Rais
Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Mwakilishi Mkazi wa Benki ya
Dunia nchini Bi. Bella Bird alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam
leo Desemba 7, 2015
PICHA NA IKULU
MWENYEKITI WA CCM JAKAYA MRISHO KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA CCM
Mwenyekiti
wa CCM na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete akiongozana na Rais
Dkt John Pombe Joseph Magufuli , Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim
Majaliwa, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa
CCM (Bara) Mhe Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana
Kinana kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya
CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015
Mwenyekiti
wa CCM na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete akiongozana na Rais
Dkt John Pombe Joseph Magufuli , Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim
Majaliwa, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa
CCM (Bara) Mhe Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana
Kinana kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya
CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015
Mwenyekiti
wa CCM na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete akiongoza Kikao cha
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo
Desemba 7, 2015
Rais
Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipigiwa saluti na Katibu Mkuu wa CCM
Ndg. Abdulrahmana Kinana kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015
Rais
Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt
Salim Ahmed Salim. wengine ni Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa,
Makamu wa Rais Mhe samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu wa CCM Ndg.
Abdulrahmana Kinana kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi asimamishwa kazi.
Na Raymond Mushumbusi- Maelezo
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli, ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu Wizara ya
Uchukuzi, Dkt. Shaban Mwinjaka kuanzia leo ( Disemba 7, 2015) na
atapangiwa kazi nyingine.
Rais Dkt. Magufuli pia amevunja Bodi ya
Bandari na kutengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari Prof. Joseph
Msambichaka na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari Bw. Awadhi Massawe.
Aidha amewasimamisha kazi Wakuu wa Vitengo
vitano vya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Bandari ya Dar es Salaam
kutokana na kashfa ya ukwepaji kodi wa makontena 329 kwenye Bandari ya
Dar es Salaam.
Uamuzi huo umetangazwa leo na Waziri Mkuu
Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa wakati akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Wakuu wa vitengo waliosimamishwa kazi ni
pamoja aliyekuwa Meneja Mapato Bw Shaaban Mngazija ambaye kwa sasa
amehamishiwa Makao Makuu Kitengo cha Fedha, Mkuu wa Bandari Kavu (ICD)
Bw. Rajab Mdoe, Mkurugenzi wa Fedha Bw.Ibin Masoud na Meneja wa Bandari
Msaidizi-Fedha Bw. Apolonia Mosha.
Wengine waliosimamishwa kazi ni Wasimamizi
wanane wa Bandari Kavu (ICD) ambao ni Bi. Happygod Naftari, Bw.Juma
Zaaar, Bw.Steven Naftari Mtui, Bw.Titi Ligalwike,Bi. Lydia Prosper
Kimaro, Bw.Mkango Alli, Bw.John Elisante na Bw.James Kimwomwa ambaye
amehamishiwa Mwanza.
Hata hivyo Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim
Majaliwa alipofanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es salaam
Novemba 27 mwaka huu aligundua utendaji mbovu ndani ya Bandari ya Dar es
salaam na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na katika kufuatilia
utekelezaji wa maagizo watendaji wa mamlaka hizo wamesimamishwa kazi
kupisha uchunguzi.
SYMPOSIUM TO MARK HUMAN RIGHTS DAY 08 DEC 2015
The United Nations Systems
in Tanzania in collaboration with the Commission of Human Rights and
Good Governance (CHRAGG), Ministry of Constitutional and Legal Affairs
cordially invites the media to the Symposium to commemorate the 2015
Human Rights Day to be held at the Peacock Hotel, along Bibi Titi Road,
Mnazi Mmoja on Tuesday,08 December, 2015, at 0800-1200 pm.
The focus of the symposium is Linkage between Sustainable Development Goals (SDGs) and Human Rights. The
debate aim to engage government officials and youth on the newly
adopted Sustainable Development Goals specifically focusing on Goal # 2 (
Quality Education); Goal 10 ( Reduced inequalities among and within
nations); SDG 15 (Life on Land) and SDG 16 ( Peace Justice and Strong
institutions) .
The Panelists at the symposium will come from the United Nations Tanzania, Haki Elimu; CHRAGG and ESRF.
There are 17 SDGs and 169 targets
that were unanimously adopted by all 193 member states at the UN general
Assembly on 25 September 2015. The SDGs build on the goal-setting
agendas of United Nations conferences and the widely successful
Millennium Development Goals that have improved the lives of millions of
people. The new agenda recognizes that the world is facing immense
challenges, ranging from widespread poverty, rising inequalities and
enormous disparities of opportunity, wealth and power to environmental
degradation and the risks posed by climate change.
