Wednesday, December 2, 2015

TUMIENI TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO IKIWEMO KUFANYA MITANDAO KWA NJIA YA VIDEO ILI KUOKOA GHARAMA – MKURUGENZI MTENDAJI WA TaGLA

UT3 
Mkurugenzi Mtendaji  Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao Bw.Charles Senkondo  akizungumza na waandishi wa habari (ambao hawapo katika  picha) baada ya kumalizika kwa Mkutano  na Sekretarieti za Mkoa kwa njia ya Video  jana jijini Dar es Salaam.
UT1 
Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Umma Bw.Peter Mushi (wa pili kushoto) akizungumza alipokuwa akiendesha  mkutano kwa njia ya video na Sekretarieti ya Mkoa wa Mara jana jijini Dar es Salaam (watatu kulia) ni Mkurugenzi Msaidizi  Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Umma Bw. Leonard Mchau .
UT2 
Baadhi ya watendaji kutoka wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma  wakiendelea na  Mkutano kwa njia ya Video  na Sektertarieti za Mikoa ya Lindi,Mara,Geita,Singida na Shinyanga jana jijini Dar  es Salaam.
……………………………………………………………………………………………
Na Anna Nkinda – Maelezo
  Watanzania wametakiwa kutumia technolojia ya mawasiliano ikiwemo kufanya mikutano kwa njia ya video ambayo itawaondolea gharama ya kusafiri na hivyo kuokoa fedha  na muda.
Rai hiyo imetolea   hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA Charles Senkondo wakati akiongea na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kazi wa video conference kati ya Ofisi ya Rais  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Taasisi zake, Sekretarieti za mikoa na Mamlaka za Serikali za mitaa.
Senkondo alisema kufanya mikutano kwa njia ya video kunamfanya mtu asisafiri na hivyo kuepukana na ajali, kutopoteza muda awapo safarini na na kupata wasaa wa  kukaa na familia yake.
“Kuanzishwa kwa TaGLA kumeongeza uwezo wa kufanya kazi kwa ubunifu zaidi, kwa njia ya kisasa, kwa maamuzi zaidi ya kiuendeshaji kwa kuangalia kila mara mahitaji ya wadau na kutumia mbinu za soko katika utoaji wa huduma bora”.
“Kabla ya kukuwa kwa teknolojia watu walikuwa wanasafiri umbali mrefu kwenda kushiriki mikutano hivi sasa wamepunguza safari zisizo na umuhimu.  Mtu atasafiri katika mikutano ya umuhimu tu zamani ilikuwa lazima mtu aje sasa hivi anafuatwa popote alipo na kuletwa katika video conference”, alisema Senkoro.

SERIKALI KUTUMIA TSH. BILIONI 5 KUHUDUMIA KAMBI ZA MADAKTARI BINGWA WA MOYO

index
Na Nyakongo Manyama -MAELEZO
Dar es salaam
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 5 katika mwaka 2015/16 kwa ajili ya kuhudumia kambi za Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu ya magonjwa hayo kwa Watanzania.
Lengo la mkakati huo ni kuhakikisha Wagonjwa wengi wanahudumiwa katika kipindi kifupi pamoja na kupunguza gharama za kusafirisha wagonjwa nje ya nchi, ambao wengi wao husafiri kwa ajili ya matibabu ya magonjwa ya moyo, figo na saratani.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donald Mmbando wakati wa ziara yake ya kutembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Dkt. Mbando alisema katika wiki ya kwanza iliyoanza wiki hii Madaktari hao wanatarajia kutoa huduma kwa wagonjwa 20 na kuifanya Serikali kuokoa kiasi cha Tsh. Milioni 500 ambazo zingetumika kuwasafirisha wagonjwa hao nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
“Tumeokoa kiasi cha Tsh. Bilioni 1 zilizopaswa kutumika kuwapeleka nje ya nchi wagonjwa hawa, tutahakikisha kuwa Wataalamu hawa wanafanya kazi kwa pamoja na Madaktari wetu ili waweze kuwajengea uwezo katika kutibu magonjwa haya”  alisema Dkt. Mmando.
Alisema Serikali pia ipo katika mchakato wa kuzijengea uwezo hospitali mbalimbali nchini ikiwemo Taasisi ya Kansa ya Ocean Road na Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa kuziwezesha hospitali hizo kuwa na Wataalamu na majengo ya kisasa kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu kwa Watanzania.
Aidha alisema Serikali imepanga kufanya mazungumzo na taasisi za kiraia na nyingine ikiwemo taasisi ya Rotary Club zilizokuwa zikisafarisha watoto wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, kuwekeza nguvu nchini kwani Tanzania kwa sasa ina wataalamu wa kutosha kwa ajili ya kuwatibu wagonja hao.
Kwa mujibu wa Mmbando alisema magonjwa ya moyo ni miongoni mwa magonjwa yasiyoambukiza, hivyo aliwataka Watanzania kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara na kuacha kunywa pombe na uvutaji wa sigara na kutazama desturi za ulaji.
Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Prof. Mohammed Janabi alisema katika kipindi cha wiki mbili ambazo madaktari hao watakuwepo hapa nchini wanaweza kuhudumia jumla ya wagonjwa 55, na hivyo kuifanya Serikali kuokoa kiasi cha Tsh. Bilioni 1.2

