Friday, January 1, 2016

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU KATIBU WAKUU IKULU LEO

1
Rais Dk.John Pombe Joseph Magufuli akiwauliza Makatibu wakuu wa wizara mbalimbali na Manaibu Katibu wakuu kama wameelewa na kukubali kusaini Kiapo cha Maadili katika Utumishi wa Umma mara baada ya kusoma maelezo yaliyomo katika kiapo hicho ambapo baada ya kuaapisha aliwauliza kama wanakubaliana na masharti yaliyomo kwenye kiapo cha Maadili ya Utumishi wa Umma na kama yupo ambaye hakuridhia masharti hayo aseme kabla ya kusaini kiapo hicho, Hata hivyo Makatibu wote wamesaini katika kiapo hicho.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-IKULU)
2
Profesa Elisante Ole Gabriel Mollel (Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi (Katibu Mkuu Maliasili na Utalii kushoto wakila kiapo cha maadili ya utumishi Ikulu leo.
3
Baadhi ya Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakila kiapo cha Maadili ya Utumishi mbele ya Rais Dk. John Pombe Magufuli Ikulu leo.
4
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiwaongoza Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu kusoma kiapo cha Maadili ya Utumishi kabla ya kusaini kiapo hicho.
5
Manaibu Katibu wakuu na Makatibu Wakuu wakisaini Kiapo hicho mara baada ua kusoma, kuelewa masharti yaliyomo na kuyakubali.
6
Waziri Mkuu Mh. Majaliwa, Kassim Majaliwa akitoa neno mara baada ya Makatibu hao kusaini kiapo cha Maadili ya Utumishi Ikulu leo.
7
Baadhi ya Makatibu Wakuu wakisubiri kuapishwa.
8
Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mh. Goerge Masaju huku Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyamnge akifurahia kabla ya kuanza kwa hafla ya kuawaapisha Makatibu Wakuu.
9
Rais Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi mara baada ya kumuapisha Amon Mpanju (Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba ikulu leo.
10
Rais Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mh. Amon Mpanju (Naibu Katibu Mkuu wizara ya Sheria na Katiba.
11
Rais Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mh. James Dotto (Naibu Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango).
12
Rais Dk. John Pombe Magufuli akumiapisha Dkt. Paulina Pallangyo (Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini)
13
Rais Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi mara baada ya kumuapisha Profesa James Epifani Mdoe (Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini)
14
Rais Dk. John Pombe Magufuli akumiapisha Profesa James Epifani Mdoe (Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini).15
Rais Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Immaculate Peter Ngwale kuwa (Naibu Katibu Mkuu)Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.16
Rais Dk. John  Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Deo  Mtasiwa (Naibu Katibu Mkuu – Afya)
17
Rais Dk. John Pombe Magufuli akumiapisha Dkt. Mpoki Ulisubisya kuwa (Katibu Mkuu – Afya)
18
Rais Dk John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Laurian Ndumbaro kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora.
19
Rais Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
20
Rais Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi Vitendea kazi  Jaji Meja Jenerali Projest A. Rwegasira mara baada ya kumuapisha kuwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani.
21
Jaji Meja Jenerali Projest A. Rwegasira akiapishwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa (Katibu Mkuu) Wizara ya Mambo ya Ndani.
22
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akipiga saluti wakati wimbo wa taifa ulipokuwa ukipigwa .
23
Kutoka kulia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mh. Majaliwa, Kassim Majaliwa , Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mwanasheria mkuu wa Serikali Mh. George Masaju.
24
Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano Ikulu tayari kwa kuwaapisha Makatibu Wakuu na Mnaibu Katibu Wakuu leo, Kulia ni Balozi Ombeni Sefue Katibu Mkuu Kiongozi.
25
Waziri wa Sheria na Katiba Mh. Harrison Mwakyembe akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu Katubu wakuu.

