Hivi karibuni kumekuwa na uvumi unaoeleza kuwa JWTZ limetoa nafasi za
kazi kwa vijana wenye fani ya Udaktari na kuwataka vijana hao kuripoti
Makao Makuu na vyeti vyao kwaajili ya usaili.
Habari hizo si za kweli,JWTZ kama zilivyo taasisi nyingine za serilikali
lina mfumo rasmi wa kutangaza habari zake hivyo jeshi linawaomba
wananchi wazipuuzie taarifa hizo.
Aidha JWTZ linawataka wamiliki wa mitandao ya kijamii kutotoa taarifa za
jeshi bila kuwasiliana na Makao Makuu ya jeshi kinyume na utaratibu
huu,unawasababishia wananchi usumbufu usio wa lazima.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu JWTZ.
No comments :
Post a Comment