MAANDALIZI YA UPANUZI WA BARABARA MWENGE MOROCCO

mi2 
Tingatinga likiendelea na maandalizi ya upanuzi  wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami.
Picha na Philemon Solomon-Fullshangweblog

THE 10th SADC DIGITAL BROADCASTING MIGRATION FORUM HELD IN TANZANIA.

index
By. Aron Msigwa, Dar es salaam.
The 10th SADC digital broadcasting migration forum is taking place in Dar es salaam, Tanzania from 2nd to 3rd december 2015
. the main theme is digital broadcasting dynamics: building a sustainable future.
Participants of the forum comes from sadc countries including Zimbabwe, Tanzania (Host Country) Seychelles, Malawi, South Africa, Swaziland, Namibia,Lesotho and Zambia.
Speaking at the opening ceremony of the forum the permanent secretary from the Ministry of Communication, Cience and Technology from Tanzania Mr. Yamungu Kayandabila said the SADC digital broadcasting terrestrial television forum is being held at a time Tanzania has completed migrating from analogue to digital broadcasting on the day of 30th April, 2015.
Mr. Kayandabila said the Government of Tanzania has invested heavily on communications infrastructure deploying the national ict broadband backbone (nictbb) which runs over 7,500 kilometers in all regional headquarters expect to bring major leap in the development of ICT in Tanzania.
Issues to be discussed by the forum member during the two day forum include digital broadcasting dynamics, building a sustainable future, post digital migration challenges: Regulatory framework for terrestrial, Satellite,Cable and online delivery also discussion on digital migration as a platform to improve consumer choice.

MKUTANO WA WAHARIRI KUHUSU MAGONJWA YASIYOPEWA KIPAUMBELE

mg1 
Mratibu wa Kitaifa wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele, Dkt. Upendo Mwingira akielezea jinsi Serikali inavyojitahidi kupambana na magonjwa hayo, ambayo   baadhia yake  ni Matende, Mabusha, Minyoo ya Tumbo, Kichocho, Trakoma na Usubi kwa baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari  katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii leo jijini Dares Salaam.
mg3 
Mratibu wa Kitaifa wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele, Dkt. Upendo Mwingira akielezea jinsi Serikali inavyojitahidi kupambana na magonjwa hayo, ambayo   baadhia yake  ni Matende, Mabusha, Minyoo ya Tumbo, Kichocho, Trakoma na Usubi kwa baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari  katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii leo jijini Dares Salaam.
 (Picha na Magreth Kinabo- MAELEZO)

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo yapongezwa kwa ushikiano inaotoa kwa wadau wa Vijana