WAZIRI MKUU AWAPONGEZA MAKATIBU WAKUU NA NAIBU KATIBU WAKUU

MAJALIWA 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewapongeza Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu, mara baada ya kuapishwa Ikulu leo jijini Dar es Salaam. 
Ametoa pongezi hizo wakati Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu wakiwa wametia saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma mbele ya waandishi wa habari.
Waziri Mkuu Majaliwa pia amewataka viongozi hao, kuwa waaminifu, kuwajibika na  kutoa taarifa ya utendaji kwa wananchi. Aidha, alisema kuwa, viongozi wengine watakao apa mbele ya Kamishna wa Tume ya Maadili ni pamoja na  Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri, ikiwa ni hatua ya Serikali kudhibiti na kufuatilia matumizi ya rasilimali fedha.
“Wakuu wa Wilaya watahakikisha fedha zilizoenda katika Halmashauri zao lazima zitumike katika shughuli zilizokusudiwa” alisema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu alitoa wito kwa watanzania kuendelea kuwa na imani na Serikali ya Awamu ya Tano, kwakuwa itatimiza ahadi zote ambazo Mheshimiwa Rais na Makamu wa Rais walizitoa wakati wa Kampeni.
Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu hao, wameapishwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli, ambapo shughuli hiyo ilihudhuriwa pia na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Mke wa Mheshimiwa Rais mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi mbalimbali.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI
S.L.P 3021
1141O DAR ES SALAAM
IJUMAA, JANUARI 1, 2016.

VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUWAOMBEA WATU WABADILI TABIA MBAYA MFANO WIZI, UVUVI NA UZEMBE

Y7
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akipongezana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye wakati wa mkesha maalum wa kuombea taifa uliofanyika uwanja wa Taifa usiku wa kuamkia leo.
………………………………………………………………………………………………………..
Na Magreth Kinabo – MAELEZO
Viongozi wa dini nchini wametakiwa kuwaombea watu wenye nia mbaya na Taifa la Tanzania  ili waweze kuwa raia wema na kuachana na tabia za kutaka rushwa, uvivu, uzembe na matumizi ya dawa za kulevyia.
 Kauli hiyo imetolewa leo na Mgeni rasmi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  katika  maombi maalum  ya   kuliombea dua Taifa na viongozi, ambaye ni  Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dares Salaam.
“Tabia  hizi zimeota mizizi zinahitaji maombi. Tunao uwezo wa kumwuunga mkono Rais. Kila mtu anao mchango wa kumsaidia Rais anayoyafanya mfano  katika vijiji kutumbua majibu madogo,” alisema Lukuvi .
Aliongeza kwamba viongozi hao wanapaswa kuelimisha jamii jinsi ya kufanya kazi  kwa bidii, hivyo wasiache kusisitiza juu ya suala hilo, likiwemo suala la, amani  upendo umoja na mshikamano.
“ Misingi hii ya, upendo,  umoja na mshikamano ilianzishwa na Serikali zilizopita na Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kuhimiza juu ya misingi hii, bila ya kujali dini , rangi, kabila, itikadi na eneo analotoka mtu,” alisisitiza.
Alisema uhuru wa kuabudu utaendelea kuwepo, ila kwa kuzingatia sheria zilizopo.
 Aidha Waziri Lukuvi alisema  Serikali itaendelea kutoa fursa sawa za kiuchumi na kijamii kwa wananchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti  wa Jumuiya  wa Makanisa ya Pentekoste, ambaye pia ni Askofu wa Huduma ya Tanzania Fellowship Churches (TFC), Askofu  Godfrey  Malassy  alisema wao kama viongozi wa dini wako pamoja na Rais John Pombe Magufuli, hivyo hawatamwacha pekee yake  katika mapambano hayo hadi Tanzania itakapokuwa mahali penye neema pa kuishi.
Askofu Malassy aliongeza kwamba ni wajibu wa Watanzania kuomba ili kuweza kuleta mabadiliko katika Taifa letu.
 Alisema madhuni ya maombi hayo ni kumwombea Rais Magufuli aweze kuendelea  kuliongoza Taifa ili liweze kuwa na maendeleo ya ustawi wa watu wote na liendane na kasi ya kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi tu!.
Askofu huyo alisema mauzo ya kitabu cha ijue siri ya amani na sadaka zitakazotokana na mkesha huo zitatumika kuelimisha jamii ya ya umuhimu wa amani, kuendelea kutoa huduma hiyo kwene mikoa ambayo hawajaifikia na kugusa jamii yenye mahitaji maalum hasa wakina mama na watoto kwa kusaidia kutoa huduma ya nishati ya umeme.

