Friday, January 22, 2016

.Rais Magufuli awasilimia Wakazi wa Jiji la Arusha pamoja na kufunga Maonesho ya Onesha Uwezo Medani Chuo cha Kijesho Monduli Mkoani Arusha

POM1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wa Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha waliojitokeza kumsalimia wakati akielekea Monduli kwa ajili ya kufunga zoezi la Onesha uwezo Medani.
POM2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisoma bango mara baada ya kukabidhiwa na mwananchi mmoja katika eneo la Kona ya Nairobi Mkoani Arusha
POM3
Umati mkubwa uliojitokeza katika eneo la Mianzini Mkoani Arusha
POM4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Arusha katika eneo karibu na chuo cha Arusha Tech. Wananchi hao walifunga barabara ili wapate nafasi ya kumuona Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli
POM5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Mianzini Mkoani Arusha.
POM6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis Mwamunyange wakati waufungaji wa zoezi la Onesha Uwezo Medani lililofanyika Monduli nje kidogo ya Jiji la Arusha.
POM7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis Mwamunyange wakati akielekea kupewa maelezo ya zoezi zima la Onesha Uwezo Medan.
POM8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa jeshi katika tukio hilo la Ufungaji.
POM9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kwenye uwanja wa maonesho akiwa pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis Mwamunyange.
POM10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa ngazi za juu wa Jeshi mara baada ya kufunga zoezi la Onesha Uwezo Medani Monduli Mkoani Arusha.
POM11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akishuhudia matukio ya zoezi la Onesha Uwezo Medani Monduli Mkoani Arusha.
POM12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipewa maelezo ya zana mojawapo ya Kivita katika Zoezi la Onesha Uwezo Medani Mkoani Arusha. Picha na IKULU
…………………………………………………………………………………………………………..
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunga “Zoezi la Onesha Uwezo Medani” lililoandaliwa na kutekelezwa na Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu ambalo ni sehemu ya Jeshi la wananchi Tanzania katika eneo la Lang’arurusu nje kidogo ya Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli Mkoani Arusha.
Akizungumza na Askari na Maafisa wa Jeshi la wananchi Tanzania kabla ya kufunga zoezi hilo, Rais Magufuli amesema katika awamu yake ya tano ya uongozi amedhamiria kulitumia Jeshi la wananchi Tanzania katika kujenga uchumi, ikiwemo kuanzisha viwanda na kampuni za ujenzi ili kuharakisha maendeleo.
Ametoa mfano wa kiwanda cha Nyumbu ambacho kipo chini ya jeshi la wananchi Tanzania na kueleza kuwa wakati umefika wa kukiimarisha na kukiendeleza kiwanda hicho, ili kiweze kufanya uzalishaji mkubwa kwa manufaa ya nchi ikilinganishwa na hali ilivyo hivi sasa.
“Zipo nchi nyingi ambazo majeshi yao yanatumika katika uchumi na yanafanya kazi nzuri ya kupigiwa mfano, wakati umefika na sisi kufanya hivyo. Hata hizi sare za jeshi na viatu, hatuna sababu ya kuvinunua kutoka nje ya nchi, tunaweza kutengeneza sisi wenyewe” Alisisitiza Rais Magufuli.
Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kuandaa “Zoezi Onesha Uwezo Medani” ambalo limethibitisha uwezo, weledi na utayari lilionao katika jukumu lake la kiulinzi.
Ameahidi kuwa ataendeleza juhudi zilizofanywa na viongozi wenzake waliotangulia za kuliimarisha kwa vitendea kazi na maslai ya wanajeshi ili liweze kutekeleza wajibu wake bila vikwazo.
Pamoja na kuwapongeza Askari na maafisa wa Jeshi la wananchi Tanzania walioshiriki katika zoezi hilo, Rais Magufuli ameagiza Askari Mgambo na Askari wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) walioshiriki zoezi hilo kuajiriwa na jeshi la wananchi Tanzania.
Akitoa maelezo ya awali kabla ya hotuba ya Rais Magufuli, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Wizara yake itaongeza na kusimamia juhudi za kuliboresha jeshi hilo kwa zana, vifaa na maslai kwa wanajeshi ili kuwajengea uwezo na morali ya kutekeleza majukumu yao ya kuilinda nchi, pamoja na kutoa msaada stahiki kwa nchi zenye kuhitaji ulinzi wa amani popote duniani.
Kwa upande wake Mkuu wa majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Adolf Mwamunyange amemhakikishia Rais Magufuli kuwa Jeshi la wananchi Tanzania lipo imara na litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi, nidhamu ya hali ya juu na uzalendo mkubwa.
Kabla ya kuwahutubia maafisa wa jeshi la wananchi, Askari na wananchi waliohudhuria ufungaji wa “Zoezi Onesha Uwezo Medani”, Rais Magufuli ameoneshwa zana mbalimbali za kivita ikiwa ni pamoja na kushuhudia upigaji wa mizinga ya masafa mafupi, masafa ya kati na masafa marefu.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Arusha
22 Januari, 2016

