Monday, January 25, 2016

Rais Dkt. Magufuli amteuwa Mahadhi Juma Maalim kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait

BKatibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam.
……………………………………………………….
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
 Mhe. Rais Dkt. Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya Nne Mahadhi Juma Maalim kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait kufuatia uamuzi wa Serikali kufungua Ofisi ya Ubalozi katika nchi hiyo rafiki.
Vile vile Rais ameagiza Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi wawili ambao mikataba yao imeisha na kuwataka Mabalozi hao kukabidhi kazi kwa Afisa Mkuu au Mwandamizi aliyechini yao leo hii.
Mabalozi hao ni Bi Batilda Salha Buriani, aliyeko Tokyo, Japan, Dkt. James Alex Msekela, aliyeko Rome, Italia.
Kwa mujibu wa Balozi Sefue, Rais pia amemrejesha nyumbani Balozi wa Tanzania aliyeko London, Uingereza, Bwana Peter Allan Kallaghe ambaye anarejea Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa ambapo atakapopangiwa kazi nyingine.
Balozi Sefue alisema kuwa hadi sasa vituo vya Ubalozi ambavyo viko wazi ni London nchini Uingereza kufuatia kurejea nchini kwa Balozi Peter A. Kallaghe, Brussels nchini Ubelgiji kufuatia aliyekuwa Balozi, Dkt. Deodorous Kamala kuchaguliwa kuwa Mbunge, Rome nchini Italia, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Dkt. James Alex Msekela na Tokyo nchini Japan, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Bibi Batilda Buriani.
Vituo vingine vya Ubalozi ambavyo viko wazi ni Kuala Lumpar nchini Malaysia, kufuatia aliyekuwa Balozi Dkt. Aziz Ponray Mlima kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa na Brasilia nchini Brazil, kufuatia kustaafu kwa aliyekuwa Balozi, Bwana Francis Malambugi.
Wakati huo Balozi Sefue alisema kuwa Rais ametengua uteuzi wa Mhandisi Madeni Juma Kipande kabla hajathibitishwa kwenye cheo cha
Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi kutokana na utendaji kazi usioridhisha.

High Level Meeting For Identification of Education Priorities for formulation of the Education Sector Development Plan (ESDP) and the 5 Year Development Plan

index
Dar es Salaam, 25 January 2016
The United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization (UNESCO) is supporting the Ministry of Education, Science and Technology in developing the Education Sector Development Plan (ESDP) for 2017-2021. The Plan intends to direct the Government of Tanzania’s quinquennium goals, objectives and strategies for its Mainland’s education sector.
In close collaboration with the Ministry of Education, Science and Technology (MoEST), UNESCO will facilitate a two days High Level workshop from 26th to 27th January 2016, at the National Council for Technical Education (NACTE).
Overall, the workshop aims to identify education priorities required for formulation of outcomes, strategies and outputs of the education sector for the next 5 years
The meeting will be chaired by the Commissioner of Education, Professor Eustella Bhalalusesa and will bring together Senior government officials from MoEST and Education Institutes, the President’s Office Regional Administration and Local Government (PO-RALG), Development Partners and Civil Society Organizations representatives as well as members of the Academia. The UNESCO team, will be led by the International Institute for Education Planning (IIEP) and further composed by experts from the UNESCO Institute of Lifelong Learning (UIL), the Education and TVET Units of the HQs and the Dar es Salaam Office.
The workshop proceedings will enable the alignment of the ESDP with the Education priorities of the Five Year Development Plan (FYDPII), taking into consideration as well the key national and international policies and agendas including the new Education and Training Policy (2014) and the Education 2030 Agenda and Framework for Action.
Following the prioritization, the exercise will continue with a smaller number of Government officials for the further formulation of the expected outcomes and targets for identified priorities.
For more information please contact;
Petro Makuru (makurupetro@gmail.com) and Faith Shayo, (f.shayo@unesco.org)

MATUKIO KUTOKA BUNGENI -MJINI DODOMA Januari 25, 2016.