RAIS MAGUFULI AMJULIA HALI MUADHAMA KADINALI POLYCARP PENGO ANAYEFANYIWA UCHUNGUZI WA AFYA YAKE MUHIMBILI

88068e07-9b41-4ff5-b66b-59f99ba35e47
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki  la Dar es salaam katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo January 1, 2016. Kardinali Pengo alilazwa hospitalini hapo jana jioni kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.
PICHA NA IKULU

MKESHA WA MWAKA MPYA

Y1
Mmoja ya wanamaombi akiongoza sala za maombi katika ibada ya mkesha maalum wa kuliombea dua taifa na viongozi iliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dares Salaam leo.
Y3
Meza kuu akiwemo mgeni rasmi ambaye alikuwa Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakiwa katika maombi maalum ya kuliombea dua taifa na viongozi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dares Salaam leo.
Y2 
Baadhi ya wananchi wakitoa sadaka kwa ajili ya maombi hayo, ambayo itatumika kusaidia watu wenye mahitaji maalum ambao wakina mama na watoto na kuendeleza mikesha hiyo.
Y4
Bandi ya polisi ikiongoza wibo wa Taifa.
Y5
Mama mmoja akiwa na mwanae akiwa katika maombi hayo.
Y6 Y7
Mgeni rasmi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika maombi maalum ya kuliombea dua taifa na viongozi Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (katikati) yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dares Salaam leo akipeana mkono wa heri ya kuingia mwaka mpya wa 2016 na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye .
(Picha zote na Magreth Kinabo – Maelezo)

WAZIRI NAPE AKICHEZA NA WANANCHI KWENYE MKESHA WA KUUPOKEA MWAKA 2016

BONANZA LA MAZOEZI YA VIUNGO KITAIFA-LAFANA

B1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiongoza Matembezi ya wanamichezo katika Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa yaliyofanyika leo kwa kuwanzia Uwanja wa Tumbaku Mjini Unguja na kumalizia Uwanja wa Amaan Studium.
[Picha zote na Ikulu.]
B2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiongoza Matembezi ya wanamichezo katika Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa yaliyofanyika leo kwa kuwanzia Uwanja wa Tumbaku Mjini Unguja na kumalizia Uwanja wa Amaan Studium.
B3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wanamichezo wa Vikundi mbali mbali kama ishara ya kuyapokea maandamano ya vikundi hivyo katika kilele cha Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
B4
Wamamichezo wa Vikundi vya mazoezi wakipita mbele ya jukwaa kubwa Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika kilele cha Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa yaliyofanyika leo ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
B5
Wamamichezo wa Vikundi vya mazoezi wakipita mbele ya jukwaa kubwa Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika kilele cha matembezi ya Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa yaliyofanyika leo ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
B6
Wanakikundi cha Amakweli Fitness Club ya Welezo Grinada wakibeba bango la Chama cha Mchezo wa Maziezi ya Vuingo Zanzibar (ZABESA) linalosema “JIKINGE DHIDI YA MARADHI YA KISUKARI PRESHA NA SARATANI KWA KUFANYA MAZOEZI”wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipoyapokea matembezi ya Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
B7
Kikundi cha Mazoezi Mwera Fitness Club kikipita mbele ya mgeni rasmi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipoyapokea matembezi wakati wa Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
B8
Kikundi cha Mazoezi Chumbuni Studio kikipita mbele ya mgeni rasmi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipoyapokea matembezi wakati wa Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
B9
Kikundi cha Mazoezi kutoka Kisiwani Pemba kikipita mbele mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipoyapokea matembezi ya Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
B10
Kikundi kutoka Dar es Salaam ni miongoni mwa vikundi vilivyojumuika katika matembezi ya Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
B11
Kikundi kutoka Dar es Salaam ni miongoni mwa vikundi vilivyojumuika katika matembezi ya Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
B12
Miongoni mwa Vikundi vya Mazoezi hapa Mjini Unguja nacho kikionesha manjonjo ya aina ya mazoezi mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika kilele cha Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguj.