 

Nyota wa kikapu wa Malawi kuzikabili timu za Dar es salaam


 Mratibu wa Sprite BBall Kitaa Karabani Karabani akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar-es- Salaam kuhusu mechi za kirafiki zitakazochezwa Jumamosi na Jumapili katika uwanja wa BBK Park na timu kutoka Malawi. Wa kwanza kulia waliokaa ni mkurugenzi wa ufundi chama cha mpira wa kikapu Malawi Obed Nyirongo, wengine ni wachezaji wa timu ya Bricks na Brave Hearts.
 Mkurugenzi wa ufundi chama cha mpira wa kikapu Malawi Obed Nyirongo  kiongeana waandishi wa  wa habari leo jijini Dar-es- Salaam kuhusu  mechi za kirafiki zitakazochezwa Jumamosi na Jumapili katika uwanja wa BBK Park na timu kutoka Malawi wa Sprite BBall Kitaa. Wa kwanza kushoto waliokaa ni mratibu wa Sprite BBall Kitaa Karabani Karabani na wengine ni wachezaji wa timu ya Bricks na Brave Hearts.
*************************
Miamba miwili ya mpira wa kikapu kutoka nchini Malawi imewasili jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya mfululizo wa mechi za kirafiki za kimataifa dhidi ya timu za bigwigs Jogoo, East Zone One, Mbezi na West Zone Three. Mechi hizo zenye hamasa ya aina yake zitachezwa kwenye uwanja Bball Kitaa Park, karibu na Ukumbi wa Gymkhana.
Kulingana na ratiba iliyotolewa na mratibu wa Bball Kitaa Karabani Karabani pazia la michezo hiyo litafunguliwa kesho ambapo East Zone One watakipiga na Bricks, mchezo unaotabiriwa kuwa ni mgumu na wa kusisimua. Siku hiyo hiyo Mbezi watacheza na Associate Team, mchezo ambao pia unatazamiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Michezo hiyo bado itaendelea kuwateka wakazi wa jiji la Dar es Salaam, ambapo West Zone Three watapambana na Bricks kabla ya Jogoo kuwakaribisha Associate team. “Tuna furaha kubwa kuandaa michezo hii ya kirafiki. Ni moja ya sehemu muhimu katika kudumisha mahusiano, vile vile kuendeleza vipaji vinavyochipukia”, Karabani alisema.
Ujio wa Bricks na Associate teams jijini Dar es Salaam imeonekana si jambo geni baada ya timu za East Zone One na West Zone Three kwenda Malawi mwaka jana. Zikiwa nchini humo, timu hizo zilishinda mechi zao kadhaa.
Karabani ambaye michuano yake ya mpira wa kikapu iko chini ya udhamini wa Sprite, amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuibua na kukuza vipaji  vya vijana kwa kipindi cha miaka mitatu ambapo michuano hiyo imekuwa ikifanyika. Vilevile michuano hii inatoa fursa ya kuendeleza ushirikiano baina ya maeneo mbalimbali ya ndani ya nje ya nchi.
 “Lengo letu ni kuanzisha michuano ngazi ya kanda mwishoni mwa mwaka huu, ambapo mabingwa kutoka Tanzania, Malawi, Zambia na Zimbabwe”, Karabani alisema na kuongeza kuwa uzinduzi wa michuano hiyo utafanyika nchini Malawi
Kwa upande wake, Meneja Biashara wa Coca-Cola nchini, Maurice Njowoka alisema anajisikia furaha kubwa kutokana na heshima waliopewa kuisapoti michuano hiyo hapa nchini na kusisitiza kuwa kampuni yake itaendeleza ushirikiano wake na wadau wa mchezo wa kikapu kuzidi kuutangaza mchezo huo.
 “Sote tunafahamu kuwa mpira wa kikapu ni moja ya michezo maarufu na yenye nguvu nchini, hasa miongoni mwa vijana ambao wanahitaji aina hii ya msaada ili kuhamasika na kuweza kuendeleza vipaji vyao”, Njowoka alisema.