ANG1Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora , Angela Kairuki akiteta na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashatu Kijaji bungeni mjini Dodoma Januari 25, 2016.
ANG2Waziri Mkuu, Kassim Majalaliwa  akisalimiana na Mbunge wa  Nkansi Ally Kessy kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Januari 25, 2016.
ANG3Waziri Mkuu, Kassim Majalaliwa  akisalimiana na Mbunge wa  Mbozi Magharibi,David Silinde kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Januari 25, 2016. Katikati ni Mbunge wa Nkansi, Ally Kessy.
ANG5Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Mbunge wa Songwe, Philip Mulugo  kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma  Januari 25, 2016. Katikati ni mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto.
ANG7Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wazee kutoka jimbo la Chemba  Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Januari 25,2016.  Kushoto kwake ni Mbunge wa Chemba Juma Nkamia.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TAMKO KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI LILILOTOLEWA NA MHE. UMMY MWALIMU (MB); WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

imagesWizara yangu inaendelea kutoa taarifa ya wiki kwa umma kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa kipindupindu hapa nchini. Hadi kufikia tarehe 24 Januari 2016, jumla ya watu 14,608 wameugua ugonjwa huo, na kati yao watu 228 wamepoteza maisha kwa ugonjwa huu. Njombe, Ruvuma na Mtwara ndiyo Mikoa pekee ambayo haijawahi kuripoti mgonjwa yoyote wa kipindupindu, tangu mlipuko huu uanze mnamo mwezi Agosti mwaka huu.
Kwa mujibu wa Takwimu za kuanzia tarehe 18 hadi 24 Januari 2016, ni kuwa jumla ya Mikoa ambayo imeripoti kuwa na wagonjwa ni 15 ambapo idadi ya wagonjwa 524 na vifo 10 vimeripotiwa. Idadi ya wagonjwa walioripotiwa wiki hii imepungua ukiliinganisha na idadi ya wiki iliyoishia tarehe 17 ambapo kulikuwa na wagonjwa 621 na vifo 14 ambalo ni punguzo la asilimia (16%). Mkoa wa Morogoro bado umeendelea kuripoti idadi kubwa zaidi ya wagonjwa ukilinganishwa na Mikoa mingine, (Manispaa ya Morogoro 89, Halmashauri ya Morogoro 36, Mvomero 17), ukifuatiwa na mikoa ya Mwanza (Ukerewe 36, Nyamagana 19 na Ilemela 13), Simiyu (Bariadi DC 29 na Bariadi municipal 23), Manyara (Simanjiro 48), Mara (Musoma Manispaa 11, Musoma DC 8, Rorya 8 na Butiama 8), Geita (Geita DC 21 na Geita TC 6) na Mbeya (Kyela 26).
Mikoa mingine ambayo bado pia imeendelea kuripoti wagonjwa ni pamoja na Dodoma (Wagonjwa 22), Arusha (21), Tabora (18), Singida (18), Lindi (12), Rukwa (7), Kilimanjaro (6) na Kagera (2).
Mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu, Wizara yangu kwa kushirikiana na wadau ilituma timu ya jopo la wataalam kutoka ngazi ya Taifa kwenda kusaidiana na wataalam waliopo katika ngazi ya mkoa na halmashauri katika mikoa 7 iliyokuwa inatoa taarifa ya kuwa na wagonjwa wengi zaidi. Mikoa hiyo ni Arusha, Manyara, Mwanza, Simiyu, Singida, Mara na Morogoro. Mafanikio ya kazi iliyofanywa na Jopo hilo yameanza kuonekana kwani katika Mikoa hiyo saba idadi ya wagonjwa wa kipindupindu imeanza kupungua. Pamoja na mafanikio hayo zipo changamoto ambazo timu hizo ilizibaini kuwepo ambazo zinachangia kulegalega kwa juhudi za kupambana na Kipindupindu nazo ni;
i. Kuwepo na idadi ndogo ya kaya ambazo zinamiliki na kutumia vyoo bora hususani katika maeneo ambayo yameathirika zaidi na ugonjwa huu.
ii. Kutokuwepo kwa miundombinu stahiki ikiwemo vyoo na maji katika Maeneo ya mikusanyiko kama masoko na minada kutokuwa na
iii. Wananchi kutokutii sheria zilizopo kwa kuendelea kuuza chakula bila kuzingatia kanuni za afya na kuuza matunda yaliyokwisha katwakatwa maeneo yasiyo salama.
iv. Utiririshaji wa maji taka kwenye vyanzo vya maji, pamoja na kujisaidia maeneo ya wazi na pembezoni karibu na vyanzo vya maji.
v. Kuwepo kwa idadi ndogo ya watu wanaopata maji safi na salama ya kunywa. Aidha utakasaji wa maji katika ngazi ya kaya kwa kuyachemsha au kwa kutumia vidonge vya kutakasia bado ni changamoto kubwa.
vi. Wagonjwa wa Kipindupindu kuchelewa kufika Kambi za Matibabu.
Kutokana na changamoto hizo, napenda kuikumbusha jamii kuwa kipindupindu ni ugonjwa unaochochewa na mazingira machafu ikiwemo ukosekanaji wa vyoo na hivyo kuletea vinyesi vyenye vimelea kuwa chanzo kikuu cha maambukizi, utiririshaji wa maji taka na vinyesi ambao unaweza kupelekea kuchafuka kwa vyanzo vya maji, kutokuzingatia kanuni za afya wakati wa utayarishaji wa vyakula na matunda, Kula vyakula au vinywaji au pombe za kienyeji zisizoandaliwa kwa kufuata kanuni za afya na kugusa matapishi ya mgonjwa wa kipindupindu au kwenye kitu chochote kilichochafuliwa na kinyesi au matapishi ya mgonjwa.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, inaendelea kusisitiza kwa jamii kuzingatia yafuatayo:
– Kunywa maji yaliyo safi na salama.
– Kuepuka kula chakula kilichoandaliwa katika mazingira yasiyo safi na salama.
– Kunawa mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka hasa kabla ya kula na baada ya kutoka chooni.
– Kutumia vyoo wakati wote na kutokujisaidia ovyo katika vyanzo vya maji vya mito, maziwa na mabwawa.
– Kutokutiririsha maji taka na vinyesi ili kuepuka uchafuzi wa vyanzo vya maji.