MKESHA WA MWAKA MPYA WAFANA DAR

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Wiliam Lukuvi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, akihutubia kwenye Mkesha Mkubwa Kitaifa,Dua Maalum ya kuwaombea viongozi na Taifa uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Mchungaji Eden Godfrey akihubiri kwenye Mkesha Mkubwa Kitaifa, Dua maalum uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

 Viongozi wakiwa wameshikana mikono wakati wa maombi maalum kwa Taifa na Viongozi wake .
Umati wa wakazi wa jiji la Dar es salaam waliojitokeza kwenye ibada maalum ya mkesha wa mwaka mpya uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru.
Wananchi wakiwa kwenye maombi ya kuliombea Taifa Amani, na kuwaombea viongozi wake afya njema.
Mwalimu Teddy Kwilasa akitoa maombi maalum kwa Taifa kwenye mkesha wa mwaka mpya.
Wananchi wakiwa kwenye maombi mazito ya kuwaombea Viongozi wa Taifa letu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (wa pili kulia) akiwa pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye pamoja na wake zao wakiupokea mwaka kwenye Mkesha Mkubwa Kitaifa, ambapo Taifa na Viongozi wake waliombewa.
Sehemu ya Vijana waliojitokeza kwenye mkesha mkubwa uliofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akitoa salaam maalum za kuwataka wazazi kuwafundisha watoto wao umuhimu wa amani ya nchi wakati wa mkesha wa mkubwa kitaifa wa kuombea Taifa na Viongozi wake dua maalum.
Bi. Christina Elias wa Aleluyah kwaya kutoka Tabata  akiimba kwa hisia kwenye mkesha mkubwa wa kitaifa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Viongozi wakiwa kwenye maombi maalum ambapo waliwakilisha Mawaziri wote nchini.

SALAMU YA MWAKA MPYA, 2016

MSANGI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.
……………………………………………………………..
KAMANDA WA POLISI MKOA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED ZAHORO MSANGI, ANAWATAKIA KHERI YA MWAKA MPYA 2016 WAANDISHI WOTE WA HABARI. “NINASHUKURU KWA USHIRIKIANO WENU KWA KIPINDI CHA MWAKA 2015 NA KUOMBA USHIRIKIANO ZAIDI KWA MWAKA 2016.
“TUSHEREHEKEE MWAKA MPYA, 2016 KWA AMANI NA UTULIVU” TUKUMBUKE “ULINZI NA USALAMA SIKU ZOTE UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE”
AHASANTENI!!!

MWENYEKITI WA BODABODA MKOA WA MWANZA AWAOMBA RADHI WATANZANIA

Na”George Binagi-GB Pazzo @BMG
Mwenyekiti wa Waendesha Pikipiki (Bodaboda) Mkoa wa Mwanza Makoye Kayanda Bunoro anawatakia Waendesha Pikipiki wote nchini Kheri ya Mwaka Mpya 2016 huku akiwasihi kutimiza majukumu yao kwa kufuata sheria na taratibu za Usalama barabarani bila shuruti.
“Tuache Mchezo na Vyombo vya Moto, Tuvae Elmenti, tusibebe mishkaki (zaidi ya abiria mmoja) tusiendeshe kwa mwendo kasi kwani ni hatari, tusitumie pombe tukiwa kazini huku tikiwapenda abiria na kujiepusha na vitendo vya uhalifu vya aina yoyote”. Anasema Bunoro.
Aidha Bunoro amewaomba radhi wale wote waliopata usumbufu kwa namna moja ama nyingine kutokana na kazi ya bodaboda na kwamba kusameheana ndilo jambo la msingi huku akiwakumbusha bodaboda  kujipanga katika majukumu yao ili kuendana na kasi ya Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli ya “Hapa Kazi Tu”.
Bonyeza HAPA Kusoma Zaidi