TIGO WAZINDUA UDHAMINI WA MBIO ZA NUSU MARATHON MJINI MOSHI

Meneja
Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu udhamini wa Tigo katika mbio za Kili NusuMarathon ambapo mbio hizo zitafanyika Februari
28, Wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka
pande mbalimbali za dunia.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.
 
 Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo, akifafanua jambo   kwa waandishi wa habari kuhusu udhamini wa Tigo kwa mbio za Nusu Marathon mbio hizo zitafanyika Februari
28, Wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka
pande mbalimbali za dunia.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.
 
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga(watatu kushoto, ).akizindua mbio za Kilimanjaro Marathon kwa upande wa Moshi. Wengine ni wadhamini wakuu wa mbio hizo kutoka kushoto, Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo, Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania-Kilimanjaro na Tanga, Richard Temba, Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro, Listone Metacha na Meneja Masoko wa Kampuni ya mafuta ya GAPCO, Caroline Kakwezi.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.
 
Wageni waalikwa ambao  ni wadhamini wa Kili Marathon wakifurahia jambo baada ya Mkuu wa wilaya Mh Novatus Makunga kuzindua mbio za Kili Marathon kwa upande wa Moshi ambapo zitafanyika hizo zitafanyika Februari
28, Wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka
pande mbalimbali za dunia.
Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.
ASHANTI YAONDOLEWA KOMBE LA SHIRIKISHO
Kikao cha Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kilichoketi jana na kupitia taarifa mbalimbali za michezo ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mzunguko wa pili, kimeiondoa klabu ya Ashanti United kwenye michuano hiyo na nafasi yake kuchukuliwa na klabu ya Africa Lyon.
Katika kikao hicho kamati ilipokea malalamiko ya klabu ya Africa Lyon dhidi ya Ashanti United kwa kumchezesha mchezaji Enock Balagashi kwa jina la Awesu Abdu katika mchezo namba 3, uliochezwa tarehe 15 Disemba, 2015 na Ashanti kuibuka na ushindi kwa mikwaju ya penati.
Kamati imejiridhisha baada ya kupitia taarifa ya mchezo huo, na kubaini klabu ya Ashanti United ilifanya udanganyifu wa kumtumia mchezji huyo kwa jina la mchezaji mwingine, huku ikitambua kuwa kufanya hivyo ni makosa na mchezo huo ulikuwa ukionyeshwa moja kwa moja kwenye kituo cha luninga cha Azamtv.
Kwa mujibu wa Kanuni no. 41 (12) ya uthibiti wa viongozi kufungiwa miezi 12, Kamati imemfungia Katibu Mkuu wa klabu ya Ashanti kutojihusisha na masuala ya mpira wa miguu kwa kipindi cha miezi 12.
Aidha Kamati pia kwa kutumia kanuni ya 37 (15) ya udhibiti wa wachezaji, mchezaji Enock Balagashi amefungiwa kwa kucheza mpira kwa kipindi ch amiezi 12 na faini ya shilingi laki tatu (300,000).
Kamati imevitaka vilabu vya ngazi zote nchini kuheshimu vipindi vya usajili kwa kufanya usajili wa wachezaji watakaowatumia, na kuheshimu kanuni na taratibu zinazoendesha michuano inayoandaliwa na TFF.
Africa Lyon watacheza dhidi ya Azam FC mznguko wa tatu siku ya Jumatatu katika Uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

