Monday, December 7, 2015

“HAPA KAZI TU” WAPIGA PICHA NA WAANDISHI WA HABARI WAKIFUATILIA TAARIFA YA WAZIRI MKUU JANA OFISINI KWAKE

01 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na waandishi wa habari, kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, jijini Dar es salaam Desemba 7,2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
1 
Wapiga picha wakifuatilia wakati Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa alipozungumza na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 7, 2015,  Mkurugenzi wa Fullshangweblog Bw. John Bukuku (kulia) alikuwa ni mmoja wapo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
2 
Wapiga picha wakifuatilia wakati Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa alipozungumza na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 7, 2015. Mkurugenzi wa Fullshangweblog Bw. John Bukuku (kulia) alikuwa ni mmoja wapo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
4 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 7, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MRADI WA VIJANA WAMFURAHISHA MRATIBU WA UN NCHINI

IMG_6094
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Issa Machibya akiongozana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez mara tu baada ya kumpokea alipowasili ofisini kwake akiwa ameongozana na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan, pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem (hawapo pichani).
Na Mwandishi wetu, Kigoma
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ameelezea kufurahishwa kwake na uwapo wa mradi wa kusaidia vijana wa kitanzania kujifunza ujasirimali na kujitegemea.
Akizungumza katika shughuli za uzalishaji mali za vijana wa Shirika lisilo la kiserikali la Nyakitonto Youth Development Tanzania la mjini Kigoma alisema kwamba shughuli wanazofanya vijana hao zinamsisimua sana.
“Tunafurahi sana mimi na wenzangu kutembelea mradi huu unaofadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ambao unachochea ujasirimali miongoni mwa vijana. Sote tunajua kwamba vijana wengi wa Kitanzania wanaume kwa wanawake wameelimika lakini hawana ajira rasmi. Na suala la ujasiriamali ni kitu ambachio mtu anaweza kujifunza, na ujasiriamali unatoa fursa kwa vijana kujiunga katika kundi la wafanyakazi kwa kujiajiri wenyewe.
“Tunajua kwamba kupitia shughuli zinazofadhiliwa na ILO katika ngazi ya jamii na kwa kufuata maelekezo ya serikalai za mtaa vijana wanaanzisha biashara mbalimbali binafsi au na jamii. Kiwanda cha kutengeneza sabuni ni mfano mzuri sana. Tunaona kwamba mradi huu unawaongezea kipato na hivyo kuweza kusaidia familia zao na kupeleka watoto shuleni na kuboresha lishe . Kwa ufupi mradi kama huu unasaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazokabili kaya maskini Kigoma” alisema Rodriguez
ILO Kigoma inaendesha mafunzo ya ujasirimali kwa vijana kwa lengo la kuwawezesha kujiajiri wenyewe na kuhudumia familia zao kwa kuziwezesha kupata huduma bora za elimu na afya kutokana na kipato chao.
IMG_6098
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Issa Machibya (kushoto) akibadilishana ‘Business card’ na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem.
Alisema kwamba amefurahishwa na mradi huo ambao unawawezesha vijana kutambua fursa mbalimbali zilizopo na kuzitumia vyema kufanikisha maendeleo ya familia zao.
Aidha alisisitiza haja ya jumuiya ya kimataifa kuusaidia mkoa Kigoma katika nyanja mbalimbali za kiuchumi hasa katika eneo la ajira kwa vijana kutokana na ukarimu wa wakazi wa mkoa huo katika kuwapokea na kuwahudumia wakimbizi kutoka nchi za maziwa makuu kwa upendo.
Rodriguez alisema pamoja na ombi hilo Mratibu huyo wa shughuli za kimataifa ambaye ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) alisema wao kama UN wakifanyakazi pamoja wataendelea kutoa misaada kwa wakimbizi hasa uanzishaji wa miradi ya kiuchumi kwa vijana na wanawake.
Kwa upande wake Mwakilishi mkazi wa Shirika la Umoja wa mataifa la Idadi ya watu (UNPFA), Dkt. Natalia Kanem alisema kuwa kupatiwa mitaji na kuanzisha vikundi vya uzalishaji kwa vijana na wanawake kunasaidia kuongeza ajira lakini pia kusaidia kupunguza ongezeko kubwa la idadi ya watu bila mpangilio.
Katika risala yao kwa uongozi huo wa Umoja wa Mataifa vijana kutoka Nyakitonto Youth Development Tanzania wamesema kuwa misaada iliyotolewa kwao imewasaidia kupata ujuzi na kuanzisha miradi ya uzalishaji mali ikiwa ni sehemu ya kujiajiri na kujiongezea kipato ili waweze kuendesha maisha yao bila utegemezi.
IMG_6105
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Issa Machibya akitoa taarifa ya mkoa wake kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na ujumbe ofisini kwa Mkuu huyo wa mkoa.
Hata hivyo vijana hao katika risala yao iliyosomwa na Meneja miradi wa shirika hilo, Anjelina Gulanywa walisema kuwa pamoja na mafanikio hayo wanakabiliwa na changamoto utaalam mdogo, mitaji na vitendea kazi vya kisasa ili kufanya shughuli zao kuwa na mafanikio zaidi.
Naye Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu, Issa Machibya alieleza kuridhishwa kwake na juhudi za Umoja wa Mataifa katika kusaidia miradi mbalimbali mikoani mwake ambayo inasadia wananchi kukabiliana na umaskini.
Mkoa wa Kigoma una mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa yakifanya kazi mbalimbali za maendeleo na za kutoa huduma za kibinadamu kwa wakimbizi.
Mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa yanayotekeleza miradi mbalimbali mkoani Kigoma ni pamoja na Shirika la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR),Shirika la Afya Duniani ( WHO), Shirika la Mpango wa Idadi ya watu (UNFPA) ,Shirika la kazi la Kimataifa ( ILO), Shirika la Kuhudumia watoto( UNICEF), Shirika la Kuhudumia wahamiaji ( IOM), Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika la maendeleo (UNDP).
IMG_6134
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akielezea dhumuni la safari yake katika mkoa wa Kigoma kwa Mkuu wa mkoa huo, Kanali Mstaafu, Issa Machibya.
IMG_6123
Afisa Mawasiliano wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) nchini, Magnus Minja akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana yenye lengo la kuwawezesha kujiajiri wenyewe na kuhudumai familia zao kwa kuziwezesha kupata huduma bora za elimu na afya kutokana na kipato chao unaofadhiliwa na shirika hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu, Issa Machibya.
IMG_6147
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwasilisha Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (Sustainable Development Golas-SDGs) kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Issa Machibya. Kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem.
IMG_6152
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akikabidhi zawadi ya Khanga ya ‘miaka 60 ya UNFPA Tanzania’, kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanal Mstaafu, Issa Machibya, huku Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem akishuhudia tukio hilo.
IMG_6156
Malengo ya maendeleo endelevu sasa yamewafikia Kigoma. Pichani ni Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu, Issa Machibya na baadhi ya wakurugenzi katika ofisi ya mkuu huyo wa mkoa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Umoja wa Mataifa Dar es Salaam na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
IMG_6161
IMG_6172
IMG_6164
Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu, Issa Machibya akiagana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyemtembelea ofisini kwake kabla ya kuelekea kambi ya wakimbizi Nyarugusu.