el1:
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (watatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Shirika la Voluntary Serverce Overseas (VSO)Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Bibi. Esther Liwa,Mkurugenzi wa Kanda wa VSO Bibi. Niki Kandirikirika, Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la Kiserikali la Volountary Service Overseas (VSO) Dkt.Philip Goodwin, Mkurugenzi wa Voluntary Service Overseas nchini Bw. Jean Van Wetter na Meneja Mradi wa ICS kutoka VSO Bibi. Imisa Masinjila
Picha na Frank Shija, WHVUM
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (kulia) akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Volountary Service Overseas (VSO) Dkt.Philip Goodwin alipo mtembelea ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuishukuru Serikali kwa ushirikiano inaowapa katika kufanikisha majukumu yao.
el3 
Afisa Mtendaji Mkuu wa shiriki lisilo la Kiserikali la Volountary Service Overseas (VSO) Dkt.Philip Goodwin akifafanua jambo wakati wa kikao baina ya wajumbe kutoka shirika hilo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (kulia) jana jijini Dar es Salaam.
el4 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (katikati) akielezea jambo wakati wa kikao baina yake na ujumbe kutoka Shirika la Voluntary Serverce Overseas (VSO) jana jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la Kiserikali la Volountary Service Overseas (VSO) Dkt.Philip Goodwin na kulia ni Mkurugenzi wa Voluntary Service Overseas nchini Bw. Jean Van Wetter.

POP UP BONGO ILIVYOFANA, TRINITI BAR OYSTERBAY CHINI YA UDHAMINI WA SMIRNOFF

Co-
founder wa Pop Up Bongo Natasha Stambuli akionesha bidhaa za duka lake
la Secret Habit ambalo nalo lilionesha bidhaa zake siku hiyo.
Andrew Mahiga na rafiki ake walikuwapo
Mmoja kati ya wanawake wajasiriamali mahiri mjini, Aika Lawere mmiliki wa   Mbezi Garden alikuwapo pia
Mbunifu wa mavazi nchini wa lebo ya Branoz Collection, Bahati Kombe (katikati) akipanga bidhaa zake wakati wa Tamasha la Pop Up Bongo lililofanyika juzi Triniti Oyster bay chini ya udhamini wa kinywaji cha Smirnoff.
Meneja chapa (pombe kali) wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari  Shija, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
Wauzaji wa bidhaa mbalimbali kutoka duka la Beauty Haven wakiwa kwenye banda lao wakati wa Tamasha la Po Up Bongo lililofanyika juzi Triniti Oyster bay chini ya udhamini wa kinywaji cha Smirnoff
    Tanya akiwa na wadau mbalimbali waliojitokeza kwenye Pop Up shop
        Atu Mynah akimtaja mshindi wa bahati nasibu siku hiyo
Kutokea banda la Beauty Heaven kulikuwa na bidhaa mbalimbali pia
Natasha akizungumza na mmoja kati ya washiriki waliojitokeza   kuonesha bidhaa siku hiyo
…………………………………………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
ONESHO la mauzo ya bidhaa mbalimbali
zitengenezwazo na wabunifu wa hapa nchini, Pop Up Bongo lilifanyika hivi
karibuni na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
 Mratibu wa onesho hilo lililofanyikia Triniti Oyster bay,Natasha
Stambuli alisema kuwa zaidi ya wajasiriamali 15 walijiotokeza kuonesha na kuuza bidhaa zao.
Alisema kuwa bidhaa mbalimbali kama vile nguo, vito, viatu na vinginevyo
viliuzwa na wajasiriamali hao walipata wasaha wa kuongeza wigo wao kibiashara
kwa kukutana na wanunuzi.
“Pop Up Bongo inalenga kuwaweka karibu zaidi wajasiriamali na wanunuzi hao
kwa kuwakutanisha mahala hapa na kisha hata wakishafanya mauzo wanakuwa na
wasaha wa kuonana hata baada ya Tamasha hili na kuendeleza uhusiano wa
kibiashara” alisema Natasha.

Pia ametoa wito kwa wanajamii kujenga utamaduni wa kuhudhuria maonesho
mbalimbali ya biashara ili kupanua wigo zaidi wa ufahamu wa aina mbalimbali za
bidhaa ziuzwazo nchini.
Natasha alisema kuwa kwa kutembelea maonesho hayo watapata wasaha wa kufahamu
aina mbalimbali za bidhaa ziuzwazo na wafanyabiashara mbalimbali na kujua ni
wapo pa kwenda kujipatia mahitaji.
Alisema kuwa Pop Up Bongo ikiwa chini ya udhamini wa kinywaji cha Smirnoff
inalenga kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali zitengenezwazo
hapa nchini na wanunuzi kwa lengo la kuwasaidia wajasiriamali wa hapa nchini
kuongeza pia wigo wa biashara zao.
Kwa upande wake Meneja chapa (pombe kali) wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL)
Shomari  Shija, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
alisema kuwa kwa kampuni hiyo inatambua nafasi ya wajasiriamali katika
kuendeleza uchumi wa nchi na ndio maana imeamua kuunga mkono Pop Up Bongo.