Watumishi NEC wapongezwa kwa kufanikisha Uchaguzi Mkuu 2015

NE1
Afisa Ufuatiliaji toka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw.  Ambrose Manyanda akielezea mafao mbalimbali yanayotolewa na mfuko huo kwa watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) hawapo pichani,  wakati wa kikao kazi kilichofanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
NE2
: Afisa Ushirika toka Manispaa ya Ilala Bi. Mihayo Malunde akielezea umuhimu wa Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuanzisha kikundi cha akiba na mikopo (SACCOS) wakati wa kikao kazi kilichofanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
NE3
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Ramadhan Kailima (aliyesimama) akiwakaribisha wajumbe na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi wakati Wajumbe hao na Mwenyekiti walipokwenda kuwashukuru na kuwapongeza watumishi wa tume hiyo kwa kuweza kufanikisha zoezi la uchaguzi kwa mafanikio makubwa.
NE4
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akiongea na watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakati alipokwenda kuwashukuru na kuwapongeza watumishi wa tume hiyo kwa kuweza kufanikisha zoezi la uchaguzi kwa mafanikio makubwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
NE5
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Ramadhan Kailima (aliyesimama) akifurahia jambo na watumishi wa tume hiyo wakati  Wajumbe na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi  walipokwenda kuwashukuru na kuwapongeza watumishi wa tume hiyo kwa kuweza kufanikisha zoezi la uchaguzi kwa mafanikio makubwa
Picha zote na Eliphace Marwa -Maelezo

RIPOTI YA TATHMINI MAZINGIRA YA KISHERI KATIKA MWITIKIO WA UKIMWI TANZANIA YA ZINDULIWA DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar (ZAC), Dk.Ali Ali (katikati), Kaimu Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Jumanne Issango (kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP), Titus Osundina wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi wa ripoti ya tahmini ya mazingira ya kisheria katika mwitikio wa ukimwi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliofanyika Makao Makuu ya Tacaids Dar es Salaam leo asubuhi.
 Viongozi hao wakiwaonesha wageni waalikwa na wadau mbalimbali ripoti hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tacaids, Elizabeth Kaganda na kilia ni Dk.Bwijo Bwijo kutoka UNDP.
 Naibu Mkurugenzi Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP), Titus Osundina, akihutubia wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar (ZAC), Dk.Ali Ali (kushoto), Kaimu Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya
Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Jumanne Issango (katikati) wakimpongeza Naibu
Mkurugenzi Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP), Titus Osundina baada ya kuhutubia.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Uzinduzi ukiendelea.
Wadau wakiwa katika uzinduzi huo.
Picha ya pamoja na viongozi.
 
Wasanii wa Hisia Threatel Group kutoka Sandali Temeke jijini Dar es Salaam wakionesha igizo linalohusu ukimwi katika uzinduzi huo.