MATUKIO MAKUBWA YA MUZIKI WA DANSI NCHINI KWA MWAKA 2015

????????????????????????????????????
Tarehe 31-Jan-2015, BMM Classic Band, ilizinduliwa katika ukumbi wa BMM Mwenge, opposite TRA.
  • Tarehe 21-Feb-2015, JJ Band yazinduliwa katika ukumbi wa. JJ Band ni bendi dada ya Skylight Band itakayokuwa inatumbuiza mjini Mwanza katika hotel ya Jembe ni Jembe Resort.
  • Tarehe 06-Mar-2015 (Ijumaa), Ruby Band ilitambulishwa rasmi katika ukumbi wa Coco Beach Pub ambapo pia ilizindua video ya wimbo mpya wa “Noma”.
  • Tarehe 18-Jul-2015 (Jumamosi), Stars Band yazinduliwa katika ukumbi wa Mzalendo Pub. Bendi hiyo inaongozwa na mwanamuziki Aneth Kushaba aka “AK47” aliyekuwa Skylight Band. Meneja wa bendi ni mpiga drums James Kibosho. Bendi hii inaundwa pia na mpiga solo Alain Kisomundele na Mao Santiago aliyekuwa Machozi Band.
  • Dec-2015, bendi mpya itakayojumuisha Mule Mule FBI, Totoo Ze Bingwa, Alain Mulumba Kashama, Montana Amarula na Didi “Number” Kayembe (Numero) aka “Dume la Mende” ipo katika maandalizi ya kuundwa na kuzinduliwa huku Mule Mule FBI akiwa rais (prezidaa) wa bendi hiyo huku Losso Mukenga, mpiga solo wa Ally Kiba, akiipigia pia bendi hiyo.
UZINDUZI WA ALBUM MPYA
  • Tarehe 27-Dec-2015, Milimani Park Orchestra “Sikinde-Ngoma ya Ukae”, ndani ya TCC Chang’ombe, yazindua album ya “Jinamizi la Talaka” sambamba na kufanya sherehe za miaka 37 tokea bendi ianzishwe mwaka 1978
KILI MUSIC AWARD
  • Tarehe 23-Mar-2015, Kililimanjaro Music Award 2015 yazinduliwa rasmi
  • Tarehe 25-Apr-2015, Academy ya Kili Music Award yakutana kuchagua majina ya washiriki wa kila kipengele.
  • Tarehe 29-Apr-2015, majina ya washiriki wa kila kipengele yatangazwa rasmi
  • Tarehe 13-Jun-2015 (Jumamosi), sherehe za washindi wa Kili Music Award 2015 zilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City. Kulikuwa na jumla ya vipengele (categories) 6 vya muziki wa dansi. Washindi walikuwa kama ifuatavyo;
    1. Bendi Bora ya Mwaka- FM Academia
  1. Mtunzi Bora wa Mwaka Bendi-Jose Mara (Mapacha Watatu)
  2. Rapa Bora wa Mwaka Bendi- Fergusson (Mashujaa Band)
  3. Wimbo wa Kiswahili Bendi- ”Wale Wale” (Vijana Ngwasuma)
  4. Mwimbaji Bora wa Kiume Bendi- Jose Mara (Mapacha Watatu)
  5. Mtayarishaji Bora wa Nyimbo Bendi-Amoroso Sound

No comments :

Post a Comment