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA)

1
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam wakati alipotangazia umma wa watanzania kuhusu hatua ambazo Rais Dk. John Pombe Magufuli amechukua dhidi ya Dickson Mwaimu  Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Taifa ya Vitambulisho vya taifa NIDA kutengua uteuzi wake na kumsimamisha kazi mara moja pamoja na wasaidizi wake ambao ni Joseph Makani Mkurugenzi wa TEHAM, Bi. Rahel Mapande Sfisa Ugavi Mkuu Bi. Sabrina Nyoni Mkurugenzi wa Sheria na George Ntalima Afisa Usafirishaji kwa kuwasimamisha kazi mara moja kupisha uchunguzi.
Taarifa zilizomfikia Rais zinaonesha kuwa NIDA hadi sasa imetumia shilingi Bilioni 179.6 kiasi hicho ni kikubwa na Rais angependa kufanyika uchunguzi na ukaguzi jinsi fedha hizo zilivyotumika, maana Rais amekuwa akipokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na kazi ndogo ya utoaji wa vitambulisha vya taifa .
Hivyo Rais ameelekeza mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya Umma PPRA wafanye ukaguzi wa manunuzi yote yaliyofanywa na NIDA, TAKUKURU na CAG kufanya uchunguzi kwa pamoja ili kubaini kama kulikuwa na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa taratibu au la.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-IKULU)
3
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam , kulia ni Kaimu mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano IKULU Bw. Gerson Msigwa.
4
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiangalia wakati Kaimu mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano IKULU Bw. Gerson Msigwa alipomruhusu mmoja wa waandishi wa habari kuuliza swali katika mkutano huoIkulu jijini Dar es salaam.
6
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa na Balozi Ombeni Sefue Ikulu leo.
7
Mkutano ukiendelea.

No comments :

Post a Comment