“SBL kwa kupitia kinywaji chetu cha Smirnoff tumeamua kudhamini Pop Up
Bongo kwa kuwa ni mahala pazuri kwa wapenzi wa kinywaji hiki kukutana huku
wakijipatia mahitaji yao kadhaa kutoka kwa wauzaji wanaouza bidhaa zao katika
Pop Up Bongo” alisema Shomari.

Mhe. Balozi Sefue aendelea kuwasisitiza watumishi wa umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao wanapokuwa katika maeneo ya kazi

index 
Katibu Mkuu Kiongozi  Mhe. Balozi Ombeni Sefue akiwaonyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) beji yenye jina lake ambayo amewaagiza watumishi wa Umma kuivaa wanapokuwa  katika maeneo  yao ya  kazi. Balozi Sefue alifanya mkutano na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam jana na kutoa taarifa ya Serikali kuhusu kesi ya Serious Fraud Office (SFO) dhidi ya Standard Bank.
…………………………………………………………………………………………………………..
Na Anna Nkinda – Maelezo
Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue ameendelea kuwasisitiza watumishi wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao wanapokuwa  katika maeneo  ya  kazi.
Mhe. Balozi Sefue aliutoa mwito huo jana wakati akijibu swali la Mwandishi wa Habari aliyemuuliza ni kwanini alikuwa amevaa beji yenye jina lake ambayo imemfanya kuonekana tofauti na siku zingine.
Alisema mwishoni mwa mwezi wa kumi na moja alifanya ziara ya kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuagiza  watumishi wote wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao.
“Nimeamua kuonyesha mfano kwa vitendo kufuatia agizo nililolitoa kwa watumishi wa Umma kwa kuvaa beji inayonitambulisha jina langu , nilisema nitakuwa wa kwanza kuvaa jina langu nimevaa. Kama mtumishi wa umma atakuwa na mashaka ajue mimi nimeshalivaa”.
“Mtumishi wa umma anapomuhudumia mwananchi ni lazima ajue amehudumiwa na nani, mtumishi wa Umma akifanya  kazi zake kwa kutenda haki sidhani kama ataogopa kuvaa beji inayomtambulisha jina lake hivyo basi kama nilivyoagiza watumishi wote wa Umma mvae beji zinazowatambulisha majina yenu”, alisisitiza Mhe. Balozi Sefue.
Mhe. Balozi Sefue alifanya mkutano na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam na kutoa taarifa ya Serikali kuhusu kesi ya Serious Fraud Office (SFO) dhidi ya Standard Bank.

MAJALIWA AAGANA NA BALOZI WA DRC

mj1 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini, Mhe. Juma – Alfani Mpango   ambaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 2, 2015 kuaga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mj2 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya kinyago Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo  nchini, Mhe. Juma-Alfani Mpango ambaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 2, 2015 kuaga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
mj3 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mhe.  Juma- Alfani  Mpango  ambaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 2, 2015 kuaga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………………………………………………………………
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambaye anamaliza muda wake, Bw. Juma-Alfani Mpango.
Akizungumza na balozi Mpango leo (Jumatano, Desemba 2, 2015), ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu alimshukuru balozi huyo kwa pongezi zake na kumuomba aendelee kuwa balozi mzuri wa kuitangaza Tanzania hata baada ya kurejea nyumbani.
Pia alitumia fursa hiyo kuwaombea heri wananchi wa DRC pamoja na Rais Joseph Kabila katika maandalizi ya uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika nchini humo mwakani.
Kwa upande wake, Balozi Mpango ambaye alisema amekaa hapa nchini kwa miaka 12, alimweleza Waziri Mkuu kwamba amejifunza mengi sana kutoka kwa viongozi wa Tanzania kubwa vikiwa ni uchapakazi na unyenyekevu. “Nimeona utawala wa Rais Benjamin Mkapa, Rais Jakaya Kikwete na sasa Dkt. John Pombe Magufuli. Ninavutiwa na hatua mnazochukua hivi sasa katika kupambana na rushwa na ufisadi,” alisema.
“Mambo niliyojifunza tangu nimekaa hapa ni uchapakazi na unyenyekevu. Unaona kabisa kwamba mtu anaamini kuwa madaraka siyo kitu cha kujivunia kwa mtumishi wa umma. Anachotakiwa kuwa nacho ni utayari wa kuwatumikia wananchi,” alisema kwa Kiswahili sanifu.
Balozi Mpango aliomba mahusiano ya nchi hizi mbili yaendelezwe kwani DRC imekuwa ikinufaika na matumizi ya bandari ya Dar es Salaam katika kusafirishia bidhaa zake kwenda nchi za nje.
“Bandari ya Dar es Salaam ni muhimu sana kwetu. Mwaka 2004 tulisafirisha tani za mizigo 200,000, mwaka 2014 ziliongezeka na kufikia tani milioni 1.3; na mwakani tunataraji zitaongezeka na kufikia tani milioni tatu,” alisema.

