Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi,
(wa kwanza kulia), akiungana na Mbunge wa viti maalum, Angela Kairuki,
(wa pili kulia), mkurugenzi w manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam,
Photidus Kagimbo, watatu kulia), mganga mfawidhi wa hospitali ya Temeke,
Dkt. Amani Malima, (wanne kulia) na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke,
Dkt. Sylvia Mamkwe, (wa kwanza kushoto), wakati PSPF ikikabidhi msaada
wa vitanda, mashuka na magodoro kwa hospitali hiyo, Desemba 7, 2015.
Msaada huo ni utekelezaji wa ahadi ya Mfuko baada ya kuombwa na Mh.
Angela Kairuki.
……………………………………………………………………………………..
Na K-vis Media/Khalfan Said
MFUKO wa Pensheni wa PSPF, imeisaidia
hospitali ya wilaya ya Temeke, vitanda,magodoro na mashuka ili kusaidia
serikali katika juhudi zake za kupunguza uhaba wa vifaa vya hospitali
za umma.
Msaada huo ambao ni utekelezaji wa maombi ya Mbunge wa viti maalum, Angela Kairuki, alioutoakwa uongozi wa PSPF, baada ya kutembelea hospitali hiyo wakati akiwa naibu waziri wa Sheria na Katiba, na kukuta akina mama wajawazito waliofika hospitalini hapo kujifungua wengine wakilala chini kutokana na uhaba wa vitanda, alisema Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Abdul Njaidi na kuongeza PSPF, kwa kuwa ni Mfuko unaotoa huduma kwa jamii nao hauna budi kutoa sehemu ya faida na kuirejesha kwa jamii kwani wengi wao wanaofika hapo hospitali kwa ajili ya matibabu ni wanachama wa Mfuko na wengine ni wanachama watarajiwa wa Mfuko.
Kufuatia maombi hayo Mfuko huo umekabidhi vifaa hivyo leo Desemba 7, 2015, ambapo Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi, alikabidhi vifaa hivyo kwa
niaba ya Mkurugenzi Mkuu.
niaba ya Mkurugenzi Mkuu.
Akipokeavifaa hivyo katika hafla iliyohudhuriwa na Mkurugenzi wa Mnaispaa ya Temeke, Photidus Kagimba, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Dkt. Sylvia Mamkwe, na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke, Dkt. Amani Malima, aliishukuru PSPF, kwa moyo huo wa kusaidia jamii.
“PSPF mmeonyesha moyo wa uungwana kwa kusaidia akina mama zetu wakati wakisubiri
kupatiwa huduma wakati wa kujifungua basi wawe na mahala pazuri pa kulala.”
kupatiwa huduma wakati wa kujifungua basi wawe na mahala pazuri pa kulala.”
Njaidi (kulia), akiangalia wakati fundi akiunganisha moja ya vitanda hivyo wakati wa makabidhiano hayo
Njaidi akisaidiana na Muuguzi mwandamizi wa hospitali hiyo, kuweka sawa shuka kwenye kitanda
Mh.
Angela Kairuki, (wapili kulia), akimsikiliza Afisa Uhusiano Mwandamizi
wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, wakati wakibadilishana mawazo kabla ya
kukabidhi vifaa hivyo. Wengine kushoto ni maafsia wa PSPF
Mh. Kairuki akipatiwa maelezo juu ya huduma zilizochapishwa kwenye kipeperushi cha PSPF
Mh. Angela Kairuki akitoa hotuba yake wakati wa kupokea na kukabidhi msaada huo
Mh. Angela Kairuki akitoa hotuba yake wakati wa kupokea na kukabidhi msaada huo
Mganga mkuu wa wilaya ya Temeke, Dkt. Sylvia Mamkwe, akitoa nasaha zake
Mh.
Kairuki (kulia), akijadiliana jambo na mafisa wa hospitali ya Temeke na
uongozi wa wilaya pamoja na Afisa Uhusiano wa PSPF, Bw. Njaidi
Wafanyakazi wa hospitali hyo wakibeba sehemu ya vitanda hivyo
Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bi.
Sophia Mjema, akipena mikono na Bw. Njaidi wakati akimshukuru kwa msaada
huoKhalfan Said Photojournalist













No comments :
Post a Comment