The UN General Assembly proclaimed
10 December as Human Rights Day in 1950, to bring to the attention ‘of
the peoples of the world’ the Universal Declaration of Human Rights as
the common standard of achievement for all peoples and all nations.
Muhumbili yapatiwa msaada wa mashine ya kisasa ya Digital ya X-Ray
Mkuu
wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk
Flora Lwakatare akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu matumizi ya
mashine mpya ya X-ray ya digitali. Dk Lwakatare amesema mashine hiyo
ina uwezo wa kupiga picha na kutumwa nje ya nchi kwa ajili ya ushauri wa
kitaalamu zaidi. Mashine hiyo haihitaji chumba cha kusafishia picha
wala dawa za kusafishia.
Mkuu
wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk
Flora Lwakatare akitoa maelezo kuhusu idadi ya wagonjwa waliopata huduma
ya kipimo cha CT Scan baada ya mashine hiyo kukamilika.
Pichani ni misaada ya shuka 200, neti 150 na Televisheni nne ikipokelewa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Pichani ni misaada ya shuka 200, neti 150 na Televisheni nne ikipokelewa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
………………………………………………………………………………
Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH) imepata mashine mpya na ya kisasa ya Digital X-ray ambayo
wataalamu wake hawatalazimika kutumia filamu kusafisha picha kama
ilivyozoeleka katika mashine za kawaida.
Mashine hiyo imegharimu Dola
200,000 za Marekani ambazo zimetolewa na serikali kupitia Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii ambayo ina uwezo wa kusafirisha picha nje ya nchi
ili kupata ushauri wa kitaalamu.
Akilelezea kuhusu maendeleo ya
mashine ya MRI na CT-SCAN , Mkuu wa Idara ya Mionzi wa MNH, Dk Florah
Lwakatare amesema matengenezo ya mashine hizo yamekamilika na kwamba
hadi sasa wagonjwa 148 wamepimwa kwa kutumia mashine ya MRI , wakati
wagonjwa 304 wamepimwa kwa kutumia CT-SCAN .
Katika hatua nyingine Hospitali
ya Taifa Muhimbili leo imepokea msaada wa mashuka 200, vyandarua 150 ,
Televisheni nne , Decoder 4 pamoja na Tv Stand 4.
Akikabidhi msaada huo ambao
umetolewa na Kampuni ya Mr. Uk Electronics Limited ya Dar essalaam,
mwakilishi wa kampuni hiyo John Solomon ametoa wito kwa jamii kuwa
na moyo wakujitolea na kushirikiana na serikali katika kuboresha huduma
mbalimbali za jamii ikiwemo huduma za afya .
NEC Yataoa Tamko Kuhusu Uchaguzi wa Wabunge Arusha Mjini na Handeni.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kulia)
akizungumza na waandishi wa habari (ambao hawapo pichani) leo jijini Dar
es Salaam kuhusu uchaguzi wa wabunge unaotarajiwa kufanyika Tarehe
13/12/2015 katika jimbo Handeni na Arusha Mjini,(kushoto) ni Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura Bw.Clarence Nanyaro
kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi.Na Anitha Jonas –MAELEZO
Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva(ambaye hayupo katika picha) leo
jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waaandishi wa habari
kuhusu taratibu zitakazo tumika katika uchaguzi wa wabunge katika jimbo
la Arusha na Handeni.
Mwandishi
wa Habari kutoka Kituo cha Utangazaji ITV Bi:Ufoo Saro akimuuliza swali
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva
(ambaye hayupo katika picha)kuhusu suala la ulinzi utakao kuwepo kwa
wananchi wa majimbo hayo wakati wa kupiga kura.
DK.SHEIN AMUAPISHA MKUU WA WILAYA MICHEWENI PEMBA
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akimuapisha Nd,Abeid Juma Ali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa
Kaskazini Pemba,kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya
Mji wa Zanzibar,hafla ya kiapo ilifanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
leo,{Picha na Ikulu}
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akimuapisha Nd,Ali Khamis Juma kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
kabla alikuwa Naibu katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji Ustawi wa Jamii
Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar,hafla ya kiapo hicho ilifanyika
ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,{Picha na Ikulu}
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba Nd,Abeid Juma Alina Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Nd,Ali Khamis Juma leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.{Picha na Ikulu}
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu mpya wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba Nd,Abeid Juma Ali (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Nd,Ali Khamis Juma (kulia) baada ya kuwaapisha kushika nyadhifa hizo leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.{Picha na Ikulu}
Watumishi wa Umma Kusaini Kiapo cha Ahadi na Uadilifu
Katibu
Mkuu,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu(kulia)
akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu
utekeleza wa Ahadi ya Uadilifu kwa Watumishi wa Umma nchini ambao
ulizinduliwa Agosti Mosi mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Bw. Charles Senkondo
Picha na Magreth Kinabo – (MAELEZO).