ni1 
Katibu Mkuu wizara ya Miundo Mbinu na Mawasiliano Juma Malik Akili akitoa maelezo kwa waandishi wa Habari wa ZBC kuhusiana na Ujenzi wa Bandari ya Maruhubi ambayo inatarajiwa kujengwa kuanzia Januari mwakani mjini Zanzibar.
ni2 
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallamwinyi Khamis baada ya kuwasili katika eneo la maruhubi ambalo linatarajiwa kujengwa Bandari kuanzia Januari mwakani mjini Zanzibar.
ni3 
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wakwanza kushoto akipata maelezo ya ramani ya ujenzi kutoka kwa Injinia Mkuu wa Shirika la Bandari Mbarouk Hamadi Mbarouk katika ziara ya kutembelea eneo ambalo linatarajiwa kujengwa Bandari Maruhubi mjini Zanzibar.
ni4 
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein katikati akitembelea eneo linalotarajiwa kujengwa Badari Maruhubi mjini Zanzibar.
ni5 
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wapili kushoto akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya miundo mbinu na Mawasiliano Juma Malik Akili wakati alipofanya ziara kutembelea eneo ambalo linatarajiwa kujengwa Bandari Maruhubi mjini Zanzibar.
PICHANA YUSSUF SIMAI -MAELEZO ZANZIBAR.

MAJINA SAHIHI YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

Kassim-Majaliwa-559x520 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anatumia majina matatu kama ifuatavyo: Kassim Majaliwa Majaliwa au Kassim M. Majaliwa.
Tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo, kumekuwa na uchanganyaji wa majina yake na hii ni kwa sababu tangu akiwa chuoni na jeshini, alikuwa akitanguliza kutaja ubini (jina la ukoo) na ndiyo maana ikawa inasomeka Majaliwa Kassim Majaliwa.
Endapo jina hilo litaanza kuandikwa na ubini, litapaswa kutenganishwa na koma kama ifuatavyo: Majaliwa, Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliteuliwa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli Novemba 19, 2015 na kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku hiyo hiyo. Aliapishwa Novemba 20, 2015 kwenye Ikulu ndogo ya Chamwino, Dodoma.

