha kiasi cha Sh. Bilioni 120 kwa ajili ya kulipa madeni na kuendeleza uzalishaji wa umeme nchini.
Alisema kiasi cha Sh. Bilioni 21.959 kimetengwa kwa ajili ya mradi wa umeme vijijini na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ina mfuko wa mradi huo ambao kwa sasa una kiasi cha Sh. Bilioni 21.9 na kuongeza kuwa huduma ya umeme kwa wananchi itaimarika.
Alifafanua kuwa Serikali imeanzisha mfuko wa maji Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambapo mpaka sasa mfuko huo una jumla ya kiasi cha Sh. Bilioni 46.3.
Aidha, BoT imetoa Sh. Bilioni 12.5 kuendeleza miradi ya maji ambapo kwa Januari mwaka 2016 Serikali imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 7.7.
Serikali imetenga kiasi cha Sh Bilioni 82.2 kwa mwezi wa Januari ili kuweza kulipa pensheni za wastaafu, na kwa wale wastaafu walio katika daftari la kudumu ambapo wametengewa kiasi cha Sh. Bilioni 33.3 kwa ajili ya malipo yao.
Wabunge wametengewa kiasi cha Sh. Bilioni 35.5 kwa ajili ya mkopo wa magari ambapo kila mbunge atapata kiasi cha Sh. Milioni 90, kiasi cha Sh. Milioni. 45 ni ruzuku na Sh. Mil. 45 ni mkopo ambao utalipwa ndani ya miaka 5.
Aidha, Serikali imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 784.3 kwa ajili ya kulipa deni la taifa.
Naye Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata alibainisha kuwa hali ya makusanyo ya mapato nchini iko vizuri ambapo kwa mwezi Januari 2016, makadirio yalikuwa Sh. Trilioni 1 na Bilioni 45 na hadi kufikia sasa kiasi cha Sh. Trilioni 1 na Bilioni 31 zimeshakusanywa.
Matarajio ya TRA ni kukamilisha kukusanya kiasi cha Sh. Billioni 14 zilizosalia.
Aidha, Kidata alibainisha kuwa uingizaji wa bidhaa kupitia bandarini bado uko vizuri licha ya minong’ono kuwa uzuiaji wa mianya ya ukwepaji kodi imepunguza uingizaji bidhaa ambapo kwa mwezi Januari Bilioni 111 zimekusanywa kutokana na ushuru wa forodha.
Kidata alitoa wito kwa kila mtanzania kulipa kodi na kutoa taarifa za wakwepa kodi ili kuweza kukuza mapato ya nchi.
Kwa upande wake Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu amepongeza juhudi za ukusanyaji wa mapato na udhibiti wa matumizi ya fedha za Serikali.
Alisema kuwa uchumi umekua na unazidi kuimarika licha ya changamoto za kiuchumi duniani ambapo uchumi wa nchi umekua kwa asilimia 7 na unategemewa kukua miezi ijayo kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji nchini.
Mfumuko wa bei unaendelea kubaki ndani ya kiwango cha tarakimu moja, licha ya ongezeko dogo katika miezi ya hivi karibuni kutokana na kupanda kwa bei za vyakula.
Alisema kuwa mfumuko wa bei ulikuwa asilimi 6.8 mwaka 2015, ukilinganishwa na asilimia 6.1 kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 2015.
Wakati huo huo mfumuko wa bei usiojumuisha chakula na nishati uliendelea kubaki katika viwango vya chini ya asilimia 2.5 kutokana na hatua mbalimbali za kisera zilizochukuliwa na BoT.
Prof. Ndulu alifafanua mapato ya fedha za kigeni yanaendelea vizuri ingawa bei ya dhahabu imeshuka kutoka Bilioni 2.5 hadi Bilioni1.3.
Sekta ya utalii imesaidia kuimarisha fedha za kigeni kwani mapato yameongezeka kutoka Bilioni 1.5 hadi Bilioni 2.2.
Sekta ya viwanda nayo imeshika nafasi ya pili katika kuongeza fedha za kigeni nchini ambapo mwaka 2015 mapato yalikuwa Bilioni 1 na kwa sasa yamefikia Bilioni1.5.
Aidha, Prof. Ndulu aliongeza kuwa sekta ya usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi imesaidia kuimarisha fedha za kigeni ambapo mapato yamefikia Dola Bilioni11 kwa mwaka.
Hadi kufikia sasa Tanzania imenufaika kutokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika uingizaji bidhaa hiyo kwa asilimia 44.
Serikali inatarajia kuendelea kuimarisha uchumi ili kufikia azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati hadi ifikapo 2025.
Imetolewa na Wizara ya Fedha na Mipango
Kitengo cha Mawasiliano
No comments :
Post a Comment