………………………………………………………………………………………………..
Na Lilian Lundo-Maelezo
Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma imeanza rasmi kutekeleza Ahadi ya Uadilifu kwa
watumishi wa Umma nchini ambao ulizinduliwa Agosti Mosi mwaka huu.
Akiongea na vyombo vya habari
leo, Katibu Mkuu Hab Mkwizu amesema utekelezaji huo umeanza rasmi
Disemba, 2015 ambapo kila mtumishi wa Umma ataweka saini ya kiapo kwa
kuzingatia taratibu zilizowekwa na mazingira ya Taasisi husika.
“Utaratibu wa Utekelezaji wa
Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa Umma umetolewa kupitia waraka wa Mkuu
wa Utumishi wa Umma Na. 2 wa mwaka 2015 kuhusu utekelezaji wa Ahadi ya
Uadilifu kwa viongozi, watumishi wa Umma na sekta binafsi wa tarehe 1
Agosti, 2015.” Alisema Mkwizu.
Mkwizu aliongezea kwa kusema,
uanzishwaji wa Ahadi ya Uadilifu ni muendelezo wa uundwaji wa vyombo
vya kusimamia maadili baada ya ongezeko kubwa la ubadhirifu, utoro
sehemu za kazi na kushuka kwa nidhamu katika kipindi cha miaka ya
themanini na tisini.
Alivitaja vyombo vingine ambavyo
vilianzishwa kusimamia ahadi na uadilifu kuwa ni Sekretariate ya
Maadili ya Viongozi wa Umma, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Mkwizu alivitaja vipengele
ambavyo mtoa ahadi anatakiwa kuvitamka ni, kuwa mzalendo wa nchi yake na
kutii Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kuhudumia Umma na
watumishi wenzake kwa heshima, kutimiza wajibu wa kutoa huduma bora kwa
umma, kutoa huduma bora kwa usawa kwa watu wote na kutofanya ubaguzi wa
dini, siasa, kabila, udugu, ukanda, jinsia, urafiki au hali ya mtu.
Vipengele vingine ni kutumia
rasilimali za Umma kwa manufaa ya Umma, kutotoa siri za Serikali au
mteja kwa watu wasiohusika isipokuwa kwa maslahi ya Umma, kufanya kazi
kwa nidhamu ya hali ya juu, kutoomba kushawishi, kutoa wala kupokea
rushwa na kutotumia madaraka kwa manufaa binafsi ya ndugu, rafiki au
jamaa.
Aidha, Mkwizu ametoa wito kwa
waajiri wote kuhakikisha kuwa utekelezaji wa Ahadi na Uadilifu
unakamilika ifikapo tarehe 31/12/2015 na kuwasilisha Ofisi ya Rais –
UTUMISHI kabla ya tarehe 25/02/2016 na utekelezaji wake kuwa kila
ifikapo Juni 30 ya kila mwaka. Fomu za Ahadi ya Uadilifu zinapatikana
katika tovuti ya Ofisi ya Rais – UTUMISHI yenye anwani www.utumishi.go.tz.
RAIS MAGUFULI AVUNJA BODI YA MAMLAKA YA BANDARI
* Atengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu TPA
* Amsimamisha kazi Katibu Mkuu Uchukuzi
* Waziri Mkuu awasimamisha kazi watumishi wengine 13 wa bandari
RAIS Dkt. John Pombe Magufuli
amevunja Bodi ya Mamlaka ya Bandari (TPA) na kutengua uteuzi wa
Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari, Prof. Joseph Msambichaka pamoja na
Mkurugenzi Mkuu wa Bandari, Bw. Awadhi Massawe.
Dkt. Magufuli pia ametengua uteuzi
wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaban Mwinjaka kuanzia leo
(Jumatatu, Desemba 7, 2015), na kwamba atapangiwa kazi nyingine.
Akitangaza uamuzi huo mbele ya
waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika leo ofisini kwake
Magogoni, jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema
hatua hizo zimechukuliwa kufuatia ziara mbili za kushtukiza alizozifanya
katika mamlaka ya bandari Novemba 27 na Desemba 3, mwaka huu.
Waziri Mkuu amesema Rais Magufuli
amevunja bodi hiyo na kutengua uteuzi wa viongozi hao kutokana na
utendaji mbovu wa muda mrefu wa Mamlaka ya Bandari na kwa kitendo cha
viongozi hao kutochukua hatua kwenye vyanzo.