TANAPA yaimarisha ulinzi wa tembo kwa kuwafunga vifaa maalum

te1 
Wataalam wa Uhifadhi wakiongozwa na Dk. Alfred Kikoti (wa kwanza kulia) wakiendelea na zoezi la uwekaji kola maalum kwa tembo zinazosaidia kudhibiti mienendo ya tembo ndani nan je ya hifadhi ya Mfumo wa Ikolojia wa Ruaha Rungwa.
te2 
Zoezi la uvalishaji wa kola maalum kwa tembo katika hifadhi ya Ruaha likiendelea.
te3 
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi (mwenye kofia) akishuhudia zoezi la uvalishaji kola maalum kwa tembo katika Hifadhi ya Ruaha.
te4 
Daktari wa Wanyamapori kutoka Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori (TAWIRI) akijiandaa kumdunga sindano ya kumzindua tembo baada ya kukamilika kwa zoezi la kumvalisha kola maalum
te5 
Picha ya pamoja ya wahifadhi walioshiriki zoezi la uzinduzi wa program maalum ya uvalishaji kola kwa tembo katika Hifadhi ya Ruaha.
te6 
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi (kulia) akiongea na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Iringa wakati wa zoezi la uvalishaji kola kwa tembo katika Hifadhi ya Ruaha.
…………………………………………………………………………………..
Na Jovina Bujulu-MAELEZO)
Utalii ni miongoni mwa sekta muhimu zinazoliingizia Taifa pato hasa fedha za kigeni zinazotolewa na watalii wanaofika nchini kwa shughuli mbali mbali ikiwemo kuangalia wanyama na vivutio vilivyopo katika hifadhi za taifa.
Sekta hii ya utalii inakumbana na tatizo kubwa la ujangili ambalo linaripotiwa kuiingizia taifa hasara kubwa kutokana na idadi kubwa ya wanyama pori hasa tembo kuuawa kila mwaka.
Hivi karibuni Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA) limezindua programu maalam ya kuwavalisha tembo kifaa maalumu kijulikanacho kama “kola” au king’amuzi maalum shingoni mwa tembo hao kinachong’amua na kurekodi mienendo yao kwa kutumia mawasiliano ya satelaiti.
Program hiyo inatekelezwa katika mfumo wa ikolojia wa Ruaha Rungwa ambapo tembo 30 wanaoongoza makundi 30 wamevalishwa kola hizo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa program hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Bwana Allan Kijazi alisema kuwa inalenga kuimarisha ulinzi wa tembo nchini. “Lengo kuu la program hii ni kupata taarifa za kina juu ya mienendo ya tembo katika mfumo wa ikolojia wa Ruaha Rungwe zitakazosaidia kubainisha maeneo shorobo (njia za wanyama) na mitawanyiko yao kwa ajili ya ulinzi wa tembo” alisema Bwana Kijazi.
Aliendelea kusema kuwa teknolojia hiyo inawawezesha kujua mwenendo wa tembo ndani na nje ya hifadhi, kujua walipo, wanapopita, kasi yao, sehemu wanazojificha, wanapokunywa maji, ikiwa wamejeruhiwa, wanapopumzika, maeneo wanayokaa muda mrefu, kama wamekufa, kama wamehama hifadhi moja hadi nyingine na taarifa nyingine nyingi, hivyo itakuwa rahisi kwa askari wa wanyamapori kufuatilia usalama wa tembo hao.
Akizungumzia uanzishwaji wa program hiyo, Bwana Kijazi alisema kuwa inafadhiliwa na taasisi ya Global Government Facility pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP); ambapo UNDP kwa kushirikiana na TANAPA na SPANET wametoa kandarasi ya kufanya kazi hiyo ya kufunga “kola” kwenye tembo kwa kituo cha kimataifa cha utafiti wa Tembo “WORLD ELEPHANT CENTRE “ kilichopo mkoani Arusha.