STANDARD CHARTERED TANZANIA WINS BANK OF THE YEAR AWARD

banker of the year
Standard Chartered Bank Tanzania Limited has been awarded the prestigious ‘Bank of the Year’ award at The Banker Awards 2015. This is the eighth time that the Bank is winning this award which was announced at a grand gala dinner programme held at an award ceremony in London last Wednesday evening.
With more than fifty lenders operating within its borders, Tanzania has a healthy and competitive Banking sector. Standard Chartered Bank Tanzania Limited has stayed ahead of the game by maximising its digital services to make banking a less time consuming activity for Tanzanians.
The Chief Executive Officer for the Bank in Tanzania, Sanjay Rughani said, “We are delighted to have won this prestigious award. It is a testimony of our commitment to serve our clients in this market consistently over so many years. With a reputation for high quality service, innovation and connecting Tanzania to neighbours and the world, we have a special offer to our clients. We are, therefore, proud to be able to make positive contributions in Tanzania.”
Initiatives which motivated the accolade from The Banker were Standard Chartered Bank’s Straight2Bank online service, a fully integrated banking platform that offers a full range of transactions for clients that continues to be a market’s leading service. Additionally, in March this year, the Bank launched the “Straight2Bank Wallet”, a mobile payment service for corporate clients in Tanzania. The service enables the Bank’s corporate clients to make almost instantaneous bulk payments directly from their Standard Chartered Bank accounts into their beneficiaries’ M-PESA and TigoPesa accounts. The Bank’s corporate and institutional services and support continues to enable companies operating in Tanzania to fund their businesses and hedge themselves against currency volatility.
For the award period under review, Q1 2014 to Q2 2105, Standard Chartered Bank in Tanzania ran a pan-Bank staff campaign called ‘MySelf MyBrand’ geared towards personalizing service thereby enhancing customer service.
The Bank also organized a number of client workshops aimed at creating more awareness on its various products and services as well as enhancing financial literacy and skills on running profitable businesses and understanding banking and regulatory requirements.
During the period, the Bank’s net profits grew by 12% and return on equity increased to 23%, reflecting a commitment to shareholder returns.
Now in its 16th year, The Banker Awards is one of the most prestigious events within the industry. The Banker is the world’s premier banking and finance magazine, read in over 180 countries around the world. The Banker is the key source of data and analysis for the industry. Its unique database of more than 4,000 banks, maps their financial strength and soundness via Tier I capital, profitability, and their performance versus their peers.
This is the eighth time Standard Chartered Bank Tanzania has won the `Bank of the Year’ award. The bank had earlier won this award consecutively from 2002 – 2005, and thereafter in 2007, 2010 and 2011.