ZANTEL YATOA 20 M/- KUSAIDIA WANAFUNZI WENYE UONI HAFIFU KISIWANDUI

ZANTEL
MKURUGENZI Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akisaini barua ya kampuni yake kwa ajili ya kuwa mlezi wa darasa la wanafunzi wenye ulemavu wa uoni wa skuli ya msingi Kisiwandui mjini Zanzibar. Zantel pia walikabidhi msaada wa shilingi milioni 20 kwa ajili ya kununulia vifaa vya matumzi ya wanafunzi hao. Wengine kutoka kulia ni Mwalimu Mkuu wa skuli hiyo Bi. Taifa Ahmed Khamis, Mkurugenzi wa Elimu ya Maandalizi na Msingi, Bi. Safia Ali Rijali, na mwisho kushoto ni Shinuna Kassim, Mkurugenzi wa Mipango ya Biashara wa Zantel.
ZANTEL2
MKURUGENZI Mkuu wa kampuni Zantel, Benoit Janin akimkabidhi Mwalimu Mkuu, Bi. Taifa Ahmed Khamis mfano wa hundi ya shilingi milioni 20 kwa ajili ya kununulia vifaa vya wanafunzi wenye ulemavu wa uoni wa skuli ya msingi Kisiwandui.
…………………………………………………………….
Na Salum Vuai
KAMPUNI ya simu ya Zantel, leo imeukabidhi uongozi wa skuli ya msingi Kisiwandui hundi ya shilingi milioni 20, kwa ajili ya kununulia vifaa vya wanafunzi wenye uoni hafifu.
Hundi hiyo ilikabidhiwa kwa mwalimu mkuu wa skuli hiyo Bi. Taifa Ahmed Khamis, na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Bw. Benoit Janin, katika hafla fupi iliyofanyika skulini hapo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Janin alisema msaada huo ni sehemu ya mikakati ya kampuni yake, katika kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata elimu bora bila kujali tofauti za kimaumbile.
Alieleza kuwa, ni wajibu wa kampuni hiyo kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata msaada kama wanavypata watu wengine, na pia kuweza kuwaandaa kwa ajili ya kuweza kufikia malengo yao kama walivyokusudia.
“Kama sehemu ya jamii, tumedhamiria kuwasaidia kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu kwa kuwapatia vifaa wanavyovihitaji ili waweze kupata elimu bora,” alieleza Mkurugenzi huyo.
Aidha, alisema kuanzia leo, kampuni yake imeamua kuwa mlezi wa darasa la wanafunzi wenye uoni hafifu katika skuli hiyo, kwa kuwapatia mahitaji yao ili waweze kusoma bila matatizo.
Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa skuli hiyo Bi. Taifa Ahmed Khamis, akiushukuru uongozi wa Zantel, alisema msaada huo ni wa kipekee na utarahisisha ufundishaji kwa wanafunzi hao wenye matatizo ya uoni, na hivyo kuwawezesha kupata elimu bora kama ilivyo kwa wengine.
“Tunawashukuru Zantel kwa kuziona changamoto zinazotukabili, na hakika msaada huu utatusaidia katika kuwafundisha wanafunzi hawa na pia kuwawezesha kufikia malengo yao,” alifafanua.
Alitaja miongoni mwa changamoto hizo kuwa ni mashine za nukta nundu, karatasi za kuchapishia, miwani pamoja na fimbo maalumu kwa watu wasioona (white canes).
Naye mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Maandalizi na Msingi Bi. Safia Ali Rijali, pamoja na kuishukuru Zantel katika kusaidia jitihada za serikali kuleta maendeleo, alisema elimu ni muhimu kwa kila mwananchi hata wenye ulemavu.
Aliwasisitiza wazazi na walezi kutowatenga watoto wenye ulemavu kwa kuwakosesha haki ya kusoma, kwani wakipewa fursa wanaweza kufanya makubwa na kuwa mfano kwa wengine.
Alitoa mfano wa mwanafunzi mmoja asiyeona aliyekuwa akisoma Kisiwandui, kwa namna alivyokuwa mahiri hata akaweza kuchukua digrii ya sheria.
Mkurugenzi huyo ameziomba taasisi na kampuni nyengine kuiga mfano wa Zantel kujikita katika kusaidia jamii kwa mahitaji mbalimbali, yakiwemo ya kielimu, kiafya na mengine.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO-ZANZIBAR- JANUARI 22, 2016