Pia alisema Katibu Mkuu
amesimamishwa kazi kwa sababu ya kutosimamia kwa makini mashirika mawili
ya Bandari na Reli ambayo yako chini ya wizara yake ambako yeye
mwenyewe alizuru Shirika la Reli (TRL) Desemba 3, 2015 na kukuta kuna
ubadhirifu wa sh. bilioni 16.5/-.
“Tarehe 3 Desemba mwaka huu
nilifanya ziara ya kushtukiza pale TRL nikakuta wametumia visivyo sh.
bilioni 13.5/- walizopewa na Serikali. Pia nilikuta wamekopa sh. bilioni
3/- kutoka benki ya TIB lakini nazo wamezitumia nje ya utaratibu. Fedha
hizi zilikuwa ni za kusaidia kuboresha miradi ya shirika lakini wao
wamezitumia visivyo. Uchunguzi bado unaendelea,” alisema Waziri Mkuu.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa amewasimamisha kazi kuanzia leo viongozi watano wa sekta
zilizotoa ruhusa ya makontena kutoka ndani ya bandari pamoja na
watumishi wanane wa bandari kavu ambao walihusika na ukwepaji kwa
makontena 2,387.
“Viongozi hawa hawakuwemo kwenye
ripoti ya ukaguzi lakini ni wahusika wakuu. Hawa ndiyo waliotoa ruhusa
ili makontena yaende kwenye ICDs. Nao ni aliyekuwa Meneja Mapato ambaye
kwa sasa amehamishiwa Makao Makuu kitengo cha Fedha, Bw. Shaban
Mngazija; aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Mkuu wa Bandari Kavu (ICD) –
ambaye amehamishiwa Makao Makuu kwa Naibu Mkurugenzi Co-operate
Services, Bw. Rajab Mdoe; Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Bw. Ibin Masoud; na
Meneja Bandari Msaidizi – Fedha, Bi. Apolonia Mosha
Pia amewasimamisha kazi wasimamizi
wanane wa Bandari Kavu (ICDs) ambao ni Happygod Naftari, Juma Zaar,
Steven Naftari Mtui, Titi Ligalwike, Lydia Prosper Kimaro, Mkango Alli,
John Elisante na James Kimwomwa ambaye alihamishiwa Mwanza lakini
kuanzia sasa anasimamishwa kazi huko huko aliko.
“Bila wao kuidhinisha hakuna
kontena linaweza kutoka au kwenda kokote. Watumishi wote hao wawe chini
ya ulinzi na waisaidie polisi kupata taarifa hayo makontena ni ya nani
na yana thamani gani,” Waziri Mkuu alisema.
Waziri Mkuu Majaliwa aliwaeleza
waandishi wa habari kwamba Desemba 3, mwaka huu aliamua kurudi tena
bandarini kufuatilia na kuangalia hatua ya udhibiti wa upitishaji wa
bidhaa mbalimbali kinyume cha utaratibu. “Ziara yangu ilinipitisha hatua
zote za upitishaji mizigo ambazo pia kwa mujibu wa Taarifa ya Ukaguzi
wa Ndani ya tarehe 30 Julai 2015, Mamlaka ya Bandari iligundulika kuwepo
kwa mianya mingi ya ukwepaji kodi ikiwemo makotena 2,387 yaliyopitishwa
kati ya Machi – Septemba 2014 kinyume cha utaratibu”.
“Vitendo hivi vinaonyesha kuwa
bandari yetu hupitisha makontena mengi bila ya kulipiwa kodi na hakuna
hatua yoyote inayochukuliwa. Serikali haitavumilia kuona watu wachache
au kikundi chochote kilichojipanga kuhujumu mifumo au kuiibia Serikali
kwa namna yoyote ile kwa manufaa ya wachache kwani bandari ni eneo
muhimu ambalo likisimamiwa vizuri, linaweza kukusanya fedha nyingi na
kuchangia Pato la Taifa,” alisema.
Desemba 3, mwaka huu, Waziri Mkuu
alimpa saa tatu tu Kaimu Meneja wa Bandari, Bw. Hebel Mhanga amletee
ofisini majina ya watumishi wote waliohusika na ukwepaji kodi huo. Pia
alimpa Meneja huyo wiki moja kuhakikisha kuwa mamlaka hiyo inabadilisha
mfumo wa utozaji malipo kutoka kwenye billing system na badala yake
kuweka mfumo wa malipo wa kielektroniki (e-payment). Mwisho wa
kukamilisha zoezi hilo ni Desemba 11, 2015.
No comments :
Post a Comment