ASYA IDAROUS KHAMSINI ANOGESHA SIKU YA MTANZANIA SEATTLE

Walimbwende wakiwa tayari kufanya vitu vyao wakiwa na vivazi vya mwanamitindo nguli Asya Idarous Khamsini kwenye siku ya Mtanzania iliyofanyika siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 Seattle jimbo la Washington nchini Marekani.
Mlimbwende akiwa kwenye kivazi kutoka kwa mwanamitindo nguli Asya Idarous Khamsini kwenye siku ya Mtanzania iliyofanyika siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 Seattle jimbo la Washington nchini Marekani.
Kivazi chekundu kikiwa na riboni ya punda milia kikimfanya mlimbwende atabasamu jinsi gani alivyopendeza kivazi toka kwa mwanamitindo nguli Asya Idarous Khamsini kwenye siku ya Mtanzania iliyofanyika siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 Seattle jimbo la Washington nchini Marekani.
Kivazi toka kwa mwanamitindo nguli Asya Idarous Khamsini kwenye siku ya Mtanzania iliyofanyika siku ya Jumamosi Desemba 5, 2015 Seattle jimbo la Washington nchini Marekani.

ALBAMU YA NYIMBO ZA INJILI YA SOGEA NA BARAKA ZA BWANA YAZINDULIWA RASMI DAR E S SALAAM NA MHE. ANGELA KAIRUKI

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo na Makazi, Angela Kairuki (kushoto), akionesha DVD ya nyimbo za injili iitwayo Sogea wakati wa uzinduzi wa albamu mbili za
nyimbo hizo ikiwepo na ya Baraka za Bwana zilizoimbwa na muimbaji Anna Shayo Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mwanaharakati Hoyce Temu na mwimbaji na mmiliki wa albam hizo, Anna Shayo. Kairuki alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo na Makazi, Angela Kairuki (kushoto), akionesha DVD ya nyimbo za injili iitwayo Sogea wakati wa uzinduzi wa albamu mbili za
nyimbo hizo ikiwepo na ya Baraka za Bwana zilizoimbwa na muimbaji Anna Shayo Dar es Salaam juzi. Wa pili kulia ni Mwanaharakati Hoyce Temu na mwimbaji na mmiliki wa albam hizo, Anna Shayo. Kairuki alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo. Kulia ni mdogo wake Hoyce Temu.
Mwimbaji na mmiliki wa albam hizo, Anna Shayo (kulia), akimkabidhi Kairuki risala yake.
Waziri Kairuki akimkabidhi Anna Shayo kitita cha sh.milioni moja.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Juvenalister Mabumba akitoa burudani katika uzinduzi huo.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Ulimbaga Mwakatobe akiimba wakati wa uzinduzi huo.
Mwimbaji Andrew Kihwelu (kushoto), akitoa burudani.
Mwimbaji  Supa Belgano (kulia), akitoa burudani.
Mhe. Kairuki akisalimiana na waimbaji wa nyimbo za injili.

MKUTANO WA MWAKA WA WATAALAMU WA MANUNUZI NA UGAVI WAFUNGULIWA JIJINI ARUSHA.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wataalamu wa Manunuzi na Ugavi nchini(PSPTB)Dk Hellen Bandiho akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Wataalamu unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa AICC jijini Arusha na kusisitiza miiko ya uadilifu katika manunuzi ya umma na sekta binafsi.
Mjumbe wa Bodi ya Wataalamu wa Manunuzi na Ugavi nchini(PSPTB)Ahmed Kilima akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Wataalamu unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa AICC jijini Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Manunuzi nchini(PSPTB)Dk Clemence  Tesha  akizungumza jambo na wajumbe wa mkutano wa mwaka wa Wataalamu wa taaluma ya Manunuzi na Ugavi unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa AICC jijini Arusha na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka mikoa mbalimbali nchini na wageni kutoka nchi jirani.
Wajumbe wakiwa kwenye ukumbi wa Simba 
Wajumbe wa mkutano ambao ni wana taaluma ya Manunuzi  na Ugavi wakifatilia mada kwenye mkutano huo leo.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa Manunuzi  na Ugavi wakifatilia mada kwenye mkutano huo leo.
Wajumbe wa mkutano wa mwaka wa PSPTB
Mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB,Dk Charles Kimei(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa fani Manunuzi na Ugavi nchini baada ya kufungua mkutano wa mwaka ambao amesisitiza umuhimu wa kufanya manunuzi sahihi yenye lengo la kuokoa fedha za umma.

