Afisa
Habari Mkuu kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Aisha Malima
akipata maelekezo kutoka kwa mfanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi ya Estim
bw. Joseph Shauri kuhusu ujenzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco.
Vifusi
vikiwa vimekusanywa katika maeneo ya Mwenge ikiwa ni hatua za awali za
ujenzi wa Barabara ya kutoka Mwenge hadi Morocco kazi iliyoanza Desemba
Mosi, mwaka huu na inatarajiwa kuisha baada ya miezi sita chini ya
Kampuni ya Ujenzi ya Estim jijini Dar es Salaam.
Afisa
Habari Mkuu kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Aisha Malima
akionesha alama zilizowekwa katika maeneo ya Bamaga ikiashiria kuwa
tayari ujenzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco imeshaanza kufanya kazi
tangu Desemba Mosi, mwaka huu na inatarajiwa kuisha baada ya miezi
sita.
Afisa
Habari Mkuu kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Aisha Malima
akiongea na mmoja wa wachuuzi wa vyungu vya maua maeneo ya Bamaga
Bw.Emmanuel Kilua ambaye tayari ameshapewa maelekezo ya kupisha eneo
hilo ili kupisha ujenzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco inayojengwa
na Kampuni ya Ujenzi ya Estim na inatarajiwa kuisha baada ya miezi sita.
Vifusi
vikiwa vimekusanywa katika maeneo ya Mwenge ikiwa ni hatua za awali za
ujenzi wa Barabara ya kutoka Mwenge hadi Morocco kazi iliyoanza Desemba
Mosi, mwaka huu na inatarajiwa kuisha baada ya miezi sita chini ya
Kampuni ya Ujenzi ya Estim jijini Dar es Salaam.
Mafundi
wakiendelea na harakati za ujenzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco
ikiwa ni moja ya hatua ya upanuzi wa barabara hiyo kutoka njia mbili
hadi kuwa barabara ya njia tano lengo ni kupunguza msongamano wa foleni.
Barabara
ya Mwenge hadi Morroco inavyoonekana katika picha kwa sasa ambayo
inatarajiwa kuwa barabara ya nia tano badala mbili kama ilivyo sasa
lengo ikiwa ni kupunguza msongamano wa foleni kwa watumiaji wa barabara
hiyo. (Picha na Lorietha Laurence –Maelezo)
asnia ya filamu nchini yachangia kutoa ajira na kuongeza pato la taifa
t
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo akielezea namna sekta ya
Filamu ilivyo piga hatua hapa nchini wakati wa mkutano na waandishi wa
habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Bi. Genofeva Matemu na kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya
Habari MAELEZO Bi. Fatma Salum.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutana wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo uliokuwa unahusu ukuaji wa sekta ya Filamu
Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Frank Shija, WHVUM
……………………………………………………………………………………………
Picha na Frank Shija, WHVUM
……………………………………………………………………………………………
Na Jovina Bujulu-MAELEZO
Sekta ya filamu imekuwa na
mchango mkubwa kwa kutoa jumla ya ajira 732,681ikiwa ni mchango wake
katika kutatua tatizo la ajira nchini kwa mwaka wa fedha 2014/2015.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Joyce Fissoo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo
jijini Dar es salaam.
Fissoo alifafanua kuwa idadi
hiyo ya ajira zilizotolewa inajumuisha wataalamu wa filamu 944 na wadau
wengine wasio wataalamu 731,737 ikilinganishwa na takwimu zilizotolewa
na Shirika la Milki Bunifu Ulimwengini liliripoti kuwa mwaka 2007 tasnia
ya filamu iliajiri watu 36.
‘Katika kipindi cha miaka ya
2000 utengenezaji wa filamu umebadilika kutoka ule wa awali wa
kuburudisha na kuelimisha na kuwa biashara inayoingiza kipato na kutoa
ajira katika jamii hivyo kuongeza kipato cha Taifa letu”. Alisema Fissoo
Aidha, kuanzia miaka ya 2000
sekta binafsi ilianza kutengeneza filamu hivyo filamu zilianza
kufadhiliwa, kutengenezwa, kumilikiwa na kusambazwa kwa kiasi kikubwa na
wadau na makampuni binafsi hivyo kupelekea ongezeko kubwa la makampuni
ya uzalishaji na usambazaji kutoka kampuni 1 miaka ya 2000 hadi kufikia
makampuni 250 mwaka 2015.
Tasnia hiyo imechangia kukuza
uchumi wa nchi na ule wa mtu binafsi ambapo kwa mujibu wa Shirika la
Milki Bunifu Ulimwenguni (WIPO) kwa mwaka wa 2007 ilichangia shilingi
2,134,860 na kufikia mwaka 2010 ilichangia shilingi 11,398,440, ambayo
ni sawa na ongezeko la asilimia 433.9.
Akizungumzia ukuaji huo wa
tasnia ya filamu, Fissoo alisema kuwa ukuaji wa teknolojia umepelekea
utumiaji wa vifaa vyenye teknolojia ya hali ya juu vilivyowekezwa na
baadhi ya wadau vinavyopatikana kirahisi kama vile kamera za kisasa, na
mashine za kufungashia kazi za filamu hivyo kupunguza gharama za
uzalishaji wa filamu nchini.
Aidha, kumekua na uuzaji wa
filamu kwa njia ya mtandao suala linalopanua wigo wa masoko na
kuitangaza nchi kwa wepesi zaidi hivyo kupelekea umahususi wa mandhari
ya Tanzania kutumika na watengenezaji wa ndani na makampuni ya nje
yapatayo 169 kutengeneza filamu mbalimbali.
Tasnia ya filamu nchini
imeendelea kukua na kushamiri kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo
na wadau wa ndani ya nchi ikiwemo kuandaa, kuratibu na kuendesha
matamasha na Tuzo za Filamu za Tanzania (TAFA),Tamasha la Filamu la Bara
la Ulaya, Tamasha la Filamu la Misri, Tamasha la Filamu la India,
Tamasha la Filamu la Bara la Asia, Tamasha la Filamu la Brazil na Arusha
African Film Festival.
No comments :
Post a Comment