AHUKUMIWA MIAKA 19 JELA KWA KUIBA MBUZI MKOANI MBEYA

Na Ezekiel Kamanga,,Mbozi.
…………………………………………….
MAHAKAMA ya mwanzo vwawa mjini wilayani Mbozi mkoani Mbeya imemuhukumu Patrick Moses(19) mkazi wa Ilembo  kutumikia jela miaka mitano baada ya kukiri kosa la kuiba Mbuzi mmoja mwenye thamanai ya Sh 85,000 mali ya Bahati Mtafya.
Akisoma hukumu hiyo hakimu wa mahakama hiyo,lazima Mwaijega alisema kutokana kifungu cha sheria 268 na mshitakiwa kukiri kosa hivyo mahakama imeamuru mshitakiwa kutumikia kifungo hicho ili iwe fundisho kwake na kwa wengine wenye nia ya kutenda kosa kama hilo.
Mshitakiwa alipopewa nafasi ya kujitetea aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwani anategemewa na familia yake,hata hivyo hakimu Mwaijega amesema kifungo hicho cha miaka mitano amepunguziwa pia kwa kuwa ni kosa lake la kwanza na kwamba.
Awali imeelezwa mahakamani na  mwendesha mashitaka wa polisi Hamis Mohamed kuwa January 20,mwaka huu saa 11 jioni  mshitakiwa alivamia nyumbani kwa Bahati Mtafya (38) na kuiba mbuzi mmoja mwenye thamani ya Sh. 85,000 huku akijua kufanya vyo ni kosa kisheria namba 229 sura ya 16 kanuni ya adhabu.
Aidha mwendesha mashitaka huyo aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa wale wenye nia ya kutendakosa kama hilo kutokana na wimbi kubwa la vijana kujikita katika wizi na kuacha kufanya kazi halali.
Katika hatua nyingine mshitakiwa huyo alipandishwa kizimbani hapo kujibu tuhuma ya wizi wa kuku 23 wenye thamani ya Sh laki 4 mali ya Evance Mwakenja mkazi wa Ilembo Vwawa 
Imeelezwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa polisi Hamis Mohamed kuwa tukio hilo lilitokea januari 20 mwaka huu saa 8 usiku ambapo mshitakiwa aliiba kuku 23 wenye dhamani ya Sh.laki 4 mali ya Evance Mwakenja huku akijua kufanya hivyo nikosa kisheria.
Hata hivyo mshitakiwa alikana shitaka linalomkabili na hakimuwa mahakama hiyo Chirstina Mlwilo amesema shauli hilo litaanza kusikilizwa Januari 27 mwaka huu,pia hakimu huyo amesema dhamana kwa mshitakiwa ipo wazi kwa ahadi ya Sh.laki 4 pamoja na kuwa na  wadhamini wawili wenye vitambulisho vya mpiga kura. 
 Hata hivyo mshitakiwa ameludiswa maabusu kwa kushindwa kutimiza masharti  la dhamana pamoja na kuanza kutumikia kifungo cha miaka mitano ya wizi wa mbuzi.
 