CHINA KUPITIA JIMBO LA JIANGSU YATOWA MSAADA WA DAWA WENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 500

kom1 
Balozi mdogo wa China aliyepo Zanzibar Xie Yunliang akitoa maelezo wakati wa sherehe ya kukabidhi msaada wa dawa zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 500 zilizotolewa na  Jimbo la Jiangsu kwa ajili ya Wananchi wa Zanzibar. Sherehe hiyo ilifanyika Bohari Kuu ya Madawa  Maruhubi Mjini Zanzibar. na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
kom2 
Baadhi ya Madaktari wa China na waalikwa wakifuatilia sherehe ya makabidhiano ya msaada wa dawa  mbali mbali za binaadamu katika sherehe iliyofanyika Bohari Kuu ya Madawa Maruhubi.
kom3 
Kamishna wa Afya na Uzazi wa Mpango ambae pia ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Jimbo la Jiangsu Hong Hao akizungumza wakati wa makabidhiano ya dawa zenye thamani ya shilingi milioni 500 (kulia) Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabiti Kombo.
kom4 
Balozi mdogo wa China aliyepo Zanzibar Xie Yunliang na Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo wakitia saini makabidhiano ya dawa hizo zilizotolewa na Jimbo la Jiangsu.
kom5 
Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo na Balozi mdogo wa China wakibadilishana hati za makabidhiano ya msaada wa dawa zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 500 katika sherehe zilizofanyika Bohari Kuu ya Madawa Maruhubi.
kom6 
Balozi mdogo wa China akimkabidhi Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo sehemu ya Dawa zilizotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kupitia Jimbo la Jiangsu (kati) Naibu Mkurugenzi Mkuu ambae pia ni Kamishna wa Afya na Uzazi wa Mpango wa Jimbo hilo Hong Hao. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.​

Wasanii SHIWATA kumpa Magufuli ufagio wa chuma

shiwata
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeamua kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano, John Magufuli la kufanya usafi nchini siku ya sherehe za Uhuru 9/12/2015 kufagia, kulima, kuzoa taka na kusafisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa usafi huo utaanzia makao makuu yao Ilala Bungoni, soko la Ilala,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mmachinga Complex, Soko la Mitumba Karume, Kariakoo, Mnazi Mmoja, Soko la Kisutu, Posta ya zamani, soko la samaki Feri mpaka Ikulu.
Alisema zaidi ya wanachama 300 wa SHIWATA kutoka fani mbalimbali za wanamichezo, wasanii, waandishi wa habari na wadau wamethibitisha kushiriki kufanya usafi huo kutokomeza ugonjwa wa kipundupindu unashika kasi katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam.
Taalib alisema kazi ya usafi huo itaanza saa 1.30 asubuhi kila mmoja aje na fagio, jembe, reki, au zana yeyote ya kufanyia usafi na kuvaa mavazi rasmi ya kufanyia kazi za usafi.
“Baada ya kukamilisha kazi ya usafi tutamkabidhi Rais Dkt. Magufuli fagio maalum wa Chuma kumuunga mkono katika operesheni aliyoianza ya kupambana na mafisadi na wezi wa mali ya umma” alisema Mwenyekiti Taalib.
Alisema fagio hilo la chuma ni mfano wa zana ambayo itamwezesha kuwafagia na kuwatokomeza mafisadi wote hapa nchini wanajilimbikizia mali wakati watanzania wakiishi maisha ya magumu ya mlo mmoja kwa siku.
Mwenyekiti Taalib alisma maazimio ya kumuunga mkono Dkt. Magufuli kwa vitendo ilifanyika Novemba 28 katika mkutano Mkuu wa mwaka wa SHIWATA uliofanyika Dar es Salaam ambapo wanachama zaidi ya 300 waliohudhuria kwa pamoja waliunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais wa Awamu ya Tano kupambana na wezi wa mali ya umma.
Alisema wasanii hao bila kujali itikadi zao kisiasa wanamuunga Dkt. Magufuli na wameahidi kumsaidia kufichua wote wanaotuhumiwa kula fedha za umma ili kuleta maendeleo ya kweli nchini.
SHIWATA yenye wanachama zaidi ya 8,000 nchini wanamuunga mkono Rais Magufuli kwa uongozi wake na wanamkaribisha kujiunga na wasanii katika kijiji cha Mwanzega Mkuranga chenye ukubwa wa hekari 300 za makazi ambapo mpaka sasa wamejenga nyumba 137 kati ya hizo 17 zinakabidhiwa Desemba 12, mwaka huu.
Pia Shiwata inalo shamba la hekari 500 katika kijiji cha Ngarambe, Mkuranga ambako wanatarajia kulima mazao mbalimbali

No comments :

Post a Comment