Twanga Pepeta kuwapagawisha uzinduzi wa Kibaha Carnival ijumaa

index 
Mwimbaji Ally Choki kushoto akiwa na Luiza Mbutu katika moja ya shoo zao, bendi hiyo inatarajiwa kufanya nyoo kabambe katia uzinduzi wa eneo jipya la burudani la Kibaha Carnival siku ya ijumaa desemba 4 mwaka huu.
……………………………………………………
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
BENDI kongwe ya muziki wa dansi  hapa nchini Twanga Pepeta ‘wazee wa visigino’wanatarajia kutoa burudani ya aina yake katika uzinduzi rasmi  wa eneo jipya  linalojulikana kwa jina la ‘Kibaha Carnival’ siku ya ijumaa Desemba 4 mwaka huu.
Akizungumza na mwandishi i wa habari hizi Katibu wa kamati ya maandalizi kwa ajili ya siku hiyo  shauri Yomba Yomba alisema kwamba maandalizi kwa ajili ya aonyesho hilo ya aina yake ambalo litakwenda  sambamba na huo yamekamilika.
Yomba yomba alisema kwamba katika uzinduzi huo utakuwa wa aina yake kutokana na maandalizi mazuri ambayo tayari yamekamilika na baadhi ya vitu vichache vinaendelea kufanyiwa kazi ili siku hiyo iwe ya kiutofauti zaidi.
“Hapa kikubwa ndugu mwandishi siku ya ijumaa desemba 4 nadhani itakuwa ni siku ya kipekee zaidi kwani ndio ile siku ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu na shauku kubwa na mashabiki wa burudani pamoja na kujionea eneo jipya la kisasa la Kibaha Carnival likizinduliwa rasmi hivyo mambo yanakwenda vizuri mpaka sasa,”alisema Yomba Yomba.
Pia alibainisha kwamba siku hiyo ya uzinduzi mbali na bendi ya Twanga pepeta kutakuwepo na burudani nyingine ambazo zitakuwepo na lengo kuu ni kuhakikisha akila mdau wa burudani ambaye atafika siku hiyo anapata vionjo vya kila aina ikiwemo wasanii  mbali mbali wa kizazi kipya ambao maskani yao ni Mkoa wa Pwani na wengine waalikwa kutoka Dar es Salaam.
Kadhalika alisema kwamba kuanzishwa kwa eneo hilo la Kibaha Carnival ni kutokana na wadau wengi wa burudani wanakosa sehemu ambayo ni tulivu ya kwenda kutembelea katika siku za mapumziko hivyo kuzinduliwa sehemu hiyo itakuwa ni mwanzo wa kuanzisha program mbali mbali za burudani na michezo ili kuweza kukuza vipaji kwa wasanii wa kibaha na maeneo mengine ya jirani.
Katika hatua nyingine alisema kwamba kutakuwepo na viongozi wa serikali katika sherehe hiyo ya uzinduzi rasmi ambapo pia kutakuwepo na mashindano ya kula nyama choma ambapo washindi watajinyakulia zawadi kutoka kwa uongozi wa Kibaha Carnival na kuongeza shghuli nzima hiyo itakuwa ikiongozwa na Mc machachari hapa nchini Mc Jura pamoja na Scope V ‘mtoto wa kasuku.

Dk. Wilbroad Slaa ampa tano Dk. John Pombe Magufuli

images
Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa amesifia kasi ya rais John Magufuli hasa katika kupambana na ufisadi nchini.
Dk. Slaa amesema kuwa alichowahi kukizungumzia awali kimetimia kwa kuwa nchi hii ilihitaji mtu kama Magufuli.
 
“Nadhani sasa unaelewa niliposhikilia msimamo wangu. Katika mazingira ya sasa Magufuli ni bora zaidi. Niliwahi kusema kuwa hii nchi kwa siku za mwanzo inahitaji udikteta kuirudisha kwenye mstari ulioonyooka, nimefurahi sana,” Dk. Slaa amelimabia gazeti la Raia Mwema.
Amesema kuwa Bunge linatakiwa kufanya kazi ya kuudhibiti udikteta huo ili usivuke mipaka lakini limuunge mkono kwa hatua anazochukua.
Katika hatua nyingine, Dk. Slaa amemshauri Rais Magufuli kuiangalia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kuifumua.
“Pasipo kuchukua hatua ya kuifumua Takukuru, sina hakika kama matarajio yatafikiwa,” alisema Dk Slaa na kuongeza kuwa hatua hizo zinapaswa kuchukuliwa haraka.

MPANGO WA KUBORESHA AFYA NA MAZINGIRA MASHULENI WAZINDULIWA SHULE YA MSINGI WAILESI TEMEKE

sk1
Wanafunzi wa Shule ya msingi Wailesi wilayani Temeke jijini Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa  uzinduzi  rasmi mpango wa Fit For School Mpango wa kuboresha Afya na Mazingira Mashuleni na kuhamasisha watoto mashuleni wanawe mikono mara kwa mara, Mpango huo unafadhiliwa na Shirika la GIZ Tanzania kutoka Ujerumani na ulizinduliwa na unatekelezwa na taaisis ya SAWA.
sk2
Mpango huo ukizinduliwa rasmi kwa kukata utepe.
sk3
Moja ya mabango yanayoonyesha malengo ya mpango huo.
sk4
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Wailesi wilayani Temeke wakinawa mikono yao mara baada ya uzinduzi.
sk5
Bango hili likionyesha hatua tano za unawaji mikono kwa wanafunzi shuleni hapo.
sk6
Wanafunzi wakimsikiliza Sekela mmoja wa waratibu wa mpango huo alipokuwa akizungumza nao shuleni hapo wakati wa uzinduzi.

Wanafunzi wakionyesha mikono yao mara baada ya kunawa.

No comments :

Post a Comment