Serikali kuendelea kutoa elimu ya Uzalishaji na matumizi endelevu ya rasilimali

AR1
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi,|Nyumba na Maendeleo ya Makazi George Pangawe akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) kuhusu wananchi kuzingatia sheria na kanuni za mipango miji  nchini pale wanapotaka kuendeleza ardhi kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira Carlos Mbuta na kulia ni Mkuu wa Idara ya Mipango Miji, Ardhi na Mazingira Manispaa ya Kinondoni Bi. Juliana Letara
AR2
Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira Carlos Mbuta akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) kuhusu elimu ya uzalishaji na matumizi endelevu ya rasilimali ili waweze kunufaika na rasilimali hizi ambapo elimu hiyo imeingizwa katika mitaala ya elimu hapa nchini kulia ni Msaidizi Idara ya Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi,|Nyumba na Maendeleo ya Makazi George Pangawe.
AR3
Mkuu wa Idara ya Mipango Miji, Ardhi na Mazingira Manispaa ya Kinondoni Bi. Juliana Letara akisisitiza jambo kwa Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam kulia ni Msaidizi Idara ya Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi,|Nyumba na Maendeleo ya Makazi George Pangawe na kushoto ni
Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira Carlos Mbuta
AR4
Baadhi ya Waandishi wa Habari  wakifatilia mkutano uliondaliwa na, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Baraza la mazingira na Manispaa ya Kinondoni uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam
(Picha na Frank  Mvungi-MAELEZO)
……………………………………………………………………………………………………………………………….
Hassan Silayo-MAELEZO
Serikali kuendelea kutoa elimu ya Uzalishaji na matumizi endelevu ya rasilimali kwa wananchi ili waweze kunufaika na rasilimali zote zilizopo katika maeneo yao kote nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na  Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) Bw.Carlos Mbuta wakati wa mkutano na vyombo vya Habari ikiwa ni moja ya mikakati ya Serikali katika kuelimisha umma kuhusu matumizi sahihi ya rasilimali ikiwemo ardhi.
Akifafanua Mbuta amesema kuwa Elimu hiyo itawasaidia wananchi kungamua na kufanya maamuzi sahihi pale wanapotaka kutumia rasilimali zilizopo katika kujiletea maendeleo.
’Elimu ya mazingira imejumuishwa katika mitaala ya shule zetu hapa nchini ili kujenga uelewa kuhusu matumizi sahihi ya rasilimali alisisitiza Mbuta
Akizungumzia faida za Elimu ya Mazingira kutlowa mashuleni mbuta alibainisha kuwa itasaidia kujenga kizazi chenye uelewa na uwezo wa kutumia rasilimali zilizopo kwa kuzingatia sheria na kanuni.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi  Idara ya Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. George  Pangawe alitoa wito kwa wananchi kufuata taratibu zote za kisheria pale wanapotaka kuendeleza Kipande chochote cha ardhi.
Aliongeza kuwa Serikali kupitia Wizara yake inasimamia matumizi sahihi ya uendelezaji wa ardhi na kuwataka wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali katika kusimamia Sheria na Kanuni zinazosimamia Sekta ya ardhi.
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Mazingira pamoja na Halmashuri zote nchini zimekuwa zikisisitiza kuhusu elimu ya uzalishaji na matumizi endelevu ya rasilimali ili ziweze kuwanufaisha wananchi.

MH. MAJALIWA AONGOZA MKUTANO WA WABUNGE

LI1
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua mkutano wa wabunge, bungeni mjini Dodoma Januari 22, 2016.  Kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai na kushoto ni Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kahilillah. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LI2
Spika wa Bunge Job Ndugai akizungumza kumkaribisha Mwenyekiti wa Mkutano wa Wabunge, Waziri Mkuu, Kassim Majliwa kufungua mkutano huo bungeni mjini Dodoma Januari 22, 2016. Kulia ni Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LI3
 Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, Nenelwa Mwihambi akitoa mada katika mkutano wa wabunge ulioongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, buneni mjini Dodoma Januari 22, 2016. Watatu kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai na kulia ni Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashilillah.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
LI4
Wabunge, Jenista Mhagama wa Peramiho (kushoto) na January Makamba  wakiteta katika mkutano wa wabunge, bungeni mjini Dodoma Januari 22, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LI5
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju akitoa mada katika mkutano w wabunge , bungeni mjini Dodoma Januari 22, 20167. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LI6 LI7
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mafinga mjini Cosato Chumi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Januari 22, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LI8
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia jambo  na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari wakati aaliposalimiana naye  kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Januari 22, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
LI11
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Januari 22, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